Ujauzito kuharibika

Bwana asifiwe, Wapendwa Mimi ni dada nimeolewa Nina umri wa miaka 28,tatizo nililo nalo nimeshika ujauzito Mara tatu na Mara zote Mimba zimetoka (zimeharibika au nimepata miscarriage)

Nahitaji Msaada wa kiroho,Mimi ni mkatoliki na wakati mwingine nimekua mvivu wa kwenda kanisani japo wakati mwingine hua naenda. Nahitaji maombi ya kufunguliwa, nahitaji kusimama katika Kristo na vile vile nimekua nikifikiria Labda nijiunge na karismatic, yeyote mwenye kujua kuhusu karismatic anisaidie nahitaji kujiunga na timu ya maombi, lengo ni kumtafuta Mungu katika maisha yangu na kupata amani.

Ndugu wapendwa naombeni Ushauri Kwani nipo katika maumivu makubwa ya moyo.

mbarikiwe sana

–Theo

Advertisements

18 thoughts on “Ujauzito kuharibika

 1. Ndugu zangu wapendwa,
  Nawashukuru wote mlionipa ushauri hapa,Asante pia kwa namba ya simu ya mama bestina.
  Katika maisha yangu sijawahi kutumia dawa za kuzuia Mimba,pia katika ujauzito zote nimekua nikihudumiwa na madaktari bingwa lakini tatizo bado,namtafuta Mungu ili nipate Amani katika maisha yangu na kubwa zaidi nipate ulinzi wa Mungu.
  Mr Edwin Seleli na Mr Milinga naomba Msaada wa kiroho zaidi,email yangu ni theodorahope1@gmail.com
  Nawashukuru sana wote mlionipa mawazo yenu ninayaheshimu na nitafanya kazi yote
  Asante pia mratibu wa strictly gospel kwa kuniwekea tatizo langu hapa
  Mungu awabarikini nyote
  Thank you & be blessed
  Theo

 2. mi najisikia moyoni kukuambia tu kama upo dar es salaam panda gari linaloelekea gongo la mboto alafu shuka kituo kinachoitwa “njia panda segerea” alafu ifuate ile barabara mpaka uvuke reli alafu muulize yeyote pale kwa mchungaji maghembe ni wapi watakuonesha, pia unaweza kuomba namba yangu ya simu kwa mwenye hii blog atakupa kwa msaada zaidi wa jinsi ya kufika, naamini utasaidiwa ukifika. Mungu akubariki usiogope kwani kwa mungu hakuna lisilowezekana.

 3. Nitatumia neno ‘Pole” japo sio la kibiblia. Pole kwa yaliyokufika
  Kuharibika mimba kunasababishwa na mambo mengi, kwa uchache ikiwemo pressure (ambayo yawezekana hujaigundua), magonjwa ya zinaa kama Syphillis km hayakutibiwa vema au hayajagundulika, lkn pia HIV among other reasons. Lakini Kubwa zaidi mbali ya magonjwa, ni uonevu wa shetani kupitia wachawi ama nguvu nyingine za giza.

  Nashauri yafuatayo;
  1. kapimwe afya yako ili ujue chanzo ktk hayo niliyokutajia na zaidi ya hayo maana mimba haikai rohoni.
  2. Kimbilia kwa Yesu ambaye ni jibu la mambo yote na sio Karismatic ambako hakuna jibu.
  3. Ukishampokea Yesu tafuta kanisa la kiroho ambalo hata halijulikani sana ili mradi lina mafundisho sahihi ili ukue kiroho na kuukulia wokovu
  4. Kubali kukaa miguuni pa mchungaji mwema Yesu Kristo thru mch huyo atakayekuchunga ili Mungu akutendee unayotamani. Isaya 1:18-19
  5. Kwa kuwa untamani kumwomba Mungu, kwa hakika kiu yako Mungu wetu kwa wema wake atakujalia ili mradi ukae kwake sio ufate mikate yake (uponyaji na faida zingine personal)

  Kwa nini nasema kanisa dogo, ni rahisi mchungaji kukufauatilia kwa ukaribu na kukusaidia unapokwama au unapokuwa na tatizo kuliko kanisa kubwa ambapo wkt mwingine ni vigumu hata kumwona mchungaji.

