Unampenda mtumishi gani kwenye biblia na kwanini?

Kitabu cha Biblia kuna watumishi wengi ambao kwa hao tunajifunza na kupata mifano mbali mbali, kuna watumishi waliokuwa imara, wadhaifu, walioshindwa, walioshinda nk.

Sasa ninalo swali kwa wasomaji wa Biblia, unampenda mtumishi yupi? na kwanini?

Advertisements

7 thoughts on “Unampenda mtumishi gani kwenye biblia na kwanini?

 1. NAMPENDA MFALME DAUDI,
  KWA SABABU HATA ALPO MKOSEA MUNGU ALIKUMBUKA KUTUBU TENA KWA KUAMANISHA.
  PIA ALIKUA JASIRI HAKUPENDA JINA LA BABA MUNGU LITUKANWE, ALIKUA TAYARI KUPIGANA KAMA ALIVO FANYA KWA KUMPIGA GOLIATI

 2. MIMI NADHANI WOTE NI WAZURI,JAPOKUWA YUPO YUDA ALIE FANYA VIBAYA SANA,LAKINI SIWEZIKUMCHUKIA YUDA KWASABABU ILIKUWA NIMPANGO WA MUNGU YESU MOKOZI WETU AFE,LAKINI PAURO NNAMPENDA ZAIDI KWASABABU ALIKUWA NA MSIMAMO WA KILE ALICHO KIAMINI.

 3. Nampenda mno Hezekia, nikibarikiwa nakienda mbinguni nitataka nionane nae, maana nadhani nafanana nae, ni binadamu kabisa, kama mimi.
  Akipata majaribu anakimbilia kwa mungu, maana ndio kimbilio lake hakuwa na kimbilio lingine, alilia, aliomba, alinyenyekea, alilalamika, na mungu alimpa hitaji lake akamuondolea majaribi yake, mara zote alipomkimbilia.
  Alipoletewa barua na mfalme aliyetaka kuleta vita nchini kwake, alienda chumbani akamsomea barua mungu, akaomba, na mungu akamjibu (2 WAF 19: 14 -20 ). alipougua nabii akamwambia atakufa, alilia, akaomba, akamkumbusha mungu fadhili zake, mungu akaghairi, akamuongezea maisha. Hezekia alikuwwa pia na matatizo, kama binadamu wa kawaida, aliwakaribisha watu waliokuja kumpa pole na akawaonyesha kila kitu, ila hakuwashuhudia jinsi alivyopata uponyaji, hivyo Isaya akamwambia, angalia vyote ulivyoonyesha vitachukuliwa, hakuna kitakachobaki. Nadhani alitubu baada ya hayo, biblia inasema alitenda yale yote mema mbele ya mungu.

  ndio maana nampenda, kuna wakati mimi kama niliyeokoka, nakosea bila kujua au kukusudia, na mungu anayenipenda ananihurumia na kunisamehe, na nikipata jaribu nikimuomba, ananijibu haraka.
  greta

 4. Bwana Yesu asifiwe…nampenda Ayubu maana aliweza kushinda majaribu ambayo shetani alidhani hangeweza kuyashinda…Pia Ayubu ni mfano mzuri ya kuwa hata ukiwa karibu ya Mungu unajaribiwa…
  Mbarikiwe sana.

 5. Mimi ninampenda sana Stefano kwa ajili ya ujasiri wake. Hakuogopa kudhuriwa wakati akikemea matendo maovu hata alipoona sasa anauwawa aliendelea tu kuwakemea. ananitia nguvu na ujasiri wa ajabu katika kumtumika Bwana. Tunatakiwa kuwa wajasiri, tusiogope kitu gani kitatukuta.QAmin

 6. Ibrahim! baba wa Imani
  1. Ile kutoka ktk watu wake nakuiendea nchi asiyoijua inanipa nguvu sana nami ninapokutana na vikwazo ktk wokovu
  2. Imani yake kuu ktk ahadi ya kuwa atafanywa taifa kubwa uzeeni huku hana mtoto ni mfano mzuri kwa familia imara
  3. Kutoa kwake Isaka wakati ndiyo mtoto pekee aliyepewa uzeeni ni mfano mzuri ktk kutoa wengi wetu tunang’ang’ania tuvitu tudogo tusito thamani, tunashindwa kumtolea Mungu tukiona tunapoteza, lakini aliinua kisu juu ya Isaka tayari kumtoa dhabihu…
  4. Hakuona aibu au woga kumuombea Luthu nduguye hadi Mungu akamnusuru na moto wa Sodoma na Gomora, ni mfano mzuri ktk kusimama kama kuhani kwa ajili ya wengine
  5. Alikuwa tayari kwa matengenezo alipokosea kwa kuzaa na Hajiri, alikubali kuwaondoa nyumbani mwake na mwanae Ishmael kutii maagizo ya Mungu.
  Imani yake kuu ninaipenda sana pamoja na utii na vile Mungu alivyomteua na yeye kuenenda ktk njia hadi kuwa mtu mkuu maisha yake yote na kizazi chake kupokea ahadi alizoahidiwa. Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s