Nahukumiwa moyoni mwangu

Shalom watumishi!
Mimi ni mgeni katika blog hii lakini nimekuwa nikisoma mada mbalimbali nami naomba msaada wenu kibiblia ktk hili:
Mimi nilikuwa binti niliyeokoka na ktk haja ya moyo wangu Mungu alinipa Mchumba ambaye naye alikuwa ameokoka lakini ktk kuendelea kwetu na mahusiano tulimkosea Mungu Kwa Kweli mi kwa upande wangu niliumia sana Moyoni na nikaomba Mungu anirehemu Lakini kwa hali nisiyotegemea nilikuwa tayari ni mjamzito jambo ambalo hadi leo naendelea kujutia na limeacha kovu kubwa ktk maisha yangu.

Kama mtu niliyekuwa namjua Mungu sikutaka kabisa kutoa mimba kwa kuogopa aibu na mwenzangu pia hakukubaliana na hilo kwa kuwa tulikuwa ktk mchakato wa kufunga ndoa tulifunga hali nikiwa mjamzito. Hadi sasa nina miezi kadhaa nijifungue na nimekuwa ktk hali ya kuomba rehema muda mwingi hata kwa ajili ya kiumbe nilichobeba Mungu akitakase,tatizo ni kwamba nimekuwa ktk hali ya majuto takribani miez 7 sasa na mara nyingi hulia machoz Mungu anirehemu ila bado ninahukumu ndani yangu na ninakosa furaha ni kweli tunaishi vizuri lakini sijui nifanye nini niweze kurejeshewa furaha ya wokovu kama hapo mwanzo napenda kumwona Mungu na najua utumishi wangu uliingia dosari nahitaji msaada wenu wa maandiko zaidi.

Neema

Advertisements

32 thoughts on “Nahukumiwa moyoni mwangu

 1. shalom! wema wa Mungu u mkuu sana na uaminifu wake udumuo kizazi na hata kizazi, 1 yoh 1:6~9, tukitubu dhambi zetu yeye n mwaminifu, nenda kwa ujasiri ikiwa umetubu kama unenavyo basi umesamehewa na tena isaya 1:18 haijalish n uovu gani ila Mungu ni wa rehema.

 2. Shalom dada Neema,
  asante kwa kuwa muwazi kabisa, uwe na amani. Mimi nilijua pengine kuwa ktk kusanyiko jipya imekukwaza kidogo ila usihofu ni kawaida utarudi tu kwenye mstari. Kama wanavyosema wengine na mwenzio pia ni wakati wa kusonga mbele. amini Mungu anasamehe na pia wewe mwenyewe msamehe mwenzio. Mshukuru Mungu pamoja na kukosa uko kwenye ndoa yako sasa, mshukuru pia kuwa tayari unatarajia mtoto wako, naomba umshukuru sana Mungu kwa haya maana sio wote wana bahati kama ya kwako
  Kadri unavyomshukuru Mungu ndivyo unavyopata amani, ujauzito pia huleta hali fulani ngeni usiyoijua jaribu kuwa unajumuika na wana ndoa changa wenzio au pia wenye uzoefu na ndoa za muda mrefu ktk kusanyiko lako ili kubadilishana mawazo na kutiana moyo.
  Tunakuombea uwe mama mzuri mwenye furaha
  Barikiwa

 3. nakupongeza ndg enjoyinghispresence jinsi ulivyomfariji dada yetu.nami namwambia kuwa mavi ya kale ni mbolea wala hayanuki hata kidogo.ya kale yamepita dada yetu hebu jisamehe nafsi yako shetani asikutishie kupitia hilo kosa cha msingi hapa nikutorudia zambi na Yesu ni yule yule alikusamehe siku ile ukapata wokovu nguvu ileile ya msamaha inafanya kazi hata sasa.songa mbele.

 4. Mwanangu Neema,

  Wewe ni Jasiri sana katika Kristo kwa kuomba toba kwa Mungu na kujutia dhambi yako baada ya kumkosea Mungu. Tendo la kumwambia Mungu kuwa unahitaji msaada na msamaha wake kupitia Jina la Yesu ndiyo ujasiri wenyewe ninaousema mwanangu. Wapendwa wengi hawafanyi hivyo lakini wewe umefanyai katika kujutia kosa la lenu. Kumbuka sio wote wanatubu kama wewe ulivyoutafuta wewe uso wa Mungu kuomba toba nakuomba ushauri kupitia blog hii “Strictly Gospel” ninayoipenda mmo.

  Silikiza Mungu hana tabia ya ukatili kwamba anamchukia kila mtu anayemwaomba msamaha na huchukia kuona mtu anakufa dhambini, lakini mauaji kukatisha tamaa, kudhoofisha, ushauri mbaya uongo nk hutoka kwa shetani kwani tangu mwanzo. Shetani anataka watu wote wapotee kama yeye alivyopotea kwa kumuasi Mungu

  Neema, Dhamira yako ya toba kwa Mungu ndiyo msamaha wenyewe kwani Mungu wetu kusamehe ndiyo tabia yake. Kwa kutusamehe sisi anatufundisha pia kusameheane sisi kwa sisi. Toba ya kweli ndiyo Msamaha wenyewe, usihofu mwanangu Neema wewe umesamehewa tangu siku ya kwanza ta toba yako.