  Nakutakia amani ya Kristo,

  Naitwa Gladys

 4. Pole sana Dada Theo.
  Hii ni hila ya shetani anataka kukunyanyasa. kwa sisi tulioamini suala la kutokuzaa, mimba kutoka au kuzaa watoto wafu haliko, kwa ujumla sisi tuko huru kwa kila kitu juu ya uzazi maana ahadi za Mungu ni nyingi sana kwetu,Isaya 65: 24, 66:9. na mingine mingi tu. Kwa kifupi ni kwamba, kuokoka tu bila kufanya deliverance hakutakusaidia kitu, mbinguni utaenda ndiyo lakini utaishi kwa taabu sana hapa duniani. Japo kuna makanisa kadhaa ya kikristo hayaamini katika Kuvunja laana”Deliverance”, lakini ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya sisi tuliokoka. Hata kama unaomba kila siku na kwa muda mrefu, tatizo litasimama kwa muda tu, na kisha linarudi tena.
  Mimi mwenyewe nilikuwa nasumbuliwa sana na nguvu za kichawi nilihangaika makanisa na makanisa, niliomba sana lakini haikusaidia sana hadi nilipovunja laana ikawa mwisho. hakuna mchawi aweazaye kuniroga. Nikiwa nimeokoka miguu ikawa inawaka moto lakini baada ya kufanya delivarance ikaisha. Kwa mfano utaona mtu ameokoka lakini bado anasumbuliwa na presure, kisukari, kansa, vidonda vya tumbo, kufa kabla ya miaka 70 na kuendelea ujue hapa kuna shida. Tuliookoka tunatakiwa kuishi huru juu ya magonjwa yote! nasema yote! ukiona umeokoka na bado mgonjwa bado yanakufuatilia ujue kuna mlango wa umeuacha wazi na pia tunatakiwa kufa katika uzee mwema! uzee! siyo kijana ni Mzee!.
  sikumbuki nilienda lini hospitali tangu nimeokoka mimi na wanangu wote tuko huru juu ya magonjwa.

 5. Isee pole kwa hayo yanayokukuta najua maumivu yake…. Nakushauri uutafute uso wa Mungu kwa kumaanisha, maana ktk mazingira kama hayo ndio MUNGU huwa anajifunua ili utukufu wake upate kutambulikana….Sasa basi kwa kuanzia okoka.. muda wako mwingi tumia kusoma biblia umuombe Roho Mtakatifu akutafsirie maana pasipo yeye hutaelewa kitu….Hakikisha kila siku unamuomba na kumsihi mungu akupe rehema, na neema zake pia akuoneshe mahali (kanisa) ambalo utamuabudu. ebu soma kitabu cha isaya 45;22-23,,,,,, 48;17-18,,,,,, 55;6-11…..na Mungu wangu akupe ufahamu….

 6. Dada Theo

  Ngoja nami niweke uzoefu wa tatizo lililokupata kwa vipindi vitatu yaani mimba 3

  Moja, msukumo huo unaoupata kwenda kwa wanauhamsho wa Charismatic anza kuufanyia kazi yaani huyo ni Roho Mtakatifu anakupa huo msukumo kuwa tatizo linalokupata linasukumwa kutoka katika ulimwengu wa roho mchafu wa shetani. kwahiyo dawa ni kuacha ukristo wa jumapili anza ukristo wa kila siku wa kuwa wanafunzi wa YESU(mwanamaombi)

  kuhusu walipo wanamaombi wa Charismatic Mama Bestina atakusaidia 0754423638 huyu mama atakusaidia maana alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya presha na kuugua mara kwa mara lakini sasa amemtwisha fedhea zake zote YESU msalabani.(yuko huru)

