Masanja Mkandamizaji atoa tahadhari!

Mchekeshaji maarufu Tanzania ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili Masanja au kwa jina jingine Mchungaji mtarajiwa, ametoa tahadhari kwa wanaombeza kuigiza wakati yeye Mungu hajamwambia kuacha. 

Msanii huyo ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na mtangazaji maarufu Millard Ayo kutoka radio moja ya kijamii. Hata hivyo hapo kabla Masanja aliwahi kunukuliwa kwamba ipo siku atakuwa mchungaji pia ataacha uigizaji Mungu atakaposema naye. 

Mbali na hayo amewatangazia wanaouza CD feki kwamba “nimemaliza kufanya album yangu ya Gospel najua wako watu mamasta wa kuburn kazi za waimbaji nimewakaribisha waburn hii yangu, yani hamna kesi hashikwi mtu atakaeburn kazi yangu kwa sababu hii ni huduma ukiburn wauzie watu hata mia mia usiziweke ndani”

Kwenye sentensi nyingine Mchekeshaji huyu wa Orijino Komedi ya TBC1 amesema “kuna watu wananiambia Masanja tumeona watu wanauza CD feki nasema kama na wewe unaweza nunua na  ukatengeneze zako kwa sababu hii ni huduma nataka watu wapate ujumbe huu wabadilike wamjue Yesu tunaemuhubiri mwanawane”

Sikiliza wimbo mzuri wa Masanja Mkandamizaji – Hakuna jipya ambao umebeba jina la Album, iko tayari!

Source: Millard Ayo

49 thoughts on “Masanja Mkandamizaji atoa tahadhari!

 1. Rose! Rose! Rose!
  Nasikitishwa na kuogoga jinsi ya wapendwa wengine mnavyokuwa bold ( nitafsirie kwa kiswahili, Halina uzito kama kwa kiingereza) yaani una ujasiri bila kuwa na uhakika wa msingi wa huo ujasiri ni hatari. biblia inasema ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke.
  Napenda kumquate martin Luther, alliyeulizwa ukienda mbinguni utashangaa vitu gani, akajibu ntashangaa mambo makubwa matatu. 1. kutowakuta wale niliodhania nitawakuta huku (mbinguni) wale ambao wako bold wanaodhania wao ni wema sana kuliko wengine na wengine wote ni wachafu na wadhambi, asipowakuta atashanga. 2. kuwakuta wale ambao hakutegemea kuwakuta, wale unaodhania hawa ni motoni moja kwa moja, akiwakuta atashangaa, maana mungu ni mwema na anasemehe, na uhusiano wa mungu ni personal wewe na mungu wako, so sio rahisi kumjua mtu amesimama wapi na mungu, maana watu wanatofautiana personalities, ulisikia ni nani alimzika Yesu, ( ni mwanafunzi wa sitri, kama ulikuwa hujui, ) 3. atakachoshangaa Martin Luther ni kujikuta yeye mwenyewe mbinguni, pamoja anajua hashitakiwi nafsini mwake kwa yale anayoyatenda na uhusiano wake na mungu, lakini anakiri ni neema tu, ndio itakayomuingza mbinmguni.
  hivyo watu wanaosema kwa ujasiri masanja na mwenzio blah blah, you should be very careful on such kind of comments, unaweza kulikaribisha jaribu utakalolishindwa, kuwa mnyenyekevu
  Gretel

 2. Hello Mr. Kinyau
  Kuna vitu vingi umesema ambavyo nisengependa kuvirudia na kuvitolea maelezo, bali niendelee moja kwa moja kwenye hoja ya msingi- Masanja.

  Lengo la kuuliza hayo maswali ambayo mnadhani kuwa majibu yake ni obvious ni haya;

  Mimi naamini kuigiza sio dhambi
  Naamini Masanja kumwimbia kwake Mungu hafanyi mizaha
  Mimi naamini Masanja ameamua kweli kuokoka
  Naamini “style” ya utumishi wake sio mizaha bali ana maanisha

  Unless u prove me otherwise Mr. Kinyau. Na kunithibitishia vinginevyo ndio kujibu hayo maswali niliyouliza.

  Ndio maana bungeni ukiomba mwongozo lazima uisome kanuni unayosimamia hata kama imesomwa tena na tena na tena. Mlitakiwa kujibu maswali yangu Kinyau,si kusema majibu yake ni obvious. Majibu yenu na yangu yawezekana ni tofauti kabisa, na inaweza ikawa ndio sababu ya kuendelea kutofautiana kwetu katika hili.

  Kwa mujibu wa 2 Tim 4:2 uliyoinukuu pale mwishoni imesema “kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri”. Hata kama hayo ambayo Masanja anayafanya yangekuwa ni makosa, sioni uvumilivu wenu bwana Kinyau katika kumkemea kwenu. Mtu huyu ambaye wengi wenu mmemsema kuwa hana siku nyingi tangu ameokoka mnamkemea na kumhukumu bila hata chembe ya uvumilivu wowote.

  Tuweni waangalifu, wokovu ni kwa neema.

  Kama kuendelea kwake kufanya sanaa ya maigizo Original comedy kunaliudhi kanisa, basi aliyemwita atamwambia aache hiyo kazi kwa wakati wake.

  Kazi ya kuigiza si dhambi Kinyau, ndio maana sio waliookoka wote hawabarikiwi na Masanja kama ambavyo wewe hubarikiwi naye. Na wala kutofurahishwa kwako na yeye sio dhambi kwako pia.

  Mimi huwa sifurahii kabisa namna kwaya zetu nyingi zinavyoimba na kucheza,
  Lakini siwezi kusema kuwa ni makosa kwa kwaya hizo kuimba na kucheza hivyo, ati kwa sababu tu mimi sibarikiwi.

  Thank u!

 3. Rose Rose Rose!
  Kwanza niseme tu kwamba ni kweli wale vijana walimdhihaki Elisha, ni kweli wale wakosaji msalabani walimdhihaki Yesu pale msalabani. Bila shaka mifano hii inakufanya ujue nini maana ya kudhihaki.
  Hao waliodhihaki wote katika hii mifano miwili walikuwa hawaigizi bali walimaanisha kabisa kumwambia Yesu kuwa alijifanya anaponya wengine mbona na yeye yamempata kama kweli ana uwezo?. Walikuwa wanajaribu kusema kuwa Yesu hana uwezo – Dhihaka!

  Steve Nyerere huwa anaiga sauti ya Nyerere – Je hiyo ni kumdhihaki Mwalimu Nyerere eh?

  Ok, Masanja niliwahi kumwona anaongea kama mchungaji mama Rwakatare – Je huko ndiko kudhihaki unakokusema?

  Kuna watu kwa utani huongea kama mzee Moses Kulola “yoooo” au kama Sauti ya mzee Kakobe – Kumbe hao nao huwadhihaki hao watumishi wa Mungu eh?

  Je kumwambia Yesu jiokoe maana uliokoa wengine kwa kumaanisha ni sawa na kuongea kama mama Rwakatare kwa kuigiza?

  Soma vizuri ulichokisema kuhusu Paulo. Hebu angalia Matendo 9:19-20 uone kama Paulo alikaa miaka miwili kama unavyosema. Unachokisema wewe ni Paulo kuanza huduma kwa watu wa mataifa, lakini kwa wayahudi alianza siku chache tu baada ya kuokoka.

  Rose baada ya Masanja kuokoka ni lini amesimama na kudhihaki tena Injili kama unavyosema?

  Tumeshaeleza nini maana ya mzaha,lakini naona unaendelea kusema Masanja anafanya mzaha. Unaweza kusema ni mzaha gani huo anafanya?

  Sio kusema kuwa kwa upande wako:

  Kuchekesha- ni kufanya mzaha
  Kutania – Ni kufanya mzaha
  Kuigiza – Ni kufanaya mzaha

  Kwa maana hiyo usingependa kumwona kabisa Masanja anafanya uigizaji. Ndio maana ilikuwa ni muhimu sana kujibu hayo maswali yangu.

  Unamjua comrade Chavala? Think about it!

  Ndio maana kama ni hivyo inabidi pia useme kuwa senema ya Yesu ni mzaha na dhihaka kubwa wala hatupaswi kuitazama kabisa. Unasemaje kuhusu hiyo Rose?

  Unaposema anachofanya hakina tofauti na alichofanya Simon mchawi, unanionesha ni jinsi gani huogopi kumkosea Mungu kwa kuhukumu wengine. Maana anachofanya Masanja hakilingani kabisa na cha Simon mchawi.

  Simon mchawi alitaka apewe Roho mt. ili akamtumie kupata pesa maana ile nguvu ndani ya Petro yeye aliona kuwa ni deal la kuendelea kutengeneza mshiko zaidi.

  Masanja yeye kasema hata cd yake wanaodurufu waidurufu kwa wingi ili watu wengi wapate habari njema,yeye hatawashitaki, wewe unaendelea kumhukumu tu kwamba anataka umaarufu!

  What is wrong to be famous by doing right? Was Jesus not famous?

  Ok, go ahead Rose, judge him!!

  May God have mercy!!!

 4. I’m sick the way the church in africa is still naive..! full of religious zealots who are good at cramming and quoting verses from the bible, while they fail to make a sensible clarification out of the same verses. they are here represented by brother samuel and fellows. their base of concern is more on phariseeic judgementalism that comes from the law. super spiritual and holier than even jesus himself. keep on men..! try even more harder!

 5. Ndugu Sungura,

  Maswali uliyouliza yalishajibiwa sana na wachngiaji wengi kwenye blog hii hapo kwanza tulipokuwa tunajadili mada inayofanana na hii kumhusu Masanja, mimi sioni sababu ya kukujibu maswali hayo. Halafu lazima ujue kwamba mtu kunyamaza kujibu maswali yako haina maana kwamba wewe uliyeuliza maswali hayo ndo uko right kuhusu mada inayoendelea. Unaweza kuuliza maswali, kama alivyosema Rosemary, ambayo yapo too obvious kiasi kwamba tukaendelea kukushangaa tu badala ya kukujibu.

  Hebu nirudi kwenye mchango wako wa tar.6/8/2012, ulioniomba nili-relax. Let me assure you mr. Sungura, I have no tension at all!! I’m so much relaxed, ila naona wewe labda umenielewa vibaya. Sijawahi kuwa na tension wakati wote nitoapo machapisho yangu ndani ya blog hii, na kwa kweli sitakuwa na tension kamwe kwa sababu najifunza sana kutoka kwenye machapisho ya watu wengine ndani ya blog hii. Kama na mimi kuna wanaojifunza au kupata kitu cha kutuwezesha kupiga vita vizuri vya imani, namrudishia Mungu sifa na utukufu. Ninajua hatari ya kuchangia chochote humo ukiwa na tension maana utaishia kuchangia kimwili zaidi badala ya kuongozwa na Roho.