  Mpenzi Neema, kuugua moyoni tunapomkosea Mungu ndiyo uhai wenyewe kiroho, wengine hawaugui kama wewe, hawakosi amani kama wewe kwao kila kitu sawa. Unapendwa sana na Mungu mwanangu.

  Aliyekufanya umkosee Mungu anaitwa shetani yeye huyo ndiye anayekufanya uone kama hujasamehewa makosa yako. Umesamehewa. Kumbuka, dhambi ni dhambi bila kujali sura ya tukio lililoisababisha. Wengine hukosa moja kwa moja kwa mawazo na wengine kwa matendo lakini hawakumbuki toba. Mungu alishakusamehe kwa dhamira yako ya kutaka toba mwanangu.

  Tangu mwanzo Mungu wetu kupitia Jina la Yesu hapendi dhambi kabisa na pia hapendi mmoja wetu apotee hata kidogo, narudia tena hapendi apotee hata kidogo iweje atuchukie tunapomkosea na kuomba msamaha kwa dhati?. Anayekukosesha amani siye Mungu kwani Mungu wetu ni wa Amani. Anayekufanya uikose amani baada ya msamaha ni shetani. Huyo hukuambia hujasamehewa na kukuzomea kwamba dhambi yako haisameheki nk.

  Mwanangu Neema, shetani usimwachie akusimulie lolote bali wewe mzomee mwambie kwa kujivuma kwamba “Shetani nakubali kwamba nilimkosea Mungu wangu kwa tendo baya, kwamba nimejutia dhambi yangu na kumwomba Mungu wangu kupitia Jina la Yesu anisamehe. Kwamba kwake Mungu kupitia Jina la Yesu kuna msamaha tele tele; kwamba usinisumbue shetani; kwamba wewe shetani ni mwongo; kwamba mimi Neema nimesamehewa na Mungu wangu hatazikumbuka dhambi zangu tena kupitia Jina la Yesu – Amina”.

  Kuhusu kumwambia mchungaji ni sawa huko uliko au kutokumwambia kama utakavyosukumwa kutokumwambia wewe binafsi; nina sababu katika hili. Hutokea mara kadhaa viongozi wengine wanaochunga au wanaotuchunga kiroho wanapopata tatizo kama hili au kama lako huliinulia bango kanisani ati wanamwaibisha shetani. Watasema, watatangaza, wengine watakufukuza, au kukufungia nk. hali hii imewaumiza watu wengi wakaacha wokovu kabisa. Ni haki dhambi ikikemewa kanisani kwa kusudi la kujenga sio kuaibisha.

  Wewe ni kama mwana mpotevu unapomrudia Bwana wako uwe wazi kwamba uliutumia uhuru wako vibaya, unapomrudia Mungu kwa kufanya toba unatakiwa ukumbatiwe, uvikwe pete na kufanyiwa sherehe kwa kitendo cha kumrudia Mungu. Sehemu nyingine makanisani unafukuzwa au ukafe mbele ya safari! Biblia nasema Hoja zenu na zijulikane na Mungu…. sio watu! Ngoja nikuambie siri hii ” Wengine tunaowaamini kihuduma wana matatizo makubwa sana kuliko yenu mbele ya Mungu” Hee Neema unashangaa juzi juzi tu kwa huzuni kiongozi mmoja wa dini nadhani Singida au Shinyanga kabaka mtoto wa miaka 12 kanisani!!! aaa la msingi tuombeane.

  Kuhusu mtoto aliye tumboni mwako mpokee katika Jina la Yesu, hajamkosea Mungu moja kwa moja kwani si kosa lake. Kumbuka watoto wote hutoka kwa aliye juu, mpende mwanao sasa, usimchukie kutokana na kosa lako ulilosamehewa; mwambie mwanangu nakupenda, mwambie nakupenda sana sana mwanangu, mtabirie mema mpaka atakapozaliwa. Usipofanya hivyo mtoto atakapozaliwa atakuwa na tabia ya kutokupendwa na mengineyo – mwisho usizikumbuke dhambi zako tena kwa Jina la Yesu.

  Jipe moyo mkuu wewe ni jasiri kusema kweli mbele za Mungu…. Ninyi ni wa thamani mno. “Natamani kama nini kuongea nanyi mkipenda kwa simu..”

  Mzee Makunzo C. H. M – 0754060996;
  Tanroads Songea.

