Waimbaji wa nyimbo za Injili ni wanafki – Stara Thomas

Mwimbaji wa zamani wa Bongo fleva ambae sasa ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Stara Thomas hivi karibuni alitaja sababu za kushindwa kushirikiana na waimbaji wengine wa nyimbo za Injili kwenye album yake ya kwanza iliyo sokoni sasa.

Aliongea haya alipokuwa akihojiwa kupitia AMPLIFAYA na Millard Ayo  “kwenye upande wa Injili waimbaji wengi bado hawajawa na ufahamu wa kufanya kolabo japo lile ni neno la Mungu linalosimama peke yake haijalishi mnashirikiana au hamshirikiani lakini kushirikiana ni jambo jema, ugumu ambao nimeuona na nimejifunza ni kuhusu unafiki mkubwa sana, mtu anaweza kukuchekea machoni lakini moyoni ni muongo, kuna wengine wasanii wakubwa niliwaona nikafikiri lakini nilipowakaribia nikagundua sio, unafiki ni mwingi, kule kwenye bongofleva kulikua kuna upendo”

Na inasemekani hii sio mara ya kwanza Stara Thomas kutoa madai hayo, mwigizaji Dokii mwanzoni alipookoka, aliwahi kusema wazi waimbaji watano wakubwa wa Injili Tanzania,  ni wanafiki, wana ubinafsi, chuki, kujisikia na kujitenga na hawakukubali kumpa ushirikiano wowote.

Millard Ayo pia aliandika kwenye website yake kwamba waimbaji wa Gospel wenyewe wameshawahi kukiri kwamba hakuna upendo kati yao, watu wanachukiana, hawana umoja. Rose Muhando, Upendo Nkone na Miriam Mauki walishalisema hilo kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM.

39 thoughts on “Waimbaji wa nyimbo za Injili ni wanafki – Stara Thomas

 1. kikweli sisi tufanyao mziki wa injili atutaki kuchangiza mawazo pamoja, mfono wa sisi wa congomani tungeungana pamoja na nyinyi watanzania kwa mziki wa injili wa pamoja ingelikuwa vizuri ila nikama vile tumesahau kama tu watoto wa Baba mmoja, halafu Mama juwa tunapo fanya wimbo wa pamoja hapo Mungu anaguswa sababu yeye ametufanya kuwa umoja katika yeye

 2. Kama mimi nilikuwa nafikiriya kwamba hata kwamba mukishirikiana pamoja na nyinyi wenyewe mmegunduwa kwamba akuna upendo ni heri kila mtu ajibebe na kundi lake.
  Lakini maneno munayoimba nimazuri sana, yakujenga nakuokowa, wengi kupitiya nyimbo zenu wamekwisha pata okovu, nanyi mungaliki pale-pale na uwadui, poleni sana. Lakini Mama Upendo nkone, Rose Muhando, pia na Ambwene mwasongwe nyimbo zenu zinanitiya moyo. Asanteni na Mungu awabariki.

 3. Mungu awasaidie waimbaji wa injili kwani,NI KWELI UPENDO HAUPO KTK WAIMBAJI WA GOSPER kwani,kujivuna,malingo,dharau,chuki, kujiinua ndvyo vilvyotawala !

 4. mimi nazani kila ajibizanaye kuhusu neno la Bwana Mungu Wetu ni mpumbavu asiye na akili timamu enyi watu mtajibizana hadili tumieni akili uyo mama kama kweli anampenda Mungu nakujitoa kwake hapaswi kumlaumu mtu ama kulazimisha watu wawe karibu nae only God anatosha kuwa karibu na mtu na si mwanadamu pia hana nia ya kumtumikia Mungu bado ana tamaa ya kupenda fedha na vilivyomo duniani ni wangu Mungu aliwainua na niwachanga kirohoo still Mungu yupo nao hadi leo na hawajarudi nyuma na hawajapata msaada hata wa wachungaji ni moyo wa mtu tu kwenye swala la wokovu bwana.

 5. Lucy:

  4.1.2013

  Shaloom.

  Bwana ana nguvu na uweza pale tu tunapomwitaji hujibu.

  Tusikae chini kulaumu au kumfundisha Stara Thomas kwani WITO, MKATABA NA MUNGU anao yeye mwanadamu ni pamoja na mimi. Inawezekana anapoandika kitu ameona tofauti, amefikiri, amezani kuwa ndivyo. Sana sana tungepeana msimamo na mwoonekano wa kila moja anapotoa makala jaribu kukaa chini, kuwa makini kwa nini mtu ameandika maneno, sentensi hiyo. Kumbuka shetani ni huyu huyu mwanadamu na mstaraabu ni huyu huyu mwanadamu. Vile vile mtu akikukataa siyo hoja! jiulize!

  Unaposema neno ushirikiano lina beba uzito mkubwa sana. Shirika ziko nyingi. Cha muhimu ni kusamehe hasa pale ambapo mtu anapojitokeza kwenye vyombo vya habari kushiriki na wewe neno. Ushikiriano upo sehemu nyingi si USANII pekee yake.

  Kuna: Kazi
  Kwaya
  Kikundi
  Umoja wa kina mama
  Wokovu
  na nyinginezo nyingi kama msiba, arusi au shughuli yeyote ambayo inabeba kikundi.

  adui wa vyote hivyo ni kama alivyosema aliyetangulia kwamba CHOYO, WIVU, CHUKI na KIBURI ni adui wa mwanzo.

  Mungu atubariki sote.

 6. Haya sasa, tarehe 22/09/2012 saa sita mchana Flora Mbasha nae kasema hakuna ushirikiano kwa wasanii wa muziki wa Injili Tanzania,zaidi ya unafiki na kuogopa kufunikana.
  Mbasha alisema hayo alipokuwa anahojiwa na George Mpela wa Praise Power radio kuhusu ziara zake za USA na Afrika Kusini.

  Kasema wasanii hawashirikiani wakati mwingine kwa sababu ya madhehebu yao, tofauti kabisa na nchi kama Marekani ambako kumejaa waimbaji wakubwa duniani.

  Kwa hiyo tuliomshambulia dada Stara Thomas kuwa anasumbuliwa na uchanga wa kiroho, basi tumwambie na Mbasha kuwa anasumbuliwa na uchanga wa kiroho. Au tumwombe radhi kwa kumshambulia wakati alichosema ni kweli.

  Na tukubali ukweli kuwa liko tatizo la kutoshirikiana kati ya waimbaji wetu wa nyimbo za injili, na tuwatake wajirekebishe.

  Ni hayo tu!

 7. kolabo ni ngumu sio kwa waimbaji wa injili tu bali hata watumishi wa Mungu, watumishi wa Mungu ndio wanasemana kila kukicha, sina haja ya kutoa mifano maana wenyewe mnasikia. Kikubwa nikuwaombea kwani hata wao wenyewe wanajikuta tu katika hiyo hali maana ni shetani yule mshitaki wetu.

 8. “Unafiki” ni neno ninalobeba maana kubwa na pana sana. Uhalisia wa unafiki ni ile hali ya kuji-pritend kuwa positive kumbe wewe ni negative.

