Mfano wetu ni Yesu aliyeshinda………Tusijitetee kwa mifano ya watumishi wa agano la kale walioshindwa!!

Hivi kwa nini watumishi wengi wakianguka katika dhambi ‘ hasa ya uzinzi’ wanajitetea/kutetewa kwa mifano ya watumishi wakubwa walioanguka katika agano la kale kama akina Daudi? Hivi mfano wetu ni Daudi au Yesu…….Kwa nini tusijifananishe na watumishi wakubwa wa agano jipya kama akina Paulo, Petro, Stefano ambao hawakuanguka katika uzinzi?

Nadhani si sahihi kabisa…Ukianguka katika uzinzi au dhambi yoyote, hatupaswi kujitetea bali ni kujinyenyekeza na kutubu mbele za Mungu, haijalishi uwe mtumishi wa madhabauni au mshirika. KUJITETEA NDIKO KUNAKOTUSABABISHIA WENGI  KUWA KUENDELEA WATUMWA WA DHAMBI zile zile kila siku.
Waebrania 4;15  ‘Yeye mwenyewe alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo, lakini Yeye hakutenda dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya saidia wakati wa mahitaji‘.
 Tito 2-11 ‘Kwa maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa. Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu wa sasa
–Dada Imani
Advertisements

11 thoughts on “Mfano wetu ni Yesu aliyeshinda………Tusijitetee kwa mifano ya watumishi wa agano la kale walioshindwa!!

 1. Amina dada Janeth John,

  Tusonge mbele Yesu awe mfano wetu pamoja na wale wanaotembea katika mifano mizuri. Tusipende kutumia sana watu kuwa mifano yetu maana ikitokea bahati mbaya kateleza basi watu wanakata tamaa wanasahau kuwa wao ni binadamu tu. Cha msingi tusikate tamaa tunapoteleza, tutubu mara moja kwa Mungu na damu ya Yesu itatuosha. Kila siku tunakua katika imani na ushindi wa dhambi.

  Barikiwa

 2. Amina da Imani. tusonge mbele tena wengi wanapenda kujitetea kwa mfano wa Daudi.

 3. Amina wapendwa,

  Tukaze mwendo, haijalishi mara gapi tunaanguka lazima tuuendee msalaba na kutubu kisha tuoshwe na damu ya Yesu…Kujitetea hakutatusaidia. Dhambi zote wapendwa, ni kweli si uzinzi tu.

  Tupo pamoja

 4. Hii fact nimeipenda.

  Si sawa kujificha kwenye makosa ya waliotangulia. Makosa yao yanatusaidia tu kujua kuwa tunaweza kusamehewa tukitubu.

  Tena ambao husema mbona fulani alifanya hivi na Mungu akaendelea kumtumia, akisahau kuwa kutumiwa na Mungu si lazima uwe mtakatifu,bali ni vile ulivyotayari.

  Barikiweni

 5. Ni kweli dada Imani unachokisema/kutufundisha. Ni vizuri tukajifunza kwa waliofanikiwa na sio kwa walioshindwa. Barikiwa sana!!

 6. Ndugu, wote wanaotenda dhambi na kujitetea si watumishi wa kweli. Hawa watu hawawezi hata kujilinganisha na Mfalme Daudi. Daudi alikuwa Mtumishi wa Mungu wa kweli, tena mtu baada ya moyo wa Mungu. Daudi alitubu dhambi yake tena kwa machozi na kujutia mbele za Mungu. Daudi aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi yake. Sasa hawa watumishi wa siku hizi wanajitia moyo wenyewe katika dhambi zao na hawataki kukubali adhabu kutokana na dhambi zao. There’s a lot of false spirituality in the Church.

 7. Ni kweli kabisa uyasemayo
  Mfano wetu mkuu ni YESU KRISTO.
  Lakini haimaanishi kuwa tusilinganishwe nao katika kabisa la hasha.Bali tuna watumishi wa kuwaiga kwa kazi yao nzuri mbele za Mungu,kwa mfano hatuwezi tukaacha kujilinganisha na Ibrahimu baba wa IMANI,Hatuwezi kuacha kumpenda na kumtaja Ayubu aliyekuwa mnyenyekevu na mkamilifu mbele za Mungu.

  Suala la kuingia Mbinguni ni jambo la mtu binafsi.Suala la kujilinganisha watumishi wa kale linaweza kukuinua au kukuangusha KIROHO,halafu ukapata au ukakosa Mbingu mpya.Ndiyo maana YESU hakukosea kusema “TAngu siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa ufalme wa Mungu wapatikana kwa nguvu.nao wenye nguvu ndio wautekao”
  Hivyo suala la mtumishi kuanguka katika DHAMBI mfano ya UZINZI, halafu akasema na kujitia moyo kuwa “hata Daudi mwenyewe alianguka,sembuse mimi”.HIYO NI KAULI MBAYA SANA.Suala linalotakiwa hapa ni wewe kusimama kipekee ukimtumaini YESU aliyeanzisha kazi njema moyoni mwako ili akutangulie…..MAANDIKO Yanasema “Iweni na ujasiri katika hilo,kwa kuwa yeye aliyeanzisha kazi njema mioyoni mwenu ataitimiliza hata ije siku ya Kristo YESU” (Filp 1:6)
  “…………………..maana pasipo mimi ninyi hamuwezi jambo lolote” (Yoh 15″5b).
  Ushauri wangu ni kwamba tujifunze kwa watumishi waliopita,walifanya nini yaliyompendeza Mungu na sio walimuasi Mungu vipi?. Bibli yenyewe inaweka wazi kuwa “Wapenzi tusiige ubaya,bali WEMA”
  Kama hilo halitoshi,Biblia inasema “Anayejidhania amesimama na aangalie asianguke”
  Mwamini Yesu daima na kuwa kielelezo chako.

  AMANI YA YESU IWE NANYI

  Elisante Daniel

 8. Ameen,ni kweli tusijitetee na hao walioshindwa,tumwanglie yesu tu. AMEEN.IMETULIA HIYO DADA WA IMANI.

 9. Amen, Dada Imani, asante kwa ujumbe wako mzuri, lakini naomba kusisitiza au kuiongeza kuwa , sio uzinzi tu bali kila uovu kwa kuwa Mungu hapendezwi na maovu,

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s