Ni ipi ilikuwa sheria ya Mussa?

Wapendwa Bwana asifiwe sana,
Ninahitaji kujua mambo mawili na nitashukuru sana kwa atakaejitolea kunijuza
1.Ni sahihi ninavyoelewa kuwa Maana ya neno “torati” ni “sheria”na nini asili ya hili neno!/
2.Nilipokuwa najaribu kujua Historia ya kanisa nimekutana mara nyingi sana na neno “sheria ya Mussa”na kwamba hapo mwanzo kabisa wa kanisa wakati wayahudi wenye asili ya kigiriki walipokimbia toka Yerusalem baada ya kuuwawa kwa Stephano na kwenda kuanza kueneza ukristu huko syria, ilikuwa ni lazima kwa wapagani kuishika sheria ya mussa kabla ya kubatizwa!!
Swali langu nia hivi……Ni ipi ilikuwa sheria ya musa?na tunayo hadi sasa?

Richard E.Mallya

Advertisements

6 thoughts on “Ni ipi ilikuwa sheria ya Mussa?

 1. nimechanganya sana pale mwisho wa maada yangu samahani kwa wote kwa kuwa nilikuwa natoa mchango ule kutota kichwani mwangu nikiwa kwenye gari!..hivyo basi mpangilio wangu haukua mzuri kwenye maada ile.naomba kuirudia yote kwa umakini kama ifuatavyo:Mwenyezi mungu alimpa nabii musa torati katika mlima sinai baada ya kuwakomboa israel toka utumwani misri.katika torati ile,mungu alimuandikia musa sheria kuu(amri 10) kwa watu wote,zilizotiwa ndani ya sanduku la agano kwa ajili ya urithi wa mataif yote au duniani kote hata milele(chakula cha wamchao).pitia katika(zaburi 111:5-9)(ufunuo 14:12).pia kupitia mkono wa musa katika chuo,mungu alimuagiza aandike maagizo ya kisheria kama 500 kwa ajili ya israel tu.dhumuni kubwa la sheria zile ndogondogo ni kutumika kama ukuta au kizuizi kati ya israel na mataifa mengine ambayo hayakuwa chini yake.pia maagizo yale yaliwaongoza kama mwalimu katika tabia zao za kimwili kama kusujudu,kutawadha nk,kuwakamilisha katika mambo ya kimwili na kiroho wafuate vema amri kumi za mungu bila kujikwaa.soma(kumbuk 4:14).Fahamu kuwa hii yote ni sheria au torati ya musa na haya ni maagizo yake katika kuitekeleza kimwili.Amri kumi na maagizo haya ni mmoja ni kama mchanganuo wake ili ifuatwe vizuri.mf ilikuwa ukifanya kosa dogo unapigwa bakora au unapelekwa katika baraza la wazee ukaonywe kabla ujaalibikiwa zaidi na kuangukia katika sheria kuu au amri 10 za mungu zinazodai malipizi ya jino kwa jino kwa kuwa mungu ni mtakatifu katika sheria zake.soma(kutoka 21:22-25).Hivyo basi mungu alimleta bwana wetu yesu kristo kuitukuza na kuiadhimisha katika ukamilifu wake, ili wote watakaomuamini mungu kupitia yesu kristo wapate njia ya kumfikia mungu,kwa kuwa sisi wenyewe ni watenda dhambi kwa hiyo tusingeweza kuitekeleza sheria ile kwa uwezo wetu,(mhubiri 7:20)(zaburi 14:2,3) na Biblia inatufundisha wazi wazi kuwa MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI…na sheria zile hazikuja kwa imani bali zilikuja kwa malipizi kwa sababu zilikuwa ni haki ya mungu na mungu ni mwenye HAKI KAMILIFU…kwa hiyo isingewezekana kabisa mungu wetu huyohuyo mwenye haki kamilifu awe na huruma wakati huo huo!!..hivyo basi,yesu kristo ni njia na kweli na uzima,soma(yohana 14:6),Tunapata msamaha wa mungu na kuokolewa kupitia yeye,soma(matendo 4:12),kwa kuwa alibeba adhabu ile ya laana ya torati pale msalabani iliotupasa sisi…sasa amekaa juu ya sheria ya mungu na kuwa daraja au njia yetu kwa neema aliotuandalia mungu,yaani:HAKI IMEKWENDA MBELE NA KUZIFANYA HATUA ZAKE KUWA NJIA,kama utabiri ule wa mungu kwanjia ya manabii wa zamani ulivyoahidi. Soma(zaburi 85:13).Hivyo basi,yesu kristo ametutoa katika matenndo ya sheria na kutuleta katika njia ya imani,Fahamu kuwa UPENDO NDIO UTIMILIFU WA SHERIA ZOTE,soma(rumi 13:8-10) kivipi?..ni kwamba torati yote ya musa inategemea amri kuu mbilitu,kumpenda mungu na jirani zetu,soma(mathayo 22:35-40)amri ya kwnza mpaka ya tano zinabebwa na amri ya kwanza yaani Upendo kwa mungu….na amri ya tano mpaka ya kumi zinabebwa na amri ya pili yaani kuwapenda majirani zetu.kwa hali hiyo maagizo yote ya mungu na amri zake katika torati ile ya musa,tunayafuata katika roho tukiongozwa na roho wa mungu kwa njia ya upendo kwa sababu tukiwa na upendo wa mungu na kuwapenda jirani zetu hatutaweza kuvunja amri yoyote katika zile amri kumi za mungu.hivyo agano lile la sheria ya musa linakamilishwa katika roho kwa njia ya upendo na wala sio kupuuza amri zile kuu za uwadilifu sana za mungu,soma(rumi 8:4-17).Hivyo hatutendi sheria ya musa katika mwili bali tunaitii sheria ile katika roho tukiongozwa na mungu mwenyewe kwa njia ya upendo kwa kuwa:MUNGU NI UPENDO,soma(1yohana 4:8,16),NA SHERIA ZAKE NI UPENDO,MAAGIZO YA MUNGU NI HAKI NA KWELI NA HIYO PIA NDIYO TABIA YA SHERIA ZAKE,soma(zaburi 119:142,172).mwisho..nawashukuru wote na mbarikiwe.

