Maelfu ya watanzania wampa Yesu maisha yao ndani ya Love Festival Tanzania

Kwa Mara Ya Kwanza katika Historia Ya Gospel Events Tanzania, Tanzania Love Festival imefana kwa Kiwango cha hali ya Juu sana.

Muinjilisti Andrew Palau ambaye amehudumu kwa siki Mbili katika Viwanja Vya jangwani amekaribia kuvunja record ya Peter Youngrey kwa upande wa Mahudhurio Ya Watu.

Katika Siku Ya Kwanza yaani ya Jumamosi, Kivutio Kikubwa alikuwa Don Moen pamoja na Masanja Mkandamizaji. Mbali na hao Wanamuziki Upendo Kilahiro, Christina Shusho wamedhihirisha wao ni Next Level katika Anga za Uimbaji wa Kimataifa. The Voice ambao wametokea kukubalika sana katika Kizazi Cha Sasa wameendelea kupasua anga la Uimbaji Wa Kimataifa Kwa aina ya Muziki wa Accapella.

Lubben, Nicolla na Don Moen wameonesha Ukongwe wa Muziki Wa Kimataifa kwa kuimba nyimbo zao ambazo zimeonekana kukubalika sana katika Nchi Ya Tanzania na Kuimbwa Na Watu wengi waliohudhuria.

Mbali na burudani hiyo ya Muziki Maelfu Ya Watanzania Wamempa Yesu Maisha yao baada ya kusikia neno lililohubiriwa na Mtumishi wa Mungu Andrew Palau.

 Professional Gospel Singer Upendo Kilahiro akiwa Juwakaani 

 International Singer Christina Shusho akisukuma wimbo wa “Thamani Ya Wokovu” Ulibamba sana

 Lubben On The Stage

 Watu waliohudhuria

 Nicolle

 Don Moen akiwa On The Stage

 Ze Blogger akiwa na Nicolle

Upendo Kilahiro na Christina Shusho  wakiwa na Nicole C Mulen

 Tanzania Love Festival Praise Team

 The Voice wakiwa na Don.

Mchungaji Mtarajiwa Masanja Mkandamizaji alikuwa kiburudisho kwa wahudhuriaji

 Wahudhuriaji

The Voice wakiimba

Michezo ya pikipiki ilikuwa kivutio

–Sam Sasali blog

Advertisements

16 thoughts on “Maelfu ya watanzania wampa Yesu maisha yao ndani ya Love Festival Tanzania

 1. These two comments from ” Esther Elias and Baika Mwessy, appears to be offensive, radical and outrages as far as the post is concerning. may be it is their own opinion on the matter

 2. Baika umesema kweli kwani kila kitu ni dar hivi unapoendelea kumuhubili ambae alisha hubiliwa wakati kuna ambao hawajapata hiyo bahati unakuwa unamaanisha nini, tubadilikeni wapendwa hata sisi tunahitaji hayo matamasha tubarikiwe. wako wengi watakaopokea wokovu kupitia hayo matamasha. na MUNGU atatukuzwa.

 3. SIku nyingine andaeni tamasha la hivyo jijini Mwanza kwani kila kitu ni dar / arusha – ina maana mwanza au mikoa mingine hakuna watu wanaohitaji kuokolewa? Waandaaji acheni ukora.

 4. kwa kweli Mungu alionekana, injili ilihubiriwa watu waliokoka, mimi pia nilipata nafasi ya kuhudhuria siku zote mbili za festival, pia binafsi nilifurahi sana kuona michezo ya kuruka juu na pikipiki, yaani, it is amazing, the way they play with motor cycle, hii michezo inaitwa acrobat, vitendo vikali, nilifurahi sana

 5. Sifa,heshima na mamlaka tunamrudishia Mungu kwa ajili ya tamasha hili,kweli Yesu alijidhihirisha Jangwani,kuanzia neno hadi uimbaji ulibariki sana.

 6. Utukufu kwa Mungu
  uzuri wake ni kushirikisha makanisa wenyeji wote ili muweze kuwaongoza waliokoka ktk mahema yenu kwa malezi zaidi. Mungu awabariki kwa kujitoa kuvuna watu ktk Taifa letu hili.

 7. Bwana Yesu asifiwe!ninafu rahishwa na mtindo mzuri wa injili.kama ingekuwa inaandaliwa kwa kila pembe ya inchi,uamusho unge uteka ulimwengu.

 8. @millinga,

  hawa jamaa walipita makanisani wakihimiza watu wafundishwe jinsi ya kulea wongofu wapya watakaopatikana mahali pale, hivyo ni jukumu lako mimi na wewe kama wakristo tulikomaa kuwasaidia hawa wapya kwa kila hali, hasa mara unapomsikia kaokoka msaidie sana.

  barikiwa

 9. Glory to God,
  AmA hakika hii sijawhi kuona,utukufu tunamrudishia yeye aliyewatuma wakaihubri injili kwa kila kiumbe,nzuri zaidi Mungu alivyokwisha kuwabariki hata sadaka hatukutoa nikashangaa sana,maana tumezoea mikutano mikubwa kama ile tunaambiwa mwenye laki moja apite mbele aombewe baraka,kweli walipata bure wametoa bure,neno la Mungu haliuzwi kwao,GOD bless u Andrew Palau and others, hizi ni siku za mwisho watakatifu wazidi kujitakasa na waovu waendelee kutenda uovu,kama ulikuwa pale hujampokea Yesu lazima ukimbie upesi kumpokea.amen

 10. Wasiwasi wangu uko kwa wale wanaompokea Yesu tu. Hivi wamepata mlezi au wanarudi kule kule kwa jana? Hivi hawa wanaye wa kuwalea kwa mafundisho na uongozi wa kiroho? Nani anawafuatilia ili wasirudi nyuma? Nani anawapa mausia ya kushinda vita ya kiroho baada ya kukiri wokovu? Mafundisho gani watapata, nani atawapa?

  Unnnnnhu, mhuuuuu, sielewi mieeeeee.

 11. kweli hawa watu Mungu amewabariki mno na amewapa ufunuo wa ajabu kwasababu walikuwa kila wakati wanawaongoza toba watu kwa staili tofauti tofauti. Kweli kwa Yesu kuna raha, mi raha nazozipata sasa ni kubwa kuliko nilivyokuwa sijaokoka, karibuni sana kwa Yesu ambao bado hamjamjua

 12. Whaoooh!
  Glory to God. Asante yesu kwa kazi njema yenye mbegu na matunda mazuri ya kudumu.
  Watumishi wa Mungu wote mlioshiriki kwa namna zote mbarikiwe.
  Hii ilikuwa ya kipekee sana, nimeipenda sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s