Kwanini umechagua kuabudu kanisani kwenu?

Una sababu gani zimesababisha uabudu mahali hapo? Kuna watu wengine wanaenda kanisani kwa sababu ya Mchungaji, Wazazi, Vyombo vya muziki na uimbaji, ukubwa wa kanisa na miujiza nk nk. Wapendwa kama uko huru tuambizane sababu gani zinatufanye tupende mahali tunapokutanika kuabudu!

 

 

Advertisements

19 thoughts on “Kwanini umechagua kuabudu kanisani kwenu?

 1. Tatizo kubwa Ni kwamba watu wanaongozwa kwa mawazo ya kibinadam sio ya bible wapendwa.
  2 kor 6:1-18
  Mtume Paulo amefafanua Vizur sana pia mwishoni akatoa angalizo/tamko kuhusu nini cha kufanya baada ya kumjua Kristo ya kwamba tusiambatane na hao waliopo katka giza.
  Maana yake ibada zao usishiriki maana Ni sumu zitakuua kiroho watoto wa Mungu,
  tuwe makini sana makanisa tuliopo maana baada ya kumpata Yesu Kristo kuna vitu lazima uviache ikiwapo dini yako kama haiendani na Misingi ya Kristo na hakuna kiongozi ambaye Ni Roho Mtakatifu mioyoni mwa watu.

  2 kor 6:12-18
  12 Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu ninyi wenyewe, na si kwa upande wetu.
  *
  13 Sasa nasema nanyi kama watoto
  wangu, wekeni mioyo yenu wazi kama.nasi tulivyofanya.
  *
  14 Msiambatane na watu wasioamini.
  Je, wema na uovu vyapatana kweli?
  Mwanga na giza vyawezaje kukaa
  pamoja?
  *
  15 Kristo anawezaje kupatana na Shetani?
  Muumini ana uhusiano gani na asiyeamini?
  *
  16 Hekalu la Mungu lina uhusiano
  gani na sanamu za uongo?
  Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema:
  “Nitafanya makao yangu kwao, na
  kuishi kati yao; Nitakuwa Mungu wao,
  nao watakuwa watu wangu.”
  *
  17 Kwa hiyo Bwana asema pia:
  “Ondokeni kati yao, mkajitenge nao,
  msiguse kitu najisi, nami nitawapokea.
  *
  18 Mimi nitakuwa Baba yenu, nanyi
  mtakuwa watoto wangu, waume kwa
  wake, asema Bwana Mwenye Uwezo.”

 2. Bwana Yesu asifiwe,
  Binafsi naabudu katika kanisa la kawaida na ninaamini niko pale kwa kuwa ni mpango wa Mungu mimi kuwa pale na kuna kazi ya Mungu ambayo natakiwa kuifanya mahali pale.Hata hivyo naamini kuwa Mungu ni mwaminifu kusudi lake likikamilika anaweza akanipeleka pengine Hivyo ni vizuri kwa mtu aliyeokoka kufahamu Kusudi la Mungu juu yake na iwapo mahali alipo ndipo Mungu anapotaka awepo.Mungu awabariki.

