Ibada ya wafu!!!


1. Maana:- Ni shughuli yeyote ya kiimani inayofanyika bila uwepo wa Mungu wa kweli, naye ni Mungu wa Israel.Au Ni tendo lolote linalofanyika bila kumshilikisha Mungu wa kweli. Mfano wa Ibada za wafu Ni;-
 Ibada ya Sanamu (Kut.32:4-6, 1Kor.10:7+14, 1Yoh.5:21)
 Matambiko
 Kupiga Bao,Kubashiri nyota,kuchanja chale, Kuchezesha Majini.
 Kuweka tumaini juu ya Mtu/kitu chochote kwamba bila huyo/hicho haiwezekani na kumsahau Mungu wa kweli.
 Mfano;- kuweka tumaini juu ya .
 Mali /mke/ mme/Miujiza/Sheria/watumishi. nk

WAFU/MFU;-
Utangulizi:-Neno wafu ndani ya Biblia limetumika likiwa na Maana zaidi ya moja, Linaweza kutumika kama
i. Ni hali ya Roho kutengana na mwili yaani Kifo cha mwili.(Luk.8:55, Mh.9:5)
ii. Ni hali ya Mtu kutengana na Mungu au kuvunja uhusiano mwema na Mungu (Kutenda dhambi) yaani Kifo cha Kiroho (Ay.21:25)
Kifo cha kiroho. Kuna aina tatu ya wafu katika eneo hili ambayo mtu anaweza kufa kiroho lakini bado anaendelea kuwa hai kimwili. Huyu anaweza akatubu na kufufuka katika wafu akawa hai tena .Pia mtu anaweza kufa kiroho na kimwili maana yake Roho imekufa na mwili umekufa hana nafasi ya kutubu tena.(Uf. 20:5). Kifo hiki ni kibaya zaidi na kinatisha. Ambacho Bwana Yesu alisema msiwaogope wawezao kuuwa mwili bali Mungu mwenye uwezo wa kuuwa mwili na Roho. (……………….) kifo cha tatu ni Mtu kufa kimwili lakini bado anaendelea kuishi Kiroho.Hapa Yesu alisema mtu akiniamini mimi na kutimiza neno langu ataishi hata kama akifa. (Mt…………..).

2 Je Ibada ya Mazishi ndiyo Ibada ya Wafu?
Utangulizi:- Watu wengi wanafikili Ibada ya mazishi ndiyo ibada ya wafu Hapana hii ni sawa na ibada nyingine kama Ibada ya Misa Takatifu, Ibada ya neno, Ibada ya uponyaji nk. Ibada hizo zote zinaweza zikawa ni Ibada za wafu kama wanaoendesha ibada hizo wamekufa kiroho Mfano;- Yesu alisema waacha wafu wazike wafu wao (………………) maana yesu hakuona tofauti kati ya yule aliyekufa na wanaompeleka kumzika wote walikuwa wamekufa. .Katika hali hiyo hata kama uponyaji utatokea (Muujiza) katika ibada hiyo. Bwana Yesu alisema siku ya mwisho watasema tulitoa pepo tulihubiri neno kwa jina lako, tulipoza wagojwa kwa jina lako lakini yeye atasema siwajui ninyi ondokeni mbele yangu enyi watenda maovu.(Mt. 7:21-23) Hebu tuangalie ibada za kumbukumbu za Watu maarufu/mashuhuri Katika jamii/familia/kanisa/Dini/ukoo. au Mathehebu nk waliotutangulia tayari mbele za haki. Je zinaonekanaje mbele za Mungu? Je zote ni ibada za wafu.? Ni jambo jema na linapendeza mbele za Mungu kuandaa ibada ya kuwakumbuka wapendwa wetu lakini la msingi je ibada hiyo inafanyikaje? kama inaondoa/inachukuwa nafasi ya Mungu kama.(Matambiko) basi hiyo ni ibada ya wafu na ni machukizo mbele ya Mungu na Mungu atashusha ghadhabu juu yao. Lakini kama inafanyika kwa sifa na utukufu wa Mungu kwa mambo mema waliofanya wapendwa wetu waliotutangulia katika haki basi ni ibada njema inayoleta utukufu wa Mungu kati ya watu na kumtukuza Mungu. Angalia Binti wa Yeftha aliwekewa siku ya kukumbukwa (Amu.11:39-40) aliwekewa siku kwa ajili ya Tendo jema alilotenda yaani kukubali kupoteza uhai wake akiwa Bikra kwa ajili ya ushindi wa taifa la Israel. Kwa kuwa tunajua na kufahamu kuwa mema/mabaya ya mtu hayaishii tu baada ya kufa bali yanaendelea. Kama ingekuwa hivyo tusingekuwa na maandiko yanayosimulia matendo ya manabii na mitume kwani hakuna haja ya kuyazungumzia wala kukumbuka kwa kuwa walishakufa. Tena kwenye Biblia hata ya wale waliotenda mabaya wapo. Kwa mantic hiyo ndiyo maana kanisa Takatifu katoliki (la popote) la Mitume limeweka utaratibu wa kuwakumbuka waliotendea mema kanisa tangu mwanzo wa ukrito.kwa kuenzi mchango wao katika wokovu wa mwanadamu kwa kuwekea tarehe zao za kuwakumbuka/ kusherehekea na hata kutoa majina kwa watoto wetu kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu na kuwa mfano na ushuhuda kwa watoto wetu na vizazi vyote kwamba inawezekana kuishi maisha matakatifu hapa Duniani (Watu hao wanaitwa Watakatifu (kama huamini juu ya watakatifu haiongezi chochote wala kupunguza ila wewe ishi tu neno la Mungu) Na huo ndiyo ujumbe wa Yesu kristo kwetu tuulete ufalme wa mungu kati ya watu (…………………….).

