Miradi Ya Kanisa

Makanisani wamekuwa wakitumia njia ya MICHANGO au kuomba MISAADA ili kuweza kutimiza mambo yanayohitaji pesa. Misaada mingine imekuwa ikiambatana na masharti POTOFU na Wachungaji wengine KULAZIMIKA kuwapendelea watoaji wakubwa wa michango kanisani. Je, KUNA UBAYA GANI kwa makanisa kuwa na MIRADI inayoweza kuzalisha PESA pia kutoa AJIRA ya kimwili kwa waumini au washirika wa Kanisa husika? Mfano kanisa laweza fungua Supermarket, kumiliki “bodaboda”, tax,; miradi ya ufugaji, benki, visima, kilimo nk??

Advertisements

10 thoughts on “Miradi Ya Kanisa

 1. Hakuna ubaya Kanisa kuwa na miradi, Wapendwa tusiendelee kuwa ombaomba; nimefurahia sana nilipokutana na mradi wa Mkombozi Bank – unaomilikiwa na RC, wengine tuige, tusiendelee kuwakamua waumini wetu kila siku.

  ________________________________

 2. Jambo la kanisa kuwa na miradi ili kujiongezea kipato laonekana ni jema. Pesa zinapokuwepo, mambo mengi yaweza kufanyika, haswa katika ulimwengu huu wa miradi.

  Lakini, kanisa, ktk maana ya kusanyiko, linapojiingiza ktk miradi ili kuweza kujikimu, linakuwa limepoteza sifa ya kuwa ‘Mwili wa Kristo’!¬†

  Kila jambo linalofanyika ktk ulimwengu wa mwili, huwa linaongozwa kutoka ulimwengu wa roho. Kwa hiyo, kanisa litakapoingia ktk miradi, ili kufanikiwa ni lazima principle zinazoongoza mambo hayo zifuatwe, pamoja na sheria zinazoongoza utendaji wake. Ushindani wa kibiashara pamoja na hila zake, utatuzi wa migogoro nk, lazima viwemo katika strategies zake katika ujumla wa utendaji wake na mambo mengi mengine ambayo yatafanyika chini ya mwamvuli wa “Utakatifu wa Kanisa”!

  Mradi mmoja uliofanikiwa huzalisha miradi mingine. Nalo kanisa huwa ni “mama” wa miradi hiyo, likiilea, kuikuza na kuilinda isidhurike. Mwisho wa siku, kama zilivyo biashara endelevu zote, huwagharimu waendeshaji, kwani mafanikio huwaletea sifa, nao mzigo wa uendeshaji, ktk maana ya kukuza mitaji huwaangukia waumini na kulazimika kuendelea kubeba mapungufu ya miradi hiyo. Basi orodha ya michango/sadaka huongezeka kadiri ya miradi, kuanzia januari hadi desemba! Waumini huingizwa ktk utumwa wa miradi na mashindano yake bila kujijua. Basi KANISA LOTE HUWA MRADI!!

  Kama ilivyokuwa kwa Israeli pale nao walipotamani kuwa kama jirani zao wakataka nao wawe na mfalme atayewaongoza vitani! Wakiwa wameukataa uongozi wa Roho Mt ktk kuwatimizia mahitaji yao, sasa wakitafuta namna ya kwao wenyewe kujitimizia mahitaji yao ktk miradi. Yaani wakijiingiza na kujiweka chini ya ‘mungu wa miradi’ – Mammon!!!

  Lakini kwa upande mwingine kanisa lapaswa kumtegemea Mungu kikamilifu ktk ustawi wake. Kusanyiko, yaani individuals, hubarikiwa na Mungu ktk kila walifanyalo ili liweze kurejesha sadaka na zaka ktk ukamilifu wake na kwa furaha. Walawi ambao huwakilisha kanisa, hawakupewa urithi wa nchi (miradi), bali wao walijumuishwa ktk ustawi wa kanisa kwa kulisimamia na kuliongoza ktk njia ya Mungu na mambo yote yaliishia hapo.

  Kwa hiyo mapinduzi ya mifumo ya kiuongozi yanahitajika ili kulirudisha kanisa ktk nafasi yake ya kwanza, yaani kuwa chini ya uongozi mkamilifu wa Roho Mt., ili liendelee kuwa baraka kwa kusanyiko, badala ya nafasi hii ya sasa ambayo inaleta manung’uniko mengi ya chini chini kwa wafuasi wake wakiilalamikia “miradi mingi” na tozo linaloambatana nayo, kwa jina la Injili!

  Mbarikiwe nyoote, kadiri mnavyolitafakari jambo hili ktk Nuru ya Injili!

 3. Bwana Yesu asifiwe.
  Wapendwa wana strictly gospel blog.
  Asante kwa wale mnaojitahidi kuniandikia emails kutaka maelekezo ya namna ya kupata nafasi za kuingia chuoni na hasa vijana waliokokoa.
  Kila mmoja anaweza kuomba siyo tu kwa wakristo.Ila mimi nilihamasisha waenda mbinguni nao wasibaki nyumba.

  Naomba kama ukichelewa kupata ufafanuzi kupitia email hii
  Unaweza kuniandikia kwa au
  Pia unaweza kunipata kirahisi kwa namba +255 755 29 66 74

  Unaweza kuwasiliana na ndugu Craig wa MUM university moja kwa moja kwa email
  Naomba mjadala huu tufunge ili nianze kukuletea masomo maana ni muda mrefu sijakuletea mafundisho.
  Mungu akubariki sana!!