  Hebu ona ulivyoandika kwenye chapisho kuhusu kukemea dhambi;

  “Waumini hawaachi dhambi kwa kukemewa, wanatakiwa kufundishwa wapate maarifa ambayo yatawafanya wajue siri za Mungu na hapo wataweza kuipinga dhambi kwa hayo maarifa kwa msaada wa Roho mt. Ukijikita kwenye kuwakemea tu bila kuwapa maarifa/kuwafundisha hawataacha dhambi, na matokeo yake watarudi nyuma tu”

  Sasa hebu soma Mtume Paulo alimwandikia nini Timotheo kwenye 2 Timotheo 4:2;

  “Uhubiri Neno, uwe tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, KARIPIA, KEMEA, na KUONYA kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri”

  Kwa hiyo upo wakati wa kufundisha na upo wakati wa kukemea na kukaripia na kuonya, kama ingekuwa ni kufundisha tu, basi mtume Paulo asingeongozwa na Roho Mtakatifu kumwandikia mtoto wake wa kiroho kufanya hayo! Yesu mwenyewe aliwahi kumkemea Petro hata akafika mahali pa kumwita ‘shetani wewe’ sembuse sisi kwa nini watumishi wasikemee dhambi?

  Umeeleza habari za yule kahaba aliyempaka Yesu mafuta katika kuhalalisha kuwa Yesu hakuwa anawakemea wenye dhambi, hiyo ni kweli kabisa hakumkemea kahaba yule, lakini hebu nionyeshe kwenye maandiko mwenye dhambi aliyekuwa anaenda kwa Yesu na akarudi na dhambi zake zaidi ya yule kijana tajiri aliyeambiwa auze mali zake awape masikini? Na kijana huyu aliikosa neema hiyo kwa ugumu wa moyo wake tu!

  Kitu muhimu tunachokipata kwa huyu kahaba ni kwamba, kwanza alizingatia moyoni mwake kwamba yeye ni mwenye dhambi na hakuwa na namna ya kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi bila kwenda kwa Yesu na kusamehewa dhambi zake. kwa hiyo alipokuwa anaenda kwa Yesu alikuwa kahaba, mwenye dhambi nyingi, lakini alipotoka kwa Yesu hakuwa kahaba tena bali alikuwa kiumbe kipya ndani ya Yesu Kristo (2 Korintho 5:17), aliyekuwa amesamehewa dhambi zake na akiwa na badiliko kubwa na mtizamo mwingine kabisa wa maisha yake.

  Sasa hebu ndugu Sungura niambie, ni wangapi leo tunaoenda au tunaoingia kwenye mahema yetu kila siku tukiwa na mizigo iliyotulemea ya dhambi na tunatoka tukiwa wepesi bila mzigo wowote kama yule kahaba? tena tunaingia kwenye mahema tukisema Mungu yupo hapa, lakini mbona hatukutani naye ili atubadilishe kama alivyombadilisha Sauli? Je hatufundishwi kila siku? Je, ni lini tutapata hayo maarifa ili tuweze kutua dhambi zetu msalabani?

  Wengi wetu tunaenda kwenye mahema yetu kwa mazoea na wengine kwa kuogopa zaidi taratibu za mahema hayo, mojawapo ikiwa ni la kutokuzikwa au kutopewa huduma na viongozi wa mahema hayo baada ya kufa kwa kuwa tu ulikuwa huendi kwenye hema husika, lakini ukitafuta badiliko la kweli la mtu au watu hao hulioni ng’o!!

  Hilo ndilo linalonisumbua mimi kuhusu Masanja. Hebu fikiri pamoja na mimi, yule kahaba aliyesamehewa dhambi zake na Yesu, kisha baada ya kutoka hapo ukamkuta tena kwenye mitaa ya Ohio, amevaa mavazi yake hayo hayo ya kikahaba, anawaita wateja wake na kuwaambia ‘Bwana Yesu asifiwe, mwenzenu nimekutana na Yesu tena nimempaka mafuta yenye harufu nzuri na amenisamehe dhambi zangu’ (kumbuka wakati huo labda ni saa sita usiku), wewe utasema huyo anahubiri injili ya wokovu?

  Mimi nimeshaweka msimamo wangu wazi kwako kwamba sibarikiwe na comedy za Masanja na wala sibarikiwi hata na uimbaji wake wa kicomedy comedy wala hayo mahubiri yake ya kicomedy pia, pamoja na kwamba anamtaja Yesu. Kwenye ile mada nyingine ambayo tuliijadili kuhusu Masanja, iliwekwa clip ya mahubiri yake naomba yasikilize ndg yangu Sungura halafu uniambie kama hayo mahubiri sio ya kicomedy comedy!

  Mwisho kabisa, nasema sioni sababu ya kujibu maswali yako kwa kuwa msimamo wangu nimeuweka wazi mbele yako.

  Endelea kubarikiwa na Bwana.

 6. Shalom ndg Sungura
  sikutaka kujibu hayo maswali maana niliona kama vile majibu ni too obvious na nilishindwa kuelewa kwanini wewe unashindwa kuliona hilo
  naomba tu nikupe mifano ujue kwanini Masanja ni issue hapa
  1. Masanja na wenzie walijijengea jina kwa kudhihaki watu, na dhihaka hii ilikuwa hata ktk watumishi wa Mungu wanavyohubiri na wanavyoombea watu, hii ni kejeli sio kwa hao watumishi ila kwa Mungu wanayemtumikia na tedno lao halitofautiani na wale vijana waliomwambia Elisha paa wewe mwenye upaa! nadhani unajua Mungu aliwafanya nini, ni sawa na wale waliomwambia Yesu msalabani uliokoa wengi jiokoe nafsi yako sasa! Mungu hadhihakiwi, na hii inawafanya watumishi sio kitu na Mungu wanayemtumikia pia. Kwa kifupi Masanja na kundi lake wanaharibu kazi ya Mungu na si kuujenga ufalme wa Mungu.
  2. Kila mtu alifurahi aliposikia Masanja ameokoka, lakini tatizo ni mtumishi anayemlea kutomwambia wazi kuwa alikuwa anakosea na anapaswa kugeuka, pili Masanja mwenyewe anatakiwa kumaanisha kile anachosema kuhusu kuokoka, huwezi kuokoka ukaendelea na mizaha anayoifanya, mbaya zaidi Injili sio kitu cha mizaha, tatu utumishi unataka mtu aliyejitoa hasa kwa Mungu na sio kutaka huku na kule. Utumishi ni kumtumikia Mungu na sio kutumika na shetani kuwapotosha watu kuhusu injili, kama wewe ulikuwa unasimama majukwaani na kudhihaki injili huwezi kusimama tena udhihaki na useme ninahubiri! Anachofanya hakina tofauti na Simoni mchawi ambaye alipoona jinsi Petro anavyofanya miujiza kupitia Yesu alitaka auziwe ili na yeye afanyie biashara, tatizo la watumishi wa sasa ni njaa na wanshindwa kuwakemea kama alivyofanya Petro. Kuna mtu anasema Paulo hakukaa kujifunza neno sio kweli. Soma Matendo ya mitume, Paulo alirudishwa kukaa na watumishi chini ya kanisa miaka miwili hadi walipofunga na kuomba na kisha kuonyeshwa wamwachie sasa yeye na Barnaba wakatumike kwa mataifa. Hawa wasanii wameonyeshwa na nani kutumika? Mbarikiwe nyote.

 7. Imani kuna maneno fulani umeyasema katika mchango wako hapo juu, nanukuu “Tuzidi kumuombea Masanja na wote walio na kiu ya kumtumikia Mungu awajaze Roho Mtakatifu wakapate kuijua kweli zaidi, hekima ya Mungu na nguvu ili waweze kutenda kazi yake kama alivyowatuma”

  Maneno ya namna hiyo yenye kujaa neema namna hiyo ndio ulitakiwa kuyasema tangu mwanzo, kuliko ulivyokuwa unamshambulia Masanja na kumhukumu.

  Wewe umeshindwa kujibu hayo maswali, nafikiri ni kwa sababu huna majibu yake sahihi.
  Nashukuru, ngoja nimsubiri ndg yangu Kinyau labda yeye atayajibu,maana nilimwomba ayajibu pia.

  Mnapojadili kitu ni vizuri kufikia hitimisho, na moja ya hitimisho inaweza ikawa kukubaliana kutokukubaliana, nalo ni hitimisho. Hamwezi kujadili kitu milele.

  Thank !!!

 8. Barikiwa sana kaka Sungura,

  Pole sana kwa masikitiko hayo, sikuwa najua kuwa unanihitaji kutoa hitimisho la mjadala huu….Nafikiri sio jukumu langu kusitisha mjadala wakati wengine wangeweza kuchangia.

  JIBU LA MASWALI YAKO KWA UJUMLA

  ‘Tuzidi kumuombea Masanja na wote walio na kiu ya kumtumikia Mungu awajaze Roho Mtakatifu wakapate kuijua kweli zaidi, hekima ya Mungu na nguvu ili waweze kutenda kazi yake kama alivyowatuma.

  – Mungu azidi kutulinda wote tusimame vizuri katika wokovu na kuwa mashahidi wa Yesu……..tuzidi kutamani kumjua na kumpendeza daima siku zote za maisha yetu

  1WATHESALONIKE 2;4-6

  Tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, Yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. Kama mjuavyo na Mungu akiwa shahidi yetu hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli kwa ajili ya kuficha tamaa mbaya. Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, si kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote.

  Mbarikiwe

  Dada Imani K

 9. Sawa dada Imani.

  Lakini nasikitika kuwa umeacha mambo ya msingi ukajibu ambalo si la msingi sana.

  Naomba unijibu maswali niliyokuuliza tafadhali ili yamkini tuweze kufikia hitimisho bora la mjadala huu.

  Barikiwa!

 10. Kuzaa ni messy! Kwanza kunatanguliwa na Uchungu, kisha mifuko inapasuka, maji yanamwagika, halafu damu, na ndipo uhai, yaani mtoto anapatikana!

  Nasi Kristo alipotuzaa kiroho, alitangulia ktk Uchungu, “kwa kupigwa kwake sisi tulipona”, akawambwa mtini. Kisha akachomwa mkuki, Maji yakamwagika na Damu ikafuata, hata nasi kuzaliwa!

  Nimewaona wengi waliokiri wokovu kwa kuongozwa sala ya toba na kukaririshwa kifungu cha Rum 10:9 out of context! Nadhani kuzaliwa huku ni kule kwa operation, hawakusukuma mtoto!!

  Mtu anapozaliwa mara ya pili, huwa hapatoshi! Mzunguko wake wote huwa panachimbika!!! Mapepo ya dini huwa hayamuachilii mtu kirahisi aende kwa Kristo!

