Makanisa yaliyochomwa na waislamu, Rais Kikwete atoa pole kwa waumini!

 Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 12 Octoba 2012 kupinga kitabu chao “kitakatifu’ cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitemea mate. (Picha na Happy Mnale)
 
Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala siku ya tukio
 Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
 Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam
HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR
 
DAR ES SALAAM, Tanzania

VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.

Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.

Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.

Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.

Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.

Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hata hivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.

Vyanzo mbali mbali vya habari, Video na ITV

Waumini wa dini ya Kiislam wamekuwa mstari wa mbele kusema dini yao ni ya amani. Lakini ni tofauti na matokeo yake. Tunawaombea wampokee mfalme wa amani awape amani ya kweli.

Advertisements

12 thoughts on “Makanisa yaliyochomwa na waislamu, Rais Kikwete atoa pole kwa waumini!

 1. WAKRISTO TOKA UHURU TUMEISHI VIZURI KILA MMOJA AKIADU DINI YAKE BILA MATATIZO KUMETOKEA NINI LEO KWAMBA NI WENGI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI NA WAKIISHI KATIKA UHUSIANO HUO MZURI TUTAKAPOACHA KUJIUULIZA HII SUMU NI YA HUMU NDANI YA NCHI AU KUTOKA NJE TUKAIONDOA YALE YANAYOTOKEA SOMALIA,NIGERIA,MALI TUYASUBIRI YANAKUJA KWA KASI SANA NCHINI TANZANIA KAMA YAMETOKEA LIBYA,TUNISIA NA MISRI TUKASHANGILIA KWA NINI YASIJE TANZANIA.MUARABU AKIWA JANGWANI ALISHAWISHIWA NA NGAMIA AMRUHUSU AINGIZE ANGALAU PUA TU KWENYE HEMA ILI AJIHIFADHI NA BARIDI ,MUARABU ALIRUHUSU PUA TU BAADAYE ALIMSHAWISHI AINGIZE KICHWA BAADAYE AKAINGIA KWA NGUVU AKAPASUA HEMA SASA HIVI HEMA LA TANZANIA LINA UFA MKUBWA TU SINA UHAKIKA MULIKUWA MUNAMUELEWA NYERERE MTUMENI MTU KUZIMU MUKAMUULIZE AWAFAFANULIE