  Ninavyojua mimi,kabla mimba hizo hazijatoka kuna NDOTO unaota kama ufanyi mapenzi na wanaume usiowajua basi kuna ishara zozote za kusemewa vibaya kuhusu maneno ya laana za ukoo na kuna mtu alishaweka agano na ndoa yako kuwa hutaifurahia(Roho Mtakatifu anaishuhudia kuwa wewe umefungwa na maneno ya watu waliokunenea kutofanikiwa(laana)

  chukua hatua usipate mimba ya nne bila kuwa na YESU, maombi yako ya kufunguliwa yatakutoa kwenye vifungo na laana

  chukua hatua. ukishakuokoka kama inavyosema warumi 10.9-15 anza kukulia wokovu ili YESU aumbike ndani yako

  ahsante! ukipokea uponyaji wako usisite kutushuhudia.

 7. Pole sana mdogo wangu! wakati mwingine ukisasa unatuponza, chunguza huko nyuma ni vitu gani ulikuwa ukitumia kuzuia kupata mimba. (birth control).
  Yote uloambiwa, Mungu hashindwi chochote! Mwombe atakusikia na atakusaidia, nami pia nitaungana na waombaji wengine ili maombi yetu wote yafanikiwe.
  Angalizo: Ukifankiwa usisahau kutoa ushuhuda hapa hapa! miezi tisa sio mingi sana kama Mungu atatubariki kuwepo hapa duniani na mtandaoni pia.

 8. Pole dada. Mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Atakusafisha, atakufuta machozi na hatimaye utapata mtoto Esther, na utasahau maumizi yoteee! Nimeona wengi wenye tatizo kama lako, walipomwita Yesu-Simba wa Yuda yote yalikwisha. Jipe moyo Utashinda Dada. UBARIKIWE.

 9. Polesana, sana, sana dada yangu Theo…..lakini nikuambie jambo…..maadamu yaliyokutokea yamekupelekea kuwaza na kutamani kua na Mungu wa kweli, kumtaka Mungu na nguvu zake, basi habari ya jambo lako mpaka hapo kwisha habari yake…wengine matatizo kama hayo huwapelekea kwenda bagamoyo,sumbawanga na Tanga kama siyo pemba, mombasa na mafia..bila shaka unanielewa!. Sasa zingatia hili pia kua kwakua siku izi pia kuna tatizo la hawa wanaoitwa waoombeji watu…wametapakaa mjini hapa kuanzia ktk majumba na makanisa makubwa mpaka numbani kwa watu,……uhuni wa ajabu na kwakua huwezi kua na ufahmu wa kujua haya kwa stage yako ya kumjua Mungu uliyonayo sasa. ningeshauri toa namba yako ya simu ili nikupigie au andika email ktk email binafsi yangu…ili nikuelekeze kwa uhakika na mahali salama kwa watumishi salama na wa kweli wa KiMungu na KiBiblia na Ki-Imani. Naogopa pia kwa majribu uliyonayo..usije tena ukaangukia ktk utapeli wa leo wa manabii na mitume wa mijini mijini tu humu na ujanja ujanja wa kuishi ktk city Dar au izi za mke,mume na watoo sijui helicopter ministries za town na majijini tu basi! ANGALIA SANA. Tuwasiliane au wasiliana na Milinga kwa ukaribu kabla ya kuanza kusaka huko na kule waombeaji na watoa sijui laana na mikosi na uchawi na balaaa

 10. Dada yangu mpendwa, Kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kupata ujasiri wa kueleza hayo yanayokusibu bila woga wowote ule Pili nataka nikufahamishae ya kwamba hakuna jambo lolote lililo gumu mbele yake Jehova Tatu napenda pia nikufahamishe ya kwamba katika makanisa ya kikatoliki au ya kikarismatiki kama ulivyoeleza mwenyewe hakuna wokovu kwahiyo Nne nakushauri utafue kanisa la wokovu ufundishwe neno la Mungu aliye hai na ukiombewa na kujiombea mwenyewe utafunguliwa.

