Niombeeni niko kwenye uchumba sugu!

Tumsifu Yesu Kristo, naomba mniombee ili uniweze kufunga ndoa kwa maana nimekaa na uchumba sugu kwa miaka 12 sasa, tayari nimeishazaa naye mtoto mmoja! Nampenda lakini sielewe rohoni mwake! nikimuliza ni lini tutaowana anajibu simple tu “unapenda sana harusi”!!! Nashindwa nifanyeje? Najisikia aibu, huzuni, kuwa mwaminifu kwake lakini sijui lengo lake wangu! Kuhamia kwake bila ndoa naona kama nitazidi kudhaurika kwa wazazi wangu na walezi wangu walio nisaidia mpaka nikapata kazi. Na umri wangu unakimbia! Napenda niwe na familia yangu. Tuishi mke na mme na siyo mwanamke na mwanaume tu. Na kuzaa mtoto mwingine na baba mwingine ni sawa na kutenda dhambi juu ya dhambi, Mungu aniepushie, Niombeeni mwenzenu!

–Pauline

Advertisements

28 thoughts on “Niombeeni niko kwenye uchumba sugu!

 1. Jacline ple sana!
  Story yako inafanana kwa sehemu kubwa na ile ya Pauline,lakini kuna vitu fulani vya ndani ambavyo vinatofautiana na ya Pauline. Wewe nia yako ni kuachana na huyo ndg kwa sababu umeshaona kabisa kuwa hayuko serious. Lakini tatizo ni kwamba kila ukijaribu kumwacha unashindwa.
  Hilo ni tatizo la kawida kabisa la tabia ya mapenzi unapokuwa umempenda mtu, kwamba ukiwa naye moyo wako unakumbuka yale yote mabaya anayokufanyia. Lakini unapofikia uamzi wa kumwacha moyo wako unaanza kukumbuka yale mazuri yote ambayo amewahi kukutendea, hapo ndipo kigugumizi cha maamuzi hutokea.

  Kwa hiyo katika hali hiyo inakuwa ;Kumwacha maumivu na kuwa nae maumivu vilevile.
  Katika hali hiyo jibu sahihi huwa ni kumwacha,ambapo utaumia lakini baada ya muda utapona, kuliko kuwa nae ambapo utaumia siku zote.

  Usifukuzwe kazi, jibu la kukuponya lipo.

  Here is the number: 0654 95 89 70

 2. Hello!
  Your request is good and the place you exposed is the right place. Many talked and prayer offered. Now I think you need to sit down face to face with true spiritual father that you trust for step by step breaking the soul tie bondage(I can sense that by the Spirit of God).
  We(Mr& Mrs Nyagawa) love you Sister.

 3. Dada Pauline, mimi sijasoma commet zote ila nimesoma ombi lako. What I know is this ”God is close to the broken hearted and saves those who are crushed in spirit.” The Bible also says ”the heart of the king is in the hand of the Lord and He turns it as He wills.” God is the one who changes people hearts. Umeomba ombi zuri that you would know this man’s heart. God know his heart and He is able to reveal that heart to you. So lets pray:
  ”Father I thank you for your amazing love and mercies. Father I thank you that you know Pauline heart and genuinely cares about her. Father I thank you that she did not go anywhere else but came running to you for answers. I thank you that you know what is best for her life. I thank you that you have a glorious plan for her life. Lord I pray that you will make plain her fiances intentions. Father I pray that she will know your will and plan for her life. Lord I thank you that through this she will be draw closer to you. Thank you that you will lead her to make the right decision for her life. Thank you Lord that she will enter marriage because it is your will for her life and not because of anything that has happened in the past. Thank you that all things works for good for her life. Thank you Lord that you do not waste anything in anybody life. Thank you that each and everything that has lead to this point in her life you are able to bring good out of it. Thank you for giving her courage to make hard decision for her life that will bring glory to you and help her move on. I pray that you will reveal yourself to her in a way that she will understand and accept you! In Jesus might name I pray. Amen.

 4. pole sana jibu ni kuzidi kumuomba mungu akutangulie na akupe nguvu ya maombi na pia ushirikishe watumishi pia usiseme unahitaji ndoa bali hebu kaa nae ujue ana tatizo gani linalomfanya aone hata ndoa ni tabu.

