Mwigizaji Tanzania kufungua kanisa, apata baraka kutoka Nigeria

Mwigizaji na aliyewahi kuwa Mwanamuziki Dotnata Posh, amesema kwa sasa ameokoka kabisa na kuamua kufungua kanisa kubwa lengo likiwa kuwashawishi wasanii wenzake kuachana na maasi na hatimaye kumrudia Mungu.

Dotnata ambaye alianza kwa kufafanua jina lake, alisema watu wengi wamezoea kumwita jina hilo bila kujua msingi wake, kwamba yeye jina lake ni Doto na ameunganisha na jina lake la ubatizo Illuminata ambapo akachukuwa jina la kwanza la Dot na kuunganisha jina la mwisho na nate na kupata Dotnata.

Dotnata anasema aliamua kwenda Nigeria kwa Mtume T.B Joshua ambaye ni maarufu sana Afrika na Dunia nzima, ili kwenda kuchukua baraka kwa ajili ya kuanzisha Kanisa hilo. Alisema baada ya kurudi kutoka Nigeria na kupata baraka hizo za kufungua kanisa, hivi sasa anasomea masomo ya Biblia ili baadae aje kuwa Mchungaji. Kwasasa yeye ni Mama wa Kanisa.

Alizidi kusisitiza kuwa katika Kanisa lake anategemea pia kuwachukua wasanii Ray C na Asha Madinda, ambao nao wameokoka. Mwisho alimalizia kwa kusema Kanisa hilo kwa hivi sasa lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili, ingawa pia limeruhusiwa kuendelea na kazi zake za ibada. Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, kwa sasa kanisa lake litakuwa na wahubiri kutoka Nchi mbalimbali na baada ya hapo ataanza kutoa elimu kwa wasanii waweze kuokoka ili kumrudia Mungu. Dotnata pia amesema kwa sasa hawezi kumlaumu msanii ambaye anafanya mambo ya ajabu ajabu kwakuwa anaamini ni ujana unamsumbua na ukifika muda atabadilika.

source–Bongo Unit.

Wakati huo huo kutoka clouds fm kipindi ya Amplifier na Millard Ayo amesema tayari amesharekodi nyimbo 3 za Injili!

Advertisements

28 thoughts on “Mwigizaji Tanzania kufungua kanisa, apata baraka kutoka Nigeria

 1. Mi napongeza sana Dotinata kwa uamzi wa kubadilisha maisha ya wasanii wenzake. mana wasanii wetu wanafanya mambo ya ajabu ajabu namuombea kila la kheri kwa hatua aliyofikia Mungu ambaliriki sana

 2. Hivi ukianzisha kanisa lazima utangaze mimi naanzisha kanisa? Nijuavyo mimi kuanzisha kanisa siyo kitu cha kukurupukia unaokoka leo kesho unafungua kanisa, kama kuanzisha genge la kuuza nyanya. Ni process ya kiroho ambayo inatokana na wito unaokua taratibu.
  Ushauri wangu kwa dada huyu : Matendo yanaongea kwa sauti kubwa kuliko maneno. Kama kweli amebadilika jamii itaona hakuna haja ya kupiga panda afanye tu matendo yapasayo toba.

 3. Naamini Mungu anaweza kumtumia mtu awaye yote kuhubiri injili, kazi kwako na kwangu sawa na neno la Mungu alikwisha sema zipimeni hizo roho, 1 Yohana 4:1

 4. Ila pia wachangiaji tusichangie kwa kuangalia hiyo picha iliyowekwa hapo juu, tunajuaje kama hiyo picha iliyowekwa ni ya hivi karibuni au kabla ya yeye kutangaza kuokoka?

 5. Tatizo watu wanafikiri kumtumikia Mungu ni kama ulivyo usanii wa Muziki au Kuigiza.Kwa kuwa fulani amepewa kibali kujulikana na watu na kuheshimika kupitia huduma yake aliyopewa na Bwana basi unakuta kesho yake mtu kafungua huduma na anaiga kila kitu. Watumishi wengi huduma zao zinafika sehemu zinakwama haziendi mbele kwa kuwa wanajiita wenyewe na wala sio Mungu aliyewaita,iwe kwa kuiga au kwa kutofuata Muongozo wa Roho mtakatifu. Unakuta inafika sehemu kwa Kuwa huduma imekuwa mzigo kwao wanaanza kuchangisha michango hata kwa staili ambazo kibiblia hazipo… Jamani..! tusione watumishi fulani wamefika hapo walipo, wametoka mbali sana si kirahisi rahisi kama tunavyofikiri… Utumishi kwa Mungu sio kuhubiri tu na kufungua Makanisa. Inawezekana umeitiwa kuwa mfanyabiashara Mkubwa kama akina AYUBU ili uweze kusaidia huduma za Mungu ziende Mbele zaidi kupitia hiyo fedha utakayopewa na Bwana….

