Nimerudisha misukule 105 na kuponya wenye Ukimwi 456

SHUHUDA;
Kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu ninafanya kazi mpaka kufikia lengo tulilopewa na YESU kuwa mtafanya makuu kuliko niliyoyafanya mimi.
1. Nimerudisha misukule 105
2. Nimeponya ukimwi watu 456
3. Kansa.
4. Fahamu za watoto shule kurudi.
5. Watumishi kujazwa nguvu ya MUNGU.
6. tasa kupata watoto.
7. Walioibiwa vitu vyao kurudishwa, kukutafutia ndg waliopotea, kwa kweli mambo ni mengi kwa ufupi ni kufundishwa na mwalimu Roho mtakatifu, sasa kubali ufundwe husuje kutafusili biblia kimwili kama unavyoitafsari sasa.

Ikiwa wewe ni mkazi wa Tanga wasiliana nami kwa simu zifuatazo

+255 713 301843

+255 767 301843

+255 786 301843
+255 773 301843

Box 5838
Tanga. Tanzania.

–Mlaka

Advertisements

20 thoughts on “Nimerudisha misukule 105 na kuponya wenye Ukimwi 456

 1. Khaaaa! yaani kama tumefiki hatua hii tunakokwenda si kuzuri kitendo cha kusema… eti..nimerudisha misukule105… eti…nawaongezea watumishi wa Mungu nguvu ninamashaka sana na huyu mtu sina hakika kama ni mtumishi wa MUNGU sijawahi kuona wala kusoma wala kusikia eti mtumishi ana muongezea mtumishi mwenzake nguvu za MUNGU hapa kuna ualakini.

 2. he he he nimerudia kusoma tena hili tangazo, aisee kumbe hata watumishi waende kwake wakapewe nguvu za MUNGU, uwiii jamani ni nini hiki???

 3. biblia inasema nyakati za mwsiho watu watatoa pepo kwa jina langu ila si mimi, manabii wauongo watakuwa wengi, simuhukumu mtu mana si kazi yangu ila wapendwa tuwe macho jamani, tupende kujiombea zaidi kuliko kuombewa, kuomba hakuna mwenyewe mana biblia inasema ombeni nanyi mtapewa

 4. Mhh! Hilo tangazo halijakaa sawa:

  1. Limejaa na kufurika kiburi cha hali ya juu!
  2. Tunda la Roho limeadimika kabisa hapo
  3. Msisitizo umewekwa kwenye mahitaji na mafanikio ya kimwili, Injili ya wokovu haipo hapo
  4. Roho Mtakatifu atamtukuza Bwana Yesu na siyo bwana au bibi mtumishi. Tangazo hili linamsifia na kumpamba huyo mtumishi

  Wapendwa, tujifunze Neno la Mungu, ili tuweze kuijua sauti ya Roho Mtakatifu, tusijeyumbishwa na watumishi kama hawa na matangazo yao yenye lengo la kuwafanya watu wawafuate, wawanyenyekee na kuwaona wao kama ndio suluhisho la matatizo yao yote.

  Kama umeokoka unaye Roho Mtakatifu yule yule aliyeko ndani ya wahubiri mashuhuri, hakuna Roho Mtakatifu 1st Class, 2nd Class au 3rd Class, ni Roho Mtakatifu yuleyule, tusikubali kudanganyika.

 5. Hakuna aliye rogwa ila kauli yake inajitambulisha kuwa yeye aweza kufanya iwapo amesema amewezeshwa na Roho Mtakatifu 1) Nimerudisha misukule 105
  2. Nimeponya ukimwi watu 456
  Kumbuka hapa kuna umimi neno nime inamaana ni yeye vinginevyo halafu lipo kama tangazo la kuaguliwa. Kwa hiyo basi kama anaongozwa na Huyu Roho Mtakatifu basi na amtangulize yeye asijipe utukufu kuwa nimeponya nimerudisha nakadhalika hatuhukumu lakini kauli yake/yetu na maandishi yake/yetu yatupasa kabla hatujachukua hatua tuyaaangalie kwanza ili kuondoa mashaka kwa wengine ili kazi ya Mungu iweze kusonga mbele pasipokuwa na dosari yeyote.