  Kuhusu unafiki wa waimbaji ni sawa kabisa; japo sio wote. Hakuna asiyejua kuwa makundi mengi ya wanakwaya wanajamiiana kingono pasipo kufunga ndoa na bado wanasimama kuhubiri neno la Mungu mbele ya Kandamnasi; huo ni unafiki mkubwa sana zaidi hata ya ule unaoongelewa na Akina Stala na Dokii.
  Kuna msemo mmoja unaosema kwamba aisifiye mvua imemnyea; na mwingine wa kiingereza unasema hivi ‘no research, no right to speak’ Nasema hivyo kwa sababu mimi katika umri mdogo nimekuwa mwimaji nikiwa nasafiri na watu wazima – dada na kaka zangu tuliokuwa tukiimba pamoja; mambo niliyokuwa nayaona ni ajabu tupu na sijui kama tabia hiyo inaweza kukemewa na kuachwa.
  Wachangiaji msiongelee kudharauliana tu; chukulieni uhalisia wa unafiki ndo tuongelee.

  Wanakwaya wangapi wapepeana mimba na kutelekezana?
  Wanakwaya / walimu wa kwaya wangapi wanatembea na wake za watu na waumini wanafahamu na kulifumbia macho?

  Hilo la kutoshirikiana kwenye uimbaji ni dogo sana tena sana; ni ile hali ya kila mmoja kulinda soko lake la nyimbo kwani siku hizi uimbaji umekuwa ni biashara tu!

  Siku nikirudi kwenye uimbaji; nitaimba kumtukuza Mungu na sitaweka maslahi mbele kwani kuweka maslahi kunaleta machafuko kwenye kazi ya Mungu.

 9. Mimi ni producer na nimeshafanya kazi ya kuandaa mziki na waimbaji wengi. Alichosema stara ni sahihi kabisa. Mimi pia nilipookoka nilijaribu kwenda Bible Study lakini hawakunipa ushirikiano. Mpaka dada Yangu Beatrice Muhone aliponipa moyo wa kusoma Bibilia mwenyewe mwanzo-ufunuo. Hapo nikakutana na Sauli(paulo) na nikakuta kwamba baada ya kuokoka alisahauliwa mpaka Barnaba alipokuja mkumbuka. Ni ukweli wa dhahiri kwamba WAIMBAJI WA BONGO FLEVA WANA USHIRIKIANO KULIKO WAIMBAJI WA INJILI!!!! upende usipende ndio ukweli. pia WAIMBAJI WA MZIKI WA DUNIANI WANASHUKRANI KULIKO WANAMZIKI WA INJILI!!!!!na pia WANAMZIKI WA INJILI NIWALALAMISHI KULIKO WANAMZIKI WA DUNIANI!!!!!
  Chanzo ni nini?
  mimi naamini
  1. KIBURI – wanamziki wengi wa injili hawaamini kwamba kipawa alichonacho ni neema tu ambayo Mungu amemtunuku. wanaamini kwamba ni juhudi na maarifa yao ama fedha waliyolipa ndiyo mafanikio yao. NDIO MAANA HATUPATI MWANAMZIKI WA INJILI AMBAYE ANAZEEKA HUKU ANAMTUMIKIA MUNGU! Wengi kazi inaishia njiani.
  2. CHOYO – Hawapendi kuwashirikisha wengine karama walizopewa na Mungu. Wakishakuwa maarufu basi wanaanza kujitenga na ndio maana ni wanamziki wachache sana wakongwe wa injili wanaosaidia kukuza vipaji vingine.
  3. SIFA – kwa wanamziki wa dunia unaposikia wanataja jina la producer ndani ya wimbo ni namna ya kukubali kazi ya producer na kumtangazia soko. Kwa sisi wa injili huwezi fanya hivyo maana itakuwa unajichukulia utukufu. Lakini nje ya hayo ni ngumu sana kumsikia mwanamziki wa injili akimtaja producer aliyemfikisha hapo wengi huweka mazingira kana kwamba ni uwezo wao ndio umewafikisha hapo na huwezi kuwasikia wakiweka mazingira mazuri ya kurudi kwa producer aliyemfikisha hapo. sana sana utasikia maneno ya kashfa kama “MIMI NAHAMIA KWENYE UPAKO MWINGINE”!!!
  4. WIVU – Pengine hili linaanzia kwa wachungaji walezi wetu. Mfano kwa maskio yangu nilishawasikia wachungaji wakimteta mwalimu mwakasege kwamba hajui kufundisha ila ni bahati tu anakubaliwa!?! wachungaji wetu wanaoneana wivu mpaka wametuambukiza watoto wao. Kwa wivu huo hawawezi kukaa pamoja maana anaona kama atamsababishia mwenzake kuwa maarufu. Pia kuna kudharauliana maana kila mmoja anajiona yuko juu. Naomba kwa leo nikomee hapa

 10. Kapinga sikuwa nimetaka kujua tofauti ya Paul na Stara, bali niliuliza tofauti ya Paul na Stara katika kutumia vipawa vyao baada ya kuokoka.

  Kwa kifupi neno alilokuwa amejifunza Paul halikuwa neno la kristo, ispokuwa alikuwa tu amejifunza kitu ambacho walikuwa wamejifunza pia mafarisayao waliomsakama na kumshitaki Yesu.

  Alichokuwa nacho Paul ni kipawa ambacho alikitumia kulitesa kanisa. Au kwa lugha nyingine alikitumia kumtumikia shetani.
  Alicho nacho Stara ni kipawa ambacho hapo mwanzo alikitumia kumtumikia shetani pia.

  Paul alipookoka alitumia kipawa hicho hicho kumtumikia Mungu. Iliwezekanaje hiyo? Ni pale alipobadilishwa nia yake ya ndani. Kwa kipawa kilekile na kwa bidii na kujitoa kulekule Paul alimtumikia Kristo.

  Stara kaokoka, anatumia kipawa hicho hicho kumtumikia Mungu, maana amebadilishwa nia.

  Halafu nani kasema kulaumu kwa kusema vile ilivyo ni jambo baya? Kwani hakuna watumishi ambao walilaumu kwa namna hiyo kwenye biblia?

  Hebu ona hapa Paul alikuwa anafanyaje:

  2Tim 4:14 (14. Alexander the coppersmith did me much evil: the Lord reward him according to his works:
  Verse 16: (At my first answer no man stood with me, but all men forsook me: I pray God that it may not be laid to their charge.

  Hapa Paul alikuwa anafanya nini?

  Nikijaribu kuangalia kwa undani zaidi katika michango ya wengi wetu ni kamba hatumshambulii Stara ati kwa sababu kalaumu. Lakini wengi wanaona kuwa yeye kuokoka na kuendelea kuimba tena ndani ya muda mfupi si sawa. Maana wengine waliowahi kusema huo ukweli wa waimbaji wa Injili kutoshirikiana, kama akina Miriam Lukindo , upendo Nkone nk hatuwasemi kabisa kama na wao walishawahi kusema maneno kama ya Stara.

  Mwisho, bwana Kapinga hakuna lugha yoyote mbaya niliyotumia kumwambia Sam. Nina miaka mingi sana hata nikiwa kwenye ndoto siwezi kutoa tusi.

  Kilichokusumbua hapo ni neno “ufukunyuku”!

  Nenda kalisome kwenye kamusi ujue maana yake ni nini Alexander, halafu uje usome tena sentensi yangu uone kama utaendelea kuhitaji ufafanuzi wangu.

  Bless u!

 11. Kapinga sikuwa nimetaka kujua tofauti ya Paul na Stara, bali niliuliza tofauti ya Paul na Stara katika kutumia vipawa vyao baada ya kuokoka.

  Kwa kifupi neno alilokuwa amejifunza Paul halikuwa neno la kristo, ispokuwa alikuwa tu amejifunza kitu ambacho walikuwa wamejifunza pia mafarisayao waliomsakama na kumshitaki Yesu.