 5. Bwana yesu asifiwe. Wachangiaji wote wamechangia vyema sana.ila dada paulina hiko hivi ndugu yangu,huyo mwanaume HAKUPENDI kabisa,unachokiona wewe kwake sio upendo ila ni UPENDO FEKI(FAKE LOVE) katika pande zote mbili yaani kidunia na kibiblia. Nianze na kidunia tu, haiwezekani mwanaume timamu na mwenye upendo wa kweli kwa mchumba wake akae miaka 12 hajamuoa tu!!? Hamna upendo hapo. Pili kibiblia ndo kabisaaa hakuna muoaji hapo maana kanuni zote za koana mmezikiuka.Sasa fanya hivi tubu dhambi zako,omba Mungu akutakase zaidi,ndoa zipo tu afu pia kuolewa au kutokuolewa humpeleki mtu mbinguni.MUNGU anajua amepanga nn juu yako ni wewe kusimama ktk neno.

 6. Jacline na Pauline
  poleni wapendwa mimi dada yenu nilipitia huko tena ni ndoa ya kanisani,
  baada ya mapito ya miaka 3 hadi kutaka kuchanganyikiwa niliamua kukaa na kumuomba Mungu kwa dhati….nilikaa na kumuomba Mungu na niliitii sauti yake. Pamoja na kuwa nilishazaa mtoto niliona isiwe sababu ya mimi na mtoto pia kuikosa mbingu kwasababu ya matatizo ya mtu mwingine. Niliondoka na nilianza moja na mtoto wangu. Leo hii ni miaka 12 nikiwa mwenyewe na Yesu wangu nina kila sababu ya kumshukuru sana kwa kuniokoa na kunipa nguvu ya kusema hapana. Jipeni moyo ni kiasi cha maamuzi tu na kuchukua hatua. Yesu anawaita sasa, wakati ni huu…Tunawaombea

 7. ambae anajua kweli anaweza kunisaidia naomba anipe namba yake yasimu angalau kusali pamoja nae nimekata tamaa hata kazi naweza kufukuzwa mda wowote kweli mshahara wa dhambi ni mauti.

 8. eeh bwana yesu nimesoma hadi machozi yamenitoka nashukururu sana kwa ushauri wenu mzuri maana tumepona wengi.mimi pia napiata mapito yako pauline najua ni jinsi gani unaumia,wakati mwingine hata kusali unakua huwezi na kufanya maamuzi huwezi jamani ni ngumu mungu pekee ndo anaweza kututoa kwenye hili shimo.nina mwanaume miaka saba na tumezaa mtoto lakini hata kwenda tu kujitambulisha nyumbani hataki licha yakumsihi sana na wazazi wangu kunishauri angalau wajue tu baba wa mtoto hata kama hana lengo namimi.amegoma jamani lakini bado anadai ananipenda na anadai anatafuta ela yakufunga ndoa.kweli kiuhalisia sioni kama yuko serious ila kila naposali nakuamua kumuacha nisonge mbele nashindwa,nasali sana jamani lakini kama saivi nina uchungu siwezi tena hata kusali naumia nakulia tu MUNGU NAKUSIHI UNISAIDIE

 9. Unapoomba kwa ajili yake kumbuka kwamba kinacho msumbua ni maamuzi tu! Yawezekana anapenda sana kuwa kwenye ndoa lakini amenaswa katika kutoa maamuzi. Hivyobasi, wewe pia unahitajika kuliangalia swala la maamuzi maana maamuzi hayo hayo ndiyo yaliyokusababisha uzae mtoto bila makubaliano ya dhati na ya baadaye na huyo ndugu.
  Wakati mwingine unahitajika kumuuliza kama kweli anampango wa kukuoa au anampango wa kuoa mtu mwingine. Inawezekana anakusubiria uanguke na mtu mwingine ili apate sababu ya kukuacha.

  Kumbuka mwanaume anayekupenda hawezi tena kabisa kukukalisha miaka 12 wakati anajua kabisa yeye ndiye baba wa mtoto. Siwezi kujua lakini omba Mungu ampe maamuzi ya busara na ya haraka ili kama hana mpango na wewe aweze kukueleza na kukuondolea msongo wa mawazo

 10. Nimesoma kwa makini sana jumbe zote, kwakweli watumishi mmemshauri vizuri sana mimi binafsi zimenisisimua sana wkt nasoma nilikuwa natamani kama nipae jinsi nivyopata raha moyoni mwangu hivi ni mtu gani au ninani angeweza kukupa ushauri mzuri wenye busara na uliotulia kama huu? Ninachoweza kusema mimi hapa nikiwa km msichana/mwanamke mwenzio achana na huyo mwanaume hakupendi kabisa kwasababu kama angekuwa anakupenda usingekaa naye mda mrefu namna hiyo unajua dalili ya uchumba mbaya ukishaona mwanaume uko naye muda mrefu hapigi hatua asongi mbele ujuwe kuna kitu kati kati yako inawezekana kabisa kwa asilimia mia yupo mwanamke aliyempenda huyo kijana ambaye ndo anakuja kuoa.

