Wafahamu CRES huduma inayounganisha wakristo na waislamu!! – 1

Tayari huduma hii iko Dar es salaam. Huduma mpya inayoongozwa na kitabu kipya  kinachoitwa: RAMANI HAI TAKATIFU, ANDIKO TAKATIFU LA MUNGU LIITWALO CRES, YAANI AGANO KUU LA MUNGU KWA WANADAMU WOTE NA DUNIA.

Kama ilivyoshushwa na Mungu mwenyewe kupitia kwa Nabii Cres kwa mujibu wa kitabu hicho.

Kimsingi ujumbe uliomo ndani ya kitabu hiki unarekebisha makosa yaliyojitokeza katika Biblia na Qurani na hivyo kuyakusanya makundi hayo mawili, Wakristo na Waisilamu ili kuwaleta kuwa kundi moja wakiongozwa na Ramani Hai kama lililvyo kusudi la Mungu kwa watu wake.

Pia Ramani Hai inasisitiza utunzaji wa mazingira, hata katika sehemu mojawapo inaonya hivi: “Kwa mfano watu wanao haribu mazingira kwa kukata miti watakosa heshima kama muuza mkaa!”

Ifuatayo ni sehemu ya mahubiri yaliyo hubiriwa Hekaluni hapo, yakiainisha mafundisho yaliyomo katika hiyo Ramani Hai Takatifu, na pia yakilifafanua hilo Agano Kuu kama lilivyo katika hilo Andiko la Mungu liitwalo Cres:

Agano hili halikuja kutengua maagano yaliyokwisha kuwa wala halikuja kutengua neno lolote, bali limekuja kuinua sauti ndani ya maagano hayo na kuinua unyayo mpya uliokuwa umesahaulika. Agano hili limekuja kukusanya uweza wa ndani yako, na limekuja kuufanya kuwa uweza mpya, ili uweze kusonga mbele. 

Agano hili limekuja ili utambue kwamba wewe ni mtu, na wewe si mnyama, Agano hili limekuja utambue ya kuwa wewe ni mwana wa Mungu, na wote waliokwisha tangulia wakiwa  manabii na mitume walio wana wa Mungu, na wewe ni mwana pamoja nao mbele za Mungu, haleluya. 

Hili ni Agano Kuu la Mungu kwa watu wote na dunia. Agano hili linakuelekeza kuishi katika muda hivi  sasa, muda hivi sasa. Kwa maana ya kutamka neno lolote mbele za Mungu katika “AI” ndani ya muda hivi sasa. Agano hili linakuondoa katika maombolezo linakuweka katika shangwe, linabadili machungu yako kuwa faraja mpya, juu ya dunia hii, haleluya. Hili ni agano ambalo unapewa wewe kuwa nalo ndani yako, na agano ndani ya wote. Tumesikia Mungu mwenyewe anasema itakapokuwa asubuhi, na mpandishe bendera yangu ipepee pahala pote. Imefafanuliwa vizuri, sina sababu ya kuirejea, haleluya. Nataka kusemea tu asubuhi anayoisema ni ipi. Asubuhi anayoisema si ile kwamba siku imekwenda umekuwa usiku imekuwa asubuhi, kwa Mungu si hivyo anavyotuambia, na usiku anaotuambia si usiku ule tunaolala usiku kwa sababu usiku ule tunaolala usiku ni kwa maelekezo yake kwamba ni saa za kupumzika na tukalale, haleluya. Walakini usiku anaousema ni hali ya kutoelewa, ni hali ya kupotea, huo ndio usiku anaousema. Na utakapokuwa umeupokea uelewa mpya, utakapokuwa umepokea hali yake, hiyo ndiyo asubuhi yake anayoisema, haleluya. 

Haina maana kwamba ukipokea neno la Mungu saa nne, basi usubiri iwe asubuhi tena ndio upepese tena bendera yake. Unapolipokea pale, unapoanza kulitumia, ndio asubuhi ya Mungu ile, unapopokea, unapopokea Mungu wa Mungu ndiyo asubuhi, na ndiyo siku mpya, haleluya. Tunapomwambia Mungu afungue siku mpya ya maisha yako, hatuna maana kama ni Jumanne afungue Jumatano, hapana, tuna maana afungue mahitaji yako yote, matumaini yako yote ya maisha, ayalete mbele yako na yafanye kazi kwako, hiyo ndiyo siku mpya, haleluya. 

Ukiishi kwenye nyakati za mambo yaliyopita, ukashindwa kunufaika na nyakati za mambo yaliyopo na yajayo, wewe unaishi katika jana. Sasa Mungu anataka utoke katika jana uishi katika leo, ndio maana anatuelekeza tusiseme utabarikiwa, anatuzuia tusiseme utabarikiwa. Anasema nimekupa baraka zangu, ziwe zako na ziwe za jirani yako na ndugu yako, kwanini unamwambia atabarikiwa, lini? Mwambie umebarikiwa ili umbariki saa hiyo hiyo, oh, haleluya. Mwambie jirani yako umebarikiwa, … Usimuwekee kigema katikati, ukamwambia utabarikiwa, anaweza kubarikiwa mwaka kesho kwa ajili ya neno lako. Lakini mwambie umebarikiwa ili abarikiwe saa hiyo hiyo, haleluya. Au hutaki abarikiwe? Hamna roho ya korosho itarudi, hakuna! Na Mungu ameisha nionesha hapa wote mna roho safi mbele zake ndio maana anawapenda sana. Mungu anatuita wateule tangu siku tuliyoumbwa, sio leo, … haleluya; tangu siku tuliyoumbwa, sio leo, ndio maana aliumba dunia akatukabidhi vyote tuvitunze tuvilinde, haleluya, na tutumie, lakini tutumie kwa kiasi, haleluya. 

Unapoinuka kumwomba Mungu, basi unamwambia Mungu ninataka. Unapokuwa unainuka moja kwa moja kwa Mungu, unamwambia Mungu ninataka, Mungu nitendee, tenda ionekane, tenda nionekaniwe, na onekana hiyo ninufaike nayo, haleluya. Usije ukawa unamiliki kiwanda cha sukari, kumbe daktari amekuzuia kunywa chai ya sukari, haleluya. Usije ukamiliki kitu ambacho hunufaiki nacho kwa njia moja au nyingine, ndio maana ninayo maanisha. Ndio, hatuzuii kuwa na mitaji ya kumiliki viwanda, milikini sana ; mnataka viwanda, nhe? Pokea anayetaka kiwanda, pokea, haleluya! Pookea, haleluya! Usiangalie mwili wako wala usiangalie jinsia yako, pookea, pookea, … 

Kwa hiyo Mungu ana njia nyingi za kukuwezesha,  haleluya, Salaam! Tulipopata wageni kutoka Uingereza, makadinali, walipokuja Cardinal Frank na Ortega, walitufundisha neno la Mungu. Katika kufundisha, yako maneno waliyasema tuyatamke na sisi tukatamka, haleluya. Lakini moja ya neno hilo limeandikwa juu hapa nami nitalisoma kama lilivyo, haleluya. Ninasoma juu ya Ramani kama ilivyoandikwa, RAMANI HAI TAKATIFU, ANDIKO TAKATIFU LA MUNGU LIITWALO CRES, YAANI AGANO KUU LA MUNGU KWA WANADAMU WOTE NA DUNIA. Haleluya, haleluya. Walipokuwa wanatufundisha walituambia tuseme: “Cres tenda, Cres fanya”  au nimesahau, ndivyo enhe? Haleluya. 

