Mafundisho kanisani!

Jamani naomba kuuliza authorship ya mafundisho yafuatayo kama yalivyotapakaa sana siku hizi; a) Nguvu za majina b) Deliverence c) Kuvunja laana d) Kuombea vitu kama maji, vitambaa, mafuta, udongo n.k badala ya mtu. e) Misukule f) Sadaka ya ukombozi g) Roho ya kukataliwa na yanayofanana na hayo.

–Alex Kapinga

17 thoughts on “Mafundisho kanisani!

 1. Kuna baadhi ya watu naona wanalifanyia kazi neno la Mungu badala ya neno kuwafanya kazi ..

  Usimuite mbwa wa jirani yako kwa jina, atakumaliza, maana wewe si mgawa chakula kwake, isiwe ukauvaa ujinga na kutembea nao kwa waliyomakini.

  Tazama upumbavu huu, kunapotokea janga watu wapuuzi ujificha, kunapotokea jambo la kuinusuru nchi wasiyo makini utokomea gizani walakini linapotoka neno kuwagusa katika nyadhifa zao na kuwaweka juani waonekane kwa wote, basi ufanya vikao kukemea, walakini huu ni udhaifu, nako nikutojua kusimama wima.

  Mmebarikiwa sana..

 2. Yes, kuna makosa mengi yanafanyika katika haya mafundisho mengi ambayo kwa sehemu kubwa tunayaona kama mageni. Lakini pia sisi tuliowengi tuko na mtazamo hasi sana kwa vitu vingi ambavyo hatujavizoe au hatujawahi kuviona.
  Kwenye msafara wa maba na kenge hawakosekani. Kuna matapeli wengi pia ambao wanatumia vibaya karama ya Mungu, lakini tukubali kuwa jinsi siku zinavyozidi kwenda Mungu anazidi kufanya vitu ambavyo hatujawahi kuona.

  Wakristo wengi wanaodhani wako na ufahamu mara nyingi hupinga sana kila aina mpya ya utendaji wa Mungu wanapouona. Sisi watu wa mambo ya “management” hii huwa tunaiita “Resisitance to Change”. Lakini tujue kuwa Mungu bado hajamaliza namna za ajabu za utendaji wake.

  Halafu hili neno kuongozwa na Roho na lenyewe naona wengi tunalisema kwa mazoe tu hata hatuelewi maana yake. Wengi mnamaanisha nini, je kufuata vile biblia inavyosema(LOGOS) au ni kufuata vile Roho mtakatifu anavyonifunulia wakati huo (RHEMA)?

  Hata mambo yaliyoandikwa kwenye biblia ambayo huwa tunayatumia kama rejea yalianza kutokea wakati yakiwa hayajaandikwa mahali popote. Sasa tujiulize wale waliokuwepo wakati yanatokea waliwezaje kuyaamini.

  Tukumbuke kwa mfano wakati ufunuo wa kutumia vitambaa unatokea haukuwa umeandikwa mahali popote kwenye Biblia kwa ajili ya rejea, tujiulize kwa nini waliweza kuuamini.
  Wao walikuwa na mtazamo chanya zaidi wa utendaji wa Mungu, kuliko leo ambavyo likitokea tu jambo geni tunaanza kuliona ni la shetani badala ya Mungu. Tukumbuke kuwa mambo ya shetani huwa hayadumu sana hata kama yana nguvu ya kutisha.

  Linaposemwa suala la Delivearance, je kuna watu wanafunguliwa kweli katika maeneo ambayo wenye kuwafanyia hiyo deliverance wamesema kuwa wanayashugulikia?

  Wokovu ni mchakato(process) ambao ndani yake kuna vitu vinachukua muda kukoma katika maisha ya mtu. Kwa sehemu kubwa watu wanahitaji uhafamu ambao uko katika vile alivyosema Mungu (Logos & Rhema) ambao ukikaa ndani yao watapunguza utegemezi wa kufanyiwa fanyiwa maombezi.

  Umechelewa kuoa – maombezi
  Unataka kwenda ughaibuni – maombezi
  Watoto wako ni watukutu – maombezi
  Biashara yako haiendi vizuri – maombezi

  Duh!!!!!!!!!

 3. Bwana Yesu asifiwe!!
  Naomba nikuulize ndg. Milinga, hivi kwanini unapenda kutumia na kulitaja kanisa katoliki katika negative way? Nafikiri ni vizuri kuchangia bila kuponda au kubagua dhehebu fulani kwani mimi naamini wapo watu wa dhehebu nyingine nyingi tu ambao hawaamini.

 4. Nashukuru sana dada Rosemary kwa maswali mazuri!! naomba niyajibu kama ifuatavyo. awali ya yote naomba ijulikane kuwa kuna udhaifu wa mwili baada ya mwili kupitia kwenye uginjwa fulani. hivyo hata mara baada ya kupona huwa kuna muda fulani unachukua kufikia kwenye kukingamaa vizuri kiafya. wakati huo huwa mtu hujitahidi kula vizuri ili arudishe mwili wake katika hali yake ya afya. tunapookoka pia bado akili zetu zinakuwa na kumbukumbu la mateso mengi tuliyokuwa nayo tukiwa dhambini. hivyo kwa hizo kumbukumbu tunakuwa wadhaifu wa imani. Yesu akawaambia wale wayahudi waliomwamini ninyi mkikaa katika neno langu mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli nanyi mtaijua kweli nayo ile kweli itawaweka huru. yaani wakiendelea kujifunza neno lake mara baada kumwamini wataijua kweli na hiyo kweli ndio itawaweka huru na hiyo kumbukumbu ya mateso ya wakati wa dhambi. Nianze sasa na majibu ya maswali kama ulivyoyapanga hapo juu;

