Dansi ndani ya Biblia!

Uimbaji ni ibada ya kumsifu Mungu. Ni ibada kama zilivyo ibada nyingine kama kusoma/kujifunza Biblia, kuomba/kusali  nk. Kwa maneno mafupi, ni uijilisti unaoshughulika na nafsi ya mwimbaji/waimbaji wenyewe na wasikilizaji. Kwa sababu ni ibada nyeti sana, uimbaji unapaswa kufanywa kwa KICHO CHA UCHAJI MUNGU.

Dansi ndani ya Biblia.

Je, ndani ya Biblia kuna michezo au dansi? Kama ni ndiyo ni michezo au dansi gani na ilichezwa wapi? Chanzo chake kilikuwa ni nini?? Je, Biblia inaturuhusu kucheza?

Ndani ya Biblia kwa mara ya kwanza, wanawake wanaonekana wakicheza (Kutoka 15:20,21) Miriamu akiwa na tari mkononi mwake…(Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza, Miriamu akawaitikia…) Tunaambiwa kuwa Miriamu na wanawake wengine walicheza. Neno la kiebrania lililotumika hapa ni ‘ Mihola’ ambalo humaanisha kutembea katika duara. Pia chunguzza tafsiri ya Biblia ya King James Version imetumia maneno ya matari na machezo timbrels and dances/chuwls (vyombo vya kutoa sauti kwa kupuliza kama vile filimbi, vinubi nk). Mihola humaanisha kutembea(matching) kwenye  mistari miwili katika mduara.

Hivyo wanawake waliomfuata Miriamu nyuma walikuwa wakienda kwa matching na siyo kwa kurukaruka na kunengua viuno. Aidha, ikummbukwe kuwa, wanawake hawa hawakua kwenye ibada kanisani bali walikuwa safarini tu kutoka Misri utumwani kuelekea Kanaani. Maana iyohiyo ya neno hili ‘ Mihola’ limetumika pia katika 1 samweli 18:6 na Waamuzi 11:34.

Mbona kuna ibada za kucheza ndani ya Biblia?

Ni kweli. Katika Kutoka 32:6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. Tukio hili lilifanyika baada ya uasi dhidi ya Amri za Mungu. Ndama alitengenezwa kinyume cha maagizo ya YEHOVA (Usijifanyie sanamu ya kuchonga…kutoka 20:4-6). Neno kucheza lilivyotumika hapa siyo sahihi. Neno la Kiebrania lililotumiwa hapa ni ‘ Sahak’  lenye maana ya kumcheka mtu fulani, kumdhihaki au kumtukana.

Hapa dhihaka ilikuwa ni kwa Mungu kwa sababu ilionekana kuwa Mungu ameshindwa kuwapeleka Waisraeli Kanaani na hivyo sasa waliamua kurudi Misri na mungu wao wa kuwarudisha huko alikuwa ni ndama wa dhahabu.  Wapendwa, kucheza dansi la Yesu ndani ya kanisa au ibada ni UASI.

Mbona Daudi alicheza mbele za Bwana??

Ni kweli. Katika 2 Samweli 6:14 tunasoma (Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani). Neno la Kiebrania lililotumika hapa ni ‘ karar’ lenye maana ya kurukaruka na kuzungukazunguka (leaping and whirling) na siyo sarakasi, minenguo ya viuno nk. Zingatia mambo yafuatayo kwa Daudi:

a.     Daudi hakuwa na maandalizi yoyote ya namna ya kucheza kama ilivyo leo kwa baadhi ya kwaya za injili kwenye makanisa yetu. Alirukaruka na kuzuzngukazunguka kama mtu anayepata furaha baada ya kufaulu mtihani, kupata mtoto, kupanda cheo nk. Ni furaha ya papo hapo tu. Daudi alipata furaha ya papo hapo tu na ambayo haikuwa endelevu kwa baadaye.

b.    Hakuwa na timu ya watu ambao walifanya maandalizi pamoja naye ya namna ya kurukaruka na kuzungukazunguka.

c.     Hakuwa hekaluni au kwenye mkutano wa ibada au mafundisho yoyote ya neno la Mungu. Daudi alijua fika kuwa ndani ya nyumba ya Bwana hakuna kurukaruka na kuzungukazunguka maana imeandikwa, Habakuki 2: 20 Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake

d.    Daudi hakucheza kama sehemu ya ibada mbele za Mungu

Na katika kitabu cha Zaburi 149:3 na 150:4 dhana  ya ‘maholi imejirudia tena hapa.’. Angali Zaburi

150: 3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa  kinanda na kinubi;

        4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

          (Mstari wa 4- kwa matari na machezo ambacho ni chombo                        

           cha muziki) 

NB:

Ikumbukwe kuwa neno kucheza kwa Kiswahili na dance kwa kiingereza hayana maaana sawa na ile iliyotumika kwenye lugha ya Kiebrania, lugha ambayo Biblia iliandikwa kwayo. Kwa mujibu wa zaburi na baadhi ya vitabu vingine ndani ya Biblia, neno kucheza lina maana ya “ maholi – matching katika mduara huku mkipuliza vyombo vya muziki vinvyotumika katika kumsifu Mungu.

