Uchumba na madhehebu!

Napenda kuuliza je! kuna uwezekano wa kumchumbia binti au kuchumbiwa na kaka wa dhehebu tofauti na ulilo wewe yaani muumini wa TAG kumchumbia binti wa Roman catholic? inawezekana?

–Abby

Advertisements

100 thoughts on “Uchumba na madhehebu!

 1. Ndugu Adam Kindole
  Kwa taarifa yako hata hiyo biblia unayoitumia leo ni MAPOKEO tena mapokeo matakatifu yaliyokusanywa kuchambuliwa na kuwekwa pamoja kama BIBLIA inavyoonekana leo na hao hao Wakatoloki unaowadharau.
  Kwa kifupi ni kwamba, Wakatoliki wanao mchango mkubwa ktk safari yako ya kwenda mbinguni. Na “ziwa la mama ni tamu hata likiwa la mbwa” Ubarikiwe.

 2. Jamani haiwezekani mmbwa kumnyonyesha kondoo, rc hakuna wokovu na ni maigizo tu, kwa sababu tumepewa jina la Yesu tu ili tuombe kwa hilo lakini wenzetu wanao waombezi wengi tofauti na mwokozi wetu na karismatic wanafanya ibada hizo, karismatic wanakiri wokovu ni kweli, lakini wanachanganya neno la mungu na mapokeo yasiyo na mashiko kibiblia, huu ndo ukweli wa kunichukia mnichukie tu, na wewe uliyeuliza swali jibu unalo ila tamaa tu zinakusumbua, timiza ulilokusudia hebu acha kutusumbua.

 3. Dada Martha,

  Kwanza, asante kwa maelezo uliyoyatoa. Pia niseme kwamba, kuhusu “Wokovu”, hiyo focus unayoitaka, yaani katika darubini zetu tulipoiangalia hii mada tulikuwa tume focus mambo ya madhehebu; bali unachotuambia sasa, ni kwamba tu Fine tune hizo darubini zetu, zile crosshairs zi focus “WOKOVU”; madhehebu yetu yakitupwa huko nyuma, blurred!!

  Mimi nadhani hii pia ni hatua nzuri ktk kutafuta Kweli ya Mungu kimahusiano, haswa haya ya ndoa, maana tusipokuwa makini ni rahisi sana majumba yetu kugeuka rumande!

  Kuhusu huo wokovu unaousema kwamba na huko Katoliki upo, na kwamba unapanda ktk viwango, sina uhakika sana na hilo, maana nafahamu kwamba wokovu ni fundisho la Biblia linalotegemea kwa asilimia Injili iliyohubiriwa na mitume ili nasi tupate kutakaswa kwa neno lao kama alivyotuombea Kristo: Yn 17:19-21
  “Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
  Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.”

  Sasa, jambo ninalotaka kukuomba ulitafakari ktk hii focus mpya ni hali ya makundi yanayokiri wokovu, Je, yanavifanania vifungu hivyo? Fundisho la wokovu ktk makundi hayo tofauti tofauti ni moja? Je, ni Fundisho la mitume?

  Na kama wokovu tulionao ni wokovu wa kidhehebu, basi bado nashauri ni vyema wanaotaka kuoana, wajitahidi kuoa ndani ya makundi yao, kuliko kucompromise makundi yao kwa mategemeo ya kufikirika!

  Asante sana dada yangu!

 4. Lwembe na Sungura, inawezekana kweli sijaelewa mada, lakini mimi nilikuwa nafocus(mtazamo) zaidi kwenye maisha ya kumtumikia na kumpendeza mungu hapa duniani ambayo ndiyo yatakuwa daraja la kwenda Mbinguni ambalo madhehbu yote wanatafuta. Maana kila dhehebu linaamini kuwa lile dhehebu lao ndilo daraja la kweli na imara la kumfikisha mbinguni, ndio maana nikaondoka kwenye madhehebu na kuongelea juu ya wokovu kama daraja la kufika mbinguni. kama nilikuwa nje ya mada basi mnisamhehe tu maana ufahahamu unatofautiana baina ya mtu na mtu. Kuhusu wakatoliki waliookoka(karismatik); hao itafika wakati wataona hata hayo ya salamu maria ni ubatilii kwani hata sasa baadhi yao wameshaacha kusali sala hizo. ni muda mfupi ujao hao waliookakoa hawatasali sala hizi. ndio maana maana nilisisitiza juu ya wakatoliki waliokoka maana naona kuna mabadiliko yanafanyika kule, maana hata kunena kwa lugha walikuwa hawaamini, hata kutoa pepo, kuponya magonjwa kwa jina la Yesu walikuwa hawaamini lakini siku hizi wameruhusiwa na wanafanya.

 5. Kwa ujumla mafarakano ya Kanisa yanafananishwa na ujenzi wa mnara uliokuwa unajengwa ili kutoboa anga na kumfikia mungu,kisha mungu akawatawanya kwa tofauti ya lugha. Tuamke sasa, mungu amewatawnya wenye kiburi.

 6. Asante Lwembe;

  Maana naona dada Martha bila shaka pasipokujua anaanza kujadili kitu ambacho si mada yenyewe.
  Mada kimsingi inahusu mtu wa dhehebu hili kwenda kuoa mtu wa dhebu jingine. Na huko nyuma nilisema kuwa hiyo inawezekana ikawa sawa kama hao watu wawili wana kitu nilichokiita ”common components of faith”.

  Hebu fikiria wewe umeokoka unaenda kuolewa na mtu ambaye hata haamini kama kuna kuokoka dunia kama rafiki yangu Siyi! Unadhani hapo maombi yenu yatakuwa yanamfikia Mungu kweli? Maana ni wapi wawili waweza kutembea pamoja pasipo kupatana?

  Halafu Martha, kwani watu tuliokoka tunatakiwa kukaa rohoni zaidi kuliko tunavyokaa mwilini? Kwani tumeubwa ili tukae ,mwilini au rohoni? Na huo muda mwingi tunaokaa huko rohoni tunakuwa tunafanya nini huko?

  Nani kwenye maandiko alipata mke wake akiwa amefumba macho?

  Kama ninapenda mwenye hips, mrefu, mwenye macho mazuri, sura nzuri kama ya Sara, Rebeka, na Rahel kuna tatizo gani,kwani si Mungu aliyeumba hao wote.

  Kinachotakiwa ni mimi kuomba kwa ‘motive’ nzuri, yeye hutupa sawasawa na haja za mioyo yetu.

  Umesema kuwa hututishi lakini kimsingi umeshatutisha tayari. Wako watu amabo wameoa wake wenye kinachoitwa sura mbaya na tabia zao ni mbaya vilevile, wako watu waliooa wenye sura nzuri na tabia zao ni nzuri vilevile.( Kinyume chake pia kipo)

  Umesisitiza sana suala la kuwa rohoni lakini cha ajabu biblia haijasema kuwa tukae na wake zetu kwa kuwa rohoni muda mwingi, bali imesema tukae nao kwa akili (mwilini)

  Tangu wapendwa wameanza kujifunza mambo ya kuongozwa na Roho katika kupata wenzi wao, haijawahi kuleta unafuu wowote juu ya changamoto za ndoa. Waliongozwa na wasioongozwa na Roho wanalia vilio vilevile kwenye ndoa. Hii inaonesha kuwa hatujagundua kinachofanya ndoa iwe safi ni nini hasa.

  Tatizo kubwa siyo jinsi ya kumpata mwenzi, bali ni jinsi ya kuishi nae. Hata mzee Ibra, Isaka, na Yakobo ndoa zao moto uliwake lakini walijua jinsi ya kuishi na wake zao. Japokuwa mzee Ibra na mjukuu wake Yakobo wake zao waliwakosesha, but walikuwa wanawasikiliza wake zao.

  Na mimi ninachojaribu kusisitiza sana kwenye mada hii si kumsaidia mtu awe na ndoa yenye furaha, bali apate mtu ambaye atamfanya ayatende mapenzi ya Mungu, bila kujali moto unawaka humo ndani au shangwe zimetawala.

  Ndoa kuwa na furaha au kasheshe hilo ni juu yako wewe mwenye hiyo ndoa, wala si juu ya Mungu( if you didn’t know).( kuna ndoa za wapagani hazina Mungu na zina furaha)

  Bless u all!!!!

 7. MNANISHANGAZA WANDUNGU, KAMA ISSUE NI KUOANA ‘WALIOOKOKA’ JE! KUNA IDADI SAWA KATI YA WANAUME (WALIOOKOKA) NA WANAWAKE (WALIOOKOKA) ILI KILA MMOJA AMPATE WAKWAKE? MASWALI YA KUJIULIZA >JE! IDADI YA WATU DUNIANI MMEICHUNGUZA? >JE! WEPI NI WENGI WANAUME AU WANAWAKE? >JE! IDADI YA WALIOOKOKA NI SAWA KWA ‘JINSI(A)’ ZOTE MBILI? >JE HAMUONI KUWA MNAKOTUPELEKA ITABIDI TUANZE KUOANA MTU NA DADAKE AU MUME MMOJA WAKE WANNE? Inawezekana umefunga na kuomba Mungu akupe mke/mume mwema, kakuletea huyo mnywa pombe ili umbadilishe umemkataa unamtaka aliyeokoka mwenzako, kwani wote walizaliwa wakiwa wameokoka? Fuatilia historia za watu duniani watu walikua wauwaji leo hii ndo wachungaji. MUNGU ANAWAJUA WALIO WAKE KABLA HATA HAWAJAZALIWA, Kazi kuwalaumu Warumi heti hawajaokoka kazaneni naona mbinguni mtaenda kwa “kwa u-T.A.G.”MNANISHANGAZA WANDUNGU, KAMA ISSUE NI KUOANA ‘WALIOOKOKA’ JE! KUNA IDADI SAWA KATI YA WANAUME (WALIOOKOKA) NA WANAWAKE (WALIOOKOKA) ILI KILA MMOJA AMPATE WAKWAKE? MASWALI YA KUJIULIZA >JE! IDADI YA WATU DUNIANI MMEICHUNGUZA? >JE! WEPI NI WENGI WANAUME AU WANAWAKE? >JE! IDADI YA WALIOOKOKA NI SAWA KWA ‘JINSI(A)’ ZOTE MBILI? >JE HAMUONI KUWA MNAKOTUPELEKA ITABIDI TUANZE KUOANA MTU NA DADAKE AU MUME MMOJA WAKE WANNE? Inawezekana umefunga na kuomba Mungu akupe mke/mume mwema, kakuletea huyo mnywa pombe ili umbadilishe umemkataa unamtaka aliyeokoka mwenzako, kwani wote walizaliwa wakiwa wameokoka? Fuatilia historia za watu duniani watu walikua wauwaji leo hii ndo wachungaji. MUNGU ANAWAJUA WALIO WAKE KABLA HATA HAWAJAZALIWA, Kazi kuwalaumu Warumi heti hawajaokoka kazaneni naona mbinguni mtaenda kwa “kwa u-T.A.G.”MNANISHANGAZA WANDUNGU, KAMA ISSUE NI KUOANA ‘WALIOOKOKA’ JE! KUNA IDADI SAWA KATI YA WANAUME (WALIOOKOKA) NA WANAWAKE (WALIOOKOKA) ILI KILA MMOJA AMPATE WAKWAKE? MASWALI YA KUJIULIZA >JE! IDADI YA WATU DUNIANI MMEICHUNGUZA? >JE! WEPI NI WENGI WANAUME AU WANAWAKE? >JE! IDADI YA WALIOOKOKA NI SAWA KWA ‘JINSI(A)’ ZOTE MBILI? >JE HAMUONI KUWA MNAKOTUPELEKA ITABIDI TUANZE KUOANA MTU NA DADAKE AU MUME MMOJA WAKE WANNE? Inawezekana umefunga na kuomba Mungu akupe mke/mume mwema, kakuletea huyo mnywa pombe ili umbadilishe umemkataa unamtaka aliyeokoka mwenzako, kwani wote walizaliwa wakiwa wameokoka? Fuatilia historia za watu duniani watu walikua wauwaji leo hii ndo wachungaji. MUNGU ANAWAJUA WALIO WAKE KABLA HATA HAWAJAZALIWA, Kazi kuwalaumu Warumi heti hawajaokoka kazaneni naona mbinguni mtaenda kwa “kwa u-T.A.G.”MNANISHANGAZA WANDUNGU, KAMA ISSUE NI KUOANA ‘WALIOOKOKA’ JE! KUNA IDADI SAWA KATI YA WANAUME (WALIOOKOKA) NA WANAWAKE (WALIOOKOKA) ILI KILA MMOJA AMPATE WAKWAKE? MASWALI YA KUJIULIZA >JE! IDADI YA WATU DUNIANI MMEICHUNGUZA? >JE! WEPI NI WENGI WANAUME AU WANAWAKE? >JE! IDADI YA WALIOOKOKA NI SAWA KWA ‘JINSI(A)’ ZOTE MBILI? >JE HAMUONI KUWA MNAKOTUPELEKA ITABIDI TUANZE KUOANA MTU NA DADAKE AU MUME MMOJA WAKE WANNE? Inawezekana umefunga na kuomba Mungu akupe mke/mume mwema, kakuletea huyo mnywa pombe ili umbadilishe umemkataa unamtaka aliyeokoka mwenzako, kwani wote walizaliwa wakiwa wameokoka? Fuatilia historia za watu duniani watu walikua wauwaji leo hii ndo wachungaji. MUNGU ANAWAJUA WALIO WAKE KABLA HATA HAWAJAZALIWA, Kazi kuwalaumu Warumi heti hawajaokoka kazaneni naona mbinguni mtaenda kwa “kwa u-T.A.G.”.

 8. Dada Martha,

  Maelezo yako dada yangu ni mazuri sana, lakini juu ya hayo, napenda nililete kwako jambo moja ambalo ninaamini ni la msingi sana katika hili tunalolijadili, inawezekana umeli overlook, kwamba unapolivusha jambo hili kutoka “Uchumba na madhehebu” kuja “Uchumba na kuokoka”, ni dhahiri kwamba tutaishia katika mkanganyiko!

  Kwa mfano, nikiirejea kauli yako hii, naona ina mapungufu ya “Imani” kulingana na Neno la Mungu kwa kadiri ya linavyotuongoza, ngoja niinukuu:
  “”Sungura na Wengine naomba hapa focus yetu iwe kwa aliyeokoka na asiyeokoka na siyo MR na M TAGmaana kuna wakatoliki ambao wameokoka na wana kiwango cha juu sana cha mawasiliano na Roho mtktf. Na pia wapo wa TAG ambao wamezaliwa humo kwa hiyo imani yao bado inalegalega, wanaishi katika kawaida za kimwili sana! Hivyo mjadala wetu ufocus kwa hao waliookoka na wasiokoka.””

  Sasa, iwapo binti wa Kipentekoste aliyeokoka ataolewa na Mkatoliki aliyeokoka, na kwa kadiri ya mahusiano ya Kikristo, mume akiwa ndiye kichwa, basi itamlazimu binti huyo kuungana na mumewe katika huo wokovu unaopatikana Katoliki. Ndipo asubuhi wangehudhuria ibada ya kawaida ya Kikatoliki inayohusisha maombezi kupitia “Bikira Maria Mama wa Mungu, Bikira wa Milele” na watakatifu wengine, na kisha ukifika muda wao wa kukutanika hao waliookoka, mambo huchangamka, hapo wangenena kwa lugha na kuombea wagonjwa, yaani vipawa vingewamwagikia kama kawaida ya Kipentekoste hata usingeweza kujua kwamba hao ni Wakatoliki!

  Kuokoka unakotuambia ndio huku?

  Gbu!

 9. Naendelea wapendwa!yaani wewe unafunga na kuomba unamlilia God akupe chombo chako alichokuumbia thn akupe m2 mcyeendana naye!eti yeye ka2mika na anaendelea ku2mika thn akupe wewe!tena ndoa za cku hizi unakuta men au binti anawaaga washikaji zake kwa kulala nao mara ya mwisho coz baadaye kwenye kuiba ruti inaweza mazingira yakawa magumu kiaina so m2 kama huyo ndiyo unasema unafanana naye!jamani ni kweli!mimi najua yeyeto aliyeokoka na akamshirikisha God asilimia zote kwenye isue hii bac God Atampa kile anacho deserve&disire.tena ya2pasa 2we na subira 2naposubiri majibu yetu,wengine kinachowacost ni uharaka,tamaa ya kuolewa au kuoa,wengine wanamwomba God bt hawakai kwenye sheria zake yaani wana DO kabla ya ndoa eti wanatest kama mambo ni safi?unaona sasa michanganyo inapoanza tayari unakuwa umeanguka na lazima utampata unayeendana naye kimtindo huo yaani acynahofu na Mungu!Coz mwenye hofu na Mungu haonjeshi wala haonji coz anajua God atampa yuleyule anayemtaka,atakayemfaa!so nadhani hapo mmenisoma.B Blessed.

