Faustin Munishi apania Kugombea Uraisi Tanzania!!

“Mimi mchungaji Faustin Munishi. Natamka kwamba Nitagombea Urais Tanzania bila chama cha kisiasa. Nitakuwa Mgombea Huru bila siasa. Nitakapokuwa Rais Nitagawana madaraka na Jeshi, pia wadau wote hasa wapiga kura. Ukiritimba wa CCM kutumia madaraka vibaya utakuwa kwenye kaburi la sahau. EE MUNGU NISAIDIE NIONGOZE TANZANIA. NIPE HEKIMA NIJUWE JINSI YA KUWAONGOZA WATU WAKO WALIO WENGI TANZANIA. AMEN.”

Na hii ni Hotuba ya mchungaji Munishi kwa Taifa

–Faustin Munishi

Advertisements

25 thoughts on “Faustin Munishi apania Kugombea Uraisi Tanzania!!

 1. kiongozi yoyote yule anayeongoza taifa katika karne hii anapata changamoto nyingi sana kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia na kuwepo kwa uwanja mkubwa wa elimu wananchi wengi wamepata elimu hivyo wanajua uozo wote katika mataifa yao tofauti na uongozi wa zamani.

  MACHACHE KWA MTUMISHI MUNISHI.
  kwanza najua unajua kuwa dunia inatawaliwa na watu wenye pesa zao na kwa kuangalia Tanzania yetu mpaka sasa hivi siyo nchi yenye demokrasia tena ni nchi ambayo imeshikwa na watu wachache sana wanao weza kufanya jambo lolote na kutoshtakiwa kokote fatilia matukio yaliyotokea nyuma kama vile sakata la Ulimboka na mengineyo.

  pili sina imani kama umzoefu katika mambo ya kisiasa kwasabu naona umeanza kugombea ngazi ya juu mno ambayo kwako ni kubwa mno kwako.hasa kwa Tanzania yetu ilivyo sasa

  tatu kwa maneno uliyozungumza katika video hiyo najua nafasi yako katika kugombea urais sidhani kama utaipa ninavyojua siasa ni kugeuza maneno tu ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli ndivyo ulivyo siasa.

  nne kutokuwepo kwa demokrasia Tanzania sas hiv rais anachaguliwa na wachache (NEC)si kwamba rais anachaguliwa na wanainchi najua mwenyewe unafatilia masuala ya uchaguzi hivyo wewe ni shahidi pia katika hili

  najua mengine yamezungumzwa………….ni hayo tuuuuuuuuuu

 2. Amina mtumishi ,yote mema.Cha muhimu ni kuliangalia kusudi la MUNGU kwako na kulitimiza.Usiongozwe na tamaa wala chuki kutafuta uongozi.AMINA

 3. Mpendwa Munisi…the Malebo man!

  Kama Munisi angekuawapo hapa na kama anasoma comments zetu…..basi kama atasahau yoooote tuliyocomment na yatakayofuata…..kwa upendo wa calvary usisahu hiki nachotaka kusema kaka yangu mpendwa. Nakushauri jambo moja tu ambalo kwa hakika it will work for.

  Kwa kua umekua haupo nchini kwa muda na kwakua muda umebaki mdogo-kwa mtu ayejua hali ya hewa ya siasa za nchi yetu ni nini, kwa wewe kujijenga na kujinet-work pia kupanga logistics nchi nzima na kwa kua nina uhakika huna pesa na mali kama za Lowasa, Sitta, Zito, Asha Migiro,Benad Membe, Sumaye na kwakua nina uhakika huna marafiki wenye utajiri kama maji ya bahari kama marafiki wa wagombea hapo juu……….my lovely ushauri na kwakukupenda mpendwa wangu…….DROP KUGOMBEA URAIS, GOMBEA UBUNGE….utapita, tena Ubunge Mkoa wa Kilimanjaro kupitia chama Chadema….vamia jimbo la Prof. Jumanne Maembe i think au la Selasini ingawa yuko Chadema …hatapitishwa kugombea tena 2015 kwa udumila kuwili wake bungeni na chamani kama alivyo Shibuda
  Besides, kugombea ubunge 2015, anza sasa…chukua kadi….hudhuria vikao….jimuvuzishe-muvuzishe jimboni kila mara…shirika social issues zao huko …ingia hata kugombea udiwani mwaka mmoja before uchaguzi….ni strategies kwelikweli in politics…….. otherwise…..ukiendelea na urais, nakuhakikishia….HUTASHINDA NA WALA KUPENYA NA UTAPOTEZA MALI,MUDA,NGUVU, FAMILIA ITAKUKOSA….MAMBO AMBAYO UNGEYATUMIA KWA KUENDELEA KUNG’ARISHA TAJI YAKO MBINGUNI YA UUIMBAJI WA MIAKA MINGI ULIOTUKUKA NA KUPONYA/KUOKOA/KUHUBIRIA WENGI HATA WAISLAMU WALIIMBA MALEBO…IT WAS POWEFUL SONGS..kwa nyimbo zile za zamani uliopikua deep na Bwana na Roho Mt.

