“Usimuongelee mabaya Mchungaji wako kwenye Facebook au Twitter Utalaaniwa” – Pastor Creflo Dollar

Pastor Creflo Dollar akielezea jinsi ya kuheshimu mamlaka za kiroho

You teamed up with the world and the devil, and became an accuser of the brethren… and what it could have accomplished won’t be accomplished anymore because you joined the Twitter and Facebook crowd to dishonor spiritual authority ~ Pastor Creflo Dollar.

Swali; kutokana na maneno hayo, Je ni sahihi wakristo kunyamaza kuhusu watumishi wa Mungu?

Msikilize hapa

Advertisements

5 thoughts on ““Usimuongelee mabaya Mchungaji wako kwenye Facebook au Twitter Utalaaniwa” – Pastor Creflo Dollar

 1. ningependa kujua tufauti ya kumuongelea vibaya na kumkosoa mtumishi wa Mungu. Je Biblia inaruhusu kuwakosoa watumishi wa Mungu?

 2. haina tija yoyote kumjadili mtu awe mchungaji au kiongozi yeyote kupitia facebook kwani kuna wengine hawapo fb so nivigumu kumfikia mhusika ujumbe ili abadilike na kuacha mabaya yake, kilichopo ni kama unamfaham mfate mweleze udhaifu wake, kama ni wakubadilika atabadilika kuliko kuteta ubaya wake, nihayo yangu tu.

 3. Nini maana ya kumwongelea mtu mabaya?

  Siyo mchungaji tu,hata kama unamwongelea mtu wa kawaida tu, ni vizuri kumwongelea kwa staha. Ndio maana ya ukristo.

 4. Shalom
  na mimi mwanzo nilifikiri kuongea juu ya watumishi wa Mungu kwenye mitandao ni njia ya kuwafikia na pengine kubadilika, lakini sasa nimegundua sio wote wanasoma mitandao kwa hivyo basi ni kosa kuwaongelea humu wakati hawasomi wala kujitetea.
  Ikiwa mtumishi wa Mungu anamapungufu ni bora umwambie wazi yeye mwenyewe, au kwa simu au email yake, tukumbuke hawa ni binadamu pia, tukumbuke shetani anawawinda na wanahitaji maombi yetu, tukumbuke kuanguka kwa mchungaji ndio mwanzo wa kupotea kundi.
  Sijawahi kusikia mtumishi ambaye anatoa mahubiri yake na kutolea mfano wa waumini wake kwa majina walionguka na kutubu, mara nyingi waumini kuanguka na kutubu huongelewa ktk vikao vya ndani vya viongozi watupu labda muumini mwenyewe aamue kutubu mbele ya kanisa.
  Wakati tukikabiliana na vita huku na kule juu ya kanisa ni bora tukawa kitu kimoja tukiombeana, kuonyana na kufundishana na kusaidiana, makosa tuambiane wazi sio kwa magazeti, mitandao, TV au radio na kusababisha kondoo kukosa mwelekeo maana hawajui washike lipi.
  Kitu cha msingi tuhubiri neno kwa ufasaha na uongozi wa Roho mt, tukemee maovu kama yalivyo, watu waliohubiriwa neno sawa sawa likawa jaa ndani yao hawawezi kupotoshwa na mafundisho ya uwongo wala watumishi wa uwongo. Kanisa litakua na injili kuenea kama tutakuwa na upendo wa kweli kati yetu na sio mashindano na majibizano yasiyoisha. Tuihubiri injili wapendwa!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s