 11. Theo, pole sana kwa msiba huu mkubwa ambao umeuumiza moyo wako kwa kiasi kikubwa, kwani hakika kupoteza watoto (mimba tatu) siyo jambo dogo.

  Naamini umefanya bidii ya kuwaona madaktari, na pia umeshauriwa mambo mengi. Pia nafahamu kuna maelezo mengi sana ya kidaktari na ya kitabibu, lakini jibu la kweli la matatizo yote ya mwanadamu hupatikana kwa Bwana Yesu, Mungu wetu. Kwake hakuna linaloshindikana, ndio sababu Sara alipata mtoto japokuwa kawaida ya wanawake ilikuwa imeshakoma kwake. Wapo waliotolewa mifuko ya uzazi kwa operesheni kwa ajili ya magonjwa, lakini kwa kuwekewa mikono na watumishi wa Mungu, Bwana aliwarejeshea mifuko mipya (matumbo ya uzazi) na wakapata watoto.

  Kwangu mimi hili ndilo la muhimu kupita ripoti na maelelezo yoyote ya kitabibu, ingawa nawaheshimu sana madaktari na nathamini huduma zao na umuhimu wao katika jamii.

  Jambo moja napenda kukushauri. Usitafute maombi pekee ili uombewe tu, utapata jawabu la muda mfupi. Nakushauri utamani wewe mwenyewe kukipata hicho kilicho ndani ya hao wanaowaombea wengine na wakapata majibu, yaani utamani wokovu. Ukiupata huo umepata vyote, hata unapoombewa maombi yakijibiwa yanadumu, na wewe mwenyewe unajengewa uwezo na Roho Mtakatifu wa kujisimamia, na wala hautaonewa wala kudulumiwa tena haki yako na Ibilisi ambaye hamu yake ni kuona wanadamu wanalia siku zote.

  Naomba usome kwa makini, na tafuta mtu akufafanulie maandiko haya: Waefeso 6:10-14.

  Mungu akupe faraja, usikate tamaa na Bwana Yesu atayafuta machozi yako.

 12. Mpendwa Theo,

  Pole sana kwa majonzi uliyonayo. Mungu anapatikana mahala popote. Unaweza kumtafuta Mungu kwa kudhamiria moyoni mwako na ukafanya maombi maalum ya kumtafuta Mungu kwa tattizo hilo. Unaweza kufanya maombi ya kufunga wewe binafsi kuanzia masaa 12 bila kula wala kunywa chochote au siku mbili yaani saa 24 bila kula na kunywa ili umhoji Mungu kuhusu tatizo hilo naye atakujibu tatizo lako.

  Maandiko yanasema kwamba usalipo ingia chumba chako cha siri kisha eleza hoja zako naye Mungu aliyeko sirini atakupa hitaji la moyo wako.Siyo lazima uwaeleze watu wote matatizo yako. Epuka kutangaza kwa kila mtu. Epuka kujiona kwamba umemkosea Mungu. Epuka kudhania kwamba kuna mkono wa mtu au uchawi.

  Jitahidi kuwaona madaktari wakupe ushauri wa kiafya kwani wakati mwingine mimba kutoka huwa ni sababu za kiafya zitokanazo na mbegu za kike na kiume kutokukubaliana kuunda kiumbe tumboni hadi kikue kwa miezi 9. Watalaam wanasema kama kromosomu za kike 23 na zile za kiume 23 zitakuwa na hitilafu mimba haitaweza kukua kabisa. Watalam wanaita hitilafu za kromosomu au kwa kimombo “Chromosomal abnormalities”.

  Soma maelezo ya kidaktari yafuatayo (kama unajua kimombo) utaelewa zaidi hiki ninachokisema.

