Je manabii wa uongo wabainishwe wazi wazi?

Bwana Yesu Kristo alituonya tujihadhari na manabii wa uongo, na akawafananisha na mbwa mwitu wakali waliovaa ngozi za kondoo (Mathayo 7:15-23). Akabainisha waziwazi kuwa namna pekee ya kuwatambua ni kuyachunguza matunda yao.Mtume Petro alifafanua baadhi ya tabia za manabii wa uongo katika 2 Petro 2:1-22, kuwa ni pamoja na

1. Kuingiza kwa werevu “uzushi wa kupoteza” – manabii hawa huingiza mafundisho ya uongo kwa ustadi wa hali ya juu (mst 1);

2. Watu wengi wanaowasikiliza watafuata ufisadi wao (mst 2) – ndio maana si ajabu kukuta wafuasi wao wana tabia kama za manabii hao;

3. Watu kuitukana imani ya Kikristo kutokana na matendo maovu ya manabii hao wa uongo (mst 2);

4. Kujipatia faida binafsi kutoka kwa wafuasi wao (mst 3) – si ajabu kukuta nabii wa uongo akiwahadaa wafuasi wake na kujipatia fedha nyingi wakati wafuasi hao walio wengi wakiishi maisha ya taabu;

5. Wanapenda maisha ya anasa kupindukia (angalia mst 13);

6. Wanapenda kufanya uzinzi (angalia mst 14);

7. Hawaachi kufanya maovu yao (mst 14) – wapo ambao licha ya kuonywa kwa njia mbali mbali hawako tayari kuacha, bali wanaendelea na maovu yao na kuendelea kusimama madhabahuni kuhubiria wafuasi wao pasipo kuwa na aibu;

8. Wanahadaa “roho zisizo imara” (mst 14) – uimara unapatikana katika kulifahamu Neno la Mungu na kuishi kwalo, kinyume cha hapo utadanganyika tu;

9. Ni kama “visima visivyo na maji” (mst 17) – kama unaenda kwenye nyumba zao za ibada ukitegemea kupata Neno la uzima, imekula kwako;

10. Wanatumia tamaa za mwili pia katika kuwahadaa watu wanaowasikiliza (mst 18) – mfano kuwahadaa watu kwa kuwaahidi maisha mazuri ya utajiri nk kwa kupitia njia ambazo Mungu hajazifundisha katika Neno lake.Mahali pengine ninasoma “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.” (Warumi 16:17-18)

Biblia ya Kiingereza inasema

Now I beseech you, brethren, MARK THEM which cause divisions and offences contrary to the doctrine which ye have learned; and avoid them. For they that are such serve not our Lord Jesus Christ, but their own belly; and by good words and fair speeches deceive the hearts of the simple. (Romans 16:17-18, KJV, capital letters mine)

Tunamsoma mtume Yohana jinsi ambavyo hakumumunya maneno alipomzungumzia Diotrefe, aliyekuwa miongoni mwao, kuhusiana na vitendo vyake ili wale Wakristo alipokuwa akiwaandikia waraka wachukue tahadhari:

“Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa. Mpenzi,
usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.” (3 Yohana 1:9-11)

Manabii hawa wa uongo, pamoja na wenzao mitume wa uongo, wachungaji wa uongo na walimu wa uongo, wanapotosha watu wengi katika zama hizi tunazoishi.

Je, waendelee kuachwa kupotosha, au pale inapothibitika matendo na mafundisho yao kuwa ni ya upotovu kwa mujibu wa Maandiko Matatifu, basi watajwe wazi wazi ili yumkini wengine watasikia na kuwaepuka?

Joel Msella

22 thoughts on “Je manabii wa uongo wabainishwe wazi wazi?

