Tuwajenge watoto kumjua Mungu!

Wazazi peke yao wanahusika na malezi ya watoto wao? watoto wanasikitisha, wamekuwa watukutu, hawawatii wazazi wao. Kizazi hiki tunahitaji watoto wenye hofu ya Mungu, tuanze kuwafundisha watoto wetu Mungu ni nani, yuko wapi, anapenda nini na kazi zake ni zipi. Pia tuwape majina mazuri ambayo yataenda na tabia zao. Na wazazi nao tubadilike, tusifuate dunia inavyoenda, tutaathiri watoto na vizazi vyetu.

Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee” – Mithali 22:6

Advertisements

12 thoughts on “Tuwajenge watoto kumjua Mungu!

 1. WAZAZI NDIYO MSINGI WA TABIA NJEMA KWA WATOTO,TULIVYO NDIVYO WATAKAVYOKUWA,UMAKINI HASA KUWASOGEZA WATOTO NA MUNGU ITAKUWA MSAADA MKUBWA NA HOFU YA MUNGU IKIWAJAA WATAKUWA WEMA.

 2. Amina Mpendwa Samuel, ninaamini siku moja tutaonana. Asante sana

 3. Watumishi wa Mungu, Shalom!!

  watoto wetu wanahitaji tuwahudumiye kama kondoo wake Yesu, mala nyingi wachungaji wanajidahi kwamba watoto wao ni watu wa kiroho sana huku wengine wakisema kwamba watoto wao wameokoka just walipo toka tumboni!! Huo ni udanganyifu mtupu!! Tusisahau yalio mpata Mzee Eli kuhani mkuu na wanawe 2. 2 Samuel 2

  Watoto wetu wanahitaji tuongeye nao, tuwaobeye, tuwazoeze kazi …

  Huku Burundi binti mmoja baba yake alikuwa mchungaji, binti akamuhitaji baba kwa maongezi maana alikuwa na mzigo mkubwa sana rohoni. Alimuomba sana mda baba ye ili waongeye na Mchungaji alikuwa hana mda maana washilika walikuwa wengi wakimuhitaji, na alikuwa mchungaji wa sifa sana ambaye anawajali wakristo.
  Sasa Binti huu alipo mukosa kabisa ( maana majibu ya baba kila siku yalikuwa haya; subili bwana! nana rendez-vous yaani ratiba na watu furani na furani) ikaonekana yeye hana na fasi ya ukristo katika kanisa linalo ongozwa na baba yake na huku akiamini shida yake itamalizwa na Mutumishi wa Munga. unajuwa alifanya nini?
  Alicukuwa simu akajalibu kumuita baba,bahati nzuri baba naye hakuweza kuyitambuwa sauti yake maana alikuwa hajawahi kuyisikia kwa simu!
  Basi binti alimuomba nafasi ili waongeye naye alipoihangalia program akamuambia aje saa 4.
  Binti saa 4 alikueko tiali baba kumuona alimufukuziya mbali akimuambia kwamba ana mgeni. Binti kwa upole akamjibu kwamba mgeni ni mimi.

  Kabla baba hajajibu, binti alimuambia kwa machozi kwamba aliona kuwa baba hamujali nawakati naye anahitaji kwenda mbinguni kama wengine, ndipo akaamuwa kujifanya ESAU.

  Mchungaji kwa machozi aliomba musamaa kwa binti na tangu siku hiyo alitubu na akamupa yeye binti na wadogo zake muda wa kutosha.

  Neema nimepata ni kwamba Mchungaji alieleza hayo kwa mafundisho nilikuwa bado sijaoa na umekuwa msada mkubwa kwangu.

  Watumisha wa Mungu Tuwalinde sana watoto wetu na Mungu azidi kutubariki na kutujaza hekima yake. Amina

  NDUGU KUTOKA BUJUMBURA BURUNDI

 4. Hey!!!! kumbi nisehemu zote bwana! hata Huko Tanzania?
  Mungu atuongezee hekima ili tuwahifadhi wageni maana ni baraka wasinyimwe haki zao ila tusisahau kwamba jamii zetu ni makanisa na Mungu atatuuliza! je tutamujibu kama alivyo jibu Kaini kwamba sisi siyo wachungaji wao?
  Ninaamini katika hekima ya Mungu kuna majibu ya kutosha kwa kila swali. Amini Mungu hamudharau mtu yeyote: Ayubu 36;5.
  Mungu akubariki sana Mpedwa Samuel.
  Salamu kutoka Bujubura Burundi.

 5. Haaaaa!!!!! Hii mifano imetulia sana. Yaani inafaa sana makanisani kote. Umeona eeeh? Yaani ni ukweli mtupu. Hata kwetu yapo hivo hivo alivosema huyo mtoto.