  Unless ukiwa na nia ya kuamsha umaarufu wako tena KWA NIA YA MBELENI….then ukigombea urais itakupaisha sana kwakua kila mahali na mtu atajua Malebo yupo but si kushinda kura..iyo ni habari nyingine kwakua hao hao wanajeshi uliosema utgawana nao madaraka….wanaweza kukudelete from the world na kukuwaisha mbinguni before time- your precious children and wife left in miserable regret

 4. CK lwembe,

  yaani wewe ni kiumbe wa ajabu sana…..yaaani nimecheka……niiiiiimecheka…hahhahahahahahahahah, uwiiiiiiiiiiiiii! Yesu ana viumbe jamani lo! we Lwembe kiboko lo! eti Gospel Matusi umenichekesha sana mtumishi critical man…..nimependa sana ulivyobaptize recent nyimbo zake kwa terminology iyo ya …..gospel matusi, sina mbavu hapa…..yaani unatoawga wapi maneno haya…..mi nilizani nina maneno but kwako lo! nataka kusurrender…Asante kamanda

  Milinga Juma Venerando

  Powerfully put my very senior spiritual kaka from Milambo men sec. Kweli tumtulize mpendwa munisi na tutakaa nae chembe ili atuambie haswaaa kilie kilichoko ndani kuleeee kilichomfanya agombee ni moyo na mzingo wa kutuhudumia au mambo yale yale ya wanadamu ….endless desire for power,influence, money. Nimesona Politics…mchakato wa mtu kupitia mpaka awe prezidaa na vigezo pia capacity is not equal to singing those nice songs such as malembo. Seriously, its good idea for brother ”Malebo” mana to think big but in politics especialy za these third world mmmmh…. wait a minute……think not big rather bigger…step by step.

 5. Munisi acha kujichanganya. Umekosa cha kufanya? Injili imekushinda?

  Kumbuka mifano ya walioshindwa Urais na walikuwa na umaarufu kukuzidi. Wewe una umaarufu gani Tanzania Kumzidi Lowassa Edward anayepania uraisi?

  Wewe una umaarufu gani kumzidi Zitto Kabwe anayewania Urais 2015?

  Wewe una umaarufu gani kumzidi Dr. Wilbrod Slaa aliyeukosa Urais mwaka 2010 na huenda akagombea tena 2015? Wewe una ubavu kumzidi?

  Wewe una ubavu gani kisiasa na kiuchumi na kijamii kugombea na kumshinda Bernard Membe anayejiandaa kugombea urais ?

  Unamkumbuka Augustino Mrema na Askofu wa FGBF Mzee Zakaria Kakobe miaka ileeeeeeeee ya 1995 na 2000? Umaarufu wote ule waliishia wapi? Hivi wewe unajulikana kumzidi mrema na Kakobe wake? Acha mbwembwe zako. Tulia kanisani.

  Unamzidi umaarfu mzee Samweli Malecera, Fredy Sumaye, Dr. Salim Ahmed Salim, nk?

  Tulia mtoto wa kuime. Tulia unyolewe nywele. Tulia na tungo za Zaburi. Au tungo zimeisha? Kwani hata kama tungo na vina vyote vimekuishia wewe si unaendelea kuhubiri mimbarani kila Jumapili? Au umeona jukwaa hilo la kanisani halikutoshi kupata unachotaka?

