Je Biblia inaruhusu mitume kizazi hiki?

Je, Biblia inaruhusu mitume kizazi hiki au ilikuwa ni kwa ajili ya waliomuona Bwana Yesu wakati alipofufuka? Naomba mistari ya Biblia tafadhali

–Nyakwar Othuon

Advertisements

26 thoughts on “Je Biblia inaruhusu mitume kizazi hiki?

 1. manabii na mitume wapo hata sasa na wanafanya kazi muda woote ila zaman tuliwaona kwa macho au kwakuwasoma lakini sasa kazi zao tunaziona basi kama kazi zao tunaziona na kuzishuhudia basi wapo

 2. karama zote zipo na huduma zote zipo kwa ajili ya kulijenga kanisa na huduma na karama huzitoa roho akimgawia m2 kama apendavyo yeye s m2 anaye tafuta ingawa biblia imesema m2 atake kuwa nazo s kwa ajili ya sifa ila ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo 1kor 12;4,12;28 tayari Mungu amewa hao mitume na s mitume peke yao bali na karama zote zipo hata wewe unaweza ukawa nayo moja wapo efeso 4;11 pasipo hivi huduma hatuwezi kukamilishwa ni lazma ziwepo ndani ya kanisa. Kwa sababu watu wameshika huduma chache na zengine wamezikataa ndo maana hatuoni Utukufu wa Mungu ila tukizikubali Mungu atatenda makubwa ya ajabu hakuna lisilowezekana kwake aaminiye. Utafute uwepo wa Mungu ili atujulishe huduma zetu na karama zetu……….angalizo si kila mtu anaye kuja mbele zako na kujita mtume, nabii mwalimu, mwinjilisti, mchungaji nk unaopaswa kumwamini bali umjaribu kama ni wa Kristo au la 1 Yohana 4:1 utakuwa salama ila mwamin Yesu na kazi zake na watu wake aliowaweka ktk kanisa.

  Barikiwa wote wanao mwamin Yesu Kristo, na wale wasio mwamini bas nawashauri kwa upendo wa Kristo alio weka ndan yangu mwamin ili mpate furaha nafsini mwenu na aondoe kila aina ya mizigo inayokusonga kwa Mungu hakuna lisilowezeka kwa yeye mambo yote yanawezekana. Ila tu ukimwamini.

 3. Ninachokiona hapa tunakataa kuamini Biblia isemavyo kwa sababu ya mapokeo na mazoea yetu.

  Moja, siyo kweli kwamba mtume ni yule aliyemwona Yesu uso kwa uso kama wale 12 wa mwanzo tu. Nimetoa mifano hapo awali lakini kwa sababu ya mapokeo au mazoea yetu ya kidini tunaikataa. Tukikataa kuwepo kwa mitume baada ya wale 12 ambao walimwona Yesu uso kwa uso halafu tukageuka na kusema kuwa Paulo ni mtume wa mwisho tayari tumeshajichanganya. Mfano, tuseme nini basi juu ya utume wa mtu kama Barnaba, maana naye ameitwa mtume (Matendo 14:14) na hakuitwa mtume kwa kumuona Yesu uso kwa uso, kumbuka alikuwa mmoja wa waamini katika kanisa hapo awali kabla ya kuja kuitwa kwenye huduma ya kitume? (Matendo 4:36)

  Pili, kuhusu manabii, walikuwepo kwenye kanisa la mwanzo pale Yerusalemu na wako mpaka leo. (Matendo 13: 1 – 2) kuna majina ya manabii na waalimu waliokuwa kwenye kanisa la Antiokia, Paulo mmoja wao, kabla hajaitwa kwenye huduma ya kitume. Kuna kundi la manabii toka Yerusalem linatajwa na mmoja wao anaitwa Agabo (Matendo 11: 27 -28) Yuda na Sila walikuwa manabii (Matendo 15:32),

  Tatu, huduma za walimu, wachungaji na wainjilisti hizo tunazikubali kirahisi zaidi leo kwa sababu ya mapokeo ya kidini tuliyokulia, mtakumbuka sio muda mrefu uliopita huduma ya mwalimu haikuwa inakubalika kama ilivyo sasa, ilikuwa inaonekana ni ya ngazi ya chini kuliko mchungaji sana sana mtu wa kufundisha watoto Sunday School. Imechukua muda kwa huduma ya mwalimu kukubalika kama huduma kamili katika mwili wa Kristo kwa sehemu kubwa. Ndivyo hata ilivyokuwa kwa huduma ya uinjilisti, tena madhehebu mengine mwinjilisti ngazi ya chini kuliko mchungaji halafu akipanda cheo ndio anakuwa mchungaji na mchungaji anapanda cheo kuwa askofu (ambayo siyo moja ya huduma zile tano, bali ni kazi ya usimamizi), hayo ndio mapokeo tuliyokuzwa nayo na ndio yanatupofua tunashindwa kuuona ukweli ulioko kwenye Neno la Mungu.