Na tunaweza kuleta Ufalme wa Mungu kwa kuelezea mema ya wapendwa wetu waliotutangulia, Kamwe si kwa ajili ya kuwatukuza watu hao na tukifanya hivyo tunakuwa tuna abudu wafu na ndiyo ibada ya sanamu. Maana Mungu amekemea vikali hata kuwatukuza watu walio hai kiroho na Kimwili kwa ajili ya mema waliotenda/wanayotenda na akasema thawabu yao imeishia hapa. (Mt.6:1+5) lakini watumishi wa sasa wanatangaza hadi kwenye Radio na televisheni Hata wakifunga siku tatu kavu watatangaza njoo upokee muujiza wako kwani tumefunga siku tatu kavu. Nao wadhaifu wa imani wanamiminika huko,Mungu atusaidie. Kwa hiyo si vibaya kwa kuadhimisha sikukuu za wapendwa wetu kwa sifa na utukufu wa Mungu. Kwa kuwa Maandiko yanaweka wazi kuwa mtu akimjua Mungu wa kweli na kuishi maagizo yake na kujua mwisho wake (Destin) Mungu atamfanyia jina (…………….)Mfano;-Mama wa Yesu aliyajua hayo ndiyo maana akasema “Tazama vizazi vyote vitaniita Mbarikiwa.(Luk.1:48) Kwa maana aliyatimiza yale yote aliyoambiwa na bwana na Mungu kamfanyia Jina. Hata wewe leo hii ukiyatimiza yote uliyoamriwa na Mungu hakika Mungu si mchoyo atakufanyia jina kati ya watu. Tamani kuwa mtakatifu kamwe huwezi kuwa mtakatifu kwa kuabudu sehemu yenye miujiza mingi kwani inaweza ikakufariji hata ukafunika dhambi zako nyingi hata ukapotea kabisa.

3.Je kusali wakati mazishi au tukiwa Makaburini hiyo ndiyo Ibada ya wafu?
Utangulizi:- Mara nyingi sisi tunampangia Mungu au kumwekea mipaka juu ya uwezo wake na huruma yake. Tutambue kuwa uwezo wa Mungu haupimiki wala kuelezeka kwa kuwa mawazo yetu ni tofauti na ya Mungu (Isay.55:8) Na kwa kuwa huruma ya Mungu hushuka hata Kuzimu na kuinua tena (Tobit:……., ISamwel:…… Zab:……..). Kwa hiyo hatuwezi kuelezea uwezo na huruma ya Mungu kwa upana na undani wake. Katika hili la kuwaombea waliokufa hatutofautiani na watu wa Agano la kale na wakati wa yesu kimtazamo. Hebu tuangalie Yule mkuu wa sinagogi alikwenda kumuomba Yesu amnusuru Binti yake aliye katika hatari ya kufa. Yesu alikuwa amesongwa na watu wengi hiyo hakuweza kufika kwa wakati hata kijana Yule akafa, Ndipo akaja Mtu akamwambia Yule mkuu wa Sinagogi “usimsumbue mwalimu binti yako ameshakufa” (Luk.8:41-43+49-55) kwa maana nyingine alimwambia usimuombee Mtu aliyekufa maana kumbukumbu lake limepotea (Mh.9:5) Lakini Yesu aliposikia akasema amini tu binti yako atapona. Basi ugumu uleule uliompata mkuu wa sinagogi na Yule mtu unamkuta pia Martha yeye alipoambiwa kuwa atafufuka alijibu “Najua atafufuka siku ya mwisho” kwa hiyo bado anamawazo yaleyale ya kumwekea Mungu mipaka juu ya uweza wake na huruma yake. Lakini nampenda sana Martha kwani alitambua ukuu na uweza wa Mungu hauna mipaka akasema Najua hata sasa ukimuomba Mungu lolote atafanya.(Yoh.11:22,Yoh.11:14-44) Basi ndugu tusimuwekee Mungu mipaka juu ya uweza wake na huruma yake.

Majumuisho:-Kanisa katoriki haliwaombei/kuwaomba wafu kama nilivyotangulia kueleza maana ya Wafu hapo juu kama umenielewa vizuri basi haitakuwa ngumu kwako kufahamu hili. Kanisa Takatifu Katoriki la Mitume linawaombea wapendwa wao waliokufa katika hali ya Neema na wala kanisa halifundishi watu wafe katika hali ya neema bali wafe wakiwa watakatifu. Kufa katika hali ya neema nitafafanua katika somo la Kutubu na Kuungama.

(Hivyo vifungu nilivyoacha wazi nitakutafutia unajua niko bize sana ila nakupenda kwa kuwa unapenda kujifunza Mungu akubariki.)

Kwa Maoni Maswali.

Na. Kaka Jeff.

Advertisements

33 thoughts on “Ibada ya wafu!!!

 1. Bwana Yesu asifiwe! Nashukuru sana kwa wote mlio changia Mungu awabariki hasa ndg. Dickinson kamugisha ndg. Umemitia moyo sana kwani huwa naumia sana kuona watu wanatoa hukumu kwa mambo wasiyoyaelewa vinzuri. Maandiko yanasema ” maana wao hutukana chochote wasichokielewa vinzuri” kuna ndg. Ck lwende ndiye aliyenipelekea mimi kuandaa somo hili La “IBADA YA WAFU “na niliandaa ktk hali ya haraka kwani nilikuwa Sina Muda wakutosha lakini hivi sasa somo hili limekamirika. Pia niliahidi kwamba tutajifunza hatua kwa hatua lakini hadi sasa hajacomment chochote ndiyo maana sikuendelea maana Mungu kanifundisha mambo mengi ambayo niliambiwa si kwa ajili yangu tu bali na wengine. Ndg. Dickinson kamugisha nakushukuru sana kama kunasehemu hujanielewa au nimekuchanganya niulize tukifikia muafaka nitaendelea kufafanua maana ya kufa ktk hali ya neema kupitia somo la KUTUBU NA KUUNGAMA. lengo ni kuleta umoja wa Imani Kati ya wakristo. Ili Kuondoa kushutumiana na kuhukumiana kwani kunampa shetani nafasi ya kutushambulia kirahisi. Soma (ef. 4:13) (Rum14:

  3+10) Kaka Jeff.