 3. 1Kor. 1.12-13a
  Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu. Maana yangu ni kwamba: Kila mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo,” mwingine, “Mimi ni wa Apolo,” mwingine “Mimi ni wa Kefa” na mwingine “Mimi ni wa Kristo”. Je! Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulibishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa kwa jina la Paulo?
  1Kor. 3:1-7
  Ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwilini, kama watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, wala si chakula kigumu, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa hicho chakula kigumu. Naam, hata sasa hamkiwezi. Kwa maana ninyi bado ni watu wa mwilini. Kwa kuwa bado kuna wivu na magombano miongoni mwenu, je, ninyi si watu wa mwilini, nanyi mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Kwa maana mmoja anaposema, “Mimi ni wa Paulo,” mwingine, “Mimi ni wa Apolo”, je, ninyi si wanadamu wa kawaida? Kwani, Apolo ni nani? Naye Paulo ni nani? Ni watumishi tu ambao kwa kupitia wao mliamini. Mimi nilipanda mbegu, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliyekuza. Hivyo mwenye kupanda mbegu na mwenye kutia maji si kitu, bali Mungu peke Yake ndiye akuzaye.
  MAFAFANUZI
  Niko ndani ya dhehebu, lakini nimegundua kuwa haya madhebu are very very dangerous katika kuzuia utukufu wa Mungu kuonekana ndani ya Kanisa la Kristo. Madhehebu niseme sio nia ya Kristo hakika, na roho iliyo nyuma ya madhehebu inafanya vita kali sana na Kanisa la Kristo. Unapoendelea kubobea kwenye misimamo ya dhehebu lako inayokutofautisha na watu wa dhehebu jingine unaendelea kuwa mchanga zaidi kiroho yaani unakuwa wa mwilini zaidi, unaendelea kuongeza ukuta unaokutenga na wakristo wenzako wa madhehebu mengine(1Kor.3:1-4). Ninaogopa kusema kuwa Kanisa la Tanzania tunapokaribia na kurudi kwa Yesu kuchukua Kanisa badala ya kukua tunaendelea kuwa wachanga siku kwa siku. Siku hizi kuna kitu kinaitwa “denominations politics” watu wanakaa wanawaza na kuwazua nini waje nacho tofauti na dhehebu jingine kwa nia ya mashindano tu, wanapigana vijembe hadi kwenye magazeti ya udaku, wakiwa na tittle za Mchungaji mkuu, mwinjilisti wa kimataifa, mtume, nabii, mwalimu n.k. (1Kor. 3:3-wivu na magombano)
  Mwanzo kanisa lilitajwa kutokana na eneo husika wale waamini wanakoishi, mfano kanisa la Filipi, Korintho, Laudekia, Kolosai n.k. Kwa maana kuwa badala ya madhehebu tunayoyasikia tulitegemea tuwe na Kanisa la Mwananyala likijumuisha Wakristo wote waliozaliwa mara ya pili katika eneo hili, Kanisa la Temeke, Kanisa la Njiro, Kanisa la Kihesa, kanisa la Lisaboni n.k. Na yupo malaika wa Kanisa la eneo husika, kwa ajili ya kuwahudumia. Lakini sasa tumekuwa kama watu wa Korintho sasa, tupo mtaa huo huo lakini huyu yuko kwa Paulo, mwingine kwa Kefa, mwingine kwa Apollo n.k. Mungu atusaidie sana. Unaweza pita mtaa fulani unakuta upande mmoja kuna jengo la dhehebu moja zuri kweli kweli, upande wa pili kuna kajengo ka dhehebu jingine kamefunikwa na mifuko ya cement, chini vumbi, paa wakati wa mvua linavuja n.k. Lakini hawa wote wanajiita Wakristo. Upande wa kwanza wanakusanya sadaka waezue mabati ili waweke vigae wakati upande wa pili bati moja ni sadaka ya wiki nzima. Na tunashangilia tunaenda Mbinguni.
  Can you imagine, watu wawili tuliookoka tupo shina moja au mtaa mmoja au hata nyumba moja ya kupanga lakini, lakini kwa sababu tu tunasali madhehebu tofauti hatufahamiani hatuna ushirika wowote. Mtu huyu huyu ana uhusiano nzuri na mawasiliano mazuri ajabu na mlokole mwingine ambaye yuko Kata nyingine au hata mkoa mwingine na wanashirikishana kuuumbea mtaa ule ule. Hivi Yesu mnayemwamini ni huyo huyo mmoja? Mbingu mnayoenda ni hiyo hiyo moja? Mungu unayemtumikia ni huyo huyo mmoja? Kwanye hiyo mistari hapo juu kuna maswali mengi sana Roho mtakatifu amekuuliza, ebu yajibu. Je! Kristo amegawanyika? Je, Paulo* ndiye aliyesulibishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa kwa jina la Paulo? je, ninyi si watu wa mwilini, nanyi mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Je, ninyi si wanadamu wa kawaida? Kwani, Apolo* ni nani? Naye Paulo* ni nani? (* weka jina la dhehebu lako)
  Kila dhehebu lina mitizamo yake inayotumiwa na adui kuwatenga, kuwapambanua, na kuwatofautisha na watu wa dhehebu jingine. Neno la Mungu linatoa agizo; Huku tukimtazama Yesu mwenye kuanzisha na mwenye kuitimiza imani yetu.( Ebr.12:2a). Swali: Aliyeanzisha imani yako ni Yesu au dhehebu lako? Unamtazama nani sasa?
  Katika 1Kor. 1: 10b Roho Mtakatifu anaagiza kuwa na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi . Umoja huu katika Zab.133:1-3 unasisitizwa hivi
  Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele.
  (i) Kama sio vyema ni mbaya, kama sio kupendeza ni kuchukiza.
  (ii) Tumekuwa tukijifariji kuwa hata kama tuko madhehebu tofauti lakini kiroho tupo pamoja. Anasema Pamoja & kwa Umoja.
  (iii) Mafuta ni ishara ya Roho Mtakatifu, utukufu wa Mungu.
  (iv) Umande mlima Sayuni ni ishara ya Baraka.
  (v) MUNGU AMEAMURU Baraka & na UZIMA unaodumu milele(permanent).
  Tunaweza kung’ang’ana kufundisha watu mafanikio ni vizuri lakini ukiinuliwa sana kiuchumi wakati huelewani na ndugu zako inakusadia nini. Kanuni ya kupokea Baraka zilizoamriwa kwa ndugu katika Kristo ni lazima make kwa pamoja na kwa umoja mkia na nia moja(Prospering & be blessed ni vitu viwili tofauti kabisa). Mitaa yetu, mikoa yetu, ofisi zetu, nchi yetu haiwezi kuwa ya Baraka zilizoamriwa sisi wana wa Mungu tusipofika mahali pa kukaa pamoja na kwa umoja. MUNGU ATUSAIDIE SANA.

