Mashindano ya kusifu na Kuabudu

Bwana Yesu asifiwe wapendwa, jamani naomba tujadili hivi kuweka mashindano ya kusifu na kuabudu alafu kukawepo na ma-judge ni kiroho hii kitu? mbarikiwe

Grace

Advertisements

42 thoughts on “Mashindano ya kusifu na Kuabudu

 1. Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu. Natumai wote m wazima. Binafsi napenda kutoa mtazamo wangu,pengine ukawa tofauti kidogo na ya wengine. Ki ukweli tunapoingia katika mashindano ya kusifu na kuabudu hupelekea kutokea kwa mambo mengi ikiwemo,miongoni mwa waimbaji ambao watafanya vizuri ,kuanza kujiinua na kusababisha kiburi. kutokana na hali hii upelekea ule unyenyekevu mbele za MUNGU kuanza kupungua. Mimi naona kuwe na matamasha ya kuibua vipaji vya watu kwa kuwafanyia tathimini ya utunzi wao na kuwasaidia kukuza vipaji vyao.

 2. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.Kwa upande wangu ninaamini kuwa suala hilo hilo kiroho ila hilo halimaanishi kwamba ni kitu kibaya.Wakati mwingine tunahitajika kuchochea karama ya taaluma ya uimbaji.Mtu anaweza akatunga wimbo wa kumsifu Mungu lakini baadaye waimbaji wengine wakaanza kuimba kwa namna toufaui na jinsi mtunzi alivyovuviwa na roho wa BWANA.MASHINDANO KWA WAKATI MWINGINE YANAHITAJIKA LAKINI SIO KWA LENGO LA KUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI ILA KWA AJILI YA KUBORESHA TAALUMA YA UIMBAJI.

 3. Mpendwa Sungura,

  Sawasawa ndg yangu, nimefurahi sana kufahamu kuwa tulikuwa kumbe pamoja. Ndiyo maana Neno linasema usimuonye mtu mbaya kwa ukali, maana utautowesha uzuri kama Nondo! Kama ungefanya haraka kunijibu kwa mtazamo kuwa nasumbua, ungeniacha hewani, nikabaki sielewi ‘konsepti’ ya Swala zima, lakini ukanivumilia na kuelewa kuwa sielewi uhalisia uliokuwa nao katika kuilinda hoja yako.Ninashukuru pia Mungu sana, kuona na kufahamu kuwa, kumbe hata wewe ulikuwa ukielewa kuwa kupiga kura ni kazi ya watu, lakini mchaguzi ni Mungu mwenyewe – Amina!

  Neno linasema ‘Maandalizi ya moyo ni kazi ya Mwanadamu bali jawabu hutoka kwa Mungu’ Endelea kubarikiwa Ndg yangu Sungura.

 4. Mabinza asante sana, ndio maana nilikwambia kuwa tunakaribia kuelewana.

  Kuhusu suala la kutokumwachia Roho mt apige kura na penyewe naona kama tumekwisha kuelewana maana chini yake umetoa jibu la swali ulilouliza ambalo hata mimi ndio jibu langu. Kwamba baada ya kumwomba Mungu akina Petro waliendelea na zoezi la kupiga kura,wala huwakusema kuwa Roho mt atamke ni nani aliyemchagua. Yaani kazi ya kuchagua mtu ilikuwa ya Roho mt. na kazi ya kupiga kura zile ilikuwa ya akina Petro(watu) ndicho nilichomaanisha.

  Ndio maana neno linasema “maandalizi ya moyo ni ya mtu,jawabu la ulimi hutoka kwa Mungu.

  Ubarikiwe Mabinza maana katika hili tumekubaliana kukubaliana

  Amen

 5. Mpendwa Sungura,

  Nimefurahi sana kunionyesha kile nilichokuwa sijakielewa, katika hili kwangu umekuwa mwalimu mzuri! Unajua, mimi nilijua kuwa mnashindanisha Vipawa au karama za uimbaji wa nyimbo za kuabudu! Kumbe kinachotafutwa ni ustadi na ufundi katika kuimba, ila nyimbo zenyewe ziwe za Injili, nimekukubali ndugu yangu. Niseme tu kwamba katika hilo sina matatizo, sikuijua maana mliyonayo! Asante kwa kunielewesha.

  Soma vizuri mistari uliyonukuu ya Mdo 1:23 – 26! Mstari wa 24 unasema, “Kisha wakaomba,wakasema,wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili…………26, wakawapigia kura, kura ikamwangukia Mathiya…….”

  Mbona Biblia inajieleza tu vizuri kwama waliomba, ili Mungu amtaje kwa kuwaonyesha aliye mchagua! Tunapoomba kupata ufahamu au ufumbuzi wa jambo lolote, hapo huwa tunahitaji Roho mtakatifu, ili aje kwetu atufumbulie kwakuwa yeye ndiye ajuaye, ndiye mwalimu nk.

  Petro anaomba aambiwe, ni nani amekwisha chaguliwa na Mungu kuwa mmoja wa mitume. Petro akiwa mwana wa Mungu alilijua hilo, kuwa Baba huwajua watoto wake, maana anawajua tangu mwanzo kila mmoja kwa jina lake.

  Sijakuelewa unaposema hawakumwachia Roho mtakatifu apige kura! Wewe huoni kuwa majibu yaliyotokana na Kura ya akina Petro yalitolewa na Roho Mtakatifu? Kura hupigwa na pande mbili zinazotaka kupata ufumbuzi ambao utaondoa ubishi, tendo la kupiga kura hufanywa na wanadamu maana wao hawana uwezo wa kujua mawazo ya Mungu, ambapo Mungu yeye huyajua mawazo yetu! Ndiyo maana kwa kupitia kura watu wanaweza kupata chaguo au kusudi la Mungu!

  Unataka naye Roho mtakatifu (Mungu) apige kura akiwa upande mmoja na upande wa pili asimame nani? na jibu la kura hiyo nani alitoe? na apewe nani? Mwenyekujua matokeo hapigi kura, hutoa tu MATOKEO!

  Baraka ya Bwana iendelee kuwa nawe Ndugu yangu.

 6. Mabinza nimependa ulivyohitimisha, inaelekea tunakaribia kuelewana.

  Mungu amesema tumwimbie Mun gu kwa ustadi, ustadi unaosemwa si Mungu anayeufundisha bali mtu mhusika anatakiwa kufundishwa na watu wenye kuzijua hizo kanuni. N kanuni tunazosema hapa ni pamoja na mambo ya notation, jinsi ya kutumia vocal cord yako, mambo ya pitch, mambo ya pumzi n.k (hiyo ni lugha ya uimbaji, bila shaka unanipata).
  Hayo mambo huwa si kazi ya Roho mt. kumfundisha mtu.

  Ndio maana nikasema atakayekuwa wa kwanza si lazima atakuwa ndio mtu aabuduye katika roho na kweli. Na hizo kanuni ni kwa ajili ya akili/hisia zetu kuiweza kuwa katika mfumo wa kukubaliana ili hatimae tumpe Mungu atukufu. Mf: katika kuimba mtu akiimba flat au off key hisia zetu haziwezi kuimba katika mtiririko

  Hatujasema wanashindana ili kupata waimbaji safi kiroho,bali ili kupata wanaoweza kuimba kwa kufuata kanuni za uimbaji wa hizo nyimbo. Mwenye kujua waimbaji safi kroho ni Mungu ndg Mabinza.