  Anyway, tunaomba sera zako tuone wewe unakuja na sera gani?

 6. Ndugu yangu Samweli, 
  Kama umefika mahali ukajiaminisha kuwa Mungu anaweza kututeulia rais wa nchi kutoka watumishi wake kwa mifano uliyonipa, yaani ukimfananisha Munishi na hao watumishi wa Mungu, basi bado una safari ndefu ya kumjua Mungu! Na kama unajiaminisha kuwa yule askofu Njoroge anayewadhulumu makahaba ujira wao anaweza kuwa nabii wa Mungu, nadhani safari yako utakuwa umefika!!

  Na kama unategemea huyo muimbaji wa “Gospel Matusi” akupe jibu la kueleweka kwa maswali uliyomuuliza, basi dunia imekwisha! Huyo hawezi kuwa na jibu la kukupa kwa sababu upeo wake ni mdogo sana ndio maana akayasema aliyoyasema kwa jinsi alivyoyasema!

  Mimi binafsi nawashukuru waliotuletea habari hizi, maana kwangu mimi baada ya kuzisikia nyimbo zake mpya zilizojaa matusi katika jina la Injili, nilisikitika na kushangaa kuwa yawezekanaje! Lakini baadaye niligundua kuwa tungo zimemuishia, na audience yake imemshawishi aanzishe huduma, na sasa anajaribu kuurudisha umaarufu wake wa miaka ya nyuma hapa Tz kwa upuuzi kama huu anaouleta!

  Lakini, penye wengi, …
  Pilato akawaambia, “Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?!!

  Ubarikiwe!

 7. Si vibaya kugombea urais lakini lazima mtumishi aangalie ni msukumo gani unamfanya agombee, asije akataka hivyo isiwe ni mpango wa Mungu.Kwasababu Mungu alishampa kazi ya kuchunga kanisa Je akiondoka kondoo watabaki salama?

 8. Wakati tunangoja ndugu yetu Munish ajitokeze atujibu, ebu tuendelee kuchanga mawazo, penye wengi haliharibiki jambo. Nimuunge mkono ndugu yangu KINYAU HAGGAI, Ili tumsaidie ndugu yetu CK LWEMBE, Mungu ana namna anavyopitisha watu wake, usidharau mtu kwa vile alivyo leo, kesho hujui atakuwaje, GIDION…alikuwa amejificha, anasaga ngano, malaika hakumsalimia kuwa ee mwoga. Alisema ee shujaa. DAUD….Wakati anachunga kondoo, mimi na wewe tungemwita Mchunga kondoo, kumbe Mungu anasema MFALME. YUSUPH…Mimi na wewe tungemwita MFUNGWA,…atatwambia nini? Mungu anamwita WAZIRI MKUU. Tumalizie kwa PAUL…..Aliitwa muuaji, hata waliompiga mawe Stephano, yeye Paul alikuwa shahidi, aliona safi, lakini Mbingu ilikuwa inamtazama vingine kabisa, ebu tuendelee kumsikiliza Munishi, kama ametumwa na Mungu, basi tutajua, kadri anavyojieleza, tuendelee kumpima, unajua hata kora alipatia nafasi ya kumdharau Musa kwa sababu ya kigugumizi. Ebu Munishi atujibu. Vile atagawana na Jeshi madaraka. Hilo ndilo nasubiri, maana nilikuwa kijiji fulani, nikiwa mwanajeshi, jeshi likaingia kutuliza kilichokuwa kinaendelea, ndugu, siwezi kueleza yaliyotokea, ebu atujibu kwanza madaraka hayo atakayowapa wanajeshi ni kufanyaje? Barikiwa.

 9. Ndugu Lwembe,
  Ndugu Lwembe,
  Amani ya Bwana iwe nawe.
  Uliyoyaandika ni kweli tupu, lakini mbona nawe umetumia lugha kali namna hii? Je umesahau kwamba biblia inatuasa kuonyana kwa upole na kwa upendo ili sisi wenyewe tusije tukaanguka kwenye mtego wa shetani?
  Kitu kingine umenishtua kidogo kwa kusema;
  “Watanzania,
  Hebu simameni kidogo mtafakari!
  Nchi yenu ina umri wa miaka zaidi ya hamsini, ambayo mmeishi kwa amani na upendo ambao ninyi wenyewe ni mashahidi. Hamjauana wala kubaguana!”