 10. Wapendwa hebu twendeni sawa!2napozungumzi swala la kuoa kuna njia za kupita ili uweze kupata huyo unayetaka kumuoa wenda utampata sahihi au cyo sahihi!njia ya kwanza ni ya ku2mia akili yako,ujuzi wako na kila maarifa ya kwako pasipo mshirikisha Mungu,njia ya2 ni kumshirikisha Mungu asilimia zote!2kianza na hili la kwanza ndiyo huwa kama unacheza kamari waweza kupata au kukosa,tena mziki wake huwa balaa.bt hili la2 ni uhakika coz God atakupa kile kifaa chako cha ukweli alichokuumbia wewe 2 yaani kinacfa zote unazozitaka yaani kama unapenda mtoto mweupe mwenye chuchu ndogo usafiri wa uhakika(miguu),c mnene wala mwembamba,c mrefu wala mfupi,mwenye lips pana,mwenye hips na mgongo wa wastan bac vyote utavipata coz God anajua saana unayefana naye yaan ile pini ya kwako kabisa!bt lazima utambuwe anayeckiwa maombi na God ni yule aliyeokoka anaye tii sheria zake.sasa wewe unatii sheria zake iwezekani vipi umwombe samaki thn akupe nyoka?yaani wewe umeji2nza,ume2lia thn akupe kicheche?acyemjua yeye kabisa!!.. inaendelea

 11. Sungura na Wengine naomba hapa focus yetu iwe kwa aliyeokoka na asiyeokoka na siyo MR na M TAGmaana kuna wakatoliki ambao wameokoka na wana kiwango cha juu sana cha mawasiliano na Roho mtktf. Na pia wapo wa TAG ambao wamezaliwa humo kwa hiyo imani yao bado inalegalega, wanaishi katika kawaida za kimwili sana! Hivyo mjadala wetu ufocus kwa hao waliookoka na wasiokoka.
  Haya hebu nichangie hapo kwa Sungura, hao watu wa Mungu wawili (Samson na Mfalme suleman na mimi naongezea na Mfalme Daudi) wote hawakuwa watii kwa Mungu, yaani hawakuwa na hofu ya Mungu wao ndio maana wakachukuliwa na tama za dunia hii, na ukisoma hadithi za hao watu utaona miisho yao ni ya majuto. Sasa wewe uliyeokoka unataka kuwa na mwisho wa Majuto? hebu soma Efeso: 5:6-11. Sasa hapa je ni dhambi au sio dhambi? ona Mungu anatoa adhabu, na kama si dhambi kwa nini Mungu atoe adhabu? Madhara ya kuoana na mtu asiyeokoka nilishataja kwa ufupi kwenye michango yangu iliyopita. Usiangalie uzuri wa sura au family background ya mtu, au future ya mtu hujui kaipataje, na hujui ana mikataba gani. kwa sababu ili mtu afanikiwe lazima afuate kanuni Fulani( nazo ni mbili tu kufuata ya giza au ya mwanga) ukiwa vugvugu hufanikiwi ng’oo!!! chunguza wote ambao unaamini wamefanikiwa utaona au wako gizani au wako katika mwanga. Sasa kila mtu hapa duniani anataka kufanikiwa katika kiwango cha juu sana! sasa wewe uliyeokoka unajua kanuni zake kama vile utoaji, kuomba, kuongozwa na roho mtkf, kusikia sauti ya Mungu, kuvunja maagano ya wazee, kuatamia maono nk. Na yote hayo ili uyatende kwa ukamilifu yabidi uwe rohoni muda mwingi, sasa umeoana na mtu asiyeokoka hajui hayo, atakukwaza na mwisho unatoka rohoni unaanza kuenenda kimwili kama samsoni. badala ya kumsikia roho Mtkf utakuwa unasikisa sauti ya mme/mke wako asiyeokoka matokeo yake unaenda uelekeo tofauti na alivyokupangia Mungu. na huko ndiko utakaopatwa na mapigo ya Mungu kama ya samson. Kuwa Makini Kijana. Tulia na Mungu wako, Mwombe roho Mtakatifu akuongoze katika kumtafuta mke/mme aliye ubavu wako wewe uliyeokoka, kisha atakuongoza kuzipata qualities(sifa) za mtu unayetaka awe mweza wa maisha yako. Maana bila roho utaanza kuomba mme mwenye gari, nyumba, pesa, sura nzuri, msomi nk au mke mwenye macho makubwa, hips, kifua, miguu sauti, mwanya, pesa, kazi nzuri, msomi. basi na matokeo yake utapata huyo kumbe ni nyumba ya mapepo. siwatishi hayo mambo yapo kwani pepo yeye antaka vitu vibaya? anataka vizuri pia lakini wapo wazuri ambao ndani yao kuna roho wa Mungu mradi tu ukiomba roho mtktf akuongoze.Siku hizi kuna mambo mengi watu wanafanya ili wawe matajiri, na kuna mambo mengi yanafanywa ili watu wapendwe waonekane wazuri. Tembea na mwanga Neno la Mungu, na Kiongozi Roho Mtakatifu.
  Mungu awabariki sana!

 12. Je! hujawahi kusikia au kuona: (i) watu wameoana wakiwa wapagani na leo ni wazee wa kanisa? (ii) watu mameoana mmoja mlokole mwingine wa mataifa na leo wote ni wainjilisti? (iii) wameoana wakiwa wameokoka na leo wanapiga ulabu/wameanguka? Amkeni acheni ‘umadhehebu’ mwombeni Mungu akupeni wake wema. Kumbuka mke/mume mwema anatoka kwa Bwana sio kwenye dhehebu fulanJe! hujawahi kusikia au kuona: (i) watu wameoana wakiwa wapagani na leo ni wazee wa kanisa? (ii) watu mameoana mmoja mlokole mwingine wa mataifa na leo wote ni wainjilisti? (iii) wameoana wakiwa wameokoka na leo wanapiga ulabu/wameanguka? Amkeni acheni ‘umadhehebu’ mwombeni Mungu akupeni wake wema. Kumbuka mke/mume mwema anatoka kwa Bwana sio kwenye dhehebu fulanJe! hujawahi kusikia au kuona: (i) watu wameoana wakiwa wapagani na leo ni wazee wa kanisa? (ii) watu mameoana mmoja mlokole mwingine wa mataifa na leo wote ni wainjilisti? (iii) wameoana wakiwa wameokoka na leo wanapiga ulabu/wameanguka? Amkeni acheni ‘umadhehebu’ mwombeni Mungu akupeni wake wema. Kumbuka mke/mume mwema anatoka kwa Bwana sio kwenye dhehebu fulanJe! hujawahi kusikia au kuona: (i) watu wameoana wakiwa wapagani na leo ni wazee wa kanisa? (ii) watu mameoana mmoja mlokole mwingine wa mataifa na leo wote ni wainjilisti? (iii) wameoana wakiwa wameokoka na leo wanapiga ulabu/wameanguka? Amkeni acheni ‘umadhehebu’ mwombeni Mungu akupeni wake wema. Kumbuka mke/mume mwema anatoka kwa Bwana sio kwenye dhehebu fulani.

 13. Kwa hiyowapendwa,

  Hebu sasa tujaribu kuelekea kwenye hitimisho. Kwamba, je, mtu aliyeokoka akioa mtu ambaye hajaokoka ni dhambi, na biblia imesema hivyo au la?

  Na ni nini madhara ya kuoana na mtu mtu asiyeokoka kama wewe umeokoka?

  Na kwa sisi wanaume, ivi tunajua sawasawa nguvu ya mwanamke ya kimapenzi jinsi ilivyo na matokeo ya ajabu katika nyanja zingine za maisha yetu?

  Kama hatujui, twendeni tukamuulize mfalme Suleman, na Samsoni watatuambia mambo yalivyo.

  Unachokiona na kukiwaza juu ya mwanamke unayempenda na jinsi unavyojisikia kabla ya kuoana, ukiingia ndani ya chumba na siku kadhaa za kuwa pamoja zikawa zimeendelea, ndo sasa utajua kama uliyenunua kwenye hilo gunia alikuwa mbuzi kweli au kitu kingine!

  Tafakari, kisha chukua hatua!!

 14. unajua, unaweza pingana na ukweli, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tu, na asili (nature) hauwezi ibadilisha ikawa artificial, maelezo yoote yaliyotolewa kuhusu kupinga kweli inaonesha namna watu wanavyojitahidi kuhalalisha uongo kuwa kweli, hata kama ukiwa mbumbumbu kwenye kuelewa neno la MUNGU, basi jitahid hata kusikiliza japo unaweza kuelewa kwa kiwango kidogo. ngoja nitoe mfano kutoka bible, hivi tuseme tumesahau au hatujawahi ckia yaliyomkuta samson aliyebarikiwa kuwa na nguvu nyingi kuliko mtu yeyote aliyewahi kuwepo na waliopo na watakaokuwepo??? lakin ni nini kilimfanya awe kipofu????
  okay, ngoja niseme hivi, kama mafuta na maji havichanganyikani ambapo hivi sio viumbe hai, lakin vinatambua kuwa mmmh, huyu sio mwenzangu, ngoja nijitenge, vipi sisi wanadam, tena tuliomwamini MUNGU wa kweli???? okay, najua kuna kale ka-imani kuwa wokovu ni popote, lakin ukweli ni kwamba wokovu wa makanisa ya kipentekoste, hasa yale ya muda mrefu ni tofauti kabisa na wa madhehebu ambayo sera yao au msingi wa imani yao sio kuhubiri habari ya wokovu hapa duniani. najua hapa mtacomment, na wengine mtacrash, lakini huo ndio ukweli. unapoenda kuchagua nazi sokoni hauchagui kutoka katika mafungu ya nyanya bali katika mafungu ya nazi, sasa kama hapa tu unakuwa makini kwa nini katika swala la mke/mume (ndoa) tusiwe makini zaidi.

  kuna huu msemo; kila mtu amepewa uhuru wa kuwa na hiari ya kufanya maamuzi yeyote ayatakayo. yaani hata kama imeandikwa usiue, lakin mtu ana hiari ya kuua au kutokuua, lakin hakuna mtu aliyepewa uwezo wa kuchagua matokeo ya maamuzi yake.

 15. Mada hii iko pouwa!Martha safiiii!Na mimi naomba nichangie kidogo!isue ya ndoa mimi huwa nashangaa saana pale wapendwa wanapoleta mzaa!tena wengine wanachukulia kama c jambo muhimu kiviile kuwa makini wakati karibu asilimia kubwa ya maisha imeshikwa na ndoa!yaani wengi wapo kwenye majuto coz walilichukulia jambo hili kiaina!God anatutel live mke/mume mwema anatoka kwake!yeye ndiyo anafahamu ubavu wako sahihi aliyeutoa akakutengenezea unayefanana naye so unapomtel anakurudishia ubavu wako uleule!sasa mziki huja hapa wapendwa 2napokwenda kinyume na maagizo yake hapo ndipo hulamba garasa!wengine ooh!hana mvuto tena mara cjui atakufa lini maana cmpendi!na maneno kibao!haya yote ni kwa7bu ya kwenda kinyume na sheria za God.Thn maandiko yanasema live God hackii maombi ya wenye dhambi how comz hujazaliwa mara ya2 uweze kupata mke au mume bora?eti na wewe umezaliwa mara ya pili unasema naolewa na mtu wa Misri!Ujuwe na wewe umekwisha anguka!wapendwa hebu 2fuate maelekezo ya SIR GOD 2pate 2navyohitaji na kustahili.

 16. wakatoliki pia wanaamin ktk utakatfu hapa dunian ndo maana Askofu wa Roma (Papa) anaitwa Baba mtakatifu.

 17. Martha, naona hujawapa vilivyo wakatoliki kuhusu mafundisho yao kuhusu wokovu. Wanasema mtu anaokoka kwa kutimiza mambo yafuatayo: kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, kutubu na kubatizwa. Ndiposa katka maisha mtu hujikuta hujikuta akikabiliwa na mambo makuu matatu ktk kuuishi wokovu hapa duniani (i) Kuzingatia mambo tajwa hapo juu. (ii) kuishi kadri ya maadhimio aliyojiwekea, mf. kumkataa shetan na mambo yake yote. (iii) anapomaliza maisha yake hapa dunian ktk hali nzuri. Kumbuka mtu anaeza kupitia hatua moja au mbili hapo juu lakn akawa na mwisho mbaya kabisa kiasi ya kwamba kuokoka kwake kukawa bure, ndio maana mkazo unawekwa ktk kuyaish mapenzi ya Yesu nakumaliza katk hali nzuri. kumbuka tu wakosaji sisi (1 yoh 1:8-10). NB: tutakutambua kama umeokoka kwa matendo yoko na sio maneno. Mkumbuke farisayo aliyemdharau mtoza ushuru. Ushauri wangu unatoka kwa Waroma (15:1-3). “Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu ma wasio na nguvu wala haitupasi kujipendeza wenyewe…”.

 18. Dittu; Kama nilivyosema kwenye comment ya tarehe 22/1/2004 kwamba sio wote ambao watapata neema ya wokovu, wengine hawatapata neema hiyo. na hao ndio wale wanaomtumikia yule Mnyama Uf.17;8. kwa hao RC na TAG inategemea kama wameokoka wote hakuna shida mambo yatakuwa safi (maana kuna RC ambao wameokoka- Karismatiki) lakini kama RC hajaokoka sijui itakuwaje maana wengine wa kundi hilo wanasema kuwa wokovu uko mbinguni duniani hakuna wokovu, wanasema kuwa mtu hawezi kuishi maisha matakatifu hapa duniani. Lakini Bw, Yesu mwenyewe anasisistiza; sisi kama tukimpenda tuwe watakatifu kama yeye alivyo. Yoh.14: 12, 14, 21 na 23. Hayo yote yanamwezesha mtu kuwa mtakatifu hapa duniani, maana Roho Mtf ndiye anayeoongoza kutenda matendo yanayotufanya tuwe watakatifu. Ndio maana Mungu hupendezwa na watatifu wa duniani… ni akina nani kama sio waliookoka?
  Hebu tuangalie maisha ya watu ambao mmoja hajaokoka; itakuwa nguma sana kufurahia maisha kwani kuna kanuni nyingi za Mungu za kufuata ili aliyeokoka awe na maisha mazuri. (Furaha, amani, utajiri, uzima na afya,kibali, maisha marefu, kufaulu mtihani nk) kwa waliokoka kanuni ya kufanikiwa katika nyanja hizi wanajua. Lakini asiyeokoka atakuambia ni mapenzi ya Mungu (kuwa maskini, magonjwa, kifo cha mapema, kutokuwa na amani, kufeli mtihani-mungu ndiye alivyompangia nk). sasa hapo sijui hao aliyeokoka na asiyeokoka wataishi kwa imani ipi nilliyosema kwanza au hii ya pili? ni vigumu sana kusonga mbele kwenye maisha kama mkiwa vuguvugu.
  Ditto: kama hujaoa/olewa muombe Mungu akupe ule ubavu wako.
  Mungu awabariki wote!

 19. Martha, Nashukuru kwa ufafanuzi wako. Ila nnayo hamu kufahamu hatima ya wawili hawa (mTAG & mRc) kunayo mambo mazur hapa ya kujifunza. Ubarikiwe!.

 20. NDUGU ZANGU INGIENI KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA. MUNGU HAANGALII WINGI BALI ANAANGALIA WANAOMTII NA KUMTUMAINIA
  KWA WAKATI WA GHARIKA WALIPONA 8
  SODOMA 3
  MUNGU AANGALII QUANTITY. CHUKUA HATUA.

 21. naongea kwa wale waliookoka, waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi (maana madhebu mengine hayaamini juu ya wokovu hapa duniani ) HIVYO oa /olewa na mtu aliyeokoka maana kuokoka ni neema iliyopo kwa baadhi ya watu na wengine hawana fursa ya kuipaa hiyo neema rejea Uf. 13:8 hao ndio wale waliopata neema lakini kuna ambao neema haitawapata Uf.17:8. Je utamjuaje huyo mchumba ambaye labda unadhani ataokoka baada ya kuoana naye yuko kwenye kundi la wenywe neema? usidhani kwamba Yesu alipokufa basi wote wataokolewa hapana, bali ni wengi kwani damu ya yesu ilimwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi la watu wengi na sio wote Mark 14:24 tena imenenwa kwamba Msifungwe nira pamoja na wasioamini. Ndoa ya hivi itakuwaje? wewe uliyeokoka ukioa/kuolewa na mtu asiyeokoa utakuwa kwenye risk ya kupoteza furaha ya ndoa yako. Mungu awabariki sana!!!
  (Dittu wakati naandika ile ya kwanza niliumiss huu wa 17:8 nadhani sasa ukisoma unaweza kuelewa vizuri.

 22. Ni vema kufikiri vizuri sana juu ya mwenzi wa kuishi naye. hapa naomba wale wanaotaka kuoa au kuelewa kuwa na uelewa wa kutosha juu yaneno la mungu juu ya ndoa, Paul anaona ndoa si tu kuishi pamoja tu ila mapatano hayo ni kwa ajili ya kusali na kuomba pia ( 1kor mlango wa 6 na saba soma kwa jino la rohoni). kumbuka majuto ni mjukuu hakuna sababu ya kuigiza kama anyetaka kukuoa au kuolewa na wewe ni lazima afikiri pia juu ya muundo wa maisha mtakayoyajenga ikiwepo familia matunda ya ndoa yenu.

 23. Martha, (ufu 13:1-9) kuna waliozaliwa ili… sjakupata ndugu, unaweza nielewesha?

 24. KAMA UMEOKOKA NA UMEJIFUNZA NENO LA MUNGU NA KUFANYA MAOMBI YA UKOMBOZI WA FAMILIA NA MTI WA UKOO, JIBU UNALO. LA KAMA HUJAOKOKA INA MAANA UKO GIZANI UTAKUWA UNAPAPASAPASA TU KATIKA KUFANYA MAAMUZI YA MAISHA YAKO MAANA HUNA MWANGA AMBAO NI NENO LA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU. MAANA BIBLIA YASEMA MKE MWEMA HUTOKA KWA MUNGU ALIYEHAI. KAMA UMEOKOKA UKIMUOMBA MUNGU ALIYEHAI KWA DHATI ATAKUPA MKE(mchumba) MWEMA( wa kufafanana nawe, ubavu wako) na aliyeokoka hawezi kufanana na asiyeokoka na hawezi kuwa na ubavu usioookoka. kwa sababu wewe ni moto ukioa/ukiolewa na aliiye baridi ndoa yenu itakuwa vugugu Je unapenda kuwa vugugu wewe? acha baridi aone na baridi mwenzake na moto aoane na wa moto wenzake maana kuna wale walioandikiwa kwenda motoni tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu Uf. 13;1-9. Angalia usiwe mateka, shika imani yako, mshirikishe mungu naye atakupa (mchumba) mtu aliye na imani kama yako.
  Mungu awabariki sana.

 25. Abby, vp ndugu yangu mlifanikiwa kuoana (m TAG vs m RC) au bado mnatafakuri ukuu wa Bwana?

 26. Bwana Bariki nashangaa kwa nini nimechelewa sana hili chapisho lako.
  Umeuliza kitu kizuri sana.

  Bila shaka uliposema madhehebu tofauti ulimaanisha kama vile mtu kutoka TAG akaoe Full Gospel, au Efatha n.k.