  Nne, kuhusu Biblia (Biblia ni neno lenye maana ya mkusanyiko wa vitabu, kama maktaba vile) kutokuendelea kuandikwa hilo siyo tatizo kwani kweli zote tunazohitaji zimo katika hivyo vitabu 66, ila ni vizuri kufahamu ya kuwa wale wanaoitwa mababa wa kanisa ndio walikaa wakaviweka pamoja vitabu vyote vinavyotengeneza Biblia yetu tuliyonayo leo kwenye karne ya 3 au ya 4 AD kama sikosei. Mfano, kuna nyaraka ya Paulo ambayo haikuwekwa kwenye Agano Jipya pamoja na kwamba aliagiza Wakolosai na Walaodikea wabadlishane nyaraka na kuzisoma (Wakolosai 4:16) matokeo yake leo tuna waraka kwa Wakolosai lakini hatuna waraka kwa Walaodikea, Yuda amenukuu kitabu cha Henoko katika waraka wake wakati kitabu hichohicho kilikataliwa na mabaraza ya hao mababa wa kanisa na hivyo hakipo kwenye Biblia yetu.(Yuda 1: 14 – 15). Ipo mifano mingine. Hivyo Biblia ni ramani yetu na Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wetu. Bwana Yesu alisema akija Roho Mtakatifu atatuongoza katika kweli yote, hakuahidi kutuachia kitabu kituongoze bali Roho wake, hivyo tusomapo Biblia Roho Mtakatifu na atutangulie na kutuongoza kuligawanya neno kwa usahihi, hata kama tutalazimika kwenda kinyume na mapokeo yetu.

  Vilevile ni vizuri kutambua ya kwamba siyo mitume wote walioandika injili au nyaraka, Luka na Marko walioandika Injili na Matendo ya Mitume (Luka) hawakuwa miongoni mwa wale mitume 12 wa mwanzo. Hivyo dhana ya kuwa kuwepo kwa mitume leo kunamaanisha Biblia itaendelea kuandikwa siyo sahihi, Mitume wengi tu hawakuandika chochote,kati ya wale 12 wa mwanzo walioachangia kuandika Agano Jipya ni Mathayo, Yohana, Petro na pengine Yuda ndugu yake Yakobo(kuna utata kama ndiye mwandishi wa waraka wa Yuda au ni mwingine), Akina Andrea, Filipo, Bartholomayo, Tomaso, Simoni Mkananayo, Thadeo (wengine husema ndiye Yuda), Yuda Iskarioti (alijiua mapema) na Yakobo nduguye Yohana (aliuwawa kwa upanga wa Herodi) wote hawa tunaweza kusema hawakuchangia kuandika Agano Jipya ila hilo haliwapunguzii chochote katika utume wao. .

  Huduma zote tano zipo mpaka leo hii, maana mwili wa Kristo bado unahitaji kujengwa ili kazi ya huduma itendeke na tukue kuufikia utimilifu wa Kristo mwenyewe ambaye ni kichwa.

 4. Shalom wapendwa
  Yaani na mie nina hiyo imani kuwa Yesu aliwachagua mitume 12 kwa ajili ya kabila kumi na mbili za Israel wakati akiwapo maana alikuwa amesema kipindi kile amekuja maalumu kwa jili ya kondoo wa Israel waliopotea. Hata alipokufa Yuda Iskarioti hakumchagua wala kuagiza mwingine achaguliwe, ila aliwaambia siku ya pentecost wakahubiri mataifa yote wakianzia na Yerusalem, Samaria na dunia yote.
  Lakini alikuja kumtokea mtume “Paulo na kumfanya mtume wa mataifa” na ili wenzie wampokee alimtokea Anania kumweleza kuwa Sauli analetwa kwake ili ampokee na ndiye chombo kitakachokwenda kupeleka injili kwa mataifa.
  Ninavyojua mimi mitume ni kama chombo kinachokuja na ujumbe mpya….
  Yohana mbatizaji alitumwa maalum kutengeneza njia kwa ajili ya ujio wa Yesu kutuokoa, na Yesu alisema huyo ndiye Eliya ajaye…na ole wao wasiomsikia, na hapatakuwapo mwingine nabii kama yeye….Mathayo

  mitume wa Yesu walihubiri injili kwa Israel iliyokuwa tofauti na ile ya sheria ya Musa, toba kwa njia ya imani na ubatizo wakati sheria ilikuwa ni kwa matendo na damu ya wanyama.Waliitwa na kuchaguliwa na Yeye mwenyewe Yesu, na ndio maana walipotaka kujiongezea mtume mwingine walitaja vigezo hivyo kwamba awe alimuona Yesu nk kisha wao ndio wakamchagua kwa kura na sio Roho mtakatifu wala Yesu mwenyewe kuwaambia.

