Mpinga Kristo ni nani?

 • Mpinga Kristo ni nani?

 • Sifa za Mpinga Kristoni zipi?
 • Ni kwa namna gani tukio la Mpinga Kristo linahusiana na Marejeo ya Pili ya Kristo.

Michael J. N. Siyi

Advertisements

24 thoughts on “Mpinga Kristo ni nani?

 1. KUKAA KATIKA HEKALU NA KUJIFANYA MUNGU

  2 WATHESALONIKE 2:3
  “Akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uaharibifu;4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu,akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”

  HEKALU GANI MPINGA KRISTO ANAKAA?

  Hekalu la Mungu likoje?

  1 WAKORINTHO 3:16:
  “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”

  1 WAKORINTHO 3:17
  “Kama mtu akiliharibu hekalu la mungu, Mungu atamharibu mtu huyo.kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”

  1 WAKORINTHO 6:19
  “au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu” wala ninyi si mali yenu wenyewe;”

  YESU ALISEMA HEKALU LA KALE LILILOJENGWA NA MIKONO YA BINADAMU LIMEACHWA UKIWA.

  Mathayo 23:38
  “Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa”
  jiulize uhalisia wa kiroho wa mpinga Kristo kukaa ndani ya hekalu na kujifanya ndiye Mungu ni upi.

  NANI ANASIMAMA BADALA YA YESU KATIKA HEKALU
  1. si sahihi kufukiza uvumba katika makanisa yetu sasa maana kufanya hivyo ni kukana Yesu amekuja katika miili yetu.

  2. si sahihi kusema una uwezo wa kumuondolea dhambi mtu wakati ni Mungu tu anaeondolea mtu dhambi,

  3.si sahihi kuwa na mahali patakatifu pa patakatifu katika makanisa yetu maana hatuna hekalu duniani la upatanisho.

  4. si sahihi kuwa na mkate wa wonyesho ndani ya makanisa Yetu japo tunamega mkate,maana mikate ya wonyesho hukaa katika hekalu,ndio neno la Mungu mioyoni mwetu

  5.Si sahihi kuwa na kinara cha taa kinachowaka muda wote ndani ya makanisa maana sisi ndio hekalu na lile la mbinguni.

  Afanyaye huduma ya Yesu kuondolea watu dhambi na kujifanya kuhani, akiendeleza huduma za hekalu la zamani ajihooji kama anaamini kuwa Yesu amekuja katika miili yetu,akitupatanisha ndani yetu na Baba.

  1 YOHANA 4:3
  “Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.”

  MPINGA KRISTO NI YULE ANAYEKANA KUWA YESU AJA KATIKA MWILI.
  2 YOHANA1:7
  “Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristu yuaja katika mwili. huyo ndio yule mdanganyifu na mpinga Kristo.”

 2. Ukweli mpinga kristo hatoki nje ya mfumo kristo. Maana tunaambiwa hivyo ltk MATENDO YA MITUME 20:28…NA pia mpinga kristo ni mfumo ambao unaongozwa na mtu anaesimamia mamlaka kiulimwengu 2WATHESALONIKE 2:3-8 kwa zaidi ya juwa kuna wapinga kristo twapaswa jua kuwa kuna mpinga kristo ambae BIBLIA inamtaja kama mtu.

 3. CHOMBO KIMOJAWAPO CHA MPINGA KRISTO

  THE KNIGHTS OF TEMPLARS

  BAADHI YA SIFA
  -WALIPIGANA VITA VYA MSALABA KWA KIVULI CHA DINI

  -WALICHORA RAMANI NA MPANGO MPYA WA KULIJENGA HEKALU LA SULEMANI, HUKO YERUSALEMU

  -WALIUA WAISRAELI NA WAARABU HUKO JERUSALEMU WATU 70,000/= NDANI YA SIKU TATU

  -WALITOKA NA KUNYANG’ANYA SHEMU ZA HISTORIA NA KUKABIDHI KWA KANISA LA RUMI

  -WALIKUWA HAWAOI

  -WALIKUWA NA IBADA YA USHOGA

  -SASA WANAONGOZWA CHINI YA FREEMASON BAADA YA KANISA LA RUMI KUHOFU JUU YA UTENDAJI WA MAMBO YAO WAZI WAZI..NA KUTIA HOFU WAUMINI JUU YA UHUSIANO WAO NA BIBLIA, KATIKA MIAKA YA 1000 NA KUENDELEA

  -WALIJENGA MAKANISA MAKUBWA YA KISASA TUNAYOYAONA LEO ULAYA KWA PESA NA DHAHABU WALIZOTEKA MASHARIKI YA KATI, ISRAELI NA UARABUNI

  -WALIIGA KUTOKA ISRAELI MBINU ZA UENDESHAJI WA FEDHA AMBAO KWETU NI MPYA..KUWEKA PESA SEHEMU MOJA NA KUCHULIA FEDHA MJI MWINGINE.
  NA KUANZISHA HUKO ULAYA.

  -NEMBO YAO NI MSALABA UNAOKUWA NA VICHWAMISHALE MINNE INAYOKUTANA KATIKATI, MAANA WALIKUWA WAPIGANAJI. HUTUMIWA NA MAKANISA YA LEO

  -NEMBO YAO YA KIDINI NI TAJI AMBAYO INA MSALABA KATIKATI ULIOINAMA, AMBAYO HUTUMIWA NA MAKANISA MENGI YA LEO

 4. Mpinga kristo kwa mujibu wa biblia inamaanishwa kila kikundi kinachopinga yale yanayofundishwa na biblia kua” YESU KRISTO NI MWANA WA MUNGU ALIYEKUJA KATIKA MWILI. Sasa, Safari hiyo imeanza kidogo kidogo kutoka kwenye dini za kidunia na makundi mbalimbali lakini mwisho wa yote ni kuja kutokea mamlaka kubwa duniani itakayo kana na kukataa waziwazi elimu ya injili ya Kristo.