 1. JE MANABII WA UONGO(MBWAMWITU) WATAJWE WAZI WAZI ILI WATEULE WAPONE??

  TUZAME NDANI YA MAANDIKO
  Hebu kwanza tutafakari maana ya ujumbe wa Yesu katika MATHAYO 13:27-30 “……..Bwana hukupanda mbegu njema(ngano) katika konde lako?Basi
  limepata wapi MAGUGU? Akawaambia adui ndiye aliyetenda hivi.Watumwa
  wakamwambia,Basi wataka twende tukakusanye? Akasema La msije mkakusanya MAGUGU na kuzing’oa NGANO pamoja nayo.Viacheni vyote
  vikue hata wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza
  MAGUGU,myafunge matita matita mkayachome,bali NGANO ikusanyeni
  ghalani mwangu”

  Mungu tunaomba utufungue fahamu zetu ili tuyaelewe haya maandiko(mathayo 22:29).Wateule wengi tumekuwa tukipotea kwa sababu ya kutoyajua maandiko kupitia uweza wa Roho Mtakatifu.Naomba hapa twende taratibu.

  Magugu ni manabii wa uongo na ngano ni wateule wa Mungu.Yesu ana maana gani anaposema inabidi wateule na manabii wa uongo wakue pamoja? Wakati tunafahamu kabisa hatuwezi kupata mavuno mazuri ya ngano kama itakua(itaota) pamoja na magugu shambani.Tena anasisitiza kwamba
  ngano na magugu vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno ndipo magugu
  yatakapo tenganishwa(kusanywa) na ngano ili yachomwe!Ni ngano ya namna gani hiyo ambayo inavumilia kusongwa na magugu mpaka wakati wa mavuno?Kwa kanuni bora za kilimo ni lazima kung’oa magugu yote ambayo yanaisonga ngano.Magugu na ngano havitakiwa kukua pamoja shambani.Swali linarudi pale pale kwanini Yesu anasema VIACHENI VYOTE
  VIKUE PAMOJA!!

  Yesu mwenyewe analijibu swali hili katika MATHAYO 7:15 “JIADHARINI na
  manabii wa uongo,watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini
  kwa ndani ni mbwamwitu wakali”.Yesu anasema TUJIADHARI na manabii wa uongo.Na katika MATHAYO 10:16, Yesu anasema tunaweza kujiadhari
  na mbwamwitu(nyoka) kwa kuijua BUSARA YAO lakini pia tuhakikishe tunakuwa na UTULIVU WA ROHO MTAKATIFU (hekima na maarifa ya Mungu) muda wote.Huu utulivu wa Yesu ni pamoja na kuwa na MACHO
  NA MASIKIO YA ROHONI.Yesu anasema sisi ni kondoo kati ya mbwamwitu.
  Vita kati ya kondoo na mbwamwitu ni mapambano kati ya Hekima,busara
  na maarifa ya wana wa Mungu na hekima,busara na maarifa ya uzao wa shetani-Ibilisi.

  Mtume Paulo katika MATENDO 20:28-31,anasema JITUNZENI NAFSI ZENU
  kwa kuwa mbwamwitu wakali tayari wamo miongoni mwenu wakisema MAPOTOVU.Paulo anasema tutazitunza nafsi zetu kwa kuepuka mafundisho(mapotovu) ya
  mbwamwitu.Tunatakiwa kuzilisha nafsi zetu Neno(mafundisho) la Yesu ili
  tusife kiroho.Na huu ndiyo unaoitwa UKOMBOZI WA NAFSI.

  ISAYA 42:18-22 inasema changamoto walio nayo wateule katika kuwatambua manabii wa uongo ni kutokuwa na MACHO na MASIKIO YA
  ROHONI!Ndiyo maana kila kukicha wanachukuliwa mateka na kufichwa kwenye magereza na mashimo.Ushauri wa nabii Isaya ni kwamba wateule
  walio na macho na masikio ya rohoni WAWARUDISHE(wawakomboe) wenzao.Isaya hajasema tupigane kwa jinsi ya kimwili ili kuwakomboa wenzetu.

  MWANZO 3:15, UFUNUO 12:7-9 na YOHANA 8:42-44 zinasema kwa sababu ya UASI na
  UDANGANYIFU wa shetani ambaye ni baba wa manabii wa uongo,ndiyo
  maana duniani kuna VITA kati ya wateule wa Mungu na manabii wa uongo.