 2. Jamani…kesheni kwa kuisoma na kuitafakari sana biblia kwa kuwa haya yote tunayoyajadili mtayaona rahisi sana kuyaelewa .Yesu alituambia hivi:HERI NINYI WATAKAPOWASHUTUMU NA KUWAUDHI NA KUWANENEA KILA NENO BAYA KWA UONGO KWA AJILI YANGU FURAHINI NA KUSHANGILIA KWA KUWA THAWABU YENU NI KUBWA MBINGUNI KW MAANA NDIVYO WALIVYOWAUDHI MANABII WALIOKUWA KABLA YENU….Kwa hiyo mkristo yeyote asiyejitambu kuwa amefanywa mnyonge katika vitu vya dunia hii..na kuwa haki katika ufalme wa mungu atakuwa ni mkristo wa mapokeo asiyeufahamu ukristo na tabia zake.Yesu kristo alituachia kielezo hiki kwa kupigwa kwake na kuteswa kwake bila hatia sisi tulifanyika haki mbele za mungu..japokuwa yeye alikuwa na nguvu na mamlaka yote hakulipiza kisasi ili aipate haki ya mungu kwa kujinyenyekeza kusikokuwa na kikomo.Na sisi wakristo tunatakiwa tufuate kanuni ile ili tufanyike haki mbele za mungu kupitia yesu krito kwa kuwa yeye ametutangulia kuwa neno la haki na sisi tunafuata kuwa wana wa haki..ndiyo maana biblia inatusisitiza:MSISHINDWE NA UBAYA BALI MUUSHINDE UBAYA KWA WEMA.Lazima wakristo tujitambue hivi:HAKI YETU MBELE ZA MUNGU INAPATIKANA KATIKA YESU KRISTO NDANI YA DAMU YAKE PAMOJA NA KUFUATA MAFUNDISHO YA INJILI YAKE KIKAMILIFU…wala sio kuitwa mkristo tu! haitakusaidia siku ya hukumu.kwa hiyo basi tusilipize kabisa ovu kwa ovu kwa maana kwa kufanya hivyo hatutakuwa haki mbele za mungu..Tusitumie nguvu nyingi sana za kimwili kushindana na waislamu bali nguvu za kiroho ndiyo silaha zetu kwa kuwa wao ni wa ulimwengu huu na sisi ni wageni wapitao…hatukupewa silaha za mwili bali tuko vizuri sana sana katika akili na silaha za roho ambazo ndiyo msingi wa mungu mwenyezi aliyetuumba sote.Tukishindana kimwili na watu wa dunia hii tutapoteza haki yetu na pia tutashindwa kuwa taa mbele zao ili nao waokoke…ndiyomaana yesu kristo anatuonya hivi:NINYI NI CHUMVI YA DUNIA LAKINI CHUMVI IKIWA IMEHARIBIKA ITATIWA NINI HATA IKOLEE?…NINYI NI NURU YA ULIMWENGU MJI HAUWEZI KUSITIRIKA UKIWA JUU YA MLIMA.(mathayo 5:13,14).Kwa hiyo tusiwalipize kisasi waislamu wala kuwachukia bali tufurahi katika roho zetu wasizoziona maana kupitia kwao maandiko yanatimia na haki ya mungu tutaipata na cha zaidi tunawahubiria injili ya kristo wao pamoja na wale wote wasiomuamini na kumfuata BWANA WA AMANI WA KWELI ALIYEIBATILISHA DAMU YA MBUZI NA KONDOO NA KUMWAGA YAKWAKE MWENYEWE ILI WATU WOTE TUFANYIKE HAKI MBELE ZA MUNGU.Mbarikiwe.

 3. Mimi ni Murundi (Burundi) na pia ni Mkristo. Sina la zaidi kwa wale waliotangulia na comments; ila ninataka kuwapa moyo Wakristo wote wa Tanzania na kuwakumbusha “kuombea ma adui wetu” ili kwa neema yake Mungu, wapate kubadilika na wampokee Mfalme wetu YESU KRISTO kama BWANA wa maisha yao. Watapo badillika, watashuhudia Neno (Kumbuka Sauli alipobadilika akaiitwa Paulo, alimtumkia Mungu). Silaha yetu ni maombi.
  ANGALISHO: Msilipishe kisasi msije kuanguka katika mtego wa Shetani.

 4. Nimepigiwa simu na mwanangu kutoka nyumbani Tanzania na kunipa taarifa ya kuchomwa kwa makanisa na habari ya kijana wa miaka 14 kukojolea kitabu kitakatifu cha Waislam (Koran). Nimepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa na tena kuumia sana. Nikafungua mtandao na kuona kumbe chanzo kilikuwa marafiki wawili watoto waliobishana juu ya uwezo wa kitabu hiki cha Korani. Hivi kweli ndiyo mafundisho ya wanazuoni kwa vijana wao kuhusu uwezo wa kitabu hiki? Je Wakristo nao wanafundishaje juu ya kitabu chao (Biblia) Biblia kama kitabu, ukikiojolea utageuka kuwa mamba?
  Ni jambo la kushangaza tena kukemea kuhusu hawa watu waliochukua hatma ya kuchoma makanisa ambayo hata huyo mtoto hatoki kwayo. Sijui mtoto huyo anatoka kwenye dhehebu gani. Ni vema kuangalia nini dini zetu zinafundisha kuhusu imani. Je kupigwa risasi binti mdogo wa miaka 14 kutokana na kutetea elimu kwa wanawake kulikofanywa na Matalibani huko Pakistani kumo katika Korani na ni msingi wa dini hii? Binti huyo sasa anatibiwa Uingereza!!!!!
  Nimesikia pia ya kwamba mtoto huyo wa Kikristo sasa anapelekwa kwenye mahakama ni kwa namna gani? Naomba shahidi wa kwanza kwenye kesi hii awe yule rafiki yake waliobishana naye kuhusu uwezo wa kitabu hicho.
  Kwa Wakristo wenzangu “KISASI NI CHAKE BWANA WETU” NInamshukuru Mkuu wa Kanisa letu KKKT Askofu Malasusa kusema ya kwamba tulinde amani yate kwa kusamehe.

