Kanisa la Leo na Utakatifu

utakatifu

Unawaza nini kuhusu kanisa la leo? kumekuwa na habari za michanganyo/vuguvugu pia kuna wengine wanasema kanisa la kisasa na la kizamani. Una mtazamo gani juu ya kulinda Utakatifu?

Advertisements

14 thoughts on “Kanisa la Leo na Utakatifu

 1. Ndugu zangu wapendwa nawasalimu katika jina la BWANA,kwanza natoa angalizo,wengi tumesema mengi,kuhusu kanisa,kuhusu kuokoka,ninachoomba tukumbuke Yesu alisema:kila neno lisilo na maana atakalo linena mwanadamu atatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu,kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa(matayo 12:36-38) ,Roho Mtakatifu kupitia Mtume Paulo akatuambia,Neno la Mungu lina sema,nastaajabu kwa kua mnamuacha upesi hivi yeye aliewaita katika neema ya kristo na kugeukia injili ya namna nyingine………,ijapo kuwa sisi au malaika wa mbinguni akiwa hubiria injili ya namna nyingine na ALANIWE…..(wagalatia 1:6-9)..bado neno la Mungu lina sema Msiwe walimu wengi,maana hukumu yenu itakuwa kubwa zaidi(yakobo 3:1).sasa Kanisa nini? neno kanisa limetokana na neno la kigiriki (ekklasia)yaani wale walioitwa kutoka katika nguvu za giza na kuingia katika ufalme wa mwana wa Mungu.yaani wale wqliokubali kuwachaa dhambi,na kukubali kufanya yalio mapenzi ya Mungu.
  Je watu watazidishwa je katika kanisa hili? ukisoma katika kitabu cha mwanzo (mwa 28:10-12),yakobo aliota ngazi imesimamisshwa kutoka duniani mpaka mbinguni,na malaika wa Mungu wanapanda nakushuka juu yake.je hiyo ngazi nini?
  jibu ukisoma katika( yohana 1:51) jibu ni YESU KRISTO.Sasa ngazi inahatua je hatua hizo za ngazi ni zipi mimi nipande kwenda mbinguni? yesu anatuonyesha moja baada ya ingine:
  1:SIKIA INJILI YAANI UFUNDISHE NENO LA MUNGU(ROM 10;17)
  2:MWAMINI YESU KUWA BWANA NA MWAKOZI WA MAISHA YAKO (YOHANA 6:40)
  3:TUBU DHAMBI ZAKO.(MATENDO 2:37-38)
  4:MKIRI YESU KRISTO MBELE ZA WATU( WARUMI 10:9-10)
  5:UBATIZWE,baada ya ubatizo sasa dhambi zako zimeoshwa,umeokoka sasa(matendo 2;41)
  6:MUNGU ANAKUZIDISHA KWENYE KANISA LAKE (Matendo 2;47
  SWALI JE KANISA HILO NI LIPI?NAOMBA JIBU KIMAANDIKO…….

 2. Ndugu zangu wapendwa Mabinza na Tunkuh, nawasalimu katika jina la Yesu mwokozi wetu. Nashukuru Mungu ametupatia nafasi katika Blog hii ili tuweze kujifunza, kila mmoja mwenye kitu analeta, kila mwenye fundisho analeta, hii ndiyo inaitwa chuma hunoa chuma. Mimi napenda sana kujifunza kwa kuwa sijui yote, na sitajua yote mpaka Yesu arudi, 1kor 8.2 Mtu akidhani kuwa anajua neno, hajui neno lolote bado,kama impasavyokujua. Ebu nieleze kidogo mimi ninavyojua kidogo kuhusu IMANI na MATENDO. Najua kuna Matendo ya aina mbili. 1.matendo kabla ya kuokoka. Na 2. Matendo baada ya kuokoka. Matendo kabla ya kuokoka hayo kwa Mungu ni sufuri, maana huwa mtu huyo ni mwenye dhambi na Mungu hawasikii wenye dhambi. Yoh 9.31 Twajua kuwa Mungu hawasikíi wenye dhambi, bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.( hapo tunaona kumbe unaweza ukawa mcha Mungu ila usiyafanye mapenzi ya Mungu) na ndiyo maana Yak 4.17 Basi yeye ajuaye kvenda mema ,wala hayatendi kwake huyo ni dhambi. Ninakubaliana kabisa kuwa ili Mtu aokoke anachaguliwa na Mungu Yoh 15.16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi, NAMI NIKAWAWEKA MWENDE MKAZAE MATUNDA.