  WAEFESO 6:12 inaeleza wazi kwamba hiyo VITA kati ya wateule wa Mungu
  na manabii wa uongo ni vita ya kiroho na siyo ya kimwili.Kwa sababu vitendea
  kazi vya manabii wa uongo ni Roho wa shetani ,neno la shetani na majeshi ya pepo wabaya wakati vitendea kazi
  cha wateule wa Mungu ni Roho Mtakatifu, Neno la Mungu aliye hai na Malaika wa nuru.KWAHIYO NI MARUFUKU KWA MTEULE KUPIGANA VITA YA KIMWILI.

  UNABII WA MUNGU KUHUSU HATIMA YA MANABII WA UONGO!
  Huu ni unabii unaoendelea kutimia ndiyo maana sasa hivi tunashuhudia jinsi
  NGOME za manabii wa uongo zinzavyoanguka kila kukicha.
  1.UFUNUO 2:20-23
  Mungu aliye hai anaendelea kumuaibisha malkia wa manabii wa uongo(malkia wa pwani) na hao manabii anao watumikisha.ANAWAPA DHIKI
  KUBWA na kuwaua watoto wao kwa mauti na wateule wanaojitambua kiroho wanakiri ya kwamba Mungu wa majeshi ndiye achunguzaye mioyo.

  2.MATHAYO 16:18-19
  Milango ya kuzimu inayotumiwa na manabii wa uongo inaendelea kushindwa na makanisa ya wateule yaliyojengwa juu ya mwamba wa Neno
  la Kristo.Wateule wanaojitambua wanazo FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI ambazo wanazitumia kufunga nguvu na kazi za manabii wa uongo katika ulimwengu wa roho na kufungulia nguvu na kazi za Yesu.

  3. 2TIMOTHEO 3:1-9
  Kasi ya manabii wa uongo inaendelea kupungua sana maana UPUMBAVU
  wao umekuwa dhahiri kwa wateule wote wanaotembea na macho saba ya
  Mungu.

  4.EZEKIELI 13:8-23,EZEKELI 33:1-10,ISAYA 42:22
  Misingi ya huduma za manabii wa uongo inaendelea KUFUNULIWA nao wanaendelea kuangamia kwa mvua ya mawe,upepo na dhoruba kutoka
  mbinguni.Wachungaji waliwaacha wateule wawe chakula cha mbwamwitu
  wanaendelea kufukuzwa kazi na Bwana anawaokoa wateule wake kwa kuwatoa vinywani mwa manabii wa uongo.
  Mungu anaendelea kuwaokoa wateule wake ambao roho zao zinawindwa
  kwa hirizi za manabii wa uongo.MKONO WA BWANA uko juu ya manabii wa
  uongo ili wasiendelee kuwashawishi na kuwashauri wateule walio wateka
  ndani ya ‘makanisa’ yao.Wateule wanaojitambua wameshaanza kumwabia
  Bwana wa majeshi AWARUDISHE wenzao waliochukuliwa mateka.

  5.1 WAFALME 18:22-40
  Mungu aliye hai anaendelea kuziharibu madhabahu za manabii wa uongo
  na kuwaua manabii wa uongo kwa pumzi ya Yesu inayoambatana na mikono ya manabii wa kweli.

  6.UFUNUO 2:14-15
  Wateule wa Mungu wanaendelea kutubu na kuzikana sanamu na mafundisho ya manabii wa uongo.