  Mtume wa mwisho Paulo alibadilisha imani ya wenzie kuwa injili ni kwa waliotahiriwa tu, yeye alitumwa maalum kwa jaili ya mataifa na ndio maana kitabu cha Biblia wakiongozwa na Roho mt hakijumuishi matendo wala nyaraka za Mathia au wengine waliofuata kwani naona ilikuwa sio mpango wa Mungu.

  Sababu hizi hunifanya kuwa na imani kuwa mtume ni mtu maalumu kwa kazi maalum sasa ninapokutana na mtume analea waumini au kutoa mafunuo yasioeleweka au yasiyo mapya kibiblia ndio nazidi kuishiwa imani kabisa na hawa mitume, kama ukiangalia mikanganyiko mingi na upotofu unatajwa zaidi kwa mitume kuliko watumishi wengine kwanini hii? jaribu kukagua hata hapa SG tu

  Mimi nadhani mara nyingi watu tunashindwa kukaa karibu na kuisikiliza sauti ya Mungu tunaanza tu kujipa huduma au majina, inaweza kuwa sio kosa ila inatukwaza kutumika kikamilifu mbele za Mungu pia inafanya watu wanakuwa na wasiwasi na nini lengo lako kujipa jina au huduma hiyo na hivyo inakuwa vigumu kuipokea.
  Natumaini nitajifunza mengi hapa, nawapenda wote

 5. Sawa bwana Nyakwar,

  Hakuna mahali biblia imesema ili uwe mtume lazima uwe umemwona Yesu uso kwa uso, au awe amechaguliwa na Yesu uso kwa uso, au atende miujiza fulani maalum. Hicho kitu mimi sijawahi kukisoma kwenye biblia. Ispokuwa vi vile wanazuoni wanavyojaribu kutafsiri kwa kuangalia wale thenashara walivyofanywa kuwa mitume.

  Kama ni lazima mtu achaguliwe na Yesu uso kwa uso, unasemaje kuhusu Mathia ambaye alichukua nafasi ya Yuda,mbona hakuchaguliwa na Yesu uso kwa uso?

  Unasemaje kuhusu Paul, mbona hakuchaguliwa na Yesu uso kwa uso?

  Na hiyo ya kufanya miujiza ambayo itakuwa ni ushuhuda pia mmeitoa wapi? Hebu nionesheni mfano mmoja wa muujiza ambao biblia inasema ni ishara ya utume wa mtu.

  Kisha naomba kuoneshwa katika biblia namna ambayo mitume waliitwa kuhubiri injili kama ambavyo ndg Nyakwar umesema “(He has to preach the Gospel according the way the apostles were call to preach it)”

 6. Brother, Sungura you are making sense but the only guidance we have is the Bible. According to my understanding of the Bible we should not add or take away from it. Now in the issue of being apostle one has to have seen Jesus, appointed face to face with him, He has to perform miracles which has to be witness, He has to preach the Gospel according the way the apostles were call to preach it. I have posted many books that support this understanding.

 7. Aliyeandika hiyo article alianza vizuri, lakini alipofika kwenye suala la miujiza na mitume, kachemsha sana. Hatuwezi kumpima utume kwa sababu ya miujiza, miujiza ni kwa kila aaminie siyo kwa mitume pekee.

  Kuna watu wametumiwa na Mungu kwa miujiza mikubwa sana na haijaandikwa na wala hawajulikani na wengi, japo ni miujiza ya kutisha sana. Kwa mfano: Kuna mzee mmoja wa Tabora alikuwa anaitwa mzee Shimba siku moja wakati anaenda kuhubiri Kongo alikuta mto umefurika maji, akapiga magoti kumwomba Mungu amwambia cha kufanya. Alipofumbua macho baada ya kumaliza maombi alijikuta tayari yuko ng’ambo ya pili. Muujiza huo haujaandikwa mahali popote lakini ni wa kutisha.