 5. MUNGU awabariki nyote mliochangia mada hii,mliyoyasema ni kweli mtupu kwa muujibu wa maandiko,lakini mimi nadhani ya kuwa bado Biblia haijatuficha kuhusu mpinga Kristo, kwahiyo naanza kwa kuuliza hivi,Mpinga Kristo asili yake ni wapi? je ni binadamu wa namna ipi?atatokea wapi, ataanzaje kufanya kazi?atatumia jeshi lipi ili kuutesa ulimwengu?je makazi yake kwa miaka mitatu na nusu ya kwanza yatakuwa wapi na miaka mitatu na nusu ya mwisho yatakuwa wapi na ni nini hatima ya huyu mpinga kristo?

 6. Aksante sana ndugu uliyejiita Lipyanda.Nitakujibu hoja zako zote japokuwa mimi siyo mwalimu wa biblia wala siyo muinjilisti…mimi ni mkristo wa kawaida niliyeokoka na kumpenda sana mungu wa kweli YEHOVA katika biblia takatifu.Lakini nakuonya kuwa usijaribu kuchomoa vipande vipande vya mistri ya biblia ili kujenga hoja zako za uongo.Isome biblia yote kwa kusafirinayo katika nyakati zake zote ili uweze kuielewa vizuri.Sasa nitaanza kukujibu hoja zako zote katika mfumo wa hoja na namba. …(HOJA NO.1) UNASEMA ETI NIWE MAKINI: Mimi nilikuwa makini kuliko wewe ambaye umeandika kuwa mpinga kristo ni yule asiyeshika mafundisho ya bwana yesu alafu unasema sivinginevyo! …hebu nionyeshe maelezo hayo ya maana ya mpinga kristo uliyatoa wapi katika biblia? na hata kama yangekuwepo yasingeweza kabisa kuelezea vizuri maana hasa ya mpinga kristo kwa sababu wasiofuata mafundisho ya bwana yesu ni wengi sana,hata baadhi ya wakristo wenyewe wapo wasiofuata mafundisho ya bwana yesu,lakini tujiulize,je,hao wote ni wapinga kristo? na je,hiyo ndiyo maana halisi ya mpinga kristo? Jibu ni LA HASHA…Biblia inatufundisha kuwa mpinga kristo ni yule ANAYEKATAA KUWA YESU KRISTO HAJAJA KATIKA MWILI…YANI SIYE MWANA WA MUNGU,Soma(2Yohana 1:7) na hapa tunawaona waisilamu ndiyo namba moja wa kukataa hilo,sasa je, ni nani ni mpinga kristo kama si nyinyi waislamu? Istoshe bado mnakazania kuwa YESU SIYE KRISTO Kwa madai kuwa eti huyo kristo ni wa paulo,na hapo pia biblia inatuthibitishia kuwa nyinyi waislamu ndiyo haswa ni wapinga kristo…tazama na uthibitishe mwenyewe kwenye (1Yohana 2:22).Sisi wakristo lazima tufahamu kuwa mpinga kristo kwa mujibu wa biblia ni yule anayekataa kuwa YESU KRISTO NI MWANA WA MUNGU ALIYESHUKA KATIKA MWILI ILI KUTUOKOA SISI WANADAMU HAPA DUNIANI…Huu ndiyo msingi wetu sisi wakristo ambao waislamu wote duniani wamefundishwa na mungu wao Allah kuupinga kabisa kabisa msingi huu…Sasa lazima tujiulize mpinga kristo haswa ni nani? Jibu ni rahisi mno ‘ALLAH NA DINI YAKE YA UISILAMU’.Nasisi wakristo lazima tujitambue vyema kuwa udhaifu wetu wa kimadhehebu hauhusiki kabisa na mpinga kristo kwa sababu kila mtu atatoa habari zake mwenyewe siku ya mwisho na biblia ndiyo njia na msingi wa kila mtu na wala siyo mambo ya mathehebu..ni kama huyu ndugu lipyanda alivyojieleza na kujijibu mwenyewe huko juu ya hoja zake kuwa ‘KUSEMA YESU NI MWANA WA MUNGU KAFA MSALABANI NA KUFUFUKA BILA YA KUSHIKA MAFUNDISHO YAKE NI MIMI KUWA MWANA MPOTEVU….(hivyo sihusiki na yule mpinga kristo ila nitahukumiwa kwa kutoshika mafundisho ya bwana yesu)…sasa hapo umeona nikuulize kati ya mimi na wewe ni nani aliyemakini na mkweli? JIBU UNALO! (HOJA NO.2) ETI PAULO ALISHIRIKIANA NA MASHETANI KUIHUBIRI INJILI: Sijui point yako ilikuwa ni nini hapo…kuamua kumuandama mtume paulo!!..labda ungejiuliza wewe mwenyewe bwana lipyanda hivi muhamadi mtume wenu aliyekiri mwenyewe katika kuruani kwamba alichezewa na mashetani kule mapangoni na kumvuruga akili zake na huyu mtume paulo mwanasheria wa mungu aliyeihubiri vyema injili ya bwana yesu kwa ufasaha kabisa tena pasipo kujiinua yeye mwenyewe kati ya hawa ni nani atakayekuwa alihubiri habari za mashetani?…muulize hata mwanao mdogo wa mwisho hapo nyumbani kwako atakupa jibu!. (HOJA NO.3) MAMBO YA SHERIA NA MATENDO ALIYOKATAZA PAULO: Ndugu yangu,mistari uliyoinukuu aliyoandika mtume paulo na ile ya yakobo na yesu kristo haitofautiani hata kidogo!!…tatizo ni wewe mwenyewe kutokuwa makini…Biblia iko wazi kabisa inatufundisha kuwa yesu kristo ametutoa katika matendo ya SHERIA na kutuleta katika NJIA AU MATENDO YA IMANI.Sasa matendo ya sheria ni yale yaliyo katika torati ya musa waliyoyatekeleza israel katika agano la kale(mambo ya mwili) sasa haya ndiyo mtume paulo anayoyakataza kuwa hatupo tena chini ya torati ya musa bali neema ya mungu kwa mkono wa yesu kristo kuhani aliye bora zaidi.Fahamu kuwa mtume paulo hakumaanisha wakristo tuamini tu pasipo kutenda matendo mema ya sheria za mungu..LA HASHA! Yeye paulo alikuwa akiipinga ile hali ya mwanadamu kujiinua kwa matendo yake kuwa ndiyo yatakayompatia haki ya kustahili mbele za mungu kwa juhudi zake hizo paulo akifundisha kuwa YESU KRISTO NDIYE HAKI YETU PEKEE.Pia tunaona ndiyo maana paulo aliwakemea wagalatia kuhusu jambo hilohilo,soma(galatia 3:1-6) ndiyo maana mtume paulo huyohuyo usiyemuelewa wewe ndugu lipyanda na kuitafasiri injili yake vibaya….anakuacha na ujinga wako na kuungana na yakobo na yesu kristo kutufundisha hivi kuhusu kuishi kwa imani na matendo mema ya utiifu kwa ujumla katika maisha yetu ya kawaida pale alipotuambia’TENA TUSICHOKE KATIKA KUTENDA MEMA MAANA TUTAVUNA KWA WAKATI WAKE TUSIPOZIMIA ROHO,KWAHIVYO KADIRI TUPATAVYO NAFASI NA TUWATENDEE WATU WOTE MEMA NA HASA JAMAA YA WAAMINIO.Soma(galatia 6:9-10).Hapo sasa umeona kuwa ni yaleyale aliyofundisha yakobo kuwa MWILI PASIPO ROHO UMEKUFA KAMA VILE IMANI PASIPO MATENDO IMEKUFA.Soma(yakobo 2:26).Sasa ndugu lipyanda lipi la ajabu hapo kama si kutaka kupotosha watu kwa maelezo yako ya uongo? Jambo la kushangaza ni kwamba hata hivi leo waisilamu wote wanaishi chini ya sheria hii hii ya bwana yesu yani NJIA AU MATENDO YA IMANI ijapokuwa hawataki kukiri hivyo…kwa sababu kama ni kweli nyie mko chini ya sheria za mungu mbona hatuwaoni mkizitekeleza majumbani mwenu? Inamaana wakina Fatuma na Zakia hawazini mkawapiga mawe ili wafe? Inamaana wakina Juma na Bakari hawaibi mkawakata viganja vya mikono?