 5. pole sana dada Neema inaonekana wewe kweli umeokoka maana majuto unayoyatoa ni kuwa unajutia kitendo hicho.dhambi kama uzinzi ni lazima ukamwambie mchungaji wako unaposalia ataamua pamoja na kusamehewa na Mungu,anaweza kukusimamisha huduma au kufungiwa kwa muda atakaoona,kusema mshikamane na mmeo kuficha dhambi eti mlitubu hapo sivyo huwezi kujua kiroho cha mwenzie,maana wengine huona mambo yote sawa nafsi ilishakufa.jiponye nafsi yako na mweleze mmeo juu ya kusudio hilo akatae akubali la muhimu ni toba kwa mch. na utapata amani moyoni mwako nakuhakikishia siyoeti kujiombea rehema mwenyewe.mungu akutie ujasiri wewe ni mtumishi wa kweli wa Mungu.

  kumbuka Daud alijaribu kuficha dhambi ya uzinzi kilichomtokea pamoja na kuomba siku saba bila kula wala kunywa mtoto yule alikufa.

 6. Pole sana dada yangu,soma Ayubu 14:7-9 kisha umuone mtumishi wa Mungu yeyote aliyejaa Roho na mwenye hekima,muweke wazi atakusaidia

 7. Kama Neema umemaliza chuo hivi karibuni, basi nisikuite dada bali nikuite binti yangu. Nimeguswa sana na manenKama nilivyotangulia kusema hapo awali “mkosaji anapotubu na kuomba toba husamehewa kabisa. Katika makanisa mengine kuna taratibu za kutubu kama vile:
  Toba ya sirini-mtu kumuungamia MUNGU wake peke yake na kama dhambi yake haijulikani kwa mwingine hakuna sababu ya kujitangaza kwa mtu. Na Mungu ambaye huona yote ya ndani humsamehe mtu wake.
  Toba ya sirini ya pili; ni mkosaji kwenda kwa Mchungaji wake na kumweleza yaliyo ndani yake kusha kuungama akiongozwa na sala ya toba. Mchungaji hapaswi kulitangaza jambo hili kanisani. Hii ndiyo nadhiri ambayo watumishi wa Mungu wamepewa, ni kama vile daktari hapaswi kutangaza ugonjwa wa mgonjwa wake hata aponapo.
  Toba ya wazi- kuungama mbele ya Wakristo Kanisani na kueleza wazi jambo lilikosewa na Wakristo au Washarika kumpokea kundini. Hapa napo huwa kuna ugumu wake maana hhuwezi kusema ya kwamba wote wataokuwepo kanisani siku ile wote hawana makosa pengine wapo pia lakini hawajajitokeza mbele. Hapa ni Mungu tu na wala si Mchungaji aonaye katiika mioyo yote.
  Bila shaka Mchungaji wa dhehebu mlilofunga ndoa yenu; aliwabariki wakati wa kuifunga bila kujua hali yenu (nasema yenu, nikimaanisha wewe mwenye kubeba mimba na baba mwenye mimba), mimi kama mtumishi wa Mungu nasema usikose mwelekeo sasa maana toba uliishafanya, majuto umejuta na ndoa umefunga. Lililobaki ni rahisi tu maana hata kama utaendelea kuficha; je, mimba siinakua na baadaye mtoto atazaliwa? Mungu akikujalie. Wapo watakaoanza kuhesabu tangu mlipofunga ndoa hadi mtoto kupatikani imepita miezi mingapi? Wanadamu hawatakosa la kuwahukumu. Ni Mungu tu ajuaye toba yenu. Shikamaneni pamoja katika hili, wewe na mme wako shika mkono wake mwendelee mbele ili Bwana ainiliwe kwenu. Kristo asema “katika unyonge ndipo ipatikanapo nguvu” kufuatana na 2. Kor.12:9
  Mwimbaji mmoja aliimba hivi:
  Have we trials and temptations?
  Is ther trouble anywhere?
  We should never be discouraged,
  Take it to the Lord in prayer.
  Can we find a friend so faithful
  Who will all our sorros share?
  Jesus knows our every weakness,
  Take it to the Lord in prayer
  Katika mikono yake atakutunza na hapo ndipo utapata amani na mwelekeo.
  Mimi pia namwomba anihurumie na kunirehemu na kunisamehe hata nitoapo maneno haya kwako.
  JIPENI MOYO MKUU

 8. Asifiwe Bwana Yesu.kitendo mlicho tenda sio chakufurahisha lakini inatendeka miongoni mwa vijana kama ninyi>mafunzo ya matayarisho ya ndoa,utakaso wa moyo,mawazo haukutiliwa maanani na wahusika wakuu wa ndoa yenu.Mungu wetu niwa huruma nyingi napia hutupa chance nyingine ili tujirekebishe,nivyema umejutia na kutubu,nenda mbele ya wahusika wakristo kujuta kwako. Kinywa chao itanena msamaha nawe utaona amani,na uzito huo utakuondoka. Yesu akumhukumu yule mama mzinzi bali alimwambia nenda na usitende hivyo tena. Mungu awabariki .