  Mabinza kujitoa sana kwa Mungu hakukufanyi uwe mwimbaji bora, bali kujifunza sheria na kanuni za kuimba pamoja na kufanya mazoezi ndio kunakufanya uwe mwimbaji bora maana mwimbaji bora ni yule ajuaye kuimba kwa ustadi, na ustadi huja kwa kujifunza si kwa kufunga na kuomba.

  Lakini kujitoa kwa mtu humfanya awe mwabudu halisi bila kujali kafuzu katika kufuata kanuni za uimbaji bora au la.

  Ndio maana katika shindano kama hili watu wanafundishwa jinsi ya kutumia kipaza sauti,jinsi ya kuwasiliana na hadhira, jinsi ya kufuata mapigo ya muziki n.k. Miimi sioni udhambi wa hili jambo jamani.

  Kuna kitu umesema hapa, nakunukuu:Mpendwa, kuwa bora katika kumwimbia Mungu, kuimba kwa ustadi na mwenye kukupa tuzo kwa huduma yako hiyo ya uimbaji wa nyimbo za injili ni Mungu tu peke yake kwa njia ya Roho mtakatifu na si kupitia wanadamu, maana yeye ndiye anayejua aina ya mwimbaji amtakaye!

  Mabinza hiki kiwango ulichokisema hapa sio tena suala la kuimba bali ni huduma ya uimbaji, ambayo kiuhalisi imebeba kipawa cha uimbaji ndani yake. Na mimi nakubaliana na wewe kuwa mwenye kushughulika na hii huduma ni Mungu(Roho mt). Na hata waandaji wa shindano hawashindanishi huduma za uimbaji bali vipawa vya uimbaji ambavyo baadae hulelewa vikawa huduma.

  Biblia inaposema neno ki-mwili katika huu muktadha tunaoongelea humaanisha akili (mind), lakini sehemu zingine ikisema mwili humaanisha flesh kwa kizungu, na mara nyingi huwa inarejea kwenye mambo ya dhambi.

  Ivi Mabinza kwa nini akina Petro hawakumwachia Roho mt. apige kura kumchagua Mathia ili achukue nafasi ya Yuda pamoja na kwamba wao ndio waliwachagua Justus na na Mathias?( Mdo 1:23 -26)

  Ubarikiwe Mabinza.

 7. Bwana Mazogola asnte kwa mchango wako. Lakini hakuna chochote ulichoongea hapo.

  Pole!!!

 8. Mpendwa wangu Sungura,
  Unacheka, nachekesha eeeh, haya cheka ndugu yangu,……..Lakini usiku umeendelea sana
  Nitaanza moja kwa moja kukujibu hoja zako kwa mchanganyiko , kama ifuatavyo:- Umesema, “Kuwaita wandaaji kuwa ni mawakala wa shetani kama ulivyosema, ni uchanga wa kiroho na kukosa hofu ya Mungu kwa kuwahukumu wemgine wakati kazi ya kuhukumu si yako”. Mwisho wa nukuu.

  Hofu ni dhambi, kutojiamini husababisha unafiki, kumweleza Ndugu yako ukweli kama unavyomuona ki binafsi si kumhukumu, hayo ni mawazo binafsi. Kila mtu anachosema ndivyo aonavyo, ndicho kilicho moyoni mwake! Kinachoonekana kwako ni hasa kutokuijua maana ya neno Hukumu, kwa faida yako na wengine ambao hawataki watu watoe ukosoaji ni kwamba, Hukumu ni hitimisho katika kuthibitisha tuhuma, kwamba kilichobishaniwa ukweli ni kadhaa au aliyekuwa akituhumiwa sasa si mtuhumiwa ila ni mhusika, kwa kifupi hiyo ndiyo Hukumu! Mimi sijahukumu nimetuhumu!

  Umeniambia ni “Mchanga ki roho na sina Hofu ya Mungu” Wasiwasi wangu hujui nini maana ya maneno hayo kimaandiko, nitakueleza baadaye kwa kirefu maana ya maneno hayo, kwakuwa si msingi wa maada hii nikujibu tu kifupi kuwa, Mchanga kiroho ni mtu anayeabudu Mungu ‘asiyemjua!’ na Mtu asiye na Hofu ya Mungu ni yule ‘Asiyeabudu!’ Mimi yote hayo mawili Sinayo, kwakuwa ni mawazo yako unahaki ya kutoa tuhuma hiyo!.

  Umenijibu hivi, nanukuu
  “-Ninashindana ili niwe mwimbaji bora mwenye kujua kufuata kanuni za uimbaji.
  -Kwa ajili ya kuweza kumwimbia Mungu kwa ustadi
  -Nipewe zawadi na walioandaa shindano”misho wa kunukuu.
  Rafiki yangu Sungura, Uimbaji ni kama ilivyo katika mpira, kukimbia, kuruka, kuogelea nk, ni karama, lakini tofauti na hayo, uimbaji ni karama ya Pekee, huwezi kuilinganisha na uogeleaji, ukimbiaji, uchezaji mpira nk, kwakuwa Uiambaji hufanywa pia na maraika na kwamba itaendelea kufanywa hata katika maisha yetu ya Baadaye! Lakini, uimbaji ni karama na karama haina majuto! Kama tunaamini kuwa Uimbaji ni huduma, na ni kwa ajili ya Kanisa, kama ni huduma tunajua wazi kuwa huduma ya Kanisa husimamiwa na Roho mtakatifu. Hivyo ukitaka uwe mwimbaji bora jitoe ipasavyo na umuombe Mungu, ili Roho mtakatifu ambaye ni mwalimu akufundishe ili uwe bora.Sasa katika hili mashindano ya nini? Tuseme wewe unayewashindanisha ili kupata, wenye kuabudu safi kiroho, majibu ya sifa ya waimbaji wa nyimbo za waabuduji kiroho ipasavyo, una uhakika gani kuwa,Roho mtakatifu amewapa majibu husika majaji wa shindano?
  Mpendwa, kuwa bora katika kumwimbia Mungu, kuimba kwa ustadi na mwenye kukupa tuzo kwa huduma yako hiyo ya uimbaji wa nyimbo za injili ni Mungu tu peke yake kwa njia ya Roho mtakatifu na si kupitia wanadamu, maana yeye ndiye anayejua aina ya mwimbaji amtakaye! Ninyi shindanisheni mambo mnayotaka yawafurahishe ninyi wenyewe na si kushindanisha watu ili kumpata mtu bora wa kufurahisha Mungu wa mbinguni! Ila kama mnayafanya haya “Mkiwa kipsa zaidi” hilo siingilii ni juu yenu, apandacho mtu ndicho avunacho! – “OMBENI NENO LOLOTE KWA JINA LANGU NAMI NITAWAPA” alisema Yesu!