…kwa taarifa yako bwana lipyanda hayo yote yako chini ya watu wanaozifuata sheria zile za mungu aliyemtakatifu mno! Na kama hamfanyi hivyo basi wote mko chini ya laana ya mungu mkisubiri hukumu yake,ili uamini haya kasome (galatia 3:9-14) (kumbuk 27:26)…njoo kwa yesu ndugu ujinusuru na mungu aliyemtakatifu mno katika sheria zake.Tena nakujibu swali lako kuwa aya zote hizo za paulo,yesu na yakobo hazipingani na zinafaa kwa mafundisho. (HOJA NO.4) MANABII WA ISRAEL WA UONGO: Ndugu umenukuu (yeremia 23:14-16) ukitaka kutuimanisha kuwa biblia imeandikwa na manabibi wa uongo!! Hali hiyo ndiyo inayozidi kunihakikishia kuwa nyinyi waislamu ni WAPINGAJI na hayo ndiyo mungu wenu Allah aliyowafundisheni…Ukweli ni kwamba manabii wote wa uongo wa enzi zile hawakupata nafasi ya kuandikwa katika biblia takatifu neno la kweli la mungu.YEHOVA mungu aliahidi kuwa manabii wote wa uongo na wanaotabiri ndoto za ubatili hawatapata nafasi ya kuwemo katika masimulizi ya biblia takatifu, soma(ezekiel 13:9).Pia Mungu alisisitiza kuwa nabii wa kweli lazima anapotabiri jambo litokee ukweli,soma(kumbuk torati 18:20-22)…ndiyo maana utabiri wa wakina yeremi,musa,ezekieli,Isaya na wale wote waliomo kwenye biblia unatimia kweli.Manabii wote hawa katika biblia ndiyo yale mabaki machache aliyo yaandaa Mungu ili kulitunza neno lake ili ulimwengu usiangamizwe kama sodoma na gomola kama ulivyo nukuku kwenye maelezo yako mwenyewe huko juu.kwa uthibitisho wa hoja yangu hii,nenda kasome (isaya 1:9).TAHADHARI: Usijaribu kuchanganya manabii wa kweli walioandika biblia neno la mungu na wale wa uongo kama wakina MUHAMAD NA WENGINEO WALIOTENGWA NA MUNGU KATIKA NENO LAKE WAKIJIFANYA NI MANABII WA ULIMWENGU WOTE WAKATI HATA UWEZO WA KUONA NA KUTABIRI MAMBO YA KWELI YA MBELENI WALIKUWA HAWANA!!.Pia usijaribu kupotosha au kugeuza ukweli wa neno la mungu tofauti na vile mungu mwenyewe alivyolikusudia kwa sababu UTAPATA LAANA MBAYA SANA SANA MAISHANI MWAKO.Ndugu yangu lipyanda mimi nakupenda na mungu pia anakupenda na anaona jinsi unavyopata tabu kumtafuta..sasa basi NJOO KWA YESU BWANA WA AMANI UTAPATA AMANI YA KWELI YA ROHONI.Biblia yetu takatifu iwazi kabisa yatuambia:’MAJANI YAKAUKA,UA LANYAUKA BALI NENO LA MUNGU WETU LITASIMAMA MILELE.Soma(Isaya 40:8). (HOJA NO.5) SALA YA(HABAKUKI 3:1-6) Je,unajaribu tena kutumaanisha kuwa ile sala ya habakuki inamzungumzia na kumtabiri mtume wenu muhamad? Je,mtume muhamadi ni mungu kama ile sala inavyotangaza? Kwanini asiwe yesu kristo aliye keti ubavuni au mkono wa kuume wa mungu akiitwa nuru ya ulimwengu? Je,muhamadi alikuwa MTAKATIFU?Kwanini asiwe yesu kristo aliyekuwa MTAKATIFU ASIYETENDA DHAMBI? Mimi sijui hayo nakuachia mwenyewe uyatafakari lakini kama unataka kufahamu aliyokuwa anazungumzia habakuki kasome zaidi kwa muda wako kwenye maandiko yafuatayo ambapo ukiyatafakari vyema utapata majibu:(kutoka 23:31) (kumbuk 32:8)(hesabu 21:24-34).Pia ndugu yangu lipyanda lazima ufahamu kuwa malaika wa mungu wa kweli HAWABANI,HAWAKABI,HAWAMINYI WALA KUWATAABISHA WATAKATIFU WA MUNGU Bali hupeleka ujumbe wa mungu kwa hali ya unyenyekevu na upendo wa hali ya juu kwa wanadamu kwa kuwa mungu mwenyewe ni UPENDO.Hutanguliza maneno mazuri ya amani na kuondoa hofu kwa muhusika,soma(luka 1:30-32)(mathayo 1:20).Ndugu lipyanda mimi naamini kuwa hili la malaika wema tu ni somo tosha ambalo pia waislamu mnatakiwa mfundishwe na kufahamishwa kuwa mlipotezwa kwenye mashetani kabisa!.Hebu fikiria ile hali iliyompata mhamadi ya kupandwa na mahoma mwili mzima hivi wewe kwa akilizako timamu inaingia akilini kuwa mungu mwenye upendo wa kweli amtokee mwanaadamu aliyemuumba mwenyewe kwa hali za ajabu na kufedhehesha namna ile? Halafu kwanini muhamadi mwenyewe alikiri kuwa yale yalikuwa ni mashetani?JIBU UNALO!!. (HOJA NO.6) KUHUSU HADITHI NA MAANA YAKE: MImi nafahamu kuwa ufafanuzi wako wa maana ya hadithi ni sahihi…lakini nilichotaka kumaanisha mimi katika ufafanuzi ule ni maana halisi ya hadithi za mhamad mtume wenu tena kipenzi chenu ambaye alianza na kuwashawishi matajiri wenye uwezo waoe wake wengi kama yeye mwenyewe alafu alipogundua kuwa kumbe kuna kufa akawatoa hofu kwa kuwaandikia kuwa mbinguni watapewa mambo hayo hayo ya mabinti wazuri,ulevi’nk…mambo ambayo mungu wetu YEHOVA ametukataza kabisa akiyaita kuwa ni mambo ya ulimwengu huu muovu wa ibilisi…hebu jiulize mwenyewe yale mambo machafu aliyoyakataza mungu aliye safi na mtakatifu tunafundishwa na mtume muhamad kuwa eti tutapewa huko mbinguni na mungu yuleyule aliyeyakataa hapa duniani hivi inaingia akilini?JIBU UNALO. (HOJA NO.6)ETI MUNGU KAUMBA MAJINI NA WATU ILI WAMUABUDU: Ndugu elimu hiyo ni kwa mujibu wa quruani siyo biblia kitabu cha kweli cha mungu.Biblia inatufundisha kuwa YEHOVA MUNGU aliumba malaika wema na mwanadamu mkamilifu ili wamuabudu.Maanguko ya mwanadamu kumuasi mungu na kutotii ndiyo yalimfanya kuwa MWANA MPOTEVU.Na maanguko ya malaika kujiinua mno mbele za mungu na kutaka kupokea ibada ya wanadamu iliyomstahili mungu pekee ndiko kuliko mletea laana ya mungu ya milele na kuitwa SHETANI akiwa na jeshi lake kubwa hapa duniani linaloitwa majini na roho zote chafu wakitokea huko mbinguni walipo fukuzwa.Soma(ufunuo 12:7-9).Quruani itawapoteza mabilioni ya ndugu zetu wanaojivunia dini yao ya uisilamu pasipo kuichunguza kwa kina chanzo chake na historia yake ya kweli.Jambo hili linanisikitisha mno lakini mchango wangu huu wa mawazo kwao natumai ni msaada ulio bora sana kwao kujitambua vyema.Quruani imewasilimisha majini kwanza huku ikijitahidi kuwavuta na wanadamu nao washiriki haswa sisi wakristo jambo ambalo halitawezekana hata kidogo!!.Hata mungu wetu wa kweli YEHOVA aliyajumuisha majini,mapepo na roho zote chafu za shetani kuwa ni kitu kimoja katika mji ule muovu wa babel,kasome (Isaya 13:21-22) na kuahidi kuja kuyateketeza majeshi yote hayo ya shetani siku ya mwisho pamoja na mkuu wao shetani,Soma(ufunuo 18:1-3).Inatisha na kusikitisha kweli kweli-ndugu zetu waislamu njooni kwa yesu huko mlipo ni kwake ibilisi lile joka la zamani!!. (HOJA YA MWISHO) ETI BIBLIA IMEANDIKA KUWA UISLAMU UMELETA SHERIA: Hebu nionyeshe ni wapi katika biblia ulipopata uongo wako huo!! Zionyeshe hizo aya tuzichambue tuone mimi na wewe ni nani hayupo makini na ni muongo…kwa hili nitakusubiri……….. Na hoja yako ya kuwa kwanini sisi wakristo hatuelewani wakati tunaongozwa na roho wa mungu ni kwamba haya ni mambo ya kawaida kwa mwanaadamu kwa kuwa sisi kwa asili yetu siyo wakamilifu.Tazama(mhubiri 7:20).Hata manabii wenyewe na mitume walitafautiana nyakati fulani.Kumbuka ayubu alimwambia mungu hivi katika kujinyenyekeza kwake mbele za mungu’ULINIONA TANGU TUMBONI MWA MAMA YANGU YA KUWA SIKUWA MKAMILIFU.Hivyo basi cha msingi sisi wakristo ni kila mmoja kwa nafasi yake ajinyenyekeze mbele za mungu kwa nafasi yake na biblia neno la mungu la kweli ndilo msingi wa kila mtu.Madhehebu na makanisa ni misingi muhimu mno tena ni alama ya yesu kristo na ndiyo mwili wake yani kanisa ni mwili wa kristo lakini ni lazima tuwemakini sisi wenyewe kwa kuyatumikia makanisa ya kweli yanayoihubiri injili ya yesu kristo na si vyenginevyo.Biblia iwazi yatufundisha hivi:WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII BALI MGEUZWE KWA KUFANYWA UPYA NIA ZENU MPATE KUJUA HAKIKA MAPENZI YA MUNGU YALIYO YA KUMPENDEZA NA UKAMILIFU.(Warumi 12:2).kwahiyo ndugu lipyanda hatuwezi kusingizia roho mtakatifu wa mungu wala kanisa fulani wala dhehebu fulani kwa kuwa biblia neno la mungu muongozo mkuu upo na kila mtu atalichukua fulushi lake mwenyewe.Namalizia kwa kusema NDUGU LIPYANDA NJOO KWA YESU,WAPAGANI WOTE NJOONI KWA YESU.WAISLAMU WOTE NJOONI KWA YESU,DUNIA YOTE IJE KWA YESU NA WAKRISTO WOTE SASA TWENDENI KWA YESU KRISTO BWANA WA AMANI YA KWELI-Kundi lote duniani lilikuwa kitu kimoja mbele za mungu lakini alichofanya ibilisi ni kututawanya.soma(isaya 53:6).Mbarikiwe.

