Ushindi wa Yesu ni USHINDI WETU!

Ndio umempa Yesu Maisha yako na ndugu n marafiki wanakupinga- Jipe moyo.

Ndio unaanza huduma na unaona vikwazo vikiinuka – Jipe moyo.

Umefaulu vizuri fedha za kukusomesha zimetoweka – Jipe Moyo.

Biashara yako ilikuwa nzuri ikileta faida sasa mtaji unatoweka – Jipe moyo.

Umepata kazi nzuri na sasa unatishiwa maisha – Jipe moyo.

Unatetea Haki na unashambuliwa kwa hilo – Jipe moyo.

Uliowainua wamekugeuka – Jipe moyo.

mkeo/mumeo alikuwa Mwema na mcha Mungu lakini amebadilika – Jipe moyo.

Mwili ni dhaifu – Jipe moyo.

“Ulimwenguni mnayo dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana Mimi nimeushinda ulimwengu.’’ Yoh 16:33 pamoja na hayo yote tun kuwa na amani ndani ya Yesu na Ushindi wa Yesu ni USHINDI WETU!

–“B”family ministry!

Advertisements

7 thoughts on “Ushindi wa Yesu ni USHINDI WETU!

 1. Halelua!!

  Yesu alipo sema kwamba yote yamekwisha, ndipo habari ya ushindi ukatangazwa .
  kumbe kwa wanadamu mambo yakiisha kwa Mungu yanaanza.
  Katika yesu ushindi ni kashi!
  Nimemuona akitokeya akiniokowa katika shida mbalimbali; kukosa kazi, kufiwa na mke wangu mpendwa; maisha ya kifungo jelezani…. nimemuona yeye ni mwaminifu katika yote.

  Sintamuacha kamwe! kwanza nitamuacha niende wapi?
  YESU NAKUPENDA SANA! NAKUPENDASANA WEWE ULIE NIPENDA KABLA MIMI KUEPO, SIFA ZOTE ZIKURUDIRIYE BWANA MILELE NA MILELE AMEN.

 2. Asante sana watumishi somo zuri, kweli tujipe moy ulimwenguni mnayo dhiki lakini Yesu aliushinda ulimwengu nasi yatapita tu. Tukitaka kila mapungufu yetu yaishe kweli tutoke ulimwenguni, ila watu bado hatusikii kila matangazo ya miujiza tunakimbilia huko, hatutaki kupungukiwa, kudhiliwa, kushuka, kuugua, kifo. Tunaanza kuwa radhi kutumia njia yoyote mradi tuwe juu daima, tusipungukiwe chochote, tusiugue, tusishushwe wala tusife. Asante kwa kutukumbusha kuwa tujipe moyo kwa Yeye Yesu tutaweza yote yaani kwa uwezo wake na si kwa ukamilifu wetu: afya zetu, mali zetu, elimu bali kwa neema yake, jina lake litukuzwe. Mbarikiwe

 3. Tuendelee kidogo, Kijana mmoja mwenye mali, Biblia inamwita TAJIRI, yeye tayari alikuwa tajiri, hakungoja ahubiriwe ati ATAJIRIKE, akamwendea Yesu, akamuuliza Bwana NIFANYEJE NIRITHI UZIMA WA MILELE? Yesu akamwambia UNAZIJUA AMRI? Akazitaja, alipozimaliza zote, akasema tangu utoto, nazijua, nazitunza. Yesu akamtazama, akamwambia NENDA UKAUZE MALI ZAKO, GAWIA MASKINI, KISHA NJOO UNIFUATE. Biblia inasema kijana AKAKASIRIKA AKAONDOKA. Unaona, huyu alikuwa aambiwe JIPE MOYO, KAUZE MALI ZAKO, GAWA, NJOO BILA KITU, Angefanya hivyo angetakiwa AJIPE MOYO. Alimwangalia Yesu, akamwona hana kitu, kama Yesu angemwambia, KAUZE MALI ZAKO, UJE NAZO, TUFANYIE KAZI, Maadam angekuwa nazo nadhani hilo lisingekuwa tatizo, na Yesu angemwambia wewe ni MSHIRIKA WA DINI YETU, ACHANA NA WENGINE HAO, LAKINI AKAMWAmBIA, Uza gawia maskini, ( tena hakusema gawia maskini wa dini yetu) huyu TAJIRI ALITAKIWA AJIPE MOYO, Alikutama na kinyume cha mategemeo yake. Ndio maana kila anayeenda kwa Yesu, anaambiwa TAABU YAKO KWISHA. Yesu akamwanbia yule Tajiri. UKIJA KWANGU UTAJIRI WAKO KWISHA. Jamani ikamshinda, alihitaji nyongeza. JIPE MOYO. JIPE MOYO. Akijua kila lenye mwanzo lina mwisho, tumpatie Mungu nafasi atuchagulie, wakati mwingine tunatengenezwa, tutulie tutengenezwe, Yesu akasema yeye ni MKATE, Alitulia akatengenezwa, akawa mkate, mahali pengine imeandikwa, ALIONEWA, LAKINI HAKUFUNUA KINYWA CHAKE. Tulia usiwe kama chapati, uwe MKATE. Mapenzi yake yatimizwe.jipe moyo. Amina.