  Umeuliza “Je unaelewa maana ya maneno haya: Kura hukomesha mashindano?
  Na kama Mungu anasema hivyo, je ni nani anayepiga hiyo kura?
  Na je hiyo kura ni ya ki-mwili au ki-roho?
  Je kwa andiko hilo huoni kuwa biblia inatambua mashindano?.” Mwisho wa kunukuu.

  Najibu kama ifuatavyo: Neno Mashindano, ni wingi wa neno shindano, na lina maana mbili, moja,ni hari au tendo linalofanywa, makusudi apatikane mshindi, na mshindi anaweza kupewa, tuzo au medari, heshima, ubingwa, umaarufu nk, lakini la pili ni Mabishano,kutokukubaliana katika jambo nk. Na hii ndiyo hasa maana inayozungumzwa katika Biblia na kuunganishwa na neno Kura, neno Kura ni ‘Ufumbuzi’ kura yaweza fanywa kwa siri au kwa uwazi, Msimamiaji wa mabishano huitisha kura ili wanaobishana au kushindana yaani hawakubaliani kwa pamoja katika jambo moja, waonekane upande upi ni wengi, na hao ndiyo washindi, na hivyo hoja yao au lile wanalolikubali wengi hao hupita! Kura huwezi kuitumia katika watu wanaoshindania Ubora katika, Mbio, Waimbaji, Waogeleaji Wacheza mpira, wacheza mieleka, Mabondia nk. Kura ni tendo lifanyikalo KIMWILI ili kutoa majibu ya kiroho kwa wahusika, inategemea Roho yupi anatakiwa ajibu kwa njia hiyo ya kura, kura si bahati na sibu, ni tendo lenye kanuni!

  Umesema “ Mabinza hebu na wewe nijibu hapo, na utafute kujua maana ya neno ki-mwili na ki-roho.” Mwisho wa kunukuu. Ki- mwili, ni tendo linalohitaji mazingilra ya mwili, yaani mtendaji lazima awe na mwili. Matendo yoyote ya kimwili yanazingatia ‘kanuni au nguvu au sheria za Asili’ za kawaida za Duniani ambazo ziliwekwa na Mungu kwa ajili ya mwili. Nguvu au kanuni hizo hazionekani kwa macho ya ki mwili, kama ambavyo aliyezibuni asivyoonekana kwa macho ya ki mwili, lakini matokeo yake hudhihilika waziwazi ki mwili, maana ni kwa matumizi ya MWILI! Nguvu au sheria hizo ni Nne, nazo ni nguvu za kisumaku, nguvu za uvutano, nguvu za nyukilia na nguvu za ki umeme.

  Ki- roho, ni matendo yote ambayo si lazima yazingatie kanuni za kimwili, kwa kifupi ni matendo ya imani na hutokezea majibu yakaonekana kwa macho ya ki mwili, matokeo hayo hujulikana kuwa ni Muujiza! Mfano, Mtu kutembea juu ya maji ni muujiza kwa mtu aliye katika kanuni za kawaida za ki mwili, maana zinasema Kitu ili kielee juu ya maji lazima kiwe na ‘Densite’ chini ya moja, hivyo ki mwili kamwe mtu hawezi kutembea juu ya maji kwani mwili wa mwanadamu umejengwa kwa vitu vya aina mbali mbali zenye ‘Densite’ tofauti tofauti, katika mwili kuana maji, kuna chma, kunachokaa mna hewa, una umeme, mna sumaku nk, na vitu vyote hivyo vinatofautiana katika densite zake! Kwa hiyo mambo ya kiroho ni tofauti na mambo ya mwili katika kanuni au sheria za kimaumbile, lakini mwili na Roho HUSHIRIKIANA ili kuleta matokeo yanayokusudiwa!.
  Mwisho, sijasema kuwa Mungu Hapendi michezo,ila nimesema kuwa hawi upande wowote katika mambo ya Michezo. Ni kama Baba wa kawaida asivyoweza kuwa upande wowote mbele ya watoto wake wachezao, akampendelea huyu na kumuwezesha kwa kumpa vichezeo vingi na bora ili amshinde mwenzie!
  Je, ukimkuta Baba wa jinsi hiyo wewe utasemaje?Hadi hapo huanishawishi nione kuwa mashindano ya nyimbo za kiroho ni jambo la Busara! kKuandaa na kuwashindanisha watu kwa maana waliyonayo waandaaji, laweza kuwa jambo JEMA lakini si BUSARA!

 9. Bwana Mabinza
  Naona hata ww pia unajua nini kinaendelea katika uimwengu huu maana ibilisi yuko ndani ya kanisa na aanawaendesha watu ili kumuabudu kaini watu hawajui. Jamaani labda niseme hili shetani kama sheta hutunia ukweli mwing lakini uongo kidogo sana ili akutoe katika mpango wa Mungu,Me nahisi watu wengi hawajalijua hilo ndo maana wanaona wokovu ni wa lele mama tu. Tunashindwa kuelewa hivi viyu huwa ni karama Mungu huwa anajaria na si mafunzo kama watu wafnyavyo.Sidhani kama kuna michezo ambayo itakuwa ni ya Mungu Mingi yao imeanzishwa na ibilisi ili tusiweze kulitafakari na kilisoma neno la Bwana kikamilifu.Kwa hiyo bwana mabinza utabishana mpaka mwisho na muafaka usipatikane maana wengine hapa wanafuata ushuhuda wa shetani sisi kwamba na yy aliimba huko mbiguni kuliko malaika wote.Ufunuo una sema tokeni kwake enyi watu wangu 18:1-4 Kwahiyo jamni shetani yumo ndani ya kanisa maana ss hivi anatumia dini kama Maind control. Kazi kwnu ss.

 10. Ha ha ha ha haaa……

  Mabinza umenichekesha sana na hoja zako,loh!

  Kwamba Mungu hawi upande wowote katika michezo, na hapendi michezo (games). Na kwamba mashindano yoyote ni michezo na michezo ni jambo la kimwili. Kwa hiyo kifalsafa umemaanisha kuwa Mungu hapendi mambo ya ki-mwili. Na bila shaka unataka wadau tukubaliane na hilo!

  Nina mashaka makubwa kama unaelewa maana ya neno Ki-roho na neno Ki-mwili, au umezoea kuyatumia tu kama sehemu ya rejesta ya kanisani hasa kwa makanisa ya kipentekoste.

  Na ninavyojaribu kukusoma ni kwamba kwako neno ki-mwili ni kinyume cha neno ki-roho,na hivyo unadhani kuwa hata huu mchango wako umeuandika ki-roho wala si ki-mwili. Tena bila shaka hapo wewe unajiona ni wa ki-roho wala si wa ki-mwili hata kidogo. Pole sana

  Kisha umeuliza maswali haya, nanukuu: Unashindana uwe nani na kwa ajiri ya nani? Upewe zawadi na nani? Ushindi ni sifa, na sifa ikiwa ya kimwili inapelekea mhusika “kuvimba kichwa” ikitokea hivyo kwa mshindi huyo wa injili, ninyi waandaaji “mtaruka” vipi kuwa nyinyi hamkuwa mawakala wa Shetani katika hilo?!