  Ni vizuri pia kufahamu msingi wa mitume na manabii unaosemwa ni kitu gani,maana tunajua hamaanishi nyumba ila ametumia tu lugha ya mfano. Na hapa tunaongelea mitume tu, vipi kuhusu manabii? Mitume ambao tumejengwa kwao tunasema ni wale waliochaguliwa na au waliomwona Yesu ikiwa ni pamoja na Paul, vipi kuhusu manabii ambao pia imani yetu imejengwa kwao kama biblia inavyosem, ni akina nani hao maana hatumwoni Yesu akichagua manabii?

  Msingi wa hoja hii ni suala la ukubwa yaani inaonekana mtu akiwa ni mwalimu wa neno la Mungu ni mtu mdogo sana, na mtume anaonekana ndo mkubwa au ana wito mkubwa zaidi, na ndio maana kwa sababu waafrika tunapenda majina (titles) utasikia watu wakipenda kuitwa/kujjita mitume na manabii. Wachache huridhika na kuitwa wainjilisti,walimu au wachungaji.

  Lakini ni vizuri sana kuangalia majukumu yaliyo katika utume kuliko jina na sifa ya kuwa mtume.
  Mimi naamini kuwa huduma ya utume bado ipo kwa kuzingatia hasa maana halisi ya neno mtume au utume. Ndio maana huwa najiuliza sana swali hili “kwa nini Biblia ilikoma kuandikwa”?
  Maana kuna watu bado wanaipeleka injili ya kitume katika maeneo ambayo Yesu bado hajahubiriwa kabisa. Kama vipi nao wangeandikwa katika mfululizo wa kitabu cha matendo ya mtume.

  Ni mtazamo wangu!

 8. Brother Patrick G Kamera You mention a lot of people but there is no where in the Bible to support that they were apostle. “Timothy, Titus, Epaphroditus, Andronicus, Junia” all these name you mention they were people who work under apostle and help apostle in the ministries but they were not apostles. And the books you provided show Jesus giving instruction to his disciple who he also called apostles. The problem today is some are called to be teachers but want to be Bishops. some called to be Bishop want to be apostle we as the body of believers we need to make sure we understand this things.

 9. Kama ilivyokuwa nyakati za Kanisa la mwanzo, kulikuwa na mitume wa kweli na wa uongo vilevile na ndivyo ilivyo hata leo.

 10. The author of that article is not being scripturally consistent, claiming that Paul was the last apostle because He saw Jesus is simply not true. The author conveniently ignores the fact that Barnabas, Apollos, Timothy, Titus, Epaphroditus, Andronicus, Junia and others were also called apostles.

  The problem with that article stems from the fact that the author had already made a conclusion and is now trying to work backwards by poorly cherry picking verses and passages to fit and support their position, A classic case of twisting scripture to fit a belief system rather than revising one’s belief system to fit scripture.

  To claim that it was only apostles who performed miracles is to contradict what the Bible says: Phillip went down to Samaria, preached the Gospel and performed miracles and he wasn’t an apostle ( Acts 8:5 onwards). Stephen who was not an apostle, performed great wonders and signs (Acts 6:8) Jesus said: these signs shall follow them that believe, not apostles only – they shall lay hands on the sick and they shall recover etc. Read Mark 16: 15 – 20. Jesus sent 70 of his disciples to preach, heal, cast out demons etc, not just the 12 apostles, Read Luke 19.

  As for Apollo’s apostleship you must have missed one scripture reference I gave earlier, here it is again: 1 Corinthians 4: 6 – 13

  Timothy’ s and Silas’s aposteships are implied here: 1 Thessalonians 1: 1 – Paul, Silas (Silvanus) and Timothy, To the church of the Thessalonians in God the Father and the Lord Jesus Christ:
  Grace and peace to you. – then fast forward to 1 Thessalonians 2: 6: – We were not looking for praise from people, not from you or anyone else, even though as apostles of Christ we (we who? Paul, Timothy and Silas) could have asserted our authority

  Titus’ apostleship is implied here: 2 Corinthians 8:23 – If anyone inquires about Titus, he is my partner and co-worker concerning you. Or if our brethren are inquired about, they are messengers of the churches, the glory of Christ.
  Notice it says Titus is a partner and co-worker or fellow worker implying their callings and functions are the same. That is why Titus could bring order to the churches at Crete by contending with false teaching and establishing elders over congregations in every city there. ( Titus 1:5) that is an apostolic function. The precedent was sent in Samaria when Phillip went down and preached with signs, wonders and miracles and many people believed in Jesus and were baptized, the church sent apostles to establish the church there. (Acts 8:14 onwards)

  The Bible is very clear that there are apostles today, actually the very fact that there are false apostles proves the existence of true ones as the adage goes, the counterfeit is fact that the real exists. I choose to believe what the Bible says, I hope you do too. Blessings!

