Ntaitambuaje Huduma yangu?

Bwana apewe sifa mimi ni kijana napenda kuuliza je ntatambuaje huduma yangu? na ntawezaje kuikuza na nini tofauti kati ya mwalimu na mwinjilisti na tofaut ya karama ya unabii na kupambanua roho? Ningependa kujibiwa kwa umakini

–Mwaijumba Baraka

Advertisements

12 thoughts on “Ntaitambuaje Huduma yangu?

 1. Bwana Yesu apewe sifa Ndg. dj shakur alicho ongea dada Anna kuhusu kulipia gharama juu ya huduma fulan uliyo nayo (alimanisha hivi) kuwa tayari kwa mapito mbalimbali atayokupisha Mungu (mapito kwa lugha nyingine huitwa shida,taabu ilikukufanya kuwa imara ktk hiyo huduma yako mf. Daudi kabla ya kupambana na Goliath ilibidi Kwanza apambane na dubu na simba akiwa anachunga kondo za mzee Yese

  pia kulipa gharama (mapito) mtu anakuwa mnyenyekevu kiburi hakuna mtu wa kunyenyekea mbele za Bwana YESU.kila ufanyalo utaona hukustahili isipokuwa ni kwa neema tu

 2. du!! nimependa xana namna ambavyo watumishi mmechangia of course nimepata kitu kipya mbarikiwe xana

 3. nimependa sana namna ambavyo mtumishi wa MUNGU lusajo amecoment crear but short

 4. HI HAMU ZURI ULIYO NAYO LAKIN ANGALIZO KATIKA KUTAKA KWAKO NI USITAKE UTUKUFU KWA MWANADAMU ILA PALE HUDUMA YAKO INAPO KUWA MRUDISHIE MUNGU UTUKUFU HUNA BUDI KUPUNGUA ILA KRISTO AINULIWE NDANI YAKO, KAMA KWA MAOMBI KWA MUDA MUREFU
  AHSANTE
  BARIKIWA

 5. Amina watu wa mungu nimejfunza meng sana. mungu awabarki.kwel kuitambua karama yako panahij juhud na hamu ya mambo ya mungu unapo zd kuyafanya ndipo mungu anazd kukufunulia . kuijua karama inahitjn uwe na mambo yafuatayo 1 uwe muombaji 2kupenda kusoma neno la mungu kwa bdii.3 kufanya ibada na kla kaz ya mungu uipende na kuiombea.ndipo roho atazd kujifunua kwako na utakuwa msaada kwa wengne. na ustake karama kwajr ya kutaka umaarufu, au sfa ila. karama yako na i2mike kwa utukufu wa mungu il mungu atukuzwe kuptia hyo huduma au karama yako.unapo zd kufanya hvyo roho mtatfu aweza kusema nawe kukuambia karama au huduma yako au kuptia wa2 wengne.au utapata msukumo wa jambo furan kama kuhubr nk. ndpo inakupasa kumwomba mungu akufunulia jns ya kui2mia hiyo karama kwa mpenz yake na kwa utukufun wake.kwa kadr unazd kui2mia ndpo inazd kukua haiwwez kukua kama umekaa 2 na kusubr ikue.soma neno omba kwa bdii kuwa mnyenyekevu isaya 66 ;1-2 mungu atakukuza ktk huduma sawa na mapenz yake. bwana awabark kwa mchango wenu. namshukuru mungu

 6. Bwana Yesu asifiwe, pia hata mimi naomba kunitumia copy ya majibu ya kutambua kipaji changu, na zaidi ya yote nimeteuliwa kuwa kwenye kamati ya maombi kanisani so hadi leo sijapata maamuzi sahihi.