 5. NISAIDIENI, NISAIDIENI,WAONYESHE KITAMBULISHO. Hii ni story ya kweli iliyotokea. Afisa Misitu alifika getini akazuiliwa na mlinzi asiingie msituni, akakasirika, akatoa kitambulisho, na matusi juu, mjinga wewe, mlinzi akanyamaza, akafungua geti. Bosi akaingia msituni. Baada ya dakika chache Bosi alisikika akilia kwa sauti kubwa, NISAIDIENI, NISAIDIENI. NAKUFA NYUKI. Alikuwa ameshambuliwa na nyuki, kumbe mlinzi alikuwa amemkataza asiingie msituni kwa ajili hiyo,(nyuki). Mlinzi akasikika akimwambiwa Bosi WAONYESHE KITAMBULISHO. Ndugu zangu Watanzania, maana ukisema MTANZANIA NI Wote, Mwislam, Mkristo, Mpagani. Wana haki sawa. Haiingii akilini ati Nchi yenye Utawala, Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri, Bunge, vyombo vya usalama, Mahakama. Eti mmoja achomewe nyumba ya Ibada, kisha kiongozi amwambie pole, angechomewa na Idd Amin kama alivyofanya, alikomeshwa, hakurudia mpaka kufa kwake.

  Bosi aliambiwa msitu umechafuka, nyuki wamepigwa, hawako kwenye mizinga yao, akapita kwa jeuri, ameshikilia kitambulisho, alipokutana na nyuki, alipiga kelele apate msaada, lakini msaada pekee mlinzi aliotoa nikumuelekeza Bosi awaonyeshe nyuki kitambulisho. Ndugu zangu, hawa viongozi wetu ni wa Watanzania , haingii akilini kuwa tungetegemea kusikia kuwa POLENI kwa kuchomewa makanisa, juzi, jana, na kesho tena. Najua watu wote hawafanani, wako ambao hawezi kuchoma Makanisa, wako pia ambao hawezi kuchoma Misikiti. Lakini hao wanaopatikana wamefanya jambo hilo wanafanyaje? Kuna wakati vitambulisho havitafaa.

  KITUKO. Nilipokuwa natafakari hiki kinachoendelea, nikakumbuka kitu kinachoitwa KITUKO, au jina lingine KIOJA. Siku moja nilikuwa napita barabarani Nairobi, mbele yangu niliona mtu anakuja usawa wangu, alikuwa ameshikilia kitu kikubwa kwa mikono yake miwili, kitu mtu alikuwa anajaribu kumpatia nafasi apite, (kumpisha) mwisho tulikabiliana ana kwa ana, nilimsikia akiniambia weka 200 hapa, weka 200 hapa. Sikuwa nimeelewa mara moja, kumbe alikuwa ameshika bonge la kinyesi, akaendelea kusema usipoweka 200 hapa nakuogesha kinyesi hiki. Mhhh, nilimwambia usinipake tafadhali, nilitoa pochi yangu mfukoni, nikatoa sh. 200 nikaiweka mikononi mwake kwenye kinyesi, akanipisha, nikaendelea na safari yangu. Nilimwacha na ile hela, mavi, harufu, mimi nikabaki safi nikaendelea. Tuwe makini na vituko vinavyoendelea wana wa Mungu, wapo watu wananuka, wameshika vinyesi mikononi, wanadai sh. 200, usipiganane nao, watakupaka kinyesi, utamsaidia kunuka.

  Yesu anarudi. Mbarikiwe.

 6. Ndugu zangu wapendwa,

  Nilisema hapa mwanzo, msimpuuzie Mchungaji Mtikila na juhudi zake za mahakamani.