Ieleweke kwamba, wahubiri na wanakwaya wanaosisitiza watu kucheza ndani ya hekalu au ibada, wako kwa ajili ya kutimiza kiu yao ya kucheza dansi ya dunia huku wakiivika dansi yao vazi la Kikristo. Kwa maneno mengine, kile kinachofanywa na watu hawa siku hizi ni “Upagani Mambo Kikristo”. Dhana ya uimbaji kama ibada ya kumtukuza Mungu haipo tena. Ibada ya uimbaji halisi alioneshwa nabii Isaya

Isaya 6: 2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

 3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

 4 Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi. 

Angali ndugu yangu mkristo, Malaika wamnamsifu Mungu kwa kufunika nyuso zao na miguu yao….  Ibada ya heshima kiasi gani!!!! Linganisha na leo watu wanavyovaa vimini, vitight nk halafu na kudansi madhabahuni eti wanamwimbia/kumchezea Mungu!!! Mimi nesema kuwa ni kweli wanamchezea (kwa maana ya kudhihaki na kumbeza) Mungu. Lakini wakumbuke kuwa Mungu hadhihakiwi…

Kama unamchezea Bwana, acha. Fuata taratibu nzuri za kibiblia za kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo na si vinginevyo.

Mwisho Shetani amefanikiwa hata kuichakachua Biblia. Biblia hiyohiyo uliyo nayo, HAIKO SALAMA NDG YANGU. Nakuchokoza kidogo tu. Hebu jaribu kulinganisa mafungu haya;

KJV-King James Version           NIV-New International Version    RSV-Revised Standard Version

Mathayo 24:36                                          Mathayo 24:36              Mathayo 24:36

Warumi 8:1                                              Warumi 8:1                    Warumi 8:1

1 Yoh 5:8                                                 1 Yoh 5:8                       1 Yoh 5:8

Je, mafungu yote haya, yanafanana???  Kama sivyo ni kwa nini?? Je, unafikiri Biblia ya Kiswahili ilitafsiriwa kwa kutumia Biblia gani kati ya hizo hapo juu??? Usiwe KINDA, chunguza na wewe!!

Naomba kuwasilisha!!

Michael Nzala

Advertisements

18 thoughts on “Dansi ndani ya Biblia!

 1. hii mada ukileta umadhehebu/udini tatizo..mimi binafsi sipendi udini,.je wewe unaejiita mroma,mrutheri,msabato nk shida ni nini??
  yakobo 1;26-27.
  mtoa mada katoa mada vizuri sana kuhusu kusifu ila kuna watu wameleta udini,.dini haimpeleki mtu mbinguni,.muhimu ni kumjua YESU,kumkiri na kubatizwa na maji mengi then kuishi kama tulivyoamriwa na YESU hapo ndo ticket ya kwenda mbinguni,.
  kuna vipindi vitatu navyotaka kuzungumzia KUHUSU HII MADA,.
  1.kipindi cha tora ambacho Mungu alikuwa akihukumu directly,na kutoa hukumu moja kwa mojakwamoja ,kipindi hiko kilikuwa ni jicho kwa jicho,jino kwa jino,.na ilikuwa ruhusa2 kutokea hayo mambo,.
  ukisoma kutoka 28;1 na kuendelea utakuta yakobo jinsi gani alivyomtumikia labani miaka7 ya kwanza kwaajili ya raheli(rachael)ila baadae yakobo akapewa lea badala ya raheli,…yakobo akalala nae na kumzalisha lea,.then yakobo akamlalalmikia laban kuwa yeye anamtaka raheli,.then akatumika tena miaka7,.kile ni kipindi cha torah,.na akina daudi,miriamu walisifu kwa desturi zao za kiisrael,kipindi hiko,.huwez kuniambia mimi nisifu kama daudi,..
  2.kipindi cha pili ni YESU kuwepo duniani,.na alifanya mengi tu na kutupa njia pana na kutuletea mataifa mengine ya ulimwengu injili juu ya Kumpokea YESU na kumwamini yeye kama njia ya kwenda kwa BABA(YAHWE)baada ya wayahudi kumkataa.wale wanafunzi wake YESU walikuwa wayahudi washika dini,.ila YESU aliwafundisha kuomba,mathayo 6;39,.sio kwamba walikuwa hawajui,ila ni formation mpya ya YESU
  so,YESU alikuja na kutupa maisha mapya ya kuishi katika kumtegemea yeye,.na alisema kuwa yeye ni Bwana wa sabato,.so wewe unajiitaje msabato??????
  point ya hapa ni kuwa kile kipindi cha pili ni ulikuwa msimu wa YESU Kutawala direct akiwa na wanadamu,na mwenyewe aliimba pia
  3.kipindi hiki cha sasa ni kipindi cha roho mtakatifu,.tumempokea YESU NA YESU yupo mioyoni mwetu,.tunaongozwa na roho mt.kama msaidizi wetu,.so kila jambo tunalofanya,tunalowaza nk,uongozo wa roho mt. unatuongoza directly,.so tuliokoka kila jambo tunaongozwa na roho mt.,
  kucheza kanisani ni jambo sahihi,.maana upako ukikushukia,nguvu za MUNGU zikiwa juu yetu chini ya uongozi wa roho mt. kila kitu kinakuwa undercontroll chini ya uongozo wa roho mt.
  kuhusu rose muhando na wengine mliowasema,je wameokoka???????
  je kabatizwa kwa maji mengi??????
  je amejazwa na roho mt????
  mtu aliokoka na kujazwa na roho mt. unamjua kuanzia matendo,utembeaji,uzungumzaji na kila kitu,…so cheza ya mtu fulani angalia kuna UMUNGU ndani yake,…kama hakuna basi uyo ni mpagani tu wa kawaida
  tuzingatie mathayo 12;8
  barikiwa…………