 11. Wapendwa kuna mahali nimekutana na hii pengine tutapata maswali zaidi!

  The Apostles Foundational Role

  Now therefore ye are no more strangers and foreigners, but fellowcitizens with the saints, and of the household of God; And are built upon the foundation of the apostles and prophets, Jesus Christ himself being the chief corner stone; In whom all the building fitly framed together groweth unto an holy temple in the Lord: In whom ye also are builded together for an habitation of God through the Spirit.

  Ephesians 2:19-22

  Here we see the church compared to a building.

  Jesus himself is the chief cornerstone. The apostles and prophets make up the rest of the foundation. This analogy helps us to see the foundational role of the apostles.

  When building a building, the first thing that is laid is the foundation. Everything else is then built upon that one foundation. Do we then go back after building a couple of stories and lay the foundation again? No. It is only done once. The foundation is laid one time in the beginning and then never again.

  The same is true of the apostles. They served as a foundation for the emerging church. We should not expect to see another group of apostles later on any more than we would expect someone building a building to lay another foundation on the fourth floor. After all, Jesus Christ, being the chief cornerstone, is a part of this foundation as well. We certainly do not expect there to be another Jesus Christ, do we?

  The Witness of An Apostle

  Apostles were to bear witness to the fact that Jesus had risen from the dead. In order to do this, they had to have seen him after he was resurrected.

  And [Jesus] said unto them, Thus it is written, and thus it behoved Christ to suffer, and to rise from the dead the third day… And ye are witnesses of these things.

  Luke 24:46-48

  When looking for someone to replace Judas, the one chosen had to be a witness unto the resurrection.

  Beginning from the baptism of John, unto that same day that he was taken up from us, must one be ordained to be a witness with us of his resurrection.

  Acts 1:22

  Jesus told the apostles:

  But ye shall receive power, after that the Holy Ghost is come upon you: and ye shall be witnesses unto me both in Jerusalem, and in all Judaea, and in Samaria, and unto the uttermost part of the earth.

  Acts 1:8

  And that is exactly what they did.

  And with great power gave the apostles witness of the resurrection of the Lord Jesus: and great grace was upon them all.

  Acts 4:33

  Paul the apostle, in defending his apostleship, appealed to the fact that he had seen Jesus after he had risen from the dead.

  Am I not an apostle? am I not free? have I not seen Jesus Christ our Lord? are not ye my work in the Lord?

  1 Corinthians 9:1

  After that, he [JESUS] was seen of James; then of all the apostles. And last of all he was seen of me [PAUL] also, as of one born out of due time. For I am the least of the apostles, that am not meet to be called an apostle, because I persecuted the church of God.

  1 Corinthians 15:7-9

  This LAST passage is devastating for those who believe that there are apostles today. In order to be an apostle one has to have seen Jesus after he rose from the dead. Paul says that Jesus was seen last of all by him. He is the last one to see Jesus after his resurrection. Since no one since Paul has seen Jesus, no one since Paul can be an apostle. Therefore, there can be no apostles today.

  The Choosing of An Apostle

  The apostles were hand-picked by Jesus himself.

  And when it was day, he [JESUS] called unto him his disciples: and of them he chose twelve, whom also he named apostles;

  Luke 6:13

  Not only were the original twelve apostles hand-picked by Jesus, Paul was as well.

  And as he [Paul] journeyed, he came near Damascus: and suddenly there shined round about him a light from heaven: And he fell to the earth, and heard a voice saying unto him, Saul, Saul, why persecutest thou me? And he said, Who art thou, Lord? And the Lord said, I am Jesus whom thou persecutest: it is hard for thee to kick against the pricks. And he trembling and astonished said, Lord, what wilt thou have me to do? And the Lord said unto him, Arise, and go into the city, and it shall be told thee what thou must do.

  Acts 9:3-6

  After Jesus appeared to him, he said of Paul:

  …for he is a chosen vessel unto me, to bear my name before the Gentiles, and kings, and the children of Israel:

  Acts 9:13-15

  Paul refers to himself as:

  Paul, an apostle, (not of men, neither by man, but by Jesus Christ…

  Galatians 1:1

  Paul was an apostle because he had been hand-picked by Jesus Christ. Since Jesus isn’t appearing to anyone today (see our last point), no one is being hand-picked, either.

