Wafahamu CRES huduma inayounganisha wakristo na waislamu!! – 2

Tayari huduma hii iko Dar es salaam. Huduma mpya inayoongozwa na kitabu kipya  kinachoitwa: RAMANI HAI TAKATIFU, ANDIKO TAKATIFU LA MUNGU LIITWALO CRES, YAANI AGANO KUU LA MUNGU KWA WANADAMU WOTE NA DUNIA.

Kama ilivyoshushwa na Mungu mwenyewe kupitia kwa Nabii Cres kwa mujibu wa kitabu hicho.

Kimsingi ujumbe uliomo ndani ya kitabu hiki unarekebisha makosa yaliyojitokeza katika Biblia na Qurani na hivyo kuyakusanya makundi hayo mawili, Wakristo na Waisilamu ili kuwaleta kuwa kundi moja wakiongozwa na Ramani Hai kama lililvyo kusudi la Mungu kwa watu wake.

Inaendelea kutoka sehemu ya kwanza…….

TOKA ZIZINI: kondoo 

470. Nalo neno hili likasikike duniani kote maana, muovu kazaa warithi na kuacha masalia nao wataka kufanya kwa unyayo wa uovu, bali kuweni macho nami nitawaonyesha yote, mkiwaona wamekuja kwenu wakataeni na kuwapuuza hakika.

471. Wekeni huruma juu ya nchi, wekeni huruma katika njia, msiwe jua kali kwa wasiyo na nywele kichwani, wala msiwe miba chini ya nyayo za wasiyovaa viatu, wala msiwe upupu mwilini mwa maungo ya mtu, mkawe mfano mwema mkiwa walimu bora na safi, ili wote wapate kujifunza kutoka kwenu.

472. Kila ajifunzaye akalitoe somo hili kwa watu wote, akaeleze kueleza maana na kuona njia safi iliyojuu ya mbingu yangu na chini katika uso wa maumbo ya dunia.

473. Ikawa mwana wa Adamu amelitoka ekalu na kuliingia zizi, naye asitambue, akawa mnyama wa kufugwa, akapelekwa malishoni achungwe na kupelekwa mtoni anywe maji na kupelekwa josho, basi amepotea, tena amejisahau kikubwa amepoteza dira na nia yake haikupokelewa kwangu kwa maana tazama, wewe si mnyama bali mwanadamu, nami nalikupa ekalu uishi wala sikukupa zizi ukawatoe wanyama na kuishi kinyama, na kwa maana hii iliyo kuu ninakutaka kwa neno hili likufanyalo kuwa mtakatifu, likurudishialo utu na ubinadamu wako, ukalitoke zizi na unyama ukaliingie ekalu safi ukawe mwanadamu hai niliye mtofautisha na mnyama, asema Mungu.

474. Tena niseme kusema kwako, ukamuona mtu akijifanya mnyama, akiishi katika mbuga kama swala muokoe dhidi ya mnyama shetani, asije akamuwinda na kumrukia amlalue na kumnywa damu yote ya shingo la mwili wake na kumuua, mpe tumaini jipya katika nuru ya Agano Kuu.

475. Wambieni hata watoto wote walijue hili, wajitenge na akili mbovu, wajitambue kuwa wao ni binadamu na makao yao ni ekaluni, nao waiona thamani yao hai juu ya vyote, waishi wakitawala na kumiliki chini ya jua na kuifanya njia juu iwafikishe mbinguni pangu wakiwa hai katika safi na bora yake kama ilivyowekwa nami iwe kwao nao wawe kwangu.

RAMANI HAITAONGOZWA…

667. Isiwe mtu akawapotosha kwa maandishi yaliyopita, yale yasemayo kale kuyaweka sasa, ikiwa wewe umeweza naye umekombolewa kutoka kale tena umeachana na awali, basi usizame tena kuitafuta hakiki iliyopita, maana wanasema tumejua jinsi ya kuanzisha dini, tena jinsi ya kutengeneza andiko, nasi twaweza bila Yahudi, bali nawambia hakika hakuna mtu mwanadamu awezaye kuanzisha dini, wala awezaye kutengeneza neno, naye aaminiye katika neno tengenezwa ni mtu bure.

668. Nawambieni ya kweli kuwa ramani haitaongozwa toka nje ya ramani yenyewe, wala haitaeleweka kwa kutumia maandishi ya waliyoandika kusema lolote juu ya neno la Yesu wala Mohamed wala Maria wala mwana wa Daudi, ya ukoo wa Yakobo si ya ukoo wa Yuda, wala ya wa Efeso si ya wakorintho, yaliandikwa kabla tena yameandikwa baada hakuna katika wao lililoandikwa nao wakati wao nayo si dhambi wala si kukosea kwa kuwa tazama zaidi ya milioni nabii na mitume wamepita walakini yaliyoandikwa yasomeke juu yao hayazidi ya mitume na manabii mia tatu, nayo yaliyopotea ni mengi kuliko yaliyoko, tena yaliyowekwa si yote ni kweli, na katika hili ninawapa si katika nyuma bali katika sasa na katika baada mwanadamu wewe uliye sasa utaishi, nayo Isto yangu itawekwa ndani yako nami nayo iwe hai kukuweka hai.