  Basi huenda Masanja yuko ktk hatua ya UCHUNGU, hata tunamuona akiiachilia kazi yake inakiliwe na wezi badala ya kuwatishia LAANA, maana hao huwa hawaogopi polisi! Basi wapendwa tumpeni nafasi Mungu amtimizie hizo hatua zilizobaki, mtashangaa atakapopangiwa kazi ya ualimu wa Sunday School!!!

  Mbarikiwe nyoote, ninyi mlio ktk kiu ya WOKOVU!!

 11. Mie mzima sana kaka Sungura….Nakusalimia sana sana katika jina la Yesu,

  Yes nimeumbwa kuwa shabiki…sababu ni balozi wa Yesu…Balozi yeyote siku zote anashabikia na kuiagilia nchi aliyotumwa kuiwakilisha……..

  Wala sina wasi wasi wa kuchelewa kuiva au kupitwa na Masanja…..Maana sigombei uchungaji…

  Na hata kama angeniita kuwa mchungaji……hata kama angehitaji niive ndani ya miaka 10 wala sina shida….hata angefanya ndani ya lisaa sina mashaka pia….

  SO HATA MIE NAMUOMBEA AIVE MAPEMA NA HARAKA SANA ILI ACHUNGE KONDOO WA MUNGU IPASAVYO….

  Barikiwa sana mpendwa Sungura

  Dada Imani

 12. Hello Mr. Kinyau relax brother!

  Mimi sijakushangaa ila nilisema “mimi sishangai wewe kushangazwa na comment zangu”. Hukusoma vizuri!

  Sijakushangaa kwa sababu wakristo wengi kwa sababu ya mapokeo wako na mtazamo kama wa kwako, hata mimi nilikuwa hivyo kabla sijajifunza. Ndio maana nimekushauri usome kitabu cha WHAT’S SO AMAZING ABOUT GRACE.
  Waumini hawaachi dhambi kwa kukemewa, wanatakiwa kufundishwa wapate maarifa ambayo yatawafanya wajue siri za Mungu na hapo wataweza kuipinga dhambi kwa hayo maarifa kwa msaada wa Roho mt. Ukijikita kwenye kuwakemea tu bila kuwapa maarifa/kuwafundisha hawataacha dhambi, na matokeo yake watarudi nyuma tu.

  Yesu hakuwa anakemea watu wenye udhaifu wa dhambi waliokuwa wanamfuata bali aliwafundisha na kuwaelekeza kwa upendo. Hebu kumbuka jinsi yule kahaba alivyomwendea Yesu akiwa katika hali ileile ya mavazi ya ukahaba, waliokuwa pamoja na Yesu walichukizwa kwa sababu alipoingia tu walitambua kuwa ni kahaba ,na manukato ya thamani aliyokuwa nayo bila shaka aliyapata hukohuko kwenye ukahaba. Lakini Yesu anamruhusu abusu miguu yake na kumfuta kwa nywele zake. “What a wonderful savior!!

  Bila shaka wengi wetu tungekuwepo tusingependa kabisa hata amfanyie Bwana hiyo ibada,kama tunavyochukizwa leo na watu kama Masanja kutumika katika madhabahu ya Mungu.

  Kama Masanja ana udhaifu, Mungu aliyemwokoa atamkamilisha awe kama atakavyo yeye ( Mungu). Kwa nini Joti na wengine wao hawajaokoka kama yeye, wao hawataki huo umaarufu tunaodhani anautafuta?

  Yeye karuhusu watu wadurufu kazi zake waziuze hata kwa miamia ili ujumbe wa Mungu uwafikie watu. Nani mwingine kafanya hivyo? hata mimi bila shaka siwezi.Kasema ataacha kazi ya kuigiza Mungu atakapomwambia kuacha.

  Kinyau hata wewe bila shaka una/ulikuwa na udhaifu fulani, lakini bado unamtumikia Mungu. Siku moja huo udhaifu utaisha. Nani kaokoka ambaye hajawahi kutenda dhambi jamani? Tunapokosea na kutenda dhambi haina maana kuwa hatujaokoka bali tuko njiani kuelekea utimilifu wa Kristo.

  Siko hapa kutetea dhambi wala udhaifu katika kanisa, not at all!. Narudia tena kusema, kama Masanja kuna dhambi anaendelea nazo simtii moyo katika hayo, anatakiwa aziache. Lakini kwa habari ya utumishi anaofanya namtia moyo asonge mbele. Kama anafanya kwa ajili ya kutafuta umaarufu anajua mwenyewe, kama anatania anajua mwenyewe,kama hajaokoka kwa kumaanisha anajua mwenyewe, wala si kazi yangu mimi.Kwa nia ya tumbo au kwa nia ya kweli injili inahubiriwa.

  Kinyau be more specific, niambie dhambi ya Masanja ni ipi. Naomba urejee maswali niliyomuuliza dada Imani hapo juu.

  Halaf nijibu swali kuhusu picha ya Yesu, nayo ni mzaha? maana ni ya kuigiza.

  Thank u!!

 13. What’s up Imani!!!
  Sidhani kama Yesu anahitaji mashabiki!

  Kwanza napenda kusema kuwa Masanja hajasema kuwa yeye ni mchungaji bali anajiita mchungaji mtarajiwa. Kujiita mtarajiwa maana yake ni kwamba yuko kweye mchakato(process) wa kuwa mchungaji. Kuna vitu bado anajifunza yawezekana ataenda kwanza hata Bible school au vyovyote mpaka atakapokuwa fit.

  Ni vema pia kabla kuandika chochote tusome tena nukuu ya kile alichosema mwenyewe.

  Pili; naona tunahubiriana sana bila kujikita sana katika hoja ya msingi. Ningeshauri twende hivi:

  Niambie nini hasa dhambi/kosa la Masanja maana tunamjadili yeye;

  1. Je ni kuendelea kuigiza original commedy wakati ameokoka?
  2.Ni kuokoka na kuanza kufanya huduma(uimbaji) ndani ya muda mfupi?
  3.Ni kujiita mchungaji mtarajiwa?
  4.Ni ile hali ya ufanyaji wake huduma ambayo inafanana kama anaigiza vile?
  5.Au kama si miongoni mwa hayo niliyotaja, naomba utaje?

  Imani, Masanja anaweza kuiva ndani ya muda mfupi sana akakuacha wewe bado unaendelea kusubiri kuiva, inategemeana na bidii ya mtu!

  Naomba unijibu swali langu la chapisho lililopita: wewe uliacha kila kitu siku moja tu baada ya kuokoka?

  Bless u!

 14. Nimevutiwa na kujikuta nafikiria kwa makini maoni ya msemaji wa kwanza kuhusu Masanja kuacha kuchekesha, kwamba ujumbe wake hautakuwa na uzito kwa vile umekuja kwa njia ya kicheko. na kunukuu Biblia kuwa Yesu alikuwa mtu wa sikitiko……… nakubali hilo, lakini sisi ni wafuasi wa Kristo, hatutaweza kwa jinsi moja au nyingine kuwa carbon copy ya Yesu, yeye alikuwa mwana wa mungu, na sisi ni binadamu kamili, Yesu mwenyewe alisema duniani mnayo dhiki, lakini jipeni moyo…………. Watu waliokwisha kuokoka, nadhani hawangependa kusikia neno la mungu kwa Comedy (mie mmojawapo) lakini unasemaje kwa wale ambao ni watoto wadogo kiroho ambao hawajaukulia wokovu? (Paulo anasema wao bado wanahitaji maziwa, sio chakula kizito) huoni kwamba comedians wanaweza kuwavuta kwa Yesu, na wakishavutika wapewe dona na maharage ili wapate afya?
  Siku moja nilipita mitaa ya kiswahili huko Dodoma (Chadulu) kwenye klabu za pombe za kienyeji, na nikasikia mwimbo maarufu wa injili ukipigwa kwa nguvu mno na walevi wakiimba kama hakuna kesho, kwanza nilishtuka, nikajiuliza na nikajijibu mwenyewe, injili ya Yesu inahubiriwa kwa vyovyote vile, kwa ucheshi, kwa userious, kwa kilio na maombolezo, kwa walevi, katika misikiti na makanisa, asije mtu akasema hakulisikia hilo neno.
  So Bravo Masanja, piga injili, kila mtu asikie.
  Ila wewe pia usije ukawaleta wenzio kwa Kristo nawe ukabaki nje. Muombe roho Mtakatifu akufundishe zaidi
  Gretel

 15. Ndg Kinyau,
  Umeeleza mengi sana, umejitahidi sana kuigombea Injili, ubarikiwe kwa hilo!

  Lakini napenda kukukumbusha uhalisia wa mambo. Kwamba baada ya hayo yote uliyoyasema, ambayo nawe wayajua kuwa si mapya, bali umeyarejea Maandiko, hata kumfikia mt Paulo, kuyasisitiza aliyoyafundisha, kimsingi hayo hayakuwa ya mwilini bali ya rohoni, ambapo hata leo hii, hayo aliyoyakemea mt. Paulo yangali yanatendeka kwa ushawishi wa roho zile zile zilizokuwa juu ya Wakorinto au Wagalatia nk. Basi ni vizuri ukajituliza kidogo kisha ukayatazama hayo yanayotokea ili uyaangalie yalipo katika Maandiko, na hilo likakupa mwanga na nguvu zaidi juu yake.

  Tazama ulichosema: “Neno la Mungu linapohubiriwa bila uongozi wa Roho Mtakatifu linakuwa halina nguvu ya Mungu na hivyo haliwezi kuchoma watu mioyo yao (Yeremia 23:26). Na hilo limetokana na watu kujibandika uchungaji n.k. bila kuitwa na Mchungaji Mkuu wa Kondoo ambaye ni Yesu (Yeremia 23:21-22).” Mimi binafsi, ninaanza kwa kukiamini hiki nilichokunukuu. Hapo nimekuelewa kuwa wapo wachungaji ambao hawajaitwa, na kama hujaitwa hautakuwa na waraka unaokuongoza katika hilo ambalo unapaswa kuwa umetumwa kulifanya. Kwa hiyo roho iliyokusukumiza kwenye hiyo kazi itakupa waraka wake ambao utakuwa ni tofauti na ule halisi.

  Basi katika hilo ni dhahiri kuwa utahubiri kinyume na Neno, ukilikana Neno na kuwalisha kondoo chakula cha mbwa! Ndio hawa kondoo walio dhoofu kiroho na sasa wanaendelea katika dhihaka za walimu wao, wakiidhalilisha Injili ktk namna ambayo haielezeki! Wanazidi kuongezeka juu ya sura ya nchi Maandiko yakitimia, 2Pet 3:3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, “ Angalia trend ilivyo, “Jamani mi nataka kuwa mchungaji sasa, mnaonaje washikaji?’ hiyo ndio tamaa yao, uchungaji, wamezaliwa wapi na mbegu hiyo? Kwenye hizo injili zinazohubiriwa pasi uongozi wa Roho Mt!!! Na madhabahu zenyewe ndio mzaha na Dhihaka Mama!