  HITIMISHO
  VITA kati ya wateule na manabii wa uongo ni vita vizuri vya imani ya Yesu!(1TIMOTHEO 6:12).Wakati manabii wa uongo wanatafuta kuua maono na hatima za wateule,Mungu anawatumia manabii wa uongo kama chachu
  ya kuwaimarisha wateule katika mapambano ili washinde na zaidi ya kushinda ndani ya upendo wa Kristo yaani hekima na maarifa ya Yesu ambayo yanawatia nguvu(WARUMI 8:31-39).Mungu hawezi kusema tunashinda na zaidi ya kushinda wakati hakuna vita.Mapambano haya yataendelea hata baada ya unyakua kwa wale watakao pita katika dhiki kuu.Jambo la kushangaza ni kwamba manabii wa uongo watamtangulia shetani katika lile ZIWA LA MOTO.Mteule USIKUBALI KUOLEWA NA FEDHA
  ILI KUVUNJA NDOA YAKO NA YESU.FEDHA ZINATAKIWA ZIYATAFUTE MAARIFA YALIYO NDANI YETU ILI ZITUTUMIKIE NA KUTUMIKA KATIKA
  KAZI YA MSALABA(1 TIMOTHEO 6:10, MITHALI 8:10-19).Wateule wanafundishwa KWELI tangu wakiwa tumboni za mama zao na mbwamwitu
  wanafundishwa UONGO na kumkufuru Roho Mtakatifu tangu wakiwa tumboni mwa mama zao!(ZABURI 58:3).Hii ni VITA kati ya watu wema na watu wabaya(MITHALI 16:4).

  KINACHOTAKIWA NI KUISHI MAISHA MATAKATIFU NA KUENDELEA
  KUPIGANA VITA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.TUKIISHI KWA MAARIFA YA YESU YANAYOPATATIKANA NDANI YA UNYENYEKEVU WA YESU AMBAYE NI NENO LA MUNGU, HAWA MANABII WA UONGO WATAENDELEA KUWA CHAKULA CHETU KAMA ILIVYO KUWA KWA YALE
  MAJITU YALIYO TAFUNWA NA AKINA YOSHUA KULE KAANANI.

  MUNGU AWABARIKI WATEULE WOTE.

 2. Kabla hamjataja wengine, mjitaje nyie kwanza, ni akina nani nyie wenye kuhukumu?

 3. Siyi, acha michezo ya kuigiza hiyo! Hivi kweli ukikaa ukatulia ukaanza kuorodhesha manabii wa uongo, hiyo orodha utaimaliza kweli?Assuming roho wa kanisani kwenu anakusaidia, najua juu ya list ataanza Papa, kwa kukisia huku chini kabisa ya list yenye urefu wa kuisoma kwa miaka miwili na zaidi, atakuwepo nabii wa mwisho aliyemtabiria Odinga urais akifuatiwa juu yake na yule aliyemtabiria Mrema, majina yao nimeyasahau kidogo, ila huko juu chini ya papa na Ribera atakuwa yule maarufu aliyewavalisha waumini wake mbawa za kushona ili waruke wakamlaki Bwana mawinguni wakati wa kuja kwake, ambapo walimsubiri hadi ndevu zikaota mvi!!! 

  Ila Siyi tuheshimiane, usinitaje mimi “nabii Lwembe” kabisa, ukitaka labda mtaje “nabii” Mkandya, maana huyu ndiye anaitabiria vibaya sabato!!!

 4. Mpendwa Siyi,

  Nionavyo mimi wewe taja tu, ili tupone! Bloger unayemhofia naye anataka kupona ninahakika.

  Uendelee kubarikiwa na Bwana Yesu Kristo.

 5. Kama bloger atakuwa tayari kuyaruhusu majina yatokee kwenye blog hii, na aseme sasa mimi nitataja baadhi ya majina ya hao manabii wa Uongo wanaowapotosha watu. Maana leo dini wameifanya kama ujasiriamali. Bloger akisema tu kuwa SIYI, wataje, mtawaona hapa baadhi yao. Nikipata fursa ya kusema mimi sikai kimya kamwe!!!!

 6. Justina,

  Tafadhali uwe wazi, mimi Binafsi sijakuelewa hata kidogo!

  Kwakifupi sana, huwezi kukiepuka kitu usichokijua au kukiona, Maana asiyekuwepo Moyoni na Machoni hayupo! Zaidi ya yote hatumwepuki shetani kwa ujuzi na akili zetu!