  Kama hawa watu wako sawa katika kile nilichokiita ‘common components of faith’ mimi sioni kama kutakuwa na shida ya kiimani kwa hawa watu, maana maana wanachoani ni kimoja na wanakiamini kwa namna moja.

  Lakini pia ningependa kusema kuwa lengo na kusudi la kuoa siyo kuishi maisha ya furaha. Furaha unaweza ipata hata kama hujaoa/hujaolewa. Kwa hiyo hatupimi kuwa ndoa fulani ni sahihi ati kwa sababu hao wanandoa wako na furaha. Unaweza ukaoana na mganga wa kienyeji na ukawa na furaha. Furaha huletwa na hulka za hao wawili walioana.

  Vilevile uwepo wa matatizo kwenye ndoa si kielelezo kuwa ndoa hiyo haiko sahihi.

  Ndoa ni taasisi takatifu na msingi wake uko kwenye maandiko matakatifu na Mungu mwenuewe ndiye mwanzilishi wake.

  Ulishawahi kufikiri ni kwa nini mwanamke anaweza akawa sababu ya maombi yako kutosikilizwa na Mungu?

  Au kwa nini Mungu aliwataka wayahudi waachane na wanawake wa mataifa mengine,hata ikabidi waachane hata na wale watoto wliozaa na wanawake hao?

  Ndg Bariki ndoa ni ibada kamili kwa Mungu, kwa hiyo sidhani kama tuko tayari kufanya ibada na watu amabo si imani moja na sisi ati kwa sababu tu tuliwapenda hivyo tukaamua kuitika mapenzi yetu kwao kwa kuamu kuoana/kuolewa nao.

  Ndio hapo Paulo anasema tusifungiwe nira na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa. Kumbuka neno asiyeamini hapa halimaanshi mtu asiyeamini kuwa Yesu ni Bwana, bali ni mtu asiyeukubali wokovu katika utimilifu wake. Na jinsi isivyosawasawa ina maana kuna ambavyo ni sawaawa. Kwa mfano aliyeokoka akiwa ameoa\ameolewa na asiyeamini huko ni kufungiwa kuliko sawasawa, lakini kufungiwa nira ya kwenda kuoa asiyeokoka huko ni kufungiwa kusiko sawasawa.

  Merry Chrismass!!!!

 27. Everyone loves it when folks come together and share opinions.
  Great website, keep it up!

 28. Na wengi ninawafahamu walifunga ndoa namna hiyo, akiwepo rafiki yangu Msabato (pamoja na rigifdity yao yote) aliyefunga ndoa na dada MRC. Ndoa ilifungwa RC lkn kila mtu anaendelea na imani yake. They are happily married.

 29. Sungura,

  Na vipi ukioa/olewa na mtu wa dhehebu tofauti (sio dini tofauti) na kila mtu akaendelea kusali kwake? Kama hakuna anayembughudhi mwenzie au kumlazimisha ahamie kwake? Ndoa inafungwa kokote kati ya hayo madhehebu (unless uniambie tena hata namna ya ufungaji wa ndoa ni kikwazo kiimani!) then baada ya hapo kila mtu anaendelea kusali na kuamini chake.

  WaRC wana hizo ndoa kwenye sheria zao zinaitwa ndoa Mseto. Wanafungisha ndoa kati ya mRC na mtu wa dhehebu jingine, na hata na muislam ambaye hakukubali kubadili dini. Na wanachofanya ni kumwambia mRC wao asibadili, na watoto watakaozaliwa “ajitahidi” kuwalea katika misingi ya kiRC.
  NB Ni kuwa “ajitahidi”. Ikishindikana basi, cha msingi alitia jitihada ambazo ni genuine.
  Najua wengi watapinga hii kuwa ni too liberal. Lkn ndio maana ya dini inayotambua diversity. Sio kuwa rigid kwa kila kitu, including maswala ya mioyo ya watu (matters of the herat kama love) ambavyo ni ngumu kuzuia watu wa imani tofauti kupendana.

  I did not post this for the sake of argument. I have explained one of the provisions n the RC’s canon laws.

 30. Hii mada kwa sehemu kubwa tumeirukia katika kuijibu kwetu, ndio maana ni vigumu sana kufikia jibu ambalo ni yamkini.

  Kwanza tulitakiwa kujua neno mkristo kwa ukamilifu wake lina maana gani( mkristo ni nani?)
  Pili tungejua nini maana ya dhehbu na nini huwa kiko ndani ya dhehebu,
  Tungepaswa kujua tofauti zilizopo kati ya dhehebu moja na jingine( eg TAG & RC) na zina matokeo gani ikiwa hawa watu watakuwa wanandoa
  Halafu tukajua ndoa kwa mkristo ina uhusiano gani na kile anachokiamini.

  Kuna tofauti moja kati ya M-TAG na M-RC ambayo mimi naijua; Waroma wanaamini katika ibada ya wafu,lakini wa tag hawaamini hivyo, maana kibiblia hiyo ni ibada ya sanamu. Kuna ile sala ya salaam Maria, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote,…….., tatizo kubwa katika hiyo sala ni kuanzia maneno haya; utuoombee sisi wakosefu,……. Maria mama wa Yesu hana wajibu wa kutuombea kibiblia. Kumwambia atuoombee kama waroma wanavyofanya ni ibada ya sanamu. Haya kuna suala la ubatizo. hawa maji mengi hawa kidogo, hawa hubatiza watoto wachanga hawa lazima mtu awe mtu mzima ndo abatizwe.
  Kuna vikorokoro vingi sana katika ufanyaji wa ibada za ki-RC ambavyo si vya ki-Mungu.Kuvipuuza vitu hivi na kudhani tu kwamba ndoa inahusu mwili peke yake inaweza ikawa njia ya kujipeleka upotevuni.

  Kuwa na ndoa yenye maana ki-imani ni lazima muwe mnatembea katika ukurasa mmoja wa kitu ambacho kinatengeneza hiyo imani mnayoamini kwayo( common components of faith)

  Tusiiwazie ndoa kuwa ni suala tu la kufanya tendo l ndoa na kufanya investment za maendeleo, kuna kitu kinaitwa huduma ndani ya ndoa kwa wakristo ambacho lazima kiwe na shida kama wahusika hawana component iliyo sawa ya ki-imani.

  Kama ni kufanya tendo la ndoa, kuzaa watoto, na kuwekeza hata kuoa mwislamu inawezekana.

  Acha niiweke hivi; wewe ni mlokole umempenda binti wa kisabato, ki-roma, au kinyume chake oh, oa tu, haishindikani. Lakini matokeo yake ki-imani ujiandae nayo, maana waweza kujikuta unaabudu miungu.

  Kama wwe ni m-RC na unasema umeokoka halafu bado unaombea wafu, na kumwomba Maria akuombee, fikiria tena.

  Tunapoongelea ukristo kwa ujumla wake huwa tunachukulia kila kitu kawaida tu, lakni tunapoongelea ukristo kwa maana yake halisi kuna vitu fulani “sensible” havipaswi kupuuzwa maana bila hivyo huwezi kumtisha hata mchawi.

  Tusiyapuuze matokeo ya ndoa juu ya kile tunachokiamini!

 31. Alex,
  U said:

  “haiwezekani kila dhehebu likawa linaamini chake alafu vyote vikawa sahihi mbele ya Mungu huyo huyo mmoja haiwezekani”

  Hilo linawezekana. Ila, kama ndivyo basi inawezekana pia kati ya madhehebu yaliyopo bado hakuna linaloamini ambacho ni sahihi. Kwa sababu madheheebu baado yanazidi kuibuka. So, inawezekana linalohubiri ukweli likawa halijaja. (I just took your premise to its logical end)

  Mimi sipendi kuamini kuwa ni dhehebu moja tu ndio litakuwa sahihi. Sitaki kuamini hivyo.. Tukubaliane hivi: Kwamba ni Mungu pekee ndiye anayejua “ukweli au usaahihi” wa kinachoaminiwa na watu kwenye hayo madhehebu. Tumwachie yeye. Na kwake inawezekana yote yakawa sawa, baadhi yakawa sawa, au pengine yote yasiwe sawa.

  Take a small example of maths: different methods lead to the same answer. (I just gave an example, don’t argue that I am likening God to Maths).

  I don’t want to believe that by saying “keep studying on your own as you have said one day you will understand the truth.”, you wanted to say imply that “the truth” is necessarily what you believe it is, and that it is that which I will one day understand. On that basis, I assume two things: (i) that we are both in search of truth; (ii) Or else, we both believe what we know is the truth itself. If so, I also urge you to keep studying and one day you will understood the/my truth!

  Enjoy your day.

 32. okey noted@bariki, lakini haiwezekani kila dhehebu likawa linaamini chake alafu vyote vikawa sahihi mbele ya Mungu huyo huyo mmoja haiwezekani na haitawezekana lakini biblia inatuwekea wazi kabisa kipi kilicho cha kweli na kipi sio cha kweli. keep studying on your own as you have said one day you will understand the truth.

 33. Eti

  “najua mambo mengi yaliyopotoshwa na hilo kanisa lako kuliko wewe unavyoelewa ukitaka unaweza kuniuliza tena kwa upole ili nikueleze ili usiwe mtu usiyejua bali uwe unajua”

  Hahahah. Kalagabaho! ni sawa na kujifnya unamjua mtu kuliko anavyojijua mwenyewwe.! hahah.

  I know the angle that your argument would take (assuming I asked you anything) It is logical that your obvious perspective is that whenever you do differently from us is what you consider to have been ‘adulterated’ You are not going to re-invent the wheel. know your thinking already. I need not add folly in my brain!

  My free advice to you is that you should concentrate on your faith. You will never grow spiritually by wasting time learning false things about my faith. First, because you do not share it, you will never appreciate it. Secondly; because it is not yours, you will never understand it, even if you purportedly do. I would kindly refer you to the definition of faith in the Bible in the book of Galatians. Read it through lense of an independent thinker, not as a brainwashed fellow..

  Enjoy your ignorance.

 34. Mimi nilisema hivi:

  “Chukulia mfano mdogo kuhusu kula mkate (Chakula cha bwana). Yesu alikaa nao akachukua mkate akabariki na divai pia wakala pamoja. tena kwenye kikombe kimoja. Then akaagiza fanyei vivyo kila mlapo kwa ukumbusho wangu.”

  Wewe ukajibu hivi:

  “Yesu hakusema kila kitu kwenye biblia fanyeni kwa ukumbusho wangu kama wewe unavyotaka kutudanga kiwazi kabisa hivi ila alisema pale alipowapa kikombe na mkate tu.”

  Hayo ya kwamba ni “kila kitu kwenye Biblia” nimeyasema mimi? halafu unanisema eti sijui ninachosema. haah.

  Sasa ni kitu gani nilichosema ambacho unabishaa? Au sentensi yangu haikumaanisha ulichosema wewe? Halafu unajifanya kuwa eti mimi nilisema isivyo sahihi na wewe ndio umesema kilicho sahihi. Kwa kifupi umerudia nilichosema.

  ayo unayosema ya mfaalme wa RC sijui alinyunyuziwa maji etc ni blah blah. Nothing concrete hapo. Umesikia sikia tu kwa wachungaji wako unabeba kama kilivyo. o facts, no back up. Incredible stories.

  Naona usinieleze hayo mengi uliyo nayo. Nakuahidi kwamba sitakuelewa, kwa vile na wewe pia hunielewi. Kila mtu aendelee na imani yake. Tuheshimiane tu kwa vile kila mmoja wetu anadhani yuko sahihi. Hata hao waislam wanaochoma makanisa, imani yao ni tofauti na hao wasiokubaliana nao. Japo Quran wasoma moja.

  Na hiyo ndiyo essense haswa ya madhehebu. Ili yaendelee kuwepo, lazima tofauti fulani fulani ziwepo. Kwa hiyo ndio maana mimi na wewe tunasimama katika misingi/misimamo tofauti katika maswala kadhaa. Na mimi naheeshimu hilo, na wala sijasema wewe umekosea. Ila nimesema tu kuwa usijione kuwa wewe tu ndio uko sahihi na wengine wasiofanya kama wewe wamepotoka. Kama alivyosema mchangiaji mmoja, Hukumu tumwachie Yeye aliye juu.

  Mungu akubariki.

 35. Naona bwana Bariki unashindana na ukuta ambao ni Biblia, biblia iko wazi katika kila jambo na kila jambo lina sababu yake maalumu na ya lazima kufanyika kama ilivyokusudiwa bila kupunguza wala kuongeza. Nashukuru kuwa umekiri hujui maana ya kubatiza ni nini na kwa sababu hiyo najua hujui hata kwa nini Yesu alibatizwa kwa jinsi ile yaani maji mengi. Na oia nachelea kuwa hata agizo la Bwana Yesu kwetu kuwa Tuwafanye matifa kuwa wanafunazi na kuwabatiza huelewi Yesu alimaanisha ubatizo gani. Lakini pia huelewi kitu hicho cha kunyunyizia maji kilitoka wapi ndio maana unakitetea na kujaribu kujihesabia haki kwa fikra zako tu binafsi eti ukiwa na imani tu inatosha bila kuelewa kuwa imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo sasa ikiwa Kristo mwenyewe aliagiza na yeye mwenyewe akafanya kwa staili ya kutumia maji mengi wewe ni nani hata uingize kitu cha kwako ambacho hakikutoka kwa Mungu alafu useme eti umeokoka? Nikueleze tu kinaga ubaga mwanzo wa hivo vitone vya maji wanavyowanyunyizia ninyi nanyi mnaamini tu bila kuelewa wenzenu wametoa wapi wakati hakipo kwenye biblia Yesu hakusema kila kitu kwenye biblia fanyeni kwa ukumbusho wangu kama wewe unavyotaka kutudanga kiwazi kabisa hivi ila alisema pale alipowapa kikombe na mkate tu. Kulikuwa na mfalme ambaye alikuwa anaheshimika sana na viongozi wa kanisa la RC na kwa hiyo wakati wa kubatiza badala ya kumpeleka mtoni wakaamua kujitengenezea kiubatizo chao uchwara eti wakamwambia akae kwenye kiti chake tu alafu watamnyunyizia hivo vitone na kumwesabia kuwa amebatizwa jambo ambalo ni upotovu mkubwa sana kwani hakuna mtu mwenye heshima kubwa kama YESU lakini pamoja na heshima yake alikwenda mto jordani kuzamishwa majini sembuse kamfalme ka dunia hii eti kabadilishe agizo la Yesu kwasababu kanaheshimiwa na viongozi wa kanisa ambao nao walikuwa wamepoteza dira. Biblia itabaki kuwa ndio kweli na ndio inayotakiwa kufuatwa na vitu vingine ambavyo sisis hatuvijui vimetoka wapi na nani kavianzisha. inasikitisha pia kuona watu kama wewe nao mnakubaliana tu kirahisi bila hata kujiuliza maswali hicho unachoaminishwa kimetoka kwenye biblia gani!!!!. KUBAKI NA MSIMAMO WAKO UNAWEZA KUBAKI NAO LAKINI BIBLIA HAITABADILISHWA NA VIMISIMAMO VYA WANADAMU KAMA WEWE NA MIMI. sisi ndio tunatakiwa tuifuate biblia na sio biblia itufuate sisi!!!! nafikiri nimeeleweka juu ya hilo sitarajii tena kuona arguments kwenye ubatizo na nikueleze tu najua mambo mengi yaliyopotoshwa na hilo kanisa lako kuliko wewe unavyoelewa ukitaka unaweza kuniuliza tena kwa upole ili nikueleze ili usiwe mtu usiyejua bali uwe unajua. Hata maana ya kuokoka yenyewe bado hujui ndio maana unasema eti matendo ndio wokovu wakati biblia inaniambia kuwa hatuokoki kwa matendo bali kwa neema ya Mungu tena bure!! we unaniambia unaokoka kwa matendo nenda kamuulize Kornelio pamoja na matendo yake kuwa mazuri aliambiwaje na MUNGU (MDO 10:1-), bado ningali nina mengi ya kukueleza lakini nahisi hutaelewa kwa sasa ngoja nikuache na hayo machache.

 36. Ndugu Kapinga umesema kuwa minachofanya ni

  “kujaribu kutetea vitu ovyo ovyo bila kuelewa hata unachotetea ni nini”.
  Naelewa kuwa hiyo umenitarget mimi (hata kama utajaribu kukataa)

  Ninachosema ni kuwa najua ninachosema, mimi sio mpumbavu. Na kila anayetumia muda wake akapost hapa anajua anachosema (hata kama wanaosoma hawamuelewi). Sio lazima kila ninachosema wewe ukielewe. Ingekuwa sawa kama ungesema sielewi unachotetea wewe ni nini. Hapo sawa, ila sio kuwa sielewi ninachotetea mwenyewe. Nimeudhika sana kwa sentensi hiyo.

  So, in short wewe ndiye hujui/huelewi ninachoesema mimi, na sio mimi nisiyeelewa nisemacho mimi mwenyewe.

  Kwa hiyo univumilie tu. Wewe ulitoa hoja zako 6. Nikakubaliana na 5, nikatofautiana na moja. Sasa hiyo tu ndio inifanye niwe mpumbavu kiasi cha kutojua ninachomaanisha mwenyewe? Tofauti zetu kimtazamo/uelewa wa mambo sio kigezo.

  Sawa Mr right.

 37. Ndugu Mosile umenena vyema katika sentensi hii:

  “Sisi wote ni wakristo lkn tuna tofauti ktk misimamo ya kiimani, hivyo tubaki ktk misngi ya imani lkn Bwana ndiye mhukumu wa mwisho”

  Na ukisoma posts zangu hiyo ndio theme haswa – yaani tusihukumiane kwa imani zetu. Usitumie vigezo vya imani/dhehebu lako kuhukumu wengine. Sisi wakristu tunajifanya kulalamikia wanachofanya waislamu sasa kumbe na sisi kwa sisi tunaojiita Wakristu tunaendekeza na kutetea tofauti zetu. Ndio zipo, lkn tuheshimiane na kutobaguana. Kama ulivyosema Bwana ndiye mhukumu wa mwisho.