  Jichungeni nyie mnaoongozwa na tamaa zenu, angalieni yaliyomfika mfalme Uzia enzi za nabii Isaya, hakuna kilichobadilika, wengi wa wachungaji na manabii na mitume na maaskofu wana ukoma wa kiroho kwa kurukia kazi kwa tamaa zao, kama nawe unataka kujiunga nao, haya we, ila Yesu haponyi tena wakoma wa jinsi hiyo, MWAFWAA!!!

  Habari ndo hiyo!

 16. Papa papa papa papa, ndugu yangu Kinyau, hayo ni makofi, ebu jamani mtu akilisha chakula cha kiroho tumwambie asante, siyo kwamba tunamsifu, japo Paul alisema ajisifu kidogo japo haipendezi, pia hii itaendelea kumweka katika msitari ya kwamba siku akiharibu na tukamwambia, atakubaliana, maana alipofanya vizuri tulimwambia. Masage hiyo ungeihubiri kanisa nikiwemo ningesimama, nikaruka ruka, nikamshukuru Mungu. Asante Kanyau. Barikiwa..

 17. Sungura,

  Endelea kunishangaa na endelea pia kumtia moyo Masanja aendelee na hayo macomedy yake siku ya Alhamisi kwenye luninga na Jumapili au siku nyingine yoyote asimame madhabahuni kukuhubiria injili ya Yesu kicomedy comedy hivyo hivyo. Na kwa sababu wengi wanamshabikia kama wewe, basi atapata wengi wa wokovu wa staili yake! Utamtoaje mtu kibanzi jichoni mwake wakati wewe una boriti kwenye macho yako yote mawili? Wengi watasema kuwa nina hukumu, hapana, hili ni angalizo tu, toa kwanza kibanzi kwenye jicho lako ndipo upate kuona vizuri boriti liliopo kwenye jicho la mtu mwingine! Wakati mwingine mara utoapo kibanzi kwenye jicho lako ndipo huweza kuona vizuri kwamba kwenye jicho la mwenzako hakuna boriti wala kibanzi!

  Ndugu Sungura, kwa vile Wakorintho walikuwa walevi na wazinzi wakubwa, unataka kuniambia basi wachungaji wa leo wakae kimya tu bila kukemea dhambi hiyo? Ndio sababu Mtume Paulo akalikemea hilo na leo wewe unasoma na kuelewa kwamba walikuwa wanazini mpaka na wake wa baba zao; Je Paulo ange-compromise nao ungelijua hilo leo? Kwa Paulo kuliandika hilo maana yake tulikemee kwa nguvu zetu zote ili kanisa lla leo ibaki kuwa takatifu kama alivyo Yeye ambaye ni kichwa cha hilo kanisa. Umeliandika hili la Wakorintho as if lilikuwa jambo jema na hivyo Paulo hakuwafukuza!! Kwenye mahema hatufukuzani badala yake tunaonyana kwa neno la Mungu ili litupe badiliko la kweli na kuyaona ya ‘dunia’ si kitu kama walivyoeleza wachangiaji wengine hapo juu.

  Kama ungesoma kwa makini chapisho langu ungeona kwamba hakuna mahali popote niliposema waumini hao wafukuzwe kama wewe ulivyo-conclude. Mimi nilisema wakemewe ili hatimaye waweze kuacha, lakini wachungaji wengi hawakemei kwa kuogopa waumini hao watayahama mahema yao na hivyo watakosa sadaka kwa sababu ni wachungaji wa mishahara!!! Na hilo umelisema mwenyewe kwamba uchungaji ni kazi kama kazi ya uhasibu n.k. Kwangu mimi naona hapo ndipo tatizo linapoanzia pale wachungaji na sisi waumini tunapoona uchungaji ni kazi kama kazi ya umakenika n.k.Hivi tujiulize makanika anachunga roho za watu? Labda Sungura atajibu kwa kutengeneza gari linalopandwa na wapendwa tayari amechunga roho zao! Nasema labda, kwa kweli mimi sijui kama ndio maana ya uchungaji unaotajwa kwenye maandiko ya Mungu!!

  Na kwa sababu hiyo wanaendelea kuhubiri Injili vuguvugu isiyochoma mioyo ya watu kwa kuwa wanafanya kazi iliyo sawa na ya umakenika! Mtume Petro alipohubiri siku ile ya Pentekoste kwenye Matendo sura ya pili,(Matendo 2:14-40), mahubiri hayo au Injili hiyo iliwachoma watu mioyo yao na wakabadilika! Ni wachungaji wangapi leo wanaposimama kuhubiri kwenye mahema yao, mahubiri hayo yanapenya kwenye mioyo ya waumini wao kiasi kwamba wale walioingia na mizigo ya dhambi wanaitua msalabani? Waumini wangapi leo wanaingia na kutoka kwenye mahema yao kila siku bila badiliko la kweli?

  Neno la Mungu linapohubiriwa bila uongozi wa Roho Mtakatifu linakuwa halina nguvu ya Mungu na hivyo haliwezi kuchoma watu mioyo yao (Yeremia 23:26). Na hilo limetokana na watu kujibandika uchungaji n.k. bila kuitwa na Mchungaji Mkuu wa Kondoo ambaye ni Yesu (Yeremia 23:21-22).

  Tutaendelea kubishana na kupeana mistari hapa, lakini yote katika yote wokovu wetu unatakiwa kuonekana katika matendo ambayo hayo ndio Yesu alisema tutawajua kwa matunda yao. Matunda yanayosemwa hapa si wingi wa watu wanaovutwa au wanaowashabikia wachungaji kama akina Masanja, bali matendo yao kwanza yaonyeshe kweli Yesu amewaokoa!!

  Hakuna hata mtu mmoja hapa asiyefurahia tangazo la kuokoka kwa Masanja kwa sababu hata malaika mbinguni wamefurahi na kushangilia kama kweli Masanja ameokoka, lakini tunajiuliza toba gani isiyombadilisha mtu? Kama Mtume Paulo angesimama na kusema Yesu amenitokea wakati naenda Dameski na kuniokoa, lakini akaendelea kutesa wakristo na kusimamia sheria kama hapo mwanzo, je kweli Mungu angemtumia kwa kiasi hicho alichotumika?

  Tumuombee Masanja katika hili, lakini pia tusifunge mlango wa kumuonya na kumshauri kwamba wokovu si maigizo wala si kitu cha mzaha mzaha. Leo unasimama mahali unafanya maigizo ya mizaha mizaha, kesho unasimama unahubiri Injili ya Yesu. Labda Sungura huoni hili kama tatizo kwa sababu kwenye hema lako mchungaji wako naye hufanya maigizo kama ya akina Masanja na kisha huendelea na kuchapa Injili!. Naweza kuonekana kama namshambulia Masanja, lakini from my innerheart, sibarikiwi na comedy za akina Masanja, it is my opinion, si lazima wewe Sungura ukubaliane na msimamo wangu. Lakini tukumbuke kwamba kila neno au tendo tulifanyalo katika uhai wetu hapa duniani tutalitolea hesabu yake mbele ya Mungu. Wakolosai 3:17 ikazidi kutuambia;

  “Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika Yeye”

  Mstari huu umekuwa check and balance kwangu kwa kila kitu ninachotaka au takiwa kukifanya!

  Ubarikiwe.

 18. Amina sana kaka Samuel;

  Mungu atusaidie kukua kiroho kila siku na kusimama imara sawa na kile Mungu ametuitia…….

  Hata mimi siwezi kukubali watu wanisifie au kwa nijiite mchungaji wakati najijua kabisa bado sijajitoa 100% kumtumikia Yesu….au bado napenda sn sifa za wanadamu….Nitaendelea kusubiri sana mpaka niive vzr.

  2 Wak; 5;15
  Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili Yake Yeye aliyekufa na kufufuka tena kwa ajili yao.

  Zabiri 1;1
  Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu,Wala hafuati njia ya wenye dhambi
  au kukaa katika baraza la wenye mizaha.

  Watu wanajiita majina kirahisi rahisi sababu hawajui gharama zake….Mwisho wa siku wanaishia kuwa wababaishaji…hawana misimamo sababu ‘Wanataka kuwapendeza wanadamu (ambako wanapata sifa nyingi kirahisi) ….na ‘kumpendeza Mungu’ (ambapo hakunaga sifa kirahisi). Inasaidia nini uwachekeshe watu, wakufurahie weeeee halafu huna msaada kiroho kwao?

  -Hii sisemi kwa Masanja tu…..ni kwangu mwenyewe na wote ambao tunatamani kumtumkia Mungu wakati tupo ‘HALF COOKED’……..’Tamaa na umaarufu wa Duniani bado vinatupelekesha’

  -Binafsi siwafurahii sana watu wanaonisifia bali wanaonionya na kunisaidia kusimama vzr na Mungu kila siku….Sifa za mwanadamu zinaweza kukuangamiza na kukufanya kipofu ushindwe kufanyia kazi maeneo ambayo haupo sawa.

  Mbarikiwe
  Imani Kapinga

 19. Dada Imani Shaloom, ebu niongeze kitu ktk mchango wako, Lililotukuka kwa wanadamu hilo kwa Mungu ni chukizo, pia kila anayejisifu ajisifu kuwa ananijua mimi asema Bwana. Wako watu wanajisifia vitu vya dunia hii, vitu gani? Pesa, magari, majumba, elimu, umaarifu ( wa dunia híi) ndio maana Daud aliwashangaa, akasema hivi.. HAWA WANATAJA MAGARI, HAWA WANATAJA MAFARASI..Mimi nitalitaja Jina la Bwana. Hapo ndipo panaleta shida siku zetu, ndio maana akawafundisha Wakorintho hivi..Angalieni ndugu zangu kwamba siyo wengi wenye elimu walioitwa, sio wengi wenye cheo walioitwa bali Mungu aliyachagua mambo mapumbaù ya dunia awaaibishe wenye hekima, tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu, tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia, ili aviaibishe vyenye nguvu.

  Tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyo dharauliwa ( na dunia, siyo vinavyosifiwa na dunia) na vilivyo dharauliwa, naam vitu ambavyo haviko, ili aviaibishe vile vilivyoko, mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. ( kama atamwita Mtu na umaarufu wake, anyoshe nao, dunia inampenda, inamshangilia, inamsifu, huyo ni wa dunia hii, na dunia inapita, na mambo yake) Yesu wetu hakuwa maarufu kidunia. Wengine wakamwambia ameyapata wapi haya, ambaye hakusoma? Wakamwambia Petro pia, hawakusoma, mmoja akawapa jibu…Walikuwa na Yesu. Dada Imani, mchango huu nimeungezea kwenye mchango wako ili tuendelee kujifunza, Mungu aendelee kutufungua macho ya rohoni tuone vya rohoni, vya mwilini Paul alivita HASARA, MAVI. Mbarikiwe.