 2. watu wanafanya kila wawezalo kuifanya dhambi kuwa halali mbele za watu, kwa kisingizio cha rohomtakatifu,,lakini kila kilicho chema kinajulikana, na hakina maswali ya kwanini. je roho mtakatifu anapingana na torati ambayo mungu kaiweka?

 3. Siyi,

  Ibada ni nini na kucheza au kudensi ni nini?

  Kama kwenye ibada hakutakiwe kuwe na kudensi, kudensi kunatakiwa kufanyikie wapi?

  Halafu unaposema Mungu anataka wanadamu na viumbe wamwimbie kwa kunukuu neno lake, unamaanisha neno lipi- lililoandikwa kwenye maandiko au neno la ufunuo linaloletwa na Roho mtakatifu?

  Kwani wakati wa akina Daudi kulikuwa na mistari yenye kusema ‘mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema kwa maana fadhili zake ni za milele’ basi? Maana tunaona katika sehemu nyingi za matukio ya uimbaji hicho ndicho waliimba.

  Neno la Mungu si lile lilliloandikwa tu, bali Mungu bado angali akisema hata leo ndani ya mioyo yetu kwa njia ya Roho mt. Ndio maana neno la Mungu liko katika makundi, yaani Logos, na Rhema.

  Kwa wimbo ninapoamua kuyasimulia matendo makuu ya Mungu maishani mwangu, obviously, nitaimba aliyonifanyia mimi siyo aliyomfanyia Musa, au Daudi, au Eliya, au Paul, kwenye biblia.

  Ndio maana Roho mt. yupo leo!

 4. Watu wa Mungu bado wamefunikwa na giza la shetani wasione wala kusikia, Tunahitaji sana mafundisho matakatifu na yaliyo ya kibiblia kama nilivyoona hapo juu, nasio yaliyo ya wanadam kama wahudum wengi wanavyofanya kwenye makanisa yaleo. Mungu akubariki sana.

 5. Uimbaji wa Watakatifu
  Mungu hukufurahia kuimbiwa na viumbe vyake –Sefania 3:17. Aidha, Yesu mwenyewe alikuwa akiimba nyimbo- Mtt 26: 30 “Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni”. Kwa uwezo wa Mungu, viumbe wa mbinguni huimba wakimsifu YEYE aliye wa milele. Viumbe hawa wamegawanyika katika madaraja- maserafi, viumbe vinne vyenye uhali vilivyo mbele ya kiti cha enzi wakikizunguka nk. Lengo langu si kuchambua madaraja hayo ya viumbe wa mbinguni bali ni kuonesha namna viumbe hao jinsi wanavyomsifu Mungu kwa nyimbo za sifa. Isaya alishangaa kuwaona viumbe hao jinsi walivyokuwa wakimsifu Mungu…
  Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi. Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi. Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu; akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa. Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi. Isaya 6:1-8

  Hata Yohana anaye alishangazwa sana jinsi viumbe wa mbinguni walivyokuwa wakimsifu na kumshangilia Bwana.. “Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye. Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. Ufunuo wa Yohana 4:6-8