  1.hizi hatua ni lazima iwe automatically kwamba ukiisha kiri wokovu unapokea na uponyaji papo hapo kwa wote.
  Jibu: Kwa habari ya uponyaji wa afya hicho Yesu anakiita ni chakula cha watoto. Hivo kupona sisi kwetu ni kama mtoto anavyotegemea chakula kutoka kwa baba yao. lakini hapa ni muhimu sana tujue kuwa kuna magonjwa yanayosababishwa na ngivu za giza kama mapepo n.k na kuna magonjwa kutoka katika mazingira tu ya kawaida. hayo ya kwanza tunapokea uponyaji wake mara tu tunapookoka ila yale ya mazingira/kawaida hupona kwa kuwekewa mikono na kuombewa ndio aliyosema yesu kuwa tutaweka mikono yetu juu ya wagonjwa nao watapata afya!! lakini pia kuna mengine kwa kuweka mikono yanatoka lakini kwasababu ya mhusika kuto jua kweli anajikuta akili yake pado ikiendelea kuhisi bado ni mgonjwa mpaka siku atakapo wekwa huru kwa neno la mungu. Mfano mtu akipimwa ukimwi akiambiwa anao huwa anajiweka tayari kwa kufa wakati wowote lakini akienda kupima sehemu nyingine wakamwambia hana utaona hata staili ya maisha yake hubadilika na hupata nguvu mpya kabisa tofauti na alivyokuwa kabla hajapima sehemu hiyo nyingine ndicho kinachotokea kwa wengi wanaomkiri yesu. Lakini wanapokuja kuendelea kujifunza haki zao kutoka kwa Mungu huwa wanawekwa huru ghafla na lile neno kwani saikolojia yao hubadilika na kujiona wao ni wa Mungu na uponyaji wao tayari yesu alishautoa pale msalabani.
  NB: Hayo mambo yanajitokeza wakati huo huo ila udhihirisho wake unategemea na kiwango cha ufahamu wa neno la Mungu ndani ya mhusika.

  2. iweje Yesu aliponya yule mtu bubu na mwenye kifafa lakini wanafunzi walishindwa na aliwaambia wazi kuwa kuna aina amabayo haitoki ila kwa kufunga na kuomba, sio siri kwamba kuna wenye karama ya miujiza na wengine ni ualimu au uinjilisti na au bila miujiza, je ikitokea mimi nimemhubiria mtu hapa akaokoka kwa kumsalisha sala ya toba na kumuinjilisha lakini vifungo vibaki palepale je itakuwa vibaya akienda kwenye kanisa na akaombewa na kufunguliwa?

  answer:
  dada naomba ujue kuwa mtu anakuwa na vifungo kama anahatia au ana dhambi. anayemfunga ni ibilisi naye hufanya hivyo kwasababu mhusika anakuwa amemwasi Mungu na hivyo kustahili adhabu. sasa mtu huyo anapotubu dhambi zake kwa toba ya kweli sio tu ya kuongozwa sala ya toba lakini kwa toba ya kweli ndani yake kama nilivyoelezea hapo juu kuhusu toba, huwa mfungaji anakuwa hana haki tena tena ya kumfunga mtu huyo hivyo vifungo vyote vinaishia pale pale na wakati huo huo. Shida kubwa ni ile hali ya akili zetu kuyawaza tena yale makosa yetu na ibilisi naye hujitokeza kwetu na kutudanganya kuwa bado hatujasamehewa lakini ukweli ni kwamba tumeshasamehewa na hapa ndipo linapokuja andiko la kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Kwa hiyo watu wengi kwa kuto kujua kazi aliyoifanya Yesu pale msalabani wamekuwa wakihangaika sana kuzungukia kwenye vituo vya maombezi ili kufunguliwa lakini ukweli ni kwamba wanahitaji sio maombezi ila wanahitaji kujua wao ni akina nani na Yesu kawafanyia nini pale msalabani. Na bahati mbaya zaidi ibilisi naye pia ameingia kwenye hiyo sector ya maombezi na kuwadanganya hata waombeaji wenyewe wanafanya vitu ambavyo sio vya kiblia kabisa mfano ndio huo wa kutoa sadaka za ukombozi n.k
  NB: Naomba pia ieleweke kuwa ugonjwa sio kifungo ila kama umesababishwa na nguvu za giza basi ndio kinaweza kuwa kifungo lakini nao unaondolewa na Yesu mwenyewe lakini kama sio nguvu za giza unakuwa ni udhaifu tu wa afya ambo sio lazima mtu aupokee pale unapomuongoza sala ya toba ila unaweza kuendelea hata baada ya pale na akakutana na mtu mwingine akamwekea mikono na ugonjwa(udhaifu wa kiafya) huo unaondoka kwa huyo mtu kupata afya.

  3. Vipi kuhusu tuliookoka, je sisi hatuwi wagonjwa? sikubaliani na watendao dhambi kama uzinzi, wizi nk kwa kigezo kuwa ni pepo ila kuna vifungo ambavyo watu wakiombewa na kuelekezwa jinsi ya kuomba wanafunguliwa, Je wapi tuweke mipaka?

  jibu:
  kama nilivyosema kuwa uponyaji ni chakula cha watoto wa Mungu na chakula sio cha siku moja tu basi uponyaji kwetu ni endelevu lakini kwa njia ya kuwekewa mikono na mtu aliyeokoka mwenzio na sio kwa kupewa vitu vilivyoombea kama vitambaa, mafunta n.k kibiblia hilo sio fundisho ila yalikuwa ni maingilio ya kimungu kulingana na uhitaji wa wakati ule au katika ibada ile.
  kama ni chakula basi ni dhahiri kuwa magonjwa yale ya udhaifu wa kiafya yanaweza kutokea/kutupata sisi tuliookoka na dawa yake ni hospitali au kwa kuwekewa mikono lakini sio kwamba ni kifungo kumbuka nimesema kifungo ni lazima kitokane na dhambi.

 5. Mungu amesema: “Maana mawazo yangu si mawazo
  yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa
  maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika
  njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo
  yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ushukavyo,
  na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali
  huinywesha ardhi, na kuzalisha na kuchipuza, ikampata
  mtu alaye chakula, ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo
  katika kinywa changu; halitarudi bure, bali litatimiza
  mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”
  (Isaya 55:8 -11).

  Yesu alisema: “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila
  mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha
  mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu………

  Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu
  akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni
  wote wawili” (Mathayo 15:8, 9, 14).