  Tena shukuru Mungu dada kwamba umezaa naye mtoto mmoja tena hujachelewa dada yangu fanya maamuzi sasa hivi uvunje hizo roho zilizokuzunguka dada yangu toa hicho kinyago ulichokiweka moyoni mwako, Mungu hawezi kujibu maombi yako kwasababu hapo ulipo ni mdhambi na umekumbatia kinyago moyoni mwako. wewe ni wa thamani sana umenunuliwa kwa gharama kubwa sana. Huyo mwanaume anakupotezea muda using’ang’anie kitu kisichowezekana mrudie Mungu hakuna kinachoshindikana kwake mtwike Mungu mizigo yako yote, wasi wasi wako, hofu yako 1petro 5:6-7.

  Mrudie Mungu toa maisha yako kwa Yesu, utaona atakachokifanya juu yako, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzake kuna ahadi kibao alizokuahidi Mungu anakupenda upeo unajua?

  kwakuwa Bwana Mungu ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu, hebu fikiri Yesu anavyokupenda alikufa kifo cha laana ili kuondoa laana sasa kwanini wewe uishi na laana kama ilishaondolewa?

  kuna ahadi kibao za kusimamia ili upate mume soma isaya 34:16 Zab 84:11

  Amua sasa dada yangu wala kuokoka si ushamba mimi mwenyewe nimeokoka na ni msichana mrembo ile mbaya sikuangalia urembo wangu nimemtazama Yesu maana yeye ndo mambo yote asikudanganye mtu lakini km utaendelea kufanya dhambi halafu unasema unaomba nisikuongopee dada yangu Mungu hakujui anawajua watoto wake maana wewe unakuwa si mtoto wa Mungu.

  Asante Mungu akubariki akupe neema ya kufanya maamuzi.

 11. Ndg yangu Samuel, sasa nimekuelewa. Kweli nilikuwa nimeelewa ulitaka maelezo kama nilivyoainisha hapo nyuma.
  Nimekuelewa vizuri nia yako ni njema. Ubarikiwe ndg.

  Dada Pauline, kama kuna mtu atakwambia kuwa anaweza kukuombea ukafunga hiyo ndoa sidhani kama atakuwa amekwambia ukweli.

  Amin nakwambia, ya kuwa huyo jamaa hakupendi. Vinginevyo labda kama anafanya hivyo akiwa hana akili sawasawa.

  Kwa nini unataka huyo jamaa ambaye hana upendo wa kweli na wewe akuoe?

  Je ni kwa sababu tu unataka heshima ya kuolewa, au ni kwa sababu unampendas sana, au ni kwa sababu tamaa ya mwili imetoa makicha makali ndani yako,nawe unaona aibu kuwa na mtu mwingine kwa vile umezaa nae?

  Hatima yako kuwa katika kristo na kutoka katika hali yako ya kujiita mkristo wa kawaida ni ya muhimu zaidi kuliko kuolewa. Kuolewa hakukupi garantii ya kuishi maisha ya furaha,kuna watu wanateseka na ndoa.

  Tafuta ufalme wa Mungu na haki yake, na suala la kupata mume utazidishiwa.

  Zingatia ushauri wa wanawake wenzako pia akina kama Imani na wengine walikushauri hapo juu, nao ni wanawake kama wewe,bila shaka wanazo hisia za vile unavyojisikia maana nao ni wanawake kama wewe.