 2. nawapenda sana wote mnaochangia mada zote za page hii, napenda tuombeane,anaesema web hii haina maana,huenda ana nia tafauti nasi

 3. “UTAKUFA HAKIKA,” VS “HAKIKA HAMTAKUFA”

  MUNGU ALISEMA MKITENDA DHAMBI NI KUFA
  SHETANI AKASEMA HAKIKA HAMTAKUFA

  YESU ALIKUFA, TUPATE UZIMA
  YESU ATAKUJA, ATAFUFUA WAFU
  MWISHO WA VITA BIBLIA INASEMA MAUTI IMEMEZWA.

  ANAETANGAZA LEO KUWA MTU AKIFA ANAENDELEA KUISHI ANAMSAIDIA SHETANI KUSEMA “HAMTAKUFA”

  MUNGU ALISEMA MKIFANYA DHAMBI MTAKUFA HAKIKA BAADAE ATATUPA UZIMA WA MILELE KWA NJIA YA KRISTO.

  LEO WATU WANASEMA WAO NI WAZIMA BAADA YA KUFA WANAISHI MAHALI FULANI.

  FUNDISHO 1:
  KUAMINI MTU ANAISHI MBINGUNI MARIAM N.K IMEWAFANYA WENGI KUWAOMBA WAFU, HUKU BIBLIA INASEMA HAWASIKII.

  FUNDISHO 2:
  KUAMINI KUWA WAFU WANATUMIKIA ADHABU IMEWAFANYA WATU WAWAOMBEE WATU HAO WAONDOLEWE ADHABU.

 4. Mara zote ninaposoma katika mktandao mbalimbali ninachoona ni kuwa kila mtu anaamini anajua, ana mafunuo, ndugu zangu kuna tofauti kubwa sana kati ya kanisa katoliki na makanisa mengine yote. Kanisa katoliki ndio kanisa pekee lililokuwepo hadi karne ya 16 baada ya Martin Luther ambae nae alikua padre wa kikatoliki “kuasi”.
  Tuongelee kipengele ambacho nimeona kinajadiliwa hapa, Kuombea marehemu:
  Kwanza ieleweke kuwa maongeze au mjadala wa suala hilo hauwezi kuwa sawa kati ya mkatoliki na mprotestant kwani wana vyanzo tofauti vya kuongoza maamuzi yao, tunajua kuwa baada ya Martin Luther “kuasi” alikataa pia vitabu kadhaa vya agano la kale kimoja wapo ni kitabu cha pili cha wamakabayo ambacho kinaeleza vizuri ibada ya namna hiyo 2Mak.12:38-45.
  Lakini tuachie hilo, inawezekana hata kusoma vilivyopo watu hawasomi kabisaaa, mfano ukisoma vizuri kitabu cha wakorinto utagundua kuwa kulikuwa na utaratibu wa wakristo kubatizwa kwa ajili ya wafu rej. 1Kor.15:29.
  Tujiepushe na mabishano na majigambo yasiyojenga tujifunze toka hekima ya waandishi wa biblia “Kama Fulani akijiona ni mchamungu, lakini hatawali ulimi wake, anapotosha moyo wake; uchaji wake huyo haufai kitu. Dini safi isiyo na hitilafu kwa Mungu baba, ndio kuwatunza yatima na wajane katika shida zao, na kujiepusha na madoa ya ulimwengu huu”. Yak.1:26-27
  Asanteni.

 5. Yesu alipokufa pazia lilipasuka ikiwa na maana kilammoja anatakiwa kumuomba Mungu moja kwa moja badala ya sala zako kupitia kwa Kuhani. kwa nini kuomba au kuombea marehemu?

 6. wapendwa kwa wale kweli wenye nia ya kuupata uzima wa milele jilindeni sana na kitu kinaitwa NIDHAMU YA WOGA. usijaribu kunyamaza hata siku moja unapooa mtu anapotoka kwa kuiacha njia ya kweli na uzima… ambayo ndiyo YESU MWENYEWE. imeandikwa zijaribuni hizo roho. pia Mtume Paulo alisema mtu yeyote atakaye wahubiri injili yeyote isipokua hii niliyokwisha uwahubiri mimi hata kama ni malaika ”MKATAENI!!!”

 7. HUU NI UNYENYEKEVU WA AJABU NA WA KUTISHA MNO KAMA UNATOKA
  MOYONI! (LUKA 14:7-11).

  Haya pia ni mafunuo ya kutisha sana.Ni HEKIMA ya Yesu mwenyewe.Kila wakati
  ili tuweze kujifunza na hatimaye KUFUNULIWA MAMBO ambayo yanatupeleka katika UTUKUFU wa juu zaidi ni LAZIMA tukubali KUJIDHIRI/KUJISHUSHA kwa ajili ya
  utukufu wa Mungu aliye hai(TAFAKARI-WAFILIPI 2:3-4).Huu ni UNYENYEKEVU ULIO HAI.Tunatakiwa kusikiliza zaidi huku tukiomba muongozo wa Roho Mtakatifu
  wa jinsi tunavyotakiwa kujibu.Hii ni muhimu sana ili TUSIMCHUKIZE Mungu wetu na kupingana na kile alichokikusudia.Kwa kweli mara nyingi kwasababu ya kiburi tumeambulia AIBU na FEDHEA!!

  Tunapokubali kushuka na kuvaa UDHAIFU NA UPUMBAVU WA MUNGU(TAFAKARI-1 WAKORINTHO 1:25),ndipo Roho Mtakatifu anapotufunulia mengi zaidi na kutupandisha mahali ambako hakuna mwanadamu anayeweza kutushusha wala kupafikia mpaka akubali kunyenyekea.

  Roho ya kujitia UJUAJI,KIBURI,MAJIVUNO,DHARAU,UBINAFSI,JEURI,UKAIDI,n.k
  haitoki kwa Bwana.Ni roho ya KUUCHUKIA UNYENYEKEVU(UCHAJI) WA YESU
  ambayo inatufanya tuambatane na uovu na kujenga nao urafiki wa kudumu!Ni roho inayoyuondolea utukufu wa Mungu na kutushusha CHINI KWENYE MAVUMBI
  (TAFAKARI-MITHALI 8:13,ZABURI 19:13,YAKOBO 4:10).