  Alichokuwa nacho Paul ni kipawa ambacho alikitumia kulitesa kanisa. Au kwa lugha nyingine alikitumia kumtumikia shetani.
  Alicho nacho Stara ni kipawa ambacho hapo mwanzo alikitumia kumtumikia shetani pia.

  Paul alipookoka alitumia kipawa hicho hicho kumtumikia Mungu. Iliwezekanaje hiyo? Ni pale alipobadilishwa nia yake ya ndani. Kwa kipawa kilekile na kwa bidii na kujitoa kulekule Paul alimtumikia Kristo.

  Stara kaokoka, anatumia kipawa hicho hicho kumtumikia Mungu, maana amebadilishwa nia.

  Halafu nani kasema kulaumu kwa kusema vili ilivyo ni jambo baya? Kwani watumishi ambao walilaumu kwa namna hiyo kwenye biblia?

  Hebu ona hapa Paul alikuwa anafanyaje:

  2Tim 4:14 (14. Alexander the coppersmith did me much evil: the Lord reward him according to his works:
  Verse 16: (At my first answer no man stood with me, but all men forsook me: I pray God that it may not be laid to their charge.

  Hapa Paul alikuwa anafanya nini?

  Nikijaribu kuangalia kwa undani zaidi katika michango ya wengi wetu ni kamba hatumshambulii Stara ati kwa sababu kalaumu. Lakini wengi wanaona kuwa yeye kuokoka na kuendelea kuimba tena ndani ya muda mfupi si sawa. Maana wengine waliowahi kusema huo ukweli wa waimbaji wa Injili kutoshirikiana, kama akina Miriam Lukindo , upendo Nkone nk hatuwasemi kabisa kama na wao walishawahi kusema maneno kama ya Stara.

  Mwisho, bwana Kapinga hakuna lugha yoyote mbaya niliyotumia kumwambia Sam. Nina miaka mingi sana hata nikiwa kwenye ndoto siwezi kutoa tusi.

  Kilichokusumbua hapo ni neno “ufukunyuku”!

  Nenda kalisome kwenye kamusi ujue maana yake ni nini Alexander, halafu uje usome tena sentensi yangu uone kama utaendelea kuhitaji ufafanuzi wangu.

  Bless u!

 12. Mungu akupe Rehema….. nilivyokusoma wewe dada yangu Stara uko kibiashara zaidi na hata hao uliowaendea ili ushirikiane nao wako kibiashara pia….. Sikiliza dada hakuna shortcut kwa mungu, nyenyekea chini yake ili upewe Roho Mtakatifu wa kukuongoza nae atakuonyesha ndugu zako wa kushirikiana nao ktk hiyo huduma uliyoianzisha. Wana wa mungu hatutoi malalamiko yetu mbele za wanadamu, tunapeleka hoja zetu kwa MUNGU Maana yeye ndiye atupae nguvu.

 13. Kuna watu wengine hata kupiga makofi tu wakati unaimba kwao ni “kidunia”. La muhimu ni kwamba mradi mashairi na ujumbe unampa Mungu sifa na utukufu, binafsi sioni ubaya wowote wa nyimbo za injili kuwa na “midundo” na wala sijawahi kusoma kwenye biblia sehemu inayokataza kupiga midundo sanasana nimesoma Zaburi ikisema “….pigeni kwa ustadi…”.

 14. Wapendwa,

  ZIFUATAZO NI ISHARA ZA MTU ALIYEKUA KIROHO:

  1. Yuko tayari kushirikiana na watoto wachanga kiroho kwa upendo na huruma

  2. Yuko tayari kukubali kupoteza ili mdogo wake apate faida

  3. Hana tamaa ya kujilimbikizia mali wakati wadogo zake kiroho hawana lolote.

  4. Yuko tayari kuwakosoa wadogo zake kiroho bila unafiki pale wanapokosea (Mtume Paulo alifanya hivyo kwa Petro pale Paulo alipomwona Petro akila chakula na watu wamataifa (wachanga kiroho) na akajitenga nao mara tu alipomwona Paulo (Galatia 2:11-16).

  5. Yuko tayari kujitolea kufa ikibidi kwa ajili ya wadogo zake wachanga. Kama wewe ni mzima kiroho lazima uwe tayari kujitoa mhanga ili wadogo zako kiroho wapone.

  6. Yuko tayari kutafuta chakula (mafundisho) kwa ajili ya kuwapa wadogo zake ili nao wakue. Hawezi kula peke yake. Ni wapendwa wangapi wako tayari kuwapa wenzao mafundisho mazuri kiroho ili wakue? Au tunakazana tu kuwashambulia kwa maneno makali pale wanapokosea kama mama mzazi awavyo mkali kwa mtoto wake akoseapo badala ya kumfundisha yeye ni kutandika bakora tu eti ndo kumfundisha adabu mtoto?

  7. Yuko tayari kumwombea mtoto mchanga kila siku ili akue kiroho na ashinde majaribu. Yesu aliwaombea wanafunzi wake. Paulo aliwaombea watoto wake kiroho. Musa naye aliwaombea sana watoto wake pale Sinai. Je, sisi tunawombea au tunawaambia watajiju? Dada Stara Thomas tunamwombea au tunamponda kwa mawe au tunamrushia madongo tu?

  8. Yuko tayari kuwaongoza wadogo zake kwa vitendo na siyo kwa maneno.

  9. Aliyekua kiroho yuko tayari kukosolewa pale anapokosea na wala hajisikii kuwa amedhalilishwa endapo amekosolewa na mtoto mdogo. Ni mfano wa mzazi kwamba akikosolewa na mtoto wake hawezi kumcharaza kwa maneno wala kwa fimbo eti kwa nini amemweleza ukweli mbele ya watu? Hata kama mzazi amejamba mbele za watu, mtoto mdogo yeye atasema ukweli tu, “Mama, baba umejamba?”. Huku ndiko kukua kiroho.

  10. Aliyekua kiroho hawezi kumcheka mtoto mdogo kiroho pale anapoanguka au kuteleza badala yake anamshika mkono na kumwinua. Ni wapendwa wangapi wamekua kiroho kwa point hii? Wengi wetu huishia kusema maneno tu au kumcheka pembeni na kusema , “si tulisema mapema, si umeona sasa, hangeweza kuendelea, angefanya hivi au vile….. ndiopo angeweza kusonga mbele……….” Haya ni maneno ya watu ambao wanajiona kuwa wamekua kiroho kumbe hata wao bado wadogo sana yaani ni wachanga.

  11. Mtu aliyekua kiroho hawezi kuwa na wivu kwa mtoto mdogo kiroho kwa sababu tu ameona huyu mtoto wa juzi amepewa zawadi fulani na mzazi. Yaani tuseme, mtoto mdogo kiroho akipewa kipawa na Mungu, wewe uliyekua kiroho huwezi kuona wivu wala ajabu. Hii ni sawa na mtoto mwenye miaka 18 na kuendelea ambaye anaona wivu kwa mdogo wake wa miaka 5 kununuliwa viatu au nguo na mzazi wake. Au akiona mzazi amenunua pipi na kumpa mdogo wake wa miaka 5 na yeye anazira kabisaa hata chakula hataki tena kula eti na yeye anataka apewe pipi ndipo aoneshe ushirikiano. Huu ndio unafiki. Naam ndio uchanga wenyewe.