 12. Mungu wangu wa mbinguni akupe rehema dada Paulina. Sikia dada hata ukiombewa kwa kuwekea mikono hadi miguu na watumishi wakubwa unaowajua wewe hautafunguliwa mpaka wewe mwenyewe ujitowe kwa kunyenyekea mbele za mungu… Kwa mungu hakuna shortcut hilo ulijue. Na wewe mwenyewe una kibali cha kujiombea,kuombea wengine kuponya n.k.Soma Lk 10:19. Mt 21:21-22. Ushauri- tubu, omba rehema, acha dhambi ikiwemo hiyo ya uzinzi, tafuta kujua habari njema na ahadi za mungu juu yako, kwa kukaa chini ya mtumishi wa mungu ambaye atakuwa kama mzazi wako wa kiroho, naye atakufundisha namna ya kumsogelea mungu. Huyo mtoto asikuumize kichwa sana, na nadhani wewe husomi biblia, biblia ina majibu yote jitahidi sana kusoma japo mstari mmoja kilia siku na kuutafakari. Ndani ya biblia hakuna huo mstari unaosema kuwa kuzaa watoto na baba tofauti ni dhambi kubwa… hilo ni wazo lako na shetani amekukamata nalo, sikia ndugu ktk biblia kuna watu walizaliwa matumbo mbalimbali na viuno mbalimbali , chukua hatua.Ebu soma Hos 4:6 unasema Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, kwakuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi,kwakuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Sasa maadam umeomba ushahuri usikatae maarifa unayopewa. Usiogope ukifanya maamuzi na kutulia mbele za bwana Roho wa mungu atakufunulia juu ya mumeo na mengine mengi tu.. na km huyo uliyenae ndiye atampa wepesi wa kukuoa kisheria. Hata sisi tulipita huko but kwa sasa tunakula bata ndani ya yesu kwa raha zetu tukiwezeshwa na nguvu za mungu. Ebu soma… Yoe 2:12-14, Rum 8:14-17 na 26,27 Rum 12;1-2, Lk 12:2-3, Gal 5:i6-26, Mk 9:23 na 29.

 13. Tumsifu Yesu Kristo, Nawashukru wote walioweza kuchangia kwa namna yoyote ile naona maswali ni mengi sana! Yote nimeyapokea! mimi ni mkristo wa kawaida tu kama binadamu wengine kama msaada wenu ndio huo pia nawashukru! sijajua vizuri kumwombea mtu mpaka huyo mtu awe ameokoka? ndio awekwe katika maombi.? kutenda kosa si kosa ila kurudia kosa ndio kosa, Nakubali nilikosea kwa akili ya kibinadamu! sasa nifanyeje? kuomba peke yangu haitoshi ama inatosha? lakini ukimshilikisha na mwingine hamwezi kuchoka! Kwa namna ya pekee nawashukru sana! na Mungu awabariki.

 14. rafiki yangu Pauline, nipigie au tuma ujumbe mimi nitakupigia kwa namba 0784265555 ili niweze kukupa ushauri wa kiroho, karibu sana. Mungu ni mwenye rehema na ni mwingi wa fadhili, njoo tuzungumze.

  Anatolia Edward

 15. Shalom wapendwa,

  Dada Pauline tunahitaji utusaidie kujibu baadhi ya maswali hapo juu.

  Kwa jinsi nilivyosoma post hii nimeona kama bado hujaokoka, so nitachangia hv;

  a) Jikabidhi kwa Yesu kwanza; kwa kuokoka, ukiweza anza kuhudhuria mafundisho ya kukulia wokovu, uanze kukua kiroho na kumfahamu Mungu kwa undani zaidi. Ongea na watumishi kwa undani zaidi wakupe msaada wa kina.

  b) Ukishampokea Bwana Yesu, tuna amini utakuwa kiumbe kipya na unaanza mfumo mpya wa maisha ambao Bwana Yesu ndiye kiongozi wako.

  c) Kwa kuwa hamkufunga ndoa, nadhani haitakuwa sawa kuendelea kuishi pamoja baada ya kuokoka. Acha Mungu mwenyewe ashughulikie hitaji lako la kuolewa. Kama huyo uliyenaye ni wako kweli basi acha amrejeshe kwa njia zake safi. Kama siye Yeye basi atafungua njia nyingine.

  Ila nashauri ungepata msaada kwa watumishi wa Mungu ana kwa ana ili uweze kupata uongozi kwa kina. Maana natambua hapa si rahisi kuweka wazi kila kitu na kujua undani zaidi.

