Steven Mwikwabe atoa ushauri kwa waimbaji wa nyimbo za Injili na wachungaji

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania, anayesikika kwa album mpya ya RAFIKI WA KWELI. Ametoa ushauri kwa waimbaji wa nyimbo za injili na wachungaji kama ifuatavyo “kabla ya yote napenda kuweka wazi kwamba waimbaji wengi tusipojitambua katika nafasi ya wokovu tuliopewa na Mungu wengi watapata hasara ya nafsi zao, asilimia kubwa ya waimbaji hawajui wito wao kama huduma, wala hawajui wanayemwimbimbia kingine hawajui tofauti kati ya nyimbo za Mungu na nyimbo za kipagani, wegi wamejaa viburi na hupokea utukufu kuliko Mungu, wengi hupenda sifa na kuweka pesa mbele

Mwimbaji huyo aliyasema haya hivi karibuni alipokua akiulizwa maswali kuhusu huduma yake ya uimbaji pamoja na album yake ya pili RAFIKI WA KWELI alisema “kuimba nilianza mwaka 1988 nikiwa katika Kwaya ya MAGOTO MENONITE wilayani Tarime, mwaka1995 nikaacha kuimba kwaya na kwenda kanisani, 1998 nikapata ushawishi wa kurapu,2001 nikatoa Singo ya Mabaya ya dunia nikiwa Mwanza,2003 nikaja Dar,nikarekodi wimbo mwingine uliofanikiwa kupendwa na wengi uliitwa Tutaokolewa na nani? Nilimshrikisha John Woka,2005 nikaokoka,2007 nikajiunga na kwaya ya EBEN-EZER ya TAG Mbagala pamoja na kikundi cha kusifu na kuabudu,2009 nikatoa albamu ya kwanza ROHO KAA NDANI YANGU.2012 nimetoa RAFIKI WA KWELI,ambayo ni albamu ya pili”

Steven Mwikwabe aliendelea kusema kuhusu wachungaji na huduma kanisani “Kuna wachungaji wanaozima waimbaji binafsi na kuwanenea vibaya juu yao Mungu awarehemu.”

Mwikwabe kwa sasa anaabudu TAG Mbagala kwa Askofu Muhiche. Pia yuko Tayari kwa mialiko yenye kumtukuza Mungu kwa maelezo zaidi wasiliana naye kwa simu 0652 500 955 Tazama baadhi ya nyimbo za Steven

RAFIKI WA KWELI

OBED-EDOM

KUISHI KWANGU

2 thoughts on “Steven Mwikwabe atoa ushauri kwa waimbaji wa nyimbo za Injili na wachungaji

  1. Yeah,
    Gospel Musics is not just like a Secular Musics, because it concerns the attraction of The Holly Spirit’s Anoint.
    Mungu aturehemu sana tuwe huru ki fikra na Kimtazamo katika utumishi.
    “Muimbaji siku zote ni Kuhani kama anafanya Injili kama kazi wala si huduma huyo si Kuhani.l
    Hiyo ni Nguzo ya Kitume

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s