  NA MATUNDA YENU YAPATE KUKAA, Ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. Nimesema kuna matendo ya aina mbil, KABLA YA WOKOVU na BAADA ya wokovu. Nikasema matendo kabla ya wokovu ni kweli ni sufuri, lakini Matendo baada ya Wokovu haiwezi kuwa sufuri, Mungu anayataka sana. Yak 2.14…26. Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo Imani, lakini hana matendo? Je Ile Imani yaweza kumuokoa? Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwanu akawaambia, enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? Vivyo hivyo na Imani isipokuwa ina matendo imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo, Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuönyesha Imani yangu kwa njia ya matendo yangu. Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja, watenda vema. Mashetani nao wanaamini na Kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewd mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? Je baba yetu Ibrahim hakuhesabiwa haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? Waöna kwamba Imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba Imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahim alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki, naye aliitwa rafiki wa Mungu. Mwaona kwamba mwanada huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake, si kwa imani peke yake. Ninachoelezea ni Matendo yetu baada ya kuokolewa, kuchaguliwa. Yoh 13.17 Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda( yapi) yale tunayofundishwa, yale Yesu aliyoyaagiza kwenye Neno lake. Mahali pengine akawaambia KWA NINI MNANIITA BWANA BWANA NA HAMTENDI NIWAAMURUYO? 2 pt 1.3…11. Kwa kuwa uweza wake wa uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe, tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya uungu mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. NAAM NA KWA SABABU HIYO MKIJITAHIDI SANA KWA UPANDE WENU, KATIKA IMANI YENU TIENI NA WEMA, NA KATIKA WEMA WENU MAARIFA, NA KATIKA MAARIFA YENU KIASI, NA KATIKA KIASI CHENU SABURI NA KATIKA SABURI YENU UTAUWA NA KTK UTAUWA WENU UPENDANO WA NDUGU NA KATIKA UPENDANO WA NDUGU UPENDO. Maana mambø hayo yakiwa kwenu na kujaa tele yawafanya ninyi kuwa si wavivu, wala si watu wasio na matunda kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo

  Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani. KWA HIYO NDUGU JITAHIDINI ZAIDI KUFANYA IMARA KUITWA KWENU NA UTEULE WANU. MAANA MKITENDA HAYO HAMTAJIKWAA KAMWE. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika Ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo. Iyoh 5.18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu HUJILINDA wala yule mwovu hamgusi. 1Yoh 3.18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, BALI KWA TENDO NA KWELI. Tunaendelea kujifunza kuhusu Matendo baada ya Kuokoka, kuchaguliwa, Math 7..24…27 Kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile isianguke, kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga, mvua ikanyesha, mafuriko yakaja , pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka, nalo anguko lake likawa kubwa. Maisha tunayoishi baada ya kuokoka kwetu tunajenga kila siku tunapolisikia Neno, na siku inakuja kazi hizo zitapimwa, kwa nini zipimwe?.

