Kila unachotamka kinafanya kazi..chunga ulimi wako!

Watu wengi wanadhani maneno tunayotamka hayana maana yoyote…si kweli!! Maneno yetu yana maana kubwa kwenye maisha yetu. Kuna watu vinywa vyao havina mipaka! wanaropoka matusi wakati wote, shuleni, kazini, nyumbani wengine wanaita watoto wao mbwa, mbuzi, changudoa, mpumbavu nk…hayo matamshi yanaumba na yanatokea kama ulivyotamka.

Kama unatatizo hili au mara nyingi kinywa chako umeshindwa kukizuia, soma maandiko haya na Neema ya Mungu iwe juu yako, ukaponywe kwa jina la Yesu.

“Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo meam, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake” Luka 6: 45

 “Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya) Mithali 12:18

“Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo” Mithali 15:4

“Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake. Bali wenye haki watapona kwa maarifa” Mitahili11:9

‘Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.” Mithali 18:21

“Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani” Mithali 16:24

“Maneno mazuri ya staha hutufanya tunapatana sisi kwa sisi ” Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu” Mithali 16:21

“Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha” Mithali 2511

Chunga sana ulimi wako….

Advertisements

7 thoughts on “Kila unachotamka kinafanya kazi..chunga ulimi wako!

 1. “ulimi kiungo kidogo matatizo yake makubwa ,”
  wimbo huu nimeuimba nikiwa mdogo sunday school ulimi unabariki ulimi unalaani ,hata mm nimeutumia vibaya wakati fulani ulimi wangu nafuta kila neno baya nililowahi nenea watoto wangu,kujinenea mwenyewe hata kuwanenea rafiki na ndugu zangu katika jina la Yesu ,Roho Mtakatifu niongoze jaa ndani mwangu katika kibao cha moyo wangu nimeliandika neno lako Bwana Yesu nisije nikakutenda dhambi.

 2. KWELI HILI JAMBO HATA MIMI NILIKUWA NA HII TABIA YA KUTUKANA WATOTO NA KUWATAJIA MAJINA YA AJABUAJABU HII NI TABIA MBAYA SANA NAMWOMBA MUNGU ANISAMEHE KWA HAYO NILIYOKUWA NIKITAMKA NI HII TABIA MAMA YANGU ALIKUWA NAYO NA MTOTO WANGU WA KIKE PIA ANAYO SANA NITAMUOMBA MUNGU AMWEEPUSHE NA KUTAMKA MANENO MABAYA KWA WATOTO WAKE NA WAYU WENGINE PIA

 3. kweli mada hii imenigusa, maana kuna muda watoto wananikera na ninawatamkia maneno mabaya, ila namshukuru Roho Mtakatifu kwani mara nisemapo neno hilo baya hunionya nami nalikemea mara. Kweli tunahitaji sana kujaza neno la Mungu ndani mwetu ili hata kusema kwetu kuwe kama Yesu, na pia katika maombi tumuombe Mungu atusaidie na atupe kutawala ndimi zetu

 4. ULIMI NI KAMA MIFANO IFUATAYO

  Ni kama upepo mdogo uendeshayo merikebu kubwa baharini

  Ni kama moto mdogo uwashayo msitu mkubwa

  Ni kama lijamu katika mdomo wa farasi ambao huendesha uelekeo na spidi ya farasi

  Yesu na atusaidie kuweza kushinda ULIMI maana kila neno atakalolinena mwanadamu atahukumiwa kwa hilo.

 5. Ni kweli, wakati mwingine mnaingia kwenye bus, unamsikia mtu anasema hivi. LEO KWELI TUTAFIKA? Au LEO TUTAFIKA USIKU. au HUYU DEREVA LEO ATATUMWAGA MTARONI. Misemo ya aina hiyo, kile kilichotamkwa kinatimia, ndipo ss waliosikia wakati akisema wanamuuliza ULIJUAJE? Hapo ndipo yeye hujigamba kuwa Niliwaambia mimi, nilijua mimi. Watu wanamuamini, anaonekana wa maana, anaonekana mtabiri, au nabii, maana anasema yanatokea. Asante kwa somo la ULIMI, maana ni kweli kile kiujazacho moyo ndicho kinatoka. Mmoja akasema MOYONI MWANGU NIMELIWEKA NENO LAKO ILI NISIKUTENDE DHAMBI. (mioyo yetu ijazwe Neno la Mungu, ndimi zetu zitanena Neno badala ya maneno.) mbarikiwe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s