Mchungaji Mtikila asema Yesu amemjibu, ashinda kesi!

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika  maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema “Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu”.

Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.

–GPL

Advertisements

17 thoughts on “Mchungaji Mtikila asema Yesu amemjibu, ashinda kesi!

 1. Ndugu zangu wapendwa,

  Je Mmeona Makanisa yanavyochomwa moto?

  Mabishano ya kitoto endeleeni nayo tu,

  Mbarikiwe,

 2. Chondechonde watakatifu wa Mungu ambao tuna uwezo wa kuingia kwenye siasa, nawasihi tuingieni kwenye huu uringo wa siasa tukatende haki ili tuinusuru nchi yetu. La sivyo historia na watoto wetu vitatuhukumu!

  Mwenye haki akitawala watu wote hufurahi!

 3. Mabinza rafiki yangu,hata mimi kuna wakati huwa namkosoa Mtikila katika utendaji wake. Kwa mfano wakati wa uchaguzi mdogo wa Tarime mwaka 2008 kama sikosei alipigwa jiwe na watu wa huko kwa sababu ilionekana kutumiwa na CCM kwa njia ya kificho. Baada ya uchaguzi alikuja akatubu mbele ya baraza la maaskofu akasema alipewa hela ili kupinga CHADEMA. Ni kweli kuna wakati huwa anakosea.

  Ili sasa wewe unavyojenga hoja yako kuhusu utumishi wake wa siasa na Mungu na jinsi unavyoyatumia maandiko si sawa.

  Kusema Yesu hakuwahi kufanya kazi za siasa kwa nini yeye (Mtikila) anafanya ni sawa na kusema Yesu hakuoa kwa nini watumishi wa Mungu( hasa huduma tano) wanaoa.

  Mawazo hayo yamesababisha kanisa liwaachie wasiomcha Mungu utawala wa nchi, kwa kujidanganya kuwa siasa na dini haviwezi kwenda pamoja. Halaf eti tunapoteza muda kuomba kwa ajili ya watawala wetu watende haki,hiyo haki tunayotaka watende wataitoa wapi wakati ndani yao hakuna kicho cha Bwana?- huu ujinga mkubwa sana tunafanya kanisani leo

  Tumedanganywa nasi tukadanganyika kwamba siasa ni mchezo mchafu hivyo si kazi inayowafaa wana Mungu. Ningependa wapendwa tujue jambo moja kuwa hao wanaoitwa wanasiasa ndio wanatufanya tuwe hivi tulivyo. Ni vigumu sana kuwatofautisha watu na siasa za nchi yao.

  Kwenye ofisi za kisiasa ndiko kunakotoka amri za jinsi tunavyotakiwa kuenenda. Wanasiasa wakisema kuabudu mwisho saa 12 jioni wanaofanya mikesha wajue huo ndio utakuwa mwisho wa kufanya mikesha katika hii nchi. Wanasiasa bwana!

  Yesu alikaa duniani miaka 33 tu,kuna mambo mengi sana hakuyafanya kwa sababu ya muda, ambayo sisi yatupasa kuyafanya kwa sababu tuna muda mwingi wa kukaa hapa duniani.

  Mchungaji mtikila kasaidia mambo mengi sana katika hii nchi hasa ya kisheria( soma Tanzania Law Report- kumbukumbu za kesi mabalimbalizilizofanyika Tanzania) na kutetea ukristo

  Mungu amsaidie mchungaji Mtikila Christopher.

 4. Nduta,
  Unaonaje, akitokea Mtu mzima aliyekwisha kuwapoteza watu wazima wakatoka katika kweli na sasa anakuja ili kuwapoteza watoto wadogo nao watoke katika kweli? Hujui hila ya Shetani anayoitumia kupita Siasa, siku ukijua utaweza kulia hata machozi!

  Swali la kwanzai, unadhani kwanini Yesu alikataa kufanywa mfalme hapa Duniani?

  swali la pili, kumbuka yesu hakufanya kazi ya siasa za Duniani sasa, kama Mtikila ameajiriwa na Yesu ili afanye kazi shambani mwa Bwana, lakini wakati huo huo hafuati alivyofanya Mwajiri wake katika kuliendeleza shamba husika. Je,atakuwa mtumishi BORA?

 5. Wapendwa,

  Mtikila anafanya kazi za watu wazima kiroho (Warumi 8: inasema “the whole creation yearns for the SONS of GOD to be revealed. Yaani uumbaji wa Mungu aunaugua kutamani udhihirisho wa wana wa kiume siyo wavulana.) ninachotaka kusema ni kuwa zipo kazi ambazo zinaweza kufanywa na watu wazima na haziwezi kufanywa na watoto wadogo, kwa kuwa watoto wadogo wanawaza kitoto na ubishi wa kitoto wala hawana la kujifunza kwao.