  ________________________________

 7. Kuifahamu huduma Mungu aliyoweka ndani yako siyo jambo gumu. Kwanza kabisa utakuwa na shauku ya kumtumikia Mungu katika huduma fulani maalum, ila hiyo haitoshi maana huduma anazitoa yeye Roho Mtakatifu kama apendavyo mwenyewe. Hiivyo kuwa na shauku ni hatua ya kwanza, pia uwe tayari kuchukua hatua ya imani na kuanza kumtumikia Mungu kwa vipawa alivyokujalia mahali hapohapo ulipo, kama ni kusaidia wengine, kutembelea wafungwa na wagonjwa au watoto yatima, kama ni kuimba au kufundisha Sunday School, kama ni kwenda nyumba kwa nyumba kushuhudia n.k, Kwa maneno mengine labda nitumie mfano huu, usitegemee utaanzia kwenye uinjilisti wa kimataifa wakati hujaweza hata kumshuhudia mtu mmoja.

  Vilevile kama walivyotangulia kusema wengine jifunze kwa waliokutangulia. Cha msingi sana ni wewe kuwa mwaminifu kulitii Neno la Mungu katika maisha yako na katika kumtumikia Mungu kila upatapo fursa bila kujali hadhi, yaani bila kujali kama unachofanya kihuduma kinatambulika au kinapendwa au kinashabikiwa na wengi au wachache. Ukiendelea kuwa mwaminifu, taratibu utagundua unaanza kutumiwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu zaidi kwenye huduma fulani kuliko zingine na matunda unayaona. Wengine watayaona matunda ya huduma yako na kuthibitisha kuwa neema ya huduma fulani ipo ndani yako na Mungu ataendelea kukufungulia milango ili uweze kuendelea kufanyika baraka kwa watu wengi zaidi kwa ajili ya utukufu wake..

  Tafadhali tumia muda mzuri usome na kisha utafakari Warumi 12 na 1 Wakorintho 12. Ubarikiwe na Bwana Yesu!

 8. Anna kweli unatuchanganya kidogo hapo juu umemalizia kusema huduma kuna gharama ya kuikuza n akuitunza eti wengi wapenda vya bure,Mambo ya Mungu yote ni bure Yesu alishalipa deni letu, hivi sasa kuna matapeli wana waibia watu kupitia jina la Yesu, wao huwaomba watu pesa ili kuwaombea baraka, naukitaka kuongea na Mungu lazima utowe pesa.

 9. Huduma Mungu anagawa kama apendavyo kwa Utukufu wake. Ukitaka kujua huduma yako usiwe na haraka tulia omba Mungu akufunulie pia uwe msomaji wa Neno la Mungu, ili hduma yako ikifanya kazi iwe na nguvu ya Mungu. Huduma kuna gharama ya kuikuza na kuitunza. Wengi wanapenda vya bure.

 10. Mungu baba wa wote akubariki ndugu mpendwa kutaka kujua mengi hayo yenye hekima na busara, ilikujua huduma yako ni lazima umpate mtumishi wa Mungu wa kweli nabii, atakwambia,nakuhusu mambo ya karama unabii na mengineyo, yote hayo ni kazi za Roho Mtakatifu,yeye ndiye awezaye kukupa majib ukamili.,nakumpata Roho Mtakatifu hapo ndio kazi,wengi husema mtu akiamini na kubatizwa atampata ni wengi kama 95% wamebatizwa lakini hawana,nafikiri Mungu hufanya apendavyo na humpa apendaye.

 11. Nimepatwa na mshtuko kusikia unataka kujibiwa kwa makini, sijajua umakini unaouongelea ni upi…Labda nianze kwa kusema….1.Huduma zote ni za Roho Mtakatifu so ukitaka kufahamu anataka kukutumia katika huduma fulani uwe na uhusiano mkubwa sana na Roho Mtakatifu yeye ukijiachia kwake taratibu atajifungua. 2. Huwezi Kuna namna nyingi za kuikuza, njia mojawapo ni kusikiliza Roho anachotaka Njia ya pili ni Unyenyekevu wengi wetu wanapoteza huduma sababu ya kiburi njia nyingine ni kujifunza kwa waliokutagulia (experience sharingi). Tofauti ya Mwalimu na Mwinjilisti sidhani kama ni tatizo sana inajulikana, Mwalimu anakazi ya kufundisha neno la Mungu Kupitia Karama hiyo, Mwinjilisti kazi yake ni kuleta watu kwa Yesu, na Wakisha kuja Mwalimu ndio anawakuza

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s