Hongera Tete Runiga

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Kenya, Tete Runiga amefunga ndoa takatifu nchini humo, kwa sasa anatambulika kama Tete Meshack. Tete anayesikika kwa album ya NIMEPATA RAFIKI ni mdogo wa Marehemu Angela Chibalonza . Tunawatakia kila la heri kwenye maisha yenu mapya.

Sikiliza wimbo wa Tete NATAKA KUWA NA WEWE

9 thoughts on “Hongera Tete Runiga

 1. Salom

  Bishop Odak , umesema kweli haya mambo yapo na yanaendelea ndani ya ukristo mpaka kwenye nyumba za ibada!!!!

  Wakina dada hebu tuwahurumie hawa watu wa mungu wanataka kuiona mbingu jamaniii!
  mh!! kilio cha wanaume hicho .

 2. Sasa jameni jameni jameni! Cha kwanza tukumbukeni kwamba kuna opendo mara pili kwa wadada kwa wazee wao na opendo kwa mwenyezi Mungu. Huyo dada anatumikia wafalme wawili mume wake na Mungu wake. Sina shida na mavazi ya mdada ambao ameolewa. May be mume wake anafurahia mavazi hayo. Shida yangu jameni jameni ni ya kwamba macho hainanga pasia. Ukweli ni ya kwamba nyakati za mwisho wasichana watazidi na urembo na ni kweli. Tangia mwaka wa 70s hakuna msichana sura mbaya. 90 % ni mwili kama malaika. Ukiongeza mavazi ya kufunika nusu mapaja na nusu nyonyo, tumbo ndio hio wazi , mdomo ni hio nyama fresh, nywele ndio hio mkia ya farazi. Yani yani yani alafu wana keti kwa viketi za mbele kuelekeza askofu aliepakwa na kufanya mujiza za uponyaji. Sasa hebu uniambie kama macho ya askofu iokoke. Tena hao ndie wa kwanza kuanza kurukaruka na maluga na kuanguka chini ovyo hovio. Jameni wadada mtusaidieni. Mjifunike mwili kizi ya kupendeza Mungu. Hayo mavazi ni za kusumbwa meili yetu. Kama vile mama anapendeza mume wake, wewe msichane pendeza Mungu wako. Wacha kuniambia eti macho yangu iokoke. Haitaokoka ukiwa na nguo nusu. Tusidanganyane. Dates za lunch zilianza lini ndani ya town jumatatu? Ilianza na mavazi za kufunika mwili nusu in the sanctuary. Alafu wanakwa wazuri kwa kutowa sadaka kwa bahasha ya kunyamazisha askofu kutaja bikini kwa mahubiri. Yani yani yani jameni. Tumecompromise injili takatifu na pesa na fashion ya warembo.

 3. Balozi wa Yesu ni yule yule mchana au usiku. Maadili au adabu si ya muda au hafla fulani tu, ni wakati wote. Kuchanaganya si sawa!

 4. Nashangazwa na wapendwa wanaopiga kelele kuhusu mavazi. Hivi wasichana wakivaa mnashawishika kuwaza uasherati na uzinzi? mi nawaomba ndugu zangu katika Bwana macho yenu yaokoke pia. ili msiwe mnafanya nao kwa kuwaza tu. Mungu aturehemu!

 5. Wapendwa,

  Ukienda kwenye sherehe za siku hizi, tena za wapendwa kabisa wa makanisa yanayohubiri wokovu na maisha matakatifu, utakutana na mabinti wasindikizao Bwana na Bibi Harusi wakiwa wamevalia nguo zinazofunika nusu ya mwili tu. Yaani nguo zinazofunika nusu mapaja, kiuno, tumbo na chuchu tu. Huu ni ukengeufu au ndiyo mafunuo mapya?

  Mimi nilitegemea kwamba nguo kama hiyo aliyoivaa dada Tete aivae akiwa sehemu ya faragha na mumewe kipenzi. Kumbuka kwenye Harusi unawavalia watu wote siyo mumeo tu. Kwenye hadhara ya watu kila mtu anakutazama kwa jicho tofauti. Hicho kifua kukiacha wazi mbele ya halaiki ya watu wakati ni cha mumeo kulalia na kukiinjoi mkiwa faragha mimi naona kama ni ukengeufu kabisa.

  Mbona kuna mavazi mengi yanayofunika makwapa na kifua cha mwanamke. Mbona mavazi hayo yanapendeza tu? Mpaka kifua kibakie kitupu hadi kwenye nyonyo? Et ndo kupendeza?

  Dada Kemi, huwezi kusema hivo eti mtu anavaa anavyotaka? Mbona unachekesha. Hivi kama ni kuvaa unavyotaka unaweza kwenda umevaa chupi peke yake kwenye harusi kwa sababu tu ni siku ya harusi? Mbona hujawahi kwenda umevaa chupi tupu au skin tight tupu? Kumbuka Harusi ni ibada takatatifu. Kumbuka pia sherehe ya harusi haina maana kwamba inapaswa kuondoa maadili ya uvaaji wa nguo kwa sababu tu ni harusi? Maadili ya mkristo hata akiwa kwenye sherehe kama harusi hayapaswi kuporomoka kwa hoja kwamba anavaa anavyotaka kwa sababu yuko kwenye harusi. Huu utakuwa ukengeufu mkuu.

  Tafakari kisha chukua hatua za kiroho.

 6. Harusi ni siku maalumu kwa wana harusi mtu anavaa anavyotaka. kwani anamvalia nani? Tumshukuru Mungu pamoja na dada Tete kwa kupata mume.

 7. Sio yeye tu mbona hata waimbaji wa nyimbo za injili wanavaa hivyo? Sio vizuri lakini hii ni harusi tu tuwashauri basi waimbaji wanaosimama kanisani wavaee mavazi ya heshima jamani.

 8. Hongera sana wapendwa.

  Baada ya pongezi nyingi, hebu wapendwa tujadiliane, haya mavazi wavaayo bibi harusi wengi yakiacha kifua wazi chote kasoro sehemu ya matiti au chuchu tu, hivi ni nguo za maadili ya kanisa la leo?

  Kwa sasa inaonekana kwamba bibi harusi wengi wanavaa mavazi yanamna hiyo. Mavazi yasiofunika kabisaaa vifua vyao au makwapa yao, je kanisa limeshayakubali kama mavazi rasmi ya kuvaa siku za sherehe na harusi?

  Huku tukimpongeza mpendwa wetu kwa kufunga ndoa, naomba wapendwa tujadiliane hoja hiyo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s