 9. Nashukuru watumishi wa Mungu wote mlionipa ushauri katika suala langu na Mungu awabariki na naendelea kuyatendea kazi maoni na ushauri wenu.
  Labda tu nijaribu kujibu baadhi ya maswali ambayo watumishi kama watano hiv wameniuliza kama ifuatavyo.
  -Ndugu Yusto Mchungaji wangu sikumwambia lolote na hadi nafunga ndoa hadi sasa hafahamu lolote juu ya hili mimi nilichofanya baada tu ya kukosea niliamua kuacha huduma zot nilizokuwa nafanya kuanzia kanisani hadi chuoni maana nilikuwa chuoni ambako nako pia nilikuwa ni kiongozi na nilifanya hivyo sikutaka kunajis madhabahu na ndoa haikufungwa kanisa nililokuwa naabudu maana ilifungwa kwao na mue wangu na hata huku tulikuwa tunaabudu madhehebu tofauti isipokuwa mkoani nilikokuwa natokea huyu mwenzangu tulikuwa tunaabudu pamoja na hadi sasa mimi nimeshamaliza masomo na nipo eneo lingine huko ndiko ninakoabudo
  -Kaka Alexander Kapinga naweza kuwa nimejibu baadhi ya maswali yako kwa maelezo yangu hapo juu,Labda katika kuomba msaada sina nia ya kujustfy toba niliyofanya nipo tayari hata kuchukua hatua nyingine zaidi ikinibidi natamani kumwona Mungu na natambua toba halisi ndiyo itakayo nisaidia nimuone Mungu.Ni kwelinilitambua kuwa hakuna mchungaji ambaye angefungisha ndoa akijua ni mjamzito sababu iliyopelekea kutoliweka wazi hili ni hofu iliyokuwa imeniandama kwani nilishakuwa nimeshuhudia dada yangu mmoja ambaye akiwa ni muimbaji kanisa nililokuwa nikiabudu huko mkoani alipata ujauzito na akategnwa kwa zaidi ya mwaka yule dada alijifungua mtoto akiwa ktk kifungo hicho mtoto aliendelea kukua yule dada hajafunguliwa na hadi ninapoongea ni zaidi ya miaka mitano sasa maana kipindi hicho mimi nilikuwa secondary hadi sasa nimemaliza chuo yule dada hakufunguliwa na alipoamua kufunga ndoa na huyo baba wa mtoto alifukuzwa kabisa pale kanisani nahajafunguliwa hadi leo na yule dada aliamua kuacha kusali pale kanisani mimi hilo lilinipa shida sana na sikutaka kukutana na kitu kama hicho hali nipo chini ya huyu mchungaji na sikutaka kuona nalea mtoto bila baba na nje ya ndoa.Lakini baadae nilishindwa kustahimili ndipo nilipoamua kuomba msaada. Lakini hata ikinibidi kutumikia adhabu kwa sheria za kanisa sipingani na hilo.
  -Ndugu Reb nashukuru kwa ushauri wako ndoa nilifunga bila mtu yoyote kujua hali niliyokuwa nayo
  Dada Rosemary ndoa nilifunga nikiwa bado nipo chuoni na baada ya hapo nilihamia kanisa analoabudu mume wangu sababu sikuendelea kuish chuoni.Kuhusu kushauriana na mume wangu hapo ndipo pamekuwa na shida maana hapo juu nimesemahuko mkoani nilikotokea tulikuwa tunaabudu pamoja hivyo hali akijua kwamba kitendo cha mimi kuliweka wazi suala hili kungesababisha kusimamishwa kwa suala zima lililokuwa linaendelea la maandalizi ya ndoa hakukubaliana nami,na mimi sikuweza kuchukua hatua pekeyangu hivyo nilikosa mwelekeo na sababu pia hata ktk misingi ya imani tumetokea tofauti japo wote ni wapentecoste mwenzangu aliamini kuwa toba yake binafsi ina nguvu zaidi na kila mtu alichukua hatua akiwa mwenyewe sababu wakati huo tulikuwa hatuishi wote.Nimejaribu kuongea nae baada ya kufunga ndoa ladba tuliweke wazi ila mimi ndiye nimekuwa sina amani mwenzangu anaendela mbele na shida ni kwamba nashindwa kuliweka wazi mimi pekeyangu maana natambua kuwa kuwa kwa sasa tunapaswa kufanya maamuzi kwa pamoja ndio maana nakosa mwelekeo.

 10. Pole neema zab ya 130 kama Bwana ungehesabu maovu ni nani angesimama? Mungu ameshakusamehe kazana kuomba kuvuka salama na anza kumnenea mtoto vile unavyotaka awe huku huko tumboni anasikia. mkumbuke Daudi alipokea msamaha ,
  Ibrahim baba yetu wa imani alipokea msamaha baada ya kuzaa na house girl.na madamu umejuta kweli kweli udumu ktk uaminifu ndani ya ndoa usimruhusu shetani akakujaribu kupitia kosa lako.

 11. Bwana Yesu asifiwe!!!!!! namshukuru Mungu katika hili kuwa Neema ametambua amemkosea Mungu na amechukua hatua ya kutubu na kuomba amani ndani ya maisha yake. La msingi ni aamini ndani ya moyo wake apepata msamaha na anachopaswa ni kusoma neno kwa bidii na maombi, kuhudhuria ibada hata za katikati iwapo hufungwi na muda na kumshukuru Mungu kwa Neema ya Msamaha ambao umepita kwako, songa mbele asiangalie na usimpe shetani nafasi k. Chapa mwendo Mungu yupo pamoja nawe,vunja mawazo ya kutosamehewa wewe sasa u huru Mungu mwenye Upendo mwingi na akutie nguvu Neema, Mungu anakupenda.