 6. wapendwa bwana. Sasa ni nani afadhali? huyu ama yale matangazo ya waganga tunayoona barabarani. Acha watu waende wataishia kwa Yesu kuliko kupotelea kwa shetani. we si umeona anasema anamsikiliza Roho Mtakatifu na huduma amepewa na Yesu? enyi kizazi cha waebrania ni nani aliyewaroga? wabishi kuamini miujiza

 7. Ahhh!!!!!!! kweli kizazi hiki kizazi za uovu hebu wapendwa tupende kuwa wadadisi wa mambo na na kumsikiza Roho Mtakatifu anasema nini juu ya maisha yetu na siyo Roho Mtakavitu . Halafu kujua Neno la Mungu ndiyo muujiza wako ebu ifike kipindi tuchunguzen na kijifunza maandiko kwa sana ili shetani asije akatupepeta kama ngano akitupeleka huku na huku na mwishowe kujikuta ukitumikana na miujiza ya watu wanaoponywa na kuamsha mishukule jamani tuwe macho, haya mambo siyo ya mchezo tusije tukatekwa huko kwenye kuamshwa mishukule na kuponywa, tuangalie neno ndiyo uzima wetu. Na huku kujisifu kumetoka wapi? iwapo kama Mungu Ndiye Mponyaji ni kwa nini asimfudishie sifa na utukufu Mungu alitenda mambo hayo na kusema nimeponya. Navunja kila Miguu inayokimbilia miujiza bila kutafakari inatoka kwa nani katika Jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. chapeni mwendo kwa yenu siyo kwenye miujiza wapendwa.
  betty kipala

 8. BWANA YESU asifiwe wapendwa.Kwa upande wangu ninaungana na wote wanaoonyesha wasiwasi na huduma ya huyu mpendwa.Unajua siku hizi wapendwa ,watu wamejipa nafasi ya Yohova mwenyewe.Kusema nimeponya,nimewarudisha…….Nime….Kuna walakini wapendwa.Roho hizi za kujitukuza hata kama uwezo huo umetoka kwa MUngu ,tayari kuna tatizo hapo wapendwa wangu.Kumbu roho ya aina hii ilimgarimu hata MUSA mwenyewe.
  Pili wakristo tunapaswa na kujihadhari na roho za makristo yanayotokea humu ulimwenguni(WANADAMU WANAOJIPA SIFA KAMA YA KRISTO MWENYEWE) Kwani hayamtukuzi MUNGU kama yenyewe yanavyosema bali yanaujenga ufalme wa ulimwengu huu ambao ukisoma katika biblia ,huo ufalme ni wa shetani.
  Wapendwa tuwe waangalifu sana .Kuliko hata mwanzo kwani NYAKATI HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO(hatari)
  AHSANTENI SANA WAPENDWA WANGU.AMINA

 9. huyu mtumishi anayeponya wagonjwa na kurudisha misukule yuko wapi upande huu kuna shida nyingi nguvu za kienyeji zimezidia watu wa huku hawana tumaini wanakata tamaa kwa nini yeye awe huko tu wakati huku hakuna miujiza kama hiyo. mimi niko Geita

 10. Chonde chonde SG,hii kitu haijakaa vizuri. Ushuhuda haueleweki ni nani anayeutoa na anautoa ili iweje..

  Kwa kifupi hayo maelezo hapo juu sijaelewa yanataka sisi wana blog tufanye nini. “Nimerudisha misukule 105″… so what?

  Binafsi sijapenda ilivyokaa kwa sababu linaweza likawa ni tangazo la uganga wa kienyeji, na kwa sababu watu wenye misiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo pia wanasoma hii blog,wanaweza wakaamua kwenda kwa sababu wako ‘desparate’, kumbe tunawapeleka kwa mganga wa kienyeji.

  Samahanini kama huyo mtu kweli ni mtumishi wa Mungu, maelezo mlivyoyaweka siyo sawa ndio maana tunasema hivyo

  Vinginevyo kama mmeiweka hivyo kwa makusudi fulani, hapo nitawaelewa!

  Bless u!!

 11. Yaliyotabiriwa sasa yanatimia! Shika sana ulicho nacho asije mwovu akakunyang’anya! Mungu atusaidie kwa kweli!

 12. we must be care ma friends whom this person if is holy spirt do this why she or he announce it ?