  Kwa kuwa yafunuliwa katika moto, na ule moto wenyewe utaijaribu KAZI ya kila mtu, ni ya namna gani, KAZI ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata dhawabu, KAZI ya mtu ikiteketea ATAPATA HASARA. Ila yeye ataokolewa , lakini ni kama kwa moto.(naitaga chupu chupu) Biblia inaeleza wazi, labda tu wavivu wa kuisoma. Mtume Paul alipogundua hayo akamalizia hivi. 1kor 9.,26..27 HATA MIMI NAPIGA MBIO VIVYO HIVYO, KAMA ASITAYE,NAPIGANA NGUMI VIVYO HIVYO, SI KAMA APIGAYE HEWA, BALI NAUTESA MWILI WANGU NA KUUTUMIKISHA, ISIWE NIKÍISHA KUWAHUBIRI WENGINE, MWENYEWE NIWE MTU WA KUKATALIWA. Ndugu zangu waenda Mbinguni, nimejaribu kuelezea uelewa wangu, ninavyoelewa, kuwa MATENDO kabla ya Wokovu ni Sifuri. Ila MATENDO baada ya wokovu yanatakiwa sana, kanisa lifundishwe, liamke, limtendee Mungu kazi. Mbarikiwe.

 3. Mpendwa Tunkuh,
  Ulichokisema ndiyo ukweli wenyewe haswaaaaa, kinachotukwamisha watu wengi ni kutokukubali kujifunza kama Neno la Mungu linavyoagiza, bali watu hupenda zaidi kushika na kufuuata mafundisho au mapokeo ya ki dini! Hakuna juhudi ya kibinadamu kwake mtu aliyechaguliwa na Mungu kwa ajili ya Wokovu. Biblia inasema, Si ninyi mulionichagua mimi ila mimi ndiye niliyewachagua ninyi. Zipo hatua tatu ili mtu afikie wokovu kamili, Kwanza. Kuokolewa, pili, unatakaswa na tatu una jazwa Romo mtakatifu ndipo unaongoka na kuwa kamili. Na katika hatua zote hizo haipo juhudi yoyote ya Kibinadamu inayotumika, hata Yesu alipata kusema kuwa “…..nitakuombea ili utakapoongoka uwakamilishe na Ndugu zako….” Hapo unaona, haipo juhudi yoyote ya mtu!
  @ Patrick G. Kamera,
  Kanisa ni nini: Kwa maana ya jumla Kanisa ni kama ulivyoainisha wewe, lakini ni zaidi sana ya maana hiyo, ingawa ukisoma, Mdo 12:5 “…nalo Kanisa likamwomba Mungu….” Yak 5:14 “….na awaite wazee wa Kanisa…” nk, inaonekana kwamba Kanisa lisemwalo hapa ni Kusanyiko la Waaminio, ni sawa sikatai, hivyo ndivyo ilivyo! Lakini maana halisi ya Neno kanisa Kwa mjibu wa Yesu ni nini? Kanisa ni pahali pa Kuabudia, sehemu ambapo pamewekwa Jina la Mungu ili watu waende hapo wakaabudu, humo ndimo Sheria ya Mungu imewekwa (Yn 4:23-24), ni hekalu ni Mtu(Yn4:23 “…Baba anawataka Watu kama hao ili wamwabudu…”)! Tena ni Mtu Binafsi ukisoma ile Mt 16:18 inasema, na juu ya Mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; Kanisa la Yesu hujengeka Juu ya Imani aliyonayo Mwamini, kwa mfano uleule wa Imani ya Petro aliyoionyesha mbele ya Yesu kwa kukili mwenyewe kuwa,”….wewe ndiye Kristo mwana wa Mungu aliye hai…” (Mt 16:!6); Na hata ukiiangalia ile 1Kor 6:19 nayo inasema, “…hamjui kuwa mwili (si miili) wenu ni hekalu….” ; Yapo maandiko mengi tu yanayofundisha na kuthibitisha kwa uzuri jambo hili.
  Lakini, pengine hoja kuu na ya msingi sana ni kwanini Makanisa haya (Makusanyiko) yameparaganyika na yanaendelea kuparaganyika kila kukicha sambamba na kuzaliwa mapya kila leo? Makusanyiko haya Kwanini hayana umoja, licha ya kwamba yanadai ni Mafuasi safi sana ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliyehai? Na je, makanisa kama haya yanafaa tuingie ndani yake tuabudu mungu aliye mtaatifu sana kama huyu tumjuaye na yafaa tuongozwe na wasimamizi wa haya makanisa ambao nao wameparaganyika kila Mchungaji na lwake?!
  Chanzo cha Mitafaruku yote ni Shetani, sasa kama ndivyo Yesu ni Mwongo alipo sema kanisa lake halitatikiswa na Nguvu za Kuzimu, ikiwa Makanisa yetu yana 100% kuwa yanakubalika na Mungu Mwenyezi kuwa yapo safi na yanawatendaji wasiyo na sababu ya kutahayali? Bila upendeleo wowote ni kwamba, makanisa mengi tuliyonayo leo si makanisa ambayo Yesu alimaanisha, kama ndivyo basi, Juhudi hizi zetu zote ni zero! Lo basi sisi ni masikini kabisa! Kumbe kama ni hivi na hali kama ndiyo hii tutapataje kupona? Njia ni moja tu, nikuondoa mawazo na utegemezi juu ya makanisa haya na Kuikimbilia Biblia na kushika yote yaliyoagizwa humo kama Mtu binafsi, hekalu takatifu ambamo sheria za Mungu ziandike humo (Isa.51:7) na ili Ibaada ipate kufanyika humo! (Yn.4:24) Kwa hiyo, kama Mtu ajitambue kuwa Yeye ni Kanisa (1kor.3:16)!
  Kosa tunalolifanya sisi tujiitao tumeokoka ni Kumwacha Kristo na kuwafuata watu wanaokuja kwa majina yao, huku wakiwahadaa kwa vivutio vya “Miujiza” Neno katika Yohana 5:43 linasema, Mtu akija kwa jina lake huyo mtampokea! Mtu akija na jina la Roman cathoric, mbio watu wanamfuata, akija kwa jina la anglikana, mbio watu wanamfuata, akija kwa jina la AICT, mbio vilevile, na akija kwa jina la Asembliz kama kawaida mbio sana tu, wanamfuata; Sasa akija kwa Jina la baba (Yesu) shida inaanza, mara Neno halipo hivyo, wanatoka! Mara, Sheria zake ni ngumu hao wanatoka, lakini kilcho kibaya zaidi wanajifanya wanamkubali sana lakini kiukweli “Hawamkubali kabisa!” Kwanini, NIAKINA YUDA,ni Waamini wa KUJIFANYA!
  Kwahiyo Mabinza unataka kusemaje, tusiende kunako makanisani? Hapana, sijashauri wala kupendekeza hivyo, Biblia inasema, KUSANYIKENI TU, MAANA HIYO NI DESTURI!