  “Neno nchi yenu’ limenifanya nifikiri mara mbili kwamba ndugu yetu Lwembe, wewe sio mtanzania mwenzetu?

  Otherwise, ushauri ulioutoa kwa sisi Watanzania ni mzuri sana wa kujihadhari na kila mtu anayekuja na lugha tamu ya kuwakomboa Watanzania, kwa kweli lugha hii imenikifu masikioni mwangu kwa muda mrefu kwa sababu huo sio ukombozi kwa Watanzania bali ni ukombozi wake yeye anayesema maneno hayo!!

  Umebarikiwa ndg yangu Lwembe na wengine wote wanaohoji hili kusudio la Bwana Munishi, hasa ndg yetu Samweli, Mwanajeshi Mstaafu.

 10. Watanzania,
  Hebu simameni kidogo mtafakari!
  Nchi yenu ina umri wa miaka zaidi ya hamsini, ambayo mmeishi kwa amani na upendo ambao ninyi wenyewe ni mashahidi. Hamjauana wala kubaguana!

  Lakini leo hii mapepo ya vurugu yameanza kuwashawishi mjiingize ktk fujo na vita ya wenyewe kwa ahadi za kijinga kuwa eti mtajikomboa! Nchi imeruhusu vyama vingi, kujikomboa gani huko kunako hitaji matusi ktk jina la injili?

  Huyo Munishi anatafuta umaarufu mpya kwa kuwafanya watanzania wapumbavu! Umaarufu wa kuimba unamuondoka na sasa amekuwa kibaraka wa mapepo ya “DOOM” akiimba matusi, hata hao wanaomwita “mchungaji” nawashangaa sana, ama kweli ukishangaa ya Musa…! 

  Ushauri wangu kwenu watanzania wenzangu, mpuuzeni huyo muimbaji aliyefilisika tungo za maana; hata sasa mnamuona akija na tungo za kupandikiza chuki ili tuinuliane mapanga kama wajinga wengine wanavyouana!

  Hivi ni nchi gani hakuna wizi? Msidanganyike na hivyo vipepo vya njaa ya umaarufu, tuendelezeni vyama vyetu vya siasa kwa amani ili tuendelee kupata nafasi ya kumuabudu Mungu wetu na si kugeuzwa wakimbizi kwa ushawishi wa watu walioanguka kama huyo aliyedandia uchungaji kwa kuimba!

  Kwanza hata u jumbe wa nyumba kumi hawezi kupewa kwa tabia yake ya matusi, hana hata staha, wala heshima kwa viongozi wa nchi, sijui kawakusanya wajinga gani huko Kenya wanaomwita “mchungaji”; au naye ni wa staili ya yule Njoroge wa “shoti”!!!

  Bwana awapeni macho ya rohoni ya kuwatambua mbwa mwitu waliovaa ngozi ya uchungaji!

 11. Wakati nasubiri jibu kutoka kwako, nililokuuliza, nimeuliza kama ni. 1. Ni Mungu amekwambia, au ni mwenyewe umewaza. Nikuulize tena swali lingine. UNAIFAHAMU KAZI YA JESHI AMBALO UMESEMA UTAGAWANA NALO MADARAKA ENDAPO UTAKUWA RAIS?. Maana kuna. 1. JESHI LA MGAMBO. 2.JESHI LA UHAMIAJI, 3. JESHI LA MAGEREZA. 4. JESHI LA F.F.U( FIELD FORSE UNIT, AU FANYA FUJO UONE. 5. JESHI LA ULINZI. Nimejaribu kukuorodheshea hapo MAJESHI. Ni lipi mtakalogawana madaraka. Tusaidie, ukiwekea wazi kuwa wewe kama Rais madaraka yako yataishia hapa, na Jeshi litatawala hivi. Pia nikuulize, JE UMEWAHI KUSHUHUDIA TUKIO LOLOTE KATIKA KIJIJI CHOCHOTE, IWE kenya unakokaa, au Tanzania, kimetembelewa na Jeshi ama la field Forse, au Jeshi la Ulinzi? Ngoja kwanza unijibu hayo, ndipo nitakupa ushauri. Naweka sawa tusije tukaruka MKOJO NA KUKANYAGA MAVI. Nilikuwa miongoni mwa Wanajeshi tulioingia Uganda kumung’oa Nduli Idd Amin, ukipata mganda yeyote aliyetawaliwa na Jeshi, muulizie kwa utafiti zaidi, japo yeye Nduli hakuwa amegawana madaraka, ndio maana nikakuuliza, nigawanyie Madaraka yako yatakapoishia, na ya Jeshi yatakapoishia. Nasubiri majibu, mwanajeshi mstaafu. Asante.