 20. Ha, ha, ha, ha, kaka Sungura Mungu akubariki sana.

  Umenifurahisha sana, IMANI ndo jina langu na litasimama kama lilivyokusudiwa.

  ‘KAMWE HUWEZI KUTOA KITU AMBACHO HUNA’ ni lazima Mungu akuandae kwanza…especialy kama Mungu anataka uwe mtumishi mkubwa ‘Hawezi ruhusu uwe half cooked ili ukasababishe confussion’…….Kwa matunda yao utawatambua………!!!!

  Mtu huwezi kujiita mchungaji wala kuitwa mchungaji mpaka mtu yeye mwenyewe akarabatiwe kwanza na kuandaliwa. Mungu ana wivu sana na watu wake hawezi kuruhusu waongozwe na watu ambao wao wenyewe hawawezi kujiongoza………!!!!

  Nnachomuombea Masanja kuwa, kama kweli anakiu ya kumtumikia Mungu akubali kujifunza na kumtafuta Mungu kwanza….aachane na tamaa za dunia na kutafuta umaarufu usio na faida mbele za Mungu……!!!!

  Una weza kujiona maarufu sana kwa kuwa wanadamu wanakusifia (tena wale wa dunia)…LAKINI ;;;ni SIFURI…kama Mungu hakuoni hivyo…HUWEZI TUMIKIA MABWANA WAWILI

  Paulo alikuwa maarufu wa dunia kwanza (kwa kuitimiza sheria na kuijua vzr)……lakini ilibidi aupoteze umaarufu wa kidunia kwanza na sifa zote….ili aanze kuwa maarufu kwa ajili ya Yesu

  Ndo maana alisema hv
  Wafilipi 3

  Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyangalinisha na faida kubwa ipitayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu, ambaye kwa ajili Yake nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo, 9nami nionekane mbele Zake nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani

  -Sungura usijidanganye na wala sitadanganyika……Kamwe sitashabikia watu…namshabikia Yesu na kweli yake siku zote………..

  Mbarikiwe

  Dada Imani

 21. Hebu ona mchango wa dada Imani hapo juu. Yeye amekosa imani (kama lilivyo lake jina) ya kumfanya akubali kuwa Masanja ameokoka, kwa sababu tu post zake kwenye face book ni kufagilia mambo ya kidunia.

  Ni kweli yawezekana bado anafagilia hayo mambo,lakini kama kweli moyoni mwake huyu jamaa amekusudia kumpenda Yesu kufanya hivyo haina maana kuwa hajaokoka, ila ni udhaifu tu na utoto wa kumjua Mungu ambao kadri anavyojifunza atazidi kuacha. Petro pamoja na kuwa mtume mkuu alikuwa na udhaifu wa kufanya ubaguzi kati ya waongofu wa kiyahudi na kiyunani mpaka siku moja Paul akamwambia sio sawa kufanya hivyo akaacha.

  Si dhani kama Masanja angeweza kuamua kuokoka kwa ajili ya kutafuta umaarufu, alikuwa maarufu tayari, na kila mtu katika nchi hii alikuwa anamfahamu.

  Imani wewe uliacha kila kitu siku moja tu baada ya kuokoka?

  Kinyau mimi sishangai wewe kushangazwa na comment zangu.

  Vipi kama ungepewa kuchunga kanisa la Wakorintho, ambao hawakuishia kunywa tu pombe na kulewa bali wengine walitembea hata na wake wa baba zao, si ungewafukuza wote warudi dhambini kabisa?

  Kinyau nanukuu hii sentensi yako “hivi wanapojifanya wao wanawake wakati ni wanaume, Sungura anaita kitu gani hicho?” Mimi hicho naita ni maigizo wala si mzaha ndg Kinyau.

  Vipi jamaa aliyejifanya kuwa ni Yesu katika kinachoitwa Picha ya Yesu,j wewe huwa unaangalia hiyo picha?

  Kinyau kuigiza kuwa mwanamke wala si sawa na kujibadilisha kuwa mwanamke. Original commedy hawajawahi kuwa wanawake hata siku moja.

  Nafikiri nimeeleza sana nini maana ya mzaha wala sihitaji kurudia.

  Pia nataka uniambie kuwa kwako maigizo ni dhambi, nitakuelewa.
  Kama Masanja bado analewa na pombe abadilike,kama bado anchukua mademu abadilike, kama bado anatukana na kuongea matusi abadilike, kama bado anasema uongo abadilike, n.k.

  Lakini kama mnachosema ninyi abadilike ni kuacha kazi yake ya kuigiza, basi hamjui mnachosema,au kama mnajua basi hakiko sahihi. kuigiza wala kuchekesha si dhambi.

  Ila kama siku moja Masanja atakuwa anahubiri kiuhalisia halafu akapanda jukwaani amevaa kike, huo utakuwa mzaha sasa!

  Watu wengi naona hamuelewi nini maana ya neema, na kama mnajua mnajua juu juu tu.

  Kinyau wewe nafikiri ni mtu msomi, tafuta kitabu kinaitwa “WHAT’S SO AMAZING ABOUT GRACE” cha Philip Yencey utagundua kitu cha ajabu sana

  Mimi nafikiri neema ya Kristo iko juu yake,tumwombee aimarike!

 22. Rose now u talk!!

  Huu mchango wako hata Masanja akiusoma kama kweli bado ana njia ambazo si sahihi anaweza akaguswa na kuamua kuacha. Ni maneno ambayo yamejaa neema kwa anayeyasoma. Hayana kuhukumu ndani yake.

  Kama umekuwa unafuatilia vizuri tunachochangia ktk hoja hii, utagundua kuwa ninapinga sana mtu kusema vile Masanja anavyoimba ni kufanya mzaha. Ndio maana niliamua hata kueleza maana ya mzaha.

  Katika vile anavyoimba na kumfuata Kristo mimi sijaona kitu chochote ambacho amekosea kiasi niseme kuwa hajaokoka na anafanya mizaha kama ambavyo wengi wamekuwa wakichangia.

  Kuna sentensi umesema nimeipenda maana ni ya ndani sana (” kipimo chetu ni Yesu hata kama hatuwi kamili lakini hatutakiwi kufurahia kutokamilika kwetu isipokuwa kukaza mwendo kuifikia hiyo ahadi”)

  Kuokoka kunatokana kumkiri Yesu na kuamini moyoni,ndiko Masanja alikofanya. Lakini kuufikia ukamilifu kunatokana kumjifunza Mungu siku baada ya siku, naamini hata yeye anajifunza siku baada ya siku.

  Ukiangalia michango ya wapendwa wengi ni kulaumu na kuhukumu tu. Hata kukemea lazima iwe kwa upendo na hekima, kuliko na nia ya kujenga wala si kubomoa.

  Lakini Rose kuhusu kutamani makomamanga ya Misri, bila shaka kwa habari ya Masanja unamaanisha kule kuendelea kwake kuchekesha original commedy. Acha niseme hivi, kama katika huko kuchekesha kuna mambo ambayo ni dhambi au hayakubaliki kibiblia huwa wanafanya, basi namshauri au tumshauri ajiepushe na hayo. Lakini suala zima la kuendelea na hiyo kazi si dhambi Rose, wala sio sahihi kuifananisha na makomamanga ya Misri kwa Wayahudi.

  Mimi naamini Masanja kaokoka, nitahuzunika sana kama atarudi nyuma.

  Tumtie moyo!

 23. Wapendwa,

  Naona wengi wetu tumetatizika na jambo hili la Masanja kuwa Mchungaji. Nadhani kufahamika kwake sana ktk fani ya uigizaji ndio kisababishi kikuu cha kutatizika kwetu. Hata hivyo, ni vizuri tukawa wakweli kwa nafsi zetu kwanza, kabla hatujadai kuwa chini ya Uongozi wa Roho Mt ktk michango yetu tunayoitoa ktk namna ya ‘kuwatuliza’ wanaotubishia!

  Kwanza hebu tuulizane; hivi hawa wachungaji wetu wote tulionao huko kwenye mahema yetu, au mapadri wetu na maaskofu wetu, tunawajua tangu utoto wao au ujana wao? Je, tunazo historia zao, labda zinazowaonesha kuwa walipofika umri wa miaka 9 kuwa walienda porini kama Yohana Mbatizaji, na waliporudi ndio wakawa wachungaji? Au walikosa C za kutosha kuwafanya waingie kozi za Udaktari ndio wakachagua kwenda vyuo vya teologia na sasa wamepewa huo uchungaji kwa elimu yao hiyo na sio Wito kama wanavyotudanganya?

  Uchungaji ni kazi tu kama uhasibu au umakanika, na zaidi sana ni sawa na nafasi za kisiasa ambazo baadaye kulingana na merit, ktk mfumo wa dhehebu lenu, mtumishi hupandishwa cheo, na nafasi ya juu hugombewa kwa kura; kama umewahi kusikia wachungaji wanakwenda kwa sangoma, basi mara nyingi huwa ni kwenye kugombea nafasi hizo za juu! Sio muanze kuniuliza maswali, nimesema “ukisikia”, kama nilivyosikia mimi!!

  Sema wakiisha kuwa wachungaji hapo ndio habari za Roho Mt huwa haziwaishi midomoni, kama yule mch Njoroge wa Kenya! Sasa ktk hili sisemi kuwa ni wachungaji wote, la hasha, ila wa jinsi hiyo wamo wengi tu kati ya makundi ya wachungaji!

  Ninachopenda ndg zangu muelewe ni kwamba, Masanja kuwa mchungaji si jambo la ajabu au kituko kama mnavyotaka kulifanya. Na hilo sharti la kwamba awe “Ameokoka” nadhani hili ndilo kituko zaidi kuliko huo uchungaji anaoutaka! Hivi wapendwa mpaka leo hamjajua kuwa “Walokole” ni target ya vipepo vyote vya Uongo, au mawindo ya ndege wote walao mizoga?? Yaani ukitaka kula pesa za walokole, jifanye umeokoka na ndugu zako wamekutenga, halafu Nena kwa Lugha fasta, wanakukubali na utapewa huduma zote mpaka pocket money!!

  Ushauri wangu kwa Masanja “mwanawane”, nenda chuo cha Teolojia, angalia usiende Roma, utazeekea chuoni! Nenda cha makanisa baridi, yaani makongwe, lakini unaweza ku score A+ au B kwenye masomo yote nane, zinacharge kweli mwanawane?? Ila huko nako wanaweza kukupeleka Nkasi, utaweza kweli na wewe umeshazoea masifa ya mijini?