  Mtikila hongera sana kwa kutetea ukristo.

 6. Mr.Milinga,

  salaam, katika kusema ya “ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe mungu” nilimaanisha kuwa, mtu hatafika aendako akifuata njia mbili kwa wakati mmoja na hata kama akiziona njia hizo ziko sambamba namna gani, ni tabia ya njia kufanya sulubi! vivyo hivyo huwezi kutumikia mabwana wawili kwa utii sawa! samweli alilalamikia jambo kama hilo la ‘kisiasa’ lakini Mungu akamwambia samweli kuwa “……hawajakukata wewe wamenikataa mimi…..”

  Tawala za Duniani ni tete kwasababu ni wachache katika viongozi wanaokubali kutii ya Mungu! Kwa kifupi nilimaanisha Mtikila ashikilie moja kama Siasa iwe siasa na kama ni kazi ya Mungu, afanye Ya mungu! Hebu angalia, Mtikila katika chama chake nasikia ni mwenyekiti (sina hakika) na Kanisani ni Muchungaji, KOTE MKUBWA ataongozaje mashua mbili – Ukiwa Dereva wa Basi la abilia na wakati huohuo ni nahodha wa Meli, ni lazima uchague unakotaka kwenda kwanza! Umenielewa ndugu yangu?

  Nduta,

  kama Mtikila anaongoza watu wazima na si watoto kiroho, yeye na wewe mjue kuwa Neno la Mungu liko wazi kwa “watoto wachanga!” Sasa asikilizwe nani ambaye Neno limefunuliwa kwake au kwa Mtu kiongozi wa watu wazima kiroho?

 7. Nampongeza sana Mchungaji Mtikila. Mchungaji anafanya kazi za watu wazima (Sons) na isyo watoto wadogo kiroho. Anafanikisha mambo makubwa kiroho kwa ajili ya kanisa. Mungu ambariki sana.

 8. shalom mtumishi hongera sana Bwana ametenda, Bwana huonekana kwa wamtumainiao ubarikiwe palipo ukweli uongo hujitenga.

 9. Mabinza,

  Nini maana ya maneno hayo uliyosema, “Ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu”? Katika mada hii una maana gani. Una maana gani?

  Natamani kupata maelezo yako.

 10. Rosemary,

  Mawazo yako Rosemary upo sawa, ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Lazima Mtikila achague kimoja, na wala kushinda kwake kesi mimi kwa mtazamo wangu asikuhusishe Yesu, maana watu wanapofikishwa mahakamani huwa hawatoi utetezi wa weli ya Moyo, wengi hudanganya kwa kinga ya sheria. Maandiko yanasema “Haiwezekani kumpendeza Mungu kwa matendo ya Sheria!”

  Mahakama imeshindwa kumtia hatiani kwa kuwa Tuhuma dhidi yake haikuweza kuthibitishwa “kisheria” Kigezo kikubwa cha sheria katika tuhuma ni ‘Ushahidi’ Lakini, katika hukumu ya Mungu kigezo kikubwa ni ‘Haki’; na haki haiwi haki pasipo na ukweli!

  Sasa mtikila anachokisema ni mawazo yake, maana ajuaye kwamba alisema kweli tupu katika utetezi wake ni yeye mwenyewe na Mahakama!.Yeye mwenyewe (Mtikila) anakili wazi kuwa Mahakama inakubali kuwa alitamka ‘mambo mazito’ Sasa, kumdharau kiongozi wa Nchi si kumdharau Mungu? Maana diye aliye muweka katika madaraka yale!

  Kama Yesu ndiye Mungu wa wacha Mungu wa kikwelikweli. Je, Mtikila kabla ya ile hukumu alikuwa akiongea na Yesu yupi?

 11. Shalom mimi nimeshauri abaki kuwa mwanasiasa lakini kwa kufanya kazi ya kuchunga na hizi kesi nyingi mara kufungwa kondoo watakuwaje? Ni mwanasiasa mzuri na mpenda haki ila kuwa na kazi ya Bwana tena mie naona hapana

 12. Rosemary asiye nadhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe. Tunahitaji wanasiasa kama hawa kutoka kanisani

 13. Hivi huyu ni mchungaji wa kanisa au? mimi naona angeendelea tu na siasa kazi ya Bwana haimfai kutokana na mambo yanayoripotiwa juu yake. Ni mtazamo tu.

 14. mimi nilitegemea angeshinda ile kesi pamoja na kwamba kuna mambo huwa siyaelewi kwa huyu Mchungaji.Yeye na Mrema huwa wanashinda kesi nyingi sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s