Ukipanda Ubaya, Utavuna Ubaya!

Ubarikiwe kusikiliza mahubiri haya yenye kukufanya usimame kwenye wokovu, Neno la Mungu linasema  “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtundicho atakachovuna” Je wewe unapanda nini? Mema au Mabaya?

Msikilize mchungaji Donis na Nnunu Nkone wakielezea vyema.

Advertisements

10 thoughts on “Ukipanda Ubaya, Utavuna Ubaya!

 1. Ndg Tunkuh thanx kumjibu ndg Mabinza, sitaenda huko kwa maandiko naomba Tunkuh tusaidiane. Binafsi nilikua natabika na jambo hilo lakini Mungu alinifungua nikaelewa sana, nina amani. Hali halisi ni kwamba kila mtu ajitoae kwa Mungu kwa ukamilifu Mungu humpa kibali na kutembea nae na kumtumia. Haijalishi ni ke au me!!!!. Maandiko yaliandikwa kwa mazingira fulani hilo lazima tulielewe wapendwa tukisoma maandiko hivi hivi bila ufunuo na kuelewa historia na mazingira yake, hatutaelewa na sio vema. Narudia tena jinsia zetu hazimfanyi Mungu asitutumie!!!!. Yeye hutumia hata punda sembuse mwanadam aliyeumbwa kwa mfano wake.
  Hata km ukisema hawaruhusiwi kuwa bishops ni sawa itakua ni claim (dai) lakini uhalisia ni kwamba anawatumia kwa viwango vya juu ktk huduma zote na karama zote na nafasi zote kwa ushahidi mwingi sana sana na udhihilisho. Biblia ni neno la Mungu lakini waandishi wakati wanaandika kulikua na mazingira fulani na historia au mwenendo wa kanisa ktk jamii ile kwa hiyo somehow kanisa lilikua na mafungamano na jamii. So wakati wanaandika yale mambo ya jamii yalikua reflected kwenye biblia somehow. Ubarikiwe. Mambo mengi tunavyomtafuta Mungu kwa moyo wa uwazi na kutaka kuelewa hutufunulia. Ubarikiwe

 2. Mpendwa, Tunkuh,
  Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii ili nijibu hoja zako kama ulivyouliza, sitapita kwa kila mstali ili kukujibu, ila nitajali zaidi sentesi na namna ulivyomaanisha kwa kadri nitakavyoelewa.Msingi wa hoja yangu kupinga wanawake kuwa kuwa Askofu au mchungaji yaani kuwa “Wafundishaji wa injili” ni 1Tim2:12 ambayo ina sema “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha………” Biblia inatoa sababu kuu mbili kwanini, mwanamke asifundishe Neno la Mungu, kwa sababu, Mwanamke yupo kwa ajiri ya Mwana Mme – hivyo Mwanamke ni utukufu wa mwanamme! Na ya pili ni kwamba, Yeye alidanganywa na shetani na akaingia makosani.

  Hizo ndizo sababu kuu mbili zinazo mfanya mwanamke asipate kibari cha kufundisha, hiyo ni Biblia na si mfumo Dume kama mabaraza na jumuia mbalimbali zinavyoonyesha kutokukubaliana na Andiko hilo! Neno katika 1Tim 1:3 linasema, “Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso……..ili uwakataze wengine wasifundishe Elimu nyingine;” Waweza kuona ni kwa jinsi gani Shetani kwa akili anaingiza ‘Walimu ambao tayari alishawapotosha’ Mitume walikwisha jurishwa hilo nao wakaagiza kuwa Waalimu wa kweli wasiende mbali na ‘shule’ zao kwakuwa, Sheta atajaribu kuingiza katika “Sistim” Walimu “Feki” ili kuwapotosha wanafunzi watarajiwa! Jiulize, kama Mwanafunzi akifundishwa na kusimamiwa na mwalimu ambaye tayari KESHA DANGANYWA kuhusu Mtaala wa Elimu husika, Mwanafunzi huyo atafauruje?

