Zanzibar na mfungo wa ramadhani….

 Stori kutoka kwenye bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania July 26 2012 ni kuhusu Swali alilouliza Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Swali la Mchungaji lilitokana na taarifa kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa tamko kuwachukulia hatua wananchi watakaoonekana wanakula mchana au kuvaa nguo fupi wakati wa mfungo wa Ramadhani. 

Mch Msigwa alimuuliza Waziri mkuu “Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nimesema haina dini, je ni wakati muafaka kwa Serikali yako kutangaza sasa kwamba upande mmoja wa Muungano una fuata sheria za kidini na upande mwingine wa Muungano hauna dini?

Kauli aliyoitoa Waziri mkuu kumjibu mchungaji Msigwa ni hii….  “Nasema hili kwa maana ya mazingira ya Zanzibar, ukienda Zanzibar tungechukua tu takwimu za jumla jumla unaweza ukaona kabisa karibu asilimia 99 hivi ni Waislamu, sasa ndio maana nasema kwa mazingira ya Zanzibar viko vitu ambavyo vinaweza vikafanyika na mimi nadhani kwa sehemu kubwa atakua alipima vilevile mazingira, usilifanye likawa jambo kuuuubwa, angekua anazungumza kwamba serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ofcourse ingekua tofauti”

–Fundi wa Kombo Blog

Advertisements

10 thoughts on “Zanzibar na mfungo wa ramadhani….

 1. mimi yameshawahi kunikuta tena hapa dsm msasani nilienda dukani kununua soda mwenye duka kaniambia kuwa angeniuzia soda kama ningekuwa na chupa nikamjibu nakunywa hapahapa akasema aliyemkodishia fremu amekataza watu wasiuziwe vitu vilivyo tayari kuliwa au kunywa kipindi hiki cha ramadhani ikawa muuza duka alinishauri kama nalazimika kunywa soda basi nijifiche nyuma ya duka watu wasinione . kweli ilinikera sana na nikawa na hasira hata kiasi cha kuwachukia watu wenyewe. Ingekuwa jambo la busara kama wanapambana na dhambi badala ya vitu visivyo kuwa na impact yeyote kwenye imani.ingekuwa thawabu kwao kama wangeshinda jaribu la kukaa na watu wanaokula kuku bila kujaribika na ingekuwa wamefunga kweli.otherwise wanalazimishwa kushinda na njaa.kuweni wastaarabu bwana kwani ustaarabu nao suna.

 2. Yes,Kwa Hoja hii,Mheshimiwa Waziri yupo Right.Ifike kipindi tuache malumbano ya dini,tufuate yaliyo sahihi.Tujaribu kuwaamini viongozi wetu kwa kuyafuatilia wanayoyasema kwa mizani ya usawa.

 3. Shalom
  asante Yesu kwa hili, naona kidogo macho ya wabunge wetu yanafunguka, asante mtumishi Msigwa kupata nguvu ya kuhoji hili tunakuombea maana upinzani juu ya hili ni mkubwa
  wengi wa viongozi wetu wako kulinda maslahi yao tu ukristo ni ktk majina yao vinginevyo ni wajaza tumbo wasiojali nini kinaendelea
  Napenda kuwajulisha kuwa hii ni hali halisi huko, na ukikutwa unakula nje unawekwa mahubusu na kubebwa kwa karandinga na vipigo kabisa, pia sio mavazi ya staha tu hata vichwa baadhi ya mitaa usipite bila kufunika utatukanw ana kusukumwa.
  waathirika wakubw ani watu wa bara ambao wameenda kufanya vibarua kula wengine mfano ujenzi na inabidi wale mchana kwa kina mama lishe huwa wanasombwa na kutupwa ndani kwakweli sio haki.
  wakati kuna watu wanafikiri muungano ukivunjwa wabara wakiondoka kutakuwa hamna Ukristo sio kweli kuna wazawa wa kule ni wa Kristo miaka mingi wakiwemo kina jaji mkuu mstaafu augustino Ramadhani, Ukristo ulianzia kule ndio ukaingia bara kama sikosei makanisa makongwe mno yapo kule. Kuwatesa na kuwanyanyasa ni kuwanyima uhuru wao wakuabudu.
  Ushauri wangu tuwaombee na ikibidi kuwatetea na kuwapa support hawa wenzetu wa visiwani, tukiweza tupeleke injili zaidi huko, na kusaidia wale waliopo tayari kule. Tukiangalia kw ajicho la Nigeria na sasa Mombasa siasa za kujitenga majimbo kwa udini na sharia zina adhari kubwa maana kama ilivyo hadithi ya ngamia shetani akiishawabadili mioyo watataka kuingiza mwili mzima (sharia) iwe nchi nzima na kuchoma makanisa kote kama Nigeria na Mombasa.
  Wapendwa kuweni macho sana na vitu kama hivi sio muda wa kulala!
  Mbarikiwe