  Angalia mambo ya msingi yanayojitokeza hapa
  1. Maserafi wanapoimba wakimtukuza Mungu, hufunika nyuso zao kwa mbawa zao mbili ili kuonyesha heshima, kicho na utii mkuu mbele za Mfalme – Mungu muumbaji. Kumbuka kuwa, hawa ni viumbe wasioijua dhambi(hawana mawaa mbele za Mungu). Kama hawa viumbe wanaimba kwa sifa na utulivu kiasi hiki, swali la kujiuliza, ni jinsi gani wanadamu wenye dhambi wanapaswa kuwa na heshima, kicho, unyekekvu na uchaji mkuu mbele za Mungu wakati wa kuimba na kumsifu? Waimbaji wote wanaomwimbia Mungu, wanapaswa kuwa watakatifu na wenye kumwogopa sana Mungu pindi wanapotoa huduma hii takatifu. Mungu hawezi kukubali huduma za uimbaji isipokuwa waimbaji wameguswa kwa kaa la moto-RM mioyoni na vinywani mwao.
  2. Jambo lingine, waimbaji wengi hujitungia nyimbo kutoka kwenye mawazo na akili zao tu, jambo ambalo Mungu halikubali. Mungu anahitaji wanadamu na viumbe wake wamwimbie kwa kunukuu neno lake takatifu. Maserafi, huimba “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana wa Majeshi, dunia yote imejaa utukufu wake…” Na Mungu hupendezwa na ibada za nyimbo za hawa maserafi. Daudi aliimba nyimbo nyingi sana kwa kunukuu na kurudiarudia neno la Mungu. Ingekuwa ni wanadamu wa kizazi chetu hiki, wimbo huu ungekuwa ulishawakinai na hivyo kuamua kujitungia nyimbo zao, kama ilivyo sasa. Ndani ya Biblia, hakuna aliyejitungia wimbo wake mwenyewe. Waimbaji wote waliimba kwa kukariri maneno ya Mungu.
  Nyimbo za kwaya zinaweza kuwafanya watu waanguke mbele za Mungu wao na kumtafuta hata kwa machozi. Nabii Yohana anasema kuwa na Hao wenye uhali wanne wanapompa utukufu YEYE aketiye juu ya kiti cha enzi, ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake YEYE aketiye kwenye kiti cha enzi na kumsujudia YEYE aliye hai milele na milele “Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele, ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa. Ufunuo wa Yohana 4:9-11
  Huu ndio uimbaji Mungu anaoutaka kwa viumbe vyake. Katika Ufunuo 4:8 tunasoma kuwa “Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja”. Ukiangalia vizuri, hawa maserafi wanatangaza sifa, uwepo na ukuu wa MUNGU tangu milele zote. Aidha, nyimbo zao, zinatangaza ujio wa Kristo kwa mara ya pili-“ Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja”. Nyimbo za hawa viumbe ni kuuambia ulimwengu ulioasi na usiotambua uwepo, na ukuu wa MUNGU, kuwa YEYE yupo na siku si nyingi atakuja kuuangamiza ulimwengu huu na kuwaokoa wanaompenda kwa moyo wa dhati.
  Tafakari nyimbo za waimbaji wetu wa leo!! Nyimbo nyingi ni za kujiinua wao wenyewe, maisha yao, na Mungu hakumbukwi tena. Maduka mengi yamejaa albamu zinazoelezea maisha ya watu, historia zao, mikasa yao maishani na kutiana moyo tu. Kumshangilia Bwana licha ya mapito tunayopitia hakupo tena.
  Kila mtu anao uhuru wa kulitii au kuliasi neno la Mungu. Mungu halazimishi mtu ayatii maneno yake. Mungu hupendezwa na utayari wetu(our willingness) na utii wetu kwa Neno lake.

  Wito
  Turejee kwenye mwonekano wa maserafi katika kumtukuza na Kumsifu Mungu kwa nyimbo. Kama maserafi hufunika miguu yao, nyuso zao kwa mbawa wakati wa kumsifu Mungu, vivyo hivyo na waimbaji(wanakwaya) wanapaswa kuvaa mavazi ya heshima waimbapo mbele za Mungu. Nguo fupi na zenye kubana, uvaaji wa suruali/masheti ya kiume kwa wanawake au sketi/blauzi kwa wanaume ni machukizo mbele za Mungu-torati 22:5. Inashauriwa mwimbaji au kwaya-waimbaji wavae majoho wakati wa kuimba. Waimbe kwa kicho, kutulia, unyenyekevu na heshima na siyo miruko na dansi kama walivyocheza waasi na waabudu sanamu. Mungu anapoagiza jambo huwa hapendi mjadala wala visingizio. Waimbaji leo wangemwelewa Mungu, huduma zao zingekuwa na utukufu mkubwa sana mbele za Mungu tofauti na ilivyo sasa.
  Mungu anapoagiza jambo huwa anahitaji utii-utekelezaji tu basi, japo utekelezaji huo huwa siyo wa lazima. Lakini pamoja na hayo kutekeleza ama kutotekeleza, vyote kwa pamoja vina malipo stahiki. Mf.
  1. Mungu aliposema ukiasi sheria zangu hakika utakufa, daima umwagaji damu ulihitajika kwa mdhambi yeyote aliyeonekana kuvunja sheria za Mungu. Kondoo, mbuzi, mafahari wasio na hatia walibebeshwa adhabu hiyo ya mauti ili neno la Mungu litimie ya kwamba, mshahara wa dhambi-mauti.
  2. Kuhani mkuu alipoingia madhabahuni kufanya huduma ya upatanisho, alifungwa kamba kiunoni kiasi kwamba akifia huko, wamvute tu na siyo mtu mwingine kuingia huko eti anaenda kutoa maiti. Kama kungekuwa na sababu ya kuvunja sheria hii, basi hii ya kwenda kutoa maiti ilikuwa sababu tosha kabisa. Lakini Mungu haangalii kama tuangaliavyo wanadamu.
  3. Uza alipoliona sanduku la agano linataka kuanguka, aliamua kumsaidia/kukiuka agizo la Bwana. Badala yake tunaona sanduku halikuanguka lakini yeye alianguka akafa palepale. Nk
  Brethrens, God has NO execuses!! Sharti tutii na kufuata neno lake tunapokuwa katika huduma nyeti za kumwabudu kama uimbaji.
  M-barikiwe nyote.