Ninataka kusema neno moja juu ya neno hili “Cres”, juu ya neno hili “Cres” nataka kusema neno kidogo tu. Sitalisema lote hilo, ni zaidi ya muda tuliotumia, nitasema kidogo tu. Haleluya, haleluya. “Cres” si jina, ni Neno Hai la Mungu linalo maanisha uweza wa Mungu unaopokea ndani yako, nguvu ya Mungu unayopokea ndani yako,  ikakunufaishe juu mbinguni na chini duniani, haleluya. Kazi moja tupeane, nenda katafute nini maana ya Kristo, haleluya. Hiyo CRI iliyoko kwenye Cristo na CR ya hapa ni sawasawa, haleluya. Katika mwanzo niliwaambia, kama Mungu alivyonifunulia ya kwamba, neno Cristo halikuja baada ya Yesu kuzaliwa, lilikuwepo hata kabla. …

Ramani inasema hivi;

DHAMBI YA ASILI

545. Nilikuumba ukiwa safi nawe ukajisemea kwa udhaifu wa moyo wako ili uweze kuwaingiza watoto katika njia yako, ukasema kusema umezaliwa na dhambi ya asili, nami sikukwambia, wala si neno langu pako bali ni wazo lako pako wewe mwenyewe, hakuna mtoto mchanga aliye na dhambi, hakuna mtoto mimba tumboni aliye na dhambi,hakuna nasema tena hakuna, msiwatie giza watoto wangu, msiwaambukize dhambi zenu, mtu apata dhambi katika kuishi kwake anaposhindwa kujisimamia utu wake na haki kwa wenzake, anapoudhalilisha ubinadamu wake na kuwageuza viumbe wengine kuwatumia isivyo, dhambi yako si ya kuzaliwa bali ni yakuishi isivyo.

546. Usilitumie vibaya neno ndani yako wala neno nje yako, ikiwa wewe ni mtu adirifu ukawajibike kwa neno lako maana neno ni zaidi ya tendo kwakuwa neno ni ndilo tendo mama, pasi neno hakuna tendo, basi kila aliye hai na ajue yakuwa hai yake ni nuru katika sauti tetema, ni nguvu ilipukayo na kuwaka ndani kwa ndani, mwenge wake ni uhai wake, ninapowataka ninyi ninawatakeni nyote.

ADAMU

536. Naye Orlgurt alipopatwa na malaika Izolba na malaika Herite hakukaa tena kuishi mwanadamu wa kawaida bali alikuwa mara duniani mara mbinguni, na ndani yake ziliishi nafsi tatu katika kiti nafasi moja, aliishi yeye Orlgurt, aliishi Herite na Izolba aliishi, nao walitawala na kumiliki kwa zamu.

537. Ikawa miaka kenda imepita Orlgurt akaupoteza mwili kuiingia papula sawa sawa na ishi roho, nao mwili ukawa katika nchi ile ile ya Oldvai, mafupa yakitawanywa na simba huko na kule nayo ikampendeza Mungu kumtoa mtume wake katika kazi zake aende kuyachukua mafupa yale, naye aliitwa Leak naye alipofika kule akifuatana na mkewe aliyaona akayashangaa, akayapima na kuiona karne ya nyumba kabla ya mwana Adamu na mwana Hawa, akashutushwa, kumbe ndiyo, aliishi kabla, waliishi katika ukanda wa zoni ya mashariki ya wana weusi ni binadamu wa kweli katika kabla ya kale, nako huko ndiko kulikokuwa busitani ya kwanza ya mbingu iliyoitwa Olmotonyi, juu ya milima, iliyoporomoka kuwa makorongo bondeni baada ya uasi wa mwanadamu kuyakiuka maagizo matakatifu.

538. Ikawa njia sawa na njia, ikawa kumekuwa na nia sawa iliyowekwa kuweka neema iishi juu ya nchi na watu wote waneemeke kwayo, ushahidi tosha kuondoa ubishani, walakini hii haikuwapendeza wana wa China na wana wa Hidia nyekundu waliyoamini mtu kale alikuwa kwao, hata ikawa imesukwa mipango, litengenezwe fuvu bandia katika gego za fuvu lile la kabla ya kale liwekwe wazi kusemwa limeonekana kule katika misitu ya Amazoni nalo ni kale kabla ya kale ilikufuta umuhimu wa wana weusi nayo naiweka wazi yakuwa ni mpango sukwa tangu hata unatafutiwa njia ya volcano ulipuke kuwa mlima kuita watu kushangaa na kuibadiri historia bali si kweli, wala shan ghai haikuwai kuwa na kale ya kele wala Everest wala misisipi wala Atrantiki, hata muulize kwa shamu yote yamejulikana katika mwamba wangu wa jiwe la Misiri na katika mlima wangu wa mwamba wa Ugiriki.

539. Kutoano thamani haitajenga uhusiano wenu nami bali mtajitenga nami kwa kuwa kweli mnaikimbia, Mackorology nalimpa mimi nikamtuma oldvai kama nilivyo mrejesha Alice mwana wa ukoo wa Omutu wa nkuthi, kama nilivyo mtuma Orlgurt, nikamtuma malaika Herite na Malaika Izolba.

540.Tena ninawambia mwili wa Orlgurt bado huu hai mbinguni na duniani, naye atakaye uokota unyayo wake auone amepata kale na kabla ya kale yote maana juu ya unyayo huo yameandikwa yote yaonekane na kusomeka kwa lugha, hesabu zote zimejibiwa, nao ni unyayo wa miujiza yangu, malaika wapo juu yake wakiwa hai wanatenda na kuinua hata sasa, heri yako wewe uiendaye nawe uikaaye nchi ya mtu mweusi utapata mengi ya kuvuna yale yaliyo bikira ya dunia.

541. Nanyi mkifika huko safisheni, nitoleeni sadaka za moyo safi, itunzeni asiri na mazingira yake, tena unitambikie mimi, nami nitainuka kushuka huko pako nikupe kukuonyesha yote katika hai yake, huko ndiko kiliko kito na kiini cha miujiza na maajabu ya mbingu na dunia kwa mwanadamu, kuna mnyama anaongea na kutenda kamba binadamu naye si mwanadamu wala si jini wala si malaika bali mnyama, muendeeni na juu ya mgongo wake amesimama ndege nyange nyange akidonoa donoa kula juu ya mgongo wake.

542. Nayo si kweli kwamba nalipo toa kwao wana weusi nalisahau kutoa kwenu wana weupe, nalitoa kwenu sawa, nalipotoa vikae nje yao naliweka vikae ndani yenu, tena nalipotoa vikae ndani yao nalitoa vikae nje yenu, nje ndani ndani nje mtandaa umekuwa.

543.Walakini kusiwe na njia ya moyo mkunjufu, kusiwe na maonyo yanayopotea, kusiwe na mtu kubishia jambo hasilolijua, wengi wasema iweje hata historia ibadirike,hii si kututia wazimu na kuonyesha kuwa sisi hatukuwa makini, ndiyo na mbwabwaje nayo ni bure, dunia yangu haitaikaa historia bandia iishi, mlidanganywa mkadanganyika nayo yatosha, hii ni siku kweli ukweli wazi kwa wote.