669. Kumekuwa na kutaka kujua mengi kupita mahitaji yako na dunia, mnatafuta ukweli kwa yaliyopita nanyi hamtafuti ukweli kwa yaliyopo na yajayo, mnataka kuishi ufu hadi lini ije? Maana kujiweka kwa elimu ya yaliyopita ni kuishi mfu, nikujikwamisha wewe mwenyewe nayo ni najisi, hakuna awezaye kupata ukweli wake na kweli yangu nje ya sasa na kesho, nayo leo ni mtaji pekee nanyi wekezeni katika kesho, msitembee kisogo mbele uso nyuma, mnakwenda wapi huko kusiko, huko ambako makaburi na shetani yamewasubiria kwa hamu, binadamu wewe hutaishi kwa maono na ndoto pekee, utaishi kwa kuijua historia, hutaishi kwa kujua mengi na kumiliki mengi bali kwa hili lililo kweli pekee nikupalo ndani ya ramani hii.

670. Ijapokuwa mtu katika chombo hakatazwi kuchungulia nje kupitia dirisha, walakini si kila dirisha litakuonyesha kwa mahitaji, kasi ya chombo imeamua, ukubwa wa dirisha umeamua, neno takatifu limeongoza, tena angalia kuna watu aina kwa aina wako, wale wote wayaonayo ya zamani wakayajua sasa, nao wakajiweka kwayo kwakuwa yamekuwa sasa kwao bali hii ni sasa mfu, nayo itakuweka ufu, ni heri mtu yule aamuaye kuishi katika kesho aichungulie leo akiketi kiti cha sasa na kunena sikiza katika neno la muda hivi.

671. Ole wake mtu yule mwenye papala ya moyo, ole wake mtu aliye weka njia yangu ya leo katika juzi naye akaiketi jana aiishi leo maana amenikiuka naye hatoweza, ajibidisha na kuiangaisha katika bure amenyakua tupu naye akimbia kuridhika, mtu huyu ni huruma, ni masikini katika jamii ya waliyo masikini pake pakavu hata mchuzi haukai.

UTATU

612. Yeye aliye hai ya uhai wetu atutaka upendo mpya, ule uliyo mkuu ndani yake petu ndani yetu kwa wote, yeye asema nasi kwa ramani yake hii iliyo ujio wake kwetu, yeye mwenyewe kwa roho wake kumfanya cres takatifu ametusamehe dhambi zetu na kutuokoa.

613. Amechukizwa mno na utengano miongoni mwetu, chuki na mafarakano, magomvi na uhasi, dharau yako itakuponza, tazama ulivyopotea, nawe umeyakumbatia mazoea, tena umeweka utatu wangu kwa Yesu, walakini nakwambia utatu ulikuwapo maana ni kwangu hata kabla ya kuumba chochote katika dhamira yangu kweli,ninyi sikuwapa kuijua namba ya dunia ionekanayo kuwa ni namba kumi? nayo kumi ufikikaje bila tatu?, nayo tatu si ndani ya tisa katika kumi onekana?.

614. Tena ninawambia, ninawapa kujua mkitambua, kuna watu wanadamu wameandika vitabu kwa mawazo yao, kwa upeo wao, nayo si kwa kibali changu, mkiyafuata kuyafananisha yatawachanganya, wamesema kwa manabii wangu, wamesema kwa mitume wangu, wamesema kwa malaika na wateule wangu wote hata kwa majini ya mbinguni, walakini wamesema waonavyo, ifaavyo pao, wamewakilisha fikira zao na ujuzi wao na upeo wao na mantiki zao nayo si yangu wala si kweli.

615. Yaliyo yangu hayana wazo lako wala hisia zako, wala upeo wako wala dhamira yako, bali ni yangu kama nikupavyo, nayo yako juu ya upeo wako, nami ninawambia mtu akitaka kulijua langu kwa kuitafuta mantiki hatoweza maana ni zaidi ya mazingira ya uwepo wake na ishi, nami utoa kila mnapoishiwa, ninawajaza kuwajazia upya yote yawafae, nayo si imani kwakuwa nimeweka huru mtu kuamini chochote wakati wowote, bali mimi ninawapa kweli kuitumia wakati wote, ukiwa wewe mkiwa wote katika vyote na yote, asema Mungu.

_________________________

125. Siku ya ishirini na tano ya kila mwezi wa kumi na mbili na iwe siku ya kukumbuka kuumbwa kwenu, maana kila mmoja wenu nimemuumba katika siku hiyo nikimsubirisha katika mfupa wa baba yake na mama yake, katika ule muungano utengenezao siku ya kuzaliwa kwako.

126. Nakwa maana hiyo isherekeeni ishirini na tano ya mwezi desemba ata kuliko siku ya kutua kwenu duniani, maana asiye umbwa awezi kuzaliwa, wala kuiona siku hiyo ya furaha isherehekewayo naye.

127. Nakatika hii amesimikwa Yesu mwana wa nazareti awe muwakilishi katika sura za wote na umbo kamili la mwanadamu, ambaye ndani yake na katika maana yake niwewe na nininyi nyote katika upamoja wenu kwa umoja wenu katika utatu mtakatifu wangu, mimi mungu mmoja muumba wa vyote.