 6. Lwembe

  Ha ha ha ha!!

  Kwanza, Kunena kwa lugha uko sahihi kabisa hata mimi nanena kwa lugha tena sana tu. Suala la msingi ni kuangaliaunanenaje? Kibiblia au kichawi? Maana hata wachawi na wasihiri, nao hunena kwa lugha. Wewe kama unanena kwa lugha kusikotajwa na Biblia, acha kujifariji hapo. Umeliwa kekundu kaka.

  Pili, Na kuhusu uponyaji wa kiMungu na ishara nyinginezo, mbona tunaamini tu!! Wewe hujui hilo? Wasabato tunaamini sana ktk hayo. Shida yako hujui kama tunaamini kuwa nguvu za Mungu ziko juu yetu na huwa zinajidhihirisha kwetu wakati wote. Usihofie ktk hilo. Tuko sawasawa kabisa. Wewe kama unabisha, jaribu uone.

  Tatu, hatuamini ktk uongo wa mwaka wowote ule!! Kama wewe unajua kuwa tuna uwongo wa 1800’s tunauamini, dhibitisha ili ueleweke kwa watu!!

  Nne, Wasabato hawakuanza miaka ya 1800’s. Ibada zetu zooote, iwe ni kwa njia ya kujifunza neno, nyimbo, matoleo, nk hufunikwa na heshima na utukufu kwa Bwana Mungu wetu na siyo micharuko ya dansi za bongofleva au awilo!! Katika suala la Ibada, wasabato, hatubahatishi kaka. Tunamwabudu Mungu kibiblia haswaaa!! Kama wewe unahalalisha dansi kwenye ibada, haya songa mbele. Lakini kumbuka kuwa, ndani ya Biblia, hakuna hata mtu/jamii au taifa lolote, lililocheza dansi, dansi ya kukata na shoka mauno, mauno, makelele na sarakasi wakiwa kwenye nyumba ya Mungu ya Ibada, tena wakati wa ibada!!!. Mmmh, kama wewe una mifano ya watu hao, lete na Siyi ajifunze kwako. But kama hakuna, jua kuwa hayo ni mapokeo na maasi yaliyoingia ndani ya kanisa. Hakuna RM hapo. Ni ibada za sanamu tu zilizojawa na mihemko na hisia za kimwili zaidi. Changamkeni kutoka babeli.

  Solowenyo!!

 7. Kaka utamu wa kunena kwa lugha ni mpaka unene, pia kucheza ktk roho nako ni mpaka ukufikie huko kucheza ktk roho atakako kuvuvia huyo roho; na akiwa ni RM basi utacheza, na furaha yako itakuwa kamili!

  Nafahamu kuwa kwako wewe ni vigumu kuyaelewa mambo haya ya Kipentekoste, hayo yanayojidhihirisha kwa akina Daudi, Miriam na wengineo wengi, kwani kusanyiko lako limezaliwa ktk nyakati za matengenezo, wa Neno la Utakaso, likiwa limechomoka kutoka ktk Umethodist; kwahiyo blanketi la Kikatoliki lilikuwa halijamalizika kutolewa juu yenu, ndio maana bado mko kwenye ibada za kifungo cha uongo wa kujinyenyekeza, kama Katoliki. Basi mambo ya rohoni kwenu ninyi wala hamuyajui, ni mapya kabisa, hayamo katika msingi uliowazaa, wewe mwenyewe jaribu kuchunguza, utaona wazi kuwa hamuamini ktk kunena kwa lugha wala uponyaji wa kiungu, wala ishara nyinginezo licha kuvitolea kauli ya kuwasahihisha Wapentekoste, lakini ktk makanisa yenu mnajifunza kuhusu hayo si ktk kutimiliwa bali elimu tu!