 12. Mtumishi wa Mungu Munishi, shaloom, kwanza kabisa nikupongeze kwa ujasiri huo uliouonyesha wa kutamka kuwa unataka kugombea Urais wa Nchi hii, nikuulize swali, NI MUNGU AMEKWAMBIA? Au UMEWAHURUMIA WATANZANIA UKATAKA KUWATOA WALIPO?. Biblia inasema Wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu. Kama ni Mungu amekwambia, hapo sina la kusema, ila ni wewe KUMSIKILIZA VIZURI ANAVYOKUELEKEZA, KIPI USEME, KIPI USISEME, WAKATI GANI UKISEME, MAANA HAPO NI WEWE NA YEYE, KAMA ALIVYOFANYA KWA MUSA. Zab 103.7 ALIMJULISHA MUSA NJIA ZAKE, WANA WA ISRAEL MATENDO YAKE. Lakini kama Mungu hajasema na wewe, eti kagombee Urais, napenda nikushauri. Rudi nchini, nenda JIMBO LOLOTE, gombea Ubunge, jipime kutoka hapo, ukifaulu uanze kuwatetea hao watu wa jimboni, wakati huo utakuwa unajiandaa kuitetea Nchi, unajua hata mfalme Daud hakunyosha kwenda Ikulu moja kwa moja kama Mfalme, utakumbuka alikaa Ikulu akipiga kinubi, wakati huo akiangalia jinsi mafaili yanavyoingia na kutoka. Mwisho akaja kuwa mfalme. Nasema kwa sababu, umeeleza ktk hotuba yako kuwa UTAGAWANA MADARAKA NA JESHI. Labda ungetufafanulia hapo, tukushauri pia, yawezekana Jeshi hulijui, unalisikia tu, na mpaka useme mgawane madaraka. Huo ndio ushauri wangu, fanya hivyo, hujachelewa, bado u kijana. Asante.

 13. Kweli ni haki ya kila Mtanzania kuwania nafasi yoyote ile katika jamii ili aweze kutoa mchango wake. Na hii pia ni haki ya Mchungaji Munishi kufanya hivyo. Lakini nina mambo machache juu yake: Nimekuwa mpenzi wa nyimbo zake muda wote. Zina mafundisho mazuri ila kuna mahali pengine najiuliza; akiwaombea Wanahabari wabadilike; kwa nini haiombei CCM nayo ibadilike? Ila anaihukumu kuwa ya imezeeka na niya majambazi? Je Wana CCM wote hawastahili kuwa Watanzania? Je yeye akija kama mgombea binafsi atasimama vipi na watakaopingana naye na kuwa na mawazo tofauti naye? Je ile amri ya Bwana wetu isemayo mpende adui yako kwake iko wapi? Siasa na Neno la Mungu ni kama maji na mafuta kama alivyoimba mwenyewe “havichangamani”! Itakuwaje leo anataka kuwa Rais wa nchi yetu? Atakuwa na mwelekeo gani kuhusu Watanzania? Kama ninavyofahamu anaishi nje ya nchi yetu kwa miaka mingi na kujitajirisha kwa njia moja au nyingine: Je ni mkimbizi?
  Kwa sasa vipo vyama vingi vya kisiasa Tanzania tumwombe Mungu ili atupe kiongozi atakaye tuongoza kwa amani.
  Kwa Mchungaji Munishi nakusihi uendelee kuimbea nchi yako na viongozi wake waliopo ili kama wana mapungufu yao Mungu awabadilishe. Utakuwa umenibariki.