  Chromosomal Abnormalities, Why it Leads to Miscarriage

  “Mismatched chromosomes account for at least 60 percent of miscarriages,” says Bryan Cowan, MD, chair of the department of obstetrics and gynecology at the University of Mississippi Medical Center in Jackson, and a spokesperson for the American College of Obstetricians and Gynecologists. Chromosomes are the tiny structures in each cell that carry our genes; we each have 23 pairs of them, one set from our mother and one set from our father. Sometimes, when the egg and sperm meet, one or the other is faulty and then the chromosomes can’t line up properly. In that case, the resulting embryo has a chromosomal abnormality and the pregnancy usually results in a miscarriage. Couples who experience two or more miscarriages in a row sometimes learn, through medical testing, that they have chromosomal anomalies that don’t affect them, but do prevent a pregnancy from taking hold.

  What You Can Do

  If you have one miscarriage, be patient. The odds are strongly in your favor that you will get pregnant again and deliver a healthy baby. If you miscarry again, however, consider preserving the tissue you pass (if possible, save it in a sterile saline contact-lens solution) and take it to your physician to be sent to a lab for chromosomal testing. “If it’s chromosomally normal, we can immediately start looking for other issues that may be responsible for the miscarriages and may be treatable,” says Jonathan Scher, MD a fertility specialist in Manhattan and co-author of Preventing Miscarriage: The Good News (Collins 2005).”

  Hata hivyo, wewe ni miongoni mwa wapendwa ambao wameshinda mtihani wa kuchekwa na jamii kwamba HUZAI. WEWE UNAZAA. KIZAZI CHAKO KIPO OKAY. Sitegemei kwamba utakutana na kejeli za wapendwa au ndugu wakuchekao kwamba huzai, mara unajaza choo, mara hana mtoto, nk. kumbuka wewe umebeba mimba na ikatoka mara 3.

  Kumbuka kwamba wapo wapendwa wengine hata mimba ya kutoka hawajawahi kuiona kabisa tangu wameolewa. Hebu watafakari hao nao. Ninao mfano wa mke wa mchungaji mahali fulani ana miaka zaidi ya 25 kwenye ndoa na hajawahi kuona hata mimba ya kuharibika na anaendelea kumtumikia Mungu. Pia kanisani ninaposali kuna ndoa za wapendwa kadhaa ambao hawajaona hata mimba inayotoka na wanaendelea kumtumikia Mungu kwa uimbaji na huduma zingine. Wewe umeziona mimba hizo 3 zikitoka. Hebu tuliza moyo wako. Hebu hesabu hayo kwamba ni maajabu ya Mungu wala siyo majaribu.

  Kumbuka kutopata mtoto siyo mwisho wa dunia. Naam elewa kwamba kutopata mtoto siyo ulemavu. Ugumba siyo ULEMAVU wala hakuna mwanadamu mwenye UWEZO WA KUUMBA. Mungu Muumbaji ndiye awezaye kuumba au kutoumba kwa kupenda mwenyewe, wala wanadam tusione kwamba ni ajabu.

  Natumaini maelezo haya yatakuwa yamekusaidia sana. Nenda kanisa lolote lenye kuwa na utamaduni wa kuombea wenye matatizo kila Jumapili au kila mara nawe utaombewa na kuona mzigo wako wa moyo ukituliwa kabisa.

 13. Pole sana kijana. Najua uko na hali mbaya hasa katika ndoa yako, lakini jipe moyo, utayashinda majaribu, muombe sana Mungu na muulize ni kwa nini uendelee kushuhudia mimba zikiharibika, ni nini mapenzi yake? Wakati mwingine ukiumwa na mbu wa malaria ni vizuri ukamuona daktari si maombi tu, hivyo na tatizo lako ni vizuri ukawashirikisha madaktari, kwani wapo kwa ajili ya Mungu.

 14. Pole siste Theo naomba jitahid kufikiria twice mi sioni kama unajua nini tatizo lakini tatizo lako na la kiroho hebu kama unataka kupona ondoa udini nenda kanisa lolote la kiroho hapo utapata soln ya tatizo lako.

 15. Pole sana dada! Ukatoliki si tatizo, tatizo liko kwako, sasa mimi nataka kujua uko wapi ili niweze kuku-recomend kanisa ili uende ukafunguliwe kabisa na uwe huru?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s