  12. Mtu aliyekua kiroho hawezi kumshangaa mtoto mdogo akiwa amekaa vibaya bila hata kuvaa chupi ya ndani. Hata akiwa anakojoa hadharani mtoto hachekwi wala huwezi kumshangaa endapo wewe umekua mtu mzima kiroho. Ukimwona mtoto mdogo amekaa vibaya au amelala uchi, au anatembea uchi mbele za watu, wewe ukiwa mtu mzima hutamcheka kwani unajua huyo ni mtoto. Mfano huu ndio unaopaswa kuigwa hata makanisani kwetu. Kama unajua fulani bado ni mtoto mdogo kiimani au kiroho au kimaandiko wewe hupaswi kumsema wala kushangaa vituko vyake kwani yeye ni mtoto mdogo bado. Ukimshangaa ujue kuwa hiyo ni ishara kwako kwamba hata wewe bado ni mchanga sana kiroho, naam hujakua na huwezi kuwa mwalimu.

  13. Mtu aliyekua kiroho halalamikiii wenzake wala hanung’unikii lolote litendwalo na wadogo zake bali hutumia fursa hiyo kuwafundisha wadogo zake nini maana ya kuokoka, maisha nini, maandiko yanasemaje, nk.

  14. Aliyekua kiroho hana tabia ya kuwadharau wenzake (wadogo kiroho) ambao hawajafanikiwa kwa vipaji au mali.

  Mwisho, Katika mjadala huu, haya mambo ninayoyaeleza ndiyo niliyoyaona yamesumbua watu wengi makanisani mwetu. Wengi hawakui kiimani, kiroho wala kimaandiko. Wengi wamedumaa. Wengi wana siku nyingi makanisani lakini hawajawa watu wazima.

  Kuna watu wengi wamejitahidi kueleza maneno mengi kumwelekea Stara Thomas wakijidhania wao wameshakua kiroho, lakini ukichunguza kauli zao, na wao bado ni watoto wadogo sana.

  HEBU TUJITAHIDI BASI TUWE WATU WAZIMA KIROHO.

 15. kwanza na ongera dd stara kwa kupata neema ya kuokolewa.
  Ndugu zangu turudi kwa ndugu zetu wa biblia kama Petro ambaye ktk mitume alipewa heshima kubwa ktk mitume 12.Kama Petro na mitume wengine 11 walishindwa kutoa ushirikiano kwa Paulo itakuwa kawa wasanii wetu? Gal 2:5-8. kitukilicho sababisha Paulo apewe ushilikiano na mitume 12 ni NEEMA haliyopewa na BWANA YESU sio kwamba alisoma sana torati? bali ni NEEMA tu aliyopewa na BWANA YESU.Dd yetu asilalamike bari aonesha NEEMA aliyopewa na BWANA YESU na amini kam ni watu wa rohoni WASANII WENZAKE WATA MPA MKONO WA KUUME WA SHIRIKA tatizo sio kiapaji nii NEEMA ALLITOPEWA itakayo mpa mkono wa ushirika.Gal 2:8. Paulo alipata mafundiho ndomana Biblia inasema”Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa ya KUPASAYO KUTENDA” MDO 9:6 AKAWA HUKO SIKU WAKADHA WA KADHA pamoja na wanafunzi walioko Dameski.mdo 9:19 Paulo kukaa dameski siku kadha wa kadha na wanafunzi wa YESU alikuwa anapata “mafundisho” akuanza kuhubuli tu bila kupewa mwongozo .Ndo maana Paulo anasema kwa abali ya ASKOFU asiwe mtu ALIYEONGOKA KARIBUNI? 1TIM 3:6? kwanini asema habari za muda wa wokovu? kwenye wokovu MUDA unaheshima kama kweli unataka kujilikana na MUNGU lakini unaweza kuwa auna heshima kama utakuwa tu Hunamalengo yoyote soma HEB 5:12. Mwisho kaka Sungura na wezako. kazi yoyote uliyopewa na Bwana Yesu itasimama atakama utapata mkono wa ushirika (MDO 5:38-39) ndo maana wakina ……………… walikimbia kwa sababu walikuwa wanafanya kwa ajili ya wanadamu.UNAFIKILI YESU kuwachagu mitume 12 aliwachagu tu bila SABABU? ndo maana YESU alisali usiku mzima kwa ajili ya kuwachagua mitume 12 (WITO). hata leo tunasoma injili yao ingawa walipata mateso makubwa wakikatazwa kuhubiri neno la Kristo na MASADUKAYO NA AKIDA na VITISHO lakini bado injili ilihubiriwa na wengiwao walikufa kwa sababu ya YESU ss km dada yetu Majungu tu yawanadamua unanyatangaza ata kwa watu wasio amini wakati mna chama cha waimbaji wa injili ambacho mnaweza kusuluisha tatizo? utaweza kutetea JINA LA YESU ATAKIFO? MUNGU atusaidie tumje sana yy. Mwisho dd kama kweli kazi hii ikiwa imetoka kwa mkono wa wanadamu ITAVUNJWA, lakini ikiwa imetoka kwa MUNGU hawataweza KUIVUJA. MDO 5:38-39. BARIKIWA.

 16. bwn Sungura naomba tu nikuoneshe tofauti ya Paulo na Stara kama ifuatavyo;

  1) paulo alijifunza neno la Mungu lakini alilitumia kama sheria, stara hakuwahi kujifunza neno la mungu wala hakuwahi kujifunza kumwimbia Mungu kabla hajaokoka.NB kuna tofauti ya kujifunza kuimba nyimbo za kidunia na kumwimbia Mungu kama huduma ya kuvuna roho za watu.

  2) paulo alishajifunza kuwa nacho na kuto kuwa nacho, kupendwa na kuto kupendwa, kuzomewa na kuto kuzomewa,kutengwa na kuto kutengwa,n.k. paulo alikuwa wa kwanza kabisa kutopewa ushirikiano na wanafunzi wa Yesu nafikiri unakumbuka jinsi ambavyo wanafunzi wa Yesu walivyomkataa alipofika kule dameski lakini sijaona alipowahi kusema wanafunzi wa Yesu ni wanafiki kama ambavyo huyu dada amesema kwa waimbaji wenzake.

  3) paulo alijua ugumu wa huduma yake kwani alikuwa ameshahesabu gharama ya kumfuata Yesu au kumtumikia Yesu na ndio maana hakupata shida na kukataliwa na walio mtangulia lakini alisimama baadaye na wenzake nao wakapata kujua kweli ameitwa kwa kazi aliyokuwa anaifanya na wala sio kwa maneno yake ya kuwakosoa aliowakuta ila kwa kufuata kile ambacho Mungu amemtuma kuja kukifanya.

  hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo mi naona yanakosekana kwa huyu dada na wengine wote wanaolaumu sijui sijapewa kolabo mara hawana upendo Yesu haiti watu kwenye kolabo ila Yesu humwita kila mtu binafsi ili asimamame kwenye zamu yake na sio kolabo isipokuwa kolabo linaletwa na Yesu mwenyewe aonavyo kuna ulazima wa kufanya hivyo. pia kolabo sio lazima litoke kwa waimbaji wakubwa bali ni yule unayeongozwa na Yesu kuwa umuhusishe ktk uimbaji wako vinginevyo ukienda kimwili basi ndio utaishia kukosa hilo kolabo na kuanza kulaumulaumu kama hivi.Bado msimamo wangu uko pale pale huyu dada anahitaji ufahamu zaidi wa maana ya huduma ya kiroho ni nini, na inaupinzani gani na nani anaiongoza huduma hiyo.

  MWISHO:
  Nimesikitishwa sana na lugha yako bwn Sungura uliyoitumia kumshambulia Samwel!!! Naomba utueleze maana ya hii sentensi kama nilivyoinukuu kutoka hapo juu kwenye mchango wako

  “Naomba tuache upambe na ufukunyuku tuchangie mambo ya msingi Sam.”