  Siyi, mnauishi uongo wa miaka ya 1800s leo hii wakati mbingu zimejaa yaliyo halisi na kweli!!

  Kwa taarifa yako Katoliki sasa hivi wana dansi barabarani na bango kuuubwa na msalaba mkuuubwa, wanapita mitaani na midundiko! Siku nyingine nikamuona mjanja kama Siyi naye wamemfungasha, hakuna kusepa!! Unaona uzalendo umewashinda, nanyi hamko mbali!!! Ingawa sijui wanadansi kwa roho gani, ila najua si RM!!!

  Inuka mtoto wa kiume ujiokoe na nyumba yako!

  Gbu!

 8. Lwembe,
  Mchango wako uko kimtazamo zaidi kuliko facts za kibiblia. Hebu changanua neno. Acha kutumia mazoea tu.
  Ubarikiwe sana.

 9. Dansi ndani ya Biblia- ndiyo mada iliyoletwa hapa.
  Bila shaka ni lazima pia kujua mambo matatu na tofauti zake:
  Traditional Dance, Praise Dance na Worship Dance. Pengine pia ni muhimu sana kutofautisha maana ya neno hili dansi na kucheza; hasa ukizingatia kwa lugha yetu ya Kiswahili neno hili dansi tumelikopa kutoka lugha nyingine.- dancing – mchezo au tendo la jinsi ya kucheza ngoma..
  Mimi ninapenda sana kudansi na kucheza ila ninaangalia ni wapi na ni namna gani nafanya hivyo. Niutumie vipi mwili wangu wakati nikiwa katika ibada, ama nikiwa na watoto wa Sunday School kwenye kipindi cha uimbaji. Nikiwa katika hali ya kusifu nidansi vipi; hilo ndilo la maana kwangu. Kama vile Musa alivyokasirishwa na Wanaisrael walipokuwa wakidansi wakati alipochelewa kurudi toka mlimani. Soma Kutoka 32:19
  Ni jambo jema kuwa na staha na wastani katika yote; maana hata viungo vyetu vyapaswa kumtukuza Mungu wetu.

 10. Hapo anapopaita Lwembe “pale” na mimi Sungura ninapaita “kuvusha”, ndio hasa pana tatizo.
  Hasa kwa wanaume, mawazo ya ngona yametawala sana jamani.

  Siku moja kanisani kwetu bandi ya kusifu tuliamua kufunga na kuomba na kufanya mkesha wa kusifu na kuwakaribisha kanisa lote kwenye huo mkesha.

  Katikati ya ile sifa sebene zikiwa zimepamba moto,kulitokea uwepo wa Mungu na ndip kiongozi akasema “sasa ni wakati wa kila mtu kucheza mtindo ambao Roho mtakatifu anavyomwongoza”.
  Wa kwanza kuruka mbele alikuwa ni mchungaji,na akina dada /mama wakiwa wamefunga vibwebwe huku wengi wao macho yao yakiwa yanabubujikwa na machozi na wengine wakisema kwa lugha mpya walicheza. Mwenye kukata mauno, mwenye kulala chini na kutambaa, mwenye kupiga samasoti. Hakuna aliyekuwa anapoteza muda kuangalia “pale” au “kuvusha”.

  Wengi baada ya hapo walisema walikuwa hawajawahi kucheza mbele za Mungu kwa namna ile.

  Lakini ukienda kuangalia ule mkanda wa tukio lile ki dunua dunia “pale” panaweza kukusumbua, na hata wahusika wenyewe waliokuwa wakicheza huwa wakijiangalia wanashindwa kuamini kuwa walikuwa ni wao waliocheza hicho kinachoonekana wakicheza.

  Tubadili nia, hakuna kitu najisi kwa asili.

  Tatizo ni “pale” na “kuvusha”

 11. Ndugu zangu, 
  Katika suala hili la dansi au kucheza katika Biblia, jambo ninaloliona ni kwamba mtoa mada kwa kiasi kikubwa ameiongoza mada katika jinsi ya ufahamu wake, au zaidi mtazamo wa kusanyiko lake kiujumla, badala ya uhuru wa jambo lenyewe kama linavyojitokeza ktk Biblia na makanisani mwetu au mikutanoni au misibani.

  Kwanza kucheza kokote kule kunakoambatana na kuimba au upigaji wa vyombo, kimsingi huwakilisha aidha furaha ambayo huambatana na ushindi/sifa, au ibada, iwe ya Mungu wetu au ya mizimu. Hakuna anaye cheza kuyakumbuka machungu aliyonayo!

