Imani katika msingi wa utakatifu inakustahirisha mti wa uzima

rev

Adamu alipowekwa kwenye bustani ya Edeni, hakuzuiliwa matunda ya mti wa uzima, alistahirishwa matunda ya miti yote isipokuwa yale ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya tu. Angalia vizuri Mwanzo 2:15-17, “Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu AKAMWAGIZA huyo mtu, akisema, matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya huo utakufa hakika.” Kabla ya hapo tunaona katika mstari wa 9 kwamba, “Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” Unaona, hii ni miti miwili tofauti, yaani mti wa uzima katikati na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Ni mti mmoja tu aliozuiliwa kula ambao ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hakuwa amezuiliwa kula matunda ya mti wa uzima. Hata hivyo alipotokosa katika utii yaani alipokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ndipo alipozuiliwa kula matunda ya mti wa uzima (Mwanzo 3:22-24) aliyokuwa anakula hapo kabla. Tena katika mistari hii ya mwisho inaonyesha kwamba mtu akila matunda ya mti wa uzima yanamfanya asife kabisaaa.

Katika agano jipya huu mti wa uzima ni Yesu Kristo mwenyewe. Yesu anasema katika Yohana 6:48,50-51 kwamba, “Mimi ndimi chakula cha uzima…Hiki chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele…” Huyu ndiye awakilishaye mti wa uzima katikati ya bustani. Dunia ni bustani, Yesu ndiye mti wa uzima ulio katikati ya dunia. Mti huu unayo matunda ambayo kwayo tunapata uzima. Matunda hayo ni kama vile Meza ya Bwana (Holy Communion), Damu ya Yesu, Mafuta ya Upako, Mantle, Sala, Kufunga, Jina la Yesu n.k. Haya yote yanatoka kwenye mti wa uzima ambao ni Yesu Kristo. Haya ni matunda ya mti huo. Tunapotumia matunda haya tunapata uzima uliokusudiwa kwa ajili yetu. Haya matunda Mtume Paulo anayaita hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi (Waefeso 3:10).
Kutokutii kulimzuilia Adamu matunda ya mti wa uzima. Hali kadharika kutokutii leo kutakuzuilia wewe matunda ya mti wa uzima kama yalivyoorodheshwa hapo juu. Adamu alizuiliwa kwenda kwenye mti wa uzima tokana na kuingia kwenye kutokumtii Mungu. Hakuweza kuyala tena matunda matamu ya mti wa uzima. Vivyo hivyo wewe utazuiliwa matunda ya mti wa uzima endapo unaishi katika kutokumtii Mungu. Umeambiwa leta zaka kamili (zaka toka kwenye mapato yako yote) – Malaki 3:10; umeambiwa kuziondoa nadhiri zako kwa Bwana (Zaburi 106:14,18). Mfano wa nadhiri ni zile dhabihu ambazo Mungu alidai tumtolee Yeye kwa ajili ya kazi yake mwaka huu. Huenda Mungu anataka kazi yake ipendeze kisha kila mmoja wetu apendeze kwa kiwango kilekile (accordingly). Sasa mtu asipotii katika maagizo ya Mungu atawezaje kuuendea mti wa uzima na kula matunda yake?
Mti wa uzima unaendewa kwa imani katika msingi wa utakatifu. Alipokuwa bado mtakatifu, Adamu aliweza kuuendea mti wa uzima na kula matunda yake. Lakini alipoacha kumtii Mungu, utakatifu ulitoweka ingawa bado alikuwa na imani kuhusu matunda ya mti wa uzima. Mungu alijua kwamba kwa imani yake hiyo angeliweza kuuendea tena mti wa uzima na kula tena matunda ya mti wa uzima kisha akaishi milele. Hii ingeliharibu mpango wa Mungu kwani dhambi ingelitukuka milele kama Mungu anavyotukuka milele. Hivyo Mungu akamzuia Adamu asiweze kufaidi toka kwenye mti wa uzima. Imani katika matunda ya mti wa uzima nje ya msingi wa utakatifu haitakufaidia kitu. Imani katika Meza ya Bwana, Damu ya Yesu, Mafuta ya Upako, Sala, Kufunga, Mantle, Jina la Yesu; endapo utii hauko mahali pake, utatumia matunda hayo kimwili tu nayo hayatakufaidia kitu kwami unakuwa umezuiliwa na Mungu kufaidi toka kwenye mti wa uzima. Katika maandiko inaonyesha kwamba Adamu alizuiliwa kimwili lakini siku za leo watu wengi wanaojiita Wakristo huzuiliwa kiroho kwani wanakuwa na uwezo wa kuyaendea matunda kimwili tu. Waweza kukuta mtu ni mkorah (asiyetii, mdhambi) kweli kweli lakini analiitia Jina la Yesu, anatumia damu ya Yesu n.k. Ebu fikiria kuhusu mtu asiyetoa fungu la kumi, huku ni kutokutii kama kwa Adamu, sasa unakuta mtu huyu naye anakimbilia kutumia damu ya Yesu ili impatie mambo ya uzima uliokusudiwa. Ndiyo, anaweza kufanya kimwili lakini kiroho kazuiliwa kufaidi kwa hiyo hatafaidika. Ikiwa waganga wa kienyeji wana kanuni na masharti, itakuwa ni kujidanganya tukidhani kwamba twaweza kujizebeza na kupotezea ukweli kisha tufaidi matunda ya mti wa uzima.
Kwa mfano, Jina la Yesu ni mojawapo ya mtunda ya mti wa uzima. Biblia inasema kwamba, “Kwa kuwa kila atakayeliitia Jina la Bwana atakoka” (Warumi 10:13). Kuokoka ni kuingia kwenye uzima kwa hiyo Jina la Bwana ni tunda la mti wa uzima. Hata hivyo mtu asiye na utii amezuiliwa kufaidi toka kwenye Jina la Yesu. Biblia inasema, “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, kila alitajaye Jina la Bwana na auache uovu” (2Timotheo 2:19). Mtu kashambuliwa na malaria lakini hana utii. Unakuta mtu huyu anapoliitia Jina la Yesu ndipo malaria inapoongezeka zaidi. Mtu yuko kwenye tatizo au magumu yoyote lakini hana utii kwa Mungu. Huyu analiitia Jina la Yesu kisha magumu au matatizo yanaongezeka.
Meza ya Bwana ni tunda la mti wa uzima lakini wapo wengi walioshiriki katika ukorah kisha wakawa hawawezi yaani wadhaifu na kadha wa kadha wakafa (1Wakorintho 11:27-30). Unaona, mtu anakimbilia matunda ya mti wa uzima katika ukorah, nje ya msingi wa utakatifu, na matokeo yake ni kuumia zaidi. Wapo Wayahudi wana wa kuhani waliodhani matunda ya mti wa uzima yaweza kutumika kiholela nje ya msingi wa utakatifu, na walipojaribu kuleta ubongo fleva wao, usanii wao, pepo liliwatandika wakakimbia wakiwa uchi huku wamejeruhiwa (Matendo 19:13-16).
Ninaiona IMANI ndani watu wengi lakini siuoni UTII (UTAKATIFU) mkamilifu. Wengi wamekuwa wakitumia matunda ya mti wa uzima pasipo matokeo, sasa mafundisho haya ni mwendelezo wa majawabu aliyonipa Mungu ndani ya siku tatu tulipoanza kufunga na kuomba kwa nguvu zote. Usikubali hali yoyote ikuzuie kutiririka katika utii mkamilifu. Mungu alimzuia Adamu kula yale matunda lakini shetani akamwambie ale. Yeyote, chochote kinachokuambia uende kimyume na maagizo ya Mungu ni shetani. Hata kama ni baba mzazi, mama mzazi, kaka, dada, mume, mke, mtoto, ndugu, rafiki n.k.
Mungu akupe ufahamu mzuri katika Jina la Yesu Kristo.
Rev. MUABUZI, Y. Primus
Advertisements