  Pamoja na hayo, nashukuru kwa kutoa maana ya hilo neno “Baptizo” kwamba ni la kigiriki na kwamba lina maanisha “zamisha ndani ya”. Mimi sijui kigiriki, so siwezi kuzungumzia uhakika wa ulisemalo. Ila pamoja na hayo nabaki na msimamo wangu kuwa kuna vitu vingi sana kwenye Bible ambavyo madhehebu mengi wanafanya ambavyo sio lazima viwe kama vilivyofanyika wakati huo. Wanafanya kwa imani zaidi zaidi ya kuiga tu sheepishly. What matters is how much faith do they attach to the act? The act could remain symbolic but the meaning/faith attached to it be very same as the one others who do it differently have.
  Chukulia mfano mdogo kuhusu kula mkate (Chakula cha bwana). Yesu alikaa nao akachukua mkate akabariki na divai pia wakala pamoja. tena kwenye kikombe kimoja. Then akaagiza fanyei vivyo kila mlapo kwa ukumbusho wangu.
  Swali langu ni je: Ni madhehebu magapi hufanya hivi? (ni mengi-karibia yote, kwa namna zao wenyewe). Pili: Je ni yapi hula na kunywa kwenye kikombe kimoja????? Kwa hili la pili sina uhakika kama wanafanya wote. Na je wasiofanya hivyo wanakosea? au hawajaokoka kwa sababu hiyo? Sio. Wanafanya maagizo yale lakini kwa namna nyingine (kama ishara ya alivyofanya Yesu). Kila kitu lazima kiendane na mazingira, posssibility za sasa (ukilinganisha na wakati ule), etc. Sio tu kuchukulia dini mechanically (nirudie hiyo lugha tena).

  Kwa hiyo ujue kuwa mimi hizo tofauti za madhehebu hazinipi tatizo, wala hazinifanyi nione hawa wako sahihi zaidi ya wale. Posts zangu zimekuwa zinakebehi (kwa makusudi kabisa) wale ambao wanataka kutuaminisha kuwa madhehebu fulani fulani ndio ukristu sahihi, na mengine fulani fulani sio wakristu, na kwa hiyo “wakristu” sahihi wasijihusishe nao kindoa etc. This has been my battle. I should be understood that way.

 38. ubarikiwe sana bwana Primi Mosile, maana umemaliza siongezi chochote ila nasisitiza tu kuwa jipimeni wenyewe kwenye hizo hatua nilizo zitaja ikiwa umekosa hata moja jua kuwa hujaokoka bado!!! kuokoka sio kwa kudhani ni neema ya Mungu na inayokupasa kufuata yote kama yalivyokusudiwa na Mungu na sio kujaribu kutetea vitu ovyo ovyo bila kuelewa hata unachotetea ni nini.

 39. Ndugu yangu Bariki mpaka leo bado unabishana kuhusu ubatizo wa maji mengi?. nina mashaka na imani yako kama uko serious na Bwana Yesu. Ukitaka kujua vizuri tafuta nini maana ya neno ubatizo halafu ndio utoe hoja yako, usitoe hoja ukisimamia dhehebu lako tu, iache biblia ijitetee yenyewe wala usijaribu kutetea imani yako.

  Neno Baptizo katika lugha ya asili iliyoandika biblia kwa upande wa agano jipya yaani Kigiriki ina maana ya kuzamisha ndani ya. Kwahiyo usijaribu kujibu kirahisi tu kwamba ni ishara ya nje na unaidharau kana kwamba haina maana. kuwa makini sana katika kujibu hoja za kibiblia maana unaweza kujikuta katika lile kundi ambalo Paulo alisema ktk Wagalatia mtu akiwahubiri injili ambayo hawajawahi kuihubiri na alaaniwe.

  Kuzamisha ndani ya haijasema Jordan au mtoni bali kinachoangaliwa ni maji, hata mitume walifanya hivyo katika Matendo ile sura ya 8 yule towashi alibatizwa penye maji tele na wala haikuwa mto Jordan.

  Katika hoja ya msingi ya Abby nadhani tumeshatoa ushauri wa kutosha kwake na wala sina haja ya kurudia tena mengi. Sisi wote ni wakristo lkn tuna tofauti ktk misimamo ya kiimani, hivyo tubaki ktk misngi ya imani lkn Bwana ndiye mhukumu wa mwisho. Cha muhimu tusimamie kile ambacho biblia inatutaka tutende na pale ilipotukataza basi tutii japo tunaweza kupingana na viongozi wetu ambao wanafanya mambo ambayo biblia imekataza.
  Mungu awabariki wote.

 40. Na Ndgu Kapinga naomba niongeze kitu kimoja: Umeorodhesha hatua 6 za mtu kufikia wokovu. Nakuballiana na wewe kwa kiasi kikubwa (japo tafsiri ya kila kimoja kila mtu anaweza kuwa na yake). Isipokuwa, kwa hicho cha nne, i.e. kubatizwa kwa maji mengi, ninaomba nitofautiane na wewe.

  Hapo umeenda moja kwa moja katika itikadi za kimadhehebu, ukitaka kuonesha kuwa wanaobatizwa kwa maji “kidogo” eg RC au Lutheran, Anglican hawawezi kuwa wameokoka. Najua hii falsafa inakoanzia: ni kwamba eti Yesu alibatizwa kwa maji mengi.
  Well, nakubali aibatizwa hivyo. Lakini bado tujue kuwa ubatizo ni ishara tu ya nje, na maji aliyatumia kma symbol ya kusafishwa kwa mwili na zaidi roho. (mkumbuke Naimani pia). Kwa hiyo, yesu alibatizwa vile kwa kuwa kwanza alitaka kufanyiwa na yohane kama wengine wote walivyokuwa wanafanya, ili wamuelewe zaidi. Na wakristu wanapobatiza wanaafanya hayo kwa mtizamo uleule kuwa ubatizo wa maji ni ishara ya nje tu. Kama ulivyosema ubatizo wa maji usioambatana na ule wa Moto na Roho Mtakatifu hauna maana. Kwa hiyo, maji membi au machache sio issue. Na kama utabisha eti kwa sababu wanaobatiza kwa maji mengi wanataka kufanya kama Yesu, basi na wafane kila kitu kama Yesu, wasiige nusu nusu. amaanisha:
  (i) Waende Mtoni, sio Kisimani (kama wafanyavyo sasa)
  (ii) Wakienda Mtoni, wasiende Wami wala Ruvu, bali Yordani kama alivyoenda Yesu;

  Utaona kuwa haya hayawezekani, na kwa hiyo ni upuuzi kulumbana kuhusu wingi au ushache wa maji ya ubatizo.

  Ninachomaanisha ni kuwa maji mengi au machache sio issue. Watu tusichukulie dini mechanically.

 41. Matendo mema yanatosha kuwa ndio wokovu wenyewe Kapinga. “Kuokoka” unakokusema ni kupi? Ni kusimama tu na kusema “kuanzia leo nimempokea Yesu awe bwana na mwokozi wangu”? Au ni kusali makanisa fulani fulani? Au ni kutokusali madhehebu fulani? Kwa mtazamo wangu hiyo sio evidence kuwa umeokoka. Kuokoka ni:

  Kwanza ni kuamini na kubatizwa. (“Aniaminiye na kubatizwa ataokoka”). Najua mabingwa wa malumbano wataibuka na hoja hapa kuwa kuamini ni nini, wataleta tofauti za kimdhehebu katika mambo fulani fulani. Kwagu mimi imani iko moyoni mwa mwenye imani hiyo, na sio mtu mwingine anayemjudge kwa kutumia vigezo vya imani yake.

  Pili ni kuzitenda zile amri kuu 2 – Kumpenda Mungu na jirani (Agano jipya) Hizi amri 2 zina-summarize zile amri 10 za agano la kale (zimo ndani yake)

  Kwa hiyo Ndgu Kapinga “kuokoka” bila matendo mema (kama wengi wanaojifannya wameokoka wafanavyo) hakukupi tiketi ya kwenda mbinguni. MImi nina ndugu yangu anadai ameokoka kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Ukimwita kwenye sherehe nyumbani haji (kisa atakutana na watu wasiookoka-wakinywa pombe etc), ukimwambia akuchangie harusi etc hataki (kisa pesa yake itatumika kwa mambo yasio ya imungu). Sawa, ila sasa yeye akiwa anaoza mwanae, au ana shughuli yoyote anataka kila mtu aende kwanza kaisani kwake kwenyehiyo shughuli (e.g. harusi) na pili nyumbani au ukumbini. Hapo anaona kua ni sahihi. Na sis huwa tunaenda tu kwa kuwa ni mkubwa hatuoni haja ya kulumbana. Hiyo ndio mana ya “kuokoka” kwake!

  Unajua watu wanaofikiri kuwa mbingu ni monopoly yao huwa wananiudhi sana. Sana sana. Wanadiriki kusema wazi kuwa wakristu wa madhehebu fulani sio “wakristu”, so hawawezi enda mbinguni. Wao wanaangalia mtu anasali kanisa gani, wana-draw conclusion. Na siku zote wanadai wao ndio waenda mbinguni. Kama mtu anaweza kuandika hapa kuwa mtu hawezi kubaki Mkatoliki na akawa ameokoka kwa sababu Wakatoliki……………………., je huoni anamaanisha kuwa wakatoliki wote destiny yao ni jehanum? Yaani kwao, mtu kuwa mktoliki hafikii hata the minimum standards of kuokoka. hahaha. Kisa wanaamini na kuabudu tofauti na yeye. Hii ni kukosa marifa. Imani ya mtu huwezi kui-judge kwa kutumia imani yako wewe. Never. Huwezi kusema wanakosea kwa sababu wanaamini tofauti na wewe. Watu wanajifanya wa ndio Mungu, wanakalia kiti chake cha hukumu na kuhukumu engine. Ndio maana nikaandika sacarstically kwenye post yangu yaa kwanza, kwa kuwa muuliza swali alitaja kabisa TAG na muRC, na baadhi ya watu akamwambia hao hawawezi kuoana kwa kuwa muRC atakuwa hajaokoka, na mTAG ameokoka.

  Nawakumbusha watu kama hao kile kisa cha Mfarisayo na Mtoza ushuru walokwenda kwenye sinagogi kusali. Mfarisayo akaanza hivi : “Mungu nashukuru kwakuwa mimi sio sawa na huyu mtoza ushuru, …………”.
  Mwishowe, sala yake ilikua ni kelele masikioni mwa Mungu.
  Muwe na siku njema, na matendo mema bila kujali madhehebu yenu. Huo ndio wokovu.

 42. Mimi sina vita na mtu Kapinga. I wanted to sound sarcastic kwa sababu ya comments zilizotangulia. Wengi hapo wana-imply kuwa kuwa tu kwenye dhehebu fulani, ni evidence tosha kuwa “umeokoka”; na kwamba kuwa tu Mkatoliki tu ni evideence kuwa wewe ni mdhambi “hujaokoka”. Hao ndio nilikuwa nawa-target na hiyo comment yangu. Baadala ya watu kuimarisha imani zao kimateno, wanabaki kulumbana kuhusu madhehebu katika mtindo wa “wao na sisi”.
  Sioni tofauti yao na Shehe Ponda!

  Sorry kama nimekwaza mtu.

 43. naona bwana Bariki una vita na watu wa TAG ila huna vita na watenda dhambi ndio maana walishikwa na madawa ya kulevya wasio wa TAG hauna shida nap ila wale wa TAG tu. Ndugu yangu jiulize wakati wa Nuhu waliangamia wangapi, issue sio uwingi au uTAG ila ni nimani sahihi. We unadhani mtu akiwa tu anajitahidi kuonesha mema tayari ndio tiketi ya mbinguni jambo ambalo sio sahihi ila kitu cha kwanza ni kuokoka alafu matendo mema ndio yanafuata mara baada ya wokovu wa kweli sio wa ulioibuka siku hizi kwenye tuvikundi mbalimbali.
  zifuatazo ni hatua za mtu kufikia wokovu wa kweli;
  1. kulisikia Neno la Mungu lililosahihi kutoka kwa mtu aliyeokoka
  2. kuliamini lile neno
  3. kutubu dhambi
  4. kubatizwa kwa maji mengi
  5. kubatizwa kwa roho mtakatifu
  6. kumtumikia Mungu
  sasa we jipime mwenyewe kama unahisi kukosa baadhi ya vitu hivyo hapo juu uwe na uhakika uko feki.

 44. Walokole wa TAG huwa mnanifurahisha sana. Hongereni sana kwa kuwa mbingu ni kwa ajili yenu wenyewe. Mtaenda kwa miguu naona. Tiketi ni uTAG tu, na sio mioyo na matendo yenu. Wakatoliki poleni sana. Wote mnaelekea motoni kuanzia Papa hadi muenda Jumuiya. Hata waliyofanya wakatoliki wenzenu kama Mother Thereza ni upuuzi mtupu. In fact, kwa sasa mother Thereza anaungua jehanam, lakini yule pastor wa TAG aliyekamatwa na dawa za kulevya anashangilia mbinguni. Kilichowaponza/kuwasaidia ni MADHEHEBU waliyokuwa wanasali. Lol.

  Maarifa ni silaha kubwa sana, kisu ni mzigo.

  Naamini nimeeleweka.

 45. Inawezekana kwa wawil walopendana then tatizo kidogo litakuja kwa wazaz ,ila huwa sio tatizo sana kwa wakristo wenyewe ukienda ktk uislam inakua balaa kidogo

 46. we martha ulikuwa wapi, hiyo mada wenzako tulishaimaliza zamani na nafikiri muhusika atakuwa mpaka kashafanya uamuzi wake tayari!!!! pole sana kwa kuwa nyuma hivyo.

 47. Mke/mme mwema hutoka kwa Mungu. Na Mungu anatuambia kuwa chochote tuombacho kwa jina la Yesu tutapa Yoh. 14:12-14. kila mtu msicha/mvulana anatamani kuwa na mke mwema. na wema wa mke sio dini. Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu ndio maana kuna dini nyingi sana na zote zinaamini kuwa zinamtumikia mungu. Suala hapa ni kupata mke/mme aliyeokoka, kw sababu Wokovu ni Mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu, ndio maana alimtoa mwana wake Yesu Kristo aliye hai ili alete wokovu kwa wanadamu.

  Sasa ndugu yangu mimi nakupa ushauri ufuatao, hata kama umeshamwonesha dalili kwamba unataka kumuoa, na wewe umeokoka. Mtafute Mungu kwanza, unajua huko nyuma mababu zetu walikuwa wanaishi na wake wengi, na pengine hata baba/mama alizaa nje au kabla ya ndoa AU ANA NYUMBA NDOGO, sasa kama wewe umeokoka na umemwomba Mungu akupe Mme/mke, na ukajiona unavutiwa na mtu asiyeokoka, rudi nyuma kaanze moja na msikilize Mungu. Maana najua ulipooomba juu ya kupata mke/mme uliomba upate aliyeokoka, sasa iweje upate asiyeokoka? na Mungu hutupa haja za mioyo yetu? je tukiomba mkate atupe nyoka? anza maombi tena, na kama bado mlango haufunguki ujue roho ya uzinzi,/mitala inakufuatilia. Maana watu wasiookoka wanatemebea na roho hizo. ndio maana ndoa nyingi za watu wasiookoka hufungwa wakati wanakuwa wameshifanya tendo la NDOA na wengi wanakuwa wameshapata watoto au mimba. Kama una mfano wa watu wasiookoka na walifunga ndoa wakiwa wameshajamiiana chunguza ndoa zao hazina uaminifu, maana ile roho ya uzinzi inadai na inatawala kwa wanandoa wale!

  Hivyo kama bado wanakuja wale wasiookoka tafuta kanisa linaloamini juu ya kuvunja laana.
  Laana ni matokeo ya Dhambi.
  Kuna laana nyingi sana ambazo watu wa Mungu wanaishi nazo ila hawaujui kama hizo ni laana maana utaombewa na kuombewa, utazunguka makanisa hadi nigeria unaweza kwenda lakini kam haikuondolewa utabaki kuwa na tatizo hilo. Nitataja chahe tu. umeokoka na unaishi maisha ya hand to mouth(yaani ukipata hela ni ya kula tu, kila mara unaomba msaada wa pesa kwa wapendwa hali una nguvu na uwezo wa kufanya kazi, umesoma na una vyeti kila ukitafuta kazi hupati. Unashika mimba lakini zinatoka. ukizaa mtoto anakufa, katika ukoo au familia ndugu wanakufa kwa ajali au kufa wakiwa vijana kabla ya miaka 80, umeokoka lakini bado huruhusiwi kula vitu fuilani kwa sababu vinakudhuru, umeokoka unafuatwa na wachumba wasiookoka, umeokoka unatamani au unafanya uzinzi,umeokoka unanyimwa haki zako popote pale, umeokoka bado wachawi wanakuloga au unafuatwa na nguvu za kichawi usiku. Kumbuka mungu alipomuumba adamu na Eva aliwapa mamalaka ya kutawala na kumiliki yaani kumiliki vitu vyote, sasa iweje mtu umeokoka ushindwe kumiliki kiwanja, nyumba, gari, radio Tv, pesa nk. Lakini je Misingi ikiharibika mwenye haki atapata nini? Misingi ya watu wengi ya Mungu iliharibiwa na wahenga na mababu, kumbuka laana hukaa kweye vizazi vinne hesabu kuanzia mtoto wako rudi nyuma je waliotangulia unajua walifanya nini? Hivyo madhara ya dhambi walizofanya ndo matatizo yanayowapata wana wa Mungu leo. na enzi hizo kulikuwa hakuana dini sembuse wokovu?!! Kumbuka maombi peke yake bia kuvunja mikataba iliyowekwa na hao mababu hayatasaidia mana tatizo litatoka kwa muda mfupi tu na kurudi tena au wewe hutaona tatizo, bali litatokea kwa watoto wako. hizo ikwa uchache tu.

  ziko nyingi sana maana wahenga waliweka mikataba mingi ya kipepo ikwa ajili ya ulinzi wa kabila, ukoo, familia na mtu binafsi. wakidhani kuwa wako salama maana hawakumjua Mungu wa kweli! maana dini hizo zilianza nchi za midle east na ulaya hapa kwetu afrika na tz ziliingia miaka ya 1900 wakati babu/baba yako ndo amezaliwa na wokovu umeingia enzi zetu sisi na je uliokoka lini, kabla ya kuokoka ulifanya mambo gani kinyume na Mungu? ulitubu ndiyo Mungu amekusamehe lakini ile laana inayoambatana na hiyo dhambi uliiondoa?
  Kwa hiyo jamani wapendwa tuchunguze katika maisha yetu ya wakokovu kitu gani kimekuganda? hakitaki kutoka mojakwa moja? Nenda na neno hili: Yeremia: 5-3, na Yeremia: 50 :20
  MUNGU WETU MWENYE NGUVU NA MAMLAKA MAKUBWA AWABARIKI SANA!

