Hadithi…Hadithi!

“”Lakini yeye akamtikisa motoni asipate madhara”.” Matendo 28:5 

Kuna hadithi ya mkulima mmoja punda wake alianguka kisimani. Kwa vile hakuwa na jinsi ya kumtoa, akataka kumzika mule. Akatafuta gari la kubeba kifusi ili amfukie punda, lakini cha ajabu kila akimwaga kifusi yule punda anakikanyaka juu yake, kila kifusi kinapokuja anakanyaga juu yake hali hii ikaendelea mchana wote. Anainua miguu yake, anajitikisa na kukanyaga kifusi. Hatimaye kifusi  kilipofika juu ya kisima kile yule punda akatembea na kutoka pale akiwa amechoka lakini punda mwenye hekima.

Kilichodhamiriwa kumfukia ndicho kilichomsaidia kumtoa nje ya kisima!

Hadithi nyingine ya Mtume Paulo…alipokuwa kisiwani kuelekea Roma, Paulo alikuwa amekusanya mzigo wa kuni na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga zonga mkononi mstari wa tano Matendo ya Mitume sura ya 28 “Lakini yeye akamtikisa motoni asipate madhara”

Kuna hadithi mbili zenye maana hapa. Kwamba unaweza kuendelea kugandamizwa kwenye mambo yaliyokukosesha furaha au kuyaachilia na kusonga mbele kuelekea kwenye kusudi Mungu alilokupangia. Kuyakung’uta yasiambatane nawe na kupiga hatua.

Mtume Paulo ambaye pia alikuwa na mambo yake ya kale anasema kwenye Wafilipi 3:13″…..nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachumilia yaliyo mbele, nakaza mwendo, niifikie niifikie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”  Sasa basi, Paulo akiyasahau yaliyo nyuma…….akiangalia mambo ya mbele yake ili aifikie mede ya mwito mkuu, afikie mahali aseme mahali hapa nimefika nimeona mkono wako, afikie mahali aseme nayashuhudia haya maana Mungu amenitoa huko!!

Wapendwa, huwezi kusonga mbele kama una mambo umeyashikilia, huwezi kuona mpenyo, huwezi kutoka kifungoni kwa sababu kuna vitu vimekusonga na kukufungia huko! unapotaka kutoka, vinakuvuta nyuma, huwezi kutegemea furaha na amani ikiwa bado hujasamehe, hujaachilia yoote yanayoutesa moyo wako.

Pengine umejiuliza au umewaambia watu “Wananidharau sana, walinicheka sana, nimeshindwa vibaya, siwezi kusahau, nitakaa hapa hapa Mungu amenipangia niwe hivi”

Si kweli, si unakumbuka hiyo hadithi ya punda kisimani, achana nayo, yakanyage yanayokusonga kwa miguu yako, utapita, tena utakuwa juu, hadithi yako itabadilika. Itakuwa funzo kwa wengine wale walioona hadithi yako ikikuvuta, ikiambatana na maisha yako!!!

Tena unakumbuka hadithi ya Mtume Paulo Jinsi alivyomtikisa yule nyoka?? Unaweza pia, tikisa shida yako, iambie haiwezi kuambatana nawe maana una mpango wa kusonga mbele. Unaona mbele, hilo tatizo lako litakuacha, lina masikio, litasikia na kukuacha!!

Kama umekuwa ni kuwaza kushindwa siku zote, kama umekuwa si mtu wa kuachilia na kusamehe, fikiria tena jinsi Mungu anavyokupenda je asingesahau maovu yako ungekuwa wapi wewe? Isaya 43:25 imeandikwa “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako tena” Unaona sasa? dhambi zako hazikumbukwi tena!

Jisamehe, fanya maamuzi ya kusamehe wengine pia, achilia, Utaona wepesi mkubwa kwenye kila eneo la maisha yako lililokusonga. Usitembelee HADITHI zako za kale na kuziambatanisha na maisha yako mpaka kukufanya ukose furaha, zimebaki HADITHI, Songa mbele!

…..twitter @MARYAKENGO
Advertisements

12 thoughts on “Hadithi…Hadithi!

  1. Mary,
    Mungu akubariki, ujumbe mzuri sana unatia moyo kwa waliokata tamaa na wanaoshindwa kujinasua kujua wapi wamenasa na wafanye nini.

  2. Dada Mary,

    Mtumishi wa Mungu ubarikiwe sana kwa ujumbe wako huu mzuri sana,

    Leonard K

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s