  The Signs of An Apostle

  Jesus gave the apostles the ability to perform miraculous signs..

  And when he [JESUS] had called unto him his twelve disciples, he gave them power against unclean spirits, to cast them out, and to heal all manner of sickness and all manner of disease. Now the names of the twelve apostles are these…

  Matthew 10:1-2

  …for in nothing am I [PAUL] behind the very chiefest apostles, though I be nothing. Truly the signs of an apostle were wrought among you in all patience, in signs, and wonders, and mighty deeds.

  2 Corinthians 12:11-12

  Paul refers to his ability to perform miracles as “the signs of an apostle”.

  And they [The Apostles] went forth, and preached every where, the Lord working with them, and confirming the word with signs following. Amen.

  Mark 16:20

  This miracle-working power was given to the apostles to bear witness that they were God’s messengers and that they were speaking the very words of God.

  Many people operate under the false assumption that all Christians in the early church were working miracles. This is simply not true.

  And fear came upon every soul: and many wonders and signs were done by the apostles.

  Acts 2:43

  And by the hands of the apostles were many signs and wonders wrought among the people…

  Acts 5:12

  If every believer had this power, why did Jesus need to give it to the apostles? They would have had it already. There is not one miracle performed in the new testament by anyone other than Jesus, the apostles, or those who were directly chosen by Jesus or the apostles.

  Those who claim to be apostles today may claim to have this kind of miracle-working power but there is little (no) evidence of it.

  Now Peter and John went up together into the temple at the hour of prayer, being the ninth hour. And a certain man lame from his mothers womb was carried, whom they laid daily at the gate of the temple which is called Beautiful, to ask alms of them that entered into the temple;

  Acts 3:1-2

  Then Peter said, Silver and gold have I none; but such as I have give I thee: In the name of Jesus Christ of Nazareth rise up and walk. And he took him by the right hand, and lifted him up: and immediately his feet and ankle bones received strength. And he leaping up stood, and walked, and entered with them into the temple, walking, and leaping, and praising God. And all the people saw him walking and praising God:

  Acts 3:6-9

  Compare this to the so-called miracles that we see today. Our would-be apostles supposedly heal people of things like: earaches, back pain, high blood pressure, and other such things that cannot be seen or verified.

  This man was lame from his birth. He had never walked. Not only did he have bone problems, he would have had muscle problems as well. Have you ever seen the legs of a person who has been in a wheel chair for a long time? They have no muscles in them. The muscles in their legs would have to be regenerated before they could walk.

  In the Bible days, when people wore robes, the change in this man’s calves would have been seen immediately. Jesus healed a man with a withered hand. His hand would have been recreated. Again, this would have been obvious to all who were watching. Jesus and the apostles raised the dead. Jesus raised Lazarus after he had been dead for days. His body was severely decomposed and even stank. These kinds of miracles could not be questioned.

  Why don’t we see people performing these types of miracles today? Because those who claim to have miracle-working power don’t actually have it.

  The Bible says this concerning the high priest and other religious leaders of the Jews:

  And beholding the man which was healed standing with them, they could say nothing against it. But when they had commanded them to go aside out of the council, they conferred among themselves, Saying, What shall we do to these men? for that indeed a notable miracle hath been done by them is manifest to all them that dwell in Jerusalem; and we cannot deny it.

  Acts 4:14-16

  It is easy to deny the works of the so-called apostles today. They are often heard about second hand, and the tale seems to grow with the telling. There are researchers, many of them medical doctors, who have tried to verify these so-called miracles. What they find without exception is exaggerations, deception and even outright fraud. They find absolutely no evidence that any true miracle has actually taken place.

  Compare that with miracles of the true apostles. Their miracles were performed out in the open for all to see. No one could deny them or speak a word against them.

  Don’t get me wrong. I believe that God still heals and performs miracles today in answer to our prayers. What I’m saying, however, is that there are no “Apostles” today. There is “healing” but there are no longer any “healers”.

  False Apostles

  The Bible tells us that there were not only “true” apostles but that there were also “false” apostles. The following passage sends a stern warning of the dire consequences that await those who claim to be apostles but aren’t.

  For such are false apostles, deceitful workers, transforming themselves into the apostles of Christ. And no marvel; for Satan himself is transformed into an angel of light. Therefore it is no great thing if his ministers also be transformed as the ministers of righteousness; whose end shall be according to their works.

  2 Corinthians 11:13-15

  Jesus commends the Ephesians for being able to spot these false apostles.