 48. Nafikiri cha msingi kuangalia hapa ni swala la…….Imani moja, Roho mtakatifu na ubatizo mmoja. Kama mna imani inayofana, wote mnaamini ujazo wa Roho mtakatifu tena mnaamini juu ya ubatizo wa aina moja (maji mengi) na zaidi sana kama wote mnaishi kwa ku-reflect lile mnaloliamini, basi kwa mtazamo wangu si vibaya kuoana, lakn kama mtakuwa tofauti katika lolole nililotaja…nafikiri si sawa kuoana.
  Kwa upande mwingine,,,,,itakuwa busara sana umuone mchungaji wako na kuomba ushauri kutoka kwake

 49. asante sana Rosemary kwa kutoa ufafanuzi ambao kwa mwenye nia ya kwenda mbinguni kweli hana budi kuufanyia kazi!!!. Minafikiri ni wakati mwafaka sasa kwa kufunga mjadala huu na kumwacha ndugu yetu Abby afanye uamuzi wake sasa wa kuendelea au kuacha. UBARIKIWE SANA ABBY, TUONANE MBINGUNI!!!

 50. Shalom wapendwa
  naomba wanaosema tunahukumu wajiulize kwa nini wakitajiwa misingi ya imani yao wanaona ni kuhukumiwa? Je sio ni dhamiri inawasuta kuwa sio sawa kibiblia? kwanini uombe kwa marehemu au wafu, usujudie sanamu kisha useme hatuviabudu? kwanini kukana? Sasa mtu akisema wazi kuwa hiki sio sawa anahukumu?
  Kinachofanya mtu asiokoke RC ni ule msimamo wa kanisa hilo kuwa hakuna wokovu duniani wala mtu kwa imani na ukiri wa wokovu (Rumi 10:9-11) anaweza kuokolewa. Wao wanaamini unatakiwa ufanyiwe utakaso kwa kupitia ibada za marehemu ndio uwe na haki ya kuokolewa na dhambi. Hiki ndio chanzo cha Luther kuondoka na mwanzo wa makanisa ya Protestants, Luther aliwaambia turudi kwenye neno kwani sisi tumeokolewa kwa neema tu na kwa kufa Yesu msalabani, tunaokolewa kwa ukiri na imani yetu na si matendo (kuombewa ibada). RC waligomea hili kwani ibada za marehemu ndio chanzo kikuu cha mapato yaliyojenga makanisa makubwa Vatican. Kila ibada inalipiwa, je wokovu ni kwa fedha au kwa kukiri na kuamini Yesu alipotufia msalabani tulipokea wokovu?
  Kwa yeyote anayekiri Imani ya RC hamna wokovu hadi ufe na kuombewa ibada za wafu, sasa ulitaka makanisa ya Protestants wamkubali muumini anayekiri hakuna wokovu kwa kifo cha Yesu? je Yesu aliposema amemaliza yote msalabani bado tukajianzishie vi ibada vyetu ndio twende mbinguni, kama sina hela? kama sina ndugu wa kuniombea? Imani hii inatia shaka…
  Madhehebu ya Protestants wanaweza tofautiana kwa kuwa aidha vuguvugu kutegemea na kiongozi au waumini lakini Biblia ni ileile sio kuwa na vitabu vipya vilivyoandikwa upya kwa utashi wetu wanadamu. Kama unaona imani yako iko tofauti basi usishangae ukiambiwa sio ruhusa kushirikiana na wengine maana ni chukizo mbele ya Mungu na Imani yao. Tuombe sana Mungu atupe njia ya kweli ya kwenda mbinguni ndiye Yesu mwanae naye alituahidi Roho mt kutuongoza, kutufundisha yote. Kama unajihisi dhamiri yako sio sawa unapoabudu au kuomba vitu usivyokuwa na uhakika navyo ni wakati wa kujiuliza na kuchukua hatua sio kulalamika. Mbarikiwe na wapenda wote.

 51. Tatizo Janeth huelewi unachosema ila unajaribu kutumia hisia zako,labda mi nikuulize swali waislamu wapo wanaomjua Mungu au hawapo? ukijibu hilo swali utaelewa kwa nini mi nimezungumza hayo niliyosema hapo juu. naomba niandike kwa herufu kubwa pengine utaelewa japo mara hii, KUHUKUMU MAANA YAKE NINI? JE MTU AKITENDA DHAMBI WEWE UKAMWONA AMETENDA DHAMBI UKISEMA HUYU AMETENDA DHAMIBUI UMEHUKUMU AU UMEELEZA KILE ALICHOTENDA? HAPO JUU NIMEELEZEA UHUSIANO WA IMANI ZA WATU NA MADHEHEBU YAO. IMANI HUJA KWA KUSIKIA NENO LA MUNGU, SASA KUMBE KAMA MTU AMESIKIA NENO LILILOPOTOSHWA HUYO MTU ANAKUWA NA IMANI ILIYOPOTOKA KWANI HAENENDI SAWASAWA NA NENO LA MUNGU KAMA LILIVYOANDIKWA KWENYE BIBLIA. KWA MFANO; MTU ANAPOKUJA KUKUAMBIA KUWA TUWAOMBE WATAKATIFU AU WATU WALIOKWISHA KUFA ZAMANI ETI WATUOMBEE AMESHAKUPOTOSHA KABISA KWANI BIBLIA HAKUNA HATA SEHEMU MOJA ILIPOSEMA KITU KAMA HICHO. SASA NAOMBA UELEWE HIVI YAWEZEKANA MTU AKAWEPO KTK TAG NA AKAWA HAJAOKOKA LAKINI HICHO HAKIBADILISHI UKWELI KUWA IMANI AU MISIMAMO YA TAG IKO SAHIHI KIMAANDIKO. SASA HAPA HATUPAMBANISHI MAJINA YA TAG NA RC ILA TUNAELEZA UTOFAUTI WA IMANI ZILIZOZAA MADHEHEBU HAYO KWANI HIZO NDIO IMANI ZA HAO WAUMINI WAO. MIMI SIJAHUKUMU MTU YEYOTE ILA NIMECHUKUA BIBLIA NA KUILINGANISHA NA IMANI HIZO MBILI NIKAONA KUWA IKO AMBAYO INAENDANA NA BIBLIA NA IKO AMBAYO INAPINGANA NA BAADHI YA YALIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA. NA HAPO NDIO NILICHOKUWA NAELEZA KWA KUTOA MIFANO YA HAYO AMBAYO YAKO KINYUME NA BIBLIA KATIKA RC. NIMEYASEMA HAYA ILI KUSAIDIA MTU AMBAYE AMEULIZA SWALI LA JE ANAWEZA KUOA AU KUOLEWA NA MRC? HIVYO NILIKUWA NAMWONESHA TOFAUTI YAKE NA HUYO MRC NA SIO KUHUKUMU KAMA AMBAVYO WEWE UNASEMA. MIMI NIMEELZA UKWELI ULIVYO AMBAO UNAWEZA KUAMUA KUUHAKIKI WEWE MWENYEWE KATIKA BIBLIA. NDUGU YANGU KUOKOKA SIO KWA HISIA TU NI KWA KUFUATA NENO LA MUNGU KAMA LILIVYO BILA KUPINDISHA NA WALA KUPOTOSHA AU KUYAACHA BAADHI KWA MASLAHI BINAFSI. MIMI SIJAHUKUMU ILA KWASABABU WEWE UNAJIHISI UMEKOSEA AU KUPOTOKA KWENYE MAANDIKO NDIO MAANA UNAANZA KUJIWEKEA ULINZI KWA KUTAKA KUNIFUNGA MDOMO NISISEME ETI NIKISEMA UKWELI NINAHUKUMU. CHA MSINGI WEWE CHUKUA HATUA KWA YALE NILIYOKUELEZA NA SIO KUANZA KUNIRUSHIA MANENO YA MBONA NAHUKUMU BILA KUTAFUTA UKWELI WA KILE NINACHOSEMA!!!.

  UBARIKIWE SANA.

 52. Mungu atusaidie sana.Ninaamini ndugu Abby anaweza akapata wakati mgumu kwa ushauri kadha alioupokea hapa tena wakati mwingine kuliko hata ajenda aliyoileta hapa.Nafikiri Mchungaji wako anaweza akasaidiana nawe katika kuhitimisha jambo hilo.Siki moja nilikuwa kwenye kanisa moja la “wapendwa” nikiabudu pale na ghafla wakati wa matangazo KIONGOZI WA IBADA ile alitangaza kutengwa kwa mshirika wao baada ya kuoana na mtu asiye wa kanisa lisilo chini ya PENTECOST.Kama utaratibu huo upo pia kwa T.A.G basi ndugu ABBY ajiandae naye

 53. Je ni kweli RC hawamjui Mungu mbona mnahukumu???? Mimi ninafahamu wapo RC ambao wameokoka kabisa na pia wapo TAG ambao hawajaokoka kabisa kabisa lakini wanasali TAG

 54. Asante sana@Baika, Bwana Primi Mosile nimefurahishwa na mchango wako mzuri uliojaa ukweli wenye lengo la kusaidia mtu na sio kuhukumu kama wengine wanavyojaribu kutafsiri michango kama hii inapotolewa. Ila naomba niongezee au nifanye marekebisho kidogo tu katika sehemu uliposema ni kweli wapo wa RC waliookoka, najua ulikuwa unamaana nzuri tu yaani ulimaanisha wako watu ambao wako huko RC ambao wamemkubali Yesu kwa toba yenye nia ya kutofanya tena dhambi walizozitubu. Lakini tunaposema tumeookoka tu tayari tunatangaza kuwa sisi sio wa RC tena kwa sababu zifuatazo;a) RC haikubaliani katika misingi yake ya imani yao au katiba yao kuwa mtu anaweza kuwa mtakatifu duniani; b) RC haikubaliani na dhana ya kuwa mtu anaweza kuookoka duniani ila mtu ataokoka mara baada ya kufa; c)ukisema wewe ni mRC maana yake ni kwamba unakubaliana na kila kitu ambacho kanisa hilo linasema yaani kuabudu misalaba, ibada za rozari n.k hata kama huwa hauendi siku za hayo matukio lakini katika ulimwengu wa Roho umefungiwa nira/patano nao watendao hivyo jambo ambalo ni sawa na kusema wako wa shetani waliookoka na Mungu wetu katu hashirikiani na shetani hata siku moja. kufanya hivyo ni kuto kueleweka kiroho au kiimani; Mambo niliyoyataja hapo juu ni mambo ambayo yapo kama misimamo ya kanisa sio tu katika mioyo ya waumini wao. Kwa hiyo ili kuwa sahihi zaidi inatupasa kusema hivi hakuna wa RC waliookoka kwani kuwa m RC NI sawa na kuwa mfuasi wa yale yote yaliyo kwenye katiba yao kama ambavyo baadhi nimeyataja hapo juu. Nasisitiza hili kwasababu watu wengi sana siku hizi wamejikuta wapo kwenye huo mtego mbaya sana wa ibilisi wa kuwadanganya watu eti wanaweza kuokoka kwenye madhehebu yao huku katiba na misingi au imani za madhehebu hayo zikibaki kama zilivyo bila kubadilika chochote na hao watu kujikuta wakizitumikia na kuzikiri imani hizo kwa vinywa vyao na wakati mwingine kuzitetea either kwa kutokujua au kwa kujua lakini wakiona haya kuacha madhehebu au imani hizo. Mimi nimechoka sana na hali hii ya kuwa katikati, yaani kukiri umeookoka huku uko chini ya madhehebu ambayo yameshafitinika ndani yake yakibadili kweli ya biblia na kuingiza mapokeo ya kibinadamu!!!!! WAKATI UMEFIKA LET US DEFINE OURSELVES TO GOD AND THE WORLD THAT WE ARE SERVED AND TRANSFORMED COMPLETELY AND NOT HALF HALF LIKE THIS. Hakuna m RC aliyeokoka kwani kukiri tu we ni mRC tayari umeshakataa kuwa hakuna mtakatifu duniani na kwamba mtu haokoki duniani ila ataokoka akishakufa. Hii ndio maana ya msifungiwe nira na wasioamini yaani wale ambao kwa misimamo yao wamekataa yale aliyoamuru Mungu katika Biblia Takatifu na kufundisha yaliyo kinyume na kweli ya Mungu. KUMBUKENI NIMESEMA IMANI YA MTU NDIO DHEHEBU LAKE HIVYO MRC IMANI YAKE NI ILE YA RC!!!!
  MBARIKIWE SANA KATIKA KUFANYA MABADILIKO THABITI YA KIROHO.!!!

 55. Abby
  umepewa ushauri mwingi sana na watu tofauti tofauti kulingana na imani za madhehebu, cha muhimu kwanza ni kumwona Mchungaji wako ambaye nina hakika anauelewa na ushauri mzuri katika swala hili, pili ni kuwa ushauri unaokuelekeza kuwa wakristo wote sawa haina neno huo haukufai kwani mbele kutakua na maumivu. Wengi wameeleza jinsi madhehebu ya RC na TAG yalivyotofautiana kiimani japo wote ni wakristo. Wako sawa katika maelezo yao ni hiyo ndio tofauti ambayo inaleta kizuizi cha kuoana.

  Kimsingi hizi tofauti ni kubwa na zitakuletea matatizo sana endapo mtaoana kwa kuwa mwenzako atataka mkaabudu kanisani kwao mahali ambapo pia kuna sanamu na unapaswa kupiga goti au kuziinamia kitu ambacho ni chukizo kwa Mungu. Labda ikiwa unataka kuyarudia matapishi kama Mtume Petro alivyosema katika 2petro 2:22-24 utuambie. Kama nilivyotangulia kusema swala sio wakristo wote ni sawa, ikiwa wewe ni mkristo misingi yako ya imani ipo sawa na neno la mungu au ni mapokeo ya wanadamu?. Je wewe unaamini katika kuomba wafu wakusaidie au unamwomba Mungu aliyehai kupitia jina la Yesu?, Je unamwombea marehemu asamehewe dhambi au unamfundisha atubu dhambi kabla ya kifo?, Je unakunywa pombe na kuibariki au pombe ni chukizo kwako?. Ukiyajibu maswali hayo utapata majibu yatakayo kusaidia.

  Wapo waliosema kuwa kuna wa RC waliookoka yaani wakarismatiki, ni kweli na hata mimi nilianzia huko huko lakini sikuona kama unaweza kukwepa kushiriki ibada ambazo hazina mwongozo wa Roho Mt. Swala la kuangalia hapa je hawa wakarismatiki wanaweza kuendelea kuabudu hapo na kuacha misingi ya imani ya RC?, biblia inasema tokeni kati yao, msifungiwe nira na wasioamini hivyo ni ngumu kuokoka na kuendelea kuabudu mahali pasipo na nguvu za Roho Mt.

  Mungu akupe kutafakari kwa kina na Roho mt akusaidie, samahani kwa aliyekwazika kwani sina nia mbaya na imani yako ila nakuombea umjue Mungu wa kweli.
  Ubarikiwe.

 56. bwana Baika Mwessy na Baika Kahuta mmejaribu kwa jinsi mnavyofikiri. Laikini naomba niwaelekeze kama ifuatavyo; unaposema dhehebu ni kikundi cha watu wenye imani moja, misimamo sawa, maadili mamoja na taratibu za ibada zao za aina moja. kwa maelezo haya utaona kuwa hakuna kitu kinchoitwa imani ya Kikisto ni ile ile kama wewe unavyojaribu kueleza hapo juu. lakini pia unaposema Imani ya Kikristo ni ile ile tu hiyo imani ni ipi? wakati tayari tunatofautiana hata katika mambo ya msingi kabisa yaliyoandikwa kwenye biblia? usijaribu kutenganisha dhehebu na imani yao,kwani tunapozungumzia dhehebu tunazungumzia imani za hao walio kwenye hivyo vikundi vinavyoitwa dhehebu. kwa hiyo hapa katika huu mjadala hatujadili majina ya madhehebu bali tunajadili watu wenye imani mbili tafauti kwasababu kila dhehebu lina imani yake na ndio sababu ya hilo dhehebu kuzaliwa. Imani za wakatoliki zinajulikana na ndio zilizosababisha akina Martin Luther wakajitenga na kuanzisha vikundi vyao/madhehebu yao. kwa hiyo wakatoliki na walutheri hawako sawa katika imani zao na matendo yao. vivo hivyo wakatoliki na waTAG hawakosawa katika imani zao.
  BAADA ya kusema hayo Naomba nikuhakishie kuwa kama ambavyo unona hatari kuoana na mwislam vivyo hivyo ni hatari kuoana na mtu ambaye hafuati neno la Mungu kama lilivyoandikwa katika biblia na badala yake huingiza uongo wake na mawazo yake katika neno la Mungu huku akijidai eti ameokoka na kujifananisha na wale ambao kwa mioyo ya dhati kabisa wameamua kulifuata neno la Mungu kama lilivyoandikwa. Mfano: sisi TAG kuomba wafu ni dhambi kwani biblia inasema ole wao wawaombao wafu lakini wengine wanasema wameokoka huku wanaomba wafu kama vile BIKIRA Maria, YOsefu, mara mtakatifu fulan utuombee wakati alishasema ombeni yote kwa jina langu. SASA KUONA NA MTU KAMA HUYO NI HATARI SANA KWA SAFARI YA IMANI YAKE HUYO Abby.

