Je, Kutumia dawa za kienyeji ukiwa Mkristo ni dhambi? Kwa nini?

Natamani kupata mjadala wenye kuweza kuleta majibu ya maandiko na mitazamo ya wengi kwani siku hizi kuna wimbi kubwa la watu kugeukia dawa za kienyeji zaidi kuliko zile zinazotolewa na hospitali za kawaida.

Wapo wachungaji wanaopiga marufuku waumini wao wasithubutu hata kidogo kutumia dawa za kienyeji na wakati huo huo kuna wengine wanasema kwamba hakuna tatizo wala siyo dhambi?

WAPENDWA TUMWAMINI NANI? JE, KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI? KWA NINI ?

Natanguliza shukrani, na mbarikiwe.

Mr. Milinga

Mada nyingine kuhusu madawa ya kienyeji tuliwahi kujadili hapa

https://strictlygospel.wordpress.com/2008/09/15/mwinjilisti-anayetibu-kwa-kutumia-tiba-asilia/

https://strictlygospel.wordpress.com/2009/08/31/dawa-za-mitishamba/

https://strictlygospel.wordpress.com/2011/03/08/ndoto-ya-dawa-ya-mugagira-imetoka-kwa-mungu-au-mizimu/

15 thoughts on “Je, Kutumia dawa za kienyeji ukiwa Mkristo ni dhambi? Kwa nini?

 1. MUNGU NDIYE ALITUMIA, KATIKA EDENI NA ATATUMIA MIMEA KAMA TIBA KATIKA NCHI MPYA.

  Ufunuo 22::2
  “na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao, matunda aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.”

 2. Yesu tusaidie maana Neno lako linasema watu wako ambao ni sisi tunaangamizwa kwa kukosa maarifa.
  Yesu tunaomba maarifa yatokayo kwako wala sio Elimu zetu FORMAL EDUCATION balii tuongozwe na ROHO MTAKATIFU katika jambo hilii.
  Ayubu 5: 3-4.
  Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi lakini mara niliyalaani maskani yake,Watoto wake wapo mbali na wokovu Nao wamesongwa langoni wala hapana atakayewaponya.
  kama mtu yupo chini ya ROHO MTAKATIFU hawezi kuitumaini mizizi.
  Yesu atubariki…Ameni.

 3. jamani, ningewaomba munapotiya comment zenu zisiwe zinatoka hakilini mwenu bali nukuweni kwenye biblia. Hatuna haja ya mawazo zenu bali tunahaja ya maandiko kutoka Biblia. Ukisema siyo zambi wala ni zambi, weka hata vesi ya biblia ambayo ina support hiyo unasema. Siyo kusema tu kama siyo zambi wala ni zambi nahauoneshe unayatowa wapi mawazo hayo

 4. KUTUMIA DAWA ZA MITI SHAMBA NI DHAMBI PIA DAWA ZA HOSPITALI PIA NI DHAMBI WANAOENDA HOSPITALI NI WATU WASIO IMANI KWANI KWA YESU YOTE YANAWEZEKANA IWE HOMA ,ULEMAMU MAGONJWA YASIYO DAWA KAMA UKIMWI/KANSA.KISUKALI,NGUVU ZA GIZA KWA YESU YANAWEZEKANA KWA MAOMBI TU

 5. Jaman mi naona lenda ameeleza vizuri sana hapo juu na mafungu ya biblia nimeyafatilia yanoeleza vizuri sana.

  Kutokana na mafungu hayo mimi nasema ya kwamba ni RUKSA kutumia dawa za miti shamba. Lakini ipo condition ya kutotumia kwa masharti ya kishetani mfano labda unaambiwa ukavywe huku umeangalia aidha dirishani au kaskazini hiyo siyo.

 6. Unajuaje kama hiyo miti huyo mganga ameipata kwa njia gani? je unajua kama akioteshwa mti huu ni dawa huyo huwa ni ibilisi,na wewe unakunywa tu.