 7. Mhina!
  Kuwa makini sana wakati wa uchangiaji wa mada yeyote ile.
  Mada inasema MPINGA KRISTO NI NANI?
  JIBU LAKE NI HILI HAPA:
  Ni yeyote yule aendae kinyume na mafundisho ya Jesus, aliyofunuliwa na mungu kwa wanadamu. Si vinginevyo!
  Mhina!
  Kusema Yesu ni mwana wa mungu, kafa msalabani, siku ya tatu akafufuka, bila ya kufuata mafundisho yake, wewe bado ni mwana mpotevu.
  Mhina!
  Mapepo wachafu/mashetani/ibilisi WANAMTABUAJE YESU?
  MARCO 1:23-25 ” 23 Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti,
  24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?
  25 Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke”
  MARCO 3:11-12 ”11 Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
  MARCO 5:2-7 ” 2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;
  3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;
  4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda.
  5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.
  6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;
  7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.
  12 Akawakataza sana, wasimdhihirishe.”
  Mhina!
  Umeona ni jinsi gani imani ya kishetani inavyofanana na ya kwako? Huoni kama Paulo kwa kulitambua hilo, ndo maana alishirikiana na shetani kuhubiri injili?
  1 TIMOTEO 1:20.
  Mhina!
  Yesu ni mwana wa mungu kama tulivyo sisi sote. Kauli hii Yesu mwenyewe kadhihirisha mbele ya wanafunzi wake ( …KWA BABA, AMBAYE NANYI PIA, NI BABA YENU, KWA MUNGU WANGU, AMBAYE NANYI PIA NI MUNGU WENU).
  Mhina!
  WAGALATIA 2:16 ”hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.”
  YAKOBO 2:8-26 ”8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.
  9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.
  10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
  11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.
  12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
  13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
  14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
  15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,
  16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
  17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
  18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
  19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
  20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
  21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
  22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
  23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
  24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
  25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
  26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa’

