Mchungaji Youcef Nadarkhani Aachiwa huru!

Ni furaha kila sehemu baada ya mchungaji Youcef Nadarkhani kuachiwa huru kutokana na kesi ya kuhubiri Injili (uinjilisti) kwa waislamu iliyompelekea kufungwa jela na kuhukumiwa kifo.

Youcef Nadarkhani ametumikia jela miaka mitatu ambapo mwaka 2009 alikamatwa na kuwekwa ndani, 2011 sheria ya kiislamu ilimpa siku tatu aikane imani yake. Pastor akasimamia imani yake na hakumkana Kristo.

Asasi mbali mbali za kimataifa zililaani kitendo cha mchungaji Youcef Nadarkani kutumikia kifungo sababu ya imani yake akiwemo Raisi wa Marekani Barack Obama.

Mitandao ya kijamii ilifanya kampeni kwa ajili ya kuitaka Iran kumwachia huru mchungaji Youcef na wachungaji mbali mbali walitaka Mungu aingilie kati. Mungu amejibu maombi

Advertisements

7 thoughts on “Mchungaji Youcef Nadarkhani Aachiwa huru!

 1. HALELUYA……,

  MI NASEMA KUNA KITU KIKUBWA CHA UVUMILIVU MUNGU ANATUFUNDISHA,KUKAA JELA,MATESO YA KISAIKOLOJIA(KIAKILI) ,KIMWILI LAKINI MUNGU AMEMPIGANIA,

  KWA UPANDE WANGU NABABAIKA CHA KUSEMA KWAKUWA NIMEWAHI KUFUATILIA SWALA HILI MWAKA 2012, MI NILIJUA ATKUFA NIKAMUOMBA MUNGU AENDELEE KUMPA NEEMA HIYO MPAKA WATAKAPOMUUA,LAKINI MUNGU AMETUFANYIA SUPRISE,

  NIMEFURAHI SANA, SIJUI NISEMAJE,BWANA YESU ATUKUZWE MILELE.

  MIMI DP.LEONARD N. MAPUNDA
  MOROGORO

 2. kaka tetea iman mbaka kufa yaan machoz hapa yananilenga machoz ya furaha na shangwe na shauku ya wa2 kama wewe walio jtolea kum2mikia had kufa songa mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee injili ihubiriwe kwa wa2 wote wamjue Mungu wa Bwana we2 Yesu Kristo simba wa kabila la yuda Bwana Yesu asfiweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee kwa wote wenye imani ya kristo amani kwenu

 3. Ashukuriwe MUNGU wa yote na kwa ajili ya yote ayatendandayo kwa watumishi wake

 4. Pastor Youcef ni ushuhuda uliosimama mbele yenu nyoote mliomuomba Bwana aingilie kati shida hiyo. Basi Mungu leo hii amewajibu maombi yenu kwa kadiri mlivyomuomba ili furaha yenu iwe kamili!!!

  Tutamsifu na kumuabudu Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo, milele na milele, Ameeeeen!!!

 5. That is what Jesus came for, stands for.That is what Stephen did.Be blessed Pastor

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s