 12. Nimefuatilia ushauri na mafundisho yaliyotolewa na wapendwa kumshauri Dada Neema. Bila shaka ni vema kutambua na kujua nini maana ya MSAMAHA. Mimi nina hakika kabisa kama Dada Neema umejutia dhambi na kosa lako kisha kumwomba Mungu msamaha, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo aliyezichukua dhambi zetu zote, basi Dada Neema umesamehewa na usiwe na shaka katika hilo. Tena dada kumbuka jinsi wazazi wako walivyokupa jina lako “Neema”. Kuna sababu hapo!

  Put in mind that, the reality of God’s forgiveness can never be explained to someone who has not experienced it, and it cannot be proved by logical reasoning. This is because we do not reach forgiveness by hard thinking or good reasoning but we are confronted by it.

  Dada yangu katika Kristo, mtu apokeapo neema na zawadi hii kubwa ya MSAMAHA wa MUNGU, basi ni lazima kuishi na kukubali kuwa kama mtoto mdogo ambaye makosa yake yamesamehewa. Nina hakika ya kwamba Mungu atakulinda hata wakati wa kujifungua maana kujaliwa kupata mtoto ni baraka kutoka kwake.

  Jipe moyo mkuu, dumu katika maombi wewe pamoja na mwenzi wako. Roho wa Mungu awasaidie na kuwatia nguvu. Amina!

 13. Dada Mungu ni wa rehema kama bado nafsi yako inakuukumu ujue kuna vitu avijakaa sawa kama cha kutakiwa kufanya rekebisha pale ulipo anguka kama ulidanganya juu ya ndoa yako, aina ya vitu ambavyo si vya kimungu ulivyotenda unaweza kuomba rehema au kukiri mbele ya mtu au watu ulio wakosea na kama jukumu la kutubu ni lako pekee mumewe yeye hausiki inabidi umshilikishe na ukiweza shilikisha watu wako wa karibu kama BWANA YESU alivyo washilikisha Yohana ,Yakobo na Petro.

 14. Shalom wapendwa
  nimejifunza mengi hapa, ila naomba tu kuongezea hasa kama walivyouliza wapendwa wengine
  je dada Neema umehamia kanisa jingine baada ya kuolewa?
  je kosa mlitenda na mwenzio, vipi yeye anasemaje kuhusu hili, na anasemaje kuhusu hali yako ya kujihukumu? pengine hukumu yako ni kwa vile unahisi mwenzio hajutii na hivyo unaona hajasamehewa, wapendwa mie naona kwanza Neema angepeleka hili suala kwa mumewe, mtu wa kwanza kumweleza shida na maombi yako (labda akatae au kupuuzia) ni mumeo. Itakuwa ngumu sisi tukushauri uanze kuchukua hatua wakati mumeo hajui hili. Nakuomba kuwa muwazi na mwenzio na kwa pamoja mtubu kwani kosa mlifanya wote ili ndoa yenu iwe na baraka na amani ya Kristo ndani yake. Baada ya hapo muombe Mungu akupe amani na uwezo wa kusahau yote uliyomkosea, jibidiishe kuomba na kusoma neno ili usipate muda wa kuwaza hayo
  Jenga tabia ya kuomba pamoja wewe na mwenza na mshirikishe haja za moyo wako, huku nje utapewa ushauri hata wa kuhama huduma kitu ambacho kinakuchanganya, muombe ushauri kama mtahitaji kwenda kumuona mchungaji kwa pamoja na si wewe ukamtajie mchungaji kosa lake! Nakushauri anza kuomba kwa ajili ya mtoto wako jichukulie kama mama sasa na si mtoto tena mpendwa wangu hebu fikiria huyo mtoto ukiendelea na hukumu yako atakuwaje, pia jichukulie kama mke na jenga ushirika na mumeo lakini uliondani ya Kristo endapo unaona kuwa kuna tatizo ktk ndoa au mwenza wako ndipo uombe msaada nje. Ni ushauri wangu. Tunakuombea.

 15. Hiyo roho ya kujisikia hatia muda wote huo ni roho ya shetani. Ikatae kwa mamlaka ya jina la Yesu. Shetani hupenda kuwakumbusha watu wa Mungu juu ya makosa waliyokwishayatenda kwa huko nyuma na kuondoa ile nuru ya msamaha maishani mwetu. Mara kadhaa tunaendelea kuumia kwa mabaya tuliyoyatendana kana kwamba Yesu alisema uongo ya kwamba njooni wangu ninyi msukao na kulemewa na mizigo ya dhambi….. La msingi, Amini kuwa ulishasamehewa tena zamani za kale. huna haja ya kwenda kwa pastor kutubu wala kwa nani ila kwa Yesu tu. Kuwa na amani. Songa mbele. Usitende dhambi tena! Kikubwa, mtafute Mungu, itafute ibada yake halisi.