  Sasa bila aibu viongozi wanasingizia eti kosa ni la yule mtoto aliyedhihaki korani.

  Kule zanzibar nani alikojolea korani? Makanisa yalichomwa kule kwa kosa gani? eti matatizo ya Muungano wanachoma kanisa. Mara kuna sinema imetoka, wanachoma makanisa. Mara kuna katuni imechorwa sijui wapi huko wanashambulia wakristo.

  Mtumishi wa Mungu mmoja kule Marekani Perry Stone anaamini kuwa dini ya Mpinga kristo ndiyo hii. Ndiyo maana kwenye kitabu cha ufunuo inasema watawachinja wale mashahidi wawili watakuotumwa na Mungu.

  Ni dini moja tu kwenye karne ya 21 inayochinja watu.

  Walikuwa wanachinja watu kule uarabuni na kuzibandika kwenye mtandao.

  Sasa pamoja na maombi ina hitajika mkakati na mipango ya kujihami.

  Yesu hakuwa mjinga alipotengeza kikoto na kuwacharaza bakora wajinga kama hawa.

  Mbarikiwe

 7. YESU JUU!!!! Ukisoma habari za Mtumishi wa MUNGU Eliya na habari za manabii wa baali 450 ktk kitabu cha 1WAFALME 18:21-40,hao mabaali walikuwa wakiipinga kazi ya Mungu na kuwauwa watumishi.Manabii wa baali waliamini baali ndiye Mungu lkn siku moja walijikuta wakiwa ktk hali ngumu baada kukutana na huyo Mtumishi wa Mungu Eliya ambapo walimuita mungu wao kuanzia asubuhi hadi jioni ili ajibu lkn alikaa kimya! Lkn Mungu aliye juu (YESU) lilipotajwa jina lake muda wa jua kupunga,alishuka na kujitwalia utukufu na manabii wote wakauawa asisalie hata wa dawa!!!“27:Ikawa wakati wa adhuhuri,Eliya akawafanyia dhihaka,akasema,Mwiteni kwa sauti kuu;maana ni mungu huyo;labda anazungumza,au ana shughuli,au anasafiri,au labda amelala,sharti aamshwe.Sasa kama wana Mungu si wamuite awatetee??au yuko likizo? Mungu gani huyo wa kusaidiwa kazi?? Wamuombe aangamize makanisa,kwanini wao wawe mbele Mungu nyuma??Yesu awasaidie kuwafungua macho waitambue njia waliyomo kwamba si sahihi na hizo si kanuni za Mungu(YESU) aliyeziumba mbingu na nchi,kama kweli wanaamini wana MUNGU basi wamedanganywa na kudanganyika.

 8. Kwa kweli sasa tunakoelekea ni wakati wa kanisa kusoma alama za nyakati kwani hata sasa shetani anathihirisha kazi zake live kabisa.Uislamu sio dini ya amani hata kidogo na hata hawanachakujitetea eti ni dini ya amani.Tukio kama la Mbagala linaonyesha wazi waislamu wote wanamuhitaji Yesu,maana yeye ni mfalme wa amani na ndio Wakristo tunamfuata na hata siku moja huwezi kusikia Mkristo amefanya na ujinga kama walioufanya .
  Kumbeni Waislamu kila mtu atatoa hesabu za matendo yake.

 9. Ukimchekea nyani utayavuna mabua!

  Kuna msemo wa kikwetu unasema “kwigwa kwa mbulu mpaga mininga mgutu”
  Maana yake “kusikia kwa kenge mpaka damu masikioni”

  Wakristo tunawafanyia mzaha waislam, kuna siku tutavuna mabua. Mzaha mzaha huu ulimfanya Esau auze haki ya uzaliwa wa kwanza.

  “Let’s say enough is enough”

  Tunajikamua sana kujenga hayo makanisa, halafu ati tunaacha tu mjinga fulani anakuja kuyabomoa mbele ya macho yetu huku tunajua kabisa kuwa tutarudi kwenye kujikamua tena ili kuyajenga upya.