 4. Helena Ntembeje, nimefurahishwa sana na mchango wako wa maoni hapa. Ubarikiwe sana. Harusi yako ninaisubiri kwa hamu sana utaifanyia Kigoma au Rukwa? au Dar?

  Mambo vipi Helena Ntembeje? Siku nyingi hatuwasiliani mtu wangu?

  Halafu hivi wewe pale unaposali unafuata nini? Siyo mchumba wako kweli?

  Kila mmoja anayesoma blog hii ajiulize kama kanisani kwake wanafundishwa kwa kina yafuatayo:

  1. Maana ya Wokovu kwa kina (Je, unao uwezo wa kueleza wengine maana ya wokovu)

  2. Maana ya kujazwa Roho Mtakatifu kwa kina (Je, umejaa Roho Mtakatifu)

  3. Uadilifu kabla na baada ya Ndoa (Kutofanya ngono kabla ya ndoa au nje ya ndoa)

  4. Ndoa za Kikristo zinapaswa kuwaje (Je, unakubaliana na ndoa za mitaala)

  5. Je, unafundishwa kwa kina maana ya Kifo cha Yesu Msalabani na faida zake.

  6. Je, kanisani kwako umewahi kuona kiongozi wako akikemea mapepo yawatoke waliopagawa (kama wapo siku hiyo) au wanaambulia kumwagiwa maji ya baraka tu? Hapo hapafai.

  7. Je, Kanisani kwako waumini wanapatiwa nafasi ya kujifunza maandiko (Free or self Bible study) au wanamtegemea kiongozi tu awasomee? Hapo hapafai kusali.

  8. Je, Kanisani kwako wanaruhusu watu kumlilia Mungu kwa mahitaji yao ya sirini (personal secret needs) wawapo kanisani? Au kila mkutanikapo kiongozi tu ndiye anayesali huku wewe ukimfuatisha au kumsikiliza? Hapo hapafai.

  9. Je, kanisani kwako kiongozi wa kanisa au wasaidizi wake wanavuta sigara na bado wanaendelea na huduma za kanisa? Kama ni Ndiyo, Hapo hapakufai. Toka kati yao.

  10. Je, Kiongozi wa kanisa lako au wasaidizi wake wana nyumba ndogo (kwa siri au kwa wazi) na huku wanaendelea kutoa huduma kanisani? Kama ni ndiyo toka kati yao?

  11. Je, kanisani kwako unaenda kwa sababu wazazi wako na ndugu zako wote umewakuta hapo hata kama kanisa hilo lina mojawapo ya matatizo niliyoyataja hapo juu? Toka kati yao. Usifuate mkumbo wa wazazi au ndugu zako. Amua leo.

  12. Je, kanisani kwako wanakemea dhambi waziwazi madhabahuni? Je, wanakemea kwa nguvu kila aina ya dhambi za vijana au watu wazima bila kuona haya wala uso wa mtu? Toka kati yao kama hawafanyi hivyo.

  13. Je, kanisani kwako waumini wanapewa muda wa kusifu na kuabudu Mungu kila mkutanapo au ni ukimwa tu na hofu hutawala kusanyiko mwanzo mwisho na hakuna kumwimbia Mungu na kumsifu kwa pamoja? Hapo toka hapafai.

  Leo naomba niishie hapo. Kama kanisani kwako hayo ni nadra tafuta kanisa lingine. Hapo ulipo hakuna Mungu bali kuna dini tu.

