Hatari kuoana na mtu asiye na imani moja na wewe!

Kuna hatari gani kuoana na mtu asiye mcha Mungu?

Alex Kapinga

Advertisements

9 thoughts on “Hatari kuoana na mtu asiye na imani moja na wewe!

 1. BWANA YESU ASIFIWE!!!!!
  zipo hatari ya kuoana na mtu asiye mcha Mungu zipo hatari nyingi kusema kweli

  1.kwanza kabisa si watu wa kusudi moja/wa kunia mamoja kwa sababu mmoja anataka kuishi maisha ya kumpendeza mungu naye anamatakwa yake aliyojiwekea tena mabayo hayampi Mungu utukufu kama vile mwenzio Mungu wake ni Mungu Bahari ndiye anayemtegema kwa yote ndiyo anaona ndiyo maisha na atataka siku moja muuambatane kwenda kwa waganga wa wakienyeji, pombe n.k ambayo hayafanani na mtu aliyeokoka . Hasa mwanandoa mwanadada haya huyu ndiye anahatari kuwa kwa sababu atabanwa kuabudu kwenye ibada za katikati, Jumapili hata katika semina mbali mbali anaweze asihudhurie na kusababisha mtu huyu kurudi nyuma kwa sababu hapati vizuri chakula cha kiroho. Chakula anachopata ni maudhi, matukano magovi na hata kupigwa pia kwa sababu ya kutokutii matakwa ya mmewe. Kuhusu kupokea wokovu kwa watu kama hawa huwa ni neema ya Mungu na Huyu Mtu anayekaanaye inabidi aingie gharama kweli ya kumwombea ikibidi afungu na kuomba na ikimpasa na uvumilivu pia. Pia kitabu cha mithali kinatuonya; Mithali17 inasema 1 Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.

  2 Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.

 2. Dada Elfina,

  Kama ndo umeokoka na umeamua kuokoka baada ya kuwa ulishafunga ndoa, tumaini la kumvuta kwa Yesu lipo.

  Hata hivyo unapaswa kufanya yafuatayo:

  1. Hakikisha kuwa unamwonesha mwenzio kwamba umebadilika kiroho, kiufahamu, kimaandiko, kimtazamo, kimatendo, kiusafi, uaminifu kwenye kila jambo hasa kwenye maswala ya fedha na ndoa, mwoneshe kuwa umekuwa kiumbe kipya kwa vitendo na si kwa maneno.

  2. Hakikisha kuwa unakuwa mpole na siyo mkali wala mwenye kiburi mbele zake. Nyenyekea kila inapowezekana. Biblia inasema, Jibu la upole hutuliza ghadhabu. Mwenzio akiwa amekasirika wewe tulia. Jibu kwa upendo na upole.

  3. Onesha kwamba wewe siyo mtu wa zamani na kwamba maisha yako ya kale yamepita na sasa wewe ni kiumbe kipya.

  4. Uwe tayari kukubali kupoteza ili yeye apate. Yaani kama yeye anajiona yuko sawa hata kama amekosea kwa wazi wewe kubali na ukiri kuwa umekosea hata kama yeye ndiye kakosea. Huku ndiko kukubali kupoteza ili yeye apate.

  5. Jitahidi kuvaa mavazi yaliyo na staha. Epuka kuvaa nguo zisizo na heshima mbele za jamii na kanisa.

  6. Anza kumshudia kuhusu habari njema za Yesu. Fanya hivyo kwa upendo wala siyo kwa hasira. Ukipingwa wala usikate tamaa wala kudhania kwamba Mungu hataweza kumwokoa kwa sabau tu anakupinga.

  7. Usimunyime mapenzi yaani tendo la ndoa bila sababu ambayo hata yeye ataielewa. Acha uchoyo kabisa linapokuja swala la kufanya tendo hilo. Jitume kabisa kwa moyo wako wote. Mpatie mahaba ambayo mwanzoni ulikuwa humpatii. Hii iwe sehemu ya mabadiliko ya moyoni. Fanya hilo kwa moyo wote wa mahaba na upendo wa dhati.