  Basi, achana na hayo NENDA kwenye chuo cha manabii cha makanisa ya KIROHO, huko Beth el au Yeriko (2Waf. 2:3,5), huko mwanawane kang’ang’anie somo la MIUJIZA, sio lazima ufaulu, wewe mradi tu uelewe, ukirudi uraiani unafungua Huduma ya “Mwanawane Ministries International” chini ya Apostle & Prophet Masanja ‘Mkandamizaji’!!! Ukianzisha tu vipawa vinakumwagikia, utashangaa siku nitakapokuja uniombee baraka za kamradi kangu katiki nami ninunue Hummer kama lako, ila ninapokutubia makosa yangu ya kukuponda kwenye mtandao, ulipotangaza kuanza Uchungaji, please usinifukuze!

  LAKINI, yote hayo 9, kumi usijaribu kuukimbilia Uchungaji mwanawane bila kumsikia mwenye kazi yake kukuita! Na akikuita Yeye, NI LAZIMA AKUPITISHE KATIKA NJIA YA MITUME, yaani atakapokuita, atakuhesabia Haki, kisha Atakutakasa na mwisho atakujaza Roho wake ili akuongoze katika utakayoyafundisha yasiyofautiane hata kwa nukta na waliyoyafundisha Mitume! Kama ni Ubatizo, basi ni LAZIMA uwe wa maji mengi, kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili upate Ondoleo la dhambi, uwe msafi hilo hekalu ndipo Roho Mt aje akae humo ndani yako au ndani ya hao utakao wahubiria hiyo Habari Njema!

  Ukikurupuka mwanawane na kaubatizo ka maji ya kifuu cha nazi, au sijui kwa jina la nani na la nani na la nanihii, ukaja ukafundisha tofauti na mitume, mwanawane, hao watakaokufuata na tumuujiza twako kama huto twa komedi unazocheza, UNALAANIWA fasta, kama Gal 1:8 inavyosema! Hapo sasa kule nanihii ndio itakuwa Ze Komedi ya ki kweli kweli, hakuna kulia huko, ni Kicheko na Kusaga Meno tu, wanasema kama ulikuwa kibogoyo, UNAPEWA MENO SUPA!!!

  Karibu Madhabahuni!

 24. Rosemary, Dada Imani, Samuel na wengine wote,

  Jina la Bwana litukuzwe kwa ujasiri wenu wa kutoighoshi Injili, na siku zote Injili isiyoghoshiwa hupingwa sana maana siku hizi watu wanapenda ‘injili’ ya kupaka mafuta na kutokuambiana ukweli. Mchungaji anajua kabisa waumini wake ni walevi na wazinzi wakubwa n.k, lakini humsikii hata siku moja akiwakemea waumini hao kwa sababu ya kuogopa kukosa sadaka zao. Hili ndilo linaloendelea hata kwenye mjadala huu. Comment za Sungura zinanishangaza hasa anaposema kwamba Masanja na kundi lake hawafanyi mizaha, hivi wanapojifanya wao wanawake wakati ni wanaume, Sungura anaita kitu gani hicho?

  Mada hii ya Masanja tulishaiongea tena kipindi kilichopita, na wengi wetu tulisema wazi kama Masanja ameamua kwa dhati Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, basi abadilike maana hakuna toba isiyobadilisha, toba lazima iwe na direction kwa maana ya kukubadilisha kule ulikokuwa unaelekea mwanzo na kumgeukia Yesu. Na sio hilo tu lazima mabadiliko hayo yaonekane kwenye matendo. Ona neno linavyosema kwenye Matendo 26:20, “…….kwamba inawapasa kutubu na kumgeukia Mungu NA KUTHIBITISHA TOBA YAO KWA MATENDO YAO”.
  Hakuna sababu ya Masanja kusema ameokoka wakati hakuna badiliko lolote ukilinganisha na alivyokuwa kabla ya kusema ameokoka.

  Barikiweni na Bwana.

 25. asante sana mchungaji mtarajiwa nakuunga mkono zaidi nazidi kukutia moyo katika huduma yako kwani unamzigo mzito sana songa mbele zaidi na zaidi usigeuke kulia wala kushoto mungu akubariki sana. wabeja

 26. Shalom wapendwa
  ndg Sungura naona mtu akichangia kuhusu hawa wasanii unagomba tusiwahukumu
  ni sawa wokovu na utakatifu wa mtu anayejua ni Mungu kwani ni kwa neema yake tu wote tumeokoka sio kwa usafi wetu wala matendo yetu. Lakini tukiisha okoka wote tunapaswa kufanana naye, kipimo chetu ni Yesu hata kama hatuwi kamili lakini hatutakiwi kufurahia kutokamilika kwetu isipokuwa kukaza mwendo kuifikia hiyo ahadi. Hakuna kurudi wala kutazama nyuma ilikuwaje, hakuna kutamani makomamanga na nyama za Misri tunayo Mana ndio neno inatosha, tunaye yule aliyeangikwa msalabani tunamtazama Yeye anatosha.
  Ni safari ambayo tuliambiwa wazi tunatakiwa kujikana nadhani unaelewa maana yake na sio ku blend na mazingira ili tufanane nayo, ni kujikana na kuipoteza nafsi yako, kuuvua utu wa kale. Kinachoshangaza ni kukuta huyu mtu ambaye bado anabeba vyote vya kale anahubiri…. atahubiri nini? si ule utu wake wa kale si yale yale ya duniani… na kibaya zaidi hata wangeficha ktk verse na maneno yao “injili” bado matendo yao yanaudhihirisha ule utu wao wa kale waziwazi sasa ktk hali kama hii mpendwa ulitaka tukae kimya? Sisi tunakemea ili wasiangamie na wasiende na wengine wanaotaka ku blend ukristo na mengineyo, wanaotaka kuwa vuguvugu.
  Iko siku utagundua hivi unavyotetea umepoteza roho ngapi na hutakuwa na uwezo wa kuzirudisha, mimi nitasema kile kilicho kweli sawa na neno wacha wachukie na watakaosikia Mungu awabariki.

 27. Nna mashaka kama Masanja ameokoka……

  Ukiangalia hata post zake kwa facebook ni kufagilia mambo ya kidunia……pombe e.t.c halafu watu wanamfurahia kweeeeli…Hasa watu wa dunia. Tusidanganyike watu wanajitafutia umaarufu tu hakuna lolote ‘TUJICHUNGUZE’

  Mbarikiwe
  Tujichunguze

 28. Sam, unaandika sana pasipo kujibu hoja za msingi.Naomba usome hoja zilizoandikwa na maswali uliyoulizwa ili katika kujibu atoe ufafanuzi wa uliyoulizwa na yaliyoandikwa. Kun vitu vingi ambavyo ndo msingi wa mada hii nimejaribu kuvielezea kwa undani kidogo eg maana ya mzaha na wakati upi mtu hufanya jambo likwa ni mzaha, nk.

  Lakini bwana Sama hujajibu kwa kuyazingatia hayo badala yake umeendelea kusema vitu vingine viiingi vya kujitetea na kujilinda tu. Ni vizuri kujua kanuni za mijadala kama hii ili kufikia hitimisho zuri.

  Sijajaribu kukuzuia kutoa mchango wako Sam,ila tunachoangalia hapa ni kwa kiasi gani hoja anazotoa mtu ni sahihi au si sahihi. Kutoa maoni ni uhuru wako hakuna wa kukuzuia.

  Mimi nimesema kuwa anachokifanya Masanja kanisani si mzaha na wala anachokifanya akiwa original commedy si mzaha vilevile. Nafikiri nilieleza vizuri jana maana ya mzaha.Ningependa kama ungethibitisha kwa hoja ni namna gani hicho anachofanya Masanja ni mzaha.

  Sam kwa mfano ni mafundisho gani ya uongo ambayo unadhani tunayashabikia hapa au ni hadithi gani za uongo ambazo unaona sisi tumezigeukia hapa kama ulivonukuu 2Tim 4:1-4?
  Mimi naona umenukuu maandiko mengi yasiyotoa majibu katika hoja iliyo mezani ila ni kwa ajili ya kujilinda tu wewe na kuzidi kuhukumu wengine.

  Nazidi kusisitiza kuwa hakuna kitu cha ibada ya kweli ambacho naweza kujifunza kwa waislam(kambi nyingine) kama ninyi mnaona kipo kajifunzeni. Kristo ndiye kielelezo chetu kwa kila kitu maana aliishi katika mwili na kupitia yote kama sisi na alifanya ibada ya kweli.

  Rose umegusia habari za Mr. Nice. Hakuna anayejua kuwa Rose Mhando,Mwaitege au mwingine yeyote atasimama na kristo au kurudi nyuma lini.Kurudi nyuma/kumwacha Yesu ni suala la hiari yeyote hata wewe ukiamua kurudi nyuma unarudi tu. Mimi wala sijui kama wewe umeokoka kwa kumaanisha au la, anayejua ni wewe na Mungu

  Hata Masanja,mimi sijui kama kweli kaamua kuokoka kwa dhati au kesho kutwa atarudi nyuma. Ninachoangalia ni usahihi wa kile anachokifanya bila kujali kaokoka jana au ana miaka 10 na kuzidi.

  Mimi sioni kosa lake katika yale anayoyafanya kwenye huduma yake ya uimbaji au kwenye kazi yake ya kuigiza. Hebu ninyi tuambieni ni dhambi gani anafaya katika hayo?

  Tuchambueni mambo wala tusihukumu wa jumla,tene kwa mapokeo tu na kunukuu maandiko wakati mwingine bila kujua hata maana halisi ya asili ya hayo maandiko.

  Amen!!!!

 29. Bora wewe umesema mch Samuel maana tuliongea haya kwa Mr Nice tukabezwa weee na mwisho wake ndio huu, wasanii wakae kwanza chini wajifunze neno, wakae chini ya waalimu na wachungaji wao wachungwe, waulize kusudi lao n akumshirikisha Roho mt ktk huduma zao iwapo wameitwa kweli. Mbona haya madudu hatuyaoni kwa kina Shusho, Mwaitege, Misholi na wengineo? Mnaopinga mtafakari na kujiuliza

 30. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Yoh 15..25 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika Torati yao.WALINICHUKIA BURE. Ndugu yangu Sungura, umesema huoni sababu ya mimi kuwakumbusha habari Lucifer, utakubaliana nami kuwa ndiye chimbuko la Kiburi, kama ndiye chimbuko, kikitajwa kiburi, sharti atajwe pia mwanzilishi wake, yawezekana wewe unajua, je unadhani watu wote wanajua? 11 pt 1.12…13 Kwa hiyo nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa ktk kweli mlio nayo, Nami nao ni haki, maadam nipo ktk maskani híi, kuwaamsha kwa kuwakumbusha. Napenda nimalizie kwa leo hivi, Hakuna mtu aliyekuzuia kutia mtu moyo, kwa njia hiyo hiyo huna ruhusa kumzuia mtu mwingine, kuonya, kukemea kama alivyoagizwa na yeye aliyemwajiri. RUM 12..6…8. Basi kwa kuwa tuna karama zilizombali mbali, kwa kadri ya Neema tuliyopewa, ikiwa unabíi tutoe unabíi kwa kadri ya Imani, ikiwa huduma tuwemo ktk huduma yetu, mwenye kufundisha ktk kufundisha kwake, mwenye kuonya ktk kuonya kwake, mwenye…,,…,. Yote haya yatendeke kwa kipimo cha Neno la Mungu. Mbarikiwe.