  Barikiwa

  Dada Imani K

 16. Sungura hukunielewa, kwanza mie ni mtu mzima kimwili na kiroho, tangu nimezaliwa, sijawahi kuuliza mtu yeyote swali kama hilo, tangu nilipoanza kumtumikia Mungu, leo ni miaka 32 sijawahi, na sitauliza mtu swali kama hilo hata kidogo. Nimeeleza vizuri hapo juu, kuwa wapo watu wanachukua, kuishi pamoja, wameokoka, au mmojawapo, ni yangu ilikuwa tuwasaidie watoto wetu hata namna ya uchumba unaanzaje? Unaanzia wapi, yapo makanisa ambayo washirika wanaamua wenyewe kukaa pamoja, kisha wanapeleka taarifa kwa mchungaji kuwa sisi tumeshaamua, mchungaji anaunga mkono, anabariki hayo maamuzi yao, ndugu Sungura kuishi kwingi ni kuona mengi, Lisemwalo lipo, kama halipo laja. Naona ulinielewa vibaya sana, nirudie tena, sijawahi kuuliza na sitauliza swali kama hili, ili iweje. Na kama hata Paulina alinielewa hivyo, amenielewa vibaya, sikumaanisha hivyo. Naomba uwe na amani ndugu yangu. Shaloom.

 17. Ndg Samuel, unataka Pauline aseme kwa mfano hivi; “Siku moja jioni nilienda nyumbani kwa Y, tukaanza kushikanashikana, nikajikuta nimeishiwa nguvu, akaniingiza chumbani ,matokeo yake tukafanya mapenzi(tukajuana kimwili)”

  Unataka kujua mchakato/process ilivyokuwa mpaka wakajuana kimwili/wakafanya mapenzi?

  Au ulimaanisha nini katika hili swali, nanukuu “mlianzaje mahusiano yenu ya kujuana kimwili bila kufunga ndoa?”

  Kama ulimaanisha kutaka kujua kitu kingine tofauti na ninachosema hapa, basi niseme kwamba sijakuelewa unachotaka aseme.

  Lakini kama ni hicho si sawa akiseme hapa hadharani,wengine hatuhitaji kujua yote hayo ili kumsaidia. Maana wengine sasa watataka aseme walijuana kimwili mara ngapi n.k.
  Ndio maana nikasema nashauri anayehitaji maelezo yote hayo wawasiliane naye kibinafsi.

  Katika hili hatuhitaji kulumbana ndg yangu, ila ni kumsaidia Pauline.

  Asante.

 18. Ndugu Sungura, najua kuwa wazo lako ni zuri kumhurumia dada yetu Paulina, lakini napenda ujue kuwa aliyetaka maombi ni PAULINA, aliye na shida ni Paulina, ambaye hakuona aibu mpaka akasema hayo ya kuzaa ni Paulina, aliye na jipu ni Paulina, aliyeulizwa Swali ni Paulina, ambaye angeona ni la ndani chumbani ni Paullina. Wewe unamkingia wakati ameeleza wazi kuwa waliishazaa, hakuona aibu, wewe ndiye unaona aibu. Wakati mwingine nadhani tutumie hata mithali za kawaida maana zipo kusaidia watu.PILI USIZOKULA ZINAKUWASHIA NINI. Ndg yangu jipu ni ugonjwa, kumkamua mtu jipu ni maumivu sana kwa anayekamuliwa, lakini ndiyo dawa ya jipu, mpaka kiini kitoke, ndiyo maana Biblia ikasema, Jeraha za watu zinaponywa juu juu. Niliuliza nikiwa na maana, wako watu wameokoka wote, wanaanguka dhambini, na wanachukuana wanaishi ama pamoja, au mbali mbali wanaendelea kuzaa, ama mmoja ameokoka na mwingine hajaokoka, wanachukuana wanakaa pamoja, au wanakaa mbali mbali huku wakiendelea na dhambi hiyo, wakati mwingine unakuta Mchungaji hamwambii au hawambii. Wakati mwingine akitaka kuwaambia wanajitokeza akina DIOTREFE.

  111 Yoh 1..9…10. Nililiandikia kanisa Neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza( kimbele mbele) kati yao hatukubali, kwa hiyo nikija nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu, wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa. Ndugu yangu, pengine utasema tena kuwa ninaandika sana, unajua kama hayakusaidii haya mengi yupo mtu yanamsaidia. Si unajua hata Paul alihubiri sana siku moja mpaka usiku wa manane, wapo watu walikuwa wanasaidika , lakini Eutiko alikuwa amesinzia, hayakuwa yanamsaidia, mwisho alianguka kwenda nje, kumbe sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa nje. Ebu mwache Paulina ajibu maswali anayoulizwa mwenyewe, aseme yeye mwenyewe kuwa anaona aibu, na sijui ni aibu gani, maana kama Biblia haioni aibu, mwanadamu ataonaje aibu? Tuwe makini roho iliyokuwa ndani ya Diotrefe isije ikatutumia, tukawa vimbele mbele, tukawasemea watu hata tofauti na mawazo yao, na hawajatutuma kuwawakilisha, hata wazazi wa kipofu japo wao waliulizwa swali. Huyu ndiye mtoto wenu aliyezaliwa kipofu? Amepataje kuona? Ndiyo ni mtoto wetu, alizaliwa kipofu, ila swala kuona Muulize mwenyewe. Ebu wajisemee, acha Paulina ajisemee. Sungura rafiki yangu ubarikiwe.