  Basi, tukikurudia kule kucheza kulikomo ndani ya Biblia, hisia zangu zinaniambia sidhani kama kuna kwaya yoyote ile inayoweza kukufikia kucheza huko kulikomo ndani ya Biblia, anayedhania kuwa Miriamu na hao wanawake hawakuwa na matayarisho, mawazo yake yatakuwa ‘so mechanical’! Ndugu zangu kucheza, iwe ngoma au chochote kile, kumo ndani yetu sisi wenye uwezo wa kucheza, na anayesema hajui kucheza, huyo amejifunga mwenyewe ndani ya furushi la uoga. Subiri furaha ilifumue furushi hilo! 

  Hebu mtazame Daudi alipocheza katika ile furaha yake. Mkewe alimshangaa na kujisikia aibu kama unavyojisikia aibu Nzala na wengine! Miriam, alipotazama nyuma kule baharini na kuuona Utukufu wa Bwana, akazungusha shingo yake nyembamba akaliona kusanyiko lake salama upande upande huu, loh, akalipuka katika furaha yenye kumtukuza Bwana, jinsi ya kucheza katika instance hiyo ikajitokeza, maana uwepo wa Bwana uliwazingira basi ule uchezaji waliotoka nao Misri, ulikuwa transformed hapo kuwakilisha ukamilifu ambao hawajawahi kuwa nao maisha yao yote wanayoyajua kwa kuyaishi. Ilikuwa ni siku kuu sana kwao, kuyaona majeshi hodari ya watesi wao yakiangamia machoni pao, bila ya wao kuinua hata mkono!! Daudi alipomuua Goliati, mji mzima ulilipuka kwa furaha, safari hii miduara sijui ilikuwa mingapi humo mjini!

  Jamani, sisi tuna hadithi tofauti na malaika. Hamjasoma shetani alitupwa huku chini? Hamjasoma Mungu mwenyewe alishuka pia huku chini atutie nguvu? Basi tunaponolewa, au katika maombi, kuna anayecheza? Au ikitokea shetani amepewa kushinda, labda mpendwa wetu amefariki, wakati wa kuaga mwili, umeshawahi kuwakuta watu wakicheza? Labda Wajaluo wanapochangishana pesa za msiba, tena huwa wamelewa!

  Ukizungumzia kukata viuno, kuna ulazima wa kutofautisha. Kuna kukata viuno kwa ngoma za kiMisri, au kimakonde au za jinsi hizo kama chakacha na nyinginezo za kienyeji ambazo maudhui yake ni kuonesha umahiri au uwezo alionao wa vitendo vya ngono wa hao wachezaji, staili ambazo zimejiingiza na kujiwakilisha kama sehemu ya starehe katika maisha yetu ya kawaida, katika madansi na matamasha ya ngoma na hata mabendi za dansi kuwa na kundi lao la wanenguaji. Nadhani ni katika kufurika kwa dhana hii mawazoni mwetu, kutokana na mashambulizi yaliyohamia majumbani mwetu kupitia Tv sets zetu, sasa kila mwanamke anapojitikisa kidogo, sisi huenda mbali zaidi, tunapatazama “pale” na kupapima!! Kanisani kama kwenye Tv!!!

  Yabadilisheni mawazo yenu, tumejichanganya sana na ulimwengu, hata namna yetu ya kuwaza si ile iliyojaa utukufu wa Mungu. Tujihadhari wapendwa, wakati huu tunaoishi ni wa hatari kuliko nyakati zote zilizopita, huu ndio haswa wakati Shetani anapozunguka na kutumeza wazima wazima! Hebu fikiria Nzala pale tunapojivika excuse ya kupima ili kujua ule ni unenguaji au la, tunapopaangalia “pale”; je, ni wangapi wanaanguka katika Uzinzi kuanzia majumbani mpaka makanisani???

  Mbarikiwe wapendwa!

 12. Alichocheza Daudi ni nini,wimbo,filimbi,ngoma au alikuwa anarukaruka tu bila kuwepo kwa sauti yoyote yenye kuashiria muziki fulani?

  Na kama kulikuwa na mziki, ulikuwa uko katika mtindo upi?
  Kama mtindo ulikuwa ni wa kucheza kwa kurukaruka basi asingeweza kucheza mtindo wa kuzunguka zunguka.

  Na kamwe siamini kama jamii nzima ya kanisa duniani kote inatakiwa kucheza kama wayahudi ambao ni sehemu ndogo tu ya wana wa Ibrahim (baba wa mataifa mengi) katika utamadun iwao

  Ispokuwa ni kweli kuna style fulani za kucheza ambazo si sawa hata kidogo.

  eg style ya kuzunguka zunguka (mduara) ambayo wengi tunadhani inaweza ikawa nzuri kuchezwa kanisani kwa vile si kukata mauno, kwangu naona bado haiko sawa ikichezwa kama inavyochezwa duniani ( mwanaume anakuwa nyuma punde tu ya mwanamke kwa zero distance). Na hii ni style ya mwambao ambayo kihistoria inatoka mashariki ya kati hukohuko.