  Yesu alituonya: “Kwa maana watatokea makristo wa
  uongo, na manabii wa uwongo, nao watatoa ishara
  kubwa na maajabu ; wapate kuwapoteza, kama yamkini,
  hata walio wateule. Tazama nimekwisha kuwaonya
  mbele.” (Mathayo 24:24-25)

  Paulo alituonya: “Maana kuna wengi wasiotii, wenye
  maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale
  wa tohara, ambao yapaswa wazibwe vinywa vyao. Hao
  wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha
  yasiyopasa kwa ajili ya mapato ya aibu.” (Tito 1:10-11)

  Twasoma tena: “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa
  elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi
  ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya
  awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya
  Kristo.” (Wakolosa 2:8)

  Twasoma tena: “Mtu asiwadanganye kwa maneno
  yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira
  ya Bwana huwajia wana wa uasi. Basi
  msishirikiane nao.” (Waefeso 5:6-7)

  Yesu alisema: “Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana,
  atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye
  afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
  Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya
  unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo,
  na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia
  dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni
  kwangu, ninyi mtendao maovu.” (Mathayo 7:21-23)

  Jamani bibilia iko wazi sana juu ya haya mapokeo ya kibinadamu na mwenyekusoma na afahamu . Huu si muda wa mtu kudanganywa ni bora kila mmoja azame ili alielewe neno la Mungu.

 6. ndugu kila siku makanisa yanazaliwa hivyo kila mchungaji anakuja na unabiii wake linda imani yako tu mana hayo yatakuchanganya.

 7. Shalom wapendwa
  naona huu mjadala wa maombezi unajirudia kila mara, nami nakubaliana na maoni ya wengi kuwa suluhisho pekee ni kuongozwa na Roho mtakatifu maana atakuwezesha wewe kama ulivyo kupambanua roho za watumishi na kutaniko ulilomo. Kukariri kwamba hapa wana wokaovu au la unaweza kupotoshwa bure maana wokovu ni mchakato ni kitu endelevu hiyo tunaiona hata ktk Biblia kuna watumishi walioinuka na kuanguka sasa kama ulikariri kuwa hapa ndio sahihi na hapa sio na huyu ndiye sahihi na yule sie unaweza kulishwa sumu huku unajiona kwa kumtegemea mwanadamu.
  Ndg Kapinga ninakubaliana na wewe kuhusu hizo hatua za wokovu, na hasa hapa
  3.kutolewa gizani na kuingizwa Nuruni
  ” kol 1:13
  Giza hapa halimaanishi giza hili tunaloliona ila ina maana kuwa katika ulimwengu uliojaa mabaya na dhambi na uasi na kila aina ya maovu. Kwa hiyo Mungu anatuahamisha kutoka katika ufalme huo uliojaa uovu na kutuingiza katiaka ufalme wa nuru ambao umejaa haki, mema na utakatifu. mfalme wa gizani ni ibilisi na mfalme wa Nuruni ni YESU KRISTO.
  ufalme wa giza ndio umejaa vitu vingi vya mateso kama vile laana, mikosi,dhambi, udanganyifu, balaa, roho zinazofuatilia, mizimu, n.k
  NB: Falme hizi mbili hazishirikiani hata kidogo yaani hakuna mtu anayeweza kusema ameookoka alfu kukawa na roho inyofuatlia tena kwani hizo hufanya kazi kwa wale tu walio gizani au dhambini bado…..”
  ila naomba kuuliza je
  1. hizi hatua ni lazima iwe automatically kwamba ukiisha kiri wokovu unapokea na uponyaji papo hapo kwa wote
  2. iweje Yesu aliponya yule mtu bubu na mwenye kifafa lakini wanafunzi walishindwa na aliwaambia wazi kuwa kuna aina amabayo haitoki ila kwa kufunga na kuomba, sio siri kwamba kuna wenye karama ya miujiza na wengine ni ualimu au uinjilisti na au bila miujiza, je ikitokea mimi nimemhubiria mtu hapa akaokoka kwa kumsalisha sala ya toba na kumuinjilisha lakini vifungo vibaki palepale je itakuwa vibaya akienda kwenye kanisa na akaombewa na kufunguliwa?
  3. Vipi kuhusu tuliookoka, je sisi hatuwi wagonjwa? sikubaliani na watendao dhambi kama uzinzi, wizi nk kwa kigezo kuwa ni pepo ila kuna vifungo ambavyo watu wakiombewa na kuelekezwa jinsi ya kuomba wanafunguliwa, Je wapi tuweke mipaka?
  4. Ushauri wangu watu tuenende kwa roho kila kitu tutajua hayo sijui ya sadaka za ukombozi na mengine utapambanua maana wokovu ni mchakato ndo kujifunza. Ni mtazamo wangu tu

 8. Bwana Yesu asifiwe!! mi naomba nianze kuelezea baadhi ya mambo ninayoyajua kuhusu wokovu tuliopewa na Mungu wetu aliyetupenda na anayetupenda upeo!!

  WOKOVU:

  kweli: kuna tofauti kati ya KUOKOKA na WOKOVU

  Kuokoka ni tendo la mtu au binadamu kumkiri yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yake.

  Wokovu ni tendo la neema la Mungu kumwesabia haki mwanadamu bure pasipo kustahili. na kwa sababu ni tendo la MUNGU ndio maana Ebrania inasema sisi je tuapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii? akimaanisha msamaha mkuu namna hii?

  Hatua 6 za kufikia kunye wokovu wa kweli.

  1. kulisikia neno la Mungu
  2. Kuliamini Hilo neo la mungu.
  3. kutubu dhambi kwa toba ya kweli.
  4. kubatizwa kwa maji mengi
  5. kuabtiza kwa Roho Mtakatifu
  6. kumtumikia Mungu katika Njia sahihi.

  toba ya kweli.

  toba ya kweli inahusisha vitu vifatavyo,
  a) akili; ili uweze kutambua kosa/kujua kuwa umekosea,
  b) hisia; ni ile hali ya kujisikia vibaya sana kwa kosa ulilotenda au dhambi uliyotenda kwa Mungu,
  c) utashi; dhamira ya dhati kabisa kwamba kuto tenda tena hilo kosa au dhambi maisha yako yote yaliyombeleni.

  NB: mambo hayo yakikosekana mojawapo katika mtu basi ni dhahiri kuwa bado hajaokoka na pia hayo hujitokeza automatically na sio kwa kujilazimisha yatokee.

  MAMBO YANAYOTOKEA MTU ANAPOOKOKA AU ANAPOTUBU DHAMBI ZAKE.
  1. kuzaliwa mara ya pili
  yn 3:1-8
  Hii ina maana ya kuzaliwa kutoka juu au kuzaliwa kwa roho yaani roho ya mwanadamu inakuwa ni mtoto wa Roh Mtakatifu kimatendo na mwenendo wote. hivo kama mtoto akikosea basi baba yake humweleza kuwa umefanya kosa na ndio maana ya Roho mt. kutushuhudia ndani yet juu ya hukumu na haki.