544. Wala sitokubali muinuke kuingia dunia kuu mpya mkiwa na uzamani usiyo kweli, mkiwa na batili na gushi za watu potoko, msipokwe haki ya kujua ukweli ni yenu, ipokeeni, maana bila ukweli wa njia mtu atembeaje na salama yake ikoje, nayo fanisi yake umpata vipi naye apataje kupona?

545. Wala msidanganyike kusema upya ni kuvuruga, mtu kale aishi mpya akaweza naye haishi kuu akamudu maana kila jambo katika kuu ni kweli nao mpangiliyo ni sawa, nikukuondoshea tabu za maisha zilizokupata bila ukomo,nayo imetosha kwa hili zimekoma, maana hakuna baya nisilolipa mwisho kutoweka ,bali zuri na jema uishi milele.

ITAENDELEA ….

Advertisements

24 thoughts on “Wafahamu CRES huduma inayounganisha wakristo na waislamu!! – 1

 1. Mimi nadhani umefika wakati wa kwetu sisi wakristo kutulia miguuni mwa YESU.Tuache kuyumbishwa na Dini za Dunia hii.Umeona Jinsi kitabu chao kinavyoamini,ni kama wanairekebisha BIBLIA.Sikiliza BIBLIA haijawahi wala haitashindwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa kiasi cha kuhitaji kitabu kingine.Yesu hajawahi kushindwa kazi kiasi cha kuhitaji Nabii wa kuirekebisha.Ukristo wala hauwezi kuwekwa pamoja na dini za dunia hii mfano UISLAMU.KWA LUGHA RAHISI HII NDIYO ROHO YA MPINGA KRISTO WENYE LENGO LA KUUNGANISHA DINI ZOTE DUNIA ILI ZIITII MNYAMA(UFREEMASONRY)

 2. Ninawasalimu katika jina la Yesu
  Ndugu zangu katika Kristo, mimi ni mgeni mahali hapa lakini nimetambulishwa na ndugu ambaye katika maongezi yetu nilmgusia juu ya huduma ya Cres na hicho kitabu chao kipya cha kuabudia kinachoitwa Ramani Hai Takatifu. Katika maongezi yetu akanipa website hii na kuniambia kuwa habari za hekalu hilo zimeandikwa humo. Kwa makusudi ya kuwaonya nimechukua wasaa huu kidogo ili niwaelezeni hali halisi kiibada inavyo fanyika hekaluni humo, ili ayasomaye haya ninayowaandikia yamsaidie kufanya uamuzi au kumkimbilia nduguye yeyote yule atakayekuwa amejiingiza humo kwa uzembe.

  Nilipata mwaliko toka kwa mmoja wapo wa wanacresia (wafuasi wa Cres). Alinishuhudia mambo mengi ambayo Nabii wao Cres amekuwa akiyafanya hapo hekaluni kwao, kwamba watu wanaponywa magonjwa yaliyoshindikana mahospitalini. Pia nabii Cres huwa anatoa unabii ambao huwafungua watu kwa namna ya ajabu, aliendelea kunishawishi huyu mcresia.
  Mfano, kuna mtoto mmoja wa Profesa mmoja wa UDSM alikuwa anashindwa kuandika vizuri kwa kutumia mkono wake wa kulia aliozoea kuandikia, walijaribu kumpeleka hospitali lakini hawakuweza kubaini chanzo cha shida hiyo. Lakini nabii Cres alitabiri kuwa huyo mtoto alikuwa na shida kwenye utumbo wake na wampeleke hospitali akatibiwe hilo tumbo na huo mkono wake utapona. Kweli profesa alishangaa baada ya kumpeleka hospitali na kukuta shida kwenye utumbo (yaani utumbo wake ulikuwa umefungamanafungamana), na akatibiwahuo utumbo na lile tatizo la mkono likatoweka.

  Kwa kweli niliamua kwenda kujionea mwenyewe yanayojili katika hekalu la Cres wa 1 lililoko huko Mwenge karibu na kanisa la askofu Kakobe.

  Ilikuwa siku ya alhamisi alasiri, nilikuta ibada yao imeshaanza, walikuwa kwenye kutafakali moja ya vifungu katika kitabu chao cha Ramani. Dada mmoja mchangamfu sana alikuwa akiongoza kipindi hicho kwa kuuliza uliza maswali na kila mtu alichangia vile alivyoelewa ile aya. Kila mtu kabla ya kuchangia alisimama na kusema au kusalimia lile kusanyiko kwa kusema, “Salaam wateule” na kusanyiko zima lilijibu “Salaam”, ndipo akaendelea kuchangia na alipomaliza, alimalizia kwa maneno hayohayo, “Salaam wateule” na kujibiwa, “Salaam”.
  Tafakali iliendelea kwa takribani saa moja hivi na baadae Cres mwenyewe alisimama na kuhitimisha somo lile kuwa limeeleweka vizuri na kila mchangiaji, kisha Cres akaitisha wenye shida wapite mbele kwa ajili ya maombezi, walitoka watu kadhaa waliokuwa na shida mbalimbali.

  Alianza kuwaombea mmoja mmoja, wengine walikuwa wakianguka chini baada ya mapepo kulipuka ndani yao wengine hawakuanguka.

  Lakini cha kushangaza ni kwamba sikusikia hata mara moja likitajwa jina la Yesu kama nilvyozoea kusikia katika maombezi ya wagonjwa mahala pengine, maombezi yalikuwa ni kwa jina la Mungu. Alikuwa akirudiarudia, pepo toka kwa jina la Mungu. Yaani jina Yesu halitajwi kabisa katika hekalu hilo, maombi yao yote yanafanywa kwaa jina la Mungu.

  Kitu kingine kilichonishangaza ni vile mtu alivyokuwa akiombewa apate kujazwa roho mtakatifu, watu watano au saba waliitwa kuja kumjaza Roho Mtakatifu huyo jamaa kwa kumnyooshea mikono mithili ya mpanzi anayezitupa punje za mbegu mbele yake huku wakisema jaa, jaa, jaa, mara nyingi sana mpaka nabii Cres alipoona inatosha.

  Jambo lingine nililoliona ni vile ambavyo mtu alikuwa na swali au shauri lolote alitaka kupata jibu, alichotakiwa kufanya ni kunuizia, yaani kuweka hilo swali/ shauri kichwani mwako na kwenda kwenye ramani ambayo iko madhabahuni na kuishika na kuomba ikupatie jibu, huku umeiweka mikono na kisha kuifungua. Pale itakapofunguka na ukapasoma patakuwa na jibu la swali / shauri lako. Wenyewe wanaita kunuizia. Hili ni tendo ambalo wanacresia hulifanya mara nyingi kupata majibu ya maswali yoyote waliyonayo kila baada ya ibada zao.

  Kwa ufupi siku hiyo ilikuwa ni ya ajabu sana kwangu, kwasababu nilikuwa sijawahi kuhudhuria ibada yeyote ambayo jina la Yesu lilikuwa halitajwi kabisa na Biblia haipo kabisa miongoni mwao. Ibada yao ni wao (wanacresia), nabii Cres wa1 na Ramani Hai Takatifu tu.

  Kwa kweli niliogopa sana na sidhani kama ninatamani kurudi tena nadhani nikwenda kuiuza nafsi yangu kwenye ngome ya adui anaye mfanyia Mungu wangu Yesu Kristo dhihaka ya wazi wazi kabisa.

  Naamini adui shetani ameamua kuja waziwazi kuwafanya wanadamu wamkufuru Mungu Yesu Kristo ili wasisamehewe leo wala katika ulimwengu ujao.

