Je una jambo la kumshukuru Mungu mwaka huu?

thanks

Zimebaki siku chache mwaka 2012 uishe.  Sijui kuhusu wewe lakini ninayo mengi ya kumshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea makubwa kwa madogo, wakati mwingine changamoto zilikuwa nyingi lakini nikiangalia nyuma nilikotoka hata hapa nilipo kwa Neema ya Mungu na ulinzi wake amekuwa pamoja nami.

Mshukuru Mungu kwa aliyokutendea 2012, Mungu amekuepusha na ajali, wengine wamepata wenzi, nyumba, hawajashinda njaa, kazi na mengineyo ni kwa msaada wa Mungu umeyaona hayo. Kuna wengine hawajajaliwa kuwanavyo!

Kwa ambayo tunangojea mwaka 2013, tuwe na subira tukimtumaini Bwana atatufanikisha.

Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima“. Zaburi 34:1

Advertisements

6 thoughts on “Je una jambo la kumshukuru Mungu mwaka huu?

  1. mungu n mwema hataunfksha hu mwaka yamepita na yamtokea matukio meng ila mungu amenvusha kwa utukufu wake

  2. mimi ninamengi sana ya kumshukuru Mungu lakini wacheniandike haya machache maana nikisema niandike yote hapa hapatatoshea ni mengi sana Mungu amenitendea kwanza namshukuru kwa huu uzima anayonipa nakuniokoa ktk majaribu mengi ya shetani nakunipigania na maadui wanavyotaka kuniangusha lakini wanashindwa maana ninaye mlizi wa ukweli ambaye hashindwi na lolote nimepitia changamoto nyingi haswa mwaka jana hakika sijawahi kuona mkono wa Bwana ukinipigania kiasi hicho kwa ujumla namshukuruMUNGU sana na nazidi kumwomba azidi kunipigani na huyu mwovu shetani na aweze kunivusha salama mwaka huu mimi na familia yangu jina la Bwana lihimidiwe sana Amina

  3. Na mimi nnamengi yakumshuru Mumgu ila kwa leo nitamshukuru tu kwahaya machache,kwanza ulinzi ktk ndoa yangu Mungu amekuwa muaminifu sana kiasi ya kwamba maisha yanguyote najiona kama nikombinguni pamoja na changamoto ninazopitia bado ushindi nimeuona

  4. sijui nikushukuruje eee Mungu wangu, kwani hata hapa nilipo ni kwa neema yako tu. Akhsante kwa yote uliyonitendea kila iitwapo leo. Bila wewe siljui ningekuwa wapi.

  5. i thank god for this year 2012.he have been extraodinary good to me no matter how i fell he rose me up again..there are hard situations that i did come across but he kept me going hoping and beleaving the sufferings made me stronger and closer to him…dears god is good all the time and he knows the plans that he have for you for2013..lets pray that we be able to walk in god perfect plan.jeremiah 29;11..be blcd.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s