  Ndugu yetu MKATOLIKI aliyetoa maoni yake kwa jina la MAJ ameonyesha unyenyekevu wa ajabu sana pale aliposema wazi kwamba TUMUOMBEE HEKIMA YA MUNGU NA SIYO MIUJIZA,UTAJIRI,MUME,KAZI,CHEO WALA JAMBO LOLOTE LA KIDUNIA.Huu ni ujumbe mzito kuliko uzito wa dunia ambao umeifanya mifupa yangu isagane kwa ndani na damu yangu ichemke kwa FURAHA NA AMANI YA KRISTO.Wakati nasoma ujumbe huu MACHOZI YA USHINDI YALIKUWA YAKINITIRIRIKA MOYONI NA SIYO MACHONI.NILITAMANI YATIRIRIKE MACHONI ILI NIYAONE LAKINI YESU AKAYAZUIA!NILIJIKUTA NAUGUA SANA ROHONI NA KUMRUDISHIA YESU UTUKUFU.Gafla Roho Mtakatifu akaniongoza kuomba maombi ya ajabu sana kwa ajili ya ndugu zetu kina MAJ,SIMA na kaka JEFF.
  UPENDO(hekima) wa kristo uwafunike na kuwatafuna kabisa!Neno KUTAFUNA linaweka msisitizo hapo.

  KWA KADIRI YA MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU kulingana na NENO la Kristo
  kuna mengi makubwa na magumu ambayo nimejifunza katika somo hili la IBADA ZA WAFU(TAFAKARI-YEREMIA 33:3).Kuna mambo ambayo tunahitaji kumuombea ndugu yetu JEFF pamoja na wengine wanaofanana na yeye ili ROHO MTAKATIFU AWATIE KATIKA KWELI YOTE.KAMA MWALIMU ROHO MTAKATIFU AKINIPA KIBALI CHA KUELEZEA BAADHI YA VIPENGELE KADIRI YA MAFUNUO KATIKA MAANDIKO KWA AJILI YA MANUFAA YETU SOTE KAMA WANAFUNZI,SITASITA KUFANYA HIVYO.Kuna mambo ambayo JEFF ameyaeleza kwa usahihi sana na nimejifunza mambo mapya ambayo sikuyajua.

  KUNA SABABU YA KIROHO ILIYOMSUKUMA KUWEKA HILI SOMO LA IBADA ZA
  WAFU HADHARANI NA BILA KUITAZAMA HIYO SABABU KWA JICHO LA ROHONI HAKIKA TUTAKWAMA NA KUZUIA MAKUSUDI YA MUNGU.

  HATUWEZI KUTENGANISHA KATI YA UNYENYEKEVU NA UPENDO WA KRISTO.MUNGU TUREHEMU ILI UENDELEE KUTUFUNDISHA KUPITIA ROHO MTAKATIFU NA KUTIMIZA KUSUDI(MAPENZI) LAKO HAPA DUNIANI(TAFAKARI-MATHAYO 6:10).

  MUNGU AWABARIKI NYOTE MLIOSHIRIKI MJADALA HUU.

 8. MNAOFANYA IBADA ZA WAFU POLENI SANA.KWANZA KABISA MUNGU SI MUNGU WA WAFU. MATAYO 22:25-33 IKIWA MUNGU SI MUNGU WA WAFU JE WALE WANAOFANYA IBADA ZA WAFU,WANAFANYA KWA MUNGU GAN?PIA MUNGU ANAONYA HIZO IBADA K.TORAT 18:9- asionekane mtu awaombae wafu.JE IBADA ZENU ZA WAFU ZIKO UPANDE GANI;WA MUNGU AU WA SHETANI?

 9. Jambo la muhimu ni kuamini katika Yesu kristo, Ila haina maana yoyote kukosoana jambo ambalo hulijui kiufasaha, kwan ni mambo yatakayo endelea kuwepo chamsingi ni kuhimizana kufanya yanayo mpendeza Muumba..