  Katika mitindo mingi ya style za dunia huwa kuna kitu kinaitwa ‘debauchery’. Neno hili kitafsiri ni sawa na neno ‘wickedness’. Na maneno haya yanahusika sana na nia ya ndani, kwamba huyo anayecheza anajaribu kumaanisha nini ndani yake.

  e.g. mwanamke anapojilowanisha makalio kisha akaanza kucheza bila shaka wajua huwa anamaanisha nini.

  Kuna mama mmoja kanisani kwetu alikuwa mnene na ana makalio makubwa,ile tu kurukaruka tunakokusema kuwa ndio style ya kanisani ilikuwa ni hatari kwa wewe(mwanaume) mwenye kumtazama na kuweka nia ya pili. Nia ya pili chuoni tulikuwa tunaiita kuvusha,yaani unamwangalia dada mpaka macho yako yanavuka mavazi yake aliyovaa.

  Lakini je mama huyo angeacha kumchezea Mungu wake ati kwa sababu ya mwili wake ulivyo? la hasha, mwenye kumwangalia kwa kuvusha alitakiwa aponywe nia yake.

  Je niache kucheza style fulani kwa sababu ni mbaya mbele za Mungu au kwa sababu ni mbaya mbele za watu wa Mungu????

  Mimi naona tatizo ni Debauchery kwa wanaocheza,
  Lakini pia tatizo ni kuvusha kwa wanaomtazama mwenye kucheza.

  Bado niko kazini!

 13. Daudi hakuwa na maandalizi yoyote ya namna ya kucheza kama ilivyo leo kwa baadhi ya kwaya za injili kwenye makanisa yetu. Alirukaruka na kuzuzngukazunguka kama mtu anayepata furaha baada ya kufaulu mtihani, kupata mtoto, kupanda cheo nk. Ni furaha ya papo hapo tu. Daudi alipata furaha ya papo hapo tu na ambayo haikuwa endelevu kwa baadaye.

 14. asante bwana nzala japo sijafuatilia hayo maandiko exactly, ila naona yanalenga kutupeleka kwenye kumcha Mungu zaidi kuliko kwa ibilisi. tofauti yake na mtu atakayetetea jambo hili ni bayana kabisa. kwangu mimi kulingana na mafundisho niliyopewa na nimeyapokea kwa moyo wote kwa nia ya kuyafuata for the rest of my life ni kwamba ibada inaundwa na vitu vifuatavyo;
  a) maombi
  b) sifa kwa Mungu
  c) kuabudu
  d) sadaka
  e) neno la Mungu lenye nguvu za roho mtakatifu
  f) ushuhuda wa matendo ya Mungu.

  hayo yakiwepo ndipo unapoweza kusema kuwa umemfanyia Mungu ibada na ni lazima yafanyike katika njia sahihi ya kiMungu.

 15. Bwana Nzala, asante kwa mada na utafiti kidogo wa kimaandiko uliofanya.

  Mimi binafsi kabla ya kuchangia mada moja kwa moja,ningependa uniambie maana ya Ibada. Na utamaduni ambao kanisa (universal church) leo linatakiwa kuutumia katika kumfanyia Mungu Ibada.

  Kwa wachangiaji wenzangu ningependa kusema kuwa mada hii ni ya kiutafiti zaidi hivyo ni vizuri tukaleta kweli za kimaandiko na kiutafiti wa maandiko katika kuchangia kwetu.

  Mwisho, sijapenda wala kukubaliana na sentensi yako kuwa Biblia haiko salama. Kuna neno jingine labda ungetumia kusema ulichokuwa unalenga kusema.

  Biblia ni neo la Mungu na neno la Mungu liko salama.

  Ubarikiwe.

 16. Na majuzi hapa Kuna mmoja amepromotiwa ila kwa wengi wanaweza sema oooohh Mungu kambariki lakini nasema mimi kuwa huyo shetani kampromoti sana kwa kazi yake nzuri ya Kuwavuta watu wengi kwa jinsi achezavyo na aaimbayo wengi mnajua machachari wa kucheza kama amepagawa na pepe ROSE MUHANDO. Hata ukiona katika top cover yake ya juu mtumishi wa Mungu hawezi kuvaa nguo Transparent kama hiyo huku akiinua vidole za alama ya ya kishetan na Kuna huyu Mwingine yy ndo anamdhihaki Mungu kwa kutumia Bibilia kuhalalisha mambio yake Bwana Masanja Mkandamizaji, Jamani Kumbuka Mungu Huwa hadhihakiwi.

 17. Barikiwa sana Bwana nzala Uko sahihi kabisa maanake watu ss hawajui kuwa shetani kaisha teka anatimiza tu makusudi yake ya kwnye isaya 14:13-14.
  Barikiwa sana tuko Pamoja sana

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s