 31. Hizi Injili mbali mbali haziwezi kwenda pamoja hata kidogo, Bwana Yesu alipokuwepo duniani, kuna watu walimtembelea, sikia walhvyomwambia. Math 22..16.Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa KWELI, NA NJIA YA MUNGU WAIFUNDISHA KTK KWELI, WALA HUJALI CHEO CHA MTU AWAYE YOTE, KWA MAANA HUTAZAMI SURA ZA WATU.( hii nayo ni injili haiangalii sura ya mtu yeyote, wala hali yake, hawahongeki hawa, hawapendwi hawa. Gal 4..16 Je nimekuwa adui wenu kwa sababu nawambia yaliyo KWELI. ( kumbuka Timotheo alivyoambiwa, watajitenga wasisikie kweli, hawatakubali kukemewa, kukaripiwa, ) ndio maana utaona watu wakiambiwa kweli, WANAHAMA, wanatafuta mahali ambapo hawasemwa, hawatakaripiwa, na ndiyo maana Isaya 9..16 Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao waliongozwa na watu hao wameangamia. Viongozi wengi wamelea watu kama chupa ya chai. Na mithali ya kiswahil…,.

 32. Mw 7.5 Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. Pamoja na hayo yote, ni vizuri tukumbushane kuwa zipo Injili za aina nyingi, paul aliainisha vizuri kabisa. Filp 1..15 Wengine wanamhubiri Kristo kwa sababu ya HUSUDA, FITINA. na wengine kwa NIA NJEMA. Akaendelea kusema. Filp 3..17…19 Ndg zangu mnifuate mimi mkawatazame wao waendao kwa kufuata mfano tuliyowapa ninyi. Maana wengi huenenda ,ambao nimewaambia mara nyingi habari zao, na ss nawambia hata kwa machozi kuwa ni ADUI WA MSALABA WA KRISTO, MWIRHO WAO NI UHARIBIFU, MUNGU WAO NI TUMBO, UTUKUFU WAO U KTK FEDHEHA YAO, WANIAO MAMBO YA DUNIANI. Mst 20 kwa maana ss wenyeji wetu uko Mbinguni. Nimesema ziko injili za aina nyingi, wapo wanaofikiri hivi. 1Tim 6,5 Na majadiliano ya watu walioharibika akili zao walioikosa KWELI, huku wakidhania kuwa utauwa ni NJIA YA KUJIPATIA FAIDA. Ndugu yetu Paul akasema anayahesabu mambo yote kuwa hasara, Filp 3. 8.Naam zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Krsto, nayahesabu mambo yote kuwa kama MAVI. ( sikukopi yote) naonyesha Injili mbali2 zilizopo, wapo watu wanaona vitu vya dunia, magari, majumba, fedha ni MAVI, wapo ambao ndio lengo lao..inaend..

 33. Ndio nikagusisia kuwa kiburi kitamaliza wengi, sisemi kuwa ni waimbaji tu, ni watu wote, awe Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mch. Na Mwalimu, yaani huduma yoyote, Mith 15..12. Mwenye mzaha hapendi hapendi kukaripiwa, wala yeye hawaendei wenye hekima.( ndio nikasema mizaha sio Neno la Mungu, mwenye miyaha hakaripiwi) Mith 9..7…8 Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha, Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu, usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia, Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.( sitaeharau mtu yeyote, hata nitamke kuwa kambi hiyo haina la kunifundisha, maana sijajua bado inavyonipasa kujua) Biblia ina mistari 31,173. Nifikirije kuwa najua yote’? Mith 30..5…6 Kila Neno la Mungu limehakikishwa, yeye ni ngao yao wamwaminio. Usiongeye neno katika Maneno yake, asije akakulaumu, ukaonekana muongo.( hii kusemaje? Kile Biblia imetwambia tufanye hivyo, pale Biblia imenyamaza tunatakiwa kunyamaza. Mw 6.22. Ndivyo alivyofanya Nuhu sawa2 na vyote alivyomwamuru Mungu, ndivyo alivyofanya. Inaendelea……

 34. Bwana Yesu asifiwe ndugu samweli kwa hiyo mnamshauri vipi ndg. Masanja. Angalieni msihukumu tu, pia mnawajibu wa kumwombea ingawa mnasema ni mchanga angalieni asije akawatangulia mkashangaa. Muombeeni msimshambulie kwa maneno maguvu ya maandiko mtakuwa hamjamsaidia swala ni kuwa naye karibu na kumshauri siyo hivi hujaokoa yamkini unaharibu. au muegemezeni kwa Mungu aliye hai yeye hubadilisha watu.

  Yamkini kwa maneno yako usije ukawa ukidhani unajenga kumbe unabomoa. Pia busara, au hekima inatakiwa unapomshauri mtu, mashambulizi hayafai watu wa Mungu. Mshauri au mwite, mwombee au mwombe pamoja Mungu huwa hujibu maombi. Kwa maana hiyo watu wasilisikilize msg zake kwa kuwa anahubiri au asifu katika Roho na kweli wewe unajuaje na unahakika gani kwenye moyo wa Masanja? kama wewe unavyosema.

 35. Ndugu Sungura Shaloom, ebu tuendelee kujifunza, mimi sijui kila kitu, 2 kor 8..2. Mtu akidhani ya kuwa anajua Neno, hajui Neno lolote bado kama impasavyo kujua. Napia najua jinsi Paul alivyomuusia mtoto wake wa kiroho, itakavyokuwa siku za mwisho. 2.Tim 4..1…4 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu waliohai na waliokufa, kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake, lihubiri Neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, KARIPIA, KEMEA, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundirho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundirho yenye uzima, ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasiisikie kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.-( hawatakataa mafundisho, ila YENYE UZIMA, WATAJIEPUSHA WASISIKIE KWELI) YOH 8.32 NANYI MTAIFAHAMU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU. Na kweli ni NENO la Mungu, ambalo watu wataiepuka, hawatakubali kukemewa, kukaripiwa..inaendelea

 36. Ndg Juntwa, nashukuru.

  Kwanza ningekushauri ujue maana ya KUSIFU na maana ya KUABUDU.
  Kwa taarifa yako hakuna kitu unachokifanya ambacho kiko nje ya ibada. Wala kuabudu si kuimba pekee. In fact kuimba ni kielelezo tu cha ibada iliyo ndani ya huyo mtu anaeimba.

  Juntwa hebu jifunzi vizuri Yesu alichomaanisha aliposema kila neno lisilo maana, si kama unavyodhani ndg yangu. Ok, unasema lolote liloovu lisitoke kinywani mwenu,sawa. Masanja kasema ovu gani katika kuigiza kwake?

  Halafu unamaanisha nini unaposema nyimbo zote ziimbwazo pasipo neno la Mungu ni za kuelimisha wala si za kumwabudu Mungu?

  Halafu narudia kusema hata kwako Mary Joshua; kuigiza sio maana yake kufanya mizaha. Kitendo cha akina masanja (original comedy) kufanya vichekesho sio sawa na kufanya mizaha kama mnavyodhani. Nafikiri hujawahi kuwaona wakiwa wanashuti huwa wako serious kiasi cha kukasirishana. Kwa kiswahili kingine ni kwamba ukiwa mtu wa mizaha hata wao hawatakubali ufanye nao kazi maana kazi wanayofanya ni serious na wanahitaji mtu serious.

  Neno mzaha maana yake kwa kifupi ni; kutomaanisha wakati unatakiwa kumaanisha au kufanya utani wakati unatakiwa kufanya kitu halisi.au kwa kizungu “to make fun of a person in an unkind way”
  Mfn:Ukiona mtu anatania kumg’oa mtu jino na akaling’oa kweli huo ndio mzaha sasa!

  Kwa hiyo hata anapokuwa kwenye kuigiza na kundi lake Masanja huwa hafanyi mizaha ispokuwa hufanya utani wakati anatakiwa kufanya utani.

  Kwa nini anaposimama kuimba anapokuwa anamtumikia Mungu mnaihusisha na anavyoigiza kwenye runinga? Je anachotakiwa kuacha ni nini; kufanya kazi Original Comedi au style yake ya kufurahisha anapokuwa anahudumu? au mnataka kusema kazi anayofanya Original comedi ni dhambi? Kwa ujumla sioni point yenu ilipo. “Stop being religious and judgemental u guys!

  Masanja nitaona kafanya mzaha kama siku moja kanisani atatuambia tusimame kuimba wimbo wa kuabudu halafu badala yake akaanza kufanya vichekesho.

  Mary hakuna kitu cha kujifunza kutoka kwa hiyo kambi nyingine, they don’t have any true worship in them. Salvation is enjoying life and not it is a parade. Roho mt. yuko ndani yako anatosha kukufundisha yote yapasayo.

  Mpendwa Samuel huhitaji kujua hayo uliyouliza kuhusu mimi hoja nitoazo hapa zinatosha kukufahamisha kuwa mimi ni mtu wa namna gani na kiwango changu cha kujua siri za Mungu kikoje. Nakushauri uongee kama unaongea na mtu anayeweza kula mifupa

  Na sidhani kama ni sawa kujadiliana nje ya blog kwa hoja ambayo iko kwenye blog, ni kuwakosesha wengine kujifunza.

  Mbarikiwe..

 37. Rafiki yangu Sungura Shaloom, natumai hujambo. Kabla sijajikujibu, ningependa kwanza nifahamu naongea na mtu wa aina gani. Yaani ikiwezekana. Umri wa kimwili na Kiroho. Umri zote mbili zina maana, ndipo nitajua pa kuanzia. Nitaelewa, pengine uko JUU sana kiroho, au uko CHINI sana kiroho. Nadhani hiyo ni muhimu. Salaam zangu kwako kwa leo. 1Sam 3.19. SAMWEL AKAKUA NAYE Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha Neno lake lolote lianguke chini. Nitakujibu maswali yako uliouliza hapo juu nikiishajua naongea na mtu wa aina gani, ndio mbna nimekuita Ndugu. Sikusema KAKA, WALA BWANA MDOGO, WALA MTOTO. Barikiwa. Ukiona hata vema tuwasiliane nje blog yote sawa, hata ningejua ulipo tungeonana uso kwa uso tukasemezana. revvictory@yahoo.com or 0765446611. 078448351.