MWANGWI WA SAUTI YA MUNGU

366. Tazama, wana wa dunia wote wameisikia sauti yangu iliyotua juu ya mwamba mnene msituni, bali wao wakimbizana na kelele za mwangwi wa sauti yangu, uliyotawanyika kila kona pahala pote, wadhani yakuwa ndiyo sauti yangu mimi Mungu wao, nao wainamisha vichwa chini kwa uwoga kwa ajili ya dhambi zao, wakimbilia kuanzisha madhehebu na makanisa kwa mwangwi wa sauti yangu, wainua vichwa vyao na kuyafuta magoti yao yaliyochoka wakisema, Mungu hayupo, bali Yesu, nao wanikufuru na kunikasirisha sana, wajitwalia wakala asiye kibali tena, nao wasema na kusemezana wao kwa wao katika vyeo waliyojipachika ,tufanye mambo mengine, tutafiti juu ya uwepo wetu, tujitafiti yakuwa sisi ndiyo Mungu, tujilidhishe yakuwa miungu,majini na malaika ni roho zetu,wajisemea kwa uhaba wa imani yao wakisema sayansi ndiyo jibu, wamesahau yakuwa wakitafiticho kimeumbwa nao wajiridhisha mioyo yao wakidhi dhaifu zao, hakika hiyo ni laani juu ya sayansi na tafiti kwa mtafiti mjinga, niupumbavu katika ishi.

367. Bali udhaifu wenu ni mkubwa katika imani ya ratiba mpya duniani na mbinguni, nao wachefua na kunyongonyesha, ufahamu wenu juu ya umungu umegota na kukwama katika kiza nene,hamko tayari kwa ajili ya mabadiriko matakatifu kwa wote, mwaofia jina lenu na nafasi zenu katika jamii ya mwanadamu kuliko kunitii mimi niliye Mungu mumba wa vyote, niamuruye na kuongoza, mtabaki nyuma kama kisigino mkiunusanusa unyayo kila uendako, nami mungu wenu sikuwaweka nyuma bali imani yenu iliyongumu kama chupu la taka.

368. Mmekoma katika kizazi cha nyoka nasasa mwajiingiza katika kizazi cha samaki, mwanuka shombo, mtavuliwa kwa nyavu na huku mnaona, msamaha wangu ni kwa yule asiyenijua ata azaliwe walakini si kwa wenye roho ngumu na jeuri ya madaraka, sikwa wale waugeukao mfumo wao na utawala wao duniani, sikwa wale waishiyo kwa mazoea ya usitarabu walo, wale wasiyonisikia tena, watumiao kauli yangu iliyopitsa kupinga kauli yangu hii mpya iliyojuu ya kauli yangu iliyokwisha tekelezwa.

MWISHO

Advertisements

23 thoughts on “Wafahamu CRES huduma inayounganisha wakristo na waislamu!! – 2

 1. kwa wanaotaka kujua habari za nabii Cres1 ,yeye ni mwenyeji wa Bukoba, Kata Katoma, kijiji Kashenge anamiliki nyumba ya mizimu inayomwongoza kufanya ibada, ukipinda kama unaenda kijiji Irogelo kutoka barabara inayoenda Gera kushoto nyumba ya nne kuna duka nyuma ya duka kuna nyaruju ya matambiko ya nabii, kwa hiyo wanaojiuliza kuhusu ramani takatifu kama ni mpango wa Mungu au shetani watapata majibu haraka na kwa wepesi , hawa ni manabii wa baali na ashera msisumbuke nao Nabii Eliya aliwachinja siku Ahabu sasa Yesu Kristo Mwanakondoo wa Mungu yeye ni zaidi ya Eliya na Yehu Ufunuo 22:10 – 15 yatosha Bwana atawahukumu kwa kazi zao na wenzao

 2. kwa wanaotaka kujua habari za nabii Cres1 ,yeye ni mwenyeji wa Bukoba, Kata Katoma, kijiji Kashenge anamiliki nyumba ya mizimu inayomwongoza kufanya ibada, ukipinda kama unaenda kijiji Irogelo kutoka barabara inayoenda Gera kushoto nyumba ya nne kuna duka nyuma ya duka kuna nyaruju ya matambiko ya nabii, kwa hiyo wanaojiuliza kuhusu ramani takatifu kama ni mpango wa Mungu au shetani watapata majibu haraka na kwa wepesi , hawa ni manabii wa baali na ashera msisumbuke nao Nabii Eliya aliwachinja siku Ahabu sasa Yesu Kristo Mwanakondoo wa Mungu yeye ni zaidi ya Eliya na Yehu Ufunuo 22:10 – 15 yatosha Bwana atawahukumu kwa kazi zao na wenzao

 3. Huduma yoyote, nabii na hata mtume lazima vipimwe na Neno la Mungu yaani Biblia. Kwa karne hii tunahitaji macho ya rohoni. Mungu atusaidie; AMINA

