Kusoma vitabu vya kukombolewa kutoka nguvu za giza!

Bwana Yesu asifiwe! Kuna Vitabu vinavyosimulia au kutoa ushuhuda juu ya kushindwa kwa nguvu za giza/kuzimu/freemasonry. Vitabu hivyo kwenye jalada lake au ndani kuna picha za alama za kipepo/shetani/freemansory. Vitabu hivyo ni vizuri na vinatoa mafundisho na kuzidisha Imani ya Mkristu kama akisoma. Lakini je zile alama za freemanson kwenye kitabu hicho ni muhimu kuwepo? na je kwa sisi tuliookoka kushika kitabu/kitu chochote chenye alama ya freemasonry/kipepo/shetani sio kuutangaza ufalme wa Giza?
Mungu awabariki sana!!!!!!

–Martha

Advertisements

8 thoughts on “Kusoma vitabu vya kukombolewa kutoka nguvu za giza!

 1. Naomba kupata msaada kuhusu maombezi nataka kuombewa kwani naumwa sana kichwa

 2. Martha,
  Kitabu ni “Neno au Ujume” na Alama au Logo inayowekwa na Mwandishi ina maana mbili, kwanza, Alama au Logo inaweza kuwa ni kielelezo cha kazi za mwandishi husika, ambapo kazi au huduma yake huitoa kwa Alama fulani kama kitambulisho chake – Alama au Logo za namna hiyo husajiriwa na kutambuliwa na Selikari na Dunia huheshimu Alama kama hizo, na kwamba Mtu akiitumia pasipo Idhini ya Mhusika huwa ni kosa kisheria. Lakini sababu ya pili, ni kwamba, Mwandishi anaweza kutumia alama au Logo za Mtu mwingine, kampuni isiyoyake au Taasisi ingine ambayo si yake kwa Idhini ya wenyewe, ili aweze kuwasilisha hoja, simlizi au ujumbe kama utangulizi kwa ufupi – Kwa lengo tu la kuwavutia wateja wake (Wasomaji) kutokana na umaalufu wa Wenye Alama au Logo husika, ili kufanya kazi yake iuzike kwa urahisi, na kwa tija kubwa!

  Watu wengi wanasumbuka na mambo mbalimbali hasa yale ya kustajabisha kwa sababu ya kupenda miujiza kupita kiasi! Watu hutekwa na mahubiri yaliyojaa vituko vya kimiujiza, mizungu yenye udanganyifu wa Shetani kuliko kusikiliza injili ya kweli. Mahali panapohubiliwa Nguvu ya Injili katika kuleta uzima na kuzaliwa upya kiroho, ujumbe au habari hii huwa haivutii kama pale panapo hubiliwa na kufanyika miujiza ya kimwili kama utajirisho na matendo ya kimaumbile kama kupata watoto nk! Isaya anasema kuwa, mwenye Injili ya kweli yaani Yesu Kristo kwamba, yeye, “…….hata tumwonapo hana uzuri, kwamba tumtamani. Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko….!”

  Hivyo utaona kwamba Yesu hufuatwa na watoto wake tu, na wasio wake hawavutiwi naye, na ndiyo walio wengi makaniasani! Shetani analijua hili vizuri sana, ndipo huamua kubuni na kutoa vitu vya kuvutia, kushangaza au kutisha ili kuupoka umati na kuupoteza kirahisi, huwajaza mishangao na hofu nyingi kwa uongo na mizungu yake. Ndipo utawaona na kuwasikia watu waking’ang’ana na Habari za Free mason, na Vitabu vya Tafsri za Ndoto, maono au Stori za nilikwenda kuzimu chini ya Bahari siku 21,30,60 nk!

  Lakini kumbuka Ukiukataa ukweli ambao ni Neno la Mungu, unapewa kuamini uongo, ili upotee! Kwa upande wa kushika au kusoma vitabu vyenye Alama au Logo zinazosemwa za Kishetani, itategemea Mtazamo wa Mshikaji au msomaji. Kwa sababu Kama ni swala la Kuutangaza Ufalme wa Shetani au kunajisika si lazima mhusika ashike au asome kitu fulani tu, hata “Kutazama” au kuwaza tu, kwaweza kumtia mtu unajisi na kujikuta amekwisha tangaza Ufalme au kazi za Shetani pia!

  – Walio wa Roho Mtakatifu huishi kiroho, wao huongozwa na Roho mtakatifu cha kufanya na si kujaa hofu za Freemason na Hadithi za kufikirika!

 3. Bwana YESU asifiwe
  kwa mtazamo wangu hizo alama sio ishu kwa sababu wakristo wanapaswa kuzijua alama zote za kipepo zikiwemo za freemason na hata Biblia takatifu imefundisha juu ya chapa ya mnyama ibilisi na shetani aliye laaniwa tangu mwanzo yaani 666 pamoja na ishara nyingine nyingi kwa ufahamu zaidi tusome Daniel na Ufunuo wa yohana.
  Vitabu ni vizuri vinafundisha tusome na tuhubili injiri kwa uwezo wetu wote watu wamjue MUNGU na waokolewe.

  Kabissa Jeremiah

 4. Bwana Yesu asifiwe.
  Mimi kwa mtazamo wangu ninasema vitabu ni vizuri.
  Cha msingi ni kusimama katika ulimwengu wa roho kwa sababu kwenye ulimwengu wa kimwili unaweza kuona ni picha tu lakini kwenye ulimwengu wa roho kuna maana kubwa sana. Angalizo kwa kuwa umepewa mamlaka kwa Jina La Bwana Yesu huna budi ukinunua kitabu au kitu chochote ukitakase kwa damu ya Yesu.
  Mungu awabariki na kuwatia nguvu.

 5. Hata tukila kitu cha kufisha hatutakufa, lazima tumepewa mamlaka ya kumpinga shetani/
  amiiina.

 6. Labda mngetaja jina la kitabu na pia alama za freemmason, maana naona wanataja kuna ishara nyingi ambazo mwingine anaweza kufanya bila kujua na kama ni hivyo sidhani kama unamkosea Mungu. Mimi nadhani kwa hali tuliyomo na siku zinavyoenda ni kusimama ktk maombi hasa ya vita tu ndio kutamfanya mtu kuweza kuhimili vishindo na majaribu juu ya imani yake. Vitabu hivyo basi ni muhimu ila tuongozwe na Roho mt ili usijeingia imani potofu. Mbarikiwe

 7. Ujumbe uliobebwa ndio wa muhimu, kama unamuuhubiri Yesu kama mshindi, hatuna budi kuwa huru kuvishika.

 8. kama Yesu alikubali kushuka duniani kulikojaa dhambi kwa lengo la kutukomboa ,kushika kitabu hicho ni muhimu maana huwezi kumshinda adui yoyote bila kumpeleleza

  ________________________________

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s