  Biblia inasema kwamba kwa kufanya matendo kama hayo atavutwa kwa Yesu hata bila wewe kumuhubiria kwa maneno. Yaani utakuwa umemuhubiria kwa vitendo. Hubiri kwa vitendo zaidi kuliko maneno. Vitendo vina nguvu zaidi ya maneno.

 3. Samahanini wapendwa! mimi naomba kuuliza nilikuwa sijaokoka. sasa hivi nimeokoka. je kuna tumaini la kumvuta kwa Yesu?

 4. Unakabiliwa na hatari saba kama ifuatavyo:

  1. Utakuwa mpweke kiimani kwani hutaweza kumshirikisha mwenzio maswala ya imani yako.

  2. Utakosa wa kuambatana naye kila siku ya kwenda Ibadani. Badala ya kuongozana na mwenzio kwenda Ibadani, labda ndani ya gari, kwa mguu, daladala, nk, utakuwa unaenda kanisani ukiwa huna kampani, yaani mwenza wako.

  3. Utakosa msaidizi wa kweli katika maswala ya ndoa hasa yanayohitaji uelewa wa maandiko na msimamo wa Imani. Imani zikiwa tofauti, na misimamo yenu katika ndoa itakuwa tofauti.

  4. Endapo mtafanikiwa kupata uzao wa watoto, mtashindwa kuwalea kwa kufuata Imani moja. Watoto watagawanyika au watajikuta hawana pa kwenda au hawajui wafuate Imani ya nani kati ya baba na mama. Kama wewe ni Mkatholiki na mwenzio ni mlokole wa pale EAGT au PAG, au TAG, nk, watoto watashindwa kuelewa ni Imani ipi wafuate. Watachanganyikiwa.

  5. Ikifika swala la kuzaa kwa kufuata mpangilio wa kisasa huenda mkashindwa kuelewana ama kwa sababu za kiimani.

  6. Kama mwenzio anaamini kuwa kwenda kupata tiba kwa waganga wa jadi wanaotumia albadiri, mizimu, majini, uaguzi, nyota, makaburi, nk kwamba siyo dhambi huku wewe ukiamini kuwa ni dhambi, hapo ndipo mtaanza kuwa na ugomvi usiokwisha nyumbani kwenu.

  7. Ukioana na mtu asiyekuwa wa imani moja na wewe mtu huyo akawa anaamini kwamba kunywa pombe, kuvuta sigara, kuiba, kuvuta bangi, kunywa gongo siyo tatizo wewe utajikuta unaishi maisha ya taabu sana. Maisha yako ya ndoa hayatapata amani kamwe. Kumbuka unapaswa kuingia kwenye ndoa ili kupata raha na kujenga familia yenye amani na utulivu. Kama utaingia bila uangalifu, hutapata amani kamwe.

  NDOA YAPASWA KUWA YA AMANI NA WALA SIYO MAHALI PA FUJO NA GHASIA. CHUNGA SANA USIJE UKAINGIA KATIKA MZOZO WA NDOA.

 5. Shalom wana SG na wote popote mlipo.

  Nionavyo mimi, hatari ni kama hizi kwa uchache,

  1. Kukosana na Mungu wako maana ameagiza ktk 2Kor.6:14- kuwa usifungiwe nira na wasioamini (wasiookoka)
  2. Ni njia nyepesi sana ya kukutoa ktk wokovu.

  Huu ni ushuhuda wa mpendwa mwenzetu(wa kike) hapa KGM, ukiusoma mpk mwisho utajemgwa. Ilikuwa hivi kwa ufupi;

  Mumewe ambaye hajaokoka alimkimbia kwa sababu ya wokovu wake na maisha ya maombi aliyokuwa nayo ambayo yalivuruga mambo mengi ya yule bwana.(Fahamu nisemalo)Maisha ya yule mama yakawa magumu sana(si kwa sababu Yesu naye alimkimbia la hasha, ila ni kwa sbb alimtegemea mwanadamu) So baada ya kupita miaka kati ya 3-5 yule mume akamwambia mkewe kuwa angerudi kama mkewe atakubali masharti yake(ambayo hakuyataja) jambo ambalo mke aliafiki pasipo kujua kinachojiri.

