Uganda yalegeza kamba, Yaondoa adhabu ya kifo kwa mashoga

Bunge la Uganda limeshindwa kupitisha sheria ya kuua watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja(ushoga) kama ilivyoahidiwa na spika wa bunge la nchi hiyo Rebecca Kadaga na badala yake bunge hilo limejikita katika kufanyia marekebisho muswada huo kwakutafuta tiba mbadala kabla ya kuisha kwa mwaka, ikiwa ni tofauti na spika huyo alipoongea na vyombo vya habari wiki mbili zilizopita alipoahidi kwamba sheria hiyo itapitishwa kabla ya kuisha kwa mwaka huu.

Lakini amerejea tena katika vyombo vya habari ijumaa iliyopita akisema kwamba hawatapitisha sheria hiyo kwasasa mpaka hapo baadaye akidai kwamba wametoa zawadi ya Christmas kwa mawaikili wa watu wanaojihusisha na vitendo vya kishoga akidai kwamba wamekuwa katika kampeni kwa muda mrefu ya kupinga sheria kali za serikali ya Uganda dhidi ya matendo ya ushoga.

Uganda ni kati ya nchi za kiafrika ambazo zina msimamo mkali juu ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, awali kwa upande wa bwana James Nsaba Buturo ambaye ni waziri mstaafu wa maadili wa serikali na kiongozi wa umoja wa maendeleo ya maadili nchini humo amesema hakuna maswali juu ya hilo anauhakika wa asilimia 99 kwamba muswada huo utapitishwa na kuwa sheria kamili.

Amesema kama kuna kiongozi yeyote nchini humo ambaye anayeonea huruma mambo ya ushoga hawezi kuthubutu kusema hadharani kwakuwa anajua waganda hawataki utamaduni huo katika nchi yao.Uganda imebakia na msimamo dhabiti juu ya vitendo vya kishoga nchini humo licha ya kelele nyingi kutoka mataifa ya magharibi ambao wameonekana kuzitishia nchi zitakazokataa maswala ya ushoga zitanyimwa misaada hali iliyofanya nchi kama Malawi kulegeza kamba juu ya vitendo vya kishoga.

christian post

Advertisements

2 thoughts on “Uganda yalegeza kamba, Yaondoa adhabu ya kifo kwa mashoga

  1. Yani Mimi Napenda Kushauri Hebu Tuikatae Misaada Ya Uzalilishaji Kama Huo! Wapendwa Mungu Hata Tuacha! Tufe Kwa Njaa Hakika Tutasimama! Ila Tukionekana Kuwa Vuguvugu Ni Kweli Tutashindwa Maandiko Yanasema IMETUPASA KUMTII MUNGU KULIKO WANADAMU!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s