 17. Naomba niwapongeze Ndugu Lwembe, Reb na Sungura ni kweli kabisa Dada Stara bado ni mchanga anatakiwa kuonyeshwa upendo ili akue zaidi kiroho, nakumpongeza kwa kuwa wazi. Dada Stara endelea kumshika na kumtegemea mungu nae atakuongoza. Usichoke kuombea roho ya unafiki uliyoiona. Pole mpendwa Mungu wetu tunaemtumaini na akutie nguvu uzidi kusimama ufanye kazi yake, hayo ni mapito tu.

 18. Kwa mara nyingine tena tena nakupongeza ndg Lwembe kwa mchango wako ambao mantiki yake iko wazi na yenye nguvu ya ukweli na uhalisia “tusafishe kambi”. Stara katumiwa na Mungu kutujulisha udhaifu ambao tuko nao ila tulikuwa hatujui kama tunao( unafiki na dharau ,a.k.a – kiburi)

  Sam, kwa wewe nimeshaelewa kuwa naongea na mtu wa aina gani ki-mtazamo na uelewa pia. Naomba turudi kuchangia hoja yetu ya msingi.

  Bless u!

 19. Wapendwa,
  Kuokoka ni jambo la faida sana kwa aliyeokoka. Yaani kuokoka maana yake halisi ni kuwa rafiki wa Mungu, kama alivyokuwa baba yetu Ibrahim. Sidhani kwamba kuna anayeweza kutoa maelezo ya kutosheleza kuuelezea ujasiri na furaha iliyo ndani ya aliyeokoka! Hata wakati mwingine ni rahisi sana watazamaji kumsoma kitofauti mtu aliye ktk wokovu, haijalishi ni mchanga kiasi gani! Na mara nyingi wale walio komaa ktk wokovu hupoteza ladha hata wasijue makinda wao huwa jasiri kiasi gani pale wanapokuwa wameuingia “moto” wa wokovu!

  Nadhani hilo ndilo tatizo tulilonalo. Wakongwe wa wokovu wameota magamba hawajui kuwa kuna katoto kanacheza na wenzake nao wamekanyima ushirikiano! Ndipo nako kanalalama, mbona huku kunakotakiwa kuwe shwari, nchi ya maziwa na asali, mbona wameniwekea sumu katika maji  niliyowaomba nilipokuwa na kiu? Angalau kule nilikotoka mwenzio kama hataki, anakuambia hataki na shauri yako utajiju!!

  Wakongwe msijidai kufunika mambo, huyo Stara bado mtoto mdogo, ktk innocence yake, kuwaumbua mlivyo ktk wokovu wenu, basi muogopeni Mungu kidogo, licha ya kuwa mmemzoea, SAFISHENI KAMBI, unafiki ni sifa ya chini saaaana kwa mkristo hata kama bado hajaokoka, acheni unafiki mpongezeni huyo dada kwa kuyaweka hayo hadharani na si kumfanya kaingilia “wokovu” wenu!!!!

  Bwana na atushushie “KAA” lake la MOTO litutakase!!!

 20. Ndugu yangu Sungura, ni kweli nimejibu kitoto, ila ni vizuri ukikumbuka kuwa Blog hii hainifundishi mimi tu. Wala haikufundishi wewe tu. Sasa ukisema nimejibu kitoto, sikushangai, kwa kuwa mtoto siku zote anajiwazia yeye tu, hata ukiwakuta wato 10 wanacheza, ukawaambia nina pipi nimpe nani, utasikia kila mmoja anasema MIMI, hiyo ni utoto, jua ya kuwa wako wengi wanaotibuka wanapoambiwa jambo tofauti ama ni Imani yao, ama mtazamo wao, pia ukasema ulitaka usijibu, huo nao ni utoto, Biblia inasema tuwe tayari kumjibu kila mtu anayetuuliza, pia mahali pengine ukasema hivi.,Sam unaandika sana, hii inaonyesha kile kinachoandikwa wala hukioni, wala hakikusaidii. Paul akawaambia Waebrania kuwa alikuwa na mengi, ila wakawa wavivu wa kuyasikiliza. Pia umesema kuwa naandika mengi kujitetea, ndugu yangu najitetea ili iweje? Rafiki yangu Mungu anatupenda ebu tuendelee kunyenyekea chini ya mkono wake, aendelee kutufundisha ubarikiwe Sungura .

 21. Ndugu yangu nashukuru kuwa wewe umeelewa kuwa mawazo yangu na yako mengi tunatofautiana, yawezekana, unajua mwanzo kabisa nilipotaka kukujibu nilikuuliza umri zako mbili, hukunijibu, nilikuwa nataka kujua kama unaelewa nini katika Miaka ya kuishi, maana kuna vitu ambavyo unavyoweza kuvieleza theoreticaly, hapo sisemi kwa Neno la Mungu, maana Neno halina mjadala, linabaki kama lilivyo. Ila kuna opinions, mtazamo wa mtu, anavyoona yeye, inakuwa tofauti na mwenzie, lakini kama wote waliookoka wangevaa uniform, hayo yasingekuwepo, Amosi 3..3. Je watu wawili waweza kutembea pamoja wasipopatana? Kama Yesu ndiye amewaunga hao watu wawili, watapatana tu, hawatatofautiana hata katika mitazamo yao, Efeso 4..1…6. Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa ktk Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa, kwa unyenyekevu wote, na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana ktk upendo, na kujitahidi umoja wa Roho ktk kifungo cha amani.

  Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, Imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. Ndugu yangu Sungura, kama kweli wawili wavaa hizo uniform hapo juu, wote watania mamoja, mtazamo wao utakuwa mmoja, ukumbuke ndiyo maana Paul akasema hivi…. 1Kor 2..14…15 Basi mwanadam wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni, lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Ndugu yangu mahali popote walipo watu wa mwilini, na watu wa rohoni, hakutakuwa na mapatano, au maafikiano katika mitazamo, huyu atatazama kimwili, mawazo, anavyoona yeye, na huyu mwingine atatazana kiroho ( kiroho, ni jinsi Biblia inavyomtaka afanye) ss kama ulivyosema kuwa tunatofautiana sehemu mbali mbali nadhani mimi niko mwilini, na wewe uko rohoni. Tuendelee kujifunza, pengine utanisaidia nifike rohoni, niliandika mstari huu, niurudie tena. .1kor 8..2 Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajajua neno lolote bado, kama impasavyo kujua. Barikiwa.

 22. Sam, umechangia kwa namna fulani ya kitoto sana. Nilikuwa nimetaka nisijibu chochote kuhusu coment yako, lakini nimeamua kukujibu.

  Aliyesema kutibuliwa ni mimi,wala usingsema “watu wengine..” ila ungesema tu Sungura ametibuliwa ningekuona ni mkomavu sana.

  Ila pia kwa ule mfano wako wa kisima cha Bethzatha ulikuwa mzuri japo hujataka kuumalizia vizuri kwamba, kama kutibuka kwake kulisababisha watu kupona basi kumbe kutibuka ni kitu chema, wala usiseme tena kuwa tusitibuke maana kumbe kutibuka ni kitu chema kinachoweza kuponya.

  Umeuliza kinachotibuka ni nini, najaribu kusoma mazingira ya mawazo yako kuwa yawezekana jibu lako au ambalo ungependa mtu fulani ajibu ni kuwa kinachotibuka ni roho chafu ndani ya huyo mtu.

  Naomba tuache upambe na ufukunyuku tuchangie mambo ya msingi Sam.