  2. kufanyika mtoto wa MUNGU
  YOH:1:12 1YOH 3:1-2
  Kwa kufanyika mtoto maana yake tunakuwa warithi pamoja na Kristo wa mambo ya Baba yetu Mungu. Pia kwa kuwa mtoto wa MUNGU TUNAKUWA juu kimamlaka kulinganisha na watumishi wa MUNGU ambao ni malaika. Hivyo mtu anposamehewa dhambi zake kupita Yesu kristo huwa anakuwa na mamlaka kuwaamrisha hata watumishi wa Mungu ambao ni malaika. hii inajibu swali la kwanini agano la kale hawakuweza kuto pepo japo miujiza mingine walifanya kama sisis leo tunavyofanya kwa jina la Yesu? sababu ni kwamba bado walikuwa hawajafanika wana kwa Yesu kristo kwani alikuwa bado hajaja. Tunaweza kutoa pepo kwasababu kwa kumpokea Yesu tumepewa kuwa wana hivyo kuwa na mamlaka juu ya malaika ambao miongoni mwao ni ibilisi pamoja mapepo ambao ni wale malaika walioasi.

  3.kutolewa gizani na kuingizwa Nuruni
  kol 1:13
  Giza hapa halimaanishi giza hili tunaloliona ila ina maana kuwa katika ulimwengu uliojaa mabaya na dhambi na uasi na kila aina ya maovu. Kwa hiyo Mungu anatuahamisha kutoka katika ufalme huo uliojaa uovu na kutuingiza katiaka ufalme wa nuru ambao umejaa haki, mema na utakatifu. mfalme wa gizani ni ibilisi na mfalme wa Nuruni ni YESU KRISTO.
  ufalme wa giza ndio umejaa vitu vingi vya mateso kama vile laana, mikosi,dhambi, udanganyifu, balaa, roho zinazofuatilia, mizimu, n.k
  NB: Falme hizi mbili hazishirikiani hata kidogo yaani hakuna mtu anayeweza kusema ameookoka alfu kukawa na roho inyofuatlia tena kwani hizo hufanya kazi kwa wale tu walio gizani au dhambini bado.

  4. kuwa kiumbe kipya
  2cor 5:17
  kuwa kiumbe kipya ina maana kuwa wewe tena hauna uhusiano na shina la uovu au hakuna kitu unachoweza kukirith tena kutoka kwa mababu au wahenga kwani wewe unakuwa umejishikiza katika shina jipya la mzabibu mwema na sio mzabibu mwitu kama hapo awali ukiwa dhambini au ukiwa katika ulimengu wa giza. Tangu wakati huo unapookoka unaanza kuchukia dhambi na watenda dhambi hauwezi kupatana nao katika matendo yao tena bali unakuwa mwonyaji wao. Yakale yote yanakuwa yamepita na tazama kwako kunakuwa na mambo mapya tu yale ya kale hayawezi kukaa kwako tena.

  sasa nirudi kwa baadhi ya mambo au mafundisho niliyoyahoji hapo juu kwenye mada yangu.

  1. nguvu ya majina
  majina ni vitambulisho tu au nembo inayowekwa kwa mtu ili yuweze kumtofautisha na wengine lakini hayana kitu chocho kile katika roho ya mtu. tukifika mbinguni hata kule nako tutapewa nembo(majina) zingine. mtu hawezi kuwa na halifulani eti kwa sababu ameitwa jinaa lenye maana fulani. Katika biblia Mungu aliwabadilisha watu majina ili kuwafanya wakumbuke kile ambacho amewaahidi kuwafanyia katika maisha yao. Na ikumbukwe kuwa waliobadilishwa majina ni wale tu ambao Mungu alifanya nao AGANO na sio watu wote. Hii inatufundisha kuwa kumbe kule kubadilisha majina ya watu haikuwa kwasababu majina yao yalikuwa na laana au nguvu ya kusababisha matatizo kwao kama ingekuwa hivyo basi Kalebu naye angebadilishwa kwani kalebu maana yake ni mbwa. pia watu wanaweza kukuita jina fulani kutokana na hali uliyonayo sio kwamba watu kwa kukuita vile ndio kulisababisha uwe vile ila ile hali ndio ilisababisha watu wakuite hivyo kama kuelezea hali uliyonayo.

  2.kuvunja laana
  Fundisho hili sio sahihi kwa sababu katika ufalme wa nuru hakuna kitu kinachoitwa laana. Hivyo kama mtu ameokoka kweli ni udanganyifu kumwambia kuwa ana laana tena wakati maana tu ya kuokoka ni kuhamishwa kutoa katika laana zote za dhambi. Laana ni tamko la mabaya kwa mtoto kutoka kwa mzazi wake kama amemkosea au ni tamko la Mungu kwa mtu mwenye dhambi KUMB 28:13-. hivo ni mzazi tu au Mungu wenye uwezo wa kusababisha laana kwa mtu na sio mababu kama wengine wanavyodhani. PIa ijulikane kuwa laana haivunjwi kwa maombi mengine yoyote zaidi ya yale maombi anayokiri mtu wakati anapotubu/ kuokoka. Mungu anaposamehe huwa hana kawaida ya kubakiza sehemu fulani ya dhambi ili ije ifanyiwe maombi baadaye ya kuvunja laana. Laana zote za mwanadamu zilimwangukia Kristo pale msalabani na mtu anawekwa huru pale tu anpomkiri Yesu na kutubu dhambi zake kwa toba ya kweli kama nilivoileza hapo juu. pia kusema unatubu dhambi za kizazi cha tatu na cha nne sio sawa kwani hakuna mwenye uwezo wa kutubia dhambi za mwingi kwani pengine hata dhambi waliyoitenda hao wa kizazi cha nne we huijui hivyo akili yako itakuwa haijahusika kwenye hiyo toba na hivyo ni batili.

  3. deliverence
  deliverence maana yake ni kugomboa au pay back the cost. sasa mwenye uwezo wa kugomboa ni Yesu peke yake tena kwa kutoa malipo ya damu yake. kwa hiyo hatuweze kugombolewa kwa maombezi ya mtu fulani bali ugombozi huo ulishafanyika miaka 2000 iliyopita pale msalabani. Mtu hawezi akasema ameokoka alafu bado tena akawa anahitaji kugombolewa kwasababu haileti kukubaliwa hata kwa fikra za kawaida mtu ameshahamisha kutoka kwa shetani we unamwambia akafanyiwe deliverence kutoka wapi tena wakati tayari yupo kwa Mungu?