  Ivi siku wakija kuchukua mke wako utawaangalia tu ati kwa vile biblia inasema kushindana kwetu si juu ya damu na nyama….!!!!!

  Something must be done.

  Wao hawasalii angani bwana, wana majengo yao ambayo pia yanaweza waka moto vilevile.

  Sisi tunadhani ni hasira tu za kawaida, lakini amini nakuambieni kuna mission kubwa nyuma yake.

  Why can’t we teach them some lessons?

  U know they are like kengez, until blood in their ears they can’t learn a lesson!!!!!

  God bless my country.

 10. Jamani ndugu zangu Wa Tanzania!!tuombe saanan Mungu ,nionavyo tunakoelekea sio pa zuri!!Hizo vurugu zinatisha!!!

 11. Wapendwa,

  Tusifarijiane, tusinafikiane, ukweli ni ukweli tu japo utamuumiza au utamkera anayeusikia. Lakini itabaki kuwa haki kwamba Kizazi cha nyoka ni kama alivyo Baba yao, yeye alikuwa muuaji tangu Mwanzo!
  Neno la Mungu wetu mkuu, mfalme wa Amani, Mungu mwenye nguvu na Baba wa Milele anasema hivi, “….toka tumboni mwa mama yako nilikuchagua na kabla ya Misingi ya Dunia kuwepo nilikujua!…..” Ukisoma kwa utulivu Biblia utagundua kuwa katika Dunia hii kuna uzao wa aina mbili Uzao wa Mungu na Uzao wa Nyoka! “Mataifa” haya mawili tangu mwanzo yanapingana vikali. Mungu ameacha hivyo ili, Mungu wetu aonekane mwenye haki na kwamba neno lake lithibitike! Nasikia tuwaombee……! Tuwaombee nini ambacho wapewe? Wao si wa kundi hili, Mchungaji hawajui, wala wao hawamjui tena hata sauti yake hawaisikii. Sasa, tuwaombee nini na kwa nani? HUWEZI KUMUOMBEA MULAANIWA!

  Kutajwa kwa Uislamu Duniani kama Adui wa Ukristo ni Propoganda za Shetani tu, yeye ni Muongo tangu mwanzo, maana hata Wakristo wa uongo wapo, lipo jambo “ZIMA” nyuma ya hii “Kava” Uislamu! Ameamua kuuchagua na kuutumia Uislamu ili kuuudhi Ukristo, lakini pia kwakuwa shetani ni “Mfitini” hata katika hao wa Islamu wenyewe si shwari kama ambavyo wanafarijiana! Nilipata kusema kwamba, Dhahabu “Feki” ikilinganishwa na Dhahabu “Orijino” zinafanana sana, hata huwezi kutofautisha kwa macho! Lakini, waweza kugundua tu ukitulia na kuchunguza kwa makini, wala hutaitaji vipimio vya kisayansi kuthibitisha ubora wa Dhabu. Kwanza dhahabu Feki hupatikana kwa wingi na kwa bei rahisi ukilinganisha na ile Dhahabu halisi, ambayo hupatikana kwa Uchache katika soko na bei yake ni Aghali!

  Nikweli kwamba katika hali ya Kimwili Uislamu hauwezi kukwepa na kujitoa katika lawama juu ya Matukio dhidi ya Wakristo, hususani hapa Tanzania ambapo matukio haya ya uchomaji na uharibifu wa Mali na Maisha ya wakristo yanazidi kushamili. Wakati ambapo Uislamu hauwezi kukwepa matokeo ya Madhara yanayowapata Wakristo wa Tanzania, vivyo hivyo Serikali haiwezi kujinasua katika Lawama hii, na lazima itegemee “Haki” Fulani itakayotendwa na Mungu, Mungu ni hakimu wa haki, hivyo kila aliye changia au anayechangia katika hili lazima ategemee kupata Haki yake! Sishangazwi na ukimya wa Serikali katika kuonewa wakristo, kwa sababu imesemwa, “….,Nitainua maadui kwako kwakuwa umekataa kutii….” JE< WAKRISTO MPO VIPI NA MUNGU WENU? (Msije kuwa mnaichukia fimbo badala ya kuchukia Matendo yenu!) Lakini pia imesemwa – lazima Wakristo WAUDHIWE sana tu! Lakini Ole wake yeye anayesababisha kutimia kwa Maudhi haya, Neno linasema hivyo! vipo visa vingi sana vya kuudhiwa kwa Wakristo Duniani! Maaudhi haya yalisemwa na Yesu Mwenyewe Kuwa "Watawaudhi" Kinachonifanya nifurahi na kutokuwa na hofu ni kile Bwana Yesu alicho sema, nikikumbuka Maneno ya “MWANAMME” huyu mimi hufarijika sana, yeye alisema, “…Tazama, mimi nitakuwa nanyi wakati wote hata mwisho wa Dahari…!” na hasa aliposema, BILA MIMI NINYI HAMUWEZI NENO LOLOTE!