 4. Kumuelewesha mtu mzima ni kazi, maana walilishwa neno bira kutafakali, ndio maana sasa hivi watu wanabaguana hata kwa salaam,alafu wanajiita walokole huo wote ni ufahamu mdogo watu wameishi kwa mazoea kwa hiyo wanafikili na Mungu ni wamazoea, hamna mtu asiye mjua Mung, labda kama nimwendawazimu, natokea zamani mababu na mababu walimjua Mung, walimuomba Mungu kwa lugha zao na walifanikiwa chakushangaza walipo kuja wageni na mambo yao, walifundishwa ya kigeni, na kuambiwa ya kwao ni yakishenzi na walikubali kwa ujinga tu, bila kutafakali, kwa hiyo wameendelea kuwa utumwani bila wao kujua na wakishangilia kama mazuzu eti wanamjua Yesu nabiblia kuliko watu wengine, haohao wakifiwa na wazazi wao wakisha wazika wanawaita mizimu hawana heshima tena, mjue walivyo watumwa wa kiroho na mwili lakini wale wageni walio eneza ijili wao wakifa hao ni watakatifu sio mizimu, kwaufupi Ramani hai takatifu imekuja kuwatoa hawa walio utumwani na kuwaweka huru, najua ni kazi nzito kuwakomboa watu walio utumwani, wa kiroho nakimwili kuliko ukombozi mwingine wowote lakini kwa maombi na nguvu za Nabii cres wa kwanza hawa watu watakombolewa kwa hiyo ukiona mtu anatukana au kukashifu dhehebu jingine arafu anajiita mlokole ujue sio yeye ni mapepo inabidi tumwombee na kuteketeza mapepo huwezi kuwa mtoto wa Yesu arafu ukawa na lugha chafu nnavyo jua watu wenye matendo machafu ni watoto wa shetani na hao tukiwaombea wakapona wanarudi kwa Yesu au Mungu Ramani hai takatifu haipingi Biblia wala Kuruhani, ndio maana ikaitwa Ramani, kama wewe ni somi mzuli wa vitabu hivi vitakatifu na mfatiliaji mzuli wa watumishi wa Mungu utagundua kuwa kila mtu anafafanua, au kutafakali kivyake yale maneno ya vitabu vitakatifu sasa Ramani hai takatifu inatuongoza pale wanapokosea tafakali ya vitabu vitakatifu. Mmebalikiwa

 5. Hv kinacholeta shidaa hapa ni nn? Au ni ibada ya pamoja bila ubaguzi wa dini!?

 6. Fungeni kwa muda wa siku tatu na kuomba kwa Mungu wetu ambaye tupo duniani kwa mpango wake, ili awapeni maono juu ya ramani yake hai takatifu, badala ya kutafakari kwa maoni yenu binafsi ambayo pengine yana upenyo wa shetani ndani yake. kumbuka Mungu ni wa mabadiliko na aweza fanya chochote juu maumbona na viumbe vyake wakati wowote!
  Mmebarikiwa sana

 7. Huduma hii hatuitaki kabisa,kwani hiyo ni mpango ya kishetani,aliewaambia kwamba Biblia imekosewa kama sio ni manabii wa uongo

 8. Salaam,
  Dini zimekuwa siasa, tumejenga chuki kwa misingi ya dini badala ya upendo. Ubinafsi na ubaguzi wa kimadhehebu umetamaraki na kuleta machafuko duniani na kumwaga damu za wasio hatia. Ni jambo jema na la faraja kuona watu wa madhehebu mbalimbali na wasio na madhehebu wanamuinukia Mungu kwa ibada ya pamoja. Tumuahsante Mungu kwa kutuletea ramani hai takatifu ‘CRES’ INAYOTUUNGANISHA na kutuonyesha njia. Unapoenda kununua samaki huna haja ya kumjua mvuvi, maana wakati unadadisi mvuvi nani utakuta kitowewo si chako. Tusiwe na tabia ya kupinga kila kitu bila tafakari ya Mungu.
  mmebarikiwa

 9. Kama kutajwa walishatajwa, tena wale wa kweli na wale wa uongo. Tatizo Watu wanataka watajiwe majina – eti waambiwe mabinza ni nabii WA kweli au mabinza bwana tunasikia ni nabii wa uongoo! Mungu anashughurika na Roho vivyohivyo na shetani naye hushughulika na Roho. Na Tabia huanzia rohoni na matokeo ya tabia YOYOTE hudhihilishwa na vitendo, KWA maana hiyo kilichopo moyoni mwako ndicho kinacho kufanya uwe wewe! Kondoo ni Kondoo na mbwa ni mbwa na kinachowadhilisha ni TABIA zao tu. Na Kama tabia ya mbwa IMO katika matendo ya Kondoo , kinafanya Kuwa na matokeo (matunda au matendo) ya uongo.KWa maana hiyo jina la kuzaliwa ni mtu kwa maana ya mwili na tabia ya mtu ni mtu KWA maana ya rohoni. Yesu alisema mtawajua kwa MATENDO yao. Sasa ikiwa tabia zao huzijui, je marina yao utayajuaje?!

 10. Wapendwa,

  Nadhani sasa ni rahisi kujua kwamba hawa ndio manabii wa uongo. Ndio walimu wa uongo. Hawa ndio mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo. Hawa jamaa huwezi kubabaika kwa kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Majibu ni kwamba hawa ndio manabii wa uongo.

  Mara nyingi huwa tunalumbana sana. Tunalumbana kwa kujichanganya sana hasa linapokuja swala la wahubiri watoao mapepo kwa jina la Yesu. Wanenao maneno ya Mungu kwa undani na ufasaha kwa mfano tumewahi kulumbana kwa kirefu sana na akina CK Lwembe na akina Mabinza LS kuhusu mhubiri wa kinaijeria Ndg T.B Joshua. Wengi hadi sasa hawamkubali TB Joshua. Wengi hawamkubali ndg Z. Kakobe, hawamkubali mzee wa upako Antony Lusekelo, wengine hawamkubali Moses Kulola na wengineo. Huwa kwangu napata taabu kuwapinga wahubiri hawa ambao wengine wetu huwapinga kwamba siyo watumishi wa Mungu aliye hai.