  AYA HIZI MBILI ZINAPINGANA. MOJA KATOA PAULO NA NYENGINE YAKOBO MDOGO WAKE YESU. SASA KAULI GANI INAFAA KWA MAFUNDISHO?
  NI NANI HAPO ANAEPINGANA NA KRISTO?
  Mhina!
  Jiulize leo hii upo pande gani?
  Sasa nakupa tahadhari na aya zifuatazo:
  MITHALI 30:5-6 ”5 Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
  6 Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.”

  YEREMIA 23:14-16 ”14 Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
  15 Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.
  16 Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha Bwana.”

  Mhina!
  Ni kweli kabisa maandiko yatwambiavyo ya kuwa Nabii MUHAMMAD(SAW) hakusoma, isipokuwa kasomeshwa na mungu kupitia malaika wake JIBRIL. pale alipoambiwa soma akasema sijui, akamshika tena kwenye mbavu akasema soma akajibu sijui na mwwisho kabisa akamshika tena ubavuni akasema soma basi akasoma.
  Maneno haya yanaendana na HABAKUKI 3:1-6 ”1 Sala ya nabii Habakuki.
  2 Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.
  3 Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
  4 Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake.
  5 Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake.
  6 Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.”

  Mhina!
  Hata yesu hakusoma, hila kasomeshwa na mungu, yaani mungu achagui nabii eti kwa sababu kasoma never!!!
  Mhina!
  Ukisikia hadith usidhani kama zile za hadith njoo uongo kolea, hadith ni simulizi wa jambo fulani mwanzo wake mpaka mwisho wake. History. Kwa hiyo, mpaka kuja kupatikana kwa qur’an leo hii, kuna mapito yake(hadith).

  Mhina!
  Mungu kaumba binadam na majini hili wamwabudu. Sasa jini mmoja akaasi, mungu akamlaani, baada ya kulaaniwa, na yeye akawashawishi binadamu na majini hili wazifuate njia zake wakatumbukie pamoja motoni. Sasa basi, katika hao majini baada ya kumfuata yule shetani kundi moja lilisikia qur’an, wakaamini wakasilimu na mungu ni mwingi wa kusamehe wakawa waislaam. Na kundi jengine ambao bado hawajaamini qur’an wapo kundi moja na binadamu wasioamini qur’ani ambao ni nyinyi. sasa tatizo liko wapi?
  Kwa hiyo basi , unapopinga uislamu wewe ni shetani kwa sababu kitabu chako kishasema.
  Uislam, umeleta sheria na hukumu, na yesu katabiri haya!
  MANDIKO YAPO WAZIWAZI NDANI YA BIBLIA YANAYOONYESHA UISLAM, WEWE BADO UNAPINGA TU.
  WE HAUSHANGAI KWA NINI MNAPINGANA WENYEWE KWA WENYEWE NA NYIE MNASEMA MNAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  KWA NINI HUYO ROHO MTAKATIFU ASIWAPITIE NYIE NYOTE MKAWA KITU KIMOJA?
  NAOMBA NIELIMISHWE!

 8. Mpinga Kristo siyo bwege kama wengi wetu tunavyodhani. Kuyajua ya kitabu cha Daniel bila ufunuo, ni kuchukua version ya Mpinga Kristo ya tafsiri ya kitabu hicho cha unabii kilichofungwa na Mungu mwenyewe!