 10. Asante kaka Jeff. Natamani kupata mafundisho mengi zaidi toka kwako. Bwana awe nawe kaka.

 11. Bwana Yesu asifiwe!
  Roho Mtakatifu na atuongoze nitajibu hoja zenu. Ndugu wapendwa lengo la mafundisho haya kamwe si mashindano bali ni kuweza kuleta umoja wa Imani kama maandiko matakatifu yanavyosema “Tuufikie umoja wa imani” (Efe.4:13) maana tu ufalme mmoja, maana ufalme unaohitilafiana hautadumu. na matengano ni kazi ya Ibilisi. Basi nitaanza na ndugu yangu Lwitiko Katule.Kufa ktk Utakatifu ni kufa ukiwa umetakaswa dhambi zako zote kwa kadili ya utaratibu wa Mungu na kanisa, kama ufunuo unavyosema ” Heri wafu wafao ktk Kristo” sasa hao ndiyo watakatifu kamili maana hawawezi kutenda dhambi tena.kufa ktk neema nilisema nitafafanua ktk somo la kutubu na kuungama.Kwa ndg. yangu Alexanda kapinga, ulikuwa huna haja ya kuuliza swali ambalo niliahidi kulitolea ufafanuzi inaonyesha hauko makini, kuhusu nukuu za vitabu ambavyo haviko kwenye biblia ya Waprotestant kumbuka wanaosoma humu si waprotestant peke yao bali hata wakatoliki na wengine wanasoma tusiwe wabinafsi ndio maana nimetoa kotekote. kuhusu utakatifu wa Maria inaonyesha hauko makini bado ktk maandiko matakatifu, Watu waliokufa ktk Kristo hao ndiyo watakatifu maana wametakaswa dhambi zao zote. kuna watakatifu waishio duniani na waliokwisha kufariki dunia. Mf.Watakatifu waliokufa Agano la kale miili yao iliinuka wakati ambao Yesu alikata Roho.Soma ( Mt.27:52).kwa hiyo kanisa linaamini Maria alikufa ktk Kristo au ndani ya Kristo hivyo ni mtakatifu kamili. Ndugu yangu Herbert Eliya uliza wapi hujaelewa kusema pote hiyo ni sifa za mwanafunzi asiyependa kujifunza (Unwilling student). Ndugu yangu Mr, Milinga na mashaka na uelewa wako maudhui ya somo ilikuwa wakatoriki hawaombei wafu. pia kwa maelezo yako bado inaonyesha unatatizo la tafsili Ndugu Milinga Miili hii haiende mbinguni bali Roho, na Roho ndio itakayohukumiwa kwa matendo ya mwili. kumbuka Roho haifi kwa maana ya kupotea kabisa bali ni kutengana na Mungu kwa sababu ya dhambi na huko ndiko kufa kwa Roho.Haya bado nimeeleza maana ya wafu linavyotumika kweye maandiko bado kwako ni shida.Alafu umenukuu maandikoyanayosema “Mungu hapendi mwenye dhambi hata mmoja afe bali wote wafikietoba”msitari huo hauna maana kwamba watu hawafi ktk dhambi bali unasisitiza upendo wa Mungu kwetu ili tutubu kabla ya mauti.( Yaani tuwe watakatifu kabla ya kufa kama yeye alivyo mtakatifu).Ndg. yangu Kinyau Haggai haya si mapokeo somo hili linafundisha kwamba ni machukizo kuombea wafu au kujiunganisha na wafu likifafanua kuwa wakatoliki hawaombei wafu kwani ni machukizo mbele za Mungu. Pia unashidwa hata kunukuu kilenichoandika mimi sijasema “Kanisa katoliki la mitume” Bali KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA MITUME” Na hilo ndlo jina la kanisa hilo ambalo huwa tunakili wakati wa MISA na wakati wa ubatizo kwa kukiri, NASADIKI KWA KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA MITUME. Kwa ndg. yangu Julius Gidion elewa sijakariri neno la Mungu bali kwa uwezo wa Roho Mt.naelewa na najua njia, kweli na Uzima, Biblia ni reference tu ya kumjua Mungu wa kweli (It is a guard-line), Kwamba Roho Mt. ndiye anayetufunulia kupitia maandiko matakatifu, kwamba Roho Mt.akishatufunulia ndiyo tunapata uthibitisho kutoka kwenye maandiko. kwa hiyo kukariri vifungu siyo kujua Biblia. Najua ya kwamba amelaaniwa yule amtegemeaye mwanadamu kuwa kinga yake. Mimi mwalimu na Kiongozi wangu ni Roho Mtakatifu. Amina. Shukranu za pekee kwa ndg. maj na Ndg. Sima.

  Na Kaka Jeff.

 12. Ndg yangu maj, soma biblia toka mwanzo hadi mwisho hakuna mahali kuna andiko linalosema tuchonge sanamu na kuziweka kanisani pia hakuna andiko linalosema tuombe kupitia Maria.Soma kitabu cha kutoka 20:4 kuhusu katazo la kuchonga sanamu. Kuhusu mwombezi wetu soma maandiko yafuatayo:Warumi 8:34; 1Yoh2:1-2; Waebrania 7:25 Yawezekana kabisa wewe siyo mbishi kama tulivyokuwa sisi wengine kabla ya kuijua kweli ambayo sasa imetuweka huru.
  Unaweza kujaza page kwa kuweka reference ya maandiko na maelezo mengi sana pengine ambayo akili zako za nafsi zinakuaminisha kuwa umesimama kwenye kweli kumbe sivyo kabisa! Je umewahi kujiuliza swali hili.Bila sanamu ibada haiwezi kufanyika?kumbuka ibada hufanyika ndani ya moyo wa mtu baada ya mtu kuuandaa moyo wake na si baada ya mtu kuangalia sanamu.Naomba unapokwenda kusoma maandiko haya kabla hujaanza mwombe Mungu kwanza ili Roho Mtakatifu akusaidie usiende kusoma huku ukiwa umeshikilia hizo hoja zako ebu nyenyekea kwanza mbele za Bwana ili Yeye ndiye akuongoze kujua ukweli ni upi na siyo wewe umuongoze kwa kile unachokijua kwa sasa.BARIKIWA

 13. Kama nimeeleweka sitaki maelezo ya kurudia nataka mwenye msuli wa imani aniombee nipate HEKIMA mbona kwa hilo ujatoa comment, ubishi tu!

 14. Ndugu yangu MAJ ukweli wa biblia huwezi kuutangua kwa maana watu wanaeleza ukweli wa maandiko wala hawana nia na kuukashifu ukatoliki, pia nukuu yako ya vitabu kama Makabayo haitasaidia kwa maana inaeleweka wazi hivyo vitabu sii sehemu ya biblia ila viliingizwa bila kukubaliwa na Canon ya biblia. Na kama umesoma historia ya kanisa ujue swala la ibada ya wafu ya kumwombea marehemu ni kitu watu walikaa kikao na kupitisha kwenye Marekebisho ya Cluny mwaka 910. Soma kitabu HISTORIA YA KANISA -VIPINDI VYAKE SABA kilichoandikwa na Fr. F . Portmann na kupitiwa na Padri Evaristi Ngawiliau ktk ukurasa wa wa 52 hai 53 utaona. Kwahiyo ndugu yangu ukiona watu wana ku-challenge ujue kwamba wanaelewa vitu vingi vinavyofanywa ndani ya kanisa katoliki sio vya kibiblia bali watu walikaa vikao na kukubaliana kuyafanya japo vinapingana na kusudi la Mungu