 16. Neema Mungu alikusikia siku hiyo hiyo ulipoomba msamaha. unachotakiwa kujua ni kwamba haijalishi ni makosa mangapi umefanya Mungu amekusamehe yote. hebu vuta tu picha kwa sasa ya kwamba wewe ni mtoto wa Mungu unayependwa sana. kisha amani itaingia moyoni mwako mara moja. unajua Mungu huwa hayuko tayari kurekebisha kinakusuta. ukiona umeshindwa mwambie Yesu naomba amani utauona utukufu wa Mungu ubarikiwe.

  Ev.Moses Kapaya Mayila
  New Hope Ministry Tanzania

 17. Tazama ya kale yamepita yote yamekuwa mapya,umesamehewa neema,ni wewe kukubali thats it.

 18. Bwana asifiwe dada Neema na watu wa Mungu mnaochangia humu kumshauri dada yetu.
  Jambo analopitia dada Neema i can feel it, lakini kama baadhi ya watumishi walivyokushauri ndiyo unatakiwa ufanye hivyo dada, kuna dhambi zingine zinahitaji kwenda mbele za kuhani kuomba msaada wa kukuokombea, maana umejaribu sana kuomba toba wewe mwenyewe hujapata amani, leo tunakushauri nenda kanisani kwa mchungaji wako mueleze vile unavyohukumiwa hata kama mlidanganya wakati wa kufunga ndoa bado mchungaji hayupo kwa ajili ya kukuhukumu atakuombea rehema na wewe mwenyewe utatubu mbele za Mungu, nina uhakika kama utakuwa wazi baada ya maombi ya toba utapata amani tu. La msingi uwe wazi dada maana Bwana Yesu hapendi hata mmoja wetu apotee bali wote waifikilie toba, kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu ndivyo inavyokuwa kwa Wachungaji ambao kweli ni wa Bwana Yesu wanafurahi mtu anaporudi na kutubu kwa kile kinachowatesa maana Maandiko yanasema kuna furaha kwa mwenye dhambi mmoja akitubu.
  kuna maswali watu wamekuuliza ni kwa nia nzuri tu, je hiyo ndoa ulifunga ilijulikana una mimba au ulidanganya pia? labda ndiyo kinachozidi kukuhukumu,
  All in all Mungu anapenda wale wanaotubua na kuanza tena maisha na yeye japo ina gharimu .
  But Mungu ni mwema tena anahuruma na ni mwenye rehema anasamehe uwe wazi utubu na amini utasamehewa na kupata amani moyoni mwako.
  Ubarikiwe na Bwana

 19. Kaka Kapinga what is the scripture basis of your ushauri? I don’t see any justification in the theology you are placing before us. Mungu ni Mungu. The law kills but the Spirit give life! Dada Neema the fact that you are married to the father of your child is good. Your child would have a loving and caring home. At this point it doesn’t matter how that marriage started but it does matter how you would life from then onward. We don’t need to know any personal details than what you disclose as brother Kapinga is suggesting. May the word of God bring healing and liberty in your life! Jesus in many instance made this statement “sin no more.” So be free and life your life for the Glory of God!

 20. ni kweli kabisa kama wengi mlivyosema kuwa Mungu anasamehe ila kama kweli dada unadhamiria kuona ile furha ya WOKOVU inarudi tena ni muhimu sana kila step uliyokosea uiweke wazi mi ninavyojua hakuna kanisa ambalo linaamini kuokoka lingekuruhusu kufunga ndoa wakati umeshaanguka. pili naomba uweke wazi ulikuwa unasali kanisa gani na je hiyo ndoa ulifungia hapo hapo kanisani kwenu? je mchungaji alijua kuwa mmeanguka alafu akawafungisha ndoa? usitafute msaada wa maandiko ili uweze kujustify toba yako ambayo unasema umeomba rehema. Mungu huwa hasikii maombi ya mwenye dhambi ndio maana anasema watu waliookoka wamefanyika makuhani ili waweze kupatanisha wanadamu wengine na Mungu kwa kuwaongoza kwenye toba. Ulipoookoka nafikiri kuna mtu aliyeokoka aliye kuongoza sala ya toba pale sio kwamba alikuwa tu anakuongoza yale maneno bali pia alisimama kama kuhani kukupatanisha na Mungu kwa njia ya KRISTO BWANA WETU.N a hata mara baada ya anguko lako basi imekupasa kumrudiA Mungu kwa njia ile ile uliyopatanishwa naye mwanzoni usibypass hata moja na usiogope hata kidogo kueleza ukweli huo kwa mchungaji wako.