  Roho ya Mpinga Kristo inayozungumziwa katika 1 Yohana 4:3 “Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.”
hiyo ndiyo hii roho inayooneshwa katika symbol ya “mpanda farasi mweupe katika Ufu 6:2 “Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.” Hii ndiyo roho iliyoingia kanisani na kuubadili mwelekeo wa Kanisa; hii ndiyo roho ya UNIKOLAI, iliyopewa taji, naye akatoka ali akishinda, na IKALISHINDA Kanisa, na kuusimika Ukatoliki kuwa ndilo Kanisa!!! Huyo ameendelea na kazi hiyo ya kulidanganya kanisa kwa kuwaingizia mafundisho potofu kwa werevu ule ule alioutumia kwa mama yetu Hawa. Na sasa wengi wamempokea huyo kama Kristo, wakamvisha taji!! Roho huyo ndiye aliyewapa ufunuo wa uongo wa kitabu cha Daniel kilichofungwa, na kuwajengea msingi mbovu wote waliompokea!

  Kwa hiyo Ukatoliki ndiyo Kiti cha Enzi ya roho huyo, na kupitia Ukatoliki roho huyo ameyatapakaza mafundisho yake katika makanisa yote. Ukatoliki uliposimikwa baada ya kulidhibiti Kanisa, ndipo katika kile kitambo lililotawala na kuwa ndilo Kanisa, matengezo ya kanisa yalipoanza wakati wa Luther na kuendelea, makundi hayo yalipojitenga na Katoliki, hao waliondoka na baadhi ya mafundisho ya Ukatoliki, kama UTATU MTAKATIFU, ubatizo wa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, ubatizo wa kunyunyiza maji nk. hayo ndiyo trademark ya Unikolai, na ndiyo yanayoijenga misingi ya makanisa mengi, kinyume na na mafundisho ya Mitume! Unajua maana ya NICOLAITANE? Niko= kushinda, kupindua, halafu Laity= walei; kwahiyo unikolai ni KUWASHIDA WALEI!!!

  Basi, hata kuingia katika Umoja wa Makanisa Duniani, kigezo kimojawapo muhimu ni ukiri wa Utatu!

  Kwahiyo mnapomzungumzia Mpinga Kristo, changamsheni akili, msidhani ni bwege!

 9. katika ufunuo 13:-3 inazungumzia habari ya kichwa ambacho kimetiwa jeraha la mauti. halafu pigo lake likapona na dunia nzima ikamstajabia mnyama huyo je hili ni taifa gani au $ katika ulimwengu huu?

 10. Bwana yesu asifiwe.Ni kweli swala la kumtambua mpinga kristo limegawanyika katika hali na maeneo mbalimbali lakini pamoja na hayo yote lazima tuelewe kuwa ALLAH NA DINI YAKE YA UISILAMU NDIYO KITOVU KIKUU AU KAMA NI JOKA BASI ALLAH NA UISILAMU NDIO KICHWA CHENYEWE.Kama wewe ni muisilamu halafu ukapitia hoja zangu hizi nitakazotoa basi nakuomba uelewe kuwa lengo langu sio kukashifu bali ni kueleza ukweli uliomo kwenye Biblia yetu takatifu ili iwe changamoto kwako kuyatafakari yote nitakayoandika kwa kuwa sitaionea haya injili maana ni uwezo au kipawa cha mungu kiletacho wokovu kwa wote…..NYOTA YA ALFAJIRI(LUCIFA) malaika yule alitaka awe sawa na mungu na kupokea ibada ya wanaadamu ambayo ilimstahili mungu pekee,soma(isaya 14:12-17)(ezekiel 28:15-19).Mungu alimlaani na kumtupa huku duniani pamoja na baadhi ya malaika zake waliomtii (majini) na yeye mwenyewe kuitwa IBILISI AU SHETANI.Fahamu ya kwamba neno shetani maana yake ni’ MPINGAJI’ na neno yesu maana yake ‘AOKOAE’.EMANUEL=Mungu pamoja nasi.Hebu tuichunguze biblia inasemaje kuhusu maelezo yanayofanana na nyendo na tabia za allah na wafuasi wake katika dini yao ya msikitini kama ni kweli au tunazusha tu…Tuanze na tahadhali za biblia kabla kuja kwa uisilamu na kuandikwa kwa quruani.Biblia inaonya hivi:Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi kwa kuwa wanamasikio ya utafiti,nao watajiepusha wasisikie YALIYO KWELI na kuzigeukia HADITHI ZA UNGO.(2 timotheo 4:3-4).Hapa tunashuhudia ni kweli kwa sababu allah na wafuasi wake wameleta kitabu chenye hadithi za uongo wakidai eti ni neno la mungu.hebu wewe muisilamu jiulize:hadithi maana yake ni nini?.,.(masimulizi ya uongo’KUTUNGA’)…Ndiyo maana mhamadi alitunga ndoa za wake wengi kwa sababu:hakuna maelezo ya kiimani yanayoweza kuhalalisha ndoa za wake wengi zaidi ya kuridhisha tamaa za mwili tu.kama ni mapenzi ya kweli basi hapo ni kudanganyana waziwazi..jambo hili halihitaji mjadala wala dini fulani bali huu ni ukweli kwa kuwa mapenzi hayagawanyiki na yanatabia ya wivu katika moyo wa mwanadamu,hivyo basi mungu hawezi kuruhusu hali hii tena haukua mpango wake.Hata manabii wa zamani waliozoea hali hii waliishia kutubu wote pale walipoyajua mapenzi ya mungu.Sulemani na fahari yake yote aliishia kukiri hivi:’UBATILI MTUPU UBATILI MTUPU MAMBO YOTE NI UBATILI MTU MWANADAMU ANAFAIDA GANI YA KAZI YAKE YOTE AIFANYAYO CHINI YA JUA? Soma(mhubiri 1:1-3)(mhubiri 2:1-2).Daudi nae soma(zaburi 51:3,4,5).Ibrahimu soma(mwanzo 16:5).Hawa wote walikuwa wajumbe kutufundisha ili tusirudie upumbavu ule,soma kwa makini(mithali 2:6-10).lakini cha kusikita ndugu zangu,tunamuona mtume wa waisilamu kupitia hadithi zake za uongo anayasisitiza yaleyale mabaya ili watu wasimjue mungu wa kweli na wazidi kupotea.Inawezekana ni kwakutokujua kwake maandiko au tamaazake mwenyewe maana quruani inasema MTUME HAKWENDA HATA SHULE!!.Tuyaache haya na turudi kwenye maada yetu…tazama sasa shetani alivyoitumia quruani kuwa Mpinga kristo wa wazi wazi kabisa!! Kwa sababu alijua kabisa kuwa mwana wa mungu na damu yake ya wokovu pale msalabani vingewaletea wanadamu wote neema ya mungu na kuwatoa katika utumwa wa dhambi na hukumu dhidi ya sheria au haki ya mungu,soma(zaburi 85:13).Akaona azuie njia ile ya mungu ili watu waangamie!!.Fahamu kuwa msamaha wa dhambi katika torati ni damu ya wanyama,soma(walawi 17:11) na msamaha wa dhambi katika njia ya mungu(injili)ni yesu kristo) soma(isaya 53:4-12)linganisha na (waefeso 1:7).Saa baada ya yote haya,namalizia na mpambano mkali kati ya MPINGA KRISTO(ALLAH NA KURUANI YAKE) DHIDI YA BIBILIA NENO LA KWELI LA MUNGU.Ndugu msomaji utakaesoma mpambano huhu sitanukuu moja kwa moja maandiko lakini nitakachokiandika,mashahidi mtakuwa wenyewe kuona kama ni kweli au uongo ya kuwa vitabu hivi vinambambana kiasi hicho..nami sitaandika uongo kamwe.Hebu tuanze: BIBLIA: ‘yesu kristo alisulubiwa. QURUANI: hapana hapana walimsulubisha mwandaazimu mwingine wakizani ndiye!!. BIBLIA:Yesu ni mwana wa mungu. QURUANI: ni uongo kwa kuwa mungu hana mwana wala hazai!!. BIBLIA:’tunapata msamaha wa dhambi kupitia damu ya yesu. QURUANI: sivyo kbsaa…mnyeeezi mungu ndiye akusameheni madhambi yenu pale mtakapoenda makka japo mara moja kuhiji. (kiswali chandu cha uzushi..wale masikini je?..ndiyokusema pepo ni ya matajiri tu?!!). BIBLIA:Majini wana asili ya mashetani,ni kundi au jeshi la yule muovu,msishirikiane nayo katika ibada wala kuwatolea sadaka.QURUANI: ALLAH asema:nimekuumbeni na majini ili mpate kuniabudu!! (swali la uzushi:shetani na majini yake yanaabudu na waisilamu ili yaende wapi wakati wao walisha laaniwa na wanachosubiri ni jehanam tu!!).jamani naomba niishie hapa maana nina mengi sana ya kuhoji nikijiendekeza hapa nitakesha,Pia niliona kwenye tv wakichoma makanisa na kufufua misalaba ya makaburi ya wakristo sijui ni dini ya vipi hii!!..hatawapagani na wahindi wananafuu.MBARIKIWE.