  Wapendwa wapo tayari kutoa Msaada kwa mafundisho, Eleweka tu unachomaanisha. Kwakupitia hii Free site, utapata Wanga wa ajabu!

 7. Tafadhali jaribu kutuma meseji kuhusu jinsi ya kuwaepuka hata mara moja kwa kila siku kwa yule ambaye muna email yake.

 8. @ Alexander Kapinga,
  Utukufu ni kwa Bwana Yesu Krsto Ndg yangu A. Kapinga – Naomba Roho mtakatifu aendelee kuwafundisha wenye nia ya kweli ya kujifunza.

 9. Edward,

  Kukaa kimya kunamaana mbili kuu nazo ni, kwanza, unanyamaza kama kinachosemwa hukijui ama jibu la swali hulijui, lakini mbili, unakaa kimya kama unakiburi!

  lakini kwa upande wa maada kama ilivyo, manabii wote wa aina zote mbili walishatajwa, kinachoendelea sasa ni kubainishwa tu wazi wazi – na kila siku wanabainika tena kila mmoja kwa jina lake!

  Tatizo, watu ‘hawazijui SURA za wahusika, kila yanapotajwa majina yao!’ Watu hawaelewi! wanagojea yatajwe majina! Mwenye kusoma majina anauliza, mbona nimewatajia majina yao sasa hivi?! Cha kushangaza, msoma mjina hashangai, yeye anakumbukumbu, hasahau kitu, anajua kuwa alisha zitambulisha sura za hao manabii wa uongo na wa ukweli hapo kabla!

  Tatizo, Watu hawajari kama cha mhimu kilikuwa kile kilichosemwa mwanzo, “zitambueni Tabia zao (ambazo ndiyo Sura zao) kwanza” ili majina yatakapotajwa usshangae. Na sasa, kumbe anataja majina! Na watu sura za wahusika hawazijui kumbe majina yakitajwa itasaidia nini? kunamshangao mkubwa ulimwenguni kote hawaji la kufanya! Kisa kimekuwa kilekile cha wayahudi, kumngoja Masiya ambaye kumbe alisha kuja wanaye! hadi anaondoka hawana habari kuwa NDIYE! maana usipoijua Sura ya mhusika, laweza kutajwa jina lake sasa hivi, na mara hiyo hiyo mhusika akapita na tena akakusalimia, nawe kwa uchangamfu ukamjibu ‘Sijambo mkubwa wangu!’ akaenda zake nawe bado usitambue kuwa yule ndiye! Kisa, humjui kwa SURA yake!

  Kumbe, waweza kuona kinachofaa katika hili tuwajue kwanza “TABIA ZAO” (yaani Sura zao za ndani).Jina hutambulisha Mtu kimwili, bali Tabia huonyesha sura ya Mtu kiroho. Maana matendo ya Mtu hutoka katika mawazo ya moyo wake, na hivyo Tabia ya mtu ndiye mtu mwenyewe! Kwa hiyo Mwili hupokea majibu toka Rohoni kwa hiyo matendo ya mtu hutegemea Tabia yake ambayo ndiyo Sura yake ya ndani, kwa maana hiyo matendo ni matokeo ya sura ya mtu wa ndani (Tabia).

  Ukisha jua hivyo, utakuwa tayari umejua SURA ya mhusika na akitajwa tu jina utakamilisha kumjua mhusika kwa ukamili. Biblia inataja kwa uzuri tabia za manabii wa uongo na wale wa kweli, tuisome na tuwe tayari kumsikiliza Roho mtakatifu ili atuainishie hilo kwa upole na uvumilivu mwingi! MAANA HOJA SI MAJINA YAO YA KIMWILI NI TABIA ZAO AMBAZO NDIZO SURA ZA MANABI HAO!

 10. Wapendwa, kama kuwataja Manabii wa Uongo mnapata kigugumizi, basi watajeni wa Kweli, halafu wanaosalia tutajua ndio hao wa Uongo!