 21. All in all Mungu ni mwenye rehema na baba asiye na makuu,,,ukikosa then ukajutia na kutubu mungu husamehe,,,dada neema ulishasamehewa amini na kemea huyo roho wa kila muda kukufanya uwaze jambo ambalo mungu amesamehe

 22. mpendwa pole naelewa unachokipitia,nami kuna namna nilipitia hali hiyo na ilinitesa sana,lakini baada ya cancelling ya kiroho nikaachilia,kwanza kikubwa ni kujisamehe,hakikisha unajisamehe Mungu wetu ni wa upendo mkuu ameshakusamehe ila wanadamu huwa tunajihukumu sana mpaka twamkosea Mungu.yaani nakuhakikishia ukijisamehe,kisha ukamsamehe mwenzako na ukampenda malaika anayekuja na ukasongambele umepona.barikiwa na hakikisha una amani wakati wote

 23. dada Yangu Mungu akurehemu, ni maombi yangu kwako< Mungu apate kukurehemu, Dada ameomba watu wa Mungu wapate kumsaidia, na nafikiri uponyaji wa nafsi yake na upendo wa Mungu unatakiwa kuendelea kupita ndani yake mpaka hali ya kusikia hukumu moyoni itakapoondoka na kumezwa kabisa, na hali mpya ya faraja, amani, iingie tena moyoni mwake, wapendwa, nafikiri tuingie kwenye maombi na kuweza kuomba pampja naye na kwa ajili yake, She has to be restored to the spiritual tone in heart and in the mind, kwasababu inawezekana ametubu na kutubu mpaka toba imekuwa kitu kigumu kwake, ndio kazi ya watu waliokoka, kuchukuliana mizigo na kusaidiana katika udhaifu, hata mimi niliwahi kupata tatizo au kuanguka harafu nikatubu lakini kwa wiki 2 hukumu kali ilikuwepo moyoni, lakini baadaye upendo ule wa Mungu na ile furaha iletwayo na ile fellowship na uhusiano na Mungu ilirudi tena, nikawa restored, hata huyu binti anachohitaji ni restoration,
  Kitu kingine ambacho wapendwa mnabidi mkiangalie, ni discipline, Mungu huwarudi na kuwaelekeza wale anaowapenda, hali kiyo anayosikia huyu binti ya kuhukumiwa moyoni inawezakena ikawa ni discipline ambayo Mungu anaifanya kwake, yaani Mungu anamrudi, wakati huu unaweza ukajisikia vibaya sana, Mungu anapokuadhibi lakini baada ya discipline kuisha utatoka safi kama vile dhahabu iliyopitishwa motoni , kwahiyo tuwe waangalifu tusije kupingana na discipline ambayo Mungu anakupa, unaweza ukawa umetubu lakini bado discipline ya Mungu ikawa palepale, na discipline ni kitu kizuri, unaporudiwa na Mungu usikasirike bali ufurahi kwasababu wote Mungu anaowapenda huwarudi.

 24. Kwa Vijana tulio katika mahusiano,Hata kama mmeokoka mnaweza kuanguka kwenye uzinifu.Basi tujifunze kwa dada yetu taabu anayopata ya kumrudia Mungu(Kama ni Ukimwi maana yake angeshaupata)Mpaka sasa ni rehema tu za Mungu zinazomfanya kusimama na kuomba ushauri.Wengine huwa wanapotea Jumla.Mungu ni wa rehema tele.Ebrania 12:7-(Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili;Mungu awatendea kama wana,Maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?Kuna mchangiaji hapo juu ameshauri dada kwenda kanisa la pool of Siloam,si ushauri mzuri.Maadam ametubu Mungu amemsamehe kabisa.Kwa msaada wa kiroho zaidi analo kanisa lake analoabudu wapo wazee wa kanisa,wamama,walezi pia Mchungaji,atasaidika vizuri zaidi naamini.

  Mbarikiwe waanzishaji wa blog hii,mimi ninajifunza mengi sana.

 25. Amen,nimekuelewa dada Neema ila ningeomba kujua yafuatayo:-Mchungaji wako alichukua hatua gani baada ya wewe kuanguka?,Ulimshirikisha ktk maombi yako? Ndoa yako ulifungia palepale ulipokuwa unamtumikia Mungu mwanzo? asante

 26. Pole sana dada Neema,

  Mungu anasamehe unapoenda kwake kuomba toba tena hakumbuki tena dhambi zako akishakusamehe,isaya 43:25, isaya 44:22 .Upendo wa Mungu ndio uliomfanya amlete Yesu kwa ajili yako kwa iyo hamna haja ya kujihukumu tena, angalia hapa ufunuo1:5b ” Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake” angalia tena hapa 1yoh2:2″naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu…..”Yesu ni kipatanisho means anakupatanisha tena na Mungu kwa sababu dhambi ilikutenga na Mungu Kwa iyo ulipotubu Yesu alikupatanisha na nafsi ya Mungu kwa damu yake 2Kor5:19″Yaani Mungu alikua ndani ya Kristo, akiupatanishaulimwengu na nafsi yake ,asiwahesabie makosa yao…”

  Kitu cha muhimu sana kwako ni kujikumbusha jinsi Mungu alivyo wa rehema ,tafakari upendo wake na neno linalosema juu ya msamaha wae kwako.Soma maombolezo 3:22-24.kama Mungu hakumbuki tena uovu wako na wewe usikumbuke tena Omba Mungu aondoe hiyo kumbukumbu ndani ya moyo wako na kurejesha tena uhusiano uliokuwepo kati yako na Mungu..
  Mungu amejaa rehema na kweli yeye anashika agano lake na rehema zake.Adui anataka akupotezee muda wa kumzalia Mungu matunda kwa njia ya kujihukumu,simama tena uendelee mbele.