  Biblia inasema wazi wazi, dhambi zote wanadamu wanaweza kusamehewa isipokuwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Naamini mtego huu ni mbaya kuliko mitego yote ambayo nimewahi kuwazia.

  Ole wetu wakazi wa dunia hii maana adui ameamua kutupa ndoano ya hatari zaidi.

 3. @MTEULE,

  NITAFURAHI KUPATA MAJIBU YA MASWALI YANGU HAYA MACHACHE, ILI NIELEWE:

  MUNGU WETU SISI TUNAOMWAMINI YESU,ANALO JINA, ANAITWA BWANA YESU KRISTO, NA NENO LAKE LOTE NA WALA SI NUSU AMELIWEKA KATIKA MIOYO YETU KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU NA LIMEHIFADHIKA VIZURI KATIKA BIBLIA, AMBAMO KUNAUTOSHELEVU WA AJABU, MUNGU WETU ANAONYA KUSIONGEZWA NENO WALA KUPUNGUZWA NENO HUMO! SASA,

  JE, HIYO “CRES” NI NGUVU YA MUNGU NANI?

  JINA LA MUNGU WA WANAFUNZI WA YESU NI KAMA NILIVYOKUTAJIA NA IKIWA WAISLAMU NAO WANA MUNGU WAO (HAWAMKUBARI YESU KUWA NI MUNGU) NAWE “CRES” WATAKA KUWAUNGANISHA WOTE (WAKRISTO NA WAISLAMU) JE, KWA PAMOJA WAKISHAUNGANA KWA IMANI HIYO WATAMWABUDU MUNGU WA JINA GANI?

  FREEMASON ANASEMA KATIKA KANUNI ZAKE KUWA MUNGU WAKE AITWAYE “SPRIM BIN” NAYE ANAUNGANISHA WAUMINI WA DINI ZOTE, TOFAUTI YAKO NA FREE MASON KIIMANI NI NINI?

  FREE MASON WANASEMA YESU SI MUNGU, ILA NI KAMA NABII AU MTUME AU MTU MASHUHURI ALIYEPATA KUWEKO DUNIANI, NAWE CRES UNASEMA YESU SI MUNGU ILA NI AU MTUME AU MJUMBE ALIYEPATA KUWEPO DUNIANI, JE, UTAWEZAJE KUKATAA KUWA WEWE SI WA IMANI MOJA NA FREE MASON?

  – ASANTE!

 4. Mteule Baika,
  Salaam!
  Huduma hii inawakusanya watu wote, ili kujitambua kwamba wote ni Wateule mbele za Mungu na pia kuwapa ufahamu kuwa wao ni watu na si wanyama hata wajifananishe na kondoo, “Agano hili limekuja ili utambue kwamba wewe ni mtu, na wewe si mnyama, Agano hili limekuja utambue ya kuwa wewe ni mwana wa Mungu”

  Huduma hii ina zaidi ya miaka miwili sasa na imeanzia hapa hapa.

  Kiongozi wake Mkuu ni Mungu kupitia kwa nabii Cres wa Kwanza.

  @ David Wambali
  “Cres” ni Nguvu ya Mungu iliyo katika Ramani Hai Takatifu ya Mungu. Ambalo ni Agano Kuu la Mungu kwa watu wote na dunia. Wateule wanakusanyika katika Hekalu lililopo Sinza karibu na roundabout ya Mlimani City, jirani na kanisa la Menonite hapa Dsm, pia Mbeya na Birmingham nchini Uingereza.

  Kwa leo nitaishia hapa,
  Amina!

 5. Ndg Mhina, asante kwa mafundisho mazuri yenye kutia moyo! 

  Ktk haya uliyotufundisha, nilipoyafuatilia kama ulivyotushauri, nikakutana na hitilafu zifuatazo:
  1: Heb 1:1-3 inasema ni mrithi wa vitu vyote na si mrithi wa manabii wote

  2: Luka 1:76 inamzungumzia Yohana Mbatizaji na si Kristo

  3: “…ndiyo maana yesu kristo anaitwa neno la mungu pia mwana wa mungu au mtumishi wa mungu…”
  Swali: Yesu kuwa “mtumishi wa mungu”; je, twaweza kupata andiko kuhusu jambo hili?

  4: “yesu siye mungu bali NI NABII KUTOKA MBINGUNI ALIYETUMWA NA MUNGU AKISHUKA DUNIANI KWA NJIA YA BIKIRA ILI KUUFUNUA UTUKUFU WA MUNGU KWA NJIA YA NENO AU HABARI NJEMA.”
  Je, maelezo haya ni katika mtiririko wa lile wazo ulilolijenga ktk ule msingi wa Luka 1:76, ambao ulimhusu Yohana kama tulivyoona, au ni jambo linalo jisimamia? Iwapo linajisimamia,  tukipata uthibitisho wa kiMaandiko, itatujenga zaidi.

  5: “Mungu aliumba ulimwengu kwa neno la kinywa chake kabla ya kulitia ndani ya mwili wa kristo, soma (yohana 1:1-5)…”
  Maelezo yako yanaonesha kuwa  ‘Mungu alilitia Neno lake ndani ya Kristo’ na Biblia ktk hivyo vifungu ulivyovitaja inatuambia kuwa “Neno ALIFANYIKA mwili”, sijui hapa ni fundisho lipi lililo sahihi, la kwako au la Biblia?

  Kwa leo niishie hapa nikiusubiri ufafanuzi zaidi kutoka kwako.

  Ubarikiwe!

 6. Hallo MR. RICHARD E. MHINA!
  Nimesoma machapisho yako yote yaliyo katika safu hii, ni mengi umesema, nimeshindwa kukuelewa, kunasehemu unakubali na kuna sehemu unakataa, sasa nisaidi nijue baadhi, hasa maana uliyokuwa nayo katika kusema hivi nanukuu ”…SWALI JINGINE NI MAHALI GANI KATIKA BIBLIA PANAPOSEMA WAZIWAZI KUWA YESU NI MUNGU MWENYEZI?…Acheni kufundishwa tuuu..mjisomee wenyewe kuthibitisha mnachofundishwa tena pia myachunguze kwa umakini maandiko na kuyatafakari vyema nae kristo atawafundisha ambaye kiroho ndiye mwalimu pekee wa kweli katika mambo haya mazito ya kiroho”

  Swali la kwanza:
  Je, zipi ni sifa za MUNGU ili awe na aitwe MUNGU?
  Swali la Pili:
  Biblia inasema mwenye kufumbua mafumbo ya Mungu ni Roho 1kor.2:10. Na inaendelea kusema kuwa,mwnadamu wa tabia ya asili hayapokei Mambo ya ROHO WA MUNGU; maana kwake ni upuuzi 1kor.2:14. Pia katika Yh.4:24, inasema Mungu ni Roho. Na katika Yh. 14:26 inasema Roho ni mwalimu! Sasa nawe unakataa YESU si Mungu mwenyezi, kisha unakubali kwamba “Kristo” ni mwalimu, unamaanisha nini, Yesu si kristo?