 5. Ajabu ni kwamba siku hizi watu wanaenda kwenye makanisa kwa sababu wanatolewa unabii na kuambiwa mambo yao ya zamani au matatizo yao ndio maana Yesu alisema akija ataikuta imani duniani?Mambo yamebadilika sana na hatari kuongozwa na mambo yanayojitokeza siku hizi,Biblia inawekla wazi kuwa waoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio Wana wa Mungu Rum8:14 Ni vyema kuongozwa na Roho kuliko kuongozwa na vitu au matukio au miujiza.Roho mtakatifu ataachilia Uhuru ndni yako kuabvudu mahali fulani..2kor3:17

  Kuna makanisa mengi ya ajabu yamejitokeza unakuta huyo mwanzilishi anajipa nafasi ya Mungu na wachungaji wanapewa nafasi ya Yesu na waumini wamepewa nafasi ya Roho mtakatifu….nilishtuka sana siku moja nilikutana na rafiki wa siku nyingi akanielezea kuhusu hili kanisa wanafundishwa kuwa hawatakiwi tena kutafuta majibu kwa Mungu bali watafute majibu kwa nabii,Na watu wengi wanafuata hayo mafundisho…..tunahitaji kuwa makini ili tusipoteze kusudi la Kristo kutuokoa.

  JAMANI TUWE MAKINI WANA WA MUNGU

 6. wengi wana soma teologia halafu wana fungua makanisa ,kwa faidazao nasio Mungu kawatuma ndio maana hakuna muujiza wowote,nahao hupinga miujiza sana sababu haiwezekani kutendeka kwao,biblia mwanzo hadi mwisho miujiza mingi ilitokea,hatutaki maneno matupu,watu wana matatizo tofauti,mapepo,magonjwa,umaskini,utasa, hawamjuwi Yesu ni vizuri watatuliwe matatizo yao iliwaone uzuri wa Yesu,Mungu ni wamiujiza .,wengine husema miujiza hutoka kwa Shetani hao hawaamini kama Mungu wao anaweza kutenda sasa wanaamini nini?hatuwezi kuacha kukataa muujiza eti sababu shetani naye hutenda,alikua mbinguni,nayeye huzuwia hata malaika waMungu mKristo hushinda kupitia yesu tu, nilazima neno tulilolipokea lizae matunda ndani yetu. Mungu awabariki wote waMpendaO Kristo.

 7. Nina abudu ninapoabudu sababu Yesu amenifanya mateka toka nilipokuwa naabudu mwanzoni,na si peke yangu tupo wengi ndio maana asilimia kubwa ya tuliopo tumetoka ktk dini na madhehebu mbalimbali wala hatuko kimtiririko wa kindugu au ukoo yaani tangu mababu yaani ktk madhehebu yetu ya asili kitu ambacho Yesu kilimfanya asulubiwe

 8. Wapendwa Bwana Yesu asifiwe!!
  Kwa nyongeza,wengine hupenda kuabudu mahali walipo kwa sababu ya kuridhi/kufuata matakwa ya kwa wazaziwao na wengine ni kufuata mkumbo wa wengine.
  Mbarikiwe sana wapendwa!!

 9. Kufuata miujiza ni kupotea kabisa, kwani hata Ibilisi naye hufanya hayo!! Mi napenda kushauri tu watu waifuate Neno la Mungu. Tunadanganyika tu eti miujiza, ooh, hamna upako, oooh uchawi nk. Fuateni ukweli wa Biblia. Maana imeandikwa, kuwa MUNGU mmoja, IMANI moja, UBATIZO mmoja…Efes 4:6.

  Leo makanisa yako mengiiiiii. Someni Neno la Mungu litawaweka huru.

 10. Bwana asifiwe. Mimi napenda mahali ninapoabudu kwasababu;
  1. Nalishwa chakula cha roho cha kushiba
  2. Kutokana na kushiba Neno naweza kusimama palipobomoka ili niweze kutengeneza kwa msaada wa Mungu.
  3. Napata huduma zote za kiroho sawa na hitaji langu kwa wakati wowote.
  Nina sababu ya kusema asante Mungu kuniweka mahali nilipo.

 11. PLEASE REFER FROPM BIBLE VERSES ….
  “msiache kukusanyika kila iitwapo leo, maana walipo wawili watatu kwa jina langu (yESU) na mm nipo.” frm MATHEW
  “FANYENI KAZI SIKU 6 NA SIKU YA 7 MPUMZIKE KWA KUMWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU” frm GENESIS

  HAYO NDO YA MSINGI MENGINE YOTE MTAKAYOSEMA NI NYONGEZA TU.