  4. sadaka ya ukombozi
  awali ya yote naomba ijulikane hivi kuwa Mungu hajibu maombi ya mtu kwasababu ametoa sadaka fulani. Mungu hujibu maombi ya mtu mtakatifu na ambaye haombi kwa tamaa zake ili akafanye uovu. pia Mungu anajibu maombi yaliyoombwa kwa jina Yesu tu na sio vinginevyo.Biblia yangu inaniambia kuwa Mungu hapokei sadaka ya wenye dhambi na pia hajibu maombi ya mwenye dhambi kwani yanakuwa kelele mbele zake. kabla hatujaenda kumtolea Mungu sada huwa tunaomba ili sadaka zetu zipokelewe lakini huwa hatuendi kwanza kutoa sadaka alafu na kutaka Mungu eti kwasababu mimi nimekutolea sadaka sasa nataka ujibu maombi yangu,hapana!!. kwa hiyo kinachomsukuma Mungu kujibu maombi ya mtu ni utakatifu alio nao na moyo wa unyenyekevu alio nao wala sio sadaka tunazotoa. Mtu hakombolewi kwa pesa wala kitu chochote kile ispokuwa ni damu ya Yesu tu nayo ni pale anapotubu dhambi alizotenda yeye mwenyewe na sio mababu au wahenga.

  5. Roho ya Kukataliwa
  kimsingi hakuna roho inayoitwa ya kukataliwa. sisi sote tukiwa dhambini tulikuwa tumekataliwa katika ufalme wa Mungu na tulipookolewa tukakubaliwa na Mungu alafu ibilisi naye akaanza kutukataa au kutuchukia lakini hiyo haiwezi kuwa hoja eti sisi twende sasa kuvunja roho ya kukataliwa na shetani eti kwa sababu tunashindwa kuajiriwa au kupewa vyeo maofisini hapana. tunachotakiwa kuangalia ni je maisha yetu hayani kona kona mbele za Mungu kama yako safi basi tunatulia na kuzini kumsihi Mungu mwenyewe kwa bidii zaidi tukijinyenyekeza kwake siku zote bila kujali ulimwengu unatuonaje. unaposema roho ya kukataliwa nina kataliwa na nani sasa wakati Mungu amenikubali kwa kunipa wokovu wake au unamaanisha sasa nianze kuwapendeza wanadamu? kinachotakiwa kueleweka ni kwamba upinzani upo katika mambo yetu hivyo tunatakiwa kila siku kuzidi kumwomba Mungu na bila kukata tamaa kwani tukikata tamaa ndio ibilisi huanza kutudanganya eti tuna roho ya kukataliwa na mengine mengi kumbe sisi ni wana WA UFALME WA MUNGU ALIYE HAI!!!! HATUKATALIWI WALA HATUDAIWI TENA!!

  HATA SASA NINGALI NINA MAMBO MENGI YA KUWAAMBIA LAKINI NIISHIE KWANZA HAPO KWA LEO!!! Mwimarike hatimaye msomapo haya!!!

 9. mbarikiwe sana kwa kutoa muda wenu kuchangia hii mada, ila mi nimesoma HIYO MICHANGO yenu nimeona wengi wenu mnachangia tu kama vile muulizaji wa swali anahukumu kuwa hayako sahihi ila mimi nilichokuwa nauliza ni mwanzo wake ni wapi kwasababu labda kwa sababu sijaimaliza biblia yote bado lakini katika yale ambayo tayari nimeshayasoma sijaona watu walipofanyiwa deliverence au walipobadilichwa majina kwasababu waliyonayo yana laana au waliposema kuwa kuna misukule sehemu imefufuka na hayo mengine; ndio maana nikauliza ili nipate mistari na sehemu alipotuagiza Yesu kuwa tufanye hizo huduma. LAKINI PIA MKO AMBAO MNASEMA ROHO MTAKATIFU HANA LIMITATION katika utendaji wake ila naona kuna makosa kwenye tasfiri ya hiyo sentensi. kwani wengi mnasema sio kila kitu ambacho mtu anafanya lazima kipimwe kwa biblia ndio maana mnasema kuwa anayejiachilia tu kwa Roho mtakatifu basi Mungu anamtumia kwa maajabu mengi ila mimi najua hata mpinga Kristo anatenda ishara nyingi na maajabu mengi sana kiasi kwamba Yesu mwenyewe alisema atadanganya wengi yamkini hata wateule!!. lakini pia Yohana katika nyaraka zake anatuambia tusiiamini kila roho bali tuzijaribu kwanza kwamba je zimetokana na Mungu au la sasa mnaposema kuwa hatutakiwi kupinga eti kwasababu zinafanywa na watumishi wa Mungu hamuoni mnataka kupotosha watu na kutufanya kila kinachokuja hata kama kinapingana na neno laMungu kwa mfano fundisho la kutoa sadaka za ukombozi wakati wanadamu wote tunakombolewa kwa damu ya Yesu tukubali tu eti kwasababu kimeletwa na watumishi ambao mi kidogo napata taabu kuwaita wa MUNGU kama wanafundisha kilichotofauti na neno la huyo Mungu. Naomb watumishi wa Mungu tuchangie kwa kutoa maandiko ambayo hayo mafundisho yanasimamia maana mi sidhani kama Mungu anasema kuwa Neno lake limehakikishwa mara saba na kuonekana liko safi alafu sisis leo tunakuja na maneno mapya ili kulifanyia editing hilo lililohakikishwa mara hizo zote alafu tukasema kuwa eti tunamtegemea Roho mtakatifu. kwa uelewa wangu mimi wa kile nilichosoma kwenye biblia ni kwamba Roho mtakatifu alikuja kutusaidia kuishi yale yaliyo kwishasemwa tayari na Yesu kwenye biblia na sio kwamba atatuletea mambo mapya ambayo wakati mwingine yanapingana hata na Yale ya Yesu mwenyewe. Mfano mtu unaponiambia eti kurudisha misukule ni jambo kuwa kuliko kufufua wafu mi lazima nikushangae sana kwa sababu kama unasema msukule ni mtu ambaye hajafa sasa je ipi ni ishara kubwa,ya kufufua aliyekufa au asiyekufa? NAWASIHI SANA NDUGU ZANGU TUNAPOCHANGIA TUSIWE NA MTAZAMO KUWA MIMI NAPINGANA NA WATUMISHI WENU WA MUNGU ILA NINACHOOMBA TUANGALIE MOJA BAADA YA JINGINE ILI TUWEZE KUWASAIDIA WATANZANIA AMBAO WANAPOTEA SANA NA SIO KOSA LAO NI KOSA LETU SISI AMBAO TUNATAKIWA KUWAFANYA WANAFUNZI. BADALA YA KUWAFUNZA KWA KWELI TUNAWAFUNZA KWA MAFUNDISHO AMBAYO HATA UKIJIULIZA KUOKOKA MAANA YAKE NINI NA NINI KINATOKEA MTU ANAPOOKOKA UKILINGANISHA NA MAFUNDISHO HAYO NILIYOTAJA UNAPATA UTATA. MI NAWAOMBA SANA TURUDISHE JAZBA ZETU CHINI NA TUANZE KUCHAMBUA MOJA BAADA YA JINGINE YAMKINI WACHACHE WATAKAO SOMA HUKU UKURASA WATAELIMIKA. Mbarikiwe sana watu mlioumbwa na Yesu Kisto.