  Mfano mwingine mzuri ni juu ya kumwomba bikira Maria atuombee kwa mwanae wakati hatuna reference ya namna hiyo. Biblia inatuambia tuombe lolote kwa jina la Yesu Yoh.14:13-14, pale mnapotumia harusi ya kana kama reference mnakosea kwa maana hapo walitumia nafasi ya mama akiwa hai, sasa ameshakufa itawezekana je ?.
  Ukija swala kama la sanamu mnajitetea sana kuwa hamziabudu bali mnaziheshimu, mi sidhani kama hiyo lugha inaweza kubadilisha maana, cha muhimu ni kuziondoa kwa maaana hazisaidii chochote, Neno la Mungu limeshasema tena kwenye zile amri kumi za Mungu usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu nchochote kilichopo juu mbinguni, wala kilichopo chini duniani, wala kilichopo majini Kut-20:4. Kwahiyo dhambi inaanza pale tu unapoichonga hiyo sanamu kwa kuwa umeshakatazwa, kosa la pili ni mstari wa 5, usivisujudie wala kuvitumikia.
  Kwahiyo ndugu yangu hii ni changamoto kwako kwa maana ni vitu viko wazi mno wala sii vya kuhitaji maarifa mengi kuvijua ila tu kwa uwezo wa Roho wa Mungu atupae kuyafunua mafumbo ya Mungu 1.Kor=2:10. Shida kubwa mnayoipata ni kwa kuwa mambo mengi yanayofanyika ndani ya ukatoliki ambayo hayana msingi kibiblia yanajibiwa zaidi kwa kutumia falsafa za kibinadamu na kwa sababu wengi wa wakatoliki hawaijui biblia basi hawawezi kuhoji bali ni kusema ndio hata kama ni jambo baya.

 15. wapendwa nilichogundua ktk web. site yenu ni ubishi na udhehebu,suala la kumtukuza Mungu halipo!.Nimesoma tena comments za watu wote , zote ni negative tena hazina base , isipokuwa mimi na Sima .Nimegundua ni kwa vile aliyetoa mafundisho hayo ni mkatoliki. kitu kingine ni ubishi, hii ni kwa vile nimeomba kuombewa Hekima ya Mungu kwa yeyote mwenye msuli wa imani na pia nikaeleza jinsi Mungu anavyonibariki pamoja na Ukatoliki wangu,hakuna aliyetoa comments, isipokuwa Chriss Munguti aliyejibu kwa kejeli eti “sala ktk mazishi”.Lakini ningeendeleza kutoa comment chanya au mafundisho kuhusu mada hii bila shaka ningepata comments za upinzani na kejeli kibao! Wapendwa kuna tatizo kubwa sana ktk Ukristo wetu wa sasa, mtume Paulo alikuwa akifurahia watu wote waliokuwa wakimhubiri Kristo bila kujali rangi,taifa,kabila,wala chochote kilichowatofautisha,bali alipenda kusema “maadam injili ya Kristo inahubiriwa” kitu ambacho naamini ndicho kinafanyika ktk Kanisa Katoliki ,jamani jina lipitalo majina yote ndiyo linahubiliwa Kanisa Katoliki na si vinginevyo ! japo kuna utofauti kidogo ambao ni mitazamo ya kiubinadamu na wala siyo ya kimungu,hainiingii akilini kuwa M/Mungu atahukumu mtu basing on kusali Rozari,misa za wafu,kusali J,pili,maungamo na vitu kama ivyo,kama ni hivyo asingetupa amri 10,kwa nini sisi tunapenda sana kukosoana,kuhukumiana na vitu kama ivyo kwa kujifanya wajuzi wa maandiko,na badala ya kuyatumia vizuri kuhubiri enjili ili watu wote waje kwa Kristu? mtindo huu umefanya Ukristu kuwa biashara na wala siyo kuwatangazia watu habari njema,na hii dhambi itakuwa juu yetu sisi tunaojifanya tunajua,nawaomba wanajiona wameokoka wokovu wao huwasaidie wale ambao hawajaokoka Rum.15:1-6 , waendelee kumgeukia Kristu,maana udhaifu wa kibinadamu bado unawakabili,pia waonyeshe kuokoka kwao kwa MATENDO na wala si kwa MANENO ili wawavute wengi kuja kwa Kristu,mtume Paulo ambaye ni mwanadamu aliyefanya kazi kubwa sana ktk safari yake ya wokovu anasema Rum.15:14- 18 , 1Petro :15-16.
  Kuhusu misa za wafu – utukufu,sifa na shukrani katika ibada hizi ni kwa Mungu wala si kwa wafu maana maandiko yanasema tumshukuru Mungu kwa kila jambo biblia imekuwa na upana sana ,ukiingalia haraka haraka bila kuitafakari hutaelewa someni hapa Zab.30:9 ,Zab 88.5,10-12 , Zab.115; 17-18 lakini biblia haikukomea hapo pia inasema soma Hekima 3: 1-4 , Daniel 12: 2-3 na kwa wale watakao weza someni 2 Mak.12: 38-45. Japo mmesema Mungu si wa wafu bali walio hai,lakini bado ni Mungu wa Ibrahim, Isaka, Yakobo, Musa, Ebednego ,Daniel,Eliya Abeli na wengine na wala atumuiti Mungu aliyekuwa wa hao waliotajwa maana wao pia ni wafu. TAFADHALI NAOMBA TENA,WALE WENYE MSULI WA IMANI,MNIOMBEE HEKIMA YA MUNGU.chooooooooooooooooooonde!

 16. Aunt Sima, hata mimi ninaposoma michango ya watu yenye kumkebehi mtu kwa kile anachoamini au anvyoelewa huwa Napata shida,ndiyo maana naomba wapendwa yule aneyejiamini kuwa na MSULI WA IMANI(maana huyo ni mpenzi wa Mungu) seriously aniombee HEKIMA YA MUNGU. Mimi siwezi kusema sijaokoka ikiwa bwana wetu Yesu Kristu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu pia na wala si za mtu,ukoo,kabila ,dhehebu au taifa moja,bali ni kwa wote hata wale wasiomkiri kuwa yeye ndiye bwana na mwokozi wao,na si hilo tu bali ni pamoja na wasiotimiza amri za Mungu,na kwa vile alijua si rahisi kwa binadamu yeyote kuyatimiza yote MSAMAHA WAKE U WAZI kwa yeyote anayetubu mbele yake. Mimi ni mkatoriki ambaye nakiri matendo makuu ambayo bwana ananitendea pamoja na ukatoriki wangu,sijawahi kuona ni wapi aliponipungukia,na kuna wakati huwa naogopa,hivi mimi ni nani hata bwana wangu anitendee haya? ndiyo maana naleta kwake yeye aliye na MSULI WA IMANI aniombee HEKIMA YAKE. Wapendwa ktk SG akili za M/Mungu zi tofauti na zetu kama zilivyo mbingu na dunia. tusije tukajihesabia haki siku ya mwisho ikawa kama someni Luka 14: 1. 7-11. Baba wa bwana wetu Yesu Kristu na awabariki nyote.