 57. Imani ya Kikristo ni ile ile tu; mkristo kwa mkristo hakuna shida (msidanganyike na madhehebu). Angalizo; msije mkajichanganya na Waislam; kwani watu hawa ni wapinga Kristo asilimia mia moja. Allah sio Jehova hata siku moja.

 58. Kimaandiko; nafikiri hakuna sehemu hata moja inayoonesha kwamba mtu wa dhehebu fulani asichumbie mtu wa dhehebu jingine. Nijuavyo mimi madhehebu ni mapokeo tu. Ila tu ili familia iwe na msimamo thabiti kiimani inakuwa vyema kama ukibahatika kumpata mchumba ambaye ni dhehebu moja na wewe. Ushuhuda kuhusu mimi ni kwamba mimi naabudu ELCT; na mke wangu wakati namchumbia alikuwa Anglican, tulipooana tu – kwa kudumisha upendo haikuwa rais kila mtu kuendelea na dhehebu lake – na badala yake tulijenga mazoea ya kwenda kuabudu ELCT – siku nyingine Anglican. Hadi sasa tuna miaka 15 tukiwa pamoja na mke wangu ni kiongozi ndani ya kanisa la ELCT; ni mhudumu mzuri na mwimbaji mzuri kwenye kwaya ya Tumaini. Amekuwa mhudumu zaidi yangu ndani ya dhehebu ambalo yeye si kwamba alizaliwa na kulelewa humo.

  Wapendwa yote tuyafanyayo ni kumpa Bwana wetu sifa na wala si kuendeleza madhehebu. mbinguni hakuna dhehebu.

  Angalizo; Mkristo kwa Mwislamu hapo ndo balaa tupu! kuweni macho na hawa wanaomwabudu Allah, hakika Allah siyo Jehova hata siku moja.

  ________________________________

 59. Ndugu yangu Alexander nimeona mawazo yako mazuri, ila nimeona tusaidiane kidogo. Biblia inasema aliyemdhaifu wa imani tusimhukumu kwa mawazo yake, hapa tunachangia lakini vilevile kwa njia hii tunajua mawazo ya kanisa mtazamo mbalimbali, na kwanjia hii UFALME WA MUNGU UJENGWE, na si ufalme wa dhehebu, dini, ubatizo, au taratibu fulani. Ni vema KWA NENO AU KWA TENDO TUMTUKUZE YESU NDANI YETU. MANENO YETU YAKOLEE MUNYU NA KUMFAA YULE MWENYE KUYASIKIA. Nakupenda Yesu akubariki.

 60. Ahsante sana Mpendwa Alexanda, umeeleza kiundani sana mimi niliogopa sana kuongelea uRC lakini kimsingi tupo tofauti kubwa sana mimi niliwahi kuwa RC na nina ndugu zangu hata Baba na Mama na wadogo zangu wapo huko na kiukoo tuna mapadri 2. na masista 4. nilihudhuria Upadri wa mdogo wangu Just 1 month back. lakini kilicho nishangaza ni kwamba hata hao karismatic ambayo kati yao ni ndugu zangu waliweza kugawa Bia hadi main table ya mhesham padri ndani ya kanisa kubwa. sasa wewe uniambie kuna wokovu hapo au ni kaaina kautauwa fulani kujitahidi mambo fulani tu??niseme tu komenti nyingi za wanaosema hakuna tatizo basi hawajaelewa vizuri URC na hawajawahikuwa huko. ninadetails nyingi sana za kiundani mno zilizokinyume na Biblia Takatifu,maana nilikuwa deep sana tu huko. Mfano Mdogo tu. Padre mdogowangu alipokuwa anaomba baraka alikuwa anasema ‘’ kwa maombezi ya mtakatifu somo yangu, na bikra maria nay a mtakatifu —— wa shirika, nawabariki kwa jina la ————-amina.
  Jiulize wewe huwa unaomba hivyo????????

  NAKUSHAURI SANA FANYA USHIRIKA NA MCHUNGAJI WAKO NA WAAAMINI WENZIO KANISANI. ACHANA NA KUJICHANGANYA NA WENGINE HAO. JAPO KANISANI WAPO WASIOOKOKA PIA LAKINI KAMA UMEJAZWA ROHO MTAK. NA UKO DEEP KANISANI LAZIMA UTAWAJUA TU.KUWA NA WATU WASIOOKOKA, MAKANISA YOTE YA KIROHO YANAO, HATA WACHAWI WAPO PIA. Hata wana ISRAel walisafiri na wamisri hujasoma kitabu cha Kutoka??? Na ndio waliosababisha fujo njiani.
  UBarikiwe sana

 61. Ndugu yangu Abby,biblia imesema ndugu wawili hawawezi kutembea pamoja wasipopatana.Tunachoangalia hapo si dhehebu ila ni kufanana kwenu katika kile mnachoamini.Hivi unajua mtu anaposema ameokoka anamaanisha nini?Unajua kuna misingi ya UPENTEKOSTE?(kile wengine wanachoita ulokole) Kumbuka kuna siku utamwambia tukambariki mtoto yeye atakuambia tusubiri awe mkubwa tukambatize,kuna siku atakuambia kuna misa ya kumuombea marehemu twende(ambayo ni ibada ya wafu),atakuambia kunywa kidogo sio dhambi nk kumbuka yaliyomkuta Samson kwenye biblia.Hata mfalme Suleman naye aligeuzwa moyo na wanawake.KAMA KWELI AMEOKOKA RUKSA BUT SHOULD BE TAKEN WITH EXTRA CARE.Hivi unadhani angeokoka angeendelea kung’ang’ania dhehebu lake?Huko ana uhakika wa MAZIWA YASIYOGHOSHIWA? ANAWEZAJE KUPATA ELIMU YA UDAKTARI kwenye chuo cha UHASIBU?Kiongozi wake wa dini ameokoka ili aweze kumfundisha?Jaribu Kufuatilia ni watu wangapi waliwahi kuoa kwa namna hiyo na ndoa zikadumu.UNAWEZA KUOA/KUOLEWA NA MTU WA DHEHEBU LINGINE ILA LENYE MSIMAMO SAWA NA UNACHOAMINI BASI.Kama dhehebu lako linafundisha ubatizo wa maji mengi(kwa mfano) lazima uishi na mtu anayeamini hivyo basi(THE VICE VERSA OF THAT IS ALSO TRUE)

 62. Wengi wenu mliochangia mara baada ya mchango wa magreth mkiwa hapo juu, mkisema eti ni sawa huyo ngugu aoe au kuolewa na MRC nina mashaka sana na uwezo wenu wa kuelewa kiingereza. ninafikiri hamwelewi hiyo lugha ndio maana pamoja na maelezo hayo yote yenye detail zote zinazohitajika ili kujua kuwa ni uovu mkubwa kuoana na MRC awe najiita ameokoka au hajiiti hivyo bado mnampoteza mtu wa Mungu kwa kumdanganya kuwa hakuna tatizo!!!. Hatuchangii hapa ili kuponda misimamo ya TAG au RC ila tunataka ieleweke kipi ni sahihi mbele za Mungu. Ndoa sio jambo rahisi rahisi tu kama ambavyo mnajaribu kulifanya nyie mnaosema ni sawa kuoa wa dhehebu lolote. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya imani ya mtu na ndo yake hivyo kama unataka kufanikiwa katika ndoa yako na wokovu wako basi acha kabisa kujiingiza kwenye hicho kitanzi cha ibilisi ambacho wengi wanajaribu kukurubuni kwa kukufariji ili ujiingize kirahisi. MIMI NAKUAMBIA HIVI HAKUNA MTU ANAYEOKOKA NA KUBAKI KWENYE KANISA ALILOKUWA NALO ZAMANI AMBALO HALIFUNDISHI WOKOVU KAMA ULIVYOAMRIWA KWENYE BIBLIA KUWA NDIO CORE BUSINESS YA KANISA. Sory 4 this lakini naomba niseme, haiwezekani mtu akaaokoka katika kanisa kama RC na akabaki hukohuko hata mara baada ya kujua mambo mengi yaliyopindishwa kwa dhahiri kabisa na mengine hayapo hata kwenye biblia lakini yanafanywa ndani ya kanisa hilo alafu mtu unjua hayo yote bado unjifariji eti mi naokoka humo humo Yesu hadhihakiwi kanisa lako lilivyo ndivyo na wewe ulivyo hauwezi kuwa tofauti na kanisa lako lilivyo. Hakuna uwezekano wa mtu aliyeokoka ambaye anaweza kuridhika kukaa katika ibada za mchanganyiko wa wasiokubali wokovu na yeye akasema mimi nimekubali sasa nakaa hapahapa. Huko RC unakotaka kwenda kuoa wao kikundi cha walioongoka (sio kuokoka) yaani karismatic ni kachama tu kakitume kama vilivyo vingine mfano Rozari,Moyo mtakatifu wa Yesu n.k ambavyo vyote hukubaliana na mafundisho ya hilo kanisa kwa asilimia zote. Mfano sisi tunaamini Yesu alibatizwa na Yohana kwa maji mengi lakini wao huamini kubatiza kwa matone ya maji kichwani, je wametoa wapi hilo fundisho? sisi tunaamini kuomba kupitia jina la Yesu tu na sio mtu au mizimu au watu waliokufa,wao huomba kupitia watakatifu na hasa bikira maria, je, fundisho hilo wamelito wapi? sisi tunaamini kuwa haturuhusiwi kutengeneza sanamu yoyote ile na kuisujudia wao siku ya ijumma kuu huabudu msalaba wenye sanamu na kuisujudia na kuipigia magoti na kuibusu, hili fundisho wamelitoa wapi ktk biblia gani? sasa Abby akili kichwani mwako kama watu wenye mambo hayo na mengine ambayo sijayataja ndio wanaokuambia eti nao wameokoka na wewe unajaribu kujishawishi kuoa au kuolewa nao basi unaweza kuendelea lakini MIMI NAKUAMBIA KWA HERUFI KUBWA HAIRUHUSIWI NA WALA HAIFANYIKI HIVYO KWA WALIOOKOKA KWELI. ITS IS AN ABOMINATION BEFORE THE LORD!! NI MACHUKIZO MBELE ZA BWANA PALE TUNAPOPUUZIA MAMBO ALIYOYAAMURU MUNGI NA KUZIFUATA AKILI ZETU ZENYE UONGO MWINGI!!

  ubarikiwe!!

 63. Shalom
  Abby mi naabudu TAG kama wewe, nadhani kuna mtu amekishauri vizuri sana hapo uangalie misingi ya imani kama inafanana kama haifanani basi hauna haja ya kuungana nae katika ndoa, Mungu alikataza wana wa Israel kuwaozesha watoto wao kwa watoto wa makabila mengine, labda kama wewe ni mchanga katika imani kwamba uwelewi mambo haya kwamba misingi ya Imani kati ya TAG NA RC ni vitu viwili tofauti, naamini hakuna mchungaji wa TAG atakayekushauri uolewe na RC labda kama Mungu amekutokea akakuambia olewa nae.
  Nakubaliana na mchangiaji aliyekuambia kamuulize Mchungaji wako, maana ndiye mshauri wako wa karibu na amepewa kukuchunga na kukuombea na kukusaidia.
  Zaidi ya yopte na amini Roho Mtakatifu amesema sana na wewe ndiyo maana umefikia hata kuuliza unajua unavyoshuhudiwa rohono mwako
  ni Hayo tu
  barikiwa.

 64. Mwombe Mungu akuambie kama huyo dada ndie mke wako, kama ndio sawa endelea na kama akikwambia sio then TII mana anajua ni yupi wa kufanana nawe. nakushauri usifanye maamuzi kama hujapata jibu toka kwa Mungu. Vijana Mungu wetu ana mipango na kila mtu, mi namjua dada ambaye Roho Mtakatifu alimwambia kabisa live kua yupi ni mume wake na akamwambia pia idadi ya watoto atakaokua nao na majina ya kuwapa wale watoto. Mungu akupe uvumilivu wakati unasubiria jibu toka kwake. Ubarikiwe.

 65. Hallow Abby mimi kama roho mtakatifu anavyoniongoza nakushauri.hakika kuna raha sana kuoa mtu ambaye imani yenu ni moja,ni shida sana kumtoa mtu katika imani ambayo yeye anahisi sio sahihi, sisi kiongozi wetu mkubwa ni roho mtakatifu na hofu ya Mungu inatawala katika maisha yetu, je? una uhakika kuoa kwako hakutasababisha kumpoteza roho wako mtakatifu? swali la pili je mweza unayetaka kuwa nae kajazwa roho mtakatifu kama unahisi mweza wako ana vigezo hivyo basi atakufaa lakini kama hana roho mtakatifu basi kwa waganga kwenda kwake sio issue nzito, na elewa kwamba watu wanapotaka ndoa wanapretend hata tabia zisizo za kwao angalia ndoa isije ikakusambalatisha na Mungu wako na roho mtakatifu, mimi nina mfano wa kijana aliyeoa kwa kigezo cha kutobagua dfhehebu kwa sasa ana juta sana mwanamke anafanya vituko kwa sababu hata hofu ya Mungu hana mume uchumi ukiyumba anarudi kwao hadi mambo ykae sawa ndio anarudi na mambo mengi tu ya kusikitisha pliz jitahidi kupata mtu ambaye unafahamu nyendo zake kuwa anampenda Mungu na mshauri wake mkubwa awe roho mtakatifu si wanadamu.

 66. Friends,

  Je kuna uwezekano kisima hicho hicho kikatoa maji ya moto na baridi?

  Je kuna uwezekano kifaranga cha Tai kilichoatamiwa na kuenguliwa na ktk joto la kuku na hatimaye kikatokea na kulelewa na kuku, kifaranga icho kikawa kuku baadaye?

  Je kuna uwezekano sheria ya mauti na kifo vikawa na shirika mkataba( definition ya ndo ni contract by the way, ni covenant fyi) sheria ya uzima na uhai?

  Je inawezekana hardware ya all iron-made materials zikawa na same software?

  Je kuna uwezekano kalamu zote nga niza wino, zikatoa wino rangi ile ile?

  By the way, pale TAG alipo mhusika…amekosa kabisa mdada/mkaka? je TAG kwingine? kote miracles zote huko over?……….well, na kule FPCT,KLPT,EAGT,RESTORATION,FULL GOSPEL,KWA MAZA, MZE(YANKI TU) WA ”UPAKO”, MISUKULE RAISING CENTRE…KOOOOTE HUKO HOLAA?! You know what…basi ize tu sasa..pick even from madina, maka na madrass-alhamudurirahi rahimi twaufiq-kuruthum al shaitwan rajiiiimu ya pale kwa bibi nyau mwananyamala…..sini kuoa tu bwana, si moyo wa huyo anayetaka ku marry haujamuongoza kote TAG, EAGT,FPCT,KLPT etc but unamuongoza to the products za vatican kwa mtakatifu sana,sana, sana BENEDICT and JOHN PAUL!

 67. Kaswahili ”majibu rahisi ni kwamba hakuna tatizo” NDIYO HAYO ANAYOTAKA. kimsingi angalia misingi ya dhehebu lako maana hapo ndio unalelewa kama TAG basi unapata taratibu za TAG otherwise unajua impact ya ushirika wako na waamini wenzio(kanisa) labda kama unampango wa kuhama dhehebu kwenda RC, au simple PCM(preach commit Marry) mie si MTAG lakini najua huwa wanawafukuza wanaooa nje ya dhehebu lao. Kama wewe unaweza nenda katoliki au mwenzio aje Kwako. @C.K Rwembe, Rozemary, Sasali, Mwl—- na ndugu wenye mlengo huu, Barikiwa sana.

 68. Abby! wewe ndo unamjua mwenzi wako, je ameokoka kweli? mi ninachoamini kuwa wapo RC waliookoka kikwelikweli, je imani yake imesimamaje kumtafuta Kristo? Kaa na utafakari na ufanye utafiti zaidi ili usije ukajikuta moto wako wa rohoni unazimika, lakini kama na yeye ana moto kumtafuta Kristo, hapo hakuna pingamizi.

  Kiukweli katika suala hili, Mungu mwenyewe ndo asimame, kwani c wanaume c wanawake huwa hawana msimamo au maamuzi sahihi, ndo maana kwa sababu ya kupenda tu, unakuta mtu alikuwa ameokoka vizuri sana, baada ya kuolewa tu au kuoa, ule moto wote unafifia. Sasa hayo co matunda mazuri katika ndoa hasa kwa wakristo waliompokea Yesu.

  Naomba Abby utafakari 2Kor 6: 14-18 and 1Kor 7:10-24 mistari hii itakupa uhakika na uelewa zaidi na ujue nini cha kufanya.

  Baada ya kusoma mistari hiyo naomba Mshirikishe sana Roho Mtakatifu katika suala hili, ili aweze kukusaidia ufanye nini! usiende kwa akili zako wala kusikiliza comment za watu, zaidi soma Neno la Mungu litakupa mwangaza bora, kwani hata sisi bado tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu. Unaweze ukakuta kwa kusikiliza maneno ya watu ukatijikuta unakatishwa tamaa, na kupoteza kilicho chako.

  Roho Mtakatifu afanye kazi ndani yako sawasawa!

 69. kuna uwezekano mkubwa maana wa RC ni wakristo kama wengine hata kama hawaji kanisa moja siku ya jpili, uwe na amani kama Mungu amekupu huyo, Nakutakia maisha mema ya Ndoa.

 70. Abby,
  Sina uhakika wa jinsia yako, lakini naungana na waliokuaddress km ndg.

  Kimsingi dhehebu lako ulilomo, hilo ndio linalokuthibitishia uhalali na ukamilifu wa ibada na mahusiano yako na Mungu kama yalivyowekwa au kufunuliwa humo. Hata misingi ya wokovu ya dhehebu lako haiwezi kuwa sawa na ya dhehebu jingine licha ya hayo yote kukiri wokovu. Yaani chini ya moyo wako unapaswa uwe umechumbiwa na dhehebu lako, kulingana na mafundisho yake na uwe umeridhika na kutosheka moyoni mwako ktk jinsi ya Imani, nahivyo kuweka nanga hapo!