 4. Hi.This is the mobile number for Rev Norbert from Pentecost Church Arusha (Oldadai Branch)
  Call him at +255 755 29 66 74
  Rev Norbert is responsible to help you with instruction in Tanzania.
  He is an agent for MUM university based in Iowa-U.S.A

 5. Mpendwa Mchungaji Norbert,nawezaje kupata email yako?au ndugu zangu wa strictly gospel wanaweza kuwa nayo? Huduma yako ni muhimu sana kweli kwa waenda mbinguni na hata wale wasiomwamini Mungu wanaweza kujifunza juu ya kile unachokifanya kupitia kanisa lako la Pentekoste,Hapo Arusha mnapatikana Oldadai eneo gani?

  Kwangu huo ni muujiza mkubwa.
  Swala la kupata sponsorship was big issue for me.I thank you and God for giving me this special chance….am now in a position to join at mum uinversity withought paying any coin.Fantastic.Tanzania inao watu hatujajua kumbe!!!!!!!!!!!
  Joel

 6. Mpendwa mtumishi wa Mungu Norbert.
  Nimefurahia kupata nafasi ya kuomba ufadhili katika chuo kikuu cha MUM
  Nilitamani siku nyingi kusoma masters in accounting lakini nilikosa fedha.
  Nimeanza mawasiliano na MUM na mwelekeo ni mzuri.
  Ubarikiwe mno!! nami nawaomba wakristo wasiache kuomba kuomba MUM kwa kuwa nafasi zao hazina mizengwe.
  Joyce Robert

 7. Bwana Yesu asifiwe sana!!
  Ni rafiki yako Rev Norbert wa kanisa la Pentekoste Arusha(Kituo cha Oldadai
  Nakushukuru wewe ambaye umenitumia shukrani kwa kupata mlango wa kusoma chuo kikuu cha MUM na kupata dalili za kufanikiwa kuingia chuoni.

  Naomba niwaelekeze siri ya kupata nafasi hizi usisahau kuandikia agent number ambapo kwa Tanzania ni TZA-001 hii itakusaidia sana!

  Pia unapoingia internet hakikisha kama wewe unaomba ufadhili kwa ajilli ya masters in computer science andika http://www.mscs.mum.edu
  Na kama unaomba masters in MBA -accounting andika http://www.mum.edu/accounting

  Wale wa bachelors niliwaeleza kwamba tembeleeni tovuti ya chuo http://www.mum.edu
  Ndogo zangu ni kuhakikisha hakuna mwenda mbinguni anaye nyanyaswa kwa sababu ya hali yoyote ya uchumi aliyonayo.
  Wapendwa wana strictly gospel,vijana na wanazuoni wengine tufunge na kuomba ili tuhakikishe watanzania wengi wanapata nafasi katika chuo hicho kwa sababu wengi wa wasomi wetu wako mitaani na hawana ajira yoyote.Inauma ni aibu ,Shetani anatucheka,kutubeza na kutuonea.
  Biblia inasemaje?sisi si mikia bali ni vichwa.
  Tushikamane sote waenda mbinguni,tusaidiane il adui akunje mkia.
  Mbarikiwe na Bwana Yesu.

 8. Ni Rev Norbert Mbwiliza wa Kanisa la Pentekoste Arusha (Tawi la Oldadai)
  Namshukuru Mungu kwa wapendwa wenzangu katika blog hii umekuwa ukiniombea kwa kipindi chote ambacho sijasikika katika blog hii kwa sababu za safari.

  Leo naomba nikukaribishe wewe mpendwa mwenzangu ambaye umekuwa ukitafuta nafasi za kusoma masters au bachelor ukakosa kwa sababu za kiuchumi.Mungu ametoa nafasi katika chuo Kikuu cha MUM kilichop IOWA-USA hawa watumishi wameanza kupokea maombi hasa kwa wale wa masters in accounting na computer science.
  Tafadhali naomba ujaze online na uwahishe.
  Kwa masters ya computer science andika http://www.mscs.mum.edu
  Na accounting andika http://www.mum.edu/accounting
  Kwa wale wa bachelor fungua http://www.mum.edu ili one kozi inayokufaa.
  Mimi ni certified agent wa MUM nakupa habari ya kutoka jikoni,natamani nione wapendwa wakipata nafasi baada ya adui kuficha mikopo mingi ya waenda mbinguni.
  Nipigie kwa ufafanuzi 0755 29 66 74

 9. mmmmm ngoja mie nijifunze kitu hapa huwa nashangaa kwanini hamna hivi vitu, sio kanisa kwa maana ya mikusanyiko ya kuabudu tu, mie nadhani hat akati yetu wapendwa kunahitajika miradi ili kujiinua na kuwezeshwa kupeleka injili. Kwa kweli kanisa liko hoi ktk mambo ya kumiliki na hivyo kuwa wanaegamia zaidi waumini au kutegemea kuombaomba. Hebu tumwombe Mungu atupe hekima na nguvu ya kutenda haya. Mbarikiwe

 10. HAKUNA UBAYA WOWOTE KWA KANISA KUANZISHA MIRADI YAKE KWA MAENDELEO YAKE KULIKO KUBAKI KUTEGEMEA ZAIDI WAUMINI.
  NAPENDA KANISA LIWE NA MFANO WA MTUME PAULO AMBAYE HAKUTAKA KUMTAABISHA MTU YEYOTE KATIKA KUPEWA CHAKULA BALI YEYE MWENYEWE ALIFANYA KAZI ILI APATE PESA ZA NAULI KUHUBIRI INJILI YA YESU PIA APATE PESA ZA KUJIKIMU KWA CHAKULA.
  ITAKUWA NI FAIDA KUBWA KWA AJIRA KWA WASIONAYO AJIRA MIRADI IKIANZISHWA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s