 7. Kutumia dawa za miti sio dhambi. Tatizo ni nani aliyekuambia kuwa huo mti ni dawa. Watu wengi wanaochimba mizizi kama dawa uwezo huo wa kuoteshwa wanapewa na yule mwovu. Kuhusu dawa za hospitalini ni Mungu kwa kuwatumia binadamu aliwapa uwezo wa kugundua dawa hizo kwa njia za ksayansi na wanatoa maelezo jinsi dawa hizo zilivyogunduliwa na zinzvyofanya kazi. Tofauti na dawa zetu za mitishamba ambazo hata kuichota ni lazima ichotwe na mhusika mwenyewe la sivyo haifanyi kazi. Hapo mwana wa Mungu lazima ujue kuna nguvu inayofanya kazi na sio ule mmea.

  Yesu atubariki.

 8. WAPENDWA TUMWAMINI NANI? JE, KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI? KWA NINI ?
  Hili ndilo swali kama lilivyoletwa na mwenye kuuliza.
  Kwa jibu langu kutokana na swali hila nasema kutumia dawa za kienyeji (miti shamba k.v muarobaini,mzugwa, mdalasini nk) kwangu si dhambi.
  Nikienda mbele kidogo kuna mambo ambayo yanahitajika kufahamika hapa nayo ni: “kuaguliwa na kutibiwa”

  “Kuaguliwa” ni pale mtu abashiriwapo mambo yatakayompata hapo baadaye au kupigiwa ramli, na kisha kupewa dawa hiyo; kama matumizi ya dawa hiyo ya kienyeji umeipata kwa “uaguzi” basi kwa Mkristo ni kumkosea Mungu na hii ni dhambi.

  “Kutibiwa” ni pale mtu anapopewa dawa au kufanyiwa matibabu au kugangwa ili apone maradhi yaliyompata. Tiba hii hutolewa na Mganga (Daktari) au Mganga atumiaye miti shamba yaani dawa zitokanazo na mimea, udongo, maji, nk. bila ya ramli hapa si dhambi.
  Tukumbuke ya kwamba dawa zote zinatokana na mimea, maji na madini (chemicals)
  Wapendwa tumwamini nani? Tumwamini Mungu!

 9. Jamani HATA hizi dawa za hospitali zimetengenezwa kwa mizizi,majani,matunda,kama unakunywa dawa za miti shamba kwa ajili ya ugonjwa fulani bila kunuiza si dhambi,sio kutoa mikosi mvuto wa mapenzi hiyo ni dhambi kuubwa ,kwani yesu pekee ndio jibu wa kuondoa mikosi,na roho mtakatifu akituongoza,Amina.

 10. Kwa kweli nionavyo mimi, kama unapewa labda mzizi huu chemsha unywe maji yake utapona ugonjwa ulionao si dhambi, shida ni pale unapopewa mzizi fulani kuutumia kwa masharti kama maneno ya kunuiza au kujivukiza na kusema maneno pale ndo kwenye kujiungamanisha na mapepo haitakiwi ndo dhambi.

 11. HAPA KUNA VITU VIWILI VINACHANGANYWA

  kuna waganga wa kienyeji ambao huchanganya mitishamba na mapepo
  mfano kurudisha mapenzi. ———Hii ni Hatari usiguse

  Na kuna wataalamu wa matumizi ya mimea asilimia—–Matunda, majani, mizizi—hakuna shida

  Dawa za Mapenzi—Kwa kuwa ndoa ni takatifu ukimwendea mtu mwenye moja ya anavyotibia ni mapenzi umepotea-Yesu ndio jibu tu. utakuwa Umepewa pepo likusaidie

  Dawa za Kukuza biashara—umepotea utakuwa umepewa pepo likusaidie

  Dawa ya Kuondoa mkosi kama kibao kinavyoonyesha hapo juu–ni mapepo ni Yesu anayetutakatifuza –

  YESU NI JIBU LA

  KUTUPA WACHUMBA
  KURUDISHA WAKE WALIPOTEA
  KUTUFUNDISHA YAJAYO KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU
  KUTUONDOLEA MIKOSI

  MISTARI YA BIBLIA

  “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto , wala asionekane mtu atazamye bao, wala mtu aatazamaye nyakati mabaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11. wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo,wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. ” KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-12

  2 mambo ya nyakati 33:6
  Mika 5:12

  watu aambao hatupaswi kuwaendea ni hao niliotaja awali ambao nguvu zao hutoka upande wa
  shetani. vibao vyao vitakutambulisha na kazi zao zitakutambulisha.