 6. Shalom Mtumishi Samwel
  nimecheka ila kwa kweli, hili ni fundisho wazazi tukumbuke kuwa tuna watoto, tukumbuke majukumu yetu kama wazazi kiroho na kimwili.
  Nami nimeishakutana na utumishi uliopiltiliza, utoaji uliopitiliza, kazi/biashara iliyopitiliza yaani ni kupita kiasi. Sasa hapo mtumishi naona anatoa kuliko uwezo ingependeza kama angemwomba mshirika yeyote mwenye uwezo ampokee mgeni au amsaidie godoro kila mgeni akija badala ya kubeba jukumu kwa kugharimu haki ya watoto wake. Hili haliko ktk watumishi tu, kuna hata sie waumini unaweza jisahau ukatoa ahadi ya kumfadhili mtu kumbe mtoto anarudishwa fees shule na kujaa uchungu itoke mara moja sawa lakini ukifanya ni kawaida watoto watauchukia huo Utoaji ambao unawasababishia mateso…
  Vivyo kuna kufanya kazi au biashara au huduma kusiko kawaida, hadi familia ina kusahau, kuna kazi, huduma, biashara mtu anapotea nyumbani wiki tatu kwa mwezi na sio mara moja, kama ni hivyo ingia gharama beba familia au lipia nauli na malazi wafuatane nawe kila upatapo nafasi. Ilikuwa hivyo kwangu, ila niko radhi kila nikipata mwanya naingia gharama wanifuate nilipo hiyo imefanya familia nami tufurahi tukisikia kuna safari badala ya kuingia huzuni wakijua unawaacha.
  Kuna watu wanaona likizo nikupoteza muda, hata weekend jumamosi kama haendi ofisini/huduma anatafuta mahali kwa kwenda na si kukaa na watoto au mwenza ajue nini kinaendelea. Upate muda wa kuomba, kusoma neno, kuwasikiliza na kuongea nao kwa ukaribu. Ni aibu wazazi tunajua neno vizuri lakini watoto unakuta hata hawajui kitu, tuanze kuwazoesha wakiwa wadogo ili neno la Mungu lijae ndani mwao na sio uovu. Na hali ngumu hii, foleni muda umekuwa mchache sana tunatoka usiku tunarudi usiku ila Mungu atutie nguvu tujitahidi kutimiza majukumu yetu. Mbarikiwe

 7. Washirika wa kanisa wanafurahia mgeni, wanazifurahia siku 7, wanatamani ziongezwe, ila watoto wa Mchungaji, wanasikitika kwa mgeni aliyekuja, atawafanya walalie kagodoro kwa siku 8, maana kitanda chao ndicho mgeni atakuwa ana lalia mpaka siku zote 7, wakajumlisha na hiyo ya 8 aliyofikia. Mmoja sikumuona kwa siku 3, siku ya 4 niliuliza nikaambiwa sikui ile ile niliyofika aliondoka kwenda kwa shangazi yake, akaaga kuwa angerudi Jumatatu, mkutano ulikuwa unaisha jumapili, na jumapili jioni niliombwa niongeze alau siku 3 zaidi, nikawakubalia, yule mtoto alirudi j3, akanikuta, alinisalimu, lakini hakuonyesha furaha yoyote. Jioni nikamwita, nikaenda naye pembeni, tukakaa, nikamuuliza rafiki yangu ulikuwa wapi? Mbona sikukuona kwenye mkutano? Sikia majibu…………… MUNGU HATUPENDI SISI, ANAPENDA WAGENI, MAANA KILA SIKU TUKIPATA MGENI TU, TUNAJUA SISI NI WA KULALA CHINI TU, MPAKA MGENI AONDOKE, NA HAPA NI KWETU KWA BABA NA MAMA, KANISANI WANASHANGILIA KUWA TUMEBARIKIWA, MUNGU ANATUPENDA, AMETULETEA WAGENI, SASA NA SISI TUSHANGILIE KUWA AMETULETEA WAGENI WATULAZE CHINI… Ndiyo maana nikasema nitoe ushauri kwa WACHUNGAJI. Unaona mtoto huyo, kwa ajili ya wageni, akawachukia, na mpaka wakaona Mungu hawapendi, ebu watoto wetu wasipatiwe shida na wageni, wao wako kwao, mgeni anapita tu, sisemi tusiwajali, hapana, wasibughudhi watoto.mbarikiwe.

 8. Shaloom wapendwa, watoto wetu tunawahitaji ili twende nao katika ufalme wa Mungu, ndio maana Bwana Yesu akawaambia Binti Yerusalem hivi. MSINILILIE MIMI, BALI JILILIENI WENYEWE PAMOJA NA WATOTO WENU. Luka 23.27…28. Hapo tumeona tunapaswa kumuomba Mungu kuhusu watoto wetu. Nitoe ushauri kwa WATUMISHI WA MUNGU ( Wachungaji) siku moja nilikwenda mahali kufanya mkutano, nikapokelewa na Mch. Nikapelekwa katika chumba ambacho nitakuwa nalala kwa wiki nzima ya mkutano, kulikuwa na kitanda kimoja, chenye godoro, na godoro dogo lingine jembamba, nadhani lingepimwa lingekuwa theluthi ya nchi, kalikuwa kameisha, kalikuwa chini, nilingia, nilikuwa nimechoka, nikajinyosha juu ya kile kitanda, niliwasikia washirika wa kanisa wakifurahia Mkutano uliokuwa uanze kesho yake, ukiendeshwa na mimi mgeni wao kwa siku 7. Walikuwa nje, lakini niliweza kuihisi furaha waliokuwa nayo, mmoja akasema hata siku 7 hazitoshi kwa vile ninavyomjua mhubiri huyo. Baada ya huyo kumaliza. MTOTO WA MCHUNGAJI, MWENYEJI AKAINGIA NDANI, WAKATI AKIWA NDANI KAKA YAKE AKAMWITA, AKAMWBIA..,NJOO NA KAGODORO, KUMEKUCHA, SIKU 8, mwenzake akasema, Hakuna jinsi. Hapo juu tumeona…..inaendelea…..

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s