  Lakini kwa swala hili la CRES, mimi sina pingamizi kabisa. Hawa nawaweka katika manabii wa uongo moja kwa moja bila hata kuchelewa wala kufanya utafiti kwani wanajibainisha waziwazi. Hakuna haja ya kusema uchunguze, uchunguze nini wakati hawaamini maandiko ya Biblia? Unachelewa kuwaweka katika makundi ya manabii wa uongo wakati hata jina la Yesu wao hawalitamki hata kidogo waombeapo wagonjwa? Wanatumia kitabu chao. Wanatumia mafundisho yaliyo na mashaka wala hayajulikani yametoka wapi? Nadhani yametoka kuzimu.

  Mara ya kwanza kusoma neno CRES ilikuwa kutoka kwa CK Lwembe wakati tunajadili mada fulani hapa kwenye blogi ya SG. Bwana CK Lwembe sikumwelewa kabisa. Kwa sasa ndo nimeanza kuelewa nini maana ya CRES. Hawa ndio manabii wa uongo. Walimu wa uongo. Mitume wa uongo. Wachungaji wa uongo na wainjilisti wa uongo.

 11. Ni ujinga mkubwa sana kufia kisimani kwa sababu ya kutokunywa maji kwa maelezo kuwa huwezi kunywa maji hayo kwa vile hayajachemshwa! Tusinge yajua hayo kama usingeenda, wewe unadhani ni kwanini MUNGU alijifanya mtu, akabeba udhaifu na kila dharau mabegani kwake? Huwezi kuzijua mbinu za Adui bila kumjua Adui mwenyewe – ingawa KUIONJA sumu huku unaijua kuwa ni sumu, ni jambo la hatali amblo watu wa kawaida watashindwa kujua kama kweli wewe huna matatizo yoyote kiakili! hata hivyo, jibu sahihi la kwa nini ulionja sumu litabaki kwako!

 12. Ninawasalimu katika jina la Yesu
  Ndugu zangu katika Kristo, mimi ni mgeni mahali hapa lakini nimetambulishwa na ndugu ambaye katika maongezi yetu nilmgusia juu ya huduma ya Cres na hicho kitabu chao kipya cha kuabudia kinachoitwa Ramani Hai Takatifu. Katika maongezi yetu akanipa website hii na kuniambia kuwa habari za hekalu hilo zimeandikwa humo. Kwa makusudi ya kuwaonya nimechukua wasaa huu kidogo ili niwaelezeni hali halisi kiibada inavyo fanyika hekaluni humo, ili ayasomaye haya ninayowaandikia yamsaidie kufanya uamuzi au kumkimbilia nduguye yeyote yule atakayekuwa amejiingiza humo kwa uzembe.

  Nilipata mwaliko toka kwa mmoja wapo wa wanacresia (wafuasi wa Cres). Alinishuhudia mambo mengi ambayo Nabii wao Cres amekuwa akiyafanya hapo hekaluni kwao, kwamba watu wanaponywa magonjwa yaliyoshindikana mahospitalini. Pia nabii Cres huwa anatoa unabii ambao huwafungua watu kwa namna ya ajabu, aliendelea kunishawishi huyu mcresia.
  Mfano, kuna mtoto mmoja wa Profesa mmoja wa UDSM alikuwa anashindwa kuandika vizuri kwa kutumia mkono wake wa kulia aliozoea kuandikia, walijaribu kumpeleka hospitali lakini hawakuweza kubaini chanzo cha shida hiyo. Lakini nabii Cres alitabiri kuwa huyo mtoto alikuwa na shida kwenye utumbo wake na wampeleke hospitali akatibiwe hilo tumbo na huo mkono wake utapona. Kweli profesa alishangaa baada ya kumpeleka hospitali na kukuta shida kwenye utumbo (yaani utumbo wake ulikuwa umefungamanafungamana), na akatibiwahuo utumbo na lile tatizo la mkono likatoweka.

  Kwa kweli niliamua kwenda kujionea mwenyewe yanayojili katika hekalu la Cres wa 1 lililoko huko Mwenge karibu na kanisa la askofu Kakobe.

  Ilikuwa siku ya alhamisi alasiri, nilikuta ibada yao imeshaanza, walikuwa kwenye kutafakali moja ya vifungu katika kitabu chao cha Ramani. Dada mmoja mchangamfu sana alikuwa akiongoza kipindi hicho kwa kuuliza uliza maswali na kila mtu alichangia vile alivyoelewa ile aya. Kila mtu kabla ya kuchangia alisimama na kusema au kusalimia lile kusanyiko kwa kusema, “Salaam wateule” na kusanyiko zima lilijibu “Salaam”, ndipo akaendelea kuchangia na alipomaliza, alimalizia kwa maneno hayohayo, “Salaam wateule” na kujibiwa, “Salaam”.
  Tafakali iliendelea kwa takribani saa moja hivi na baadae Cres mwenyewe alisimama na kuhitimisha somo lile kuwa limeeleweka vizuri na kila mchangiaji, kisha Cres akaitisha wenye shida wapite mbele kwa ajili ya maombezi, walitoka watu kadhaa waliokuwa na shida mbalimbali.

  Alianza kuwaombea mmoja mmoja, wengine walikuwa wakianguka chini baada ya mapepo kulipuka ndani yao wengine hawakuanguka.