  Basi unaporudi ktk Maandiko kutafuta nafasi yako ktk hilo jambo unaloliendea, Upako unaotokana na hilo Neno linalokupa nafasi hiyo ambayo linakuambia “wewe ni kichwa”, ukiisha lipokea hilo, haijalishi binti anatoka wapi, maana kwa huo Upako ulioupokea kutoka ktk Maandiko, utamuongoza huyo mchumba wako mpaka kwa mchungaji wako wazazi wake wakiwa wamemuachilia aende kama Rebeka! 

  Lakini usipolipokea lile Neno, mchumba wako atakuongoza pole pole mpaka RC, “unajua, sote ni wakristo, hata RC kuna wokovu”! Balaam aliwadanganya Israeli kwa kauli kama hizo, wakawachukua mabinti wa madhebu mengine, Mungu akawaadhibu! Usioe nje ya dhehebu lako, utapata taabu kubwa huko mbele. Imani ya kwamba Mungu yuko ktk kila dhehebu ni uongo, ni siasa za dini; vinginevyo tungekuwa na dhehebu moja tu, kila mtu alipo kwenye dhehebu lake ndipo Mungu alipo! Hakuna wokovu nje ya dhehebu lako, hiyo ndiyo imani isiyotetereka. Kwa hiyo huwezi kuuacha ubavu wako ktk sehemu ambayo haina usalama!

  Basi ndg yangu, jipime kwanza ktk mambo ya Mungu, ili uone kama mmeelewana naye? Unaweza kuwa kichwa? 

  Nakuombea Hekima!!

 71. Haiwezekani,
  Kimsingi wana wa nuru hawawezi kuchangamana na wana wa giza. Ikiwa ni dhehebu linaloamini wokovu ni sawa wanaweza kuoana lakini kama hawaamini wokovu haitawezekana. Tatizo sio kwamba wote tu wakristo, tatizo ni kwamba misingi ya imani yenu iko sawa?. Kuna imani nyingi sana ndani ya ukristo kwa nyakati hizi. Mfano wengine wanabariki pombe na wanafanya matambiko na kwenda kwa waganga wa kienyeji huku wanaenda makanisani na kusema wanamwamini Mungu mmoja hiyo sio kweli kwani ukienda kwa waganga wa kienyeji na ukishafanya matambiko unaabudu mizimu ambayo ni chukizo kwa Mungu. Sasa mtu aliyeokoka hayo mambo hafanyi kwani ni machukizo kwa Mungu, hebu fikiri mkioana mtapatana?.
  Hivyo kimsingi mimi sikushauri kuoana na mtu asiyeamini kwani hapo hamna ushirika wowote ni sawa na nuru na giza. Soma vizuri neno la Mungu litakuongoza usifanye haraka mwombe Mungu atakuongoza na utampata aliyetoka kwa Bwana. Ikiwa ni mkatoliki basi ukimpata mkatoliki mwenzako au kkkt, Anglikana ni sawa kwani imani yao haijatofautiana. Ikiwa umeokoka basi yapo madhehebu ya waliookoka mengi tu soma 2 korinto 6:14-18.
  Walioana kabla ya kuamini hawana tatizo endapo mmoja akaokoka na mwingine akakataa wanaweza kuishi bila tatizo na maisha yakaendelea. soma 1 Korinto 7:10-24

 72. Nashukuru kwamba nami najifunza maana nipo kwenye wakati ufananao na ndugu ABBY japo mimi amekataa katu katu kuja kwangu ili tujenge umoja zaidi wa kiroho na kuwa na hatma njema ya watoto wetu.Mpaka ninavpoandika hapa nimembariki kwamba kila mmoja ajihoji tena upya kwa maana ya kusimamisha safari yetu.Yeye yupo tayari tufunge ndoa lakini kila mtu awe anaabudu kwake yaani yeye aabudu R.C na mimi Luetheran kwa kweli nikakosa amani katika hilo na baada ya msuguano mwingi nikafiki basi atafute mbadala japo si rahisi sana kwa pande zote mbili kwani safari imeishia njiani.Barikiweni wapendwa.Aggrey from Lutheran

 73. Tumsifu Yesu kristo:- Kwanza kabisa na mshukuru Mungu kwa mada hii. Jina la Bwana Ribarikiwe sana. Napenda kuchangia Mada hii kwa kusema kwamba hakuna Tatizo kumpata mchumba aliye tofauti na dhehebu maana wote tunaabudu Mungu Mmoja, Nia yetu ni Moja,Safari yetu ni moja, Narudia kwamba Mungu wetu abagui sote ni wamoja na wote tunakiri kwamba yeye ni YESU KRISTO NI BWANA TENA NI MFALME WA AMANI. BUT inahitajika hekima burasa upendo maelewano, na akili ya ziada na kumkaribisha roho mtakatifu ambaye sasa atakuwa kiongozi wenu maana bila yeye. shetani anafanyakazi 24hrs lazima tu kutakuwa na marumbano mmoja kati yenu aweza kujiinua nakuona yeye ndo yuko eneo sahihi. kwa upande wangu naona hakuna shida wala tatizo. Nikuelewana, kupendana, kueshimiana, kuthaminiana hata mwaweza kuzaa matundo yalio bora zaidi mbele za mungu na ndoa ikadumu katika kristo. ONDOA SHAKA YOTE YANAWEZEKANA KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU, Mungu wangu wa mbinguni Akubariki sana.

 74. “Neno la Mungu liko wazi usihukumu maana umekwisha kuhukumiwa” na ajidhaniaye amesimama aangalie asije akaanguka.

 75. Shalom wapendwa
  naona ndugu wote mmechangia vizuri kumwelekeza ndugu yetu huyu nini cha kufanya.
  Mimi nami kadri ninavyoongozwa ninaomba kuongezea kitu hapa

  Kwanza ndugu yetu Abby amegundua kuwa kuna TOFAUTI ya kiimani kati yake na huyo mwenzie, kama sivyo angeongoza tu moja kwa moja kwa mchungaji kujitambulisha na kuandaa ndoa, labda nikuulize wewe je unaweza kubadili imani ukawa RC au huyo mwenzio akawa TAG? kama sivyo basi ni nini kikwazo? hili ni muhimu sana.

  Pili kuna wanaosema kila mtu aitwaye Mkristo au kila dhehebu ni sawa mbele ya Mungu sio kweli na ukitaka kuangalia anzia na nyaraka za mtume Paulo kwa makanisa mbalimbali ndipo utaelewa kuwa unapoabudu na kulishwa neno na kukusanyika ina umuhimu kwa usalama wako na hatima yako kiroho hata kama wewe utasema uko tofauti maana “umeokoka”. Ukiangalia Wakorintho I anawaonya juu ya mengi, mahusiano, matumizi ya karama na umoja ndani yakanisa, Wagalati kuongozwa na kuendenenda kwa mambo ya mwilini badala ya rohoni, Waefeso anawaagiza kusimama na kupigana vita, Wafilipi anawasifia na kuwaimarisha nk. Sio kwamba kati yao hakuna wema ila usalama wako kiroho n ahatima yako pia inategemea wapi unaabudu. Hii inadhihirishwa na barua zile ktk Ufunuo wa Yohana kwa makanisa mbalimbali.
  Hivyo ndugu zangu kama unapoabudu ndio palipokulea ktk wokovu wako jiulize sana na upate jibu sahihi kama unapaswa kuhama au kuchangamana ktk ndoa na mtu wa imani/dhehebu jingine. Tunaambiwa mtu akitaka kuliangamiza kundi atampiga au kumpoteza mchungaji basi ina maana kile kiongozi wako anachokulisha kila leo kina umuhimu mkubwa ktk safari yetu ya wokovu hivyo simama imara (Waefeso 6) na pia uyashike na kuyatafakari yale tu uliyofundishwa (Wafilipi 4)

  Tatu kuna mtu amesema tusibaguane ni kweli inatupasa kuwa na upendo kwa wote hili ni agizo ila tumeamriwa kujitenga na ndugu au watu wanaojiita Wakristo kwa maana kuwa wameishaisikia kweli au Injili lakini wanaishi kinyume chake
  1Korintho 5: 10-13 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani? Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu. (Ina maana usichangamane na watu wanaojiita wa Kristo ila wanaishi kiunafiki, kwa kutosimama ktk neno)

  Nne jiulize sana kila mara nini kusudi la Mungu ktk maisha yako, kuna mtu anasema kuna ndoa kati ya waamini na wasio amini zina amani, sio kweli labda kwasababu wamepoa na wala shetani hajishughulishi nao maana ndie mkuu wa ulimwengu huu. Lakini amani ya kweli ya Mungu utaipata kwa kuwa na mwenza aliyekuchagulia Mungu, dada Magreth Mkiwa hapo juu ameelezea jinsi gani tunapaswa kumtafuta mwenza, chukua mfano wa Isaka na Yakobo ambao Mungu ndio aliwachagua kuwa taifa lake teule walijitaabisha kurudi kwao ili wasioe wake za Kanaani. Essau yeye alioa tu je wote si mnauona mwisho wao kila mmoja ukoje, kizazi chao kila mmoja kikoje, hatima ya mahusiano yao na Mungu kila mmoja ikoje. Mungu alikuokoa kwa kusudi maalumu muulize na ujiandae kumtumikia sidhani kama utatazama binti za mataifa na kuona wanafit kwenye plan ya maisha yako ya wokovu. Ndio anachosema mwingine kuwa kuna ndoa kati ya waumini zenye matatizo ni kutotulia mbele za Mungu ujue nani amekupangia kuwa nae ktk kumtumikia.

  Tano ndugu yetu Abby kaa ujifunze neno na kumuomba Roho mt akufundishe kuzipambanua roho, akupe macho na masikio ya rohoni ili uweze kujua nini maana ya wokovu maana kama ungekuwa unajua thamani ya wokovu wako usingeuliza haya. Kwa kifupi tu NDIO kuna tofauti kubwa na si salama kwa wokovu wako kuoana ktk madhehebu hayo na ni vizuri uwe na tabia ya kushiriki fellowship za wenye wokovu wenzio kujifunza neno na kuomba kwa pamoja ili uweze kukua kiroho na kuweza kupambanua tofauti kati yako na wasio na wokovu. Kama hujui hili muulize hata huyo mwenza kwanini haokoki au aje kuabudu kwenu utaijua tofauti yake, kama ni kwa kutokujua atakubali lakini kama ni kwa kujua kama hao ndugu Wakorintho hapo juu atakukatalia. Kama ana nia ya wokovu kweli mwache aukulie wokovu wake chini ya uangalizi wa wengine na si wewe na si kwasababu anataka kuolewa bali kumpokea Yesu, msome dada Magreth hapo juu, fellowship na wasioamini kwa kigezo cha kuwahubiria ndio chanzo cha wengi kuvutwa kuoana na watu wasioamini.
  Mwisho ninamwomba Mungu akupe macho ya rohoni, akupe nguvu ya kusimama imara ktk wokovu wako kulishinda kila jaribu linalokujia, Efeso 6: 1-18, Efeso 2: 1-22, Efeso 1: 17-23, Filipi 4. Kumbuka Mungu anakuwazia mema tu siku zote muombe lakini kuwa na saburi Yeremia 29: 11, Zaburi 84: 11-12 na Zaburi 27. Ubarikiwe

 76. INAWEZEKANA, ILA KABLA YA KWENDA KUKUBALI KUFANYA HIVYO FANYA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU AKUAMBIE KAMA NI YEYE AALIYE KUONGOZA

 77. Mpendwa Abby, nashukuru kwa swali lako ambalo huwasumbua watu wengi. Kwa ufupi ni kwamba inawezekana ukachumbiwa au kuchumbia mtu aliye tofauti na Dini au Dhehebu lako. Unajua mpendwa, watu wote duniani wameumbwa na Mungu mmoja. Isitoshe Mungu anapotaka kumpa mtu mwenzi, haangalii kama sisi tunavyoangalia. Kitu cha kuzingatia ni kwamba Ndoa ni fumbo au siri kubwa.
  Kwanza ufikirie wakati Mungu anamuumba mwanadamu (Mwa.1-2) zaidi ktk Mwa.2:21-24, Mungu hakuwa na mahojiano na Adam kuhusu kumpa mwenzi. Vilevile soma Mwa.2:23, pale Adam anaposema, ”Huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu…….”.
  Kwa mantiki hii mpendwa unagundua kuwa ndoa ni siri kubwa, na ni zaidi ya Dini/Dhehebu.
  Naamini ulishashuhudia mme na mke wa Dini/Dhehebu moja, wameoana, lakini maisha yao hayana AMANI, migogoro na migongano kila kukicha. Sasa kwa ufupi, waliponzwa na mawazo ya kufikiri kuwa Dini/Dhehebu ni ndoa.
  Vilevile naamini ulishashuhudia mme ne mke Dini/Dhehebu tofauti,lakini maisha yao ni ya AMANI. Hao waliongozwa na Mungu na mme akaupata ubavu unaofit.
  Yupo aliyenukuu Mtume Paulo 2.Kor.6:14 ”Msifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi ISIVYO SAWASAWA…….”. Maana ya Paulo hapa alimaanisha kuwa kuna jinsi mbili, ISIVYO na ILIVYO. Sasa kumpata mwenzi tofauti na Dini/Dhehebu lako aliye UBAVU WAKO ni jinsi ILIVYO SAWASAWA.
  Kwa hiyo Mpendwa kama Mungu kakuonyesha mchumba aliye tofauti na Dhehebu ua Dini yako ni sawasawa kabisa.
  Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu,si mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu. Yeye Mungu mpango wake ni katika Yesu Kristo aliyekuja kwa ajili ya wote wakiwamo wale tunaowaona hawastahili.
  UBARIKIWE SANA.

 78. Parents must only consider like-minded Christians as potential mates for a son or a daughter. This point means first of all that unbelievers should never be considered as potential mates for a covenant child. This is a common, prominent, explicit teaching of Scripture. In Genesis 24 we read that Abraham sent his servant to another country to find a God-fearing mate for his son. Leupold writes: “[T]he patriarch’s chief concern was to find a wife for Isaac who with him knew and believed in Yahweh and so would share with her husband a common faith and so allow for the deepest of all harmonies in the home, spiritual harmony. For again, only in a home where true spiritual harmony prevailed would the special heritage of Abraham be jealously guarded and faithfully transmitted to coming generations.” [132] In Deuteronomy 7:3-4 God warns the covenant people of the consequences of mixed marriages. “Nor shall you make marriages with them. You shall not give your daughter to their son, nor take their daughter for your son. For they will turn your sons away from following Me, to serve other gods; so the anger of the LORD will be aroused against you and destroy you suddenly.” God warns us that intermarriage with unbelievers is unlawful and dangerous. Such behavior led to the destruction of the pre-deluvian world (cf. Gen 6:2) and the syncretism of religion under Solomon that resulted in the division and eventual destruction of the Jewish nation (cf. 1 Ki. 11:4-14).

  The New Testament reiterates this same teaching that Christians are to marry “only in the Lord” (1 Cor. 7:39). Paul writes: “Do not be unequally yoked together with unbelievers. For what fellowship has righteousness with lawlessness? And what communion has light with darkness? And what accord has Christ with Belial? Or what part has a believer with an unbeliever? And what agreement has the temple of God with idols? For you are the temple of the living God” (2 Cor. 6:14-16). This passage applies to all unlawful alliances with unbelievers and therefore prohibits marriage (the most permanent and intimate relationship possible) between Christians and the heathen. [133] Under such circumstances Christian harmony cannot flourish because two completely contrary and antithetical world-views will exist under the same roof. Also, the intimate fellowship involved with a pagan would almost certainly compromise a consistent Christian walk. Robert Shaw writes: “The Christian who unites himself to such a partner exposes himself to many powerful temptations. He must necessarily mingle in the society of those whose views and pursuits are of a character entirely opposite to his own. His opportunities of religious improvement will be greatly lessened. Family worship can scarcely be maintained. His endeavors to train up his children in the fear of God will be counteracted by the example and instructions of his unbelieving partner. Instead of an help-meet for him in his Christian warfare, she will prove a snare to his soul. From this cause, many have apostatized from the faith, and others who have maintained their integrity have pierced themselves through with many sorrows.” [134] “Can two walk together, unless they are agreed” (Am. 3:3). Further, children raised in such a home will be thoroughly confused regarding which parent’s world-view to follow.

  The predominance of mixed faith marriages (e.g., Judaism and Romanism) in America is a reflection of the ethical relativism in our culture. Even though many people who marry come from different cultural and religious backgrounds, as public school indoctrinated Americans they often share a core world-view commitment to hedonism, materialism, and idolatrous self-worship. Therefore, their world and life views are really as not as far from each other as they appear.

  This command not to be unequally yoked also applies to apostate and heretical forms of Christianity such as Roman Catholicism and Arminianism. The Westminster Confession speaks clearly and correctly regarding this issue. “[I]t is the duty of Christians to marry only in the Lord. And therefore such as profess the true Reformed religion should not marry with infidels, papists, or other idolaters: neither should such as are godly be unequally yoked, by marrying with such as are notoriously wicked in their life, or maintain damnable heresies” (24:3). Although it is possible for a papist or Arminian to be inconsistent with his or her own church’s teaching and still be a genuine Christian, it is our responsibility to act upon a person’s outward confession and walk. If a person truly believed in the gospel of God it is extremely unlikely that such a person would remain in a church that denies the biblical doctrine of salvation.

  When people in Reformed churches marry Arminians (and such behavior is actually quite common), they are allowing the poison of false doctrine into their households. They are saying by their actions that biblical doctrine and even the truth of the gospel is really not that important. As Reformed believers who have professed the true gospel as taught by Christ and the apostles we should be obsessed with maintaining purity of doctrine in our households and churches (cf. Is. 8:20; Ac. 20:28-31; Rom. 16:17; 1 Tim. 1:3-4; 4:16; 6:3-4; 2 Tim. 4:2-4; Tit. 1:9; 2 Jn. 9-11; Col. 2:8, 20-23; etc.). It is our duty to pass sound doctrine on to our children and future generations.