 2. Umejibu vizuri nadhani umechanganya mwishoni kama sijakuelewa vizuri

 3. nawashukuru sana wachangiaji walionitangulia kwani michango yao ni kweli na lengo lao ni kuelimisha kama ninavyotaka kufanya mimi.MWAJINA WANGU NA WAAMINIO WOTE SHIKENI SANA SANA MAFUNDISHO YANGU YAFUATAYO YA SHERIA AU TORATI YA MUSA KAMANITAKAVYO FAFANUA: MUNGU alimpa sheria kuu(amri kumi) nabii Musa pale sinai akiziandika kwa mkono wake ktk mbao mbili za kutumia israel na dunia yote au vizazi vyote mpaka miisho ya dunia.hili ni agano kwa watu wote,tena mungu atalikumbuka na kufanya hukumu kwa sheria hiyo kuu,soma(zabur 111:5-9)(ufunuo11:19,14:12).Pia mungu alimpa nabii musa maagizo ya kisheria(sheria ndogondogo)zaidi ya 500.Visheria hivi walipewa israel tu! Kupitia mkono wa Musa ili viwaongoze wao kwa kuwa waliifuata sheria ile kuu kwa mambo ya kimwili na kiroho(jino kwa jino) soma(kumbuk 31:24-26) na hayo yalikuwa ni maagizo ya mungu ili kuwafundisha dhambi waione ilivyokuwa mbaya sana(kioo cha tahadhali).pia visheria hivi vilitumika kama mwalimu au mfunishaji kuwaleta kwa kristo mkombozi wa njia zile ngumu za torati.soma(galatia3:19)(rumi 5:20).pia kwa ujumla soma(kumbuk 4:12-14).Hivyo basi,wakristo tunaendelea kufuata sheria kuu tu(AMRI 10) milele,hii ni sheria kuu ya mungu kwa watu wote,lakini fahamu kuwa hatuifuati katika mwili na adhabu kwa kuwa yesu kristo alisha kufa katika mwili soma(isaya 53:4,5,6) na kuitukuza na kuitimiza yote,soma(isaya 42:21-23)(mathayo 5:17)Zilinganishe na(luka 24:44-48) na kutuleta katika muafaka kamili wa mungu yaani tuenende katika roho na wala si katika mwili ambapo maagizo yote matakatifu ya mungu na sheria zote tuna timiza katika roho na wala si katika mwili soma(warumi 8:4-6).Hivyo yesu kristo ametuleta katika muafaka kamili wa mungu kwa kuwa lazima tukumbuke kuwa baba yetu adamu wa mwanzo ndivyo alivyokuwa,yaani hakuandikiwa sheria za mungu bali alizifuata katika roho(alikuwa mkamilifu).Hivyo basi na sisi tumekuwa watoto wa mungu na tunaishi tukifuata mambo ya roho na wala si ya mwili,upendo wa mungu ukituongoza kupitia roho wa mungu na injili.kwa njia hiyo tunakuwa watoto wa ahadi kwa ibrahimu sawasawa na urithi.Mungu alimwambia ibrahimu:KATIKA WEWE MATAIFA WATABARIKIWA.SOMA(MWANZO 12:3).Waifuatao sheria hawawezi kupokea ahadi hii kwa kuwa wanaishi chini ya laana ile ya sheria takatifu kwa kushindwa kuifuata vyema torati,soma(kumbuk 27:26)(galatia 3:10) na wala hatuwezi kutii kwa kuwa nia ya roho ni uzima lakini nia ya mwili wetu ni mauti,hivi viwili vinapingana tangu zamani soma(warumi 8:7,12,14).Thax mwajina.