 14. Bwana Yesu apewe sifa ndugu zangu,

  Ni jambo zuri kugombea urais lakini kuna vigezo vingi vya kuzingatia kwa mfano ni kiasi umejikita kwa watu ambao ndio wapiga kura wako. Umaarufu wako ni kiasi gani unajulikana miongoni mwa jamii ya watanzania bara na visiwani. Sera zako kama zinakubalika kwa watu hasa vijana, wasomi, wakinamama, wafanyakazi wa serikali, wafanyabiashara, wajasiriamali nk. Ni watu kiasi gani wanakusapoti yaani ni watu wangapi wako nyuma yako endapo kama leo utatisha mkutano wa hadhara pale Jangwani ni watu wangapi wanaweza kujitokeza kukusikiliza na kusimama na wewe?? Unahitaji fedha ili uweze kumove kutoka eneo moja kwenda jingine na uwe na wafadhili wa kukusaidia.

  Kwa upande mwingine, ndugu yangu na mtumishi mwezangu sijakusikia huku TZ miaka mingi mambo huku yamebadilika sana hasa kisiasa sasa ni kiasi gani umejiandaa ili uweze kupenya katika ulingo huo.
  Halafu sheria ya mgombea binafsi haijapitishwa kwa maneno mengine mgombea binafsi haruhusiwi sasa wewe unakuja kuvunja sheria za nchi??
  Ushauri wangu, ombea mabadiliko ya katika yaweke hicho kipengele ili wagombea binafsi waruhusiwe pia toa maoni yako popote ulipo kuhusiana na hilo.
  Kingine sasa rudi TZ uanze kujijenga kwa miaka mitatu utakuwa umekwishakomaa, umejulikana, umepata watu nk ili ukigombea usipate tabu.
  Vilevile nauliza ni kwanini unaanza juu sana?? kwanini usianze na Ubunge?? halafu ukapanda Glory to Glory??

  Blessed!!

  Rev. Damasus F. Mkenda
  Redeemed Gospel Church Tanzania
  Jesus Celebration Centre Dar es salaam
  Off Shekilango Road Near Kinesi (Urafiki) Football Grounds
  P O BOX 55667
  Dar es salaam – Tanzania
  Tel: +255-787-661125/+255-754-585415/+255-712-340953

 15. NI VIZURI SANA WATUMISHI WA MUNGU NAO WAONGOZE INCHI .
  KWASABABU WANAEZA ONGOZA VIZURI KAMA WATU WANAWOGOPA DHAMBI NA MUNGU.
  MUNGU AKUONGOZE NA AKUPATIE USHINDI.
  NITAKUWOMBEA
  MTUME VEDASRE NIZEYIMANA
  FOUNDING PRESIDENT WA KANISA CHRISTIAN LIFE OPPORTUNITIES CENTER (CLOC)
  +250788355197
  E-mail:nizeyimanavdaste@yahoo.com

 16. wakati umefika wa nchi hii kutawaliwa na viongozi wenye hofu ya Mungu – big up mtumishi

 17. Hongera kwa wazo lako,
  Mungu akutie nguvu na akupe hekima kilifikia lengo lako hili.
  Ila naona ingependeza angefuata kanuni sahihi, kutangaza nia sio tatizo, tatizo naona lugha anayotumia juu ya uongozi au serikali iliyopo. Wakati ni sahihi kutaja maovu ili wajisahihishe lakini kama neno lisemavyo bado tunapaswa kuitii kila mamlaka iliyo juu yetu, hii ni kutusaidia wenyewe tusije kubanwa na sheria za nchi na kuishia kufungwa mfanao Mtikila.
  Atanagaze nia yake kwa moyo na lugha safi na watu watamuainua mbele za Mungu kama ni kusudi lake kumuweka nafasi hiyo. Mungu akuongoze mtumishi.

 18. Sawa mchungaji, tunakubariana na wewe kwamba kila kitu kwa Mungu kinawezekana! na kweli tunahitaji viongoi wanao muheshimu Mungu wa mbinguni na Neno lake.

  So kaza mwendo sasa. from Burundi

 19. Go for it man of God. When righteousness rules, the people rejoices. We pray for you and would even come support where we can. God bless you.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s