 11. marekebisho ya fungu:“HERI ASOMAYE NA WAO WAYASIKIAO MANENO YA UNABII HUU, NA KUYASHIKA YALIYOANDIKWA HUMO; KWA MAANA WAKATI U KARIBU.” Fungu hili lililonukuliwa hapo juu ni kutoka Ufunuo wa Yohaha 1:3 nasio kama ilivyotajwa hapo juu 1Yohana 1:3

 12. Tunapotaka kumjua Mpinga Kristu tujaribu kugawanya katika makundi haya;
  TUNA PASWA KUMJUA KAMA KAMA MTU YEYOTE AMPINGAYE KRISTU.
  “Watoto, ni wakati wa mwisho na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo.”
  1 Yohana 2:18
  MPINGA KRISTO NI YULE ANAYE TAKA KUSIMAMA BADALA YA MASIHI.
  “Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama kristo yupo hapa, au yuko kule,msisadiki”
  Marko 13:21
  MPINGA KRISTU NI YULE AKETIYE KATIKA HEKALU NA KUJIFANYA MUNGU.
  “Akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uaharibifu;4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu,akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”
  2 Wathesalonike 2:3
  2. MPINGA KRISTO NI YULE ANAYEKANA KUWA YESU AJA KATIKA MWILI.
  “Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristu yuaja katika mwili. Huyo ndio Yule mdanganyifu na mpinga kristo.”
  2 Yohana1:7
  MPINGA KRISTO KAMA ROHO ISIKIRI KUWA YESU HATOKANI NA MUNGU
  “Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.”
  1 Yohana 4:3
  Wachungaji wengi wamekataa kuhubiri juu ya Kitabu cha Ufunuo na Daniel ambavyo ni vitabu vitiavyo macho nuru na kufunua mwana wa kuasi (MPINGA KRISTO). Japo tunaambiwa
  “HERI ASOMAYE NA WAO WAYASIKIAO MANENO YA UNABII HUU, NA KUYASHIKA YALIYOANDIKWA HUMO; KWA MAANA WAKATI U KARIBU.” 1Yohana 1:3
  Lakini bado tuliaswa “NASI TUNA LILE NENO LA UNABII LILILO IMARA ZAIDI, AMBALO MKILIANGALIA, KAMA TAA ING’AAYO MAHALI PENYE GIZA, MWAFANYA VEMA, MPAKA KUTAKAPOPAMBAZUKA, NA NYOTA YA ASUBUHI KUZUKA MIOYONI MWENU.” 2 Petro 1:19