 6. Hongera kwa kuokoka,bali ktk swala la uchungaji nakushauri,uwe ktk maombi ya kufunga kwa muda mrefu ili kama,swala hilo limepata kibali liambatane na baraka za Mungu,mana shetani hata ktk sula ya uchungaji anaweza kumtumia mtu blakujua2timotheo2:26

 7. mimi niko nje ya mada naombe mtu anayejua ktk biblia kifungu gani kinasema na asiye fanya kazi na asile na swali la pili nini maana ya fanya upole kiasi na sio sana maana upole kwani nidhambi ikiwa mpole kupita kiasi naombeni jibu wapendwa

 8. Mwigizaji Tanzania kufungua kanisa, apata baraka kutoka Nigeria!

  Amepata baraka kutoka Nigeria. Ni kweli inawezekana kupata baraka mahali mtu alipoziomba, maana hata Jakobo alipopulukushana na malaika wa Bwana alisema hatamwachia hadi atakapombariki-ilikuwa mahali fulani. Angalizo langu ni hili baraka zote za wacha Mungu wake hazitolewi na mwanadamu bali Mungu mwenyewe. Ikiwa Dada huyu atashuhudua ya kwamba baraka hizi amezipata toka kwa Nabii wa TB basi hapo naona kuna upungufu wa NENO la MUNGU. Tena ifahamike ya kwamba watu hawaanzishi makanisa ila wanaanzisha madhehebu. Hapa ni lazima tufafanue nini maana ya Kanisa kama mwili wa Kristo na kanisa (Church) kama jengo la mahali pa kikundi fulani kufanya ibada zao na pia dhehebu (denomination) lina maana gani.. Naomba Dada anifahamishe kama ameanzisha Kanisa au Dhehebu.

 9. ni kweli wasikiaje wasipohubiriwa, lakini ni kwa nini wanahubiriwa zaidi wa mjini tu, kwa nini Nigeria imekuwa kitovu cha kupata nguvu za Mungu?ina maana Mungu yuko huko zaidi ama?sina tatizo na mtu kumtumikia Mungu mana ni jamabo jema nala maana kuliko lolote mtu awezalo fanya, but iwe kwa ajili ya Mungu kweli na sikujitengenezea kivuli kwa mambo binafsi,tuwe macho wapendwa, kila mtu amtafute Mungu kwa nguvu na si kupenda kusimamia miguu ya watu wengine, ni ngumu sana kutofautisha roho wa Mungu na roho ya shetani kama huna roho mtakatifu ndani yako.huo ni mtazamo na mawazo yangu katika kuiendea hii safari ya mbinguni, tujitwike misalaba yetu, tujikane kishe tusonge mbele

 10. Tumuombe Mungu atusaidie, kumtafuta yeye huyu aliyekuwako na aliyeko katika roho na kweli,maana sasa tunakoenda sijakuelewa hata kidogo,maneno tunayo meeengi,lakini matendo ni kidogo. Kama ni wacha Mungu wa kweli ,sioni sababu ya kuanzisha makanisa na tena mijini tu,wakati yaliyopo bado hayajajaa na kuna vijiji hawana sehemu za kuabudia. Tunachotafuta ni nini? USO WA MUNGU au AU MAFANIKIO YA KIDUNIA?

 11. Really??!! Wish her a nice travel in her ambitions. My only advice is that, she makes it quick abandoning the former groups, if she only need 2 persist. God bless her. Good night.

 12. Really??!! Wish her a nice travel in her rissing ambitions. My only advise is 4 her quickly try 2 4get the former world that she belonged b4. God blez her in Jesus name..

 13. Hizo pete na mikufu aliyovaa hazina alama za freemason? Au mimi natazama tofauti?

 14. Sam,

  Mimi ninaongelea jambo ambalo ninalifahamu.

  Ni kweli huyu Dotinata Ameokoka na Ni kweli alikwenda Nigeria.

  Mimi ninabahatika kuwafahamu baadhi ya watu waliokuwa pamoja katika msafara huo.

  Kuanzisha kanisa sio tatizo ikiwa Mungu amemwita. Na mimi sipingi kuanzishwa makanisa. Mungu amesema ombeni Bwana wa Mavuno apeleke watenda kazi kwa kuwa mavuno ni mengi.

