Muda wa Sensa waongezwa, Raisi Kikwete awataka wananchi kuwapuuza wanaoendesha kampeni kususa kuhesabiwa!!

Kwenye hotuba yake ya Taifa ya kila mwezi Raisi amewataka wananchi kuwapuuza wanaoshawishi wengine kutohesabiwa.

Muda wa kuhesabiwa umeongezwa mpaka September 8 mwaka huu ili kuhakikisha kila mwananchi aliyebaki anahesabiwa. Pia Kamishna wa Sensa kutoka NBS Hajjat Amina Mrisho Said alipokuwa na waandishi wa habari, amesema ni vema wananchi ambao hawajafikiwa na Makarani wa Sensa watoe taarifa katika Ofisi za Serikali za Mitaa au Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuhesabiwa.

Hajjat Amina alisema taarifa zinazotakiwa ni pamoja na taarifa za wanakaya waliolala katika kaya yao usiku wa kuamkia tarehe 26 Agosti mwaka huu.

Alitoa wito kwa wale ambao hawajaandikishwa hadi hivi sasa kuwa wanatakiwa watume taarifa kwa namba 2122724, 0754583415, 2129622 , 0713335429, 0713574622 na 0713312699 .

Advertisements

One thought on “Muda wa Sensa waongezwa, Raisi Kikwete awataka wananchi kuwapuuza wanaoendesha kampeni kususa kuhesabiwa!!

  1. je walio nje ya nchi ambao ni watanzania mtawaandikisha vipi na lini? maana wangependa kuhesabiwa vilevile.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s