  Swali la Tatu:
  Biblia inasema Yesu ndiye Neno, Katika Yh.1:1-3, inasema hapo mwanzo kulikuwepo na Neno, naye Neno alikuwa Mungu na kila kitu kilifanyika kutokana naye…! Pia imesemwa katika Ebr. 5:10 na Ebr. 7:1-3 kuwa, Yesu hana baba, hana wazazi, hana mwanzo wala mwisho wa uhai wake, ila amefananishwa na mwana wa Mungu! Katika Isa.9:6, Yesu anasemwa ni MUNGU mwenye nguvu na ni Baba wa milele! (a) Je, Biblia yako haikuandikwa hayo? (B) Kama imeandikwa hivyo, wewe unapata wapi ujasiri wa kumpinga Bwana Yesu Kristo kuwa si mungu mwenyezi?
  Nitafurahi kupata majibu ya maulizo yangu hayo matatu, ili nipate kujifunza kitu kwako!

 7. Haleluya?msifungamanishwe nira pamoja na wasioamini,pana uhusiano gani kati ya haki na uasi? 2kor 6;14 -15.Au yeye anayaeamini ana sehemu gani na yeye asiyeamini?
  Neno linaendelea kusema tokeni kati yao mkatengwe nao,msiguse kitu kilichokichafu nami nitawakaribisha.
  Amiina mbarikiwe sana.

 8. HITIMISHO KWA LEO: sijaona hoja inayopinga labda mawazo yangu yamegusa wengi na kueleweka.Namalizia na hoja inayosema:JE,ALAMA YA MSALABA INAMAANISHAA NINI KATIKA BIBLIA?…NI MUNGU WATATU KAMA BAADHI YA WAKRISTO WANAVYOFIKIRI AU NI MUNGU ALIEGAWANYIKA KAMA SAMBUSA KAMA BAADHI YA WALIOPOTEA WANAVYOZIDI KUJIPOTEZA KWA UZEMBE WAO WA KUZIDI KUIPOTOSHA BIBLIA NENO PEKEE KABISA LA MWENYEZI MUNGU?….La hasha!!si kwa maana hizo hata kidogo…okoa nafsi yako kwa kujifunza vyema maana zake usije ukayumbishwa:KWA JINA LA BABA…ni kumkiri na kumkubali mwenyezi mungu kuwa ndiye muumba wa mbingu ardhi na vitu vyote mbinguni na duniani…yaani BABA YETU MKUU WA VYOTE KATIKA WOTE.Soma(zaburi 115:16)…KWA JINA LA MWANA:ni kumkiri yesu kristo kuwa ndiye njia pekee na dhabihu ya haki aliyotuandalia mungu kuwa fidia ya pekee ya kutufanya kuwa haki na kutupa njia mbele zake.(matendo 4:12)…KWA JINA LA ROHO MTAKATIFU:inaonyesha sisi tunaoamini tunaitambua roho takatifu ya mungu inayotutia nguvu ili tufanye mapenzi ya mungu.soma(zaburi 104:30)(yohana 14:26).Kumbuka kuwa mungu ni roho,soma(yohana 4:24) na alituumba kwa mfano wake katika hali na tabia za kiroho,soma(mwanzo 1:27)…hivyo basi,tukiishi kwa kufuata roho,uwezo wa mungu utatushukia na kutuwezesha kumtii mungu ipasavyo pia tutaishi tukiwa watoto halisi wa mungu lakini tukifuata mambo ya mwili na tamaazake tutakufa.soma(warumi 8:12-16).Haya ni mambo ya kiroho sana ni vigumu sana kueleweka kirahisi kwa kila mtu..lakini natumai tumejifunza vya kutosha.mwisho kabisa mbarikiwe.

 9. NB:sasa niingie katikati ya watoto wa mungu wasiojengeka vizuri na kuchangia mawazo kwa kuipotosha biblia kwa kutokujua kwao:HIVI NI WAPI MAANDIKO YA BIBLIA YANATUFUNDISHA KUWA MUNGU WAKO WATATU…ETI MUNGU BABA MUNGU MWANA ROHO MTKTF?…ETI WANATEGEMEANA TENA PASIPO YESU MUNGU HAWEZI NA PASIPO ROHO MUNGU HAWEZI NA PASIPO MUNGU YESU HAWEZI?…SWALI JINGINE NI MAHALI GANI KATIKA BIBLIA PANAPOSEMA WAZIWAZI KUWA YESU NI MUNGU MWENYEZI?…Acheni kufundishwa tuuu..mjisomee wenyewe kuthibitisha mnachofundishwa tena pia myachunguze kwa umakini maandiko na kuyatafakari vyema nae kristo atawafundisha ambaye kiroho ndiye mwalimu pekee wa kweli katika mambo haya mazito ya kiroho.soma(mathayo23:10-12)(mathayo 11:27).Mungu wetu mwenyezi hawako watatu wala hawagawanyiki…MUNGU NI MMOJA TU…NARUDIA TENA IWE KUMBUKUMBU NA USHAHIDI MAHALI HAPA:MUNGU NI MMOJA TU…NA MPATANISHI AU NJIA KATI YA MUNGU NA WANADAMU NI MMOJA TU NAYE NI YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU KATIKA IMANI MOJA.soma(efeso 4:5-7)…yesu siye mungu bali NI NABII KUTOKA MBINGUNI ALIYETUMWA NA MUNGU AKISHUKA DUNIANI KWA NJIA YA BIKIRA ILI KUUFUNUA UTUKUFU WA MUNGU KWA NJIA YA NENO AU HABARI NJEMA.kwa hiyo maneno ya yesu ni YA MUNGU MWENYEWE YENYE UTUKUFU WA MUNGU MWENYEWE,ndiyo maana yesu kristo anaitwa neno la mungu pia mwana wa mungu au mtumishi wa mungu…katika kazi zote hizi yani AOKOAE akiwa mrithi wa manabii wote aliyeletwa na mungu.soma(waebrania1:1-3)..ndiyo maana malaika alituletea ujumbe uliosema hivi:NAWE MTOTO UTAITWA NABII WA ALIE JUU…yaani nabii kutoka kwa mungu.soma(luka 1:76).Sasa iweje wakristo wa leo waseme YESU NI MUNGU NA MUNGU WAKO WATATU WAKISAIDIANA?…siyo sahihi kabisa ijapokua mmeipokea imani na kuikubali!…Mungu aliumba ulimwengu kwa neno la kinywa chake kabla ya kulitia ndani ya mwili wa kristo,soma(yohana 1:1-5)…umeona neno alikuwa kwa mungu yaani neno la mungu mwenyewe lenye pumzi ya mungu mwenyewe..anasema NENO ALIKUWA MUNGU MWENYEWE.Kwa hiyo ndugu wakristo,yale ni maneno ya mungu alipokuwa akiuumba ulimwengu na wala siye yesu kristo yule!!.thibitisha zaidi kwa kusoma(mwanzo 1:1-6) linganisha na(waebrania 11:3).kwa hiyo,mungu alipomtuma yesu kristo alitia maneno yake ndani ya NABII WAKE YESU KRISTO ILI ATUFUNDISHE,ATUONGOZE NA KUTUAMURU YALE YOTE ALIYOAMRISHWA NA MUNGU….NENO LIKAFANYIKA MWILI .Soma(yohana 1:14)…ndipo alipoufunua utukufu wa mungu akiongozwa na roho mtakatifu wa mungu.soma(isaya 42:1).Tufahamu kwamba nabii anapoongozwa na roho wa mungu anaongea maneno ya mungu mwenyewe na kuwa na hali za kiungu,soma(kutoka 7:1)..ndipo hali hiyo ya kiroho ilipompata yesu kristo na kuitwa mungu…siyo mbaya sana kiroho lakini lazima tufahamu vyema kuwa ni UWEZA WA MUNGU UTENDAO KAZI NDANI YAKE NA WALA SIYE MUNGU MWENYEZI…Kwa kuwa biblia inatufundisha kuwa: HATA MWANA MWENYEWE ATAJITIISHA MBELE ZA MUNGU ILI MUNGU AWE YOTE KATIKA WOTE.soma(1wakorintho 15:28).mbarikiwe