  Bila shaka unajaribu kniponda kwa sababu katika michango mingi mimi na wewe tunatofautiana kimawazo. Wala usijali tunajifunza tu,wala si lazima tukubaliane.
  Ubarikiwe Samuel.

 23. Rose nilisema mmenitibua wala sikusema nimekwazika. Mimi huwa sina tabia ya kukwaziki.

  Naomba msome tena alichokisema Stara,wala hajahukumu,ila kasema jambo alilokutana nalo na kugundua alipotaka kufanya kolabo na wasanii wa injili na kalisema hilo kwa hekima kubwa sana. Naomba sana soma tena maelezo yake hapo juu halafu useme ukweli ni wapi alipohukumu.

  Halaf kumbukeni maelezo yale yamesema hata Dokii alipookoka alisema hilo jambo la kutopewa ushirikiano na wasanii wa injili, tena yeye kasema kabisa wasanii wakubwa. Angao Dokii ndo kajaribu hata kuwahukumu lakini sio Stara. Mmemshambulia bila kusoma kwa undani.

  Kapinga I don’t know how much punctual u are in the statements u write” I’m a man of deatail!

  Look here:- Paul alikuwa amesoma torati na alikuwa anamtumikia shetani.

  – Stara amejifunza kuimba na alikuwa anamtumikia shetani au dunia

  – Paul alipookoka alibadilishwa nia akaanza kumtumikia Mungu kwa kipawa
  kilekile alichomtumikia nacho shetani.

  -Stara kaokoka kabadilishwa nia ameanza kumtumikia Mungu kwa kipawa
  kilekile alichotumikia dunia

  Sasa niambie ni nini ambacho Stara alitakiwa akae aendelee kujifunza ambacho Paul hakutakiwa kukaa kujifunza kwanza kabla ya kuanza kumtumikia Kristo baada ya kuokoka kwao ?

  “In other words; Tell me the difference between Stara and Paul in applying their talents to serving christ after they were born again”

  Umesema hatupimi huduma ya mtu kwa kuangalia amarekodi album ngapi,ila kwa kuangalia kama inabadilisha watu,…… sijui hapa suala la kurekodi album na kupima huduma za watu limetoka wapi.

  Kapinga kama Stara alipokuwa kwenye bongo fleva alikuwa anapewa ushirikiano na kufanya kolabo na wasanii wengine, ulitaka asemeje, kwamba alikuwa anachukiwa?

  Na aliponyimwa ushirikiano na wasanii wa injili ulitaka asemeje, kwamba alipewa ushirikiano ati kwa sababu tu kwa kuwa kwa kristo kuna upendo wa kweli?

  Inashangaza sana kwa nini huku kwa kristo kuliko na upendo wa kweli hawa waimbaji hawakumwonyesha upendo.

  Sanga let’s be realistic and logical in what we say here!

 24. Tunaendelea kujifunza, Blog hii hakika naipenda maana inatusaidia sana. Maana wapo watu wengine WANATIBULIWA, kwani wamekuwa kisima cha Bethzatha? Ndicho maji yake yalikuwa yanatibuliwa na malaika, na aliyekuwa anaingia wa kwanza alikuwa anapona. Yoh 5..2…4. Ebu tusitibuke, au tuambizane hicho kinachotibuka ni kitu gani’? Halafu pia inashangaza kuwa wengine Wanakwazika. Lakini Biblia inatufundisha hivi..Zab 119..165..WANA AMANI NYINGI WAIPENDAO SHERIA YAKO. WALA HAWANA LA KUWAKWAZA.. Blog hii tuendelee kuiombea, ili iendelee kutusaidia, KUTIBUA, na KUTIBULIWA. Pia hata leo imetufundisha kuwa. Mtu akiijua sheria ya Bwana, HAKWAZI, wala HAKWAZIKI, kwa ndani yake hakuna KIKWAZO. Mbarikiwe.

 25. bwana Sungura nafikiri unatumia hisia kuelezea jambo ambalo limeshaelezwa na biblia kwa uwazi kabisa. Yesu alisema mtu akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe na ajitwike msalaba wake na anifuate. pia anasema imetupasa kuhesabu gharama za kumfuata Kristo kabla hatuja amua kufanya hivyo. mimi nilichokisema kwenye maoni yangu ni juu ya wale wanaomuongoza huyu dada kwenye wokovu wake. Unapomtaja Paulo na kusema alijifunza kwa muda mfupi nashindwa kukuelewa kwa sababu Paulo alikuwa amesomea sheria zote za torati kwa Muda mrefu wala hakutumia muda mfupi vile kujua yale yote yaliyomsaidia kushinda majaribu mazito namna ile yaliyompata ktk huduma yake. kwa hiyo usichanganye Paulo alisoma zile sheria za torati kwa muda mrefu sana ila alikuwa ankosea application yake tu ndio alichokifanya Yesu alipomwokoa alibadilisha ile application yake na akawa imara sana bila kutetereka hta walipomkatisha tamaa hakuanza kulalamika alisema niko tayari hata kufa. kuimba kwa ajili ya Kristo sio tu kujua kupangilia sauti lakini ni wito maalumu sana wa Yesu kwa mwanadamu. Ndio maana nikasema watu wengi wanaokoka kutoka kwenye nyimbo za kidunia na kufika moja kwa moja kuimba injili wanashindwa kuendelea kwani wamekosa ile maana ya kumwimbia Mungu badala yake wanafikiri ni kupangilia tu sauti. huku tunaimba ile mtu aweze hata kuacha dhambi,kuponywa magonjwa, kushukiwa na Roho mt. nk. hii sio kazi ya kupanga tu sauti ila inahusisha kuharibu kazi za shetani hivyo upinzani wake ni mkubwa lazima uwe umevaa silaha zote ili uweze kushindana.
  Alichokosea huyu dada ni ile tendo la kusema eti kule nilikotoka kuna upendo kwani mi najua upendo wa kweli uko kwa Yesu pekee na sio kwa wasio na Yesu ila wao wanaweza kuwa na ushirikiano wa kawaida tu na wakadhani ni upendo. soma vizuri ktk 1coritho 13 ili upate kulinganisha kama hayo mambo yaliyotaja hapo yako kwa hao wamataifa ambao huyu dada anasema wana upendo au ibilisi anajaribu kumdanganya ili arudi nyuma.
  Waimbaji wengi huduma zao zimeanzia chini ya wachungaji wao katika kwaya za makanisani kabla ya kuanza kurecodi albamu binafsi sasa we jiulize je kumtumikia Mungu gani kwa uimbaji ambako kunaibuka tu ghafla bila kujua misingi ya uimbaji ni ipi.
  nina uhakika kabisa kama huyo dada ataulizwa huduma yake ilianzia wapi na maono yake nini anaweza akashindwa kutueleza kwa ufasaha.
  Naomba bwana sungura uelewe kuwa hatupimi mafanikio ya huduma kwa kuangalia tu umerecodi albamu ngapi ila tunaangalia huduma hiyo inabadilisha watu? je ina huisha roho za watu? lakini pia je hiyo huduma yako inapopata upinzani je unakabiri vipi huo upinzani? au unaanza kurusha lawama kama hivi?
  Hii ni dalili either umekosa ufahamu au sio wito wako kamili kutoka kwa Bwana. Ndio maana nilisema ni vizuri wale wanaomlea kiroho waanze kumjenga vizuri ili asiwe naye miongoni mwa watu wanaolaumu wengine wanapokutana na upinzani.

  Maoni yangu ni kwa ajili ya kumsaidia huyu dada sio kumvunja moyo kama atayachukulia positive!!!!