  The father should protect his son or daughter by never permitting the courtship of unbelievers, Roman Catholics, Arminians and other dangerous heretics. Believers should never fall into the trap of thinking it is ok to court heretics and unbelievers with the hope that such people may change down the road. Like so-called “evangelistic dating” what often happens in such situations is that professing Christians get emotionally attached and comfortable with someone they have no business getting married to and end up making a wrong decision based on feelings instead of the Spirit-guided (i.e., through the study of the Word) intellect. Another great danger is that the unbeliever or damnable heretic may pretend to be a Christian in order to get married. The only biblical and safe policy is to stick to strict Reformed believers.

  When a father considers potential mates among Reformed Christians it is important that the person being considered be like-minded theologically. Reformed “conservative” denominations are not what they used to be. Many issues need to be discussed before a betrothal takes place. For example: What are a person’s views regarding public schools, home schooling, Christian schools? If a potential husband believes that public schools are fine and intends to send his children to a state school, the father should reject him immediately. What are a person’s views on worship? Obviously someone who holds to a strict interpretation of the regulative principle of worship (and therefore does not sing uninspired hymns, celebrate extra-biblical holy days or partake of human innovations in public worship [e.g., musical instruments, performances, children’s church, etc.]) should not marry someone who rejects biblical worship. What is a person’s view of God’s law? Many Reformed people today are implicitly dispensational in this view of the Old Testament moral case laws. One could multiply examples of issues that should be discussed. The point of raising the issue of theological like-mindedness is that fathers must take an active role in the screening process of potential mates in order to insure theological harmony in a marriage relationship. People who ignore this process can have serious disagreements and problems after marriage has already taken place. Christian women can end up being pressured to submit to things they regard as unlawful. The historical pattern has been for most women to eventually become virtually identical to their husbands theologically for good or ill. Many men also will end up dong things they regard as wrong in order to please their wives (e.g., immersing their children in non-commanded pagan-papal holy days). Parents must be diligent in the theological screening process not only because it is their job, but also because they have the wisdom and theological training necessary to do the job right.

  As a parent considers the doctrine and like-mindedness of a potential mate for a son or a daughter he should attempt to determine if a potential spouse’s doctrine is a dead orthodoxy or is expressed in a living faith. There are people who have an intellectual understanding of Reformed theology yet who don’t apply it to their own lives. If a man or a woman is dishonest, sexually immoral, can’t control his or her temper, worships money and material things, doesn’t place Christ first in all areas, etc., then such a person should not be considered no matter how orthodox his or her creed is. Further, there are young people who were raised in Christian homes that attend church each week who take Christ and truth for granted and thus are exceedingly lukewarm or even unregenerate. Such people go through the motions because of the love of family traditions rather than a zeal for the cause of God and truth. Parents should seek out mates that have a holy zeal for Christ’s kingdom. “What does it profit, my brethren, if someone says he has faith but does not have works? Can faith save him?…Thus also faith by itself, if it does not have works, is dead” (Jam. 2:14, 17).

  3. Biblical courtship involves the covenant protection of a child by the father and parents. This means that a father has a responsibility to make sure that a son or daughter is never alone with a prospective mate. This point is important because some people have an unbiblical view of father-controlled courtship. That is, he screens a prospective marriage partner yet still allows unchaperoned dating. Such a man may have good intentions and may even send a daughter to a public place such as a restaurant or shopping mall. However, once the daughter gets in the car and the car drives away, there is no chaperone. The father in such a situation can only hope and pray that his daughter’s “date” will behave himself and keep his hands to himself. With biblical courtship a couple is never allowed to spend time together in empty apartments, cars or parks.

  A father who practices biblical courtship will allow a daughter or son to spend time getting to know a prospective marriage partner in a chaperoned setting. For example, a young suitor can come over for dinner and then sit on the porch and discuss various issues with a daughter. He can take the daughter for a walk in the park as long as a chaperone or chaperones are following close behind (e.g., The scene in the movie The Godfather in which the character played by Al Pacino goes for a walk with a girl he wants to marry, followed by around 30 relatives). A couple can interact verbally and get to know each other easily even when the parents are close by. It is rather ironic that people who insist on complete privacy (and thus spend a lot of time necking and petting) are actually learning very little about each other (except perhaps each other’s anatomy).

  Covenant protection also means that prior to a covenantal commitment (i.e., engagement or betrothal) couples are not permitted to become emotionally involved. The goal of the biblical courtship process is not romance or physical affection but marriage. The courtship process is a largely an intellectual endeavor. It is primarily a data-gathering mission. Obviously there are personality and physical attraction considerations. However, these things do not at all necessitate touching of any kind or romantic expressions. Once an engagement occurs romantic poetry and speech is appropriate. But, physical sexual touching is not to occur during the betrothal period. It is only to occur after the marriage covenant takes place. “Marriage is honorable among all, and the bed undefiled; but fornicators and adulterers God will judge” (Heb. 13:4).

  4. Once a believer in consultation with his/her parents, decides it is time to seek a mate, he/she should take an active approach in the search for a partner. Some people are of the opinion that one should pray and simply trust God to provide the right partner. While prayer is a necessary and an essential aspect of seeking a spouse that does not mean that Christians are to be passive and wait for a mate to drop out of the sky. Jesus says that we are to pray for our daily bread (Mt. 6:11) and Paul says that if we don’t work we should not eat (2 Th. 3:10).

  The Bible contains examples of fathers, sons and even daughters using lawful means to bring about a godly relationship. In Genesis 24 Abraham takes the initiative and sends his most experienced servant to his homeland to find a mate for his son Isaac. In Genesis 28 Isaac sends his son Jacob to Padam Aram to find a godly wife. There also is the example of Ruth and Naomi. Ruth places herself in a position to be observed by and meet a godly eligible man-Boaz (Ruth 2:2). When Ruth’s mother-in-law discovers that Boaz is godly, eligible and a possible kinsman redeemer for her, she instructs Ruth to conduct herself in a manner that will most likely lead to marriage. “And her mother-in-law said to her, ‘Where have you gleaned today? And where did you work? Blessed be the one who took notice of you.’ So she told her mother-in-law with whom she had worked, and said, ‘The man’s name with whom I worked today is Boaz.’…. Ruth the Moabitess said, ‘He also said to me, “You shall stay close by my young men until they have finished all my harvest.”‘ And Naomi said to Ruth her daughter-in-law, ‘It is good, my daughter, that you go out with his young women, and that people do not meet you in any other field.’ So she stayed close by the young women of Boaz, to glean until the end of barley harvest and wheat harvest; and she dwelt with her mother-in-law. Then Naomi her mother-in-law said to her, ‘My daughter, shall I not seek security for you, that it may be well with you?'” (Ruth 2:19, 21-23; 3:1). Matthew Henry writes: “Naomi’s care for her daughter’s comfort is without doubt very commendable, and is recorded for imitation. She had no thoughts of marrying herself, Ru 1:12. But, though she that was old had resolved upon a perpetual widowhood, yet she was far from the thoughts of confining her daughter-in-law to it, that was young. Age must not make itself a standard to youth. On the contrary, she is full of contrivance how to get her well married.” [135]

  In a time of general apostasy and serious declension when solid Reformed churches are scarce in our land, parents (with their sons and daughters) should think of ways to find potential mates. Some possibilities are: attending Reformed conferences and seminars; making friends through the internet (and telephone) with people in other Reformed churches; visiting college age groups at larger Reformed churches; advertising in Reformed match-making services, etc. Some may argue that such a pro-active approach reveals a lack of faith in God’s providence. Historical examples in Scripture, however, teach us that while we are to pray and trust in God’s sovereign good pleasure we are to put to use our minds and plans as valid secondary agents. Abraham, Isaac and Naomi did not sit on their hands and hope for the best. They took action. They helped their children find godly mates.

  5. In biblical courtship a man must recognize the authority of a prospective woman’s father by approaching him and asking his permission to court his daughter (Gen. 2:22; 24:50-51; 29:19-20; Ex. 22:16, 17; 1 Cor. 7:36-38). It is unbiblical for a man to seek to win over a Christian woman without her father’s oversight and then if he is unsuccessful have her put pressure on her father to cave in to her autonomous decision. When a suitor approaches a Christian father and asks his permission, he gives the father the opportunity to exercise loving oversight on behalf of his daughter. If the young man is already well known by the family and church involved, the father may (after consulting with his daughter) give permission quickly. However, if the man is not well known or is a recent convert, the father will have to interview the young man extensively and do some serious investigating on behalf of his daughter. The father will want to investigate the man’s family, work experience, financial situation, recent past (e.g., what does the man’s family, friends, and co-workers think of him), conversion, doctrinal positions, future plans and so on. Given the fact that approaching a young woman’s father can be intimidating, fathers should be courteous and gracious to potential suitors. They should engage in the screening process in a friendly manner. He should set the young man at ease by explaining the biblical reasoning behind these procedures. A father does not want to scare off potential suitors by being arbitrary, intimidating or unnecessarily harsh.

  As churches return to the biblical practice of courtship, young men will understand the importance and necessity of such procedures. A man who seeks to circumvent this biblical process or who takes great offense at the screening process by fathers should obviously not be allowed to court a daughter. Such a man does not have a proper respect of lawful authority and does not want to submit to the Scriptures on this matter. A godly man will cooperate with a father and will encourage him to do his biblical duty. A Christian woman with a father who takes his responsibility seriously will be even more attractive to godly men. Such men will understand that this woman comes from a household that cherishes biblical law and applies the word of God to all areas of life.

  6. Once the courtship process begins, it is important that all parties involved understand that a father’s permission to court a daughter does not involve any promises or covenants. In other words, any of the parties involved may cease and desist from the courtship process at any time. A father may discover a serious defect of character in a potential suitor and stop the process. A daughter may decide that the man involved does not really interest her any more and cut off the procedure. The young man involved may also decide the woman is not right for him and move on. People involved in the courtship process are not in a covenantal relationship. They are involved in a fact-gathering mission-a screening process. Once it is understood that a person involved is not the right one, there is no reason to continue the process. One of the great advantages of biblical courtship is that it eliminates the desire or temptation to stay in a useless relationship because of feelings or an unbiblical concept of commitment outside of betrothal and marriage.

 79. me i think there is no probem for couples from different denominations like TAG and RC to get married provided that they do that in a manner worthy of GOD for they are both christians.if real God said that the RC are not of him ie they are not born again meanwhile the TAG are born again don’t consent for a marriage then,but we are all of GOD serving him no matter of our denominations.i give u all my blessings,go ahead in jesus name..i belong to AIC denomination

 80. Anthony, unamaanisha nn “Majibu rahisi kwetu?” jisemee peke yako bwana…. Joe, safi sana..! make kuna watu hapa duniani kwa sababu ya kiburi cha ukabila wa kidini na kujihesabia haki, wameshajihakikishia kuwa mbigu ni mali yao tu peke yao. wanasahau kwa kristo hatambui dhehebu. isipokuwa kanisa, yani jamii yote ya watu wanaomwamini na kumfuata kristo…. juntwa na mkristo, mliyouliza ni maswali ya msingi ya kujiuliza! …. ten mkristo umeeleza vizuri sana…. mimi ni mlokole ila nasikitishwa na ukabila ktk mwili wa kristo! ….safi sana mwl. sarakikya! nakuvulia kofia kwa swali hilo!! ….safi sana rova olombi!

 81. Dada swali lako ni raisi sana kujibu. Ya kwanza kanisa unaposhiriki sio ile ulipoanza naye kama sikudanganywa ya pili akuna fasi inapohandikwa kwenye Biblia ya kama kuowa ama kuolewa mpaka ku kanisa unaposhiki. Mungu alisema kitambo nendeni mukachaze Dunia na tena Bwana wetu akarudi kusema nendeni duniani pote kuhubiri NENO la BABA yake wowote atakapohamini na mumubatize kwa maji mengi.kama alipopita Yordani.
  NB kitu iko tabiya yangu ndio itamubadirisha ama tabiya yake itakubadirisha aina acha ya kuliza Pasta ama mutu yoyote.

  POLICE ya moyo wako ni ZAMIRI safi ndio Roho Mutakatifu ndio AMINA

 82. Wapendwa mimi nasisitiza kitu kimoja, tusiwe wabaguzi kwa maana tunayemfuata hakuwa mbaguzi, aliponya kwa imani ya mtu tu nawala hakuuliza wewe ni dhehebu gani kabla ya uponyaji. Hakika ninachoamini mimi nikuwa madhehebu yetu hayatatufikisha mbinguni kwa maana Yesu christo hakuwa na dhehebu lolote…
  Tushike amri kumi na maagizo yake yote na wote tutaokolewa.
  Kuoa au kuolewa na mtu wa dhehebu lingine inawezekana chamsingi nikukubaliana walau kuwa mnasali dhehebu moja ili kuongeza upendo baina yenu na kuepusha mkanganyiko na mgawanyo kwa watoto..
  Mimi ni msabato ila usabato wangu hautanipeleka mbinguni ila nikwakushika na kufuata amri kumi na maagizo yake.
  TUPENDANE..

 83. Kristo asifiwe.

  Abby “Mtumishi wa Mungu”, ukiweza kujibu swali hili basi utakuwa na jibu sahihi la swali lako:-

  Je? Jambo jema laweza kutokea nazareti?

  Mwl. Sarakikya P S

 84. Kama Unauliza Uwezekano….Mimi Nasema Kunauwezekano……Ila Kuna Vitu Vya Kuangalia, Maana najua Kuna Wa RC wameokoka, Kuna Walutheri Wameokoka na Kuna Wa TAG hawajaokoka…….Ukitaka Maelezo Zaidi Ntatoa na Mifano

 85. Ina maana ukiwa mkatoliki we si mfuasi wa Yesu kristo? maaana sisi wakotoliki tunasikitishwa sana na tabia ya kubaguliwa na wakristo wenzetu eti kwamba mimi ni mlokole na yule si mlokole mbona tunahukumiana humu duniani? ni vizuri kuangalia Yesu alitufundisha nini ktk mafunzo yake kuliko kumjudge mtu eti mimi ni mu ATG na yule ni mu rc. Mimi naona kama kweli nyinyi wakristo mliookoka kwa utashi wenu kama kweli mnaupendo wa kristo ndani yenu kwa nini msiandae mafundisho ya kuwa mkristu safi kwa kuongea na bataza la uongozi wa umoja wa makanisa ili mwende huko Rc na Rutherani mkatoe mafunzo ili basi sisi wa Rc na walutheri kwa mfano, tuwaelewe na tutoke huko ili tuje ATG.? Pili swala la mtu wa RC kuoana na mtu wa ATG mimi naona ni sawa na ni sahihi kwa sababu wote niwakristo, cha msingi ni nyinyi wanandoa kukubaliana baada ya ndoa mtakuwa mnasali wapi au kanisa gani. je wewe mu ATG kufunga ndoa na mkatoliki au kufunga ndoa na mwislamu kipi sahihi kwako?Mi ni Rc lkn huwa nasoma na kujifunza mengi sana kupitia blog hii na hata biblia pia naijua vilevile na ninaisoma kadiri roho mtakatifu anavyoniongoza na naweza sema pia hata mimi nimeokoka pia, kuwa Rc haina maana sijapokea wokovu pia.

 86. mayolwa john neno WASIOAMINI linaenda kwa dhehebu la dini au kwa mtu dada yetu anamchumba wa dhehebu la cathoric na yeye ni mTAG ss unaposema usifungwe nira na wasio amini mi sijui una maanisha nini? kwa dhehebu au kwa watu? dada yangu tukisoma vizuri biblia tunatakiwa kuoana watu wenye imani moja kwamba ss ni wana wa MUNGU mambo ya madhehebu na mafundisho ya wanadamu waliyo weka madhehebu yetu ndo yanayo tutofautisha ndo maana wengine wanaitwa wasio amini na wengine wanajiona wao ndo wananao amini. lakini ni vizuri mue na maali pamoja pakuabudu ilikuondoa matatizo kwa watoto wenu. mnaweza kukubariana mmoja wenu abadili dhehebu. na amani ya KRISTO iwaongoze katika ilo.shilikiana na wachungaji wenu na baadhi ya wachungaji wa madhehebu mengine upate ufahamu zaidi. nakutakia ndoa yy furahaa na baraka katika CHRISTO YESU AMENI

 87. ni vyema kabisa ila cha msingi ni kutazama pia huyo unayetarajia je amesimama kama wewe ili asikupeleke pabaya ukamsahau mungu kwa sababu ya ndoa,ambapo ukifa unarudi kwake.je utajibu nini? tafakari.

 88. Jamani kwani kwa wakatoliki hakuna wokovu??me mbona nina marafiki zangu wengi tu wakatoliki waliookoka..cha msingi mtoa mada huyo mchumba wako ameokoka?kama ni ndio you just go ahead with it..Mungu na awatangulie

 89. Apate mke ……anajipatia kibali kwa Bwana. suala la kuoa na kuolewa nashauri weka vigezo vya msingi wa imani ya kikristo na si mambo madogo yanayotutenganisha wakristo kama Udhehebu, Ubatizo, Rangi, Kabila au sehemu ya mtu atokako. ZINGATIA SANA;-AMANI YA KRISTO NDANI YAKO, MAANA NDIYO MTAJI WA MAISHA YA NDOA, KUWA NI PARADISO YAKO HAPA DUNIANI.

 90. Hasha!!! Haiwezekani kabisa. IMEANDIKWA 2 Wakorintho 6:14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? But both of you, you are lost. TAG dont keep 10 commandments of God annd RC changed them. Woee to you all,, unless you must change and follow the bible alone John

 91. NINGEKUSHAURI KWANZA KAULIZE MCHUNGAJI WAKO USITAKE MAJIBU RAHISI KWETU, MAANA MIMI MKATOLIKI KULINGANA NA IMANI YA DHEHEBU LANGU NITAKUSHAURI KWAMBA HAKUNA TATIZO.

  PILI KUNA USHIRIKA GANI KATI YA WALIO KWENYE NURU NA GIZA?

  TATU WEWE REFARII WAKO NI ROHO MTAKATIFU, JE HUYO MWENZIWE JE?

  NAENDELEA KUJIFUNZA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s