Dondoo za kitabu cha HOSEA

Utangulizi:
Hosea ambaye maana ya jina lake ni ‘‘wokovu,’’alikuwa mwana wa Beeri (1:1) Hakuna mambo mengi yanayofahamika kuhusu nabii isipokuwa machache yaliyo katika wasifu wake kwenye kitabu hiki..

Nabii Hosea alikuwa mzaliwa wa ufalme wa kaskazini, yaani, Israeli, ambao yeye anauzungumzia pia kama Efraimu. (Majina mawili ya kwanza ya ufalme wa kaskazini) na kwa Samaria ambao ndio uliokuwa mji mkuu wa ufalme huo). Yawezekana kwamba alianza huduma yake kabla ya kifo cha mfalme Yeroboamu II ambaye alikufa mwaka 753 K.K. Huduma ya Hosea kwa ufalme wa kaskazini ilikaribiana sana na ile ya Amosi (nabii kutoka Yuda aliyetabiri kuhusu Israeli).

Amosi na Hosea ndio manabii wawli pekee wa Agano la Kale ambao vitabu vyao viliandika kuhusu ufalme wa kaskazini na uangamivu wake ujao. Hosea aliitwa na Mungu ili kutabiri juu ya matarajio yaliyoshindikana kabisa ya ufalme wa kaskazini (Israeli) katika kipindi chake cha mwisho cha zaidi ya miaka 30, kama Yeremia alivyokuwa akifanya kwa ufalme wa kusini (Yuda).Wakati Hosea alipoanza huduma yake katika miaka ya baadaye ya utawala wa Yeroboamu II, Isareli ilikuwa inafurahia ustawi wake wa kiuchumi na amani ya kisiasa iliyosababisha kuwepo kwa usalama pande zote. Mara baada ya kufa kwa Yeroboamu II mwaka 753 K.K., taifa lilianza kuharibika kwa haraka n a hatimaye kuangamia mnamo mwaka 722 K.K. Katika kipndi cha miaka 15 baada ya kifo chake, wafalme wane waliuawa, katika kipindi kingine cha miaka 15 Samaria iliteketezwa kwa moto, Waisraeli walipelekwa utumwani Ashuru na baadaye kutawanywa katika mataifa mbalimbali.

Wazo Kuu:
Kiini cha ujumbe wa Hosea ni kuonyesha upendo wa Mungu kwa wenye dhambi, yaani, upendo wa Mungu kwa Israeli aliyegeuka na kumwacha Mungu. Ujumbe huu wa Hosea ulionekana kwa dhahiri katika maisha ya ndoa ya huyu nabii. Yale majina aliyowaita watoto wake watatu kwa kufuatana kulionyesha kule kuvunjika kwa uhusiano wa upendo wa Israeli kwa Mungu.Jina la mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ”Yezreeli,”linaonyesha hukumu ya mfalme anayetawala, yaani Yeroboamu , aliyekuwa wa ukoo wa kifalme wa Yehu (2Wafalme 10:1-14).Jina la binti yake “Lo-ruhama” ambalo maana yake ni “Asiyehurumiwa,” likitoa ujumbe wa Mungu kwamba alikuwa anakaribia kuondoa huruma Yake kwa Israeli. “Lo-ami,” jina la mtoto wake wa tatu, linamaanisha “Sio watu wangu”, likiashiria Mungu kuwakataa Israeli watu Wake.

Kukosa uaminifu kwa Gomeri, mkewe Hosea, kunaonyesha ile hali ya kukengeuka kwa Israeli kutoka kwenye uhusiano wao wa agano na Mungu. Badala ya kuupokea kwa shukrani neema ya Mungu waliyopewa kwa kuwapatia baraka za vitu, Waisraeli walitumia mazao yao kutolea sanamu kafara. Dhuluma, rushwa, kuwaonea wengine, haya yote yanaonyesha udhaifu wa upendo wao kwa Mungu na kati ya wao kwa wao.

Mambo Muhimu:
Hosea anaelezea hali ya taifa akitumia hali iliyojitokeza katika maisha ya kila siku: Mungu anafananishwa na mume, baba, simba, chui, dubu, umande, mvua, nondo, n.k. Israeli inafananishwa na mke aliyekosa uaminifu kwa mumewe, mtu mgonjwa, mzabibu, zabibu, mzeituni, mwanamke anayejifungua, jiko la kuokea, ukungu wa asubuhi, makapi, moshi n.k.

Mwandishi:
Hosea mwana wa Beeri (“Hosea maana yake ni wokovu”).

Mahali:
Ufalme wa kaskazini (Israeli), ambao nabii anautaja kama Efraimu. Mji wake mkuu ulikuwa.Samaria.

Tarehe:
715-710 K.K.

Wahusika Wakuu:
Hosea, Gomeri, watoto wao.

Mgawanyo :
• Maisha ya Hosea katika familia. (1:1-3:5)
• Hali ya dhambi ya Israeli. (4:1-6:3)
• Adhabu kwa ajili ya Israeli. (6:4-10:15)
• Hukumu ya Mungu na rehema Zake. (11:1-14:9)

Advertisements

3 thoughts on “Dondoo za kitabu cha HOSEA

  1. Kwa sasa, Mungu asema kuwa watu wake watakuwa wageni katika nchi ambayo sio yao na watateseka kwa miaka 400, hii ni katika nchi ya Misri. Basi kuna mpango wa Mungu kwa watu wanaoenda katika haji – picha ya maisha yako duniani hadi mbinguni. Kama Mungu anapanga miaka 400 ya mateso kwa watu wake (Mwanzo 15:13) mbele ya nchi ya ahadi, tusishtuke wakati anatuambia, “kupitia mateso mengi ni hakika utaingia katika ufalme wa Mungu” (Matendo ya Mitume 14:22).

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s