  MUNGU AKUJAZE FURAHA YAKE KATIKA ROHO MTAKATIFU NEEMA.

 27. Pole sana dada Neema kwa masahibu yaliyokukuta. Mungu ni Mwenye Neema dadangu. Mara nyingi sisi binadamu hukosa mbele za Mungu, Lakini tukitubu kwa moyo Mungu hutusamehe. Amini kwamba Mungu ameishakusamehe. Jambo ambalo uliamua vizuri, ni kutokutoa mimba hiyo. Usiendelee kusikia hatia rohoni mwako. Mungu ameishakutangazia msamaha, na tunakuombea ujifungue salama ili mtoto utakayejifungua awe mtoto mwema na mwenye furaha.

 28. mimi ni mtumishi ushauri wangu mungu ukitubu anasamehe na kusahau ila wewe bado unajihukumu nenda kwenye kanisa la the pool of siloam utakutana na watumishi wa mungu nao watakuombea na tatizo hilo litakwisha kabisa watakufundisha neno la mungu kuvunja misingi mibovu tabia ya asili utakuwa huru kabisa

 29. Your sins have been forgiven because you have accepted The Lord Jesus Christ as your Lord and personal Saviour, and you have been assured to enter heaven and live eternally. No one will ever take away your salvation, no matter what!

  Whenever yo backslide, you need to repent and forget.

 30. Dada Neema mwenye amekupa huo usaidizi wa kwanza yuko sawa. Yale ambayo amesema ni ya kweli sana. Mungu amesikia kilio chako na sasa ni wewe kuamini kwamba Mungu husikia wanao mlilia kutoka kwa moyo, na huwapa chochote wamwombao kupitia jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo. Amini kwambo umesamehewa na ueendelee kuishi maisha yenye furaha.

 31. Dada Neena BWana YESU apewe sifa.mimi najua wakristo wengi tuna shida ya kusimamia neno la MUNGU,unajua hakuna ujanja zaidi ya kusimama kwenye neno na kuliamini na kulikiri kinywani mwako.ikiwa umefanya maombi ya rehema na toba biblia inasemaje kuhusu toba?je MUNGU hakusema japo dhambi zako zikiwa nyekundu kama bendera zitakua nyeupe kama theluji? Je si MUNGU aliyesema anatusamehe dhambi zetu kwa ajili yake mwenyewe? Je hakusema kuwa ataziweka mbali nawe dhambi zako kama mashariki na magharibi zilivyo mbali na kamwe hatazikumbuka kabisa? Dada hadi hapo huna sababu ya kujihukumu maana kama MUNGU amekusamehe hakuna hukumu tena moyoni bali huja furaha ya wokovu kupitia Roho mtakatifu.hivyo napewnda nikwambie wazi anayekukumbusha kosa ulilotenda ni adui shetani anajaribu kukuonesha kuwa hujasamehewa na ukiendelea hivyo hutaona furaha ya wokovu hivyo utareconcile na dunia na kurudi mwilini ukaacha wokovu. Fanya hivi anza kumshukuru MUNGU kwa kukusamuhe,mkaribishe Roho mtakatifu abubujike ndani yako na mkemee shetaniNtumia mamlaka uliyopewa mpinge shetani naye atakukimbia,funga roho za hukumu fanya maombi ya vita dhidi ya uongo wa shetani haitachukua muda utafurahia maisha. Acha kumwamini shetani amini na usimame kwenye neno la MUNGU
  Download the latest BlackBerry® applications from Zantel on http://www.zantel.com/zantelapps

 32. Dada Neema pole sana ila jua kitu kimoja the day you cried out to God and asked Him for forgiveness, God forgave you! You now need to forgive yourself. You can not really go back and undo what has already been done. You can only repent, learn from it, learn to overcome and move forward. It is now part of your past. Learn to acceptance God’s total forgiveness for your life. God sees your heart and knows your love for Him. He has forgiven you but have you forgiven yourself? All things works for good for those who love God for those who have been called according to His purpose. No matter what has happened, God purpose for your life will stand. There is no one who had suffered more shame and humiliation than Christ. He also come to remove that shame in our live so that we can walk in freedom, liberty and confidence. Even the mighty can fall but it’s how they finish the race that matters. Success is the ability to take our failure, pick ourselves up, be able to move on with life and fulfill God’s purpose in our lives. Hakuna dosari kwenye huduma yako bali God has now given you grace to be an encourager and someone who will proclaim His grace, mercy and forgiveness in greater depth. Believe what God word says about you! You are blessed because your transgression are forgiven and your sins are covered!

  Roman 8:1 and 8:15
  Isaiah 61:7
  Psalm 103: 3-4
  Psalm 32:1-2
  2 Cor 7:10

  May God restore the joy of your salvation and your confidence to go before Him!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s