 19. Samuel umeuliza maswali mazuri kutaka kujua kama dada ameokoka na mwenzake pia.

  Lakini lile swali la tatu (” Kama wote mmeokoka mlianzaje mahusiano yenu ya kujuana kimwili bila kufunga ndoa?” ) siyo. Details unazozitaka hapa rafiki yangu ni za chumbani sana,kiasi kwamba ni kumpa kazi ngumu sana dada kuzisema kwenye public kama hii. Labda kama unazihitaji kwa ajili ya ushauri tafuta kuwasiliana nae kibinafsi

  Barikiwa.

 20. Dada usijilaumu sana,wala kujuta sana. Wewe si wa kwanza kuwa katika hali kama hiyo,na kwa kila tatizo kuna njia ya kutokea.

  Kwa maelezo yako unachotka kutoka kwetu wana blog ni kukuombea ili huyo jamaa akubali kukuoa, wala hujajitokeza hapa kutaka msaada kuwa ufanyeje katika hali kama hiyo.

  1.Unasema kuwa ungependa kuhamia kwake lakini unaona aibu.
  2.Una wasiwasi maana umri wako umeenda
  3.Unaogopa kuzaa mtoto na mwanaume mwingine ni kutenda dhambi juu ya dhambi

  Kwanza nikupongeze kwa kutambua kuwa kitendo cha kukutana na huyo jamaa kimwili na mpaka mkazaa mtoto ni dhambi na kwamba usingependa kurudia hiyo dhambi na mwanaume mwingine.

  Piili ningependa kukuambia kuwa hauhitaji maombi ili huyo jamaa akuoe, bali unahitaji ushauri wa kukutoa katika hilo shimo na kukupa mwanga mwingine. Pia unahitaji ushauri na maombi ya kukutoa katika ugonjwa w hofu ya umri ambao unawasumbua akina dada wengi sana ambao wanadhani umri wao umeendelea sana.

  Na hilo suala la umri ndio limeibua hoja niliyoipa namba moja na namba mbili hapo juu wala si kwa sababu ya upendo ulio nao kwake.

  Napenda uamini hiki nikuambiacho,maana mimi ni mwanaume pia anayejua hisia za kiume juu ya mwanamke. Kwa hiyo pokea hii kutoka kwenye moyo wa mwanaume ambaye anakwambia ukweli ambao huyo jamaa hawezi kukwambia mwenyewe.

  Ni kwamba huyo jamaa hakupendi hata kidogo zaidi ya kwamba ana hisia tu za kingono juu yako. Ni kwamba, hicho anachokufanyia mwanaume huwa anakifanya tu kwa mwanamke ambae hampendi. Wala usipoteze muda wako na machozi yako,na kuumiza magoti yako kuomba akuoe. HAKUPENDI. Labda tukuombee ili Mungu akupe nguvu ya kuachana nae maana najua moyo wako umenatishwa kwake.

  Baada ya kusema hayo, ningependa sasa ujibu swali alilouliza Samuel hapo juu kuwa Je wewe umeokoka na yeye ameokoka?

  Usiogope, hilo tatizo Mungu anakwenda kulimaliza na kukuweka mahali pazuri.
  Amini

 21. Dada Pauline pole sana,
  nachoweza kukiona hapa ni kama unampenda sana mwenzio lakini yeye hakupendi kwa kiwango kilekile, maana kama mngekuwa mnapendana kwa kiwango sawa angejali maumivu yako pale unapomuuliza kuhusu kufunga ndoa, na angeheshimu hisia zako kuwa muda wote huo unaomuuliza kuhusu future yenu. Mimi kwa upande wangu ninachoweza kukushauri ni kwamba jaribu kutulia utumie muda wako mwingi katika maombi ili umwulize Mungu kama huyo kweli ndiye mume wako, pengine unapoteza muda tu na mtu ambaye sio ubavu wako. Kuzaa nae sio kibali cha kuhalalisha awe mume wako, huenda Mpango wa Mungu ni kukupa mume mwema ila kwa kuwa wewe umewekeza muda wako na akili zako na hisia zako zote kwake ndio maana unahisi eti kwa kuwa umezaa nae ni lazima huyohuyo ufunge nae ndoa. Tulia miguuni pa Mungu nae atakuondolea maumivu yako na mahangaiko yako ya moyo.