  Yule mume alipofika tu, jambo la kwanza ilikuwa kumwambia mkewe ‘watoke, ‘out’ ambalo pia mke alikubali(bila kujua mtego uliomo)

  Kilichomshangaza ni kuona mumewe anamwigiza bar, alipotaka kukataa mumewe akamwambia kumbuka masharti tuliyopatana ili nirudi. Mke akawa hana jinsi coz alishamkubalia. walipoingia bar mume akaagiza bia 2, mke alipoagiza soda akaulizwa “una pesa ya kulipia hiyo soda?” jibu likawa “sina” mume akasema utakunywa nikupacho maana Biblia yako imekuagiza kumtii mumeo ktk mambo yote, na mimi ndiyo mumeo. Mwanamke akawa hana la kufanya. Akajifariji kwa neno hilo (pasipo kutambua shetani amemuweza na amemshinda pia) Akanywa zile bia mbili akaanza kulewa. Mume akamuongeza ya tatu mke akawa hoi. Baba akakodi gari akampeleka mkewe home. Kesho yake alipoamka akaanza ku-recall kilichotokea, akahangaika sana, Roho Mtakatifu alivyo mwaminifu akamwongoza kwenda kwa waombaji wenzake ili atubu. Walimsaidia na kumwonya asirudue kitendo hicho maana imetupasa kumtii Mungu na sio wanadamu (Mdo.5:29)

  Zikapita siku kadhaa mumewe akamwambia tena watoke, mke akashangaa maana haikuwa mazoea ya mumewe huko nyuma, akakataa, lakini kwa hofu ya kuachwa na mumewe huyo ikamlazimu akubali. Hali ikawa ileile. Alipowaendea waombaji wakamkatalia kumwombea(kibinadamu waliona anawakejeli). Alirudi nyumbani kwake, kukaa kidogo tu akapitiwa usingizi, akaona kamba ndefu sana kutoka juu ikimwelekea na kisha sauti ikamwambia, shika kamba hiyo panda uje huku. Alishika kamba ile na alipofika katikati alijiona kuserereka hadi chini alikoanzia, akatupiwa tena mara ya pili ikawa hivyohivyo, ikaja sauti kusema ‘MARA MBILI HIZI NIMEKUSAIDIA(NIMEKUSAMEHE), UKIRUDIA LAZIMA UFE’ kwa mshtuko alioupata alipotoka usingizini alikimbia tena kwa waombaji kuwaeleza aloyoyaona, wakamwombea rehema na kumshauri kumtii Mungu pekee.

  Kwa neema ya Mungu tu yule mama hakurudia kutii lolote aliloamriwa na mumewe kinyume na mapenzi ya Mungu.

  Swali langu ni hili, wajuaje kama nawe ukijaribu kufanya hivyo utarehemiwa?
  Kolosai 2:21 tumeagizwa; MSISHIKE, MSIONJE, MSIGUSE.

  Mwenye masikio na asikie.
  Mngojee BWANA kama nimngojavyo, kwa UAMINIFU alionao hawezi kukuaibisha, unachotaka kuwahi ni nini, ni nani aliyekwambia umechelewa? na umechelewa wapi?
  Kanuni ya Mungu wetu ni hii, miaka 1000 kwake ni sawa na siku 1.
  Siku 1 ni saa 24, robo saa ni dk15
  Robo ya 1000 ni 250, je umeishi miaka mingapi wewe mpk uwe na hofu hivyo? ni dakika ngapi ulizokwiaha ishi wewe? Maana hata robo saa hujaishi bado kwenye kalenda ya Mungu, sasa unawahi wapi na unawahi nini? Mwenye haki wa Mungu huishi kwa IMANI. (Ebrania 10:38)
  Ishi kwa imani ukijua kabisa kuwa hatuongezeki bila kuzaana na hatuwezi kuzaa bila kuoa ama kuolewa. So mlingane Mungu akupe mwenzi sahihi Lakini sio kuoana na yeyote!

  Mungu wa mbinguni na akubariki sana

  Naitwa Gladys

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s