  MBARIKIWE SANA WOTE

 26. Kila neno atakalo linena mtu ata toa hesabu siku ya mwisho hivyo kabla ya kuongea au kuchangia hapa SG na tujipime ikiwa hayo tunyoongea au kuandika yamepata kibali kwa
  Mungu.
  Zaidi sana huyu mama anhitaji maombi na mafundisho,tukumbuke hata kina Petro walimuuliza
  Bwana Yesu watapata nini baada ya kuacha vyote.Baada ya kufunguliwa walitulia kwa Yesu so
  the lady needs to know the Glory of the kingdom then she must not complain of any thing.

 27. Shalom ndugu Sungura
  pole kwa kukwazika
  baraka za Mungu hazichangamani na majuto, kama hukumu katoa yeye kwanza mie namshauri tu, kama uko nae peleka ujumbe usimjibie. Hatugombani tunajifunza taratibu kaka.

 28. Naomba niwe muwazi hapa!

  Rosemary na Kapinga mmenitibua sana.

  Rose Stara hajaenda kwa hao waimbaji kutafuta msaada ispokuwa ushirikano na ushirikiano/umoja katika mwili wa kristo hauwahusu tu watu wachanga kiroho bali hata waliokomaa. Na mbona mnamsonga sana Stara wakati maelezo hapo juu yanasema hata Rose Mhando, Miriam Mauki, na Upendo Nkone walishawahi kusema hayo maneno kwenye redio ileile na kwenye kipindi kilekile na kwa mtangazaji yuleyule? Why Stara Thomas? Just stop and encourage that lady please

  Halafu hebu tuambieni mtu akiokoka anatakiwa akae muda gani ndipo aanze kumtumikia Mungu?

  Mtume Paul alikaaa muda gani akaanza kumhubiri kristo baada ya kuokoka kwake?
  Mbona kuna watu wengi tu Yesu alipowasamehe dhambi zao au kuwaponya walianza kufuatana nae saa ileile au kumtumikia Mungu ni kupi?

  Stara alipookoka hakutakiwa kuanza kujifunza kuimba,kuimba alikuwa anajua tayari alichotakiwa kufanya na amekifanya ni kubadilishwa nia, na kubadilishwa nia kunaleta kubadilisha ujumbe. Sauti yake ni ileile nzito na kipawa ni kile kile tofauti ni nia ya ndani.

  Mbona mnakuwa kama mafarisayo jamani; ati angemuuliza Mungu ajue kwa nini walikataa!

  Si afadhali wangekataa kuwa “hatutaki kushrikiana na wewe”, lakini sasa walimchekea kana kwamba wako pamoja nae lakini kumbe kwa ndani hawakuwa pamoja nae = unafiki.

  Kwa nini hatutaki kukubali kuwa tunazidiwa mara zingine upendo na wasiookoka?

  Mungu akimwokoa mtu maarufu wala msidhani kuwa atamwondolea umaarufu wake, ataendelea kuwa maarufu lakini akiwa amejawa nia ya kristo. Kwani mtume Paul/ Sauli aliondolewa umaarufu wake alipookoka?

  Rose ulitaka Stara amkimbilie Yesu mara ngapi? Kutaka kushirikiana na mtu mwenye jina sio kutokumkimbilia Yesu- tafakari vizuri.
  Yeye alisoma biblia inasema muwe na umoja kama mimi na Baba tulivyo umoja akajua kuwa wapendwa hao wanalishika neno hilo kumbe kakuta ni wanafiki. Sasa kosa lake nini hapo mpaka mmsemeseme hivyo?

  Halafu kwa taarifa yenu wapendwa, Stara si mchanga kama mnavyodhani. Mimi sijui hasa ni lini kaokoka, lakini nina zaidi ya mwaka na nusu nimemwona akiwa ameokoka na nikasali nae mara kadhaa. Mtu wa mwaka mmoja na zaidi kama ana bidii ya kujifunzi si mchanga huyo.

  Hata hivyo hatusubiri kukua ndipo tuanze kumtumikia Mungu, maana kukua kiroho hakuna mwisho.

  Kwani walipokataa kumtia moyo kashindwa kurekodi? si huyo karekodi jamaa, na atafanikiwa kama atatia bidii!

  USIMPINGE ALIYEFANIKIWA- JIUNGE NAE!

  “Please stop judging, rather encourage”

 29. Shalom wapendwa
  kwanza nampongeza Stara Thomas kwa kuokoka, pili kwa kuwa muwazi kuwa kazi anayoifanya ni ngumu….
  Tuliwahi kuongelea sana kwamba mtu akiokoka na fani yake au kipawa cha kuimba / kuhutubu sio vizuri palepale anapewa huduma kuongoza au kuhubiri maana bado hajakomaa kiroho hii ilikuwa kwa Mr NIce na tukasema inamnyima fursa ya kukaa chini ya walimu viongozi na kukua kiroho maana tayari na yeye anakuwa anahudumia wengine na matokeo yake wanaishia njiani. Pamoja na kupingwa na kelele nyingi ila wote tunamuona Mr Nice alipo….sio kuwa tunawatakia mabaya ila tunaomba viongozi wao wawe na hekima ktk kuwalea na sio kuogopa majina na uwezo wao na kuwaachia wafanye watakavyo…
  Tukirudi kwa Stara uimbaji ni utumishi ni uinjilisti, kila mtu Mungu amempa kusudi lake, mfano Paulo alikuwa mtume wa mataifa na Petro wa Wayahudi…Hata hapa watu wamemuona Mwl Mwakasege miaka nenda rudi anahubiri na kuzoa watu hajawahi kuwaza kuwa hawa niliozoa niwachunge hapana labda sio kusudi lake…..

  Sasa ndugu yetu Stara arudi ajikague:
  je ni kweli ni kusudi la Mungu yeye ahubiri kwa njia ya kuimba?
  Je ni wakati wake huu au aliombwa kusubiri?
  Je alitumwa kuhubiri au kutumika kwa kina nani?
  Je alipoona ugumu alimuuliza Mungu nani mshirika wake ktk huduma hii…kwani hana anapoabudu, kwanini asiwashirikishe waumini wanaoabudu nae au kwaya ya hapo au hiyo ni kujishusha?
  Vyote hivi vinahitaji muda mrefu wa kukaa magotini na kumuuliza Mungu na kuweza kusikia sauti yake na kutii, mwambieni akae karibu na mchungaji wake na kanisa lake simsikii akilitaja nalo wamekataa kumpa mkono wa shirika?
  Akane na kukataa kila sauti ya shetani inayorudi rohoni mwake kumwambia afadhali alikotoka, kweli kule kuna upendo wa kweli? asitudanganye
  Akae chini na kujifunza neno sio kila mtu ni kusudi lake kuimba au kuhubiri na wewe, angesoma neno na kulielewa asingethubutu kukimbilia kila muimbaji mwenye jina bali angemkimbilia Yesu kwa kila hitaji lake na angempa Roho mt amuongoze, Yesu alisema atatupa msaidizi ndiye Roho atakayetufundisha yote.
  Pengine ni kwa nia njema tu wenzie wamekataa kushirikiana nae wakiongozwa na Roho mt kwa hiyo aache roho ya uchungu na kulalamika bali arudi magotini na kuomba aonyeshwe washirika wake na ajikague kama anasimama ktk kusudi lake ipasavyo. Mungu amtie nguvu

 30. hao waimbaji wa gospel au kwaya wote hao ni biashara tu wala hakuna mambo ya kumtumikia Mungu wanapoimba wanauza kanda ili kupata pesa wanakuja kuimba kwenye ma hotel tunawapa pesa hukutukiburudika………….hata wanavyoimba nakucheza kwao hakuna utofauti kati yao nasisi ambao hatumjuwi huyo Bwana wao………….