4 thoughts on “Imani katika msingi wa utakatifu inakustahirisha mti wa uzima

 1. 1 Kisha malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima maangavu kama kioo yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo. 2 Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uzima unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa. 3 Hapana kitu chochote kilicholaaniwa kitakachokuwa katika mji huo. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwa katika mji huo, na watumishi wake watamwabudu. 4 5 Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.

 2. Rev. Muabuzi,

  Ubarikiwe kwa mafundisho mazuri na ya msingi na yenye kujenga mwili wa Kristo!

  Yote uliyoyasema ni ya haki, ambayo tukiwa kama waaminio, inatupasa kuyatimiza hayo kwa furaha, ikidhihirisha Utii wetu kwa neno la Mungu uliozaliwa katika Upendo, ambao kwao tumefanywa wana. Hapa nikilizungumzia Fungu la Kumi, ule utoaji. Jambo hilo ni kwa upande mmoja, wa huyo mtoaji.

  Upande wa pili wa transaction hiyo, yuko mpokeaji. Kwa kadiri ya Neno la Mungu, upande huu wa mpokeaji husimama Mungu mwenyewe kuyapokea hayo matoleo yetu, na katika hilo humsimamisha muwakilishi wake aliyemsimika kwa ajili hiyo. Kwa siku ya leo mwakilishi huyo ni Kanisa au Huduma za kinabii/ kitume kama zilivyoshamiri leo hii.

  Swali nililonalo moyoni mwangu ni hili, Je, Kanisa au Huduma ya kinabii/kitume, ambayo imejengwa nje ya Utii wa Neno la Mungu, inao uhalali wa kupokea Fungu la Kumi?

  Asante na ubarikiwe!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s