  Namwambia Mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete Raisi wetu kuwa, wala asihofu, Mkristo halipizi kisasi, Mkristo hutii Neno la Mungu lililomo katika Biblia. Na Biblia inasema “KISASI NI JUU YA BWANA” Ila tu ajue kuwa Baadhi ya Wakristo nikiwemo mimi tunasikitika kwakuwa Serikali “HAISHUGHURIKI” kwa kwakuonewakwa wakristo, kitendo cha kuwaacha wanaotuonea watuonee tu bila hatua zozote kuchukuliwa na Serikali zenu zote mbili ile ya muungano na ile ya Zanzibar, mimi naona kuwa ni Ubaguzi mkuu! Serikali haiko “TAFU” vya kutosha dhidi ya vitendo vya Waislamu. Nafikiri serikali ijue kwamba, “MUNOA KISU HUMKATA MWENYEWE!” Maana Haijapata kutokea vitendo vya uvunjifu wa amani uletwao na Waislamu kwa kiwango kikubwa kama wakati wa utawala huu wa awamu hii ya MH. JK Murisho, kwa nini?
  Tunajua Vita hivi ni vya MPINGA KRISTO, hivyo Kristo mwenyewe atajitetea! LAkini “……Mungu alipoona DHURUMA imezidi sana juu ya Nchi, akaleta Gharika” Mimi najua kuwa Neno la Mungu haliongopi, kama ndivyo, basi, MWENYEKUDHURUMU LAZIMA AFE KWA MAJI! Kunapotokea Mafuriko na Uzamaji, kabla ya lolote KUMBUKENI nini na nani AMEDHURUMIWA?! Usijifariji eti mbona wanaozama au kupatwa na Mafuriko wamo pia wasioonekana kudhurumu? Labda utasema, mbona wamo wakristo na waislamu safi?! IKUMBUKE SIKU YA NUHU WALIPONA WATU NANE TU, DUNIA ZIMA YA WAKATI HUO! Ukiona haitoshi jikumbushe pia Siku ya Lutu, WALIPONA WATATU TU KUTOKA KATIKA MAJIJI MAWILI!

  Endeleza na endekeza Dhuruma UTAKOMA TU MAANA WEWE NI WA KUSHINDWA!

 12. So sad, mie naona walinzi ktk kanisa msimame kwa zamu zenu, ila pamoja na kuvunja majengo Yesu wetu yupo ndani yetu ibada ziliendelea tu kwani Mungu wetu sisi yu hai na ni Roho. Pia ukiangalia jinsi majibu mepesi yanayotolewa kuhusu hizi vurugu utaona kuwa wanabebwa na wanajua hawatafanywa chochote. Sisi Mungu wetu ni roho tusimame kiroho tu, vita ni vyake atasimama na kujipigania nadhani kule Zanzibar wanajua hilo, eneo hilo lilijaa watu wa pwani ambao wengi ni waislamu lakini kama ilivyo kwa visiwani pia Ukristo unaenea utachoma majengo lakini injili imeishafika tutaenea kama mchanga wa bahari….:nao ufalme wake hautakuwa na mwisho” just a matter of time. Barikiweni

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s