 38. Kwanza niwaunge mkono wenye msimamo wa injili halisi,Tuache kupakana mafuta, niseme baada ya mizaha ya muda mrefu, na BWANA AMEMTUMIA, sasa mch. mtarajiwa awe serious nasukumwa kusema kuwa , asije jikuta anakuwa mchungaji, na mizaha hiyo inaendelea ktk kundi atakalolichunga fikirini litakuwa ni kanisa la namna gani, sipati picha; nadhani awe serious kumtafuta Mungu, aone kama hatasema nae juu ya jambo, kuliko kulisemea kijujuu namna hiyo, pia hata watu wengine wanaposema ni sauti ya Mungu.Tujifunze kwa kambi nyingine, wanaabudu baali lakini hawana mizaha na huyo mungu wao, hata mtu mwingine akikosea tu cha moto atakione, kwa nini sisi wenye Mungu wa kweli tusiwe hivyo?

 39. kaka sungura kumsifu MUNGU si kwamba MUNGU anataka kusifiwa NO MUNGU anasema “lakini saa inakuja ,nayo saa ipo,ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na KWELI kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” KWELI yoh 17:17 “uwatakase kwa ile KWELI; NeNo lako ndiyo KWELI. MUNGU ni NENO yoh 1:1 Tuta wezaje kumwabudi Mungu nje ya neno lake? kaka unakosea nyimbo zozote ziimbwazo pasipo na neno la MUNGU ni nyimbo za dini au kuelimisha si za kumwabudu/kumtukuza MUNGU kama tunataka wasani wetu waimbe nyimbo za kuelimisha waache waendelee kuimba hizo nyimbo zisizo na NENO LA MUNGU mwisho kwa wasanii wakumbuke kuwa MATH 12.36..37 BASI NAWAAMBIA, KILA NENO LISILO MAANA, WATAKALOLINENA WANADAMU, WATATOA HESABU YA NENO HILO SIKU YA HUKUMU, KWA KUWA KWA MANENO YAKO UTAHESABIWA HAKI, NA KWA MANENO YAKO UTAHUKUMIWA. “yoh 4:23 lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu,bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia EFE 4:29,” kaka samwel ubarikiwe mtumishi wa MUNGU kwa kusimami neno ambalo ndilo msingi wa wokovu.

 40. Kumwambia mtu alize watu kuliko kuwachekesha ati kwa sababu Yesu alikuwa mtu wa machozi ni sawa na kuwaambia watu wawe masikini ati kwa sababu Yesu alikuwa masikini.

  Yesu alilia ili sisi tucheke,alipigwa ili sisi tupone,alikuwa masikini ili sisi tuwe tajiri,alikuwa na huzuni ili sisi tuwe na furaha. Huajasoma ufunuo pale Yohana alipoambiwa asilie maana yuko atayekifungua kile kitabu? Maana ya kutokulia kwa aliyekuwa analia ni kucheka.

  Halafu kuchekesha siyo sawa na kufanya mizaha.Mzaha ni mzaha uwe ni wa kuchekesha au ambao uko “serious” au wa kuliza. Na kuchekesha ni kuchekesha kuwe kwa kuigiza au serious, ni vitu viwili tofauti kabisa.Kuna aina fulani ya maigizo yanayoitwa Tanzia,ukikaa kuyaangalia huwezi ukacheka maana ni huzuni. Lakini bado ni maigizo.

  Tusiende mbali; picha ya Yesu ambayo wengi tumeiangalia na tunaendelea kuiangalia siyo kitu halisi,na wala huyo si Yesu mwenyewe ila ni watu/wazungu tu wameigiza. Lakini wengi inapofika wakati wa mateso huwa tunashindwa kujizuia kulia,pamoja na kwamba si kitu halisi.

  Nyie ambao mtakuwa mnamwona Masanja kuwa anaigiza wakati anafanya kitu halisi nyie ndo mna matatizo wala si yeye.

  Ivi mnadhani Yesu yeye alikuwa hacheki,hachekeshi wala hachekeshwi eh!!!!!

  Tafakarini vizuri.

 41. Bwana Samuel, ni nini hasa unachojaribu kuwaasa waimbaji hapa?

  Kwamba wasipopeleka nyimbo zao kwa wachungaji zitakuwa na mapungufu?

  Na kwa nini unajaribu kuwakumbusha waimbaji habari za Lucifer, kwamba na wao wananyemelewa na kiburi?

  Kwani kiburi kinakuja kwa mtu kwa sababu anaimba tu,je kwa wachungaji na watumishi wengine hakiwezi kuwajaa?

  Bora nini, Masanja kuimwimbia Mungu au kuimba nyimbo zisizo za injili?

  Ulitakiwa umpongeze Masanja kwa kazi nzuri anayofanya. Kama anaifanya kwa mzaha au kwa kutafuta pesa kama wengi wanavyojaribu kumwona hiyo ni juu yake na Mungu,nyinyi wala sio Mungu muanze kumhukumu.

  Kama nyimbo anazoimba zina mapungufu ya Kitheolojia ni kwa sababu bado ni mchanga, kesho atafanya vizuri zaidi.

  Nachukia sana wapendwa kuanza kutanguliza shetani kwanza katika kila jambo jema linapoanza kutokea. Mtu akianza kutumiwa na Mungu na kuvuta umati mkubwa wa watu tayari mawazo kwamba yawezekana si Mungu anayemtumia yanaanza.

  Anyway,sishangai sana maana hata Yesu walimwambia hivyohivyo.
  Kuna watu katikati yetu leo kama Yesu angekuja katika kipindi chetu wangekuwa wabaya na wenye kumhukumu kuliko mafarisayo.

  Samuel tuweni watu wa kutia moyo kuliko kuwa na mashaka na kutahadharisha kwingi, Mungu ana nguvu mbali sana kuliko shetani

 42. Ndugu Mkandamizaji, Mch. Mtarajiwa, nadhani ni vizuri niweke wazo lingine hapa, naamini litasaidia WAIMBAJI. Niwakumbushe hivi, aliyekuwa mwimbaji zamani, mnamjua, kama hamumjui, nitawatajia anaitwa. LUCIFER. Leo hana uhusiano mzuri na Mungu kwa kuwa KIBURI kilizaliwa ndani yake Ez 28.13…. Soma utaona, ona mst 15 ULIKUWA MKAMILIFU KTK NJIA ZAKO TANGU SIKU ILE ULIYOUMBWA, HATA UOVU ULIPOONEKANA NDANI YAKO. Ninawaomba nyimbo zenu mkiisha zitunga, pelekea Mch. Wako akukagulie kama zinaendana na NENO. Wakati mwingine tunakutana na nyimbo zinazoimbwa, au zinazosema kinyume kabisa na Neno, tayari zimerushwa, wakati mwingine zimepunguza au zimeongeza. Soma.,..kumb. 4..2 Mith 30..6 na Uf 22..18….19 hayo maandiko yote yanaonya mtu ASIONGEZE wala ASIPUNGUZE. Nawatakia baraka tele waimbaji wote wa nyimbo za Injili. Barikiweni.

 43. Mi sidhani kama Masanja kwa hiyo huduma anakosea, neno la Mungu linafikiwa kwa njia tofauti, ujumbe wa Mungu upo pale pale cha msingi je mameno anayosema yapo sahihi? kwani akisema Jehanam kuna mateso msg haifiki. Mwanadamu asipoamua kupokea message ya Mungu ameamua, wapo wengi wapo serious lakini u-serious wao haukuwabadilisha watu.

  Kaka Samweli we unasema kuwa Mungu amesema sasa basi Masanja aache kuigiza afikishe neno la Mungu kwa njia nyingine, Roho Mtakatifu huwa hasemi na mtu mmoja. Neno Roho Mtakatifu akitaka kumwambia mtu lazima liwe na mashahidi 2 au 3. Na Roho Mtakatifu ni mmoja tu, so kama kweli Mungu asema muda wa kuchekesha umeisha hatakushuhudia wewe peke yako, bali atashuhudia wengi, na kwa kuwa Masanja lengo lake ni kumtumikia Mungu, bac atafuata kama Mungu anenavyo.

  Mungu akubariki sana mchungaji mtarajiwa, akuongezee, AMEN

 44. Mkandamizaji, umesema vizuri kabisa kuwa anayeburn c.d. Zako yeye aburn tu, azisambaze, ili ujumbe ufike, hongera kwa kuwa na moyo huo, kwani huo ni moyo mtumishi, siyo mfanya biashara kama waimbaji wengine. Pia umesema, utaendelea kuigiza mpaka Mungu akuambie basi. Sasa nakwambia hivi, Mungu anakwambia hivi. BASI MUDA WA KUIGIZA, KUCHEKESHA, UMEKWISHA. Anza ukurasa mpya, nashukuru kwamba ulikuwa unaigiza/ unachekesha, mpaka atakapokwambia, ulikuwa tayari, karibu kwenye ulingo wa Injili ambayo haina maigizo ni ORIGINAL, ubarikiwe Mch Mtarajiwa.

 45. Ndugu Mkandamizaji, kabla ya maswali yangu kwako, napenda tusome Biblia, mistari kadhaa. 2Tim 3.16..17 KILA ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU LAFAA KWA MAFUNDISHO, NA KWA KUWAONYA WATU MAKOSA YAO, NA KWA KUWAONGOZA, NA KWA KUWAADIBISHA KATIKA HAKI, ILI MTU WA MUNGU AWE KAMILI, AMEKAMILISHWA APATE KUTENDA KILA TENDO JEMA. MITH 19.29 HUKUMU ZIMEWEKWA TAYARI KWA WENYE MZAHA. MATH 12.36..37 BASI NAWAAMBIA, KILA NENO LISILO MAANA, WATAKALOLINENA WANADAMU, WATATOA HESABU YA NENO HILO SIKU YA HUKUMU, KWA KUWA KWA MANENO YAKO UTAHESABIWA HAKI, NA KWA MANENO YAKO UTAHUKUMIWA. Swali. UMEOKOKA? Kama jibu ni hapana, basi. KAMA NI NDIYO………….UNATAMKA VICHEKESHO, YANI VITU VISIVYOHALISI, NI VYA KUFANYA WATU WACHEKE, KWA LUGHA NYINGINE MIZAHA, HUWA UNAWAAMBIA WATU KUWA NATANIA, NA WAKATI UKISEMA KITU HALISI ? Au unawaachia watofautishe wenyewe! Huoni hata ukiimba nyimbo za Injili, bado watadhani unawachekesha, hata ungewaambia hivi,.,……MWANA WANE JEHANAM NI MATESO, watacheka, badala ya kulia. YESU AKAWAAMBIA JILILIENI NA WATOTO WENU. Lk23…28..31. Mkandamizaji, kama umeokoka,ebu sasa geuza, usichekeshe watu, ebu liza watu, Yesu hakuitwa MCHEKESHAJI. Ebr5.7..Alilia sana na machozi. Isaya 53.3 Mtu wa huzuni nyingi, ajuae sikitiko. Mch. Mtarajiwa, ubarikiwe unapotafakari hayo.asante.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s