  ___________________________________________________________________________

  Maneno mengine yamefutwa na blog hii…dj Shakur, tafadhali ukirudi siku nyingine kuandika hapa tumia lugha nzuri ama sivyo hatutaruhusu tena maoni yako.

  —Strictly Gospel Blog

 31. sina uhakika sana na wokovu namna watu wanavyoupokea. Ila ninachokiona kama tatizo hapa ni kwa wale ambao walimhubiria injili huyu dada na wakamwacha ajitegemee mwenyewe kabla ya kumpa mafundisho madhubuti. Amekuja kwa Yesu na kuingia kwenye huduma moja kwa moja bila kujua utofauti wa kule alikokuwa na kule alikoingia saizi. Kuokoka ni maisha mapya kabisa ambayo hayawezi kufananishwa na maisha yetu kabla ya kuokoka hata kidogo. pia watu wengi wanatoka kwenye nyimbo za kidunia na kuingia kumwimbia Mungu huwa wanaingia wakiwa na mentality ya kuhisi wanaweza kumbe huduma ya Mungu hauwezi tu kusema mi najua kwani ina upinzani mwingi sana kutoka kwa shetani hivyo mtu asipoitwa kiukweli na Mungu kwenye huduma hiyo atakata tamaa haraka sana na kuanza kulaumu wengine kama huyu dada anavyofanya. Naomba wale wanaohusika na wokovu wake waangalia sana ktk kumsaidia huyu dada. watu huwa wanafukuzwa mpaka nyumbani kwao kwa sababu tu ya kumtumikia Yesu na sijawahi kusikia wakisema kwenye media kuwa hawa watu hawanaupendo au kule nilikotoka kuna unafuu kuliko huku hiyo sio sawasawa. Alafu ktk huduma ya KiMungu hatushirikiani tu na watu ovyoovyo ni lazima tuwe tumewahakiki kweli wameitwa na Mungu na kweli wanaishi maisha matakatifu na wamefundishika na kukua vizuri kiroho.
  Mbarikiwe sana.

 32. Aisee!!! Naomba Mungu awasaidie wawe na upendo ili kazi ya Mungu isonge mbele waifanye kwa umoja mshikamano na upendo wote wa Kristo. Ili kusudi la Mungu kwa uimbaji wao liweze kutimia wasiwe wabinasi .

 33. This is painful indeed!

  Hii ni kwa sababu wengi wao walipoanza kuwa maarufu walikoma kukua katika kumjua Mungu wakaona hawahitaji kuhudumiwa bali wao tu ndio wa kuwahudumia wengine. Ndiposa utakuta muda wote waimbaji wengi wako kwenye ziara.
  Umaarufu bila kumjua Mungu sawasawa unaweza kuwa chanzo cha maangamizi kwa hawa watu.

  Waimbaji wengi pamoja na wanamziki huwa hata hawaendi na biblia zao kanisani au kwenye ziara wanakokwenda kufanya huduma. Mara nyingi wao kanisani husubiri kuimba tu na wakishamaliza wanatoka nje,au wanaondoka kbisa kanisani kama wanajua hawataimba tena,au wanakaa ndani lakini hawana biblia wala mahali pa kuandika yanayofundishwa.

  Si lazima kuwa na biblia kanisani,lakini si mazoea mazuri kwa mtu anayemjifunza Mungu kutokuwa nayo na kutoandika kinachofundishwa.

  Kwa nini wanakuwa wanafiki; ni kwa sababu wanaogopa wakishirikiana nawe utawafikia umaarufu walio nao ikiwezekana na kuwazidi. Lakini wanasahau kuwa hata bila wao mtu atainuliwa tu hata kama ni kwa ugumu mkubwa.

  Ukweli waimbaji wetu wengi ni waimbaji tu wala si waabudu(they are not worshippers). Ndio maana jumbe za nyimbo nyingi ni butu au zinazojirudia rudia sana au wamerudia tu kuimba maandiko kama yalivyoandikwa kwenye biblia.

  Bahati mbaya sana pia watu wetu wengi wanapenda hizo jumbe na melodi nyepesi. Angalia waimbaji wachache ambao wanaimba jumbe nzito wengi wao nyimbo zao huwa hazipokewi kwa urahisi sana.

  Siku “mindset” ya watanzania itakapobadilika,hawa waimbaji wanafiki watatiwa nidhamu na kuwa wanyenyekevu, na siku hiyo haiko mbali sana.

  Ni aibu kwa waimbaji wa Injili kuzidiwa upendo/ ushirikiano na mafarisayo,lol!!!!!!!!!

 34. ulipokuwa unaitwa ili utumike kwa YESU alikuitwa pekee yako kwa ajili ya wengine,
  sasa inakuwaje tunaanza kugeuza injili sehemu ya kuzogoana kama watu wa dunia

  ukiokoka Matatizo yanayoonekana kwa macho yanatatuliwa kwa maombi.Tuliokoka kulaumu siyo sehemu yetu,bali ule uweza wa MUNGU ndani yetu ndiyo tunautumia kuleta mabadiliko. hata kwa YESU kuna kufahamiana na pia kuna ushirika na wale MUNGU anaokuongoza ushirikiane nao.

  yaani leo tu unataka ushirikiane wakati bado hata hatujachanagamana nao

  Ukiona watu hawajakupa mkono wa ushirika ujue kuna pahali unatakiwa kupaweka sawa

  Ahsateni

 35. Kama mnaimba kwa kujitukuza wenyewe na si kumpa Bwana Mungu sifa , basi hizo nyimbo zenu hazina upako kabisa.. Mungu anakaa katika sifa na si magombano.. kama wewe stara Thomas umeona waimbaji wengine wa injili wanafki..unachotakiwa ni kuwaombea hili wamjue Mungu wa kweli na siyo kueneza eneza mambo kwenye media.

 36. Mungu atusaidie wapendwa, kinachoniumiza ni sentensi ya dada huyu aliyosema” kule kwenye bongo fleva kulikuwa na upendo”,hii inaonyesha ni jinsi gani tusivyokuwa nuru ya ulimwengu huu maana Bwana Yesu alisema nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni Mathayo 5:16 na Bwana Yesu akaendelea kusema maana nawaambia kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo ya waandishi na Mafarisayo,hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni Mathayo 5:20

  Mungu atusaidie tatizo ninaloliona hapa si kwa waimbaji tu ni kwa wa kanisa kwa ujumla tunahitaji kuwasidia wakristo wachanga wanaoamua kumfuata Yesu ili wauone upendo wa Mungu, tusiwe kwazo kwao kwa namna yoyote ili wasikumbuke kule walikotoka au wasiyasifu yale walioamua kuyaacha maana najua huku walikuja ni kuzuri sana kuliko kule walikotoka ,basi tuwasaidie kwa upendo tukiwaonyesha uzuri wa kumfuata Yesu,lakini sisi wenyewe tusiwe wa kwanza kuwakatisha tamaa jamani Mungu wa Mninguni atusaidie katika hili
  Mungu awabariki

 37. Kama ndivyo, huenda kuna mambo mnafanya ambayo wao hawayapendi, Jaribuni kujitazama wenyewe kabla hamjaanza kuwalaumu wanamuziki wa Injili.Stara na wenzako.Mbona Marehemu Ongara alipookoka alishirikiana nao vyema!Iwaje nyie.Huenda kunatatizo katikati yenu, either roho ya kujikweza au laha.Examine yourself first before sending complaints to media

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s