  Dada yangu nimeandika hivi kwa kuwa mimi pia nilipitia maumivu karibu na yako,Nilikuwa katika mahusiano na kijana wa kiislamu kwa muda wa miaka 7 ingawa sijazaa nae mtoto, ila kwa kipindi hicho chote nilifungwa sana, maana niliona dunia nzima hakuna mwanaume mwingine zaidi yake, na ni kweli alikuwa mtu mstaarabu, mkarimu na alikuwa na sifa zote ninazohitaji ndani ya mwanaume, lakini alikuwa muislamu, ni mpaka pale neema ya Yesu Kristo ilipoingilia kati ndipo nilipokuja kujua kuwa njia niliyokuwa naiendea haikuwa sawa, na ikabidi mimi mwenyewe nichukue jukumu la kumuacha, haikuwa rahisi nililia usiku na mchana nikijiuliza kwani Mungu si ni mmoja, kwa nini niteseke hivyo, lakini Neema ya Mungu ni kuu mno. Mpaka sasa nimeweza kusimama na Yesu, nimesharecover na sasa imani yangu ni kwa Mungu tu, na najua hakuna lisilowezekana kwa Yesu, na naamini Mume nitakayepata atanifanya niione ile miaka 7 niliyopoteza nilikuwa mjinga! Kwa hiyo dada tulia na Yesu, yeye atakuondolea mahangaiko yako yote ya moyo!!

  Mungu akusaidie, na neema ya Mungu isikupungukie ukae katika uwepo wake!

 22. Shaloom! Dada pole sana, naungana na wewe katika maombi. Najua ulifanya kosa kuzaa kabla ya ndoa mbaya zaidi na mtu ambaye hakuwa na muelekeo chanya na wewe. Ninaamini kosa hilo unalijitua. Mimi ni mwanamke kama wewe na ninajua unavyojisikia. Najua tamaa ya moyo wako ni kuolewa na mchumba wako ambaye ulimpenda na mkabahatika kupata mtoto lakini nina wasiwasi na mwenzako kama ana malengo kama yako. Swala hapa si kuokoka au kutookoka maji yameshamwagika hayazoleki kwa hivyo tunatakiwa kumshauri dada yetu nini afanye baada ya kukaa kwenye uchumba sugu kwa miaka 12. Mimi nakushauri msimamo wako wa kutohamia kwake endelea nao na ikiwezekana anza maisha upya ukiwa na YESU ndani yako, naamini kwake hakuna jambo lisilowezekana. Namaanisha tuliza akili yako, muombe MUNGU naamini atakupa mchumba mwingine ambaye utafanana naye. Huyo uliyezaa naye fanya ni kama bahati mbaya, endelea na maisha yako. Wanaume wa aina ya baba mtoto wako wapo wengi, hapo anachosubiri ni anakuvizia ukosee jambo ili apate sababu ya kukuacha kabisa. BE BLESSED!

 23. Standing FIRM and MOVING FOWARD!

  THE POWER OF POSITIVE THINKING

  Hivi huyu dada kuomba ushauri kwenu unadhani amekosea?
  kwani sisi humu siyo wachungaji?
  Hivi huyu dada kukiri dhambi zake mbele yenu mnadhani hakiri dhambi hiyo mbele ya MUNGU?

  Jicho letu la Rohoni Yamkini tunaona kama dunia hii inavyoona na kutafusiri?

  DADA PAULINE kama moyoni mwako unashuhudiwa huyo ni mmeo ANGALIA ROHO MTAKATIFU ANACHOKUSHUHUDIA KWA AJILI YA HUYO?

  KWA AJILI YAKO ITAMPONYA KAKA HUYO,KAMA UMEMJUA YESU YEYE BADO

  1 WAK 6.14..18 INAHOJI WALA SIYO KUWA INAHITIMISHA! MBONA TUMEOKOKA MBADO TUNASHIRIKIANA NA WASIOMJUA YESU? BASI TUNGETENGEWA SEHEMU YETU TULIOKOKA? JE KAMA MMEOANA MMOJA AKATANGULIA KUMJUA YESU(AKAOKOKA?) JE HUYU NAYE AMUACHE MUME/MKE WAKE KWA KUWA HAJAOKOKA? ROHO MTAKATIFU TUSAIDIE NAPO HAPA TUMEKWAMA.!