 4. Sharom watumishi…..
  Mimi naungana na ndugu yangu Patrick hapo juu…kuhusu nini maana ya kanisa na utakatifu ni nini… Binafsi pia naona Kanisa la kale, juzi, leo na hata keshokutwa litakuwa nii lilelile. Hayo magunduzi yanayoonekana leo huku kwetu yalikuwepo toka enzi za kale ukitaka ushahidi fanya utafiti ktk historia ya Izrael… na soma Bible. Tatizo letu wapendwa wengi hatujishughulishi ktk kumjua Mungu kibinafsi na kwa kudhamiria, tunamjua kiujumlajumla sana.. hatutaki kutumia nguvu zetu kumtafuta, ndio maana tumekuwa waoga tunapoona mabadiliko na tumekuwa watu wa mapokeo zaidi kuliko kuwa watu wa rohoni…
  Nijuavyo mimi kila m’damu aliyeokoka ana Roho Mt. afanyae kazi ndani yake ebu tumsikilize yeye maana atatupa majibu ya maswali yetu yooote. Tusilahumiane, tusishutumiane, tusitafsiriane mabaya n.k. Kwani sote sisi ni kanisa la Mungu..sote tu Bibi Harusi wa Bwn. Harusi mmoja ambaye ni YESU KRISTO.