 10. Acheni utoto ninyi..mnakua kama hamjaokoka bwana!!.Maada hii inatakiwa ijadiliwe na watu wasiojua neno la Mungu..tena inafaa iandikwe kwenye magazeti ya udaku sio mbele za watoto wa Mungu kwa kuwa shetani anatumia hila za ujanja sana ili atumeze kwa kuanza kuchafua akili za watu taratibu taratibu kulingana na elimu za ufahamu wa watu,ndiyomaana biblia ilisisitiza hivi:UMKAMATE SANA ELIMU,USIMUACHE AENDEZAKE MSHIKE MAANA YEYE NI UZIMA WAKO.Soma(mithali 4:13).Je,mkristo ulieokoka unafahamu kuwa yule elimu ni Yesu Kristo na injili yake ambaye kwa jina la kiroho anaitwa NENO LA MUNGU?..Soma(ufunuo 19:13)(yohana 1:14).Hivyo basi silaha ya mwisho ni injili na wala sio elimu nyingine yoyote.,hata kama elimu nyingine haitengui biblia itakua imeongeza maneno ya unabii ule ambapo kibiblia tayari ni kosa!!..soma(ufunuo 22:18-19).Neno la Mungu limejitosheleza katika biblia,la msingi hapo sio kubadilisha maandiko bali ni kuyafuata maandiko usiku na mchana ili tujengeke vizuri.Hakuna maandiko mengine wala suluhu nyingine zaidi ya biblia,wanadamu ndiyo wanapaswa kunyenyekea maandikokupata suluhu sio maandiko yanyenyekee watu!!.Hivyo basi Yesu Kristo ndiye njia pekee leo jana na hata milele.Tena biblia inatukumbusha hivi:MSICHUKULIWE NA MAFUNDISHO YA NAMNA NYINGINE NYINGINE.Soma(waebrania 13:8-9).SASA TUJE KWENYE MAADA YA DHAMBI YA ASILI,JE WANADAMU WOTE TUMERITHI DHAMBI YA ASILI ? JIBU NI NDIYO TENA BILA SHAKA…KAMA HUJAPATAELIMU HII FUATILIA HAPA KWA UMAKINI SANA UKIWA NA BIBLIA YAKO ILI IKUTHIBITISHIE:Hebu tuanze na amri ya tisa katika amri kumi za Mungu,Mungu alisema hivi:NAWAPITILIZA WANA UOVU WA BABA ZAO HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIZAO.Soma(kumbukumbu 5:9-10).

  Hivyo basi Baba yetu adamu alipomuasi Mungu baada ya kumsikiliza na kumtumikia ibilisi alipoteza uwezo wa kutii viwango vya haki vya sheria ya mungu na kuleta hasara kwa uzao wake wote ambao ni sisi ndipo tukakosa rehema za mungu na kutokuwa wakamilifu.soma(kumbuk 5:10).Hili sio fundisho la mtume paulo kama waisilamu wanavyodai..bali ni fundisho na maneno ya kweli ya mungu katika biblia yetu kutokana na UTAKATIFU WA MANENO YA MUNGU MWENYEWE KWA KUWA MUNGU WETU SIO MTU HATA ADANGANYE.Hata manabii wa zamani walilijua hilo,hebu msikilize mfalme daudi na fahari yake yote alivyokiri hivi:MIMI NALIUMBWA KATIKA HALI YA UOVU,MAMA YANGU ALINICHUKUA MIMBA HATIANI.soma(zaburi 51:5)…Naye Ayubu katika mafundisho yake anasisitiza hivi:MTU AWEZAJE KUWA HAKI MBELE ZA MUNGU? AU AWEZAJE KUWA SAFI ALIYEZALIWA NA MWANAMKE?..soma(ayubu 25:4-6)…istoshe bado ayubu aliendelea kutufunulia waziwazi pale aliposema:NI NANI AWEZAYE KUTOA KITU KILICHO SAFI KITOKE KATIKA KITU KICHAFU? Soma(ayubu 14:1-5)..Hivyo basi katika hali hiyo,mungu alimpa musa torati iliyokuwa na kanuni ya kafara ya damu za wanyama ilikuwaongoza israel katika njia ya kutubu thambi zao na pasipo njia ile hapakuwa na kusamehewa dhambi mbele za mungu.soma(waebrania 9:20-23)…pia mungu aliwakataza israel kwamba wakitumia njia ile ya damu na wanyama na kuzishika amri zake kwa ufasaha…wasiseme tena wamerithi thambi ya asili kwa kuwa watasamehewa dhambi zao zote na kuwa watoto wa mungu.soma(kumbuk 7:9-13).Mungu aliwajenga israel zaidi kwa kuwaambia:MSISINGIZIE WAZAZI WENU TENA KWA KUWA ROHO YA MTU ITENDAYO THAMBI NDIYO ITAKAYO KUFA.

  Kwa hiyo hata sisi wakristo tukitubu kwa njia ya damu ya Yesu Kristo hatuwi chini ya laana ile ya adamu aliyopewa na mungu.Kwa fundisho hili tunaona hata watoto wadogo hawazaliwi kamilifu lakini hawahukumiwi kwa kuwa bado wadogo hawana maarifa ya kujifunza sheria ya mungu…na biblia inatufundisha kuwa pasipo sheria dhambi haihesabiwi kwa kuwa sheria ndiyo inayofunua dhambi na kumuadabisha mtu kufuata njia ya mungu.Yesu alisema:WAACHENI WATOTO WADOGO WALA MSIWAZUIE KWA MAANA UFALME WA MUNGU NI WAO.kwa hiyo wanadamu wote tumerithi laana ya kifo na kuwa watenda dhambi ndiyo maana tunahitaji utakaso ili tumrudie mungu kwa kuwa dhambi ile ilienea kizazi kwa kizazi kama mungu alivyosema kwenye mri zake.Pia mtume paulo alitukumbusha kuwa dhambi ya adamu ilienea kwa watu wote,soma(rumi 5:12)…hivyo hakuna mkamilifu hata mmoja kwa kuwa tunafanya dhambi kwa njia tofauti tofauti,soma(mhubiri 7:20)…Yesu Kristo amekuja kutukomboa kutoka katika mtego ule wa ibilisi kwa kutuunganisha na mungu akiwa NJIA NA NENO WA MUNGU.kivipi?…NJIA: Kwa sababu amekaa juu ya sheria na kutufanya sisi kuwa haki mbele za mungu pale tunapomuamini yeye na kushika mafundisho yake ya injili ambayo ni maneno ya uzima ya mungu mwenyewe,kwa hali hiyo ameitimiza sheria ile ya mungu kuwa njia ya wokovu.soma(zaburi 85:13).NENO WA MUNGU,kivipi?…sheria ya mungu inasema hivi:PANA MADHARA MTATOZA UHAI KWA UHAI.soma(kutoka 21:23)…

  Baba yetu adamu alitugharimu uhai wetu mkamilifu kwa kuupoteza kwa hiyo mungu kwa kutupenda alimleta kristo kwa njia ya bikira ili awe mtu mkamilifu wa kutukomboa kwa haki mbele za mungu kwa kuwa mungu wetu ni mwenye HAKI KAMILIFU KATIKA MANENO YAKE. Soma(mwanzo 2:17). Hivyo basi,katika adamu TUNAKUFA HAKIKA LAKINI KWA NEEMA YA MUNGU KATIKA KRISTO TUNAISHI HAKIKA!!…Ndiyo maana biblia yetu inatufundisha hivi:kasome(warumi 5:19) na (1wakorintho15:22).Hitimisho:USIDANGANYWE HATAKIDOGO ,YESU KRISTO PEKEE NDIYE MWAMBA NA NJIA YA WANAADAMU WOTE KUMFIKIA MUNGU..HAKUNA CHA CRS WALA CS..NIMATAPELI WA NENO LA MUNGU HAO WANAOTAKA KUPOTEZA WATU WASIO NA MISINGI DHABITI.mbarikiwe.