 10. Wapendwa,
  Msiwe na haraka ya kuhitimisha, mimi naona jibu halijapatikana! Alex anachouliza ni hivi, nanukuu
  “Jamani naomba kuuliza authorship ya mafundisho yafuatayo kama yalivyotapakaa sana siku hizi; a) Nguvu za majina b) Deliverence c) Kuvunja laana d) Kuombea vitu kama maji, vitambaa, mafuta, udongo n.k badala ya mtu. e) Misukule f) Sadaka ya ukombozi g) Roho ya kukataliwa na yanayofanana na hayo.” Mwisho wa kunukuu.

  Nilivyomwelewa Alex, anataka kujua hivyo vitu alivyovitaja hapo juu ni Fundisho la Biblia? kama ndiyo mpeni mistari. Naona watu wanatoa majibu ya jumla sana. Mwelezeni Alex, ni wapi katika Biblia pana Habari za Misukule, kuvunja laana , Sadaka za ukombozi nk?! Mimi pia ninashaka na Mafundisho kama hayo! Miujiza si tatizo, na si kila muujiza ni wa Mungu. Hoja ni kwamba, MAFUNDISHO HAYO yametajwa wapi katika Biblia? Au ni Mafunuo? Tusaidieni jamani msijenge tu hoja kupitia mnavyojua na kuamini, toeni Mistari, Si Biblia Mnazo? TUONYESHENI.

 11. Kaka Michalel Nzala amechangia vema ila nadhani kuna kila sababu ya kuongozwa na Roho Mtakatifu kama ambavyo tunavyoongozwa na neno la Mungu katika Galatia na Warumi, tunaambiwa tuenende kwa Roho. Sasa utaenendaje kwa Roho ikiwa unashikilia principle zako? au kumfanya Mungu ana principle fulani tu?katika mchango wangu hapo juu nilionesha kuwa Bwana Yesu mwenyewe amewahi kuponya vipofu mara 3 au zaidi ila mara zote hizo alitumia njia tofauti

  je utamwekea Mungu vikwazo na kumwekea Principle za utendaji??
  je Biblia haituambii akili za Mungu zi juu sana na njia zake hazitafakariki wala hazichunguziki?

  Mimi naona vema hivi badala ya kuwasema na kuponda watumishi wa Mungu hebu muombe Mungu ili Roho mtakatifu akufunulie ujue mambo ya rohoni, tuache kuwa wachanga wa kiroho yatupasa kukua hata kufikia cheo cha Kristo.

  Sasa tukisema tushikilie principles za utendaji wa Mungu, basi kuna tofauti gani kati ya agano la kale na agano jipya? maana wenzetu wa kale hawakua na Roho mtakatifu hivyo walimwabudu Mungu manually lakini sisi tumejaliwa kuwa na Roho mtakatifu sasa kwa nini tusimtumie?? je si biblia inatuambia Mungu anawatafuta watu watakaomwabudu ktk roho na kweli?

  Kama watumishi wa Mungu wangekua wanakariri principle za Mungu basi Eliya asingekubali kutoka katika kijito cha kerithi lakini alitii akaenda serepta why??? ili aendelee kupata riziki na utaona kuwa alipofika serepta kwa mama mjane kitu cha kwanza kudai ni msosi sasa je pale kerithi kwani alikua analala njaa???

  Jamani kanisa la sasa linahitaji sana kuongozwa na roho kuliko siku zote maana ndo linalotakiwa kuwa na utukufu mkubwa, sasa ikiwa hata viwango vya mitume hatujavifikia tunakalia mabishano matupu je huo utukufu wa mwisho ambao ni mkubwa si tutachelewa kufika??

  Huu mchezo wa kumkariri Mungu kuwa anafanyaga hivi si vile kutawazuilia baraka watu wake maana watawaambia watumishi wa Mungu wachawi, mara freemason, mara wanaenda nigeria yaani wakristo utadhani tumelogwa yaani tunawaona hao freemason na wachawi wa nigeria kuwa wana nguvukuliko MUNGU WETU JAMANI!!!! NO LAZIMA TUSIMAME TUMTAFUTE MUNGU TUJIFUNZE NENO LA MUNGU SIO TU KUKALIA MAHUBIRI TUJIFUNZE NENO YAPO MAKANISA WANAFUNDISHA NENO LA MUNGU NENDA KAJIFUNZE TUKUE NDUGU ZANGU.

  Paulo akijua umuhimu wa kuishi rohoni alisema hivi ktk Efeso1:17 anawaombea anasema ” Mungu wa bwana wetu Yesu kristo ,Baba wa utukufu awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye, macho ya mioyo yenu yatiwe nuru…” kumbe kumjua Mungu si principle fulani ni ufunuo ndugu zangu, na ufunuo huja kupitia Roho mtakatifu hivho tumkamate sana huyu roho mtakatifu Pleeleeessseeeee!!!!!!!!!!!!!!!

 12. Ndugu Millinga,

  Nikupongeze sana ndugu yangu kwa yote uliyoanisha hapo juu.

  Shida kubwa imeikalia kanisa la leo kiasi kwamba haliamini kila kitu Mungu anachotenda kupitia kwa watumishi wake.