  Umenukuu Isa 3: 4 na12a, ni vema, hebu tuusome mstari mzima, tuanzie na huo uliosoma wewe ule wa (12a) katika sura hiyo ya Isa 3:12, ungegundua kuwa inasema, “Kwa habari za watu wangu, watoto ndiyo wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala…….Lakini ile sehemu ya mwisho ya mstali huo (12b) inasema “Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako” ”Hapa nataka tujue kuwa WANAWAKE ULIOJICHAGULIA NA KUJIWEKEA KAMA VIONGOZI, WANAKUPOTOSHA! Hayo nayo ni maandiko na ni Neno la Mungu, lililonukuliwa zamani ya miaka elfu kadhaa kabla ya kuzaliwa huyo mwandishi wa ile 1Tim 2:12!

  Hebu ona, Mungu amesema katika Isa. 3:4 (ambayo nayo umeinukuu) ni kweli, anaweza kuruhusu wanawake na watoto watawale, lakini katika hiyohiyo sura angalia mstari wa 5, anaeleza kitakachotokea iwapo, Wanawake na watoto wakitawala, amesema Watu watadhurumiana, watazarauliana kwakifupi haki itakuwa hakuna! Je, huyo ndiye mtu wa namna ya kiongozi umtakaye?

  Nukuu zingine zote ulizonukuu, ni kama zilivyoandikwa, lakini zinazungumzia tu utendaji wa karama kwa mtu, ujue karama haina majuto. Mwanamke anaweza kutumika kwa vyovyote vile katika Kanisa, anaweza hata kuwa Nabii lakini hoja, ni kwa Mstari upi katika Biblia takatifu unampa Mwanamke haki ya Kufundisha Neno la Mungu? (Maana siyo siri sasa wapo wachungaji, maasikofu, Mitume, naibu mitume, naibu mchungaji kiongozi, mchungaji kiongozi nk Wanawake!) na kazi hiyo ni yakufundisha ili wapatikane wanafunzi, kama ambavyo Yesu aliwaagiza wanafunzi wake.

  Kama wachungaji wanafanya kazi za kitume, ni mtume yupi wanayemfuata wa KIKE aliyechaguliwa na Yesu? Mara nyingi tunawasikia katika mafundisho ya wanawake hao wakisema “Tumeagizwa na Bwana yesu kuwafundisha ili mkiamini tuwabatize…….Tufungishe ndoa nk…!” Yesu aliwaagiza jambo hilo wanawake? Any way, Hoja yangu ni MSTARI UPI KATIKA BIBLIA UNAOWAPA RUHUSA WANAWAKE KUFUNDISHA INJIRI?
  Mbarikiwe na Bwana.

 3. Mpendwa, Tunkuh

  Asante kwa maelezo na ufafanuzi mzuri uliotoa, tafadhali naomba unipe mda kidogo ili niipitie kwanza ile mistari uliyoinukuu ili nijiridhishe, nakuomba uniruhusu nikurudie baadaye ndugu yangu.
  Uendelee kubarikiwa na Bwana!

 4. Sharom
  Ndugu Mabinza……
  Sitaki kukubishia kwa kuwa neno la mungu alibishaniwi isipokuwa, linafundishwa na linafunuliwa kwetu kwa uwezo wa Roho Mt pekee…

  Ni kweli biblia inamtaka mwanaume kuwa kichwa ktk nyanja zote za kitawala, iwe kifamilia, kiimani (ikiwemo nafasi ya kuhubiri neno) n.k.. Lakini kuna mazingira yanayosababishwa na huyohuyo m’me ya kutotambua kusudi la Mungu juu yake na kusimama katika zamu yake km M’me, ebu tusome Isa 3:4 na mstari wa12a…..Hapa nataka tujue kuwa mungu anauwezo wa kuruhusu si W’ke tu kuhubiri bali hata watoto (wachanga kiroho) kuhubiri na kufanya mambo mengine ya kiutawala kutegemeana na W’me wenyewe wamesimamaje…

  Pia tujue kuwa mungu ni wa wote wenye mwili na anashughulika na Roho ya mtu si jinsia yake…. na anapomruhusu Roho mt. kugawa vipawa aangalii jinsia huangalia karama na huduma iliyopo ndani ya Roho ya mtu haijalishi awe wa jinsia ya ke au me.. ebu tusome 1kor 12;4-11…soma tena Yohana Mt.13;20 anaposema mtu yoyote hamaanishi jinsia moja tu bali zote mbili..Kwa msisitizo ebu soma Gal 3;27 ahadi na urithi ni kwa jinsia zote ke na me….na ahadi au urithi huja baada ya kuhudumu vizuri na kwa haki mbele za Mungu, haijalishi ni wa jinsia gani amehudumu..