 13. Shalom wapendwa
  mimi sijali wamefunguliwa wangapi ila sifa iende kwa Mungu, pia ushuhuda ulipaswa kutolewa na wengine na si wewe, Mtu anayejitwalia utukufu wa Mungu ninapata wasiwasi na anaponya kupitia nani? Kupata karama na kipawa ni kuwa imara na Roho mt sasa kama huko vizuri naye sijui hiki kipawa ni cha nani? wapendwa tuzijaribu Roho labda awe mtu mwingine ndio kaja kumwekea tangazo ana uelewa mdogo ili kama ni yeye anayehudumu…..

 14. nimeshangazwa sana na watu mnaocomment kusema huyo ni Yesu au huyo ni roho mt. Mimi naona kizazi cha sasa wachotaka kuona ni miujiza tu bila kupima! hebu someni hayo maelezo ya huyo jamaa halafu jiulize maswali kabla hujaamini au kukubaliana nayo. kwanza anasema NIMErudisha misukule (yesu hakurudisha misukule Yesu alifufua wafu) pili anasema NIMEponya ukimwi (angalia hapo utukufu unaotafutwa ni wa nani) halafu ukishaona mtumishi yeyote anaipigia debe huduma yake pamoja na kutoa namba za simu lazima kuna shida mahali. (watu wa Mungu acheni fimbo ya haruni ichipue yenyewe!) nachomaanisha ni hiki kama Mungu amekuwekea kitu ndani yako huitaji kujitangaza wala kutoa namba za simu watu wenyewe watatakuja kutoka mashariki,kaskazini,kusini,magharibi kutokana na kile ambacho mungu atakuwa anafanya kupitia wewe!! watu wenyewe watasimuliana yale ambayo mungu ametenda kupitia wewe! acha niishie hapo ila kwa huyu mtumishi aliyepost huo ushuhuda nina wasiwasi na huduma hiyo maana the way umeitangaza ni kama waganga wa kienyeji wanavyojitangaza! samahani kama nitakuwa nimekosea!

 15. Wapendwa,

  Hii ni nini tena? Kwanza hii lugha ya “Nimerudisha au Nimeponya”, ni lugha ya mtu wa Mungu kweli? Huyu ndugu anaponya na kurudisha misukule kwa uwezo wake? Je, amesahau Yesu alivyosema ‘bila mimi ninyi hamwezi lolote” au amesahau ule mstari wa Waefeso 3:20?

  Kwangu mimi hapa pana utata mkubwa!! Misukule 105 Tanga peke yake??? Je baada ya kuirudisha hiyo misukule ameihubiria Habari Njema za wokovu ili wasimame imara katika Bwana wasichukuliwe misukule tena? Na je misukule yote hiyo kabla ya kuchukuliwa kuwa misukule ilikuwa katika imani au niseme dini gani? Na je baada ya kurudishwa tena wamesimama katika imani gani? Wameokoka? Bila huyu ndugu kunijibu maswali hayo mafupi, bado naweza kusema kama wengine walivyosema hapo juu, huu ni uganga wa kienyeji tu!!! Hakuna tofauti na wapiga ramli.

  Na kwa jinsi wakristo wa majina walivyo wengi watamiminika kwenda Tanga kumuona huyu ndugu na kutaka ndugu zao waliokufa warudishwe, lakini nasema OLE WENU WENU MSIPOZITAMBUA ROHO ZITENDAZO KAZI KATIKA KIZAZI HIKI.

 16. Nimesikia maelezo yako. Umetoa address kwa watu wa Tanga Je watu wa mikoani wao huwezi kuwasaidia?

 17. Yes, hizo ni kazi za Roho Ttakatifu ambazo ni karama za rohoni,tumepata bure utukufu kwa Bwana tunamrudishia yeye,tusijifu kwa kutoa pepo bali tufurahi kwa kuwa majina yetu yameandikwa mbinguni

  Asante mtumishi kwa kuifanya kazi ya Mungu aliyokutuma,kuwatoa watu waliosetwa na shetani,na kudumu ktk maombi na Neno ili majina yao yaandikwe ktk kitabu cha uzima

  amen!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s