 4. Mpendwa Richard
  Walionitangulia kujibu maswalii yako wamesema vema. Nami napenda tu kuongezea kidogo tu:
  1.Torati yaani Torah kwa Kiebrania ni Jina la vile vitabu vitano vya kwanza (Tanakh) katika Biblia ambavyo kwa Kiebrania vimepewa majina kutokana na Neno au maneno ya mwanzo, vinajulikana pia kwa jina la asili ya Kigiriki la Pentateukhos-Pentateuko (penta=tano na teukhos= kitabu). Torati lina maana :
  Kitabu cha Mwanzo (Bereshit=Hapo Mwanzo)
  Kitabu cha Kutoka (Shemot=Majina)
  Kitabu cha Mambo ya Walawi (Vayikra=Aliita)
  Kitabu cha Hesabu (Bamidbar= Ndani ya Jangwa)
  Kitabu cha Kumbukumbu la Torati (Devarim- Maneno)
  Kwa asili yake Torati inatokana na maneno ya mwongozo na mafundisho ambayo Mungu alimpa Musa pale kwenye Mlima wa Sinai na pia katika madhabahu ambayo Musa aliyaaandika. Ndio maana vitabu hivi huitwa pia “Vitabu Vitano vya Musa”. Vitabu hivi si mkusanyiko wa sheria bali ilikuwa ni msingi wa imani ya Waisraeli ambao pia umekuwa msingi wetu Wakristo kutokana na maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo kusema ya kwamba yeye hakuja kutengua torati bali kuitimiliza.
  2. Kufuatana na Ukristo yatupasa kuishi kwa maadili na mafundisho yazingatiayo sheria kuu mbili:
  “Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote”
  “Mpende jirani yako kama nafsi yako”
  Na NEEMA yake Kristo Masihi yatosha kwetu.

 5. Ndugu Richard, labda nijaribu kujibu maswali yako kama ifuatavyo:

  1. Torati – Ni neno lenye asili ya Kiebrania, limetokana na neno Torah, kimsingi torati tafsiri yake ni “mafundisho/maelekezo” siyo “sheria” . Torati ni vile vitabu vitano vya kwanza kabisa katika Agano la Kale, yaani Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati.

  2. Ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume utaona kwamba Wayahudi waliomwamini Bwana Yesu walipotawanyika baada ya kuuwawa kwa Stefano na mateso kuanza Yerusalem walikwenda wakihubiri injili na wengi waliamini, mfano Filipo alikwenda Samaria kuhubiri kule na wengi waliokoka. Baada ya mataifa kuokoka baadhi ya waumini wa Kiyahudi waliwataka waishike sheria ya Musa, yaani wafuate mila na desturi za Kiyahudi wakianzia na tohara, hilo lilipelekea mvutano mkubwa ikafikia mahala wakatuma watu kwenda Yerusalem kuwauliza mitume wafanyeje. Katika Matendo 15: 1 – 33 unaweza kusoma yaliyotokea.

  Kwa kifupi siyo lazima kwa mwamini asiye Myahudi kuishika ya Musa isipokuwa mambo machache ambayo ilipendeza Roho Mtakatifu pamoja na mitume kuwaambia watu wazingatie:

  yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu. – Matendo 15: 29

  Ubarikiwe na Bwana Yesu!

 6. Richard,

  Sheria ya Musa si moja, bali ni yale yote ambayo Musa aliambiwa au kukabidhiwa na Mungu na yako katika vitabu Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kitabu cha Kumbukumbu la Torati…..Haya yote yanaitwa Sheria ya Musa. Na baadhi ya Wayahudi wamejaribu kuzihesabu sheria zote katika vitabu hivyo, na idadi inayokubalika na wengi ni ile ya Rabbi Simlai katika karne ya Tatu…..na idadi yake ni kwamba sheria za Musa ziko 613…..!Na ndio maana hatuwezi kabisa kwa kutumia sheria kuifikia Haki ya Mungu….Sheria ilikuwa ni mwalimu kutuleta kwa Kristo….!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s