 4. Ndugu zangu, nawaite ndugu zangu kwani Mwenye enzi Mungu katuumba hivyo. Ni vema sisi sote kujua nini maana ya kufunga. Nakumbuka utabiri wa Marehemu Sheik Yahaya mwaka fulani aliposema ya kwamba katika mfungo ule Tanzania walikuwepo watu wawili tu waliokuwa wamefunga kikweli. Na wengine woooote walikuwa wanashinda na njaa tu. Tena nasema hivyo maana mimi mwenyewe nina ndugu zangu wa damu ambao ni Waislamu na wanapofunga mwezi wa Ramadhani hawanikani na kuniona kuwa si ndugu yao. Ninawapenda ndugu zangu na hata Waislamu washikiao maadili ya dini yao; ila siungani na watu wapendao kuvuruga amani ya nchi yetu iwe kwa kupitia Muungano au vinginevyo. Namkubali Rais wetu na Makamu wake na ninamwomba Mwenye enzi Mungu awajalie hekima katika kutuongoza wote bila kujali udini. Sikubaliani hata kidogo na yeyote awe Mkristo au Mwislamu kutuletea siasa ya Udini nchini mwetu. Kumbukeni ya kwamba hata Wakristo nasi huwa tunafunga na pengine hata baadhi yao hushinda na njaa tu bila kufahamu nini maana ya mfungo wao. Katika nchi nyingine hasa za Ulaya watu hufunga kula kwa ajili ya kupunguza unene au vitambi “je utauita huo ni mfungo”?. Ombi langu kwetu sote ni kwamba tuishi kwa amani. Tena kila mwenye imani yake azingatie mafundisho ya kweli. Mimi kama Mkrissto nawatakia “mfungo mwema” ndugu zangu Waislamu – msisahau kuwakumbuka maskini wakati wa kufturu na ibada.

 5. Dada stela, sio hali ya kawaida hiyo, kwani mfungo unazuia nini wengine wasile, nini maana ya mfungo yabidi watu tujiulize, je unalazimishwa? na kama sio kwanini haya yankuwa hivi na nchi yetu haifungamani na dini…Simama kwa nafasi yako mkristo

 6. Wapendwa, shetani hana nguvu ya kutawala, tuna haja ya kumuomba sana Mungu afanye kitu juu ya muungano huu,ili lililo lake na lifanyike kwa amani pasi vita, tunakoelekea wakristo walioko z’bar hawatakuwa huru na wataweza uawa kama hata viongozi wanasapoti udini kwa kiasi hiki, lililo baki ni kuhalalisha tu.Tusimame sana ili Mungu asimamishe lake tena kwa amani.

 7. Thetheeee !
  Jamani mie huwa nikifunga hata ukae mbele yangu na kula sishtuki,kwani naishi kati ya watu tofauti tofauti, na siwezi kumlazimisha mtu kufunga ,Wenzetu wakoje jamani Mungu hapendi kuhukumu

 8. Muungano hapa haupo; tukubali tusikubali. Hivi ni viashiria tu vidogo vidogo vinavyoendelea kujitokeza kuhakikisha kile kilichoasisiwa kinyemela kinatoweka mchana kweupe.
  Hapa ninachokiona ni kwa Watanganyika kuukataa kufumbuka macho na kujitenga na hawa jamaa wenye kuhusudu mila na desturi za waarabu wakati wao ni Waafrika tu.
  Wao wana rais wao, bunge lao, bendera yao, wimbo wa taifa lao, na sasa wanatangaza rasmi dini ya taifa lao. Tunawagang’ania ili iweje? Sisi wakristo tunawathamini sana lakini wao hawatuthamini hata kidogo, ndo maana walichoma makanisa yetu lakini serikali ya CCM ikalifumbia macho.
  AMKA WATANGANYIKA, AMKA WAKRISTO

 9. Haaaa haaa, Wapendwa,

  Mtoto wa mkulima hapa alitaka kukwepa lawama. Anawajua wazanziberi kwamba wangeandamana hadi kieleweke kama angesema tofauti, Hapa Waziri Mkuu alikuwa anajiosha tu.

  Ukweli ulivyo ni kwamba Zanzibar ni dola huru lililokosa tu uwakilishi kimataifa kwa kukosa bendera katika Umoja wa Mataifa. Lakini ukweli ulivyo Zanziba ni dola la kiislam linalosubiri siku moja kujitangazia uhuru wake toka Bara au Tanganyika.

  Ukiwa Zanzibar kwa mwezi huu wote huruhusiwi kula chakula mchana hata kama wewe siyo Muislam. Kwa nini? Huku ni kulazimishana kufuata matakwa ya dini usiyoitaka. Kama siyo dola la Kiislam kwa nini serikali ya CCM kule zanziba ilazimishe watu kushinda njaa kisa eti 99% ya wakazi wake ni waislam? Huu ni ujinga wa ajabu.

  Hivi ukienda mji kama Tanga, au Bagamoyo au Lindi ambako zaidi ya 80% ni waislam, utawalazimisha watu woooooote ikiwa ni pamoja na wageni kutoka nje washinde njaa kisa eti wakazi wa hapo ni waislam kwa wingi? Ajabu sana.

  Zanziba hata kama ina wakazi wengi waislam busara ya kawaida ingependekeza kwamba kwa wageni wanaoitembelea Zanziba na hata wale wasiokuwa waislam waishio visiwani humo wasikatazwe kula chakula mchana. Hii ni haki yao. Kuwazuia kula mchana ni kuwatesa. Eti mpaka mtu ajifiche ndo ale chakula? Nchi gani hiii? Maajabu. Kwani wasio waislam wakionekana wanakula wewe ambaye ni muislam inakupunguzia nini?

  Mbona huku Tanzania bara waislam wanawaona watu wanakula na hawapungukiwi jambo? Zanziba inakuwaje tofauti wakati Katiba yake siyo ya Kiislam? Muislam ukimuona asiyekuwa muislam anakula mchana wewe inakuuma? Au inakuwaje? Huu ni utumwa wa kidini kama siyo wa mawazo na fikra.

  Wazanzibari tufunguke tusiwe watumwa wa dini. Kwani asiyekuwa mwisla akila chakula mchana mimi muislam inanipunguzia nini? Hebu tuifanye Zanziba yetu iwe ya amanai na utulivu na tusiicomplicate saaaaana. Huwezi kulazimisha kila mtu awe muislam.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s