  DADA NAKUULIZA SWALI BADO MNAENDELEA KUZINI AU MNAKAA KAMA MUME NA MKE KWA MIAKA 12 HAMJAFUNGA NDOA?

  KAMA UNAMPENDA YESU, ANZA KUOMBA KWANZA WEWE MWENYEWE NDIPO UOMBE MSAADA SIYO WENGINE WAOMBE MZIGO WAKO WAKATI WEWE UJAGUSWA

  SOMA MWANZO 30:11-15 NA MATHAYO 7:24 JE UMEJENGA MSINGI WAKO KWA YESU AU KWA WANADAMU?

  TAFUTA KITABU CHA “THE POWER OF POSITIVE THINKING” BY NORMAN

 24. Shalom Pauline
  pole kwa yanayokufika,pamoja na hayo naomba nawe ujikague, sikiliza mausia waliyokupa hapo juu, pia usiwe mwepesi sana wa kuingia mahusiano ya kimwili na watu bila ndoa maana naona unasema unahofia kuzaa na mwingine kivipi?
  Mwombe Mungu kama huyu ni mtu wako kweli mtubu mumrudie Mungu na kufunga ndoa hata bila sherehe lakini muape mbele za Mungu kwa watumishi wake. Kama si mtu wake aliyekuchagulia Mungu muombe akupe ujasiri kukataa mahusiano hayo na kuanza upya ndani ya Kristo. Huyo kwa sasa usimhesabu kuwa mume na kumpa haki zote za mwili wako, hivyo jione uko huru kuomba Mungu akupe mume mwema na wewe uwe tayari kutubu na kusimama ktk neno au njia yake kwa kumpokea Yesu ktk maisha yako. Ulimwenguni kumejaa matapeli na watu katili utaendelea kuumiza moyo wako bure uje uikose mbingu na hata kumharibia future huyu mtoto wako. Kabidhi maisha yako kwa Yesu sasa na atakupa haja za moyo wako na amani ktk maisha yako. Ubarikiwe sana.

 25. Dada yangu pole sana! miaka 12,ha! si jambo jepesi. lakini ningependa nikuulize, je mtu huu unampenda kweli? je unauhakika kwamba naye anakupenda?
  Elewa jambo hili, ndowa sio shelehe baali ni mapatano kati ya watu 2. Ndiyo umeisha zaa naye kinyume na sheria lakini nanahofia kwamba dhambi inaweza kukuwa na ikaja kuwa kawaida na baadaye ikawaletea baraa! Ninaomba umuendee mchungaji wako na atakusaidia la kufanya. ujuwe ndogo ndogo huumiza tumbo.
  Ubarikiwe na Mungu akusaidie

  Kaka yako ktk Kristo kutoka Burundi

 26. Dada Paulina, Shaloom, ili tuweze kukuombea, ebu uwe wazi, ujibu hili ninalookuliza. Katika Biblia Ikor 6..14…18 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawa sawa, kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na Sanam? Kwa mama sisi tu hekalu la Mungu alizehai, kama Mungu alivyosema, ya kwamba, nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu, kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha, Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike. ( Biblia inaeleza kama mtu ameokoka anakuwa Nuru, asiyeokoka ni giza, aliyeokoka ni Hekalu la Mungu, asiyeokoka ni Sanam) nimesema uwe wazi na tutajua jinsi ya kukuombea. Je umeokoka ? Je mwenzako ameokoka? Kama wote mmeokoka mlianzaje mahusiano yenu ya kujuana kimwili bila kufunga ndoa? Ebu uwe wazi, pia itakuwa msaada kwa watu wengine. Ubarikiwe.

 27. Mungu ni mwenye Rehema Sijui kama unajua ulikosea kuzini kabla ya ndoa? na uliamua kuukabithi mwili kwa mtu ambaye si mmeo so ushauri ndoa si kuvaa gauni jeupe bali ni patano la kweli kwa watu wawili na kristo akiwa kati, endelee kumwomba Mungu atakusaidia akufungulie milango.

 28. Dada pauline,
  Inaonyesha mwezako ni asiyeamini utafungiwaje nira nae?
  au nimekuelewa sivyo?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s