  Ndugu yangu Samuel nataka kukazia na kukumbushia.. kwa nini Biblia imesema kuokoka ni kwa Neema….Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake kuwa ili mtu aje kwake (aokoke) ni lazima awe amechaguliwa na Mungu (Na hiyo ndio neema yenyewe).. hivyo mpaka Mungu aingie mkataba na wewe ujue ameshakuandaa kimatendo pia… maana anakujua tangu tumboni kwa mama yako na amekuweka ktk kitanga cha mkono wake…Baada ya kukuchagua ndio utapokea huduma zote za kiungu ikiwa na kumkiri Yesu ni Bwn na mwokozi wako, baada ya hapo utapokea Roho Mt. ndiye atakaye kuelekeza amri, sheria, ahadi na silaha za Mungu…. Ndio maana Mt.Paul alisisitiza kuwa kuokoka ni kwa Neema (maana ndani yake kuna mengi yakiwemo Matendo) si Matendo, Matendo mema ameumbiwa M’damu kuyatenda awe ameokoka au la….. lakini hayana kibali machoni pa Mungu mpaka muhusika awe amepata ile Neema ya kuchaguliwa na Mungu kuwa mwokovu….

  Asanteni sana.

 5. Wapendwa katika Bwana, nawasalimu wote katika jina la Yesu Bwana wetu na Mwokozi wa maisha yetu. Swala hili ni zito kama mtu akitulia akalitafakari. Ila mtu akilichukua juu juu a aliona kama jepesi kabisa. Ndio maana hata Maandiko mengi yamepotoshwa kulingana na tafsri mbali mbali, nakumbuka Petro kuna mahali alisema Nyaraka za ndugu yetu Paul ni nzito, na watu wasio na elimu huzipotoa, ebu nitoe mfano, unasikia mtu anasema, TUMEOKOKA KWA NEEMA, WALA SI KWA MATENDO, MBINGUNI TUNAENDA KWA NEEMA TU WALA KWA MATENDO. Hapo mtu anadhani amemaliza, ili mradi amemkiri Yesu kwa kinywa, amemwamini moyoni, amepata haki, amepata na wokovu. Anaingojea Mbingu, sasa tusome andiko linalotamka kuhusu NEEMA hiyo. Tito 2.11…14 Maana Neema iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo yatufundisha…..KUKATAA UBAYA, KUKATAA TAMAA ZA KIDUNIA, TUPATE KUISHI KWA KIASI, KWA HAKI, KWA UTAUWA KATIKA ULIMWENGU HUU WA SASA, Inamalizia kuwa WALE WALIONA JUHUDI KATIKA MATENDO MEMA. Ndugu wapendwa ktk kitabu cha ngu kiitwacho NJIA NI HII IFUATENI, nimeelezea kuwa NEEMA ni AJIRA. Maana ukisema kifupi tu kuwa tumeokoka kwa Neema kitu ambacho ni kweli, lakini Neema hiyo INATUFUNDISHA CHA KUFANYA, CHA KUKATAA. Ndiyo maana Yesu akasema..Kwa nini mnaniita Bwana Bwana na hamtendi niwamuruyo? Ndiyo imeandikwa, Imani bila matendo imekufa, ndio maana imeandikwa Hakuna kinyonge kitakachoingia Mbinguni. NEEMA hiyo ndiyo ile aliambiwa NUHU atakavyofanya apone, NEEMA hiyo naweza iita kuwa inatuonyesha au inatuchorea Ramani, nimesema niliita AJIRA, chukua mfano wa mtu aliyeajiriwa, anapewa utaratibu wa Ajira yake, Nini anatakiwa akifanye, Nini anatakiwa asikifanye, Muda gani aripoti kazini, muda gani aondoke kazini, akitimiza masharti ya kazi ndipo atakuwa na haki ya kulipwa mshahara, Niseme hivi kila kazi ina miiko yake, ambayo mwajiriwa hatakiwi kuivuka, Ajira ya mtu inamchorea mipaka, mwajiriwa anajichunga asiivuke, kwa mifano hiyo niliyoiainisha KANISA nalo ambalo ni MWILI wa KRISTO lina mipaka yake ambayo NEEMA inatuchorea, hicho ndicho kinacholeta tofauti kati ya KIWANDA na KIWANDA, Ndicho kinaleta tofauti kati ya SHIRIKA na SHIRIKA. Ndiyo maana nikasema mwanzo kuwa swala hili ukiliangalia kijuu juu litakuwa jepesi tu, lakini ukitulia, ukatafakari mafundisho ya Bwana Yesu, ambaye ni Bwana Arusi, atakayekuja kulichukua KANISA LISILO NA ILA WALA KUNYANZI, KANISA TAKATIFU. Linatakiwa kujiandaa.

