Moyo wako unaendeleaje?


Tunafikiri kwamba mioyo yetu ni sehemu ya kutunza hisia zetu. Kuna wengine wanasema “sikiliza moyo wako” fuata moyo wako”. Lakini ni zaidi ya hayo! ni mzizi wa matamanio yetu, haja zetu, nia zetu, makusudio yetu, mawazo yetu. Ndiyo maana Mungu anasema “Linda sana moyo wako kuliko yote ulindayo….maana ndiko zitokako chemchem za uzima!!”

Kila jambo huanzia moyoni, ndipo baadae tunaona matokeo kwa nje katika mwili, ni kama mfano wa kuweka mafuta yasiyofaa kwenye gari lako, gari itaenda vibaya pengine kuharibika kabisa.

Yesu alisema katika Luka 6:45 “Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yaujazayo moyo wake.

 Kilicho ndani yako kinakutambulisha kwa sababu ya unachokisema na kufanya kama Wagalatia 5:19-21 ilivyoandikwa. Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano.

Sasa nakuuliza leo, Mawazo gani unayowekeza  moyoni mwako? majibu ya maswali haya inategemea umejaza nini moyoni mwako!

Heri wenye moyo safi maana hao watamuona Bwana. Mathayo 5:8

Barikiwa.

Advertisements

4 thoughts on “Moyo wako unaendeleaje?

  1. Eee moyo wangu! moyo wangu! moyo wangu! Yesu naomba unisaidie mooyo wangu uwe wa kukupendeza wewe tu!
    Amen!!!

  2. Amen. Ee moyo wangu husinipeleke kwenye uhasi maana hata Neno linasema “Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo………..!

  3. Kuna sehemu pameandikwa moyo ni mdanganyifu. Mungu nisaidie kuwaza yaliyo mema.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s