  Majibu:
  -Ninashindana ili niwe mwimbaji bora mwenye kujua kufuata kanuni za uimbaji.
  -Kwa ajili ya kuweza kumwimbia Mungu kwa ustadi
  -Nipewe zawadi na walioandaa shindano

  Swali la mwisho linahitaji maelezo, si kweli kwamba sifa ya kimwili huvimbisha kichwa,ispokuwa sifa yoyote inaweza imfanye mhusika awe na kiburi kama ni mjinga. Lakini kwa mwenye ufahamu hujua mwenye kumwezesha ni Mungu, kwa hiyo humpa yeye utukufu.

  Kuwaita wandaaji kuwa ni mawakala wa shetani kama ulivyosema, ni uchanga wa kiroho na kukosa hofu ya Mungu kwa kuwahukumu wemgine wakati kazi ya kuhukumu si yako.

  Je unaelewa maana ya maneno haya: Kura hukomesha mashindano?
  Na kama Mungu anasema hivyo, je ni nani anayepiga hiyo kura?
  Na je hiyo kura ni ya ki-mwili au ki-roho?
  Je kwa andiko hilo huoni kuwa biblia inatambua mashindano?

  Mabinza hebu na wewe nijibu hapo, na utafute kujua maana ya neno ki-mwili na ki-roho.

  Nadhani wewe ndo unatakiwa ku- take care” zaidi maana hauko mbali na kukosea!!

 11. Wapendwa katika Mashindano ya kusifu na kuabudu,

  Mtapamba pamba sana, lakini ukweli utabakia palepale kwamba Shetani yumo kanisani, wakristo wameamua kuishi maisha “Miksa!” kama ilivyo Tanzania. Tuna sera na misemo ya Kijamaa lakini maisha na vitendo ni vyakibepari! maisha Miksa! Heri kuwa baridi au Moto ili ijulikane moja! Mungu hawi upande wowote katika michezo; Mashindano yoyote ni Mchezo na Michezo ni mambo ya Kimwili tu, hakuna mashindano ya Ki-Roho mtakatifu, kwa hiyo hakuna Michezo ya Ki-Roho mtakatifu!! Kwanini waandaaji msiseme tu kuwa munaiga wanao fanya Bongo staa sachi,Tikisa, Maisha plasi, Mama Afrika nk, ili nanyi mpate PESA?! Tusifichane, muwe wazi mnataka “Kuzungusha” pesa? Pesa kweli ni nzuri, lakini uzuri wake si tofauti na moto, ukiuwasha nje wakati wa upepo utaunguza Nyumba – Nyumba yako ikiteketea usilaumu ‘Faya’ laumu kichwa yako!

  Nimesikia mara nyingi Watu wakisema “…….Mungu simamia huduma yangu ya uimbaji,….uijilisti,…..uchungaji,….!” nk. Je, ni huduma yako hiyo? Acha kujitapa wewe ni Mtumishi tu, mwenyehuduma akiona kuwa hufanyi ipasavyo anakunyang’anya huduma yake, ingawa wewe utaona hujanyang’anywa lakini kiukweli ulishanyang’anywa zamani, umebaki wewe na “huduma yako kweli!” Hauna tofauti na Maiko jaksoni! Tofauti yake tu wewe unamtaja Yesu katika kibwagizo cha nyimbo zako, wakati Maiko ana bwagiza kwa kusema “hu zat gero”

  Unashindana uwe nani na kwa ajiri ya nani? Upewe zawadi na nani? Ushindi ni sifa, na sifa ikiwa ya kimwili inapelekea mhusika “kuvimba kichwa” ikitokea hivyo kwa mshindi huyo wa injili, ninyi waandaaji “mtaruka” vipi kuwa nyinyi hamkuwa mawakala wa Shetani katika hilo?!

  Biblia inatoa kisa cha mama mmoja alimwendea Yesu na kuomba kuwa,wanaye wawili wapate kibali, cha kukaa mmoja kulia na mmoja kushoto mwa kiti cha “Enzi” Yesu alimjibu mama huyo, “Haujui uombalo!” Shetani ni mwongo na ni Baba wa huo, na uongo ukileta matokeo mazuri kwa muongo hiyo kwake ni “dili”

  “Teki kea!”

 12. Ndg Mazogola, kwanza samahani kwa kukosea jina lako katika chapisho langu lililopita na kukuita Mazogoda.

  Ukifanya jambo kubwa halafu watu wakakusifu hawatakuwa wamefanya kosa lolote,wala wewe uliyesifiwa hautakuwa umefanya kosa lote. Lakini wakikusifu wewe wewe kwa kuonesha kuwa umefanya hayo kwa nguvu zako na wewe ukakubali kuwa umefanya hayo kwa nguvu zako utakuwa umefanya kosa kubwa sana.

  Kama ambavyo kuna hekima ya mwanadamu kuna hekima ya Mungu pia, kama ambavyo kuna utukufu wa Mungu kuna utukufu wa binadamu pia. Hekima ya Mungu ni ya Mungu wala haikaribiani ya binadamu na utukufu wa Mungu ni wa Mungu wala hata kidogo haukaribiani na wa binadamu.

  Wewe ukifundisha neno la Mungu vizuri tunakuopongeza,lakini ni wajibu wako wewe kujua nani kakuwezesha kufundisha vizuri ili umpe utukufu. Ukijua kuwa aliyekuwezesha ni Mungu halafu ukaacha kumpa utukufu wewe ndiye mwenye matatizo.

  Tumesema kuwa majaji hawapo hapo kuhukumu nani kaimba katika roho na kweli, hiyo si kazi yao na hata wakitaka kuifanya hawataweza. Kazi yao ni kuangalia nani kaimba vizuri kwa viwango vya kanuni za uimbaji. Na ujue anayeimba vizuri kwa viwango vya kanuni za uimbaji si lazima kuwa ameimba katika roho na kweli.

  Mimi nashindwa kuelewa kwa nini hili suala linakuwa gumu sana kueleweka kwa wengi. Suala la kuimba ni la kimwili na kiroho pia. Sasa nyinyi naona mnalipeleka upande mmoja tu wa kiroho. Kipawa cha kuimba si sawa na kipawa cha kuomba (intercession) ambacho ni cha kiroho tu.

  Nasema tena, mashindano hayo si ya kutafuta anayeimba katika roho na kweli ila mwenye uwezo wa kuimba kwa kufuata kanuni za uimbaji ( singing skillfully)

  Atakayeshinda ni wajibu wake kumpa Mungu utukufu au kutompa, ni wajibu wake kuimba katilka roho na kweli au kuimba kimwili wala sisi hayo halituhusu.
  ataunachoangalia ni je anapatia kanuni za uimbaji!!!

  Bila shaka tunaelewana!!!

 13. Linaweza kuwa shindano la kawaida kwa ajili ya kuborehsa vipaji vilivyopo katika jamii ya waaaminio lakini sidhani kama wandaaji watakuwa wana mtazamo na fikra za kuwashindanisha washindani kiroho na kupima kiwango chao cha uabudu halisi hayo maswala ya vipimo vya kiroho na uabudu halisi anabaki navyo mchunguza mioyo na viuno Yehovah Mwenyewe ila tusisahau suala la ufundi linahitajika sana kwenye kitengo hiki siyo kila mtu anayetamani kuimba ni muimbaji.

  huo ni mtazamo wangu tu. wandugu.