  Muwe na UJASIRI!

 11. Mr. Milinga,

  Ni haki ya msingi kumtuhumu Mtu, lakini kuhukumu kunasimama katika utimilifu wa Sheria husika. Kwa maana hiyo, Kutuhumu ni jambo moja na Kuhukumu ni jambo jingine. Mtu anapotaja jina la Mtu fulani kwa tuhuma fulani, mtajaji hajahukumu (kuponda mawe) ila anatuhumu tu. Ni jambo la msingi na ni la haki ya kisheria Mtuhumiwa kujitetea, lakini akikaa kimya, Mahakama (mwamzi) anaamini kuwa mtuhumiwa ameikubali tuhuma ile na hapo ndipo hukumu inapopitishwa dhidi ya mtuhumiwa. Kwa maana hiyo, kutajwa jina si kupondwa mawe bali ni kutuhumiwa, kupondwa mawe kutakuja baada ya ile tuhuma kuonekana ni ya kweli!

  Kulielewa hilo kwa uzuri, turudi juu ya Yesu katika lile shitaka lililoletwa kwake juu ya yule mwanamke aliyekuwa kafumaniwa katika uzinifu. Habari hiyo ipo katika Yh.8:3-11, katika mstari wa 4, panasomeka hivi ‘wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini…..’ utaona kuwa hiyo ilikuwa tuhuma. Na ule mstari wa 5 ‘Basi katika Torati, Musa alituamru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii;…..’ Hapo ilitajwa aina ya hukumu impasayo mwanamke akipatikana na hatia kama hiyo. Katika mstari wa 10, ‘……..wako wapi washitaki wako?…..’ kwa msemo mwingine wako wapi wanaokutuhumu? (hakusema wako wapi wahukumu wako?) kwenye ule mstari wa 7, Yesu, anakubaliana na tuhuma (shitaka), lakini Yesu anaainisha sifa ya mwenyekutoa hukumu (adhabu) hiyo ya kupiga kwa mawe kwa mjibu wa ipasavyo Torati…..na hapakutokea afaaye kuhukumu! ……Yesu naye akasema hatamhukumu yule mwanamke (mstari wa11), si kwamba Yesu aliona wamemsingizia, au hawezi kumhukumu kwa vile naye ni kama wale waliomleta (wasiohaki), la hasha, bali Yesu hakuja kutoa hukumu ya kimwili! (mstari wa 15).

  Lakini cha msingi hapa si jina la huyo NABII wa uongo ili umkwepe katika mafundisho yake! Cha MSINGI ni kuzijua TABIA za manabii wa uongo, ili usijiingize humo! Maana hata wewe waweza kuwa Nabii wa uongo kama utafanya sawasawa na tabia za manabii hao, hata kama utatenda bila kujua au kuelewa! Haulazimishwi na mtu kujifunza ili uzijue tabia za manabii wauongo; bali jua tu kwamba HUTASIKILIZWA SIKU ILE KWA MAELEZO KUWA SIKUELEWA JAPO NILIAMBIWA, maana KUTOELEWA SHERIA si kinga ya kosa!

  Nimekukubalia Mr. Milinga, ASIYE NABII WA UONGO AWE WA KWANZA KUMPONDA NABII WA UONGO JIWE! Ila nakukatalia Mr. Milinga, kuwa kumtaja nabii wa uongo ni kuponda mawe!

 12. Watumishi,

  Kama kuna mtu anajua kwamba yeye ni msafi, kwa kila kitu naomba awe wa kwanza kurusha jiwe. Wewe wataje tu siyo lazima utangaze redioni, TV au magazeti, ingawa nadhani hata rafiki zetu wa SG hawatakuwa tayari kuruhusu majina yao yaende hewani kupitia blog hii. Kama bloger wa SG yuko tayari, tunamwomba amruhusu mpendwa yeyote anayejiamini kwamba orodha aliyonayo kwenye notebook yake ni ya manabii wa uongo awataje haraka.