  Ni kweli Nabii anaweza kutoa baraka kwa watumishi. Na sina tatizo lolote kama kweli T. B. Joshua ametoa baraka.

  HOJA YANGU NA ANGALIZO LANGU NI KUWA : UMEZUKA MTINDO HATA TANZANIA NA KWINGINEKO WATU KUTEMBELEA KANISA LA SCOAN NA WAKIRUDI WANAKUJA NA UZUSHI.

  WENGI WANADAI WAMETUMWA WAJE KUMWAKILISHA, WENGINE WANADAI WANADAI WAMETABIRIWA UONGOZI, KILA MMOJA NA LAKE.

  NIMEAMUA KUTOKUTAJA MAJINA YA WATUMISHI WALIOFANYA HIVYO KWANI SIO MAADILI (LAKINI MAJINA NINAYO)

  SASA HAKUNA TATIZO LOLOTE KAMA KWELI UMEPATA KIBALI CHA NABII. TENA NI BARAKA. LAKINI IKIWA NI UDANGANYIFU TU NA ULGHAI HIYO SIO SAWA.

  SASA SIJUI SAM ANAONA UBISHI UKO WAPI HAPO?

 15. Ila mbona bado ana mapozi ya kidunia ambayo ni kimtego wa kimahaba wa kuuza sura zaidi kuliko kutangaza Yesu?
  Natoa wito kwa wamiliki wote wa makanisa , tumie alama ya msalaba kwa kulitanga kanisa na sio sura zenu na majina yenu kulitangaza kanisa, Utakuta bango la kuelekeza kanisa lina picha kubwa ya mtumishi halafu kamsalaba kadogo,
  Hizi ndizo baraka zitokazo Nigeria
  Roho Mtakatifu tupe hekima ya kupambanua hizo roho za Nigeria

 16. Mimi Sikuzote kwa uelewa wangu najua baraka anatoa Mungu, kumbe hata TB Joshua anaweza kutoa Baraka kama afanyavyo Mungu. Hapa ndipo ninapochanganyikwaga na hizi habari.

 17. Bwana Asifiwe,

  Sina haja ya kumvunja moyo huyu dada. Lakini kuna walakini fulani hapa. Kwanza siamini T.B. Joshua alisema chochote na huyu dada. Kwa sababu huyu dada alienda Nieria kwenye Kanisa la T. B. Joshua akiwa ameandamanana na watanzania wengine. Ninachokifahamu mimi ni kuwa TB Joshua hakusema chochote na huyu dada kuhusiana na chochote.

  Sasa hivi umezuka mtindo wa “wachungaji” na watumishi mbalimbali kutembelea SCOAN na wakirudi wanakuja na uongo kibao wakitumia jina la Nabii kwa ulaghai. Ninawafahamu kibinafsi watumishi kadhaa waliokuja na uzushi.

  Sasa watanzania tuache “usanii wa kiroho”.

  Kanisa siyo mzaha na shughuli yake ni nzito. Ni vita kali kweli kweli ya kiroho.

  Hilo ni angalizo tu.

 18. BWANA apewe sifa na tunamshukuru Mungu afanyaye anayotaka kwa wakati wake na kwa mwenye anataka; huu wakati wake kwa mama huyu wa Kanisa! Abarikiwe na saana kwa nia hiyo nzuri na safi anayokuwa nayo.

 19. KAZI IPO , YAN SIPATI PICHA MIAK5 AU 10 IJAYO DUNIA ITAKUWAJE////?????
  Eeee///!!!! Mungu Utusaidie….!!!

 20. iwe kweli na sio majivuno au ndio mnaenda kuchukua madawa ya kuangusha watu kanisani kwenu.kuokoka si kama kutafuna kitumbua ujitoe haswa. maana Mungu si wa kumbip; jua kwamba Mungu hapendi mtu wa vuguvugu, ya dunia unayapenda na Mungu unampenda. Ila Mungu awe na wewe kama kweli umeokoka kaza mwendo.

 21. Mungu akubariki umechukua maamuzi yaliyo sahihi, hivyo ndo inavompendeza Bwana,mana wamwabudu watamwabudu Mungu katika roho na kweli. barikiwa kwa sana dada

 22. ubarikiwe dada ni vizuri, kumtumikia Mungu ni vizuri lakini hakikisha amekuita umtumikiye.unasema unataka kua mchungaji safisana.lakini kumbuka biblia inasema katika 1TIMOTHEO 2:12 mwanamke haruhusiwi kuhubiri, nawe wataka kua mchungaji haaaaa labda uwe muimbaji,lakini ni wanawake wengi wamevunja wakisema haki sawa .

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s