 4. Neno hili limenigusa na limenibariki, mpaka nikawakumbuka vijana wale watatu, Shadrack, Meshack, na Abednego, walianya kusema MUNGU WETU ATATUOKO TU, waliendelea kungoja, hakuna kilichotokea, wakasema HATA KAMA HATATUOKOA, HATUTABADILIKA, kumbe Mapenzi ya Mungu yalikuwa ni kuingia kwenye moto, unaona waliambiana TUJIPE MOYO, Ebu nikushukuru kwa ujumbe wako ndugu yangu wa KUJIPA MOYO, Ubarikiwe na Bwana. Amina.

 5. Kama Yesu alisema MASKINI MNAO SIKU ZOTE. Hakuwatajirisha, naye ndiye alivitengeneza hivyo vyote, mimi NITAWATAJIRISHA WOTE? Yesu aliingia katika Hekalu la Mlango mzuri, alimpita yule KIWETE ALIYEKUWA ANAOMBA SADAKA, ALIJUA NI MTAJI WA PETRO, HAKUMSHUGHULIKIA, MPAKA PETRO AKAJA KUFANYA MTAJI, SS TUNATAKA KILA KILEMA ATEMBEE, Tujifunze kumalizia MAPENZI YAKO YATIMIZWE. Kumb 3.23..28 Musa mtumishi wa Mungu, aliomba aingie Kanaan, Mungu akamkatalia, tena akamwambia, NISIKUSIKIE TENA, PANDA MLIMANI UFE. 2 kor 12.7..10. Mtumishi wa Mungu Paul alimuomba Mungu amuondolee mwiba, jibu., NEEMA YANGU YAKUTOSHA. Huyu anatakiwa hilo neno, JIPE MOYO. 1pt 2..18…23. ENYI WATUMISHI, WATIINI BWANA ZENU KWA HOFU NYINGI, SIO WAO WALIO WEMA NA WENYE UPOLE TU, BALI NA WAO WALIO WAKALI, MAANA HUU NDIO WEMA HASA, MTU AKIVUMILIA HUZUNI KWA KUMKUMBUKA MUNGU. PALE ATESWAPO ISIVYO HAKI, KWA MAANA NI SIFA GANI KUSTAHIMILI, MTENDAPO DHAMBI NA KUPIGWA MAKOFI? LAKINI KUSTAMILI, MTENDAPO MEMA NA KUPATA MATESO. HUU NDIO WEMA HASA MBELE ZA MUNGU, KWA SABABU NDIYO MLIYOITIWA, MAANA KRISTO NAYE ALITESWA KWA AJILI YENU AKATUACHIA KIELELEZO TUFUATE NYAYO ZAKE, YEYE HAKUTENDA DHAMBI, WALA HILA HAIKUONEKANA KINYWANI MWAKE, ALIPOTUKANWA, HAKURUDISHA, ALIPOTESWA HAKUOGOFYA, ALIJIKABIDHI KWAKE AHUKUMUYE KWA HAKI. Alijipa moyo. Mapenzi ya Mungu yalitimizwa. Barikiwa.

 6. Shaloom, yote uliyaorodhesha wapo watu wanapitia, ni kujipa moyo, kujipa moyo maana yake ni KUJIKAZA KIUME UENDELEE NA HALI HIYO, ITAFIKA MWISHO WAKE, KWA KUWA ILIKUWA NA MWANZO ITAKUWA NA MWISHO PIA. Nakubaliana na wewe kabisa, hiyo ndiyo Injili ya kweli, baada ya maombi, tunamalizia hivi. MAPENZI YAKO YATIMIZWE. Hayo ndiyo maombi ambayo yameachwa, tunampangia Mungu msururu wa vile tunataka, kisha tunamwbia TUFANYIE HIVYO TUNAMALIZIA Amina, Biblia inasema, Yesu akaendelea kuomba, akiyarudia yale yale, kwa nini? Alikuwa amemwachia Mungu amwamulie, vinginevyo angesema Amina, abebe kilago aondoke Gethseman, Malaika angekuja akute ameshaondoka, angekuwa ni mtoro, wengi wetu ni watoro, hatuko Gethsemane, pia tukumbuke sio kila tunachomuomba atatupatia, ndiyo tunaandika kwenye postas LETENI VILEMA, VIWETE, VIZIWI. Je tukiwaleta wanaponywa wote? Kwa nini tumewaita kwa njia hiyo”? Asipopona tunamwanbia hana imani, (hana imani na amekuja). Yesu hakufanya kazi hivyo, hata siku moja alisema. MASKINI MNAO SIKU ZOTE. Leo watu tunawambia NJONI MTAJIRIKE. “( wote watatajirika)? Kumb 15.11. KWA MASKINI HAWATAKOMA KATIKA NCHI MILELE. Kama maskini hawatakoma ktk Nchi milele, na umati wote unaambiwa njoni tu mtatajirika, lile neno JIPE MOYO, MAPENZI YAKO YATIMIZWE HALIPO. Na tukumbuke kilichotarajiwa kikikawia moyo huugua, kabla haujaugua ni mgonjwa tayari, una ugonjwa wa kufisha. Inaendelea….

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s