 14. Nashukuru sana kwa changamoto tunazotiana hizi zote ni katika kujua ukweli wa Nwno la MUngu

  Nikirefer kwa jibu alilonipa MR Milinga
  Alisema kuwa ” Lusifa ndiye aliyekuwa akiendesha zoezi hilo kabla hajakorofishana na Mungu. Wapendwa mmesahau hilo. Lusifa kutokana na kuimba kwake vizuri kuwashinda malaika wote, hadi Mungu akampa tuzo zote na heshima kubwa, Lusifa aliingiwa na kiburi na akataka afanane na Mungu kwa kila jambo ikiwemo kutaka aabudiwe na malaika wengine walioshindwa kuimba kama yeye.” hapa inaonesha kuwa ww si wa kristo tena ila ni wa ibilisi ama lusifa maana kwa kufanya hivyo alijiinua kuwa kama Mungu ndiyo ambayo roho hiyo inawasumbua watu wengi hata wewe ukiwemo.

  Angalia hili andiko (Ufunuo 5:12) kuwa sifa na utukufu tumpe Bwana, kama mtu atakuwa anaimba katika roho na halafu kuna majaji wapo inamaana majaji wanauwezo wa kumuongoza roho wa Mungu na sio yy kutuongoza, hapo sitakaa nikubaliane na nyie kamwe,mtu akipigiwa makofi akipongezwa, akisifiwa hata kushinda huo sio utukufu kwa ajili ya Mungu wetu ila ni Yule Mtu aliye kuwa akifanya hivyo.Maana hata injiri ya ss utaona hadi kwaya huungiwa kwa viingilio nalo hili utaniambia ni la kiroho maana LUsifa ndie akupae mwongozo,Hakuna katika bibilia kunaonesha yalifanyika mashindano ya kuimba yaliyo kuwa katika misingi ya Kristo, MAana maandiko yanasema hata shetani hujibadilisha kuwa malaika wa Nuru yamkini awaangushe hata wale wateule wa Mungu so chunga sana maana hii ni Mitego ya ibilsi.

  Kwahiyo bwana Milinga endelea sana Kufuata ushuhuda wako

  Amina

 15. Bwana Msanjila na Mazogoda acheni kulazimisha mambo kwa maandiko ambayo hayahusiani na mada.

  Kama kweli mnajua mnachokiongea toeni upembuzi yakinifu,onyesheni maandiko ambayo yanaonesha kuwa kushindana kuim
  ba ni dhambi.

  Maana mpka hapo naona mnaongea fikra zenu ambazo kwa bahati mbaya nazo si za kweli,maana hakuna hata moja yafikra hizo
  iko sahihi kimaandiko. Ispokuwa mmenukuu
  maandiko na kuyaweka ktk mitazamo isiyosahihi.

  Msanjila kuna swali hujanijibu pia,jibu usikwepe.

  Asanteni.

 16. amen dada grace,swali zuri sana,hiyo inaonesha ukomavu na pia kuwa na ongezeko katika uimbaji,mwimbaji pia anakuwa mjasiri na anasoma kutoka kwa wenzake,sivibaya kwa kuwa kando na kuwa mwimbaji,anaongeza maarifa na ustadi katika utunzi wake. ——————————

 17. Mr msanjila
  Asante kwa kuliona hilo maana hata ukisoma Mathayo15:1 inasema maana mnavunja maagano ya Mungu kwaajiri ya mapokeo yenu pia mathayo anasema maana hamjiu mnachokiabudu maana kuabudu kwenu ni bure ,Mathayo 15:7-9.Tuseme nini basi juu ya hili roho wa Mungu hawezi kumuongoza mtu kujipinga mwenyewe.Ndo maaana hata maneneo ya Bwana yanasema tufanye kila kitu kwa utukufu wa bwana maana mtu anapokuwa ameshinda anakuwa ametukuzwa yy na sio Mungu. Kwahiyo ndugu zangu tusidanganyike maana watu huuangamia kwa kukosa maalifa watu huishia katika kumsikiliaza mchungaji hawana Muda wa kuzichunguza roho Na sis sio wa dunia hii na hatuwezi kufanya mabo ya kidunia Huko ni kushulutishwa na roho mchafu maana kujiinua ni roho ya ibilisi yy ajiinue juu ya kitu kinachoitwa Mungu. Isaya 14:13:14.

  Wapendwa yachunguzeni maandiko yanasema nini juu ya kumtafuta bwana tusipeane moyo kwa mambo ambayo hayampendezo bwana hata kidogo.
  Amina

 18. Waabuduo halisi watamwabudu Baba ktk roho na kweli,nyie majaji hamna kipimo cha kumpima mtu roho yake anapoabudu, {Yohana 4;23}.
  Tuseme tu ukweli ninyi majaji mnafuata kawaida ya ulimwengu huu kama efe 2;2 isemavyo na kwa kweli macho ya mioyo yenu yatiwe nuru maana sisi watu wa Mungu tumehama huko ndio maana tulitoka huko,labda kama ninyi bado mpo huko siwalaumu sana. Maana lazima ujue kwamba hupaswi kushindanisha karama ya Mungu, kama ni sauti Mungu ndiye amemgawia kila mtu kama apendavyo yeye,kama ni moyo wa kuabudu kihalisi Mungu ndiye ajuaye,mtakuja kushindanisha na wahubiri,wainjilisti,wachungaji au kushindanisha wanaonena kwa lugha kwa muda mrefu zaidi nk maana ni kipawa kilekile. Jamani hiyo kazi muachieni Mungu mwenyewe,hiyo ni kuudhalilisha wokovu,na kama mliookoka mmejiingiza huko acheni na muombe rehema kwa Mungu,maana tangu niokoke sijawahi kusikia kwaya za walokole zinashindana.Tukubali tu kwamba huo ni UDHAFU.

 19. Nashukuru Sana bwana mlinga
  Kumbuka mandiko yako wazi kabisa kuwa mwili u dhaifu ila roho i radhi sasa tunapoingiza mambo ya kimwili kwa kuyafanya ya kiroho hapo ndipo inapokuwa tatizo,Kwanza mtu wa kiroho huwa haongozwi na akili yake mwenyewe ila ni roho wa Mungu aliyeko ndani yake ndiye afanyae kazi ya kumuongoza sasa tukija katika mashindano hayo ya kuimba sijajua dhamiri yake ni nini roho kushindana na roho au hisia za binadamu kushindana na binadamu.

  Jamani nahisi ni muda wa kukumbushana sana juu ya wakati kama huu maana shetani pia hutumia hayohyo maandiko ya Mungu kuupinga ukweli wa Mungu vile vile pia shetani huwezi kumshindda kwa kuvunja ngome ni lazima umshinde kupitia hayo hayo maandiko Ona mathayo4:1-11 twaona vile Bwana wetu Yesu alivyo mshinda ibilisi.