  Zaidi ya MANENO vinywani, ndio maana imeandikwa, MSIPENDE KWA NENO BALI KWA TENDO. Ndiyo maana Mungu hakukaa tu mbinguni atuletee salaam za upendo, kuwa nawapenda, alimtoa mwanae, naye hakukaa tu atutumie salaam, alijitoa akafa msalabani. Nimalize nikisema tuiangalie Biblia vizuri, ndiyo ina mchoro wa ramani ya safari yetu. Mbarikiwe.

 6. Kuhusu habari za kanisa, la sasa ni kweli kabisa zinachanganya, sababu nyingine amboyo inasababisha ni pamoja na uelewa tofauti katika biblia,ukiangalia 1wakorintho 12:12-31 inaeleza kwa uyakinifu kuhusu umoja katika kanisa, yamkini kila mmoja ambaye ameshaugusa mlango huu hawezi kufanya mafarakano katika kanisa, pia biblia yasema ‘tusipunguze wala kuongeza neno la mungu’ Amin.

 7. bibilia inasema shika sana ulichonacho asije mwingine akakupokonya hivyo tulinde imani zetu na tuwe makini na makanisa yanayozuka kila kukicha

 8. Hakuna utakatifu wowote utakokuwepo kama watu hawatarudi kuyaangalia maneno ya Mungu juu ya kanisa lake. Tunapaswa kuyarudia mapito ya zamani ya wazee wetu. Kuheshimu sabato ya Bwana

 9. Wapendwa, mimi nadhani ni vizuri tukirudi kwenye Neno La Mungu ambalo ndio dira yetu. Tuanze na maswali ya msingi kabisa ambayo ni haya:

  1. Kanisa ni nini?
  2. Utakatifu ni nini?

  Tukishapata majibu ya maswali hayo kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, ndipo tutaweza kuongelea Kanisa la Leo na Utakatifu kwa usahihi, vinginevyo tutaishia kuzungukazunguka tu na mafundisho ya wanadamu na mapokeo yetu ya kidini.

  Kwa kifupi tu, Neno “Kanisa” au kwa Kiyunani (lugha ya asili iliyotumika kuandika Agano Jipya) tafsiri yake ni “Kundi la watu walioitwa kwa kusudi maalum”, yaani “called out”. Hivyo basi Neno Kanisa lilitumika kwa vitu vingi tu kama vile vyama, mabaraza au makusanyiko maalum, hata vilabu vya michezo n.k. Kwa maana hiyo tunaweza kuhitimisha kuwa Kanisa ni kundi la watu waliokusanyika pamoja kwa kusudi na lengo maalum iwe ni siasa, michezo, imani, n.k.

  Kwetu sisi tuliookoka Kanisa ni Mwili wa Kristo na kila aliyeokoka anafanyika kuwa sehemu ya Kanisa. Pamoja na kwamba tumezoea kuliita jengo tunalokutania kuwa ni Kanisa au Kanisani lakini kimaandiko sivyo ilivyo. Tukienda kimaandiko tutaona ya kwamba Kanisa linakutana ili kujengana, kutiana moyo, kuonyana, kufarijiana, kuhimizana na kuhudumiana kwa kadiri ya neema na vipawa ambavyo kila mmoja wetu amejaliwa na Roho Mtakatifu.