  Kama wewe uko safi naomba uwe wa kwanza kuwarushia mawe hao manabii.

  Karibuni sana, muanze kuwataja. Nawasubiri kwa hamu.

 13. SINDAGA,

  Manabii wa uongo walishatajwa zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita, kwakuwa tabia zao zilishaainishwa vizuri katika Biblia zisome kwa makini, hiyo itakusaidia kuwajua, anzia kanisani kwako au mahali popote ulipo zioanishe tabia zao na zile zilizotajwa katika Biblia, kwakuwa watu hao utakuwa unakaa nao, wanakuhubilia ama unakula nao hivyo utakuwa unawafahamu, kama ndivyo, hakika haitakusumbua kujua majina yao. (Lakini elewa majina siyo ‘Ishu’ bali tabia zao!)

 14. me nadhani kwa kutusaidia wengine ambao ni wachanga kiroho hao manabii wa uongo mngewataja hapa sasa hivi kuliko kuzungukazunguka kwa maneno mengi. Tuwataje na tujadili kwa kina mmoja baada ya mwingine na katika hili kwa hakika tutapona.

 15. Mpendwa OMBENI,

  Wala hunahaja ya kuogopa, wenye hekima walisema, ‘MTU MWOGA HAMPENDI MUNGU!’ wokovu ni lazima! Ndiyo maana katika sala mojawapo ya Bwana Yesu kristo, alituombea ‘ulinzi’ na katika ile sala yake mashuhuri aliyowafundisha wanafunzi wake alitaja “…usitutie katika vishawishi, ….au katika majaribu……au utuepushe na yule mwovu” kwa maana hiyo Yesu alijua kuwa vita iliyopo nikubwa kwa kiwango cha kushangaza, Neno katika Biblia linasema “kama siku hizo zisingefupishwa yamkini hata wateule, wacha Mungu, wenye njaa ya kweli ya Neno la Mungu na kadhalika nao wasingeokoka hata mmoja!” lakini wokovu ni kwa Mtu binafsi, kila mtu atakaye na aje ateke maji bure, ndiyo Neno linavyosema. Hakuna ushirika katika NURU na GIZA, ila yapo mahusiano kati ya Nuru na Giza; Bila ya Nuru Giza halina kazi, na bila ya Giza nayo Nuru haiwezi kudhihilika! Lakini katika vitu hivyo viwili kamwe HAVINA USHIRIKA – Havishirikiani, yaani kazi ya Nuru haiwezi kufanywa na Giza vivyo hivyo kazi ya Giza haiwezi kufanywa na Nuru!

  Yesu alisema mojawapo ya kazi ya Roho mtakatifu ni KUTUFAHAMISHA YOTE, umeuliza, tutaponea wapi? Biblia haisemi tutaponyeshwa na Mahubiri au Mafundisho ya hao ‘Watumishi’ Atakaye mwagalia yule Nyoka wa shaba, ndiye atakaye pona, japo ajapoumwa na Nyoka! Lisikilize Neno la MUNGU,ziangalie Ahadi zilizomo katika Mgodi huo wa ajabu (Biblia) kila atakayesikizishwa Neno lisilo la kweli aliangalie lile la Kweli naye atapona!

  Umeuliza “Hizo tabia mbona ndio wanazo watumishi wengi wenye huduma kubwa ninazozijua ?” umenukuu 2 Petro 2:1-22,. Nikweli hivyo ndivyo Neno linavyosema, lakini ujue wakati wote kwamba “Njia iendayo uzimani ni nyembamba na waipitayo ni WACHACHE” Haiwezekani katika njia nyembamba watu wakapita kwa wingi, vivyo hivyo haiwezekani Vifaa “Orijino” vikawa vingi katika soko kuliko vifaa “feki” iwapo mahitaji ya vifaa hivyo ni makubwa katika soko husika! Watu wanatakiwa waijue kweli ili kweli iwaweke huru kweli kweli! Kweli ni nini? kweli ni Neno la Mungu! Sasa basi, kitakachotuponyesha ni NENO la Mungu na Si WINGI wa watumishi feki!

