Ukuu wa Mungu

Uzito wa dunia ni tani 6.58 sextillion(6,580,000,000,000,000,000,000tons). Speed ya dunia kujizungusha kwenye mhimili wake ni 1,669.8Km/hr. Speed ya dunia kulizunguka jua ni 107,300Km/hr(29.78Km/Sec). Wakati dunia ikiwa katika mizunguko hiyo mimi huwa sioni kama ipo kwenye hiyo speed movement, inawezekana niko kwenye gari linalotembea(basi) na ndani ya hilo basi ninatembea humo humo ndani. Mambo ya ajabu kweli haya. Kitu kinapokuwa kizito zaidi inahitajika nguvu kubwa zaidi ya kukisukuma kuliko kile chepesi. Kwa uzito wa dunia, inahitajika extra power kuiwezesha kwenda. Lakini kwa mizunguko yote miwili na kwa speed nilizoainisha hapo juu inahitajika extra ordinary miraculous power kuiendesha dunia. Lakini ingewezekana ni kuiendesha dunia kwa siku moja nguvu ingekuwa kidogo, lakini kuiendesha dunia siku zote hizo(4.6billion years) inahitajika nguvu ambayo huyo mwenye kui-create atakuwa anatisha tena ni mkuu kuliko mwanadamu anavyoweza kujua huo uwezo. Lakini endelea kutafakari dunia ni moja tu ya sayari nyingi na ni ndogo sana kuliko sayari nyingi(Jupiter ni kubwa mara 318 ya dunia), zipo pia nyota zisizohesabika, miezi na viumbe vingi vinginevyo katika anga. Vyote hivi viko kwenye movement na zipo kanuni zilizowekewa kufuata na hazizikiuki. (Ingia kwenye mtandao wavuti ya planetfacts.org)

Kuna dhambi moja huwa binafsi nimefanya mara nyingi, ninapokutana na tatizo linanitikisa sana, moyo unainama, ninasononeka, ninapoteza matumaini n.k. Lakini ninashindwa kulinganisha tatizo langu na huyu muumbaji wa mbingu na nchi Jehova. Nimeimba mara nyingi nikisema “hakuna aliye kama wewe” lakini nimegundua sikujua ninachokisema, sikuishi nilichokuwa nakikiri. Nguvu na uweza wa Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Muumba wa Mbingu na nchi ni mkuu sana sana. Kumlinganisha na jaribu ninalopitia ni kama kumdhalilisha Mungu. Nguvu zake zimeumba dunia na sayari nyingine, nguvu zake zina uwezo wa kuizungusha na kuiendesha dunia in such as that great speed. The power of my challenges are nothing before Almighty(Mwenye enzi) God. Kujua uwezo wake na nguvu zake ukalinganisha na jaribu lako kunakusaidia kumwinua Mungu juu sana ya jaribu lako na kulidharau jaribu hilo sana, haswa unapolilinganisha na uwezo wake. Ukiwa na ufahamu huo ukaenda mbele za Mungu kuhitaji msaada, utauona wema wa Bwana ghafla.

Soma Mathayo 8: 24- 27 Naye alipoingia kwenye chombo, wanafunzi wake wakamfuata. Ghafula kukainuka dhoruba kali baharini hata chombo kikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!’’ Naye Yesu akawaambia, ‘Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?’ Kisha akaondoka na kukemea dhoroba na mawimbi, nako kukawa SHWARI KUU.  Wale watu wakashangaa, wakisema, “NI MTU WA NAMNA GANI HUYU? Hata upepo na mawimbi VINAMTII! Wanafunzi walikaa na Yesu lakini hawakumfahamu vyema ingawa walimwambia awaokoe wanazama. Mbele za Yesu jaribu lako litasikia agizo kuu la kuwa kimya/ shwari kuu.

Unavyomjua Yesu Kristo vizuri, ya kuwa yeye ni Mfalme wa uzima(from Amplified Bible -Source or Author of life) (Matendo.3:15), Ya kuwa vyote viliumbwa na Yeye na kwa ajili Yake(Kolosai 1:16) Kwa Yeye(Yesu) vitu vyote vilivyoko mbinguni na JUU YA NCHI viliumbwa, vile vitu vinavyoonekana na vile visivyoonekana, kama ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala, vitu vyote viliumbwa na Yeye na kwa ajili Yake. Ukisoma pia Mithali 8:23-36.

Nikutie moyo ndugu unayemwamini Yesu Kristo na uko kwenye mapito magumu, USIKATE TAMAA KUMTUMAINI YESU(DON’T LOSE HOPE IN TRUSTING JESUS). Inawezekana umeshatazama milima mingi ukitafuta msaada,  sasa nakushauri mtazame Yesu aliyeziumba Mbingu na nchi. Soma Zaburi 121. Yeye ANAJISHUGHULISHA sana na mambo yako, mtwike fadhaa zako, majaribu yako dhiki zako. (1 Peter 5:7-AB)Casting the whole of your  your anxieties, worries, concerns, once and for all on Him, for He cares for you affectionately and cares about you watchfully.

Godleader Shoo

Advertisements

4 thoughts on “Ukuu wa Mungu

  1. Kwa anayeamini, sayansi ni ushuhuda wa ukuu wa Mungu. Hata kwa huyo unayesema mwanasayansi anayemkana Mungu humkiri pasipo kujua, Maana itafia mahali atakuambia “nature” kwa maana ya asili ndiyo imefanya hivyo. Hiyo space ambayo hizo sayari na nyota zimo unaambiwa haina mwisho. Tafakari juu ya hilo ili kujua ukuu wa MUNGU.

  2. Je, Sayansi inatusaidiaje kuujua UKUU wa Mungu? SAYANSI KATIKA MAISHA YA KAWAIDA HAKUNA ATAKAYE BISHA, wengi wanakubali kuwa INATOA MCHANGO MKUBWA KATIKA NYANJA ZOTE! Kiuchumi, kisiasa kielimu, maswala ya Kijamii, kwa kifupi Sayansi ndiyo maendeleo.

    Hakuna Mtu asiye’Aplai’ sayansi katika Maisha yake ya Kawaida ya kila siku na hasa katika siku hizi, ambapo teknolojia inachukua kasi ya kutisha katika Nchi zinazoendelea! Lakini Je, Sayansi inatusaidia kwa namna yeyote katika kumjua Mungu? Kama ndiyo au siyo, kwa vipi? na je, Biblia inaisemeaje Sayansi? Maana nimepata kusikia watu wakisema “Wana Sayansi hawaanini kuwa Mungu Yupo!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s