 17. Ndugu yangu “Maj” pia nimependa jinsi ulivyotoa maoni maana kati ya maoni yote niliyosoma juu ya hii mada, ni wewe tu ndie hukuonesha kebehi. Inawezekana kabisa kaka Jeff akawa ametoa mafundisho ambayo si sahihi au ni sahihi, sipendi sana kuongelea hilo ila ninachokiona mimi kwa wale mnaochangia mngeonesha basi wapi si sahihi kwa njia ya kufundisha zaidi na si kukebehi maana kwa jinsi tunavyotoa tu maini inaonesha ni jinsi gani tunampa Mungu wetu utukufu hapa, au ni jinsi gani wengine tunajihesabia haki mbele ya Mungu tayari. Kwani kama mtu ametoa mafundisho yasiyofaa ni kwa nini basi sisi tusirekebishe kwa kutoa yale tunayoamini yanafaa kwa upendo na si kwa kebehi? Mf. baadhi tu ya nukuu ambazo kwangu mimi naona hazimpi Mungu wetu utukufu katika kuchangia ni pamoja na ” tehe tehe tehe tehe tehe!! duuuu! hii nayo mpya hii mi sijawahi kuisikia hata kidogo………., “Kwa ufupi sijakuelewa,pia inaonekana hujui unacho jaribu kufundisha,pia nahisi wewe umeandaliwa somo ukapewa na bila kulichunguza ukaamua kuliweka hapa bila kulichunguza” na nyingine pia.

  Kwa maoni yangu- kwa wale ambao wanaona wamesimama thabiti katika neno na wanaelewa maandiko vizuri basi hebu fundisheni kwa upendo ili wanaosoma hapa waone upotofu wa Jeff na ukweli wa maandiko kutoka kwenu ili wote tuweze kupelekana kwa Mungu na asibaki hata mmoja.

  Samahani kwa nukuu nilizoweka kama nitakuwa nimewakwaza wahusika

  Mbarikiwe

 18. Jeff rafiki wa Mungu,inaonekana una hekima ya Mungu . Endelea kuitafuta ,maana inaonyesha unafundisha watu wanaoonekana nia yao si kujifunza bali ni kubishana tu. Lakini ujaonyesha kukwazwa nao. Mungu wa bwana wetu Yesu kristo akubariki. Yeye ambaye atatuhukumu kwa yatutokayo ndani ya mioyo yetu wala si kwa ibada za wafu,Rozari,watakatifu,maungamo na mambo kama hayo,ambayo yanaonyeshwa na wapendwa kama ndiyo kigezo cha hukumu mbaya toka kwa Mungu. Wapendwa wa bwana ni vema tuwafundishe watu mambo yanayowatia unajisi . Naomba yule anayejiamini ana MSULI WA IMANI,ambaye huyo ni RAFIKI wa YESU. Naomba mniombee HEKIMA YA MUNGU sihitaji MIUJIZA,UTAJIRI,MUME ,KAZI ,CHEO wala jambo lolote la kidunia. nawaomba mnisaidie kuomba.

 19. kaka jeff nakuonea huruma sana na hata kama ni kumdanganya mtoto mdogo hawezi kukubaliana nawe, nakushauri rudi kwanza ukafunzwe upya ukikomaa ndo uje na nakushauri sana uwe makini na neno la MUNGU usije ukaongeza wala kupunguza hata chembe ya neno lake,na nimecheka sana uliposema kwamba nafasi ya vifungu ulivyoacha wazi utavitafuta ya kwamba upo bize,unawezaje kufundisha watu juu ya somo fulani kuhusu biblia na hujui vifungu unavyotakiwa kufundisha na unatoa tu maneno kinywani mwako na kama ulikula kiapo kwa hao binadamu wanaokufundisha. neno la mungu linasema ni ”heri kumtii MUNGU kuliko mwanadamu”ubalikiwe

 20. Maana ya somo ni kufundishwa kile usichokielewa vinzuri, usipoelewa tena uliza pale usipoelewa vinzuri. Muulize mwl. Usijumuishe. Kaa vinzuri na Mungu wako atakufunulia. Na hilo somo soma zaidi ya mara tatu, roho mtakatifu atakufunulia. Sikutoa kwa watu.

 21. Bwana Yesu asifiwe! Ubarikiwe unaefuatilia kwa lengo la kujifunza. Baadhi ya vifungu nilivyoacha wazi kuhusu uwezo na huruma ya Mungu hushuka hata kuzimu 1sam.2:6,hek.16:13,tob.13:2 samahani kwa niliyemkwanza kwa nukuu za Tobit. Acha soma hivyo vingine.

 22. Bwana Yesu asifiwe. Hata mimi sijaelewa naomba ndugu Jeff urudi utueleweshe. Naendelea kujifunza.

 23. Msingi wake anaotaka kujengea fundisho lake toka mwanzo umeshapotoka, hata ukimsubiri amalize fundisho lake, atakuwa amejenga kitu kwenye msingi mbovu, nimekwishauona msingi wake toka mwanzo, ni msingi ambao haujakaa katika neno la Mungu, sijui huo ukuta anaotaka kupandisha utakuwaje?

 24. Watakatifu wa Bwana,

  Niliposoma fundisho hili nilivuta subira ili mtoa mada amalizie kile ambacho amesema atakifundisha juu ya kufa katika neema.