  Tahadhari wapo ambao hutoa dawa za kawaida miti asilia lakini huwa wameziombea kwa miungu yao. Au anapokupa anaombea kimoyomoyo wakupulizia pumzi kutoka midomoni mwa mfano wabudha.—–waepuke!!!!

  MISTARI INAYORUHUSU MIMEA ASILIA NA SIO KWA AJILI YA—- MAPENZI,MIKOSI N.K

  Na karibu na mto, juu ya ukingo wake,upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake ahayatanyauka……matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa. Ezekiel 47:12
  Zaburi 17:22
  Isaya 38:21
  Luka 10:34aya
  jeremiah 46:11
  Isaya 1:6
  2 wafalme 2:20-22
  2 wafalme 20:5-8

  Mungu akuwezeshe kuelewa.Amina

 12. Wapendwa,

  Nimejaribu kupitia michango ya watu wengine iliyowahi kutolewa huko nyuma wakati wa Babu wa Loliondo alipovuma kama baragumu mwaka jana. Hata hivyo, nimekuta wengi walioshiriki kutoa mawazo yao hawakujadili muktadha huu wa sasa. Swali hili nimelileta kwenu wapendwa ili kupata michango ya watu wapya zaidi kwenye blog hii kwani hata mimi wakati ule sikushiriki kwenye mijadala yote iliyorushwa hewani na blog hii.

  Hoja ninazo zitarajia kwenye mada hii kwa wakati huu ni katika kutoa majibu yanayokata kiu pande mbili zinazokinzana kuhusu utumiaji wa dawa za kienyeji au za asili au mitishamba kwa mkristo. Sitarajii watu kujadili mada hii kwa kurejea kazi zifanywazo na Wapiga ramli, sangoma, wasomaji wa nyota, albadili, utabiri wa nyota, na wengine kama hao.

  Nategemea wachangiaji wa mada wawe wenye kujikita katika hoja zenye kuliweka kanisa sawa badala ya kulitawanya. Natazamia wapendwa wenye uelewa wa maandiko na sayansi watusaidie ujuzi wao zaidi hata kama waliwahi kutoa maoni yao kwenye mada zilizopita mwaka jana, nawaomba hapa wachangie kwa kutazama au kutoke kona nyingine.

 13. Mpendwa, Lwembe

  Naomba uache utani tuwapo kazini. Hapa we are doing a serious business. We need people in heavens of God.

  Kama unaweza kutusaidia hoja tatu au tano hivi utakuwa umetusaidia sana. Kanisani ninakosali mimi hadi sasa tuna mkanganyiko. Wapendwa wengi hawajui wafuate uelekeo upi?

  Labda nikuhakikishie tu kwamba hata kama ningeenda kwa Babu (bahati nzuri au mbaya sikwenda) bado hoja za maandiko zinatakiwa zitumike kwa nini usitumie dawa za kienyeji kutibu ugonjwa ulionao.

  Lwembe acha utani kazini. Come on with Biblical supporting arguements on this matter. I am serious ooh. Aiseeeeee, tafadhali sana.

  Wapendwa mnisaidie ili nami niweze kusaidia wapendwa wengi kanisani kwangu ninaposali. Natamani kupata michango ya wengi zaidi.

 14. Mtafiti wangu Milinga,

  Au ulikunywa KKKT (Kunywa Kikombe Kimoja Tu)??? Si unajua kuwa huyo Babu wa Samunge ni Nabii!!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s