 20. Ubarikiwe Sungura. Umeeleza vizuri mpaka raha. Shindano ni la kimwili matokeo ya shindano ni kiroho.

 21. Nimefuatilia kwa sehemu hoja za waliotangulia kuchangia, nimegundua kuna mambo ambayo bila shaka ndio tatizo au kikwazo katika hili suala.

  Kwanza ni neno shindano

  Pili ni neno Kiroho

  Tatu ni neno mshindi

  Nne ni uwepo wa waamuzi(judges)

  Neno shindano si geni kwa wasomi wa biblia,hata Paul kalisema sana. Kasema habari za kushindana kwetu si juu ya damu…., lakini pia kasema habari za washindanao katika michezo/ machezo.

  Kwa hiyo tatizo si shindano bali ni mitazamo juu ya shindano.

  Neno “kiroho” linahitaji ufafanuzi, maana watu wengi wwamesema suala hili si la kiroho. Nini maana ya kiroho?
  Ni jambo lifanywalo ambalo matokeo yake yanahusiana au yanaathiri roho ya mwanadamu.Kwa hiyo suala la kuimba ni la kimwili ambalo matokeo ya kinachoimbwa ndo kinaweza kugusa roho na hisia za mtu.
  Si lazima kila kuimba kwetu kuwe kwa kiroho,bali kunaweza kuwa kwa ki-akili pia.

  Kwa hiyo hao wanaoshindana hawashindani kuimba kiroho bali wanashindana kuimba. Na kwa sababu wao wamezaliwa mara ya pili ni lazima waimbe nyimbo ambazo kiroho ni za kibiblia.

  Ili uweze kuimba na kugusa roho ya mtu lazima uwe umeweza kuimba na kugusa moyo au akili zake kwanza, na ili kugusa akili lazima uwe umepatia kanuni za kuimba/uimbaji.

  Kitu wanachofanya majaji hapo ni kupata watu wanaoweza kuimba kwa kufuata kanuni za uimbaji, wala hawachagui mtu anayemwabudu Mungu katika roho na kweli. Kwa hiyo wanachofanya si kuingilia kazi ya Roho mtakatifu kama wengi wanavyojaribu kusema.

  Na mshindi anayetafutwa si mshindi wa kuabuudu katika roho na kweli, bali ni mshindi wa kuimba kwa kufuata kanuni za uimbaji wa nyimbo za kuabudu, ambaye kiukweli ndio mtu anayeweza kuimba katika roho na kweli pia.

  Neno wa kwanza atakuwa wa mwisho lina muktadha wa shindano ndani yake!

 22. Bwana Msanjila siku unajiandaa kufanya mtihani wako wa ngazi yoyote ya elimu baada ya kuwa umeokoka ulifanyaje maombi yako, je uliomba wengine washindwe ili wewe uwe wa kwanza au?

  Bwana Nshimirimana unaweza kutupa jibu la swali hili; kwa nini Yesu Kristo aliwakataza wana funzi wasitoke Jerusalemu kabla ya kupewa uwezo wa Roho mtakatifu?

 23. Naam nimekusoma ndugu Sasali, nimeelewa na ni kweli uliyosema kwa upande wa utetezi wako nisahihi na imekaa vizuri.

  NDUGU Millinga, nadhani jaribu kuweka vizuri, sidhani kama uliyo sema yanatokana na neno la Mungu au ni fikra zako. kwamba ”Lusifa ndiye aliyekuwa akiendesha zoezi hilo kabla hajakorofishana na Mungu. Wapendwa mmesahau hilo. Lusifa kutokana na kuimba kwake vizuri kuwashinda malaika wote, hadi Mungu akampa tuzo zote na heshima kubwa, Lusifa aliingiwa na kiburi na akataka afanane na Mungu kwa kila jambo ikiwemo kutaka aabudiwe na malaika wengine walioshindwa kuimba kama yeye” sijui sana juu ya hili jambo la lusifa, ila ninachojua si kwamba yeye aliwashinda malaika wengine bali ALIPEWA KAZI HIYO, NI KAMA MICHAEL ALIVYOPEWA UPANDE WA VITA. nitarejea ukifuta hili.

  barikiwa
  Anthony

 24. Suala la mashindano linaweza kuibua kiburi ndani ya yule atakayeshinda kama hatakuwa makini, na hatimaye kumuangusha kiroho maana kiburi huwa kimejificha sana, ndicho kilichomuangusha Lusifa tukumbuke, tuwe makini katika hili, na waandaaji pia wawe makini katika kuwaelekeza washiriki nia ya shindano, maana inawezekana kuna motive nzuri tu ndani ya waandaaji katika kuwainua worshipers watakaoweza kuabudu katika Roho na kweli, lakini umakini ukikosekana tutainua viburi ndani ya watakaoshinda kwenye shindano hilo.

  Tuendelee kujifunza.

 25. Mpendwa Mazogola,

  Ujumbe wako haujaeleweka. Hebu jaribu kujifunza maandiko tena upya na ulete hoja zenye mashiko hapa. Hivi unaposema “atakayekumfuata Yesu ni sharti kwanza ajikane mwenyewe” ndiyo kusema kwamba kushiriki mashindano ya kuimba unakuwa hujajikana wala kumfuata Yesu? Nini maana ya KUJIKANA NAFSI?

  Tatizo ni kwamba watu wanashindwa kuelewa maandiko katika mktadha au nje ya mktadha wake. Kuendesha mashindano ya kuimba imekuwepo tangu enzi za kale kule mbinguni. Lusifa ndiye aliyekuwa akiendesha zoezi hilo kabla hajakorofishana na Mungu. Wapendwa mmesahau hilo. Lusifa kutokana na kuimba kwake vizuri kuwashinda malaika wote, hadi Mungu akampa tuzo zote na heshima kubwa, Lusifa aliingiwa na kiburi na akataka afanane na Mungu kwa kila jambo ikiwemo kutaka aabudiwe na malaika wengine walioshindwa kuimba kama yeye.

  Mashindano ya kuimba hayana tofauti na Shule ya Muziki. Kuwachukua waimbaji na kuwashindanisha mbele ya hadhara ni Kibiblia kabisa kwani haina tofauti na watu wanaokwenda vyuo vya Biblia kusomea Theolojia ya maandiko. Mbona hata huko vyuo vya Biblia watu wanafanya mitihani na mtu akishindwa mitihani ya Biblia anapaswa kutoendelea mbele kwa madarasa zaidi. Wapo wanaoishia kupata Cheti tu, wapo wanaopata Diploma, Degree, PhD, nk. Haya nayo ni mabaya? Je, siyo kiroho kwenda chuo cha Biblia?

  Kumbuka wewe unayesema kwamba hayo nayo ya kwenda Chuo cha Biblia ili ukashindane na wenzako kwenye mitihani darasani siyo ya kiroho; uelewe kwamba nyakati za Manabii kulikuwa na Chuo cha wana wa Manabii. Hawa walifundishwa kila kitu kuhusu fani ya UNABII, Je, leo hii tunavyo vyuo vya kufundisha watu kuwa manabii?