  Kanisa hili la leo lingekuwepo hata wakati wa Musa hakika lingemtuhumu Musa kwamba anatumia nguvu za giza katika mambo mengi aliyoyafanya kwa maelekezo ya Mungu. Kila ninapoisoma biblia na kuona miujiza iliyotendeka enzi hizo za Agano la Kale bila kutiliwa shaka na wazee wetu hao, hurudi nyuma na kujiuliza hivi hawa wenzetu walikuwa na imani ya namna gani kiasi cha kutotilia shaka kila lililotendwa na watumishi wa Mungu, tena kwenye kipindi ambacho tunaambiwa na Neno la Mungu kwamba hakikuwa kipindi cha Agano lililokuwa bora kama tulilonalo sisi wa kipindi hiki!!

  Kipindi hiki tumemtukuza na kumhofu zaidi shetani kwamba anaweza kutenda miujiza kuliko Mungu wetu kupitia kwa watumishi mbali mbali; mbaya zaidi hata miongoni mwa watumishi wenyewe kwa wenyewe wanashutumiana mno juu ya huduma zao, je, unategemea sisi kondoo zao tufanyeje?

  Haina maana kusema hivyo kwamba hakuna watumishi waovu wanatumiwa na shetani, bali nataka kusema kwamba haiwezekani Mungu atuache na kutusahau kiasi hicho mpaka ifike mahali kila mtumishi anaye simama kwenye madhabahu yake awe anatumia nguvu za giza katika miujiza inayoendelea. Mungu wetu hajatuacha na kutusahau kiasi hicho hata asijifunue kupitia njia na matendo mbali mbali ya miujiza!!!

  Lazima watu wa Mungu tukumbuke kwamba tangu kale Mungu amesema njia zake za utendaji kazi na namna ya kujifunua kwake katikati ya watu wake ni tofauti sana na jinsi sisi tunavyoweza kuwaza au kujua. Kama Mungu alimtumia punda kusema na kusikika, kwa nini sisi hatuamini kwamba anaweza kutumia kitu chochote kuwaponya watu wake?

  Cha msingi na cha muhimu kuliko uponyaji wowote ule ni ule unaoponya roho za watu ili zisiangamie milele kwenye lile ziwa liwakalo moto! Kama watumishi watakazania zaidi material things kwa waumini wao bila uponyaji wa roho za watu, hapo lazima kuna walakini, na watumishi hao tuwakatae kwa nguvu zetu zote za kimwili na kiroho pia. Yesu alisema wazi itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote kisha aipoteze roho yake!!? Hapo alikuwa anataka kutuonyesha kilicho cha muhimu ni kuokolewa kwa roho zetu na baada ya hapo material things yatakuja tu yenyewe maana vyote viijazavyo dunia hii ni mali ya Bwana, naye huwagawia wanawe yaliyo mema.

  Ubarikiwe Millinga, nadhani umejibu karibu kila kitu alichouliza Kapinga.

 13. shalom, ni kweli Mungu hana mipaka, au ukomo wa kibinadamu, tatizo letu ni kujiwekea ukomo , hizi theologia zetu zinatufanya tuweke mipaka kwa Mungu kujidhihirisha, kama wapendwa walivyosema ukijiachia kwa Roho Mtakatifu na akakutumia basi linainuka kundi na kusema eti ni imani potofu, sikatai kwamba imani potofu hazipo, zipo, lakini tuzipime kwa maandiko, tusikariri miujiza au matendo makuu ya Mungu, Yeye ni Mungu mkuu , ana njia nyingi.Nimeona watumishi wengi wanaoshika saaaaana katiba zao na miongozo ni kama wamebana utendaji wa Mungu, lakini wale wanaonennda kwa kumsikiliza ROHO MTAKATIFU , Mungu anawatumia sana, matokeo wanaambiwa imani potofu au freemanson. Tubadilike tusiwe wepesi tu kuhukumu bila kupima.Leo kanisa linachechemea kwa sababu ya kunyosheana vidole, badala ya kumtafuta Mungu, tumebakia tukikatishana tamaa, Kama Yesu mwenyewe alisema amwaminiye YEYE, atafanya kazi kubwa kuliko zile….. (Yoh 14:12) yeye alifufua wafu, je si zaidi ya msukule ambao hawafi wanachukuliwa na kubadilishwa kichawi. Yer. 33;3 Mungu amesema tumwite , ataitika na kutuonyesha mambo MAKUBWA NA MAGUMU tusiyoyajua, yaani ambayo akili za kibinadamu zinashindwa kukubali.
  mbarikiwe.

  MARY JOSHUA, LINDI.

 14. Kuna shida hapo. Wengi humsingizia Roho Mtakatifu tu. Kazi ya Roho Mtakatifu, Kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna uchawi unaendeshwa hapo. Ukiona hayo yanatendeka, jua hivyo tu. Mungu hana principles hizo katika maombezi ya watu wake. Atendapo miujiza, hahitaji vitambaa, maji ya upako, kurukaruka kibwetani/madhabahuni, sadaka ya lazima ya maombezi nk. Ukiona hayo, jua unaibiwa pesa na kupoteza muda wako hapo. Kimbia kabisda.
  Nenda ukasome Biblia uone kama wanavyofanya ndivyo inavyoelekeza. Ukiona sivyo, ng’ang’ana na Biblia tu. Mungu ana dini moja tu, ubatizo mmoja, mafundisho ya aina moja tu, na siku moja tu ya ibada. Isome Biblia itakuelekeza tu namna ya kumwabudu Mungu. Mengine yaliyopo ni udanganyifu tu.
  Mimi nimesema

 15. Mungu hafanyi kazi kwa mazoea. Kama umezoea kuweka mikono tu juu ya mgonjwa na kapona hiyo njia pia wakatoliki wanaihoji kila siku na kusema siyo ya Mungu. Wanasema miujizailikuwa nyakati za kale ya mitume na manabii wa Biblia siyo nyakati hizi.

  Mungu alitumia fimbo ya Musa kuonesha miujiza yake mbele za Farao. Mungu alitumia Kijiti kuinua shoka lililozama ndani ya Mto wakati wa Eliya na Elisha.

  Mungu alitumia fimbo yaMusa kuchapa jabali likatirirka maji na wana Israel jangwani wakanywa maji wakapona.

  Nyakati fulani Mungu alitumia maji ya mto Yorodani kumponya kamanda wa jeshi aliyekuwa anaumwa ukoma. Kwa kujiogesha mara saba tu ndani ya mto Kamanda wa Jeshi alipona na akawa na ngozi kama ya mtoto mchanga.