  I know thy works, and thy labour, and thy patience, and how thou canst not bear them which are evil: and thou hast tried them which say they are apostles, and are not, and hast found them liars:

  Revelation 2:2

  It’s easy to spot false apostles today. Since there are no true apostles today, anyone who claims to be an apostle is a false apostle.

 12. This is good learning for me brothers, I am using this as a learning stone for spiritual growth. Now I don’t remember anywhere in the Bible, where it refer Timothy or Titus as apostles please help me with this. Apollos for sure I am not sure where the Bible refer to him as an apostle. The biggest thing for me,when come to the apostle they were given a power to heal which means, that the person who was being healed did not have to believe in Jesus it was all on the apostles. The real apostle perform miracle making a real cripple person walk which was a evidence of their work which was entrusted in them by Jesus.

 13. Swali zuri hili, nichangie kifupi kuwa Mitume wapo hata leo. Ila tufahamu kuwa kuna kulia na kushoto, mbele na nyuma, halisi na feki. Hata Yesu hayuko mmoja, kuna YESU KRISTO. Kuna BARI YESU. Kuna YESU YUSTO. Kuna MUNGU MUUMBA VYOTE. Kuna mungu wa dunia hii. Efeso inasema kazi ya Huduma 5 ni KUWAKAMILISHA WATAKATIFU ( kanisa) ina maana tukizikosa huduma hizo 5 kanisa halitakamilika, litabaki changa, toto siku zote. Ukiwaangalia watoto wakati wanakicheza, utakuta wanagombea hata nyumba ya udongo walioijenga, hawawezi kulalamo, paul alisema anahesabu vitu vyote kuwa kama MAVI. Fil 3.8. Kanisa linahitaji Mitume wa kweli, na wapo, pia wapo feki. MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO. Ndio wanazaa Wakristo Feki. Barikiweni.

 14. To say that the word “was” is key in concluding that the gift of apostle is no longer operational is incorrect, if you extend that same logic then you’d be forced to conclude that since it was the same Jesus who gave(notice the past tense) the other ministry gifts as well, then they are also no longer operational. So by the same token we don’t have pastors or evangelists or prophets or teachers but that is not the case.

  There were others who were called Apostles who hadn’t been with or seen Jesus in the flesh, one such apostle that comes to mind is Apollos, who was from Alexandria and knew only of the baptism of John but was mighty in scriptures and when Priscilla and Aquila heard him preach in the synagogue they took him aside and explained the gospel to him. He was later called an Apostle. There are other examples too, most likely Timothy (heard the gospel from his grandmother Lois and his mother), Titus (a gentile believer from Ephesus IIRC), there are others as well. Blessings!

 15. wengi hupinga utume wa Paulo wakidai kajiita mtume mwenyewe je?kuna andikololote linalo mpinga?

 16. I thank you all for this discussion but, if I understand the Ephesians 4:11-12 correctly It (was) he who gave some to be apostles which is correct all those you mention people were call to be apostle the key word (was). In the book of Act 1:21-22 and 1 Corinthians 9:1 but this book talk about those apostles were either with Jesus or seen Jesus. thus my Question.

 17. Katika kizazi hiiki mitume wanaruhusiwa kabisa kama zilivyo huduma nyingine za unabii,ualimu,uchungaji na uinjilisti kadhalika na huduma ya utume ipo.Ukisoma Waefeso 4:11-12pamoja na huduma nyingine mitume wamewekwa na Mungu katika kizazi hiki ili kukamilisha watakatifu na mwili wa Kristo ujengwe.

  Lakini pia ukisoma 1kor12:28 Mungu ameweka mitume wa kwanza katika kanisa Kwa iyo ile tu kwamba kanisa lipo na MUngu anataka likamilishwe ndani ya Kristo na Mwili wa Kristo ujengwe means hata huduma ya utume ipo pamoja na hizo nyingine kwa kusudi aliloweka Mungu.

  Cha Muhimu katika utume ni kusudi la Mungu kwa sababu klila mtu anayetumikia kusudi la Mungu amewekwa na Mungu lakini kujiita tu mtume kama hujapewa hiyo huduma na Mungu mwenyewe haifai.

 18. Jibu ni ndiyo, mitume wapo mpaka leo, ni huduma iliyolewa na Bwana Yesu kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu – Waefeso 4:11. Hakuna mahala ambapo Biblia imesema kuwa hakuna mitume baada ya Pentekoste. Kuna mitume wengi tu walioitwa kuwa mitume baada ya Pentekoste, kama akina Paulo, Barnaba, Apollo, Yakobo (nduguye Bwana Yesu) n.k.