  Mashindano ya kumpata mwimbaji bora wa nyimbo za kusifu na kuabudu natamani yaanzishwe nchi nzima au kila kanisa la kiroho ili tuwapate waimbishaji wa sifa na kuabudu majumbani, mikutanoni, makanisani, na mashuleni.

 26. Jina la Bwana lisifiwe, Watu hawasomi bibilia ndo maana hata bibilia inaandika kuwa watu huaangamioa kwa kukosa maarifa kwa saababu sasa watu wanafuata yaliyo maagizo ya mwanadamu maana me naona hiyo ni baraza la watu wenye mizaa halfu pia ni mambo ya kidunia ambayo Mungu siku zote anayakataa maana yule aupendaye ulimwengu anafanyika kuwa adui na Mungu hivyo wapendwa wokovu sio wa lelemama au rahisi kama watu wanavyodhni ndo maana siku hizi kuna mitindo na mambo mengi yaaanaanzishwa ya kidunia ukiuliza utaambia hiyo ni disco la Yesu,Ndombolo ya Yesu au staili ya Yesu.

  Lakini Yesu alisema yeye atakae kumfuata nisharti kwanza ajikane mwenyewe kisha ajitwikwe msalaba wake amfuate.Sasa sisi hilo ndilo linawashinda wengi wanajikuta wanajipenda hata kuliko Mungu. Kwa sasa huwezi amini hadi katika kanisa la Mungu shetani kaisha jiingiza ndo maana unakuta katika madhehebu mengi mambo yanayotendeka mule ni tofauti sana na bibilia, kwa sababu watu huzoea kwenda kanisani kwa mazoea hawana ule wakati wa kuchunguza maaandiko yanasemaje kuhusu Imani ya Bwana wetu Yesu kristo, Hivyo kwa kushauri na kutiana nguvu ni kila mtu awe wakili wa nasfi yake na ajitoe kwa Mungu ili awe dhabihu safi mbele zake.

 27. Inategemea na nia ya mashindano hayo. Mi nachoomba tusiende sawasawa na mataifa yanavyoenda. Kama inaboreshwa iwe ya kiroho zaidi watu watanufaika.

 28. Nimeyapenda hayo mashindano! Natamani yawepo na mashindano ya uinjilisti (maana yatakuwa na impact ya kuchochea karama ya kuleta wengi kwa Yesu); mashindano ya ualimu wa Neno la Mungu (maana yataibua na kuchochea karama ya ualimu ili wengi walielewe Neno na kukua kiroho); mashindano ya utume na unabii (ili kuibua na kuchochea ofisi za mitume na manabii); na vivyo hivyo mashindano ya wachungaji!

 29. Merci beaucoup Mtumishi wamungu!
  Sasa ninaendelea kukutega sikiyo kwa mengine.
  Ubarikiwe sana na Jéhovah.

 30. Neno Kiroho lina pande 2, it either Kwa Shetani ama Kwa Mungu…..What makes kitu kiwe ni dhambi kwenye maisha yetu sometimes not always ni Motive. Inawezekana Wanachokifanya Wao Ni Kibaya lakini With a right Motive mfn. Kahaba kutoa Sadaka Kanisani pengine anachofanya kinaweza kuwa Kibaya lakini Motive ni nzuri. Ama Ananinia na Safira walikuwa Wanatoa Kitu Kizuri kwa Motive Mbaya. Na Motive Zote zinaweza kuwa kwenye “Ukiroho”. Ndio Maana Swali lilipoulizwa Kama ni Ukiroho ama Sio. Nikajibu ni Ukiroho sababu lina positive and negatives.

  Personally nimewahi kaa ni Viongozi wa Worship Experience Tanzania na Kuwasaidia Hatua za Mwanzoni on How they can make it better.

  Ukisoma Dhumuni kuu la hawa Jamaa ni Kutaka Kusaidia People With Talent Of Singing Katika Category ya Worship. My First question kwao ilikuwa why Worship and How will they Know?. Walichonieleza ni Kwamba kumekuwa na “Worshipers” Wachache sana wanaotengeneza Albam za Nyimbo za Kuabudu kuliko Wanaotengeneza Nyimbo za Praise na Nyimbo za Kawaida kama Zile Nibebe. Kwa Sababu hiyo ipo haja ya Kuibua Worshipers wengine kama Lisu nchini Tanzania.

  Nilipowauliza Kuwa Watajuaje huyu ni Worshiper huyu Sio Wakasema katika Hatua ya Kwanza itakuwa ni Random ambapo washiriki watakuwa wakijichagulia nyimbo na Kuimba. A Worshiper anajulika hata bila shindano. If anyone ana experience na Music hata ule wa Kusikia, huwezi niambia Bon Mwaitege ama Rose Muhando ni Worshiper kwa sikio tu lakaida hata kama hakuna Vigezo vyovyote when a worshiper take a Microphone to Sing utajua. Kama kuna mtu ni Mwalimu akianza kuongea ama kuhubiri utajua huyu ni mwalimu. Hii ni General Judgmental ambayo kila mtu anaweza kufahamu huwezi sema Mwl. Mwakasege ni Muinjilisti hata kama bila shindano Ukianza Kutaja Waalimu Wa Neno la Mungu huwezi mtaja Bishop Kulola. Haiitaji uwe ulimwengu wa Roho kusema fulani ni Mwalimu, fulani ni Muinjilisti, fulani ni Nabii. Is the same to Worshiper unless huwezi kutofautisha a worshiper from normal Singers.

  Hao mnao waona sasa hivi sio zoezi limeanza leo. Baada ya Mchujo wa Mara ya Kwanza hawa watu wamewekwa Kambini ambako kuna Waalimu Kabisa Wanawafundisha how to sing. Wimbo gani ni Wimbo Wa sifa, Wimbo gani ni Wimbo Wa Kuabudu, Wimbo gani ni Wimbo wa Kawaida, Wimbo gani ni wimbo wa Kutia Moyo. Mbali na Kufundishwa Kuimba wanafundishwa ni Kwa namna gani Worshiper anatakiwa kuishi huwezi kuwa Worshiper kama huna neno la Mungu Wala Huna maombi, a worshiper cannot separated from the Word of God and Prayer. Huwezi kumwabudu Mungu kama Huna Neno la Mungu. Mbali na hapo Wanafundishwa Kuomba. For a Worshiper to write songs it depends his or her intimacy Relationship with God.

  Mwisho wa siku Waimbaji wote 10 sijui 15 Watatengeneza Albam yao ya Worship Songs Collection na yule atakayefanya vema zaidi (mshindi) ata record Albam ya Audio and Video. Mchakato huuu wote Hakuna fedha kutoka kwa Waimbaji wala Raia Wa Kawaida kwa Sasa. Nia ya mwenye maono kuwepo na Watu ambao Wakipata Nafasi Tanzania iwe na Worshipers. Lakini hata wale ambao watakuwa hawajashinda Watakuwa impacted Kiroho, kwa kujifunza kuabudu, neno la Mungu na Maombi.