  Lakini cha kushangaza ni kwamba sikusikia hata mara moja likitajwa jina la Yesu kama nilvyozoea kusikia katika maombezi ya wagonjwa mahala pengine, maombezi yalikuwa ni kwa jina la Mungu. Alikuwa akirudiarudia, pepo toka kwa jina la Mungu. Yaani jina Yesu halitajwi kabisa katika hekalu hilo, maombi yao yote yanafanywa kwaa jina la Mungu.

  Kitu kingine kilichonishangaza ni vile mtu alivyokuwa akiombewa apate kujazwa roho mtakatifu, watu watano au saba waliitwa kuja kumjaza Roho Mtakatifu huyo jamaa kwa kumnyooshea mikono mithili ya mpanzi anayezitupa punje za mbegu mbele yake huku wakisema jaa, jaa, jaa, mara nyingi sana mpaka nabii Cres alipoona inatosha.

  Jambo lingine nililoliona ni vile ambavyo mtu alikuwa na swali au shauri lolote alitaka kupata jibu, alichotakiwa kufanya ni kunuizia, yaani kuweka hilo swali/ shauri kichwani mwako na kwenda kwenye ramani ambayo iko madhabahuni na kuishika na kuomba ikupatie jibu, huku umeiweka mikono na kisha kuifungua. Pale itakapofunguka na ukapasoma patakuwa na jibu la swali / shauri lako. Wenyewe wanaita kunuizia. Hili ni tendo ambalo wanacresia hulifanya mara nyingi kupata majibu ya maswali yoyote waliyonayo kila baada ya ibada zao.

  Kwa ufupi siku hiyo ilikuwa ni ya ajabu sana kwangu, kwasababu nilikuwa sijawahi kuhudhuria ibada yeyote ambayo jina la Yesu lilikuwa halitajwi kabisa na Biblia haipo kabisa miongoni mwao. Ibada yao ni wao (wanacresia), nabii Cres wa1 na Ramani Hai Takatifu tu.

  Kwa kweli niliogopa sana na sidhani kama ninatamani kurudi tena nadhani nikwenda kuiuza nafsi yangu kwenye ngome ya adui anaye mfanyia Mungu wangu Yesu Kristo dhihaka ya wazi wazi kabisa.

  Naamini adui shetani ameamua kuja waziwazi kuwafanya wanadamu wamkufuru Mungu Yesu Kristo ili wasisamehewe leo wala katika ulimwengu ujao.

  Biblia inasema wazi wazi, dhambi zote wanadamu wanaweza kusamehewa isipokuwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Naamini mtego huu ni mbaya kuliko mitego yote ambayo nimewahi kuwazia.

  Ole wetu wakazi wa dunia hii maana adui ameamua kutupa ndoano ya hatari zaidi.

 13. shalom,
  hii huduma ndo nilisikia makao yake makuu yako kigamboni ? hatajwi Yesu wala muhamadi bali ni Ibrahim amabye anaaminiwa na waislam na wakristo kama baba wa imani. Yesu atusaidie jamani wakristo tuombeni na tujifunze sana neno, mambo ya kupenda miujiza yatapoteza wengi sana.

 14. Wapendwa,

  Shalom!

  Ndugu zangu, kwanza niwapongezeni nyoote mliochangia.
  Dada Beatrice, kauli uliyoitoa ni kubwa na iliyojaa ujasiri sana! Ni kweli huduma hii haitokani na Mungu. Laana uliyowapa ni sawa kabisa, hao ni wale waliolaaniwa tangia zamani na sasa wapo juu ya nchi kuithibitisha LAANA hiyo.

  Yawezekana wapendwa wengine au mlio katika huduma hiyo, ambao mliwahi labda kuuonja ukristo, mkashindwa kunielewa ninaposema huduma hiyo imelaaniwa. Lakini, mtakuwa hamjachukua wasaa kidogo katika kuyarudisha mafundisho yanayoonekana katika kitabu hicho cha Ramani na kuyaleta ktk Biblia ili kuiona maana halisi ya huduma hiyo. Huduma hii ndugu zangu, ni HUDUMA YA KUFURU! Siyo mambo ya hadithi za Abunuwasi, hapana, mambo haya yametufikia sasa hivi. Tena, hilo PEPO LA KUFURU liitwalo “Cres”, hilo linalojifananisha na Kristo bila aibu, limeibukia hapa kwetu Tanzania kutoka kuzimu, likijitanua kutokea huko Sinza! Huu ndio ule UKENGEUFU tulioelezwa kuuhusu mapema na sasa tunaushuhudia!

  Hebu yatazameni haya mafundisho, “Ikawa mwana wa Adamu amelitoka ekalu na kuliingia zizi, naye asitambue, akawa mnyama wa kufugwa, akapelekwa malishoni achungwe na kupelekwa mtoni anywe maji na kupelekwa josho, basi amepotea, tena amejisahau…” Hii ni dhihaka inayofanyiwa Biblia pale Kristo anapoitwa “Mwana-Kondoo”. Basi hayo ndio mambo ya huyo roho aliyoyaleta ili kuwaingiza watu wasio na hatia katika HATIA isiyo na msamaha, maana kwa kujiunga na huduma hiyo wao pia wanakuwa ni sehemu ya hiyo na hivyo wanayatimiza Maandiko ktk 2Petro 3:3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, …” basi ndugu zangu mmewaona hao watu wa dhihaka, LEO HII MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MBELE YA MACHO YETU! Asanteni sana SG!!!