 12. BWANA YESU APEWE SIFA HESHIMA NA UTUKUFU SASA NA HATA MILELE. NINAPENDA KUSHIRIKI KIKAMILIFU ENEO HILI KWANI LIMENIGUSA SANA. MIMI BINAFSI NIMEOKOKA TANGU JANUARY 2002. NIMEKUWA NASHINDWA KABISA KUHAMA KANISA KWANI KWA UFAHAMU WANGU NATAMBUA MUNGU NI MMOJA NA WOTE WANAOMWABUDU WANAMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI. KWENDA KWANGU KANISANI ROMA SIJAJUA KAMA NINAKIUKA MASHARITI YA WOKOVU. NA IKIWA KUNA TATIZO NAOMBA SANA MUNGU ANIFUNGUE MACHO YA ROHONI NIWEZE KUKUTANA NAE. NIMEWAHI KUSIKIA WAUMINI WENGI WAKISEMA WAMEKUTANA NA YESU NA AMEWAELEKEZA KANISA LA KWENDA KUABUDU. MIMI MBONA SIJAWAHI KUSIKIA HIYO SAUTI? MARA ZOTE NIMEKUWA NIKIONA KATIKA MAONO NIKIABUDU KANISANI KWANGU. SASA BASI KAMA KUNA SHIDA NAOMBA NISAIDIWE. NAITWA HELEN VUMILIA JINA LA UOKOVU HELEN SARA.

 13. Una sababu gani zimesababisha uabudu mahali hapo?
  1. Imani ya kanisa au kusanyiko hilo wanamuamini na kumuabudu nani
  2. Msingi mkuu wa Imani unaofuatwa – Biblia
  3. Maono ya kusanyiko husika na kama yanafuatwa
  4. Mwenendo wa kusanyiko – kuongozwa na Roho mt, kutadhihirishwa na matunda yaliyodhahiri ktk kusanyiko upendo, utu wema, upole (matunda ya roho) na kama kimwili matunda ya mwilini zinakuwa dhahiri kwa waumini hapo au mitaani au ktk maisha yao.
  5. Ishara na miujiza, kama hamna hata ishara mfano kupokea Roho mt pia ni ishara, kufunguliwa mapepo kwa wanaoamini basi pia ni kitu cha kujiuliza. Ingawa isiwe sababu ya kwanza kwani ishara na miujiza vitafuatana na wote waaminio ikiwapo wewe binafsi kama sivyo basi hata wewe ni tatizo.
  6, Mwisho kuwepo ktk kusanyiko inaweza kuwa hakuna vigezo hivyo vyote au baadhi ila umeongozwa kubaki kwa ajili ya matengenezo, kwa hiyo kuwepo kwako mahali ni muhimu ujiulize wewe pia malengo yako yankutuma kufanya nini hapo, kumbuka mzabibu usofaida unaharibu hata ardhi hivyo utakatwa na kutupwa motoni. Tunajifunza

 14. Asante, kwa swali nzuri, kwanza ni mtazomo wa mapokeo, watu wengi wanakwenda kanisani kwa msisimko tu, awajuwa wawo ni wakinani ndani ya Yesu, na hivyo kupelekea kuandu watu na dini zao.

 15. Kizazi hiki kinatafuta Ishara na Miujiza,lakini hakitapata bali ishara ya Yona

 16. Bwana Yesu asifiwe,
  Kuna sababu nyingi zinazomfanya kila mtu akaabudu kwenye kanisa alilopo. Wengi siku hizi wana sababu za miujiza tofauti na miaka ya nyuma kidogo,siku hizi watu wapo kwenye makanisa kwa sababu kuna miujiza inafanyika hapo.
  Binafsi kinachonifanya niabudu nilipo ni uhuru wa ndani wa kuabudu sio kwaya sio miujiza wala vyombo vya muziki.
  Roho mtakatifu ndio mshauri wa kweli tuliyepewa ni vizuri mtu yeyote kuabudu mahali fulani kwa kuongoza na Roho mtakatifu na sio vitu au miujiza.2kor3:17

  Mungu awabariki

 17. ndugu, usifuate miujiza kanisani, fuata neno la Mungu litakaloweza kukuweka huru, neno ni Yesu mwenyewe, miujiza hukoma ila neno linadumu milele, usiweke imani katika miujiza weka imani katika neno la Mungu, ni nyakati za hatari hizi kuwa macho.

 18. miujiza ni muhimu kanisani ili kuzibitisha andiko la biblia lisemalo,na ishara zitafatana nao waaminio,la kushangaza makanisa mengi hayana miujiza Je? makanisa yote yasiokua na miujiza hawaamini? kwani ni makanisa machache tu ndio wanaombea watu wanapona,na miujiza itokeapo yale makanisa yasio na miujiza, wanalalamika kwamba ni nguvu za giza. Sasa tunataka matendo na sio hadithi na maneno mengi.

  Mbarikiwe wana wa Mungu halisi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s