  BWANA NA ATUPE UWEZA WA KULIWEKA NDANI YETU NENO LAKE KWA WINGI, AMINA.

 16. Duu Ajabu . kwa mujibu wa 2 Petro 2:1-22 hizo tabia mbona ndio wanazo watumishi wengi wenye huduma kubwa ninazozijua ? Sasa tutaponea wapi ? Eee Roho Mtakatifu utufungue macho tuweze kuwaona wazi wazi

 17. “BIBLIA INASEMA YAACHENI MAGUGU YAKUE PAMOJA NA NGANO” UKIONA KITU HALISI JUA NA CHA UONGO KIPO. CHA UONGO NA KILE HALISI HUFANANA SANA, KASORO TU NI KWAMBA CHA UONGO HUPATIKANA KWA WINGI NA KWA URAHISI KULIKO KILE “ORIJINO” WAPENDWA, NI VEMA KUISIKILIZA BIBLIA INAVYOSEMA JUU YA JAMBO HILO. UNAJUA BILA “FEKI” “ORIJINO” NAYO HAKUNA! HEBU TURUDI PALE MWANZO, EZEKIELI ANASEMA SHETANI ALIWAHI KUWEMO EDENI,ALIKUWEMO KU KUFANYA NINI? SIJUI! SASA FIKILIA KWA NINI MUNGU ALIMWACHA AISHI? MANABII WA UONGO KUJARIBU KUWAKOMESHA NI KUIFANYA BIBLIA NI NENO LA UONGO! CHA MSINGI MSIKILIZENI ROHO MTAKATIFU ANAVYOFUNDISHA ILI MUISHI. BIBLIA INASEMA “LIKO JAMBO LINALOONEKANA NI JEMA MACHONI PA MWANADAMU KUMBE NI NJIA YA MAUTI” SASA, JIEPUSHENI NAO, TOKENI KATI YAO! KUWAKOMESHA NI KUJIPA KAZI AMBAYO HUKUPANGIWA KUIFANYA, AMA HUNA UWEZO TOKANA NA ELIMU YAKO, UJUZI WAKO, UZOEFU WAKO AU NGUVU ZAKO, MAANA ‘AMRI ISIYOTEKELEZEKA NI AIBU KWA ALIYEITOA’ NGANO NA MAGUGU LAZIMA VIKUE PAMOJA, USIJARIBU KUINGILIA KAZI YA MVUNAJI!

  BWANA YESU AENDELEE KUWABARIKI.

 18. SOMO NI ZURI UKWELI USEMWE NA UBOVU UWEKWE WAZI ILI KUSUDI LA MUNGU LISONGE MBELE.

 19. hongera sana bwana Joel Msella kwa mada nzuri ambayo mi naona itasaidia sana kuweka wazi ukengeufu ulioingia katika imani zetu siku za leo. Mimi kwa kweli nakubaliana kabisa na wewe kuwa watajwe lakini ninaona ugumu wa kufanya hivyo kwa sababu ya sheria zetu ambazo haziruhusu kuwasema wengine waziwazi kwa kisingizio kuwa utakuwa unakashifu imani au dini za wengine ila mimi nafikiri tunaweza tu kuyasema tu yale yanayofanyika ambayo sio ya kimungu kwa watu ili wanapokutana nayo yakuhubiriwa sehemu yoyote basi waweze kujiepusha nayo. Kama utapata nafasi pia unaweza uka search kwenye youtube nimepost clip na nitaendelea kufanya hivyo ili tuweze kujua hizo imani potofu ni zipi ili tuweze kukomboa kizazi hiki chenye kutaka sana mafanikio ya mwilini na hivyo kuvutwa kirahisi sana na mafundisho ya uongo. HUKO YOUTUBE andika tu alexander kapinga basi utaweza kuzipata hizo clips. I am very happy with you for such a wonderfull post you have made.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s