 11. Bw. David Wambuli, kwa imani tunayoiamini, MUNGU ana nafsi tatu…ambazo zinaukamilisha Uungu wake…yaani Mungu Baba, Mungu Mwana (ambae ndio Yesu) na Mungu Roho Mtakatifu. kwa maana hiyo basi kuna kosa gani mimi kusema Yesu ndiye Mungu? hawa wote watatu ni wamoja. na kumfikia Mungu kamwe hakuwezekani bila ya kupitia Yesu kama maandiko yanavyosema.
  Hawa cress hawawezi kupinga lolote, wala kutudanganya kwa lolote…wao ni wapinga Kristo..wanajidai kuja kwa njia ya kujificha kujidai wanaunganisha dini za watu…lakini kwa uhakika tumeshawashtukia ni waabuduo mashetani..tena wakuu. na Moto wa Damu ya Yesu uwaunguze na kuwaangamiza. hata siwajui wako wapi, wanakutanika wapi, mie nachojua ni kwamba natuma Damu ya Yesu ikawaangamize na kuwateketeza mojakwamoja.
  Wakome kupotosha kanisa/watu wa Mungu.

 12. MUNGU WETU MKUU ANAENDELEE KUTULINDA SAWASAWA NA NENO LAKE, MIMI BINAFSI SINA HOFU HATA KIDOGO NA NINAFURAHI KUSIKIA NA KUONA HAYA YAKITOKEA! NASEMA SINA HOFU KWA SABABU IMEANDIKWA HAYO HAYANABUDI KUTOKEA – KWAKWELI NENO LA (MUNGU BIBLIA) LIMEHAKIKISHWA, MAANA KILA KITU KINATOKEA VILEVILE! LA MSINGI JE, KATIKA MADHEHEBU YETU HAKUNA MAHUBIRI KAMA HAYO YA CRESS? KAMA HAYAPO KWANINI “RAMANI” HIYO YA CRESS ISHUGHURIKE NA UISLAM NA UKRISTO? (HASA “Ukristo wa sasa”) AMBAPO WATU WANATAKA UPAKO, UTAJIRISHO NA UPONYAJI WA MWILI KWA SANA. YESU ALISEMA “…..KIZAZI HIKI KINATAKA MIUJIZA….” (SIPINGI MIUJIZA)

  WAPENDWA CHUNGUZENI KWA MAKINI, LAWAMA, TUHUMA NA UDINI HAVITASAIDIA KATIKA VITA HII! RAMANI HIYO INASEMA HAIPO “KUTENGUA” AGANO LOLOTE KATIKA YALE YALIYOTANGULIA, INASEMA IPO KUONGEZEA KILE “KILICHOSAHAULIKA!” LAKINI KUMBUKENI PALE BWANA YESU ALIPOKUWA NA SHETANI KULE JANGWANI WAKATI WA ULE “MFUNGO WAKE MTAKATIFU”….SHETANI AKASEMA IMEANDIKWA…” – MAANDIKO ALIYOYASEMA SHETANI, YAKO VILEVILE NA YAMEANDIKWA VILEVILE KAMA ALIVYOYASEMA, LAKINI CHA MSINGI PALE NI KILE SHETANI ALICHOTAKA YESU AKIFANYE KUPITIA TAFSILI YA MAANDIKO HAYO! JE, KINACHOTAJWA NA KUTUMIKA KATIKA UNABII, MAOMBEZI NA MAHUBIRI YA VIONGOZI WETU HAYANA “TONE” LA CRESS HATA KIDOGO? KUJUA NA KUELEWA NINACHOKISEMA ICHUNGUZENI KWA MAKINI CRESS! “NAOGOPA” ISIJE KUWA INARUSHIWA MAWE “RAMANI” NA WANA RAMANI WENYEWE!

  WATOTO WA KWELI WA MUNGU, YESU ALIWAOMBEA ULINZI. VILEVILE ALITUTAKA TUWE WELEVU, LAKINI KIZURI KULIKO VYOTE NI KWAMBA ALIAGIZA KWA KILA JAMBO TUMTUMAINI YEYE! ALISEMA “…….BILA MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE” (Yhn. 15;5)

  BWANA YESU KRISTO, ALIWACHIA MITUME WATUFUNDISHE, NA TUKAE NA KUFUATA MAAGIZO NA MAFUNDISHO HAYO YA MITUME. NENO LINASEMA “IWAPO ATATOKEA, IWE MALAIKA, AU MTU YEYOTE ATAHUBIRI AU KUFUNDISHA SI MAFUNDISHO YA MITUME NA ALAANIWE!” NENO LINAENDELEA KUSEMA, OMBENI NENO LOLOTE KWA JINA LANGU, NAMI NITAWAKILIMIA. TENA, JINA LITUPASALO KWALO TUONDOLEWE DHAMBI NI JINA LA YESU, HIVYO KAMA MTU ASIPO LIKUBALI NA KUTENDA KATIKA JINA LA YESU, ANAWEZAJE KUSEMA YEYE HAYUMO KATIKA “IMANI” YA CRESS? Mdo 2:38, inasema, NI YULE TU ALIYEBATIZWA KWA JINA LA YESU NDIYE ANAPATA ONDOLEO LA DHAMBI, NI WANGAPI WAMETEKELEZA HILO KATIKA WALE TUNAOJIITA TUMEOKOKA (Sawa sawa kabisa bila kupiinda ile Mdo 2:38)? LAKINI NENO LA MUNGU LIMESEMA “KAMA MTU hATAFUATA MAELEKEZO NA MAFUNDISHO YA MITUME AMELANIWA”!

  VIONGOZI WETU WA DINI WANASEMA HATUNA DHAMBI NA TUNA KWENDA MBINGUNI LAKINI HATUJAITEKELEZA NA KUBATIZWA KAMA ILIVYOAGIZWA NA NENO KATKA ILA Mdo 2:38, JE, TWAWEZAJE KUIRUSHIA MAWE CRESS AMBAYO NAYO KATIKA KITABU CHAKE “RAMANI” INASEMA WATU HAWANADHAMBI ISIPOKUWA MTU ANAKUWA NA DHAMBI KWA MATENDO? (KWA MAANA HIYO NI KAMA KUSEMA KUWA, UKIISHI BILA UZINZI, WIZI, URAFI, UONGO, USIWATENDEE WENGINE MABAYA, YAANI KWA KIFUPI UKIWEZA KUISHI KWA MATENDO MAZURI YA KIMWILI, BILA YA KUMKIRI YESU, WEWE NI MTU WA “MBINGUNI”!) KAMA KUMAANISHA KUWA, MATENDO YAKO NDIYO YATAKAYO KUOKA! KUMBUKA Yhn. 15:5 INAEMA, BILA MIMI NINYI HAMWEZI NENO LO LOTE! SASA JIULIZE JE, HATUJASIKIA WATU WAKIULIZANA, WEWE HUNYWI POMBE, HUVUTI SIGARA AU UNA MKE MMOJA, UMEOKOKA MWENZETU?