  Angalia mistari yote iliyoorodheshwa hapa katika hii mada, hakuna hata sehemu moja inayoyazungumzia yaliyomo ndani ya Quran zaidi ya kuitaja tu! Vyote vilivyoandikwa humo katika kitabu hicho cha Ramani vyatokana na Biblia, umetumika upako wa kuzimu kuziweka kufuru hizo katika mtiririko unaovutia kusoma lakini usio na maana yoyote ile, ni upuuzi mtupu! Hebu tazama hiki anachowaahidi watu, anawauliza kama wanataka kumiliki viwanda? Wafuasi wakamjibu kwa furaha wanataka, akawaambia “mnataka viwanda, nhe? Pokea anayetaka kiwanda, pokea, haleluya! Pookea, haleluya! Usiangalie mwili wako wala usiangalie jinsia yako, pookea, pookea, …”, mbele anapoendelea na mahubiri akawachomekea kuwa Mungu atawaleta wawekezaji na hivyo wao kupata ajira viwandani!!! Unaona hiyo sadism iliyomo ndani ya Cres? Hiyo ndio kazi inayofanya roho hiyo, kuwadhihaki mpaka walioiitikia huduma hiyo maana haina jema lolote ndani yake! Angalia inavyowadhalilisha wauza mkaa: “Kwa mfano watu wanao haribu mazingira kwa kukata miti watakosa heshima kama muuza mkaa!” Jamani, kitabu kizima cha Ramani ni kufuru!!!

  Wapendwa muwe macho, SG wametimiza jukumu lao kwa kutuletea habari za ujio wa huduma hii hapa kwetu, tayari inafanya kazi, huko kuna miujiza inatendeka. Watu wanaponywa, wanaotaka viwanda ndio hao watapewa ajira badala yake, mapepo yanakemewa kwa “jina la Mungu”, na mkwara uliowekwa mbele yao ili kuwang’oa kabisa macho ya kiroho, yule pepo kwa kuogopa kukaguliwa na kisha kugundulika, basi anawaambia, “Nawambieni ya kweli kuwa ramani haitaongozwa toka nje ya ramani yenyewe, wala haitaeleweka kwa kutumia maandishi ya waliyoandika kusema lolote juu ya neno la Yesu wala Mohamed wala Maria wala mwana wa Daudi, ya ukoo wa Yakobo si ya ukoo wa Yuda, wala ya wa Efeso si ya wakorintho, …” unaona anavyowakataza wasitumie Biblia? Tena anawalewesha kwa maneno mengi yasiyo na maana ili mradi kuwapumbaza tu!

  Ninawasikitikia sana wote walionaswa katika huduma hii, maana KWA UHAKIKA WAMEPOTEA! Kitabu chao hicho “RAMANI HAI TAKATIFU, ni kweli, hiyo ni Ramani inayokupeleka KUZIMU moja kwa moja. Na“Cres”, ndiyo Nguvu au Upako wa kuzimu ulio juu ya Ramani hiyo ambayo kwayo wote watakaojiondoa katika uwepo wa Mungu na kuisogelea hiyo huduma, wataishia huko, maana huko wanatiwa alama kwa kushiriki KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU, dhambi ambayo haina msamaha!

  Basi wapendwa, kuiondoa mada hii, ni sawa na kuiondoa tahadhari na hivyo hata yule mmoja ambaye kwa kule kupita katika blogu, akakumbana na jambo hili, hivyo kwa kuyajua haya mapema anaweza kuwaponya wengi na huo udanganyifu ambao ni mauti ya moja kwa moja, uwezekano huo utakuwa haupo tena kwa njia hii, ambayo mimi na wewe tumeyajua haya na mengine mengi sana. Liacheni liwepo tulimwagie acid, lile Neno, ule Upanga! Kwanza kwa kulileta hapa limekwisha kufa!!!

  Unajua jambo likifika, huwa limefika. Hakuna wishful thinking inayoweza kuliondoa. Huu udanganyifu umetufikia tayari na kuanza kuwavuta watu, basi adui ndiye huyu hapa mlangoni. Mungu alisema atainua kiwango cha kumkabili, hakutuambia tumkimbie, au tujifiche, tukifanya hivyo, watoto wetu na waliobaki huko majumbani kwetu si wataangukiwa na adui! Mungu alituambia atainua kiwango cha kukabiliana naye, inukeni, vaeni silaha tukabiliane na udanganyifu huu kikamilifu, ifukuzeni roho ya uoga na ushawishi wake, tumponde kichwa huyo joka!

  Katika ule mjadala wa “SHETANI ALIKWISHA KUFA” kuna watu wawili habari hizi ziliwachomoa kutoka ktk kambi hiyo baada ya kuona jinsi isivyowezekana jambo hilo kutokea kama walivyoaminishwa! Mawimbi ya Neno la Mungu ni makubwa sana, lineneni hilo Neno kwa ujasiri kama dada Beatrice, watu wapate kupona!

