Naomba kujua kuhusu misukule

Bwana Yesu asifiwe napenda kujua biblia inasemaje kuhusu masuala ya misukule? ni kweli huwa wanarudigi?

–Giga

Advertisements

16 thoughts on “Naomba kujua kuhusu misukule

 1. Shalom wapendwa

  Mimi naona ni vizuri kwa watu walio na uhakika kama hao misukule wapo na kama jambo hili limesemwa katika biblia bora wakalisema lvizuri bila kuleta mashaka
  Lengo sio kumtukuza ibilisi ila kuwa na uhakika wa kile mtu anachotakiwa kusimamia. Huwezi kuomba kumrudisha msukule kama hata huna uhakika kuwa ni kitu cha ukweli. Maana kuna vitu wazungu wanaviita MYTH, ni vitu vinavyofikirika tu ila havina ukweli wowote.
  Kuna ndugu wanafiwa na wapendwa wao katika mazingira ambayo ni vigumu kupokea na hawa mara nyingi ndio huwa na wasiwasi juu ya jambo hili, je kaitwa kweli na Mungu au ndo kafanywa msukule. Sasa wanaoamini kuwepo kwa kitu kama hiki wangetusaidia kujua haya na ikiwezekana kujua ni mazingira yapi mtu anakufa na kuwa msukule au anaitwa na bwana. Maana unaweza kupoteza muda kutaka kumrudisha mtu ambaye BWANA amemwita.

 2. hakuna mtu aliye chukuliwa msukule ktk biblia hao wa misukule watuambie hiyo elimu wametoa wapi

  hizo ni shuhuda za wachawi na waganga zimeingia kanisani na zimekua mafundisho eti misukule! ha! Hapana!!!!

  tupe kifungu cha biblia wewe unaye amini misukule. aliye ludishwa

  lazoro hakuchukuliwa msukule biblia inatuambia kuwa alikufa kabisa na kuanza kuonza sasa akafufuliwa

  hakuna msukule

  YESU NI ZAIDI YA YOTE

 3. Nawashukuru wote mliochangia kujibu swali langu la msukule, sababu kubwa ya kuuliza hili swali ni kwamba ndugu yangu alipata ajali akiwa na wenzake kwenye gari na akafariki hapo hapo lakini huyo kijana aliekua anaendesha hilo gari hakufariki na familia yake ni matajiri sana wanafanya biashara ya madini ya tanzinite na hiyo familia ina kashfa kubwa ya uchawi mjini na ndugu yangu alipofariki usiku huo huo mdogo wake aliamka usiku na kusema ametokewa na marehem na kwamba yeye na mwenzake waliepata nze ajali na kufa hawajafa bali wamechukuliwa. Nimemuuliza huyo ndugu wa marehem mara nyingi tu kama anauhakika alikua haoti? Amesisitiza marehemu alimtokea na kumwambia hajafa kachukuliwa. Na watu wengi wamekua wakisema ndugu yangu hajafa hao marafiki zake ni wachawi.
  Sasa mimi kama ndugu wa marehemu nimekua nikijiuliza maswali mengi maana mazingira ya kifo cha ndugu yangu yamejaa utata. Na ninashauku yakujua je lisemwalo ni kweli mbona mungu akaruhusu hili litokee kama nikweli? Najua ndugu yangu alikua hajaokoka alichagua kujihusisha na marafiki wenye kashfa ya uchawi japo yeye hakuamini kama marafiki zake ni wachawi

 4. Mpendwa, Rosemary Sharom.

  Asante sana ndg yangu. Kwa sasa nimekupata vizuri sana.

