Nguruwe zaidi ya 60 wachomwa, Ruvuma!

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki

Nyumba zipatazo sita, magari mawili na nguruwe zaidi ya 60, vinavyosadikiwa kuwa ni mali ya Wakristo vimechomwa moto na watu wasiofahamika katika Wilaya ya Tunduru Mjini, mkoani Ruvuma.

Akizungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo licha ya kutokubainisha idadi ya nyumba na mali zingine zilizoteketezwa.

Nsimeki aliongeza kuwa matukio haya yametokea kwa siku tatu mfululizo tangu Septemba 7 hadi 10, mwaka huu.

Nsimeki aliongeza kuwa tangu vitendo hivyo vya uhalifu vianze kutokea, hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na kwamba Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo inaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda kutoka wilayani humo, wamedai kuwa matukio hayo yametokea kati ya Septemba 17 hadi jana.

Kiongozi wa Kanisa la Pentekoste Tanzania lililoko wilayani Tunduru, Mchungaji Stephen Milinga, alisema usiku wa kuamkia juzi, magari mawili, moja likiwa ni mali ya mzee wa Kanisa la EAGT na lingine lenye namba za usajili T134 BGJ, mali yake yaliteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana.

Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo usiku huo walipeleka taarifa katika kituo cha polisi cha Tunduru Mjini. Aliongeza kuwa watu hao waliwahi kufanya tukio lingine usiku wa kuamkia Aprili 25, mwaka huu kwa kung’oa uzio wa magogo wa kanisa hilo na kuuchoma moto.

Alisema usiku huo pia walikwenda kutoa taarifa katika kituo hicho cha polisi ambapo ilifunguliwa kesi namba TUN/IR 405/2012, lakini hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa. Mchungaji alisema kati ya Septemba 17 -19 mwaka huu, nyumba zaidi ya sita na mabanda ya nguruwe vilichomwa moto na kusababisha zaidi ya nguruwe 60 kufa.

Alisema usiku wa kuamkia Septemba 19, mwaka huu watu hao walifanya jaribio la kuchoma moto mashine ya kusaga mali ya mkazi mmoja na kugonganisha nyaya za umeme, lakini  kabla ya kuleta madhara ulizimwa na wasamaria wema.

Kati ya Septemba 19-20, mwaka huu mabanda mawili ya nguruwe moja likiwa ni mali ya mchungaji wa Kanisa la Biblia na Padre wa Kanisa  la Anglikana yalichomwa moto.

–NIPASHE

Advertisements

3 thoughts on “Nguruwe zaidi ya 60 wachomwa, Ruvuma!

  1. KAMA NYERERE ALIPOKUWA HAI WALIOTUHUMIWA KUWA NI WACHAWI KWA KUWA NA MACHO MEKUNDU WALIUAWA PAMOJA NAALIBINO SHETANI ALIKUWEPO ILA ALIOGOPA UWEPO WA NYERERE SASA HIVI HAYUPO KAMA SHETANI ALIKUWA ANATEMBEA KWENYE BARABARA ZA VICHOCHORO SASA ANATEMBEA KWENYE LAMI NA AMEENEA BARABARA NZIMA MAKAFIR MUTAIPATA FRESH MUOMBENI MUNGU MUWE NA HATA CHEMBE MOJA YA UPAKO

  2. Magreth mkiwa, salama?

    vita ya shetani na watoto wa Mungu haipiganwi kwa Bunduki na wala watu wa Mungu hawalindwi kwa uwezo wa kipolisi! Watumishi na watoto wa mungu wanalijua hilo – juwa kwamba, siku zote ukimtegemea mwanadamu umelaniwa!. Sasa, tujiulize, je, watu wanautafuta ulinzi wa Mungu kwa bidii katika nyakati hizi za hatari kama ambavyo wanautafuta utajirisho katika maombi ya kuvunjiwa laana? Nina wasiwasi kama, nyakati tunazisoma na kuzielewa sawasawa! – maana Mbweha wanaelekea mapangoni kulala! Lakini wajiitao wacha Mungu ndiyo kwanza wanatoka “out!” Neno linasema halitatokea jambo bila manabii wa Mungu kujua, je, manabii wa Mungu wapo? na kama ndiyo, Je, sisi ni watoto wa Mungu sawasawa ili tupewe ujumbe toka kwa Mungu kwa njia ya manabii wake? Usiwalaumu kuku bila kuangalia ulivyoanika mtama wako!

  3. viongozi wa nchi wanasemaje? au wanaliacha kama la ma- albino kukatwa mikono?
    are you real protected as a citizen?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s