  Binafsi simo kwenye Kamati lakini nilitamani Kujua kwa Kina Nini wanachofanya nini makusudi yao, na nikasaidia pale ninapoweza kusaidia kama hawatafuata ama watafuata hilo halinihusu sana ila Kile ambacho Mungu aliniambia nisaidie nilisaidia.

  Inawezekana Kile Wanachofanya ni Kibaya kwa Mtazamo wetu lakini Kama Jambo lenyewe Linaleta Impact kwenye maisha ya Watu Kiroho hilo Jambo kwangu nila Kiroho. Kuandika mitandaoni na Kukosoa na KUJUA KILE tunachopaswa kufanya na tusifanye basi Mungu atanyanyua Mawe yafanye.

  Huu ni Mchango wangu wa Ufahamu Wangu mdogo kuhusiana na Jambo hilo kama kuna mawe ya kurusha na yarushwe maana najua mpaka Yesu anarudi hatutakuwa tunakubaliana katika kila jambo, our Differences isn Not Enmity and Unit is not Iniformity.

 31. Mimi ni kati ya majaji/ na kamishna wa mashindano ya kuimba (sisemi mashindano ya kusifu na kuabudu). Ninapotangaza mshindi huwa nawaambia kuna zawadi za aina tatu
  1. Zawadi ya kupigiwa makofi na watu waliohudhuria ukumbini
  2. Zawadi ya kuwa mshindi wa kwanza/pili/tatu nk
  3. Zawadi ya kukutana na Mungu

  Sasa zawadi ya kwanza inatokana na jinsi, ulivyowafurahisha watazamaji kwa kuvaa, kutoa sauti nzuri au jinsi ulivyo maarufu kwao, watakupigia makofi au kukutuza kwa sababu hizo- hizi ni zawadi za kijamii (social rewards)

  Zawadi ya pili inatokana na namna ulivyofuata sheria za kuimba: kufuata ,mapigo, kumwangalia mwongozaji, kutii masharti ya noteni, na masharti ya jukwaa nk- hizi ni zawadi za kimaonyesho- (perfomance rewards)

  Zawadi ya tatu ni namna Roho yako inavyoimba (kuabudu katika Roho na Kweli), hapo ndipo Mungu atakulipa kadri ya mapenzi yake na haja ya moyo wako.

  Sasa kwenye mashindano hayo, si lazima upate zote. unaweza ukapata moja au ukakosa zote.

  Kwa uzoefu wangu, mashindano haya yanaimarisha sana UTAALAMU WA MUZIKI, lakini kiroho yako chini sana. Mara nyingi yanachochea wivu, uadui, na chuki katika ya vikundi na vikundi na hata vikundi na waamuzi.

  Nadhani kuna namna ambayo yangeweza kuboreshwa, ili kuyaweka yawe na tija kiroho.

 32. Jamani mimi sikerwi tu na mashindano yakusifu na kuabudu lakini hata ingekuwa mashindano ya kwaya bado si halali,hivi hao wanaokwenda kushindana ,wanamuomba Mungu gani,na anakemea wenzie washindwe ili yeye ashinde ? ”kushindana kwenu si juu ya damu na nyama” biblia iko wazi kabisa,kwa kweli zamani mashindano ya kwaya yalikuwa tu kwa madhehebu fulani lakini sasa hata walokole,ama kweli tuko mwisho wa mambo yote.

 33. Ndugu SAMSASALI Bwana Yesu asifiwe!

  Mimi binafsi sina maelezo ya kutosha kuhusu neno shindano, kwanza na kiswahili changu siyo cha ndani kabisa ila neno hili nadhani ya kwamba ni kazi inayo fanyika kati ya watu zayidi ya 1 ili kwa kazi hiyo awonekane ni nani amefanya kazi hiyo vizuri kuwashinda wengine.

  Sasa kwa topic hii nimekuona juu ukisema ni NI KIROHO: Kama uko karibu ningependa unielezee kwa marefu vipi mashindano haya ni ya kiroho. Samahani sana sijapinga hata kidogo, napenda nikuzwe na kujengwa kiroho na wandugu ktk Kristo.

  Ninakusubiri sana kwa hamu na Bwana Yesu Kristo akubariki sana.

 34. Nakerwa na waandaji kukazania waimbaji peke yake. Tunataka wajitokeze waandaji wa kutafuta watumishi wengine,wanaonena kwa lugha kuliko wengine, wachungaji, mitume, wainjilisti, mitume nk.

 35. Bwana Yesu asifiwe sana!
  Wapendwa hili ni jambo la kushangaza sana; biblia inasema kwamba Bwana anataka watu wamuabudu ktk Roho na kweli, sasa ni nani anaweza kumu judge Roho mtakatifu? Biblia iko wazi kabisa, huwezi kumchunguza Roho lakini yeye huchunguza watu wote.
  Tujihadhari sana kumuabudu Bwana siyo mchezo wa kuigiza bali ni kazi ya Roho wa Mungu anayo yifanya ndani yetu. hapo ndipo tunaabudu sawa sawa na mapenzi ya Jehovah.
  Tukumbuke ya kuwa wote wanao ongozwa na Roho wa Mungu ndiyo wana wa Mungu, kwahiyo siyo sisi wa kumuongoza Roho mtakatifu bali yeye wa kutuongoza na kama siyo yeye kutuongza, tunaongozwa na mapenzi yetu wenyewe! sasa tukifanya mashindano ya kusifu na kuabudu maana yake tunataka tuonekane sisi wenyewe na hiyo ni hatari kubwa!!!
  Hebu wa ndugu tujiulize, kwa nini Yesu Kristo aliwakataza wana funzi wasitoke Jerusalemu kabla ya kupewa uwezo wa Roho mtakatifu? kuna sababu kubwa!!!!
  Tunapo fanya kazi ya Mungu Tunapenda sisi tushuke chini sana na Bwana aliye ndani yetu ainuliwe sana, sasa tukienda ktk mashindano kila mmoja wetu ataka kuwa wa kwanza yani awonekane yeye ni wa mbele ya wote, sasa mbona Yesu ni mmoja atakubari kujigawa ilin sehemu yake moja iwe ya kwanza na nyingine ya mwisho? la hasha!! kumbe kwenye mashindano ni sisi wenyewe na tama zetu na ni upotevu mkubwa.

  TUMPE NAFASI ROHO MTAKATIFU ATUONGOZE KULINGANA NA MAPENZI YA BABA WA MBINGUNI NA HIYO NI SIRI YA MAFANIKIYO KAMIRI.

  SHALOM? SHALOM!!

  Ev. Emmanuel NSHIMIRIMANA kutoba Bujumbura Burundi

 36. Amen sister Grace, Mimi naona si la ki Roho kabisa, kwani kwa kufanya hivyo wana prays watakuwa wanafanya kwa kuigiza ili washinde na sio kuimba ktk uwepo wa Mungu. Labda libadilishwe jina ili tusi haribu utendaji wa Mungu.

 37. Wamwabuduo Bwana wanamwabudu katika Roho na kweli. mimi ninachoona hapa anaweza kuabudu kwa roho lakini ili kushawishi majaji lakini si katika kweli. bado najifunza kutoka kwenu wadau

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s