 5. Shalom Mabinza
  naona hukunielewa mie nilichojibu hakina tofauti na wewe nimesema kwa uelewa wangu wa tukio la msukule pekee utotoni sioni tofauti na mtu mwenye pepo ingawa pia kuna mtu anaweza kuwa na pepo tusijue na kuna wale wenye pepo kama yule kichaa aliyekuwa na jeshi wote mie kwangu naona ni pepo tu amb ao watamtii Mungu wakikemewa au mtu akiokoka.
  Ninaposema iwapo mtu umekata shauri kuokoka umeenda ktk kanisa umesalishwa toba na kukiri kumpokea Yesu ndipo mapepo yanajidhihirisha je wakuache ukae nayo au? Ndio maana yangu kusema muhimu watu waombewe na kulijua neno hayo ya sijui elimu majini, misukule siko huko sio agizo letu ni mapepo tu wote watatii nguvu ya Mungu.

 6. Wapendw,mnakwenda wapi tena?

  Hamjambo lakini?
  Msukule ni Mtu aliyefanywa kuwa hivyo na Shetani. Maana ya Neno msukule halitajwi popote na Biblia. Sijaelewa kwa nini Watu wanataka kujifuza na kujua habari za Misukule! Maana na Sifa za Misukule anazijua Shetani, yeye ndiye huwafundisha waganga na wachawi maana na sifa za Maneno au kazi zake! Kazi yetu ni moja tu KUZIHARIBU kazi zake zote, bila kujali ni Msukule, Kichaa, Mwehu, Punguwani, Taahira ya ubongo, ana Jini amelogwa au hata amekufa! Wala haipo haja ya kupata historia ya mgonjwa huyo, Sisi hutamka tu “Kwa Jina la BWANA YESU KRISTO haya…….!” Awe Msukule au la, Shetani atajijua mwenyewe!

  Nimepitia maelezo yote hapo juu kwa utulivu, sijaona hata mmoja anayeeleza maana na Sifa za Mtu-msukule kwa fundisho la Biblia. Nafikili ni kutokana na Neno lenyewe kutokuwemo katika Biblia takatifu. Ni kweli Biblia haifundishi Maana na sifa za Misukule, Je, ipo haja gani kujua nakujadili hilo?
  Au kuna Mtu kati yetu anahisi kuwa huenda tayari keshakuwa Msukule, au anataka kuwa msukule hivyo anataka kujua Sifa za Msukule? Kama sivyo, kwanini kusumbukia Misamiati ya Shetani? Usiteseke kwa Fundisho lisilotoka kwa Mungu! Hofu huwafunika wasiompenda Mungu, Biblia husema Mtu mwoga hampendi Mungu! Kama huna Yesu kikweli, hata ukijua aina zote za Mapepo na Lugha zao zote HOFU kamwe haitaondoka kwako, maana USHINDI UPO KWA WASHINDITU!

  Biblia inasema NENO lolote lililomo katika Biblia NDILO pekee linafaa kwa kufundishia! Haijasemwa kuwa tutayashinda Mapepo kwa kuyajua aina zake au majina yake! Kujua maana na namna ya Miskule kunakuimalishaje Kiroho? Kwakuwa Shetani mwenyewe kupitia wanganga na wachawi wake anaijua misukule, ni BORA kila anayetaka kujua maana na Sifa za misukule, AWE mwafunzi wa Shetani japo kwa Dakika moja ili ajue Maana au Sifa za Misukule ili aishibishe tama ya moyo wake! Ukiwa na hamu ya Kuamini UONGO unapewa kuamini huo, ili upotee!
  Huwezi kujua Jambo la Sayansi kwa Mwalimu wa Historia – kila Mwalimu na Kipindi chake!

  @Rosemary, sijakuelwa vizuri; yawezeka kweli Mtu aliyeokolewa na Yesu Kristo akawa na Pepo na kuhitaji kuombewa tena?

  Nisaidie tafadhali.

 7. Naomba kumalizia ushauri wangu sio kuwapinga wanaoombea watu ila tujiulize iwapo wewe unahubiri neno na watu wanaookoka wana mapepo ungefanyeje? Hili ni swali ambalo Yesu pia aliwauliza mafarisayo waliohoji kuponywa mtu siku ya sabato au ibada. Vilevile sitofautishi na wale waliotilia shaka uwezo wa Yesu kuponya kama sio unatokana na pepo mkuu au Beelzbuul. Yesu alisema endapo watu wanatubu na kuponywa yaani wanamrudia Mungu na wanafunguliwa kutoka utumwa wa shetani basi ufalme wa Mungu umetujia! Kuna shukrani kubwa na utukufu mkuu kwa Mungu ikiwa nguvu za giza zinashindwa, ndio maana Yesu alisema yule mwanamke aliyejitolea marmar ya bei mbaya kwake na kumsujudia ni vile alisamehewa dhambi na kuponywa pepo waliomsumbua sana hivyo ile ilikuwa njia yake kuonyesha shukrani. Kanisa bila ya nguvu za Mungu kudhihirika mimi kwangu naona sio sahihi ingawa siungi mkono kabisa elimu za majini wa aina za misukule isipokuwa kulijua kwa undani neno la Mungu na kulitenda nalo litakuweka huru. Mbarikiwe

 8. Shalom
  naomba nichangie vile ninavyoelewa kutokana na live experience nikiwa mdogo.
  Kuna kipindi niliishi Mwanza na wazazi wangu, ilitokea watu waliwakamata “misukule” ambao sijui jinsi ya kueleza ila walikuwa ni binadamu hawajitambui wana nywele ndefu, kucha ndefu na hawaongei ila kuguna na kula kwa namna ya ajabu. Waliwakuta kwa bibi mmoja amabye watu walimshuku mchawi kwani alikuwa mzee sana ila analima mashamba makubwa bila vibarua. Nnachokumbuka ni kuwa walijitokeza wazazi wao ambao walidai kufiwa na watoto wawili kwa wakati mmoja hapo kijijini wanaolingana umri na hao misukule….tulikuja kuhama Mwanza na sielewi nini kiliendelea ila nilitaka tu kuwaambia kuwa hivi vitu vipo kabisa hapa Tanzania.
  Tukija kwa muuliza swali yeye ameomba kujua hili kibiblia, mie ninachoona maelezo ya hao misukule hapo juu hayatofautiani na yule mtu aliyekuwa na pepo wengi wakati wa Yesu na aliyekaa porini na kutumikishwa na hayo mapepo, sioni tofauti yake, nadhani hata hao misukule ni wachawi wanawatumia kwa kuwa wana pepo kuwafanyisha kazi. Kila mtu anaweza kuita vifungo kwa majina mbalimbali kulingana na mazingira na mila za mahali husika, watu wa Iringa walikuwa wakiita vinyamkera, watu wa pwani majini, watu wa kanda ya ziwa misukule nk lakini tukubaliane tu kwamba vyoote hivi ni pepo wachafu ambao wanaweza kuwa na mtu au ndani ya mtu na kumuadhiri kwa viwango tofauti kama ilivyokuwa ktk Biblia mfano mwanamke mvuja damu hakuwa hata anajulikana hata angeficha kuponywa kwake, mtoto bubu mwenye kifafa na kisha mwanaume aliyekuwa na jeshi la pepo waliotolewa na kuwaingia nguruwe. Hii tunaona hata Yesu mwenyewe alituasa wazi kuwa kuna aina ya pepo huwezi kukemea au akatoka tu bila ya kuwa na nguvu ya ziada kwa kufunga na kuomba. Ni mtazamo wangu

 9. Sina haja ya kujua sana kuhusu misukule ila natafuta kumjua sana Mungu aliyeumba mbingu na nchi ndio msaada wangu Ayubu 22:21, watu wengi wamebaki na hofu nyingi na kubaki kuzijua zaidi habari za ibilisi kuliko habari za Yesu na kujikuta wametekwa pasipo kuwa imara ndani ya Kristo. Kuna watu kila iitwapo leo tangu asubuhi mpaka usiku vinywa vyao vimetawaliwa na misukule na shetani na huku wakimtaja Yesu mara chache. Tubadilike wapendwa na tumwishie Mungu ili tuyatende mema

  Siku moja nilisikia mhubiri mmoja akihubiri kanisani eti kuna majini 99 hivyo akawa anawafundisha waumini juu ya aina hizo na kila jini na kazi zake, Sidhani kama itakuwa msaada kwetu zaidi ya kuwafanya watu kuwa na hofu, hii ni kuingiza uganga wa kienyeji makanisani. Ukikaa vizuri na Mungu mambo ya misukule haitakuwa issue kwetu maana Bwana anajua na anashughulika nayo pasipo kufanya kama ndio ajenda ya kila siku.

  Sina nia ya kuyakashifu makanisa yanayofanya maombezi ya misukule ila ushauri wangu isiwe ndio ajenda ya kila siku. Ndani ya nyumba ya Bwana kuna mambo mengi sana na mafundisho mengi na muhimu kwa kanisa hivyo tubadilike tusibaki katika misukule na mapepo tu kila siku.
  Mungu awabariki wote.

 10. Shalomu,

  Pamoja na kuwa si mimi niliyeuliza swali hili, lakini nilipenda kujua kuhusu suala hili, hivyo nimepitia majibu ya watu mbalimbali waliojibu hapo juu, hata hivyo nimeshindwa kupata majibu yenye uwiano wa maandishi.

  Ndugu Edwin Richard ametueleza kuhusu CD ya aliyekuwa mganga/mchawi. Pamoja na kuwa sijaiona CD hiyo, lakini haijitoshelezi kuweka kutumia ushahidi wa CD ya mtu bila kuwa na uhakika wa kimaandiko.

  Ndugu James Lue umenukuu Ezekiel 28:14, Isaya 42:22 na Ufunuo 18. Nimesoma Ezekiel na Isaya na sijaona uhusiano wa hicho anachokisema na maandiko hayo. Nakuomba ndugu James usisimamie tu kwenye msitari mmoja, jaribu kusoma angalau aya nzima ili kupata nini kilikuwa kinazungumzwa katika aya hiyo.

  Nitafurahi ndugu waliochangia na wengine wenye ufahamu kuhusu suala hili watusaidie kwa kuweka maandiko.

  Mungu awabariki

 11. Njoooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!Rudishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kwa jina la yesu.uchawi upo na wamewachukuwa wengi na sasa ni zamu yetu kuwarudisha kwa jina lipitalo majina yote, wanarudi kwa jina la yesu .wachawi walikuwa hawajawaza kuwa kuna kuumbuka walifika mahali wakajiona mungu hawakujua kuwa yupo MUNGU wa miungu wamepigwaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!-NI SAA YA UFUFUO NA UZIMA

 12. Jana nilijibu swali la Giga lakini kumbe sikuwa makini kiasi cha kutosha hivyo jibu langu halikufika mwisho. Giga anauliza kama hawa misukule wanaweza kurudishwa. Katika mstari wa kutabu cha Isaya nilionukuu, yaani sura ya 42: 22, Bwana anasema: “lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye Rudisha.

  Maana yake hapa ni kuwa, hakuna mtu anayemwambia shetani rudisha hao watu uliowaficha. akitokea mtu wa hivyo, basi kwa shetani ni lazima atawarudisha watu hao; hii ndiyo maana iliyo kwenye mstari huu. Kwa hiyo, kwa kifupi jibu ni NDIYO misukule wanaweza kurudi.

 13. Kuna CD moja waweza kupata imeandikwa Mwalimu wa wachawi aokoka imeelezea vizuri kuhusu misukule.

  Nilichojifunza kwenye CD hiyo ni hiki hapa.

  Mganga(Mchawi) akitaka kumchukua mtu msukule kuna miti fulani ya asili ambayo huwa ikichanganywa pamoja hutoa povu maalum ambalo ni matokeo ya sumu inayotokana na kuchanganywa kwa miti hiyo ambayo haipatani.Mara baada ya povu ilo kutokea kuna aya maalum za kipepo zinasomwa katika povu ambalo linaweza kuwa kwenye beseni.Mtu anayetaka kuchukuliwa msukule Jina lake linatajwa na anatokea kwenye ilo povu maalum lilosomewa aya za kipepo halafu anaanzwa kuitwa kwa jina lake huku akibembelezwa kabisa.Huyo mtu huko alipo ufahamu wake huanza kupotea na kujikuta akiaanza safari kimwili kabisa kuelekea huko anakoitwa hata kama hapajui atafika tu!Akifika huko huvuliwa nguo zake zoote na kuanza kupakwa lile povu mwili mzima na kwa kufanya hivyo inamsaidia mtu huyo kufichika popote atakapoenda hawezi kuonekana,kama kiungo chochote kwenye mwili wake hakitapakwa povu basi popote atakapoenda ataonekana hicho kiungo.Akishapakwa povu kuna jini linaletwa jirani na huyu aliyepakwa povu linakuja kwa sura ya mtu kabisa halafu nalo linapakwa povu kisha ngozi lilokuja nalo hubabuka na kuchukua sura na mwili halisi kabisa kama mtu yule aliyechukuliwa msukule.Kisha baadaye jini hili(Pacha ya mtu halisi) hutumwa kurudi kule alipokuwa yule mtu aliyechukuliwa msukule na kuigiza kuugua kwa muda,mara nyingi huchukua siku saba za kuugua halafu baadaye hufa,baadaye watu huzika wakizania wamemzika mtu halisi kumbe ni kuigiza tu.Offcourse kama hatatengenezwa jini pacha basi tunapata picha kwamba anayechukuliwa msukule anaweza kupotea jumla bila hata kufa.Kule alipochukuliwa mtu msukule huendelea na maisha ya mateso na huweza kufa kama kawaida,Cha muhimu ni kuwa na Yesu kama huyu Mwalimu wa Wachawi (Sheik Salum alikuwa mwalimu wa chuo cha kiislamu Alnoor-Temeke) Yesu alimuokoa,basi tumshike Sana Yesu wetu.

 14. Misukule ni jambo linalohusiana na uchawi. Na uchawi ni suala ambalo Biblia katika sehemu nyingi tu inakiri kuwa upo.

  Jambo moja la kukumbuka ni kuwa mbinu kubwa kabisa ya shetani kufanya kazi zake kwa mafanikio ni kujificha ili kwamba kile anachokifanya kisionekane au kionekane kwa sura isiyo halisi. Maandiko yanamwita shetani “kerubi afunikaye‟ (Ezekieli 28:14).

  Sasa anafunika nini? Anafunika kila kitu anachofanya. Mojawapo ni watu anaowaiba na kuwaficha. Anawaibaje? Mara nyingi ni kupitia “kifo.” Yaani watu wengi amewachukua, lakini ili kwamba sisi tusishtuke, anatuonyesha kwa nje kana kwamba mtu huyo amekufa, kumbe ni mzima kabisa na amefichwa mahali fulani kwa nguvu za rohoni za giza.

  Ukisoma Ufunuo 18, Biblia inaongelea kuanguka kwa Babeli mkuu, yaani ibilisi. Na hiloi linawafanya wafanyabiashara wasikitike sana. Sasa kati ya bidhaa ambazo walikuwa wanafanya naye biashara, ni miili na roho za watu. Tazama mstari wa 13 hapa chini:

  13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.
  Swali ni kuwa, watu hawa wanaouzwa wanapelekwa wapi? Isaya anatujibu vizuri kwenye sura ya 42: 22: “lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye Rudisha.
  Rafiki, kuna mamilioni ya watu waliofichwa hapahapa duniani kwenye mashimo ya kiroho ya ibilisi. Hawa ni watu ambao sasa sisi huwaita misukule. Ni watu ambao kimsingi hawajafa. Ni wazima kabisa. Lakini huwezi kuwaona kwa macho haya ya nyama. Ni mpaka ufunguliwe macho ya rohoni. Wamefunikwa na kerubi afunikaye ili sisi tusiwaone. Inawezekana kabla ya kuchukuliwa waliugua, kisha sisi tukaona kama wamekufa, tukazika, na tunaamini kuwa walishakufa. Kumbe wapi! Ni wazima kabisa. Hili jambo ni halisi kabisa.
  Mungu akubariki.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s