  1Kor 14;3-5 hapa tunaona kwamba kuhutubu (kuhubiri) ni karama muhimu kuliko kunena kwa lugha kwasababu ndiko kunakojenga kanisa ebu unganisha na 1Kor 11;5 hapa M’ke anasisitizwa kufunika kichwa pale anapohutubu,,kwa huu mstari mwandishi anamaanisha basi.. M’ke kuhubiri si kosa..

  Ebu tuangalie mistari michache ili kuona Wanawake wanavyotumika katika kulijenga kanisa Tito2;3, Mdo18;24-26 hapa tunaona wanawake wanavyotakiwa kutumika kama waalimu…
  Pia katika Rum16;3-4 hawa ni wanawake ambao hawakusita kufanya huduma yoyote (ikiwemo kuhubiri) ambayo Mungu angetukuzwa hata kama ingebidi kukata vichwa vyao…

  Nahitimisha kwa kusema hivi Biblia(Gombo) ni ujumbe unaotafsiriwa kwa njia za Rohoni zaidi kuliko za mwilini….Na ashukuriwe Mungu maana ametupa uweza wake wa kutafsiri ulio ndani yetu kwa kupitia Roho Mt….Na asomaye apate kufahamu… Amina.

 5. Mpendwa Juma Hamis,

  BIBLIA ni Neno la Mungu, halibadiliki, lipo kwa ajili ya utimilifu wa nyakati, yaani lipo bora bila kupungua kwa matumizi ya wakati uliopita, uliopo na ujao! Iwe in Paulo au mwingine yeyote alisema, kama jambo hilo lilinukuliwa katika kitabu hiki kikuu Biblia, basi hilo ni Neno la Mungu, Mungu hajichanganyi, habadiliki na wala hafungwi na nyakati. Akisema amesma, Neno lake halipingani! Yeye ni Amina, na ni Alfa na Omega. Neno linasema, Asikofu ni lazima awe mme wa mke mmoja, vile vile maandiko yanatupa tahadhali jinsi ya kuishi na Wanawake, Neno linasema ni Wadhaifu tuishi nao kwa akili!

  Je, Unaonaje kama Rais akawa na nguvu kuliko “Bodigadi” wake? itakuwa kitendo hicho kimezingatia itifaki? Unadhani kwanini Shetani alisubilishia hadi alipo muona eva (wengine wanamwita Hawa) ndipo akampotosha? unadhani Shetani alikuwa hamuoni Adamu, au alikuwa hajui alikokuwa akiishi? Ukijua hilo, utakubaliana na Paulo na pia utasadiki ya kuwa Wanawake wanamichango yao lakini si kuwa Maasikofu nk.

  Ndugu yangu Juma, ulisema unaushahidi wa Maandiko kuwa wanawake kwa sasa na kwa hali ya Tanzania na Duniani inasapoti wanawake kuwa Maasikofu, naomba unipe hayo maandiko nipate kuelewa, pengine mimi nimejaa mfumo Dume tu sina lolote ila uonevu tu!

  Asante.

 6. Ndg Mabinza hebu tuache mfumo dume ambao hata ushahidi wa kweli unajitosheleza ktk kumtumikia Mungu kipindi tulichonacho. Kwa wakati fulani kweli Paul aliwakataza wanawake kulingana na jinsi walivyokua wakienenda. Lakini kwa ukweli tangu awali kila mtu ajitoae kwa Mungu anapata kibali na kumtumikia Mungu. Ukweli utabaki palepale kua wanawake pia wanamtumikia Mungu kama wanaume. Nina maandiko mengi ya kusapot ila nataka tutumie logic ya kawaida tu na hali halisi ya sasa Tanzania na duniani kote.

 7. Sijajua kama wanawake wanaweza kusimama kuhubiri Neno la Mungu! Je,
  maandiyo yapi yana waruhusu Wanawake nao kuhubiri?

 8. comment zingine bwana, kwanini msitoe comment kuhusu mafundisho yao, eti couple ime match, wewe ndicho unachokiangalia katika maisha yako, pole!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s