  LAKINI LINGINE CRESS WANASEMA, NANUKUU “536. Naye Orlgurt alipopatwa na malaika Izolba na malaika Herite hakukaa tena kuishi mwanadamu wa kawaida bali alikuwa mara duniani mara mbinguni, na ndani yake ziliishi nafsi tatu katika kiti nafasi moja, aliishi yeye Orlgurt, aliishi Herite na Izolba aliishi, nao walitawala na kumiliki kwa zamu.” MWISHO WA KUNUKUU, JE, NANI ANAWEZA KUBISHA KUWA CRESS HAWAMO KATIKA IMANI YA “MUNGU UTATU MTAKATIFU” ?(BILA KUZINGATIA WANAVYO MTAJA) JE, KAMA MADHEHEBU YETU YANATUELEZA NA KUTUFUNDISHA MAFUNDISHO YAYOHAYO, IPO TOFAUTI GANI NA CRESS? NDIYO MAANA NASEMA ISJEKUWA RAMANI YA CRESS NITUPIWA MAWE NA WANARAMANI WENZAKE!

  MAANA, YEYE ASIYE NA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KURUSHA JIWE – AMINA!

 13. Peace of God be with you

  This is very interesting, you mean their is Third testament. I ll expect it to clear many contradictions on the current, old and new testaments. I know some you might not like this but its obvious eg my sister Beatrice L.Mtui on her comment she is says “Yesu ni Mungu ” I personally find it confusing and misleading

  I would like to know more about cress message

 14. Hii Kali..! Lakini..

  Maubili yametulia, kama anavyoseme ” Agano hili halikuja kutengua maagano yaliyokwisha kuwa wala halikuja kutengua neno lolote, bali limekuja kuinua sauti ndani ya maagano hayo na kuinua unyayo mpya uliokuwa umesahaulika”.

  Kitu ambacho sijaelewa anpozungumzia cr ya cress na cr ya christ. Je, nikweli kweli christ ilikuwepo kabla ya Yesu? na nini maana ya CHRIST??..

  Jamani.. hii dhambi ya asili hata mimi inanichanganya.! kwanini Mungu atuumbe tukiwa na dhambi???

 15. Biblia yetu imeandikwa chini ya uongozi wa ROHO MTAKATIFU hivyo ROHO MTAKATIFU HAKOSEI.samahani jaribuni tena baadaye

 16. Yababababa!!!!!!!!
  Wapendwa; Yesu ndiye Alfa na Omega; na huyo cres anaenda wapi jamani??!!!!!!

 17. Hii ni mpya!
  Imeanza lini? Kiongozi wake Mkuu ni nani? Na kwa hapa Tanzaniia imeingizwa kama kitu gani?

 18. Kila kinachotokea hakipaswi kutushangaza, maana yalinenwa kuwa yatatokea. Ebu niwasaidie Cres hivi. BIBLIA HAINA MAKOSA YOYOTE AMBAYO MWANADAMU AWAYE YOTE ATASAHIHISHA. Na Mungu aliweka ulinzi ndani yake, Kumb 4.2 MSILIONGEZE NENO NIWAAMURULO WALA MSILIPUNGUZE, MPATE KUZISHIKA AMRI ZA BWANA, MUNGU WENU, NIWAAMURUZO. Mith 30.5..6 KILA NENO LA MUNGU LIMEHAKIKISHWA YEYE NI NGAO YAO WAMWAMINIO, USIONGEZE NENO KTK MANENO YAKE, ASIJE AKAKULAUMU, UKAONEKANA U MWONGO. UF 22.18…19 NAMSHUHUDIA KILA MTU AYASIKIAYE MANENO YA UNABII WA KITABU HIKI,MTU YEYOTE AKIYAONGEZA, MUNGU ATAMWONGEZEA HAYO MAPIGO YALIYOANDIKWA KTK KITABU HIKI, NA MTU YEYOTE AKIONDOA LOLOTE KTK MANENO YA UNABII WA KITABU HIKI, MUNGU ATAMWONDOLEA SEHEMU YAKE KTK ULE MTI WA UZIMA, NA KTK ULE MJI MTAKATIFU, AMBAO HABARI ZAKE ZIMEANDIKWA KTK KITABU HIKI. Huo ni ulinzi, Cres waendelee, lakini ni vizuri wakiyajua hayo, Yesu ndiye NJIA PEKEE. Yoh 14.6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, KWELI na UZIMA, Mtu haji kwa Baba, ila kwa NJIA YA MIMI. Acheni njia hizo zingine zitawafikisha kubaya.

 19. Tuzidi kuombeana wapendwa, kwa namna hii, hali si shwari kama inavyodhaniwa, Yesu amekaribia kurudi tuwe tayari, muda na saa yoyote.

 20. Bwana asifiwe….Dunia imeisha jamani YESU ndie njia sasa hii cres ni ya nini inamana mitume na manabii wa kwenye biblia nao walikuwa na cres jibu ni hapana hao ndio wapinga kristo asante YESU nimeijua njia yako tumshike YESU wapendwa.

 21. asomaye haya na afahamu kuwa yale yaliyonenwa na Yesu kristo yanatimia!!!!!! hivi ni vichekesho vitupu; ndugu zangu tuliookoka na tuendelee kushika sana tulicho nacho sana.

 22. mh! kazi ipo mpaka Yesu aje…madudu kibao yanaibuka!heri tuliyoidaka kweli mapema, hakuna wakutung’oa badala yake kila pando lisilopandwa na Baba sharti litangolewa.

 23. Mimi nadhani na sio kudhani tuu ila naamini hizi ndizo siku za mwisho na haya yote ni udhihirisho tu. Manabii wa uongo ndo hawa na hakuna pingamizi. Yesu Kristo alisema yeye ndio njia pekee ya uzima na mtu hawezi kumfikia Mungu bila kupitia kwa yeye Yesu. sasa hii cres ya kumuunganisha Yesu na vingine imetoka wapi? Biblia haina upungufu wowote kama hawa Cres wanavyosema. wao ndo wanaupungufu kwa kutotambua mamlaka na Nguvu alizopewa Yesu na Mungu. sasa mimi nalaani hii huduma tena ishindwe na isiweze kuwapoteza watu wa Mungu. nyie ndo wapinga Kristo ambao tumeambiwa katika maandiko matakatifu ya Biblia kuwa mtatokea. Sisi hamtubadilishi imani yetu, Yesu ni Mungu na ndiyo tunamngojea aje kutuchukua. Nyie na cres yenu pamoja na mtawala wenu shetani/ ibilisi moto wa milele unawangojea. mahubiri gani hayo yasiyolitaja jana Yesu? njia ya kumfikia Mungu ni moja tuu..na hakuna kupinda wala kupindisha…ni kupitia YESU KRISTO basi.
  Wana wa Mungu msitetereshwe na haya ya dunia…shika sana ulichonacho na asije mtu akakunyang’anya.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s