  Hebu jiulizeni jambo hili, huyu pepo anasema hakuja kuitangua Biblia, kwa kusema hivyo, hilo linaashiria kuwa anaijua Biblia, basi ahadi yake iko wapi humo? Kristo anasema hakuja kuitangua Torati na pia kutuhakikishia anahusika na hiyo Torati, anatuonesha Maandiko yanayohusu ujio wake na mamlaka atakayokuwa nayo, lakini hili pepo limekurupuka na uongo na kuwalambisha watu kifo! Mimi naliona hili pepo ni lile lililowapagawa wale manabii 400 wa Ahabu, wakamtabiria uongo akaishia kifoni! Jichungeni wapendwa, kwa kupenda miujiza, msije mkakalishwa katika kiti cha Ahabu na pepo hilo Cres likaanza kuwatabiria mafanikio yatakayowaingiza katika katika kifo cha kiroho na kimwili, yaani MAUTI!!!

  Mbarikiwe nyooote,ninyi mlio askari wake, Bwana wa Majeshi,
  Amina!

 15. Ramania hai inaseme hivi…

  Naam,niseme nanyi,ninyi msemao mmeokoka,kuokoka si kosa ni wema mkuu,walakini ulokole ukuondoshao katika misingi ya jamii unayoishi nayo,usiyokupa elimu ya shule na kukupa muda wa kutelekeza kazi ya ajira, huo ni ulokoo,na kamwe si ulokole wala siuongofu,salaamu yako ya bwana iwe kwa wote na si kwakundi, huruma yako na matembezi yako yawe kwa wote na si kwa kundi, nyendendo zako ziwe za kuigwa na ziletazo furaha na uhai wa faraja, usiwe kikwazo cha mifumo hai iliyo bora na sahihi, usiwe kero kwa waliyonyuma bado, usiwe mdhanifu uwe mhakika daima.

  Uwezo wako uwe nuru gizani, uwe mwanga uonekanao na uonyeshao, ule umulikao bila kubagua, ulokole si kwa aliyeokoka bali ni kwa mdhambi na muovu, ni ndoana imvuayo mtu toka kina cha maji ya dhambi na uovu ikamuweka katika kina cha maji safi ya imani takatifu ya Mungu Baba na katika tendo safi limtukuzalo Mungu daima, uolokole ni mfano hai katika kilele kionekanacho na wote, mlokole ajitangazi maana aonekana ata bila kusema neno, ulokole wake waenea kama harufu ya ua la jasimini, yeye ni lulu juu ya anga, angara kuliko almasi,ndiye madini adimu yenye thamani kuu duniani,na kila amuonaye atamani kuishi naye na kuwa kama yeye ili apate kuwa kwa Mungu baba kwa matendo safi ya kumtolea mungu na kumtumikia daima.

  Mmebarikiwa sana..

 16. Binafsi sikubalini na cres maelezo yao yatolewe. inasaidia sisi kujua nini kinaendelea na kuwa makini. Tatizo la walokole ndio hilo hampendi kujua ukweli wa imani mpya na potofu na ndio wa kwanza kukimbilia kupata miujiza huko.

 17. SALAAM KATIKA JINA LA BWANA YESU KRISTO, MIMI NAUNGANA NA BEATRICE SIO KWAMBA HII HUDUMA YA CRESS INACHANGANYA KTK KUIELEWA BALI INAFANANA NA MAELEZO YANAYOISAHIHISHA BIBLIA AU KUIPA MBADALA BIBLIA. WAKATI IKO WAZI KWAMBA , BIBLIA NI KITABU AMBACHO NDIO MWANGOZO WA MAISHA YA MKRISTÓ ANAPASWA KUKIFUATA, SO ME NAONA HAYA MAELEZO YA HII HUDUMA YA CERSS MUYAONDOE KTK HII BLOG. AU LA KAMA MTAENDELEA TOA MAELEZO YA HII HUDUMA YA CRESS BASI MTAKUA MMEAMUA KUTUKWAZA SISI WENYE KIU YA KUJIFUNZA NENO LA KWELI LA MUNGU. AHSANTEN SANA MBARIKIWE SANA

 18. YESU NDIO NJIA PEKEE YA KWELI NA UZIMA..
  NYIE WAPINGA KRISTO MBONA MWATAPATAPA SANA??? MNAJITAHIDI KUBADILISHA MWONEKANO ILI WATU WAWAONE WEMA NA WASAFI KUMBE NI KIZAZI CHA LUSIFA KILICHOLAANIWA…MIMI NASEMA MKOME NA MUONDOE MAFUNDISHO YENU YA KISHETANI NA MSHINDWE KWA JINA LA YESU KUWAPOTOSHA IMANI WATU WA MUNGU.
  NIMESHASEMA TENA BIBLIA HAINA UPUNGU WOWOTE, NYIE NDIO WENYE MAPUNGUFU NA LAANA KWA KUIPOTOSHA ILE KWELI.
  YESU ATABAKI KUWA MUNGU NA JUU YA VYOTE KWA USHINDI ALIOUPATA KWA KUTUFIA MSALABANI, KWENDA KUZIMU KUMNYANG’ANYA SHETANI FUNGUO NA KISHA KUFUFUKA KWA USHINDI NA SASA YUU HAI.
  PINGENI MSIPINGE, YESU NI MSHINDI NA BIBLIA NI NENO LA MUNGU LISILOKUWA NA MAPUNGUFU YEYOTE.
  KWA KIFUPI HII HUDUMA YA CRESS HATUITAKI. IONDOENI..

 19. ile aya ya korani inayosema Mungu wenu siyo Mungu wangu na mnachokiabudu ninyi sicho ninachokiabudu mimi imefutwa pia?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s