  Maandiko:

  Matendo 14: 14 – Barnaba na Paulo wanatajwa kama mitume

  1 Wakorintho 4: 6 – 13 – Apollo anatajwa kama Mtume

  Wagalatia 1: 19 – Yakobo nduguye Bwana Yesu anatajwa kuwa Mtume (Ndiye aliyeandika waraka wa Yakobo)

  Kuhusu watu kujiita mitume hapo kuna mambo ya kuangalia, Paulo alijiita mtume mara nyingi tu tena kwa ujasiri na kutetea utume wake akisema ishara za kitume zimeonekana katikati yao, soma 2 Wakorintho 12:12 ,

  Hivyo utambue ya kuwa ukijiita mtume watu watakupima kulingana na Neno la Mungu na itaonekana wazi kama ni mtume au siyo, maana ndivyo neno linavyotuagiza.

  Katika Ufunuo 2: 2 waliwajaribu waliojiita mitume na ikaonekana kwamba siyo mitume na Bwana Yesu aliwapongeza kwa hilo.

  Kanisa leo linahitaji huduma zote tano maana Waefeso 4:12 – 13 bado haijatimia. Mbarikiwe

 19. Rev Lee Cosmas asante sana kwa ufafanuzi wako ila sijakuelewa kama unasema Biblia inaruhusu Mitume kwa Kizazi hiki au hapana?

 20. Je, Biblia inaruhusu mitume kizazi hiki au ilikuwa ni kwa ajili ya waliomuona Bwana Yesu wakati alipofufuka? Hili ndilo swali alilouliza Nyakwar Othuon.

  Kabla ya kujibu kwa haraka swali hili napenda sana kuchanganua maana ya neno “Mtume”
  Jina hili kwa lugha yetu ya Kiswahili limetafsiriwa kutokana na neno la Kigriki “apostolos” lenye maana ya “mtu atumwaye” yaani “aliyetumwa” yaani ana bosi wake aliyemtuma. Neno hili apostolos lilichukuliwa pia na lugha nyingine kama vile Kilatini, Kiingereza na hata Kijerumani. Katika Agano la Kale “aliyetumwa aliitwa “schaliah” (2 Mambo ya Nyakati 17:7-9)
  Katika Agano Jipya “aliyetumwa” yaani apostolos (2 Korintho 8:23) alikuwa mtumishi wa Ushirika. Hivyo utume au huduma hii ya mtume wa Yesu Kristo unafanana bila shaka na ule wa wa Agano la Kale yaani “schaliach”, lakini pia kuna tofauti zake.
  Mtume wa Yesu Kristo huwa amepewa wajibu/jukumu maalumu akiwa mtu binafsi. Mtume basi huwa ni mwanafunzi wa Yesu (a disciple of Jesus Christ). Mtume huyu hutenda kwa jina la Yesu na Yesu hutenda ndani yake.
  Ni vema kujua ya kwamba kila “mtume” ni mwanafunzi (disciple). Lakini si kila mwananfunzi huitwa kuwa mtume au kujifanya kuwa mtume. Mtume hajiiti mwenyewe bila ya kuwa na aliyemtuma. Kama kuna mtu au watu wanaajiita wao ni mitume bila ya kutumwa basi hapo kuna kasoro.
  Soma: Matendo ya Mitume 1:1-8
  Injili ya Yohana 20:19-23
  Basi yapo mambo mengi ya kutafakari juu ya neno hili.
  Ubarikiwe.

 21. Asante sana dada Stella suala la huduma tano naelewa na najua kuwa kulikuwepo na mitume kama Paulo na wengine lakini swali ni kwamba kama biblia inaruhusu kuwa na mitume kwa kizazi hiki. Nimekutana na maandiko yanayopinga kuwepo kwa mitume baada ya ya siku ya Pentekoste.

 22. Haleluya!
  efeso 4:11-12, maandiko hayo lazima yatimie kwetu leo,Sisi tumejengwa chini ya misingi ya mitume na manabii ili mwili wa kristo uwezwe kujengwa,lazima hizo huduma tano ziwepo nadani ya kanisa. barikiwa

 23. Mitume ni wale waliomuona Yesu uso kwa uso. Na zaidi ya hapo hapajatokea mitume wengine.

 24. Mi nadhani hapaswi kuwepo Mtume peke yake ndani ya Kanisa/Huduma bali wawpo pia Wachungaji , Maaskofu na Wenye karama zote il mwili wa Kristo utimie.
  hii kusema Mtume/nabii anasimama peke yake kuhudumia kanisa zima ni upotofu wa kuelewa biblia na kutafuta mambo yake mwenyewe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s