  “Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakataliwa mbali naye atakuwa hana kitu; NA WATU
  WA MKUU ATAKAYEKUJA WATAUANGAMIZA MJI, na patakatifu;”Daniel 9:26
  Basi tukiweza kujua Masihi alikataliwa wakati wa Utawala wa nani Dan 9:26 nani tutakuwa tumemjua Yule aongozaye Kumpinga Kristu tena yeye kwa kauli zake akijiita Mungu. (ambaye wahubiri injili ambao hawakuionea haya injili wamewahi kuhubiri juu yake na karne ya ishirini na moja tukakana unabii tukakimbilia mafundisho ya fedha )
  SOMA DANIEL 8: 13, DANIEL 9:27
  Tena manabii hawakutuhubiria juu ya unabii ule wa kweli bali wametuletea maono ya uongo wengine wameoteshwa, wawabatize watu kwa kuwamwagia maji ya ndoo. Wengine wawanyweshe watu cocacola, wengine vikombe vya sumu. (ZAIDI UFUNUO 16:13)
  MANABII KAMA WAPINGA KRISTO
  Manabii na wachungaji wamekataa kumshuhudia Yesu kutohubiri unabii Hivyo wameshirikiana na mpinga Kristo.
  “ Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii”UF.19:10
  Wala hawajaenenda kwa sheria na ushuhuda “na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na hili , bila shaka kwa hao hapana asubuhi.”Isaya 8:20
  KAMA MANABII HAWATAENDA NA USHUHUDA WA YESU, WASIPOKIRI KUWA SIRI ZOTE ZA WOKOVU ZIKO KATIKA VITABU HIVI. HAKIKA HAKUNA ASUBUHI. KWA WALE AMBAO HAWAVISOMA NA KUKUBALI TAFSIRI YAKE YA HAKIKA.
  TUTABAKI KUPANDA MELI INAYOENDESHWA NA NAHODHA MWANAMKE YULE MLEVI ANYWESHAYE MVINYO MANABII WA UONGO NAO HUNYWESHA WAUMINI WAO. HUKO VIDOLE VIKINYOOSHWA UPANDE WA PILI HUKU TUMEPANDA MELI YA MPINGA KRISTO.
  Mkutano wa Vatican II uliwasihi makanisa yote duniani kutoiita dola ya kirumi Mpinga Kristu ambayo karne na karne imetajwa kubeba sifa zote zilizotajwa awali za upinga Kristo. Mpaka leo wachungaji wetu hawahubiri juu ya hilo Baada ya mkutano huo. Na wakatupilia mbali UFUNUO NA DANIEL huku wanapoulizwa kupotosha tafsiri zake wakati Mungu anasema;
  “na ndoto hii ni ya hakika, tafsiri yake ni thabiti” Daniel 1:45
  AONGOZAYE UPINGA KRISTO HATAFUTWI NJE YA YALE MAKANISA KWA KUWA TUMEAMBIWA ATAKUWA KATIKA HEKALU LA MUNGU.
  Maswali na mahitaji
  1. Kwanini Yuda (mwana wa kuasi alimbusu Yesu) Na Ni nani ? leo hii anambusu Yesu huku akipotosha yaliyo katika biblia.
  2. Soma habari ya Augustino na watoto wa mama Mdogo na namna gani hukubali Vitabu Injili huku wakikana Yesu si Mungu wala hakufanywa mwili.
  3. Soma habari ya Mitreya roho chafu ambayo ilitokea Kenya mwaka 1978 kama Yesu na Kufanya miujiza kujifanya Yesu na kutokea duniani mara nyingi hata sasa. Na hata sasa ndiyo hutumika kwa makanisa yasiyo ya kweli na kufanya miujiza.
  “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha Yule joka, na katika cha yule mnyama, na katika kinywa cha Yule nabii wa uongo. UFUNUO 16:13
  MPINGA KRISTU NI NANI? JIBU
  1. Joka 2. Mnyama 3. Nabii wa uongo na wote wanywao mvinyo/mafundisho ya babeli katika Kikombe cha Yule mwanamke huku wakiikana kweli kwa dhamiri zao maana kuikana kweli ni kumkana Kristo Baada ya kuijua kweli (kanisa) la Ufunuo 17:4)
  1 Yohana 2:18, 2 Wathesalonike 2:3, Marko 13:21, 2 Yohana1:7, 1 Yohana 4:3
  KILIO CHANGU KWA WASOMAJI NI NENO HILI
  “NASI TUNA LILE NENO LA UNABII LILILO IMARA ZAIDI, AMBALO MKILIANGALIA, KAMA TAA ING’AAYO MAHALI PENYE GIZA, MWAFANYA VEMA, MPAKA KUTAKAPOPAMBAZUKA, NA NYOTA YA ASUBUHI KUZUKA MIOYONI MWENU.” 2 Petro 1:19
  Neno hilo ni imara sana ndio maana wale wote wasiotaka kweli hawapendi tusome na hata hawatuhubirii kweli ya vitabu hivyo maana ndiyo siri ya akili ya maarifa ya Nuru.
  “Hapa ndipo penye hekima” UF.13:18

 13. Joshua,

  Nimekubali, hebu nisaidie

  Umesea nanukuu “2 Yohana 1:7 Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.” mwisho wa kunukuu. Ni kweli maandiko ndivyo yanavysema, UONGO ni mojawapo ya sifa ya mpinga kristo, lakini vipi madai kuwa Yesu ni nafsi mojawapo (ya pili) ya Mungu, si kumpinga kristo huko? – maana andiko lisemalo Yesu ni nafsi ya pili ya Mungu halimo katika Biblia.

  Nitafurahi kupata jibu toka pia kwa yeyote, mbarikiwe sana.

 14. Dada Julie unaniuwa sana!!!!!
  unasema watoto wa mama mdogo ndio wapinga Kristo?

 15. 2 Yohana 1:7 Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.

 16. Wapendwa wana SG,

  Yanenavyo maandiko ktk 1Yohana 2:22; (nanukuu)

  “Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye MPINGA KRISTO. Yeye amkanaye Baba na Mwana”. ( mwisho wa kunukuu) maana yake nyepesi ni hii; Kila anayemkana Yesu ya kuwa SIYE KRISTO HUYO NI MPINGA KRISTO.

  Mimi nimechokoza tu mjadala kwa mstari huo, na huyo ni mpinga Kristo type 1 lakini HUENDA wapo wengi. Naomba kila mwana SG aupitie mstari huo ili umpeleke kwenye mingine mingi na kwa msaada wa RM pia tutajua yatupasayo.

  Mbarikiwe na mtiwe nguvu,

 17. NAJUA MPINGA CRISTO NI YULE AMBAYE ATA KAMATWA NA NABIHI WAUONGO NASHETANI NAKUTUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.

  ________________________________ De�: Strictly Gospel ��: egliseapeco@yahoo.fr Envoy� le : Lundi 17 septembre 2012 1h23 Objet�: [New post] Mpinga Kristo ni nani?

  Strictly Gospel posted: ” Mpinga Kristo ni nani? Sifa za Mpinga Kristoni zipi? Ni kwa namna gani tukio la Mpinga Kristo linahusiana na Marejeo ya Pili ya Kristo. –Michael J. N. Siyi”

 18. Hii ni mada nzuri sana!!! ambayo inatutaka kurudi kwenye biblia full na nafikiri tutaifurahia sana. ngoja nami nikusanye data nitakuja nazo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s