  Lakini ukweli ni kwamba mtoa mada amefundisha kutoka kwenye mapokeo ya dhehebu lake na wala sio kutoka kwenye neno la Mungu lisiloghoshiwa. Mafundisho kama haya ni hatari sana kwa wale ambao bado wachanga kiroho maana hayana kitu chochote cha kuwafanya wakue zaidi ya kuwadumaza.

  Halafu inashangaza sana mtoa mada analiita Kanisa Katoliki la Mitume, mimi sijawahi kulisikia kanisa hili labda ni dhehebu lake jipya na ndio sababu analeta mafundisho mapya ambayo si ya kibiblia. Nina imani hata wakatoliki waliosoma mada hii wanamshangaa mtoa mada kwa kuliita kanisa lao ‘Kanisa Katoliki la Mitume’.

  Hebu ngoja tumsubiri atueleze, yaani amalizie kile ambacho anataka kukifundisha juu ya kufa katika neema maana yake nini na mtu anapokufa katika neema inakuwaje na anayekufa nje ya neema anakuwaje. Hapo ndipo mimi nitakapokuwa na maswali lukuki.

  Barikiweni ninyi nyote wenye kuyachunguza maandiko ya Mungu kama walivyofanya Waberoya!

 25. Hapa hata me ainiingii akili.~me nina swali~Ivi ni nani anaejua huyu ni mtu ni mwema na mdhambi??

 26. Kwa kweli Mr jeff hueleweki, na hatujui unamfundisha nani akubaliane na mafundisho manyonge kama haya. Ibada ni kitu muhimu sana na endapo utamshirikisha Mungu na wafu umepotea. Cha muhimu fahamu ya kuwa mtu akishakufa tunapaswa kumzika inavyostahili na sio kumwombea marehemu sala yoyote kwa maana haitamsaidia marehemu chochote wala wewe unayemwombea marehemu hutapata chochote zaidi ya kujiunganisha na wafu.

  Kama wewe ni msomi mzuri wa historia ya biblia imekuwaje ukanukuu kitabu cha tobiti ambacho kimsingi hakipaswi kuwa ni neno la Mungu. Biblia ina vitabu 66 tu, hivyo vitabu vilivyoongezwa na wakatoliki havikubaliki katika canon kwani mafundisho yake yanapingana na neno halisi la Mungu. Kutokana na kunukuu kitabu hicho inadhihirisha wewe ni mkereketwa wa dhehebu na sio mwanafunzi wa kweli wa Bwana Yesu.

  Soma Gal 1:6-10 utaona jinsi Mtume Paulo anavyoonya mtu akiwahubiri injili ambayo sio yenyewe mtu huyo na alaaniwe. Kuwa makini sana usije ukajikuta chini ya laana kwa kuhalalisha mafundisho ambayo hayana msingi katika neno. Ibana ya wafu ni chukizo mbele za Mungu na kama unaona yafaa basi hapa sio mahali pake pa kufundishia. Mungu si Mungu wa wafu bali wa waliohai. Barikiwa.

 27. Ujumbe huu mie ndo kabisaaaa sijaupata. Yaani sijauelewa una mktadha gani. Kuombea wafu? Unawaombea waende wapi? Wao walishakufa na miili yao ilikwishaoza. Unaombea nini sasa?

  Kaka Jeff, naona unachanganya sana hoja. Hoja zako hazina mpangilio thabiti. Mtririko wake hauko sawa. Unaenda mbele, mara unarudi nyuma, mara unaenda kulia mara kushoto. Kufa katika neema ndio nini? Kufa katika hali ya utakatifu ndio vipi? Ni maandiko yapi yameeleza au kusisitiza kuwaombea waliokufa badala ya kuombea ambao hawajafa ili wasife katika dhambi? Maana maandiko yasema, Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa…..” Aidha, maandiko yasema Mungu hapendi mwenye dhambi hata mmoja afe bali wote wafikie toba. Na mtu afapo tu kifuatacho ni hukumu kulingana na mtu alivyoishi duniani. Wewe hayo mahubiri umeyapata wapi?

  Naomba urudi tena darasani au kwa paroko wako au kwa Askofu wako au chuo cha Biblia ukajifunze upya hizo nadharia zako kuhusu wafu. Mimi naona hujaeleweka au hujasoma maandiko na kama umeyasoma hujayaelewa vyema.

 28. Kwa ufupi sijakuelewa,pia inaonekana hujui unacho jaribu kufundisha,pia nahisi wewe umeandaliwa somo ukapewa na bila kulichunguza ukaamua kuliweka hapa bila kulichunguza.

 29. tehe tehe tehe tehe tehe!! duuuu! hii nayo mpya hii mi sijawahi kuisikia hata kidogo ndio naisikia leo eti kuna kufa katika neema na kufa kusiko kwa neema. Naona pia na kitabu kimya kimewekwa hapo kinachosapoti kinaitwa Tobit. pia naona furaha kusikia kuwa maria ali sema tangu sasa mataifa wataniita mbarikiwa na hakusema tangu sasa wataniita mtakatifu kama ambavyo wengi wanakazana na kumwomba kabisa eti awaombee.

 30. Ndugu yangu nimejaribu kusoma somo lako, ninaona mikanganyiko mingi sana, “Kanisa Takatifu Katoriki la Mitume linawaombea wapendwa wao waliokufa katika hali ya Neema na wala kanisa halifundishi watu wafe katika hali ya neema bali wafe wakiwa watakatifu” kabla hajaendelea kufafanua hii sehemu niliyonukuu, tayari kitu chenyewe kina hitilafu kubwa tu hata kabla haujaanza kufafanua, na hata ukianza kufafanua utajenga juu ya makosa kwasababu msingi wako tayari utaotaka kujengea sio sahihi, nasubiri ufafanuzi wake wa kufa katika neema na kufa katika utakatifu ” Biblia inasema katika ufunuo heri wafu wafao katika kristo au wakiwa ndani ya kristo” naona unataka kutoka nje ya hiyo mistari, Je kuna utakatifu au neema ambayo ipo nje ya Yesu? .

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s