  Utakatifu ni nini? Kimaandiko utakatifu ni kuwekwa wakfu kwa ajili ya Bwana, kutengwa kwa namna maalum, kipekee kwa ajili ya Mungu wetu, Kumbuka ni Kuhani Mkuu pekee kabla ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu alikuwa anavaa chapeo yenye maneno haya kwenye paji la uso wake: “UTAKATIFU KWA BWANA” Kama Kuhani Mkuu huyo sadaka ya damu anayoingia nayo Patakatifu pa Patakatifu ikikubaliwa na kupokelewa na Mungu na huyo Kuhani Mkuu kupata kibali mbele za Mungu basi na taifa zima la Israeli linapata kibali mbele za Mungu na dhambi zao kufunikwa kwa mwaka mzima. (Kutoka 25 – 27)

  Hiyo ilikuwa katika Agano La Kale, katika Agano Jipya Bwana Yesu ndiye Kuhani Mkuu wetu asiye na doa wala waa lolote naye aliingia Patakatifu pa Patakatifu na Damu yake Mwenyewe aliyoimwaga kwa ajili yetu na kukamilisha ukombozi wetu. Hivyo basi tukiwa ndani yake Bwana Yesu tunahesabiwa kuwa wenye Haki na Watakatifu mbele za Mungu. ( Waebrania 4 – 10)

  Mbarikiwe Watakatifu wa Bwana!

 10. Mungu atusaidie tufike tuendako? maana kanisa la sasa kweli ni wachache sana wanaoenda kanisan wakiwa na nia dhabiti ya kumtafuta Mungu. Na walio weng wameshafanya kama fasion

 11. Wapendwa, kwani Neno la Mungu linasemaje kuhusu Kanisa la Kristo?. Bwana Yesu mwenyewe alisema, nitalijenga kanisa langu na milango ya kuzimu haitalishinda. Ninaamini mpaka leo hii Bwana Yesu anaendelea na ujenzi wa Kanisa lake. Kanisa la Kristo linazidi kukua kwa idadi na kwa ubora vilevile maana anakuja kwa ajili ya Kanisa lisilo na waa wala kunyanzi lolote na yeye mwenyewe ndiye anayelijenga na kulitunza.

  Utakatifu ni matokeo ya mtu kuwa ndani ya Kristo maana yeye ndiye chanzo au kiini cha Utakatifu. Matendo yako binafsi hata yawe mazuri kiasi gani hayakufanyi kuwa mtakatifu mbele za Mungu bali kifo cha Bwana Yesu pale msalabani na ufufuo wake ndio vinatufanya kuwa watakatifu tunapomuamini yeye. HIvyo kama umemwamini Bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wako, mbele za Mungu umehesabiwa kuwa Mwenye Haki na tayari umekwisha tengwa kama Mtakatifu wake. Mbarikiwe!

 12. Bwana Yesu asifiwe wapendwa ktk Kristo.Kiukweli kanisa la leo lina changamoto sana,kumekua na makanisa kila kona,na kila kanisa linajiona sahihi kuliko jingine.Manabii,mitume,maaskofu,wachungaji wanaibuka kila kukicha,na wote wanakuja kwa jina la Yesu wakitenda miujiza,na wamekua wakijipatia waumini wengi sana,lakini je ni watumishi wa Mungu kweli?(siwahukumu maana hiyo sio kazi yangu).Biblia inasema” watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Wapendwa tumuombe sana Mungu atuwezeshe kuijua kweli ili hiyo kweli ituweke huru.Mbarikiwe wapendwa.

 13. n vigumu kuuelezea huo utakatifu maana zaman watu waliamin mambo bila ya kuulza maswali meng na pia elimu ilikuwa n ndogo sana kwa kipind kile ndo maana.
  kwsasa watu wanachanganua mambo sana hvyo kupelekea kuona kana kwamba bible haina mashiko sana kulinganisha na misimamo mingine ya kimaisha.
  By conlusion n kwamba elimu ndo imepelekea ule tunaodhan ni utakatifu kupoa au kufifia.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s