  Mungu alitumia nyoka wa shaba kuwaponya wagonjwa walioitazama tu walipona sumu za nyoka. Tena ilikuwa kwa kuitazama tu pale ilipotundikwa mbele yao. Soma maandiko uelewe.

  Paulo alitumia vitambaa kuwaponya wagonjwa wengi sana.

  Mungu siyo jiwe wala mti hata atende kazi zake kwa style moja. Mungu yu hai. Kwa kuwa hai hatendi kazi kwa mazoea ya wanadamu.

  Mungu aweza kutumia maji, mafuta, fimbo, vitambaa, neno, kugusa, kuamru tu na jambo likawa, TV, Magazeti, Internet, Blog, Facebook, Twitter, nk kuwaponywa watu madhambi yao au magonjwa na mateso yao.

  Mazoea ya kilokole ya tangu miaka ya 1980 ndiyo yanayotupotosha. Mungu anaendelea kujifunua kwetu kwa njia mbalimbali hata ambazo hazikuandikwa kwenye Biblia. Ni juu yetu kamini Nguvu na Uweza wake tu wala tusianze kutafuta au kuwasema watumishi wanaotumia vitu hivyo kwamba wanatumia uchawi au wamepotoka. NOOOOH. Huenda wewe ndiye umepotoka.

  Mungu ataendelea kutumia vitu, Neno, Maji, Mafuta, Nguo, nk hadi siku ya kiyama kila anapotaka kuwasuprise wanadamu au anapotaka kuwaongezea Imani.

  Obed Venerando Milinga, Kigoma.

 16. BWANA YESU SIFIWE WAPENDWA!

  Biblia iko wazi kabisa, inasema kwamba wote wanawoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.
  kwa kweli kuna mambo ya siri za Mungu na mtu hawezi kuzijuwa kabisa mpaka Mungu mwenyewe amufunuliye siri hizo, na njia zake ni nyingi mno!! Mungu wetu ni mwema anapenda sana kufenya kazi na sisi wanaye (wanaoongozwa na Roho wake),
  Yesu alisema kwamba wamwaminio watafanya kazi kubwa sana hata kuliko zile alizo zifanya mwenyewe kwa maana yeye alienda kwa baba. Ninaamini Yesu alipo rudi mbinguni alijuwa kuna kazi nyingi sana za kufanya hapa duniani, na huwezi kufanya kazi duniyani kama huna mwili ili uweze ku communicate na dunia yenyewe physically lakini mwili wenyewe hutoshi kama hakuna uwezo wa kujuwa mambo yasiyo onekana yani ktk ulimwengu wa roho. kwa hiyo tunahitaji sana ushilika wa ndani sana na Roho mtakatifu ili tujuwe ni wapi, saa ngapi na nini tufanye kazi ili iyitwe kazi ya Mungu kabisa. kwa maana kinacho itwa kazi ya Mungu ni kile kinacho fanyiwa kwa imani, na imani siyo kufanya kile ambacho furani alifanya jana na akafanikiwa( huu ni mchezo wa kuigiza)! bali ni kuhakikisha unacho kifanya ni Mungu mwenyewe amkuambia? na kama ni yeye ,je saa ndiyo hii? na kawa wakati ni huyu , ni wapi anapenda ukifanyiye? na pamoja na nani?

  Sasa kuna shida kubwa leo katika Imani, watu hawataki kumusikiriza Roho mtakatifu, shuguli kubwa ni kuiga wengine na hii inaleta shida sana katika makanisa yetu, yaani watu wanataabika sana.
  Mimi juzi nimetembelea chumba kimoja ca waombaji na nimeshangaa sana nilipoona wote wanakuja na madumu ya maji , liter 10, 20l na wale wenye nguvu ndogo wanakuja na liter 5 wote wakisema wanahitaji maji ya baraka! nilisikitika sana watu wanateseka sana na wengine wanakufu kwa kukosa maarifa, uchovu ni mwingi sana lakini Yesu yeye amekubali kutupumzisha kabisa. Wengine wanatonda kwenye foreni wakiomba ma nabii eti wawambiye mabo yawo, sidhani kwamba hili ni agano jipya kwanza ni gumu kuliko hata agano la kale. Maana watu nikama wanaaguza kabisa!!
  Yesu anasema kwamba tukijuwa ukweli tutakuwa huru kweli kweli, na ukweli ni neno lake.
  So ushauli wangu ni kwambu tusome neno la Mungu na tumtege sikiyo Mshauri wetu Roho Mtakatifu ndipo tutaweza kufanya kazi ya Bwana na kufanikiwa. Mungu ana haja ya kuongeya na kila mwanaye, sasa watu hawapo wako, wana shughuri zawo wenyewe!! na ndiyo maana solutions ni ndogo sana.

  Kumaliza ninaomba kiswahili changu kisiwe sababu ya kukwazika maana siyo rugha yangu.
  Emmanuel kutoka Burundi

 17. Mimi nafikiri hilo jambo kama huliamini lisikupe shida maana linafanywa na wanadamu ambao ni watumishi wa Mungu, hata sisi unaotuuliza hapa jukwaani ni wanadamu pia watumishi wa Mungu, nadhani itakua sahihi sana kumuuliza Roho Mtakatifu maana hakuna jambo au huduma kati ya hizo unazozitaja na kuziulizia zinazoweza kufanyika bila ya Kuhusika kwa Roho Mtakatifu moja kwa moja. Hebu komaa fanya maombi hadi upate mpenyo ongea na Mshauri wetu, mwalimu wetu mzuri atamaliza mzizi wa fitna.

  Hapa jukwaani itakua ni mada isiyo na mwisho maana kuna watu wanaoamini huduma hizo na wengine hawataki kuzikia n.k. Lakini Mungu wetu anaweza kufanya kazi kama apendavyo wala huwezi kumtabiria kwamba sasa Mungu atatumia njia hii.

  Mfano: Bwana Yesu katika huduma yake aliponya vipofu si chini ya mara tatu ila alitumia njia 3 tofauti kwa tatizo moja wasomaji wa biblia mnajua kuna mtu alimwekea mkono machoni akaona, mwingine alitema mate akamtupia machoni akaona, kuna mwingine akapakwa matope machoni kisha akaambiwa